SOME LEMONADE FOR YOU.. PART 3 - MWISHO

  • September 01, 2018
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 0 Comments




HUU NI MWENDELEZO WA SEHEMU YA 1 NA 2, KAMA HAUKUSOMA SEHEMU YA 1 NA 2  TAFADHALI NENDA PAGE INAYOFUATA...


______________________________________


CAUTION/ TAHADHARI:

MPENZI MSOMAJI USOMAPO HADITHI HII JUA KUWA HII NI HADITHI TU KAMA HADITHI ZINGINE - NI MOJA KATI YA BURUDANI ZILIZOPO DUNIANI

TAFADHALI USICHUKULIE BINAFSI (PERSONAL) 

____________________________ 


SEHEMU YA 8
C. LIMAO YA MAOMBOLEZO NA VITA




Carrie akiwa kwenye mawazo yake yale yale ya nitafanyaje sijamaliza mwezi tangu mume kufa, blah blah blah kibao.
Mzungu wa watu yupo magotini akamjibu: Chris Nakupenda kwa dhati umenipa raha nashindwa hata kukueleza kiasi gani nimeshukuru ujio wako, you are a heaven sent

Chris: akaangalia chini akajua hapa nimeshatoswa, dah! bado yupo magotini Carrie akaendelea,

Carrie: Naomba nipe muda nifikirie, kesho ni Arobaini ya familia yangu, watanionaje nikienda nimevaa pete!

Chris: oh! Pole sana, sawa haina shida, akainuka magotini hao wakaendelea kujiandaa kurudi Capetown. Walipomfikisha Chris hakutaka kuingia ndani, akamwambia mimi nalala hotelini kesho usiku naondoka, nitakuwa kwenye hoteli hii mpaka saa 3 usiku, ndege inaondoka saa 6 usiku, siwezi kuhudhuria 40 ya George kwasababu ya maneno ya watu.

Carrie: akashangaa kwa kuduwaa lakini ndio hana la kufanya, Chris akajiondokea kichwa chini na pete yake ya uchumbaaa.

40 on Fleekest!

Masista duu wakaja wampiga vimini balaaaa wengine, vitaiti, watoto wa Soweeeeetooo wamenona hao nahisi Chris angekuja lazima angedaka mmoja wa kujipooozea maana sio kwa ile mishepu.

Wakatoa pole kwa Carrie na wazazi wa George, utadhani wamekuja Disko!
Carrie: analia ila sio kama zamani analia tu basi ameshawakosa, ibada ikafanyika wakamshukuru Mungu kama familia wakatoa Sadaka ya shukrani, watu wakala, baada ya mambo yote kuisha Carrie akafunga nyumba yake akaondoka kuelekea Makaburini saa 10 jioni, akaenda kukaa kaburini walipozikia familia yake, akawa anaomboleza analia wee mara asali mpaka saa 12 jioni.

Carrie: sitawasahau kamwe hata kama Mungu amewapenda zaidi, bado mpo moyoni mwangu nawapenda, lakini George swala lililonikuta ni gumu, kulichukulia maamuzi kirahisi namna hii, nakupenda Mume wangu lakini sidhani kama nakusaliti kwa haya niliofanya, akakaa makaburini akiomboleza mpaka saa 2 usiku akaondoka kurudi kwake

    HUKO BONGO:
Wana maombi siku hiyo walishinda wanaomba tuu, wakaingia kulala hamna mtu alietaka kula, kila mtu aliangalia wanae na kusepa kulala, asubuhi kila mtu na njia yake ofisini akabakia mama mkwe, mama mtu mzima na Chanel.

Adrienne akiwa ofisini Jeff anazidi kumfuatilia lakini waapi, Adrienne kamlia kobis mbayaa.

Doreen amejaa upweke ofisini, kam-miss Lucifer, James, kamiss game, kujipiga bao hawezi maana si sawa kama next level za machine!

            HUKO BONDENI:
Chris: akawa anajiandaa kutoka aende Airport hapo saa 4 usiku, ile anafungua mlango mrembo Carrie huyooo na kivazi chake, akamfuata na kumvamia na mabusu, Chris anashangaa tu, movement za hapa na pale mechi ikapigwa, Chris kuangalia saa saa 5 nanusu usiku, akamwambia Carrie nakudai dola 80 ya kubadilisha ticket ya ndege.
Carrie: akampandia kwa juu, akimwangalia Chris mzuuuuriiiijeee akamjibu Yes I will marry you..
Chris akafurahi akainuka kuchum, chum chum na wewe, akatoka kitandani akaenda kwenye mfuko wake wa suruali akatoa pete akarudi kumvisha Carrie.
Carrie kuangalia bonge la Pete 25 Karat with Diamonds Ring!
Pete ni kali mara mbili ya aliopewa na mumewe, akarudisha shukrani kwa Chris sio kwa mamilioni yale alizowekewa kidoleni.
                               HUKO ULAYA:

 

KAKARACHA na Body Gurad James wanaelekea Msituni, KAKARACHA ana maumivu makali kweli kwenye mwili wake..

Nyuma ya pazia Shawn anawatraki akina James, akawaagizia mapolisi kuwahi kumdaka KAKARACHA.

KARAKACHA akainuka akimbie, James ikaamua kambeba KAKARACHA maana alikuwa na maumivu makali baada ya kupewa ngumi na Zubeda.

Huku nyuma Lucifer akakaribia kumfikia KARAKACHA anawaona walee wanakimbia lakini hakuona kuwa nyuma yake yupo Zubeda na nyuma ya Zubeda yupo Pedeshee, patamuuu.

Wakafika sehemu kumbe wamepita mwambani kwa juu, chini bonge la shimoo - dead zone,
Eeh! Majanga, James akamweka chini KAKARACHA, akamwona Lucifer anakuja, KARAKACHA maumivu yamepoa kidogo akakaa lakini kuongea hawezi.

Lucifer kufika akamnyooshea Bastola James akamwambia aondoke, James akaondoka akarudisha bunduki kwa KAKARACHA.

Lucifer: Upo chini ya ulinzi, ile anataka kumshika mikono akasikia teke la mgongo, kugeuka Zubeda,

Lucifer: Unafanya nini?
Zubeda: akachukua bunduki ya Lucifer ilioanguka akamnyooshea Lucifer, anataka kuifyatua, Pedeshee huyoo kamvaa Zubeda, risasi ikachomoka ikampiga KAKARACHA mkononi, tobaaa,

James: kusikia risasi akarudi bwana kujua kuna ushindi kumbe hamna kitu.

Pedeshee nae noma mfupi lakini yumo kwenye ngumi! Piga pigana na wewe, Zubeda alichapwa hakuna mfano wake, midamu inammwagika.

Lucifer:Akainuka kaja kumdaka KAKARACHA, kumrudisha kwao, wakaondoka wakawaacha akina Pedeshee na Zubeda wanapigana, kuna wakati Zubeda alipata nguvu akamchapa Pedeshee, akachukua ile bastola akampiga risasi za miguuni Pedeshee 3 akamalizia ya kifua, akajua amekufa Zubeda akaondoka

Kufika mbele wakaona nyomi ya maadui, KAKARACHA akacheka, watu wake wamekuja.

James na Lucifer wakaanza mkono, mkono wee KAKARACHA akakimbia, piga pigwa piga pigwa, mpaka wakawamaliza, kumwangalia KAKARACHA hata nguvu hawana, wakawa wanatembea kumtafuta wakamwona yuleee wakajikongoja  mdogo mdogo mara wanamwona Zubeda kamfuata KAKARACHA anamsaidia bega, wakajitahidi mpaka wakawafikia.

Zubeda kuwaona akamwachia KAKARACHA akaishika ile bastola akaifyatua;

Lucifer akaiona akainama, lakini James hakuiona, risasi ikaenda kumpiga James kifuani kwenye mbavu akaanguka chini.

Lucifer akakimbia akampiga Zubeda, piga na wewe, akaichukua ile buastola akamnyooshea Zubeda,.

Zubeda anamwomba asimdhuru, Lucifer akamuwasha moja ya usoni chaaaa! Zubeda chinii aheraaa mojaaa!

Akabakia KAKARACHA, anaomba asimdhuru, akampiga risasi ya mguu wa kulia na moja ya mguu wa kushoto KAKARACHA akalala chali anasikilizia maumivu!

Lucifer akarudi kwa James, madamu yamemmwagika mbayaa, akawa anamshikilia kuzuia damu, James anataka kuongea Lucifer anamzuia.

James: akatoa kitambaa akamwambia Lucifer sidhani kama nitapona, safari yangu imeishia hapa, nilimpa ahadi Doreen kuwa nitarudi lakini sitaweza, akakichovya kitambaa kwenye damu akamwambia Lucifer ampe Doreen, naamini yupo mikononi salama akiwa nae.

Lucifer: analia kwa uchungu masikini!

James: Nimekusamehe yote ulionitendea lakini hii ni kazi, tunalitumikia Taifa. Kishujaa nimeishi na kishujaa ninakufa, nawatakia maisha mema wewe na Doreen na watoto wenu, mpende Doreen wala usim-cheat, Nikiwa Mbinguni nitakuwa nawaangalia maisha yenu nikiwa juu kwa Mungu Baba.

Lucifer: analia kama mtoto mdogo.
James: akakata roho!
Lucifer: alilia kama mwanamke anaezaaa, kalia KAKARACHA kuamka anamkuta analia, akataka kuamka akijua Lucifer atakuja kumuua miguu yake haiwezi kutembea anajikokota kwa matako na tumbo ili akimbie Lucifer akamfuata akamshika alimdunda, alimduuuundaaaaaa, KARAKACHA alipigwaaaaaa, akaenda kuchukua ile bastola ammalizie, kumbe risasi zimeisha, KAKARACHA akapumua!
                  
BAADA YA DK 2:

Mapolisi haoo wakaja, wakamkamata KAKARACHA ile wanataka kumwingiza kwenye gari, KAKARACHA akachomoa bastola ndogo ya polisi aliekuwa anaongea na polisi mwingine akampiga nayo Lucifer kwenye mguu, wakamshika KAKARACHA fasta wakampiga ngumi na kumnyang’anya bastola, wakamtupa kwenye gari kama gunia.

Lucifer: anaugulia maumivu ya mguu mapolisi wengine wakaja wakaanza kumhudumia, mara gari ya Ambulance ikaja ikambeba James na nyingine alionekana Pedeshee ameshawekewa drip anapelekwa Hospitali.

Lucifer: anashangaa Pedeshee huku kaja kufanya nini? Mara anaona maiti ya Zubeda inapita, mara ya Sungura mara ya Body guards zinawekwa kwenye Ambulance zingine!

Baada ya siku 3 Lucifer akarudi ofisini, Shawn akafurahi kumwona Lucifer yupo hai.
Lucifer: James amekufa ila Pedeshee yupo hospital ana recover!
Shawn akaondoka kwenda kumsabahi Pedeshee amsalimie, kumwangalia uuuuuwi Pedeshee mguu mmoja hana!
Shawn: Dokta imekuwaje?
Dokta: Risasi aliopigwa imemuharibu mguu sana na walichelewa kumleta hospitali mguu umekuja haufai.
Shawn wa watu anashika kichwa hajui anamwambia nini Chanel! Chanel akijua itakuwaje!?
                      HUKO BONGO:
Weekend, Warembo wakatoka kwenda Beach! Wakaelekea Sea Cliff nyumba nzima wakaifunga.
Chanel akawa anacheza na mapacha wa Adrienne mara akaskia Pwaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Maji yanamtoka kwenye mwili wake, Hamadi!
Mama mkwe wa Doreen: Tumkimbize hospital atajifungulia hapa, kimbizana na wewe wakafika salama, wakakaa kama masaa 4 wanasubiria wajue dokta anasemaje, mpaka body gurd ana midadi!
Maana sio kwa kupendana kule, Dokta akatoka theater Doreen anamshika vipi Dokta Chanel vipi na mtoto vipi, Dokta akatikisa kichwa na uso wa Mbuzi!
Doreen: Usiniambie Chanel na mtoto wamekufa!
Dokta: Am sorry mama, tumefanya kila tunachoweza kumwokoa mama na mtoto.
Adrienne: Yeeeesu jamani hapaaanaaa!

TUONANE LEO SAA 2 USIKU YA TANZANIA 

____________________________ 


D. LIMAO YA MAOMBOLEZO 



Mama Mkwe wa Doreen akatokea jaman kuna nini hapa mbona mnapiga kelele, tupo hospitali hapa sio baa.
Adrienne na Doreen: wamekaa chini wanalia.
Dokta: anajaribu kuwanyanyua watu wamjaa.
Mama mkwe: dokta kwani kuna nini?!  
Dokta: nyie ndio ndugu wa Mrs Majoka?!
Mama mkwe: mh hapana, kwani Doreen Chanel mumewe anaitwa majoka,
Doreen: Akanyamaza kulia, mh sijui hilo sio jina lake sie mgonjwa wetu ameletwa akaanza kumwelezea Dokta akasema ah basi sio yeye mimi namwongelea mgonjwa mwengine yule yupo salama amejifungua salama mtoto wa kiume si Mrs Marion?!
Adrienne: akadakia ndio huyo huyo. Ah samahani sana kuna ndugu wa Mrs Majoka walikuwa wamejaa hapa sasa nikajua ndio nyie poleni sana kwa usumbufu.. wakafurahi machozi yakakauka.
Tunaweza kumwona.
Dokta: Subirini kwanza akipelekwa wodini mtamwona wakawa wanafuraha sasa, wanatamani wampigie Pedeshee wamwambie wakakaa nje na watoto wao muda ukaenda watoto wamechoka kukaa pale ikabidi body guard awapeleke watoto nyumbani pamoja na mama mkwe na house girl mama mzee, wao wakabakia mpaka mwisho!
     
HUKO ULAYA:

Shawn akamsogelea Pedeshee amelala, Shawn anatetemeka akiangalia ule mguu umekatwa mwengine upo vizuri.
Mara Pedeshee akafungua macho kukuta ni Shawn akafurahi, wakwa wanaongea Shawn anampa pole Pedeshee anacheka,usiogope Shawn hii ni moja ya kazi zetu mimi nina amani zote.
Pedeshee: akamuomba Shawn asimwambie mke wake kabisa maana anamjua asije akamuacha akaenda kwa Mark.
Shawn akakubaliana na yote.
Lucifer: mambo yake yapo supa ingawa kidonda bado amefungwa bandage ila kutembea anaweza lakini anatembelea fimbo ya mkono.
Akaenda kumsalimia Pedeshee anashangaa hana mguu. Akaelezwa na Shawn akatoa pole wakawa wanaongea. Pedeshee akamwomba asimweleze mkewe.
Baadae akaomba apumzike wakina Shawn wakaondoka . 
Shawn akapigiwa simu na Body gurd, anamwambia akina Adrienne wanampigia simu Pedeshee hayupo wanataka kuongea nae hapatikani.
Shawn akampigia mke wake wakaongea sana, akauliza kila mtu akaambiwa wapo vizuri.
Shawn: Mpenzi nimebakisha mwezi mmoja nirudi nyumbani kwa familia yangu nimewamiss sana, vipi Chanel ameshajifungua?
Adrienne: amejifungua mtoto wa kiume!
Shawn akafurahi kama wa kwake.
Adrienne: bado hajampa jina anamsubiri aongee na mumewe upo nae hapo jirani aongee na mkewake.
Shawn: hapana mpaka kesho tena uwe unakaa karibu na simu tutakupigia.
Adrienne: sawa.. akampa Doreen aongee nae,
Doreen:mwambie na Lucifer namtafuta anipigie.
Shawn: sawa.
Doreen:James vipi hajambo.
Shawn: naona kama unakatika haloo, haloo sikuskii akaikata simu maana umbea wa kutoa habari za misiba hataki.
  
HUKO BONDENI:
Bondeni kumenoga, wamemaliza wiki hotelini kama wana honey mooners.
Carrie: Chris twende wote Switzerland mimi sitaki kukaa hapa. Ile nyumba natafuta dalali anaipangisha nikilala nachanganyikiwa napata mawazo ya mume wangu huyu hapa na nini kwakweli siwezi.
Chris: akafurahi wakaondoka kwenda kuongeza tiket ya pili ya ndege.
Carrie: itabidi nikawaage wakwe zangu, nisubiri hapa hotelini ukija italeta shida. Akaenda kwa wakwe usiku wakamwambia alale, ikabidi ampigie Chris kuwa ameambiwa alale.
Asubuhi yake akafunguka kwa wakwe,
Carrie: Mimi siwezi kuishi hapo tena memories za familia zarudi na mimi siwezi ku control nilitaka nisafiri niende kuangalia Biashara zetu za Switzerland, pia nataka niipangishe hii nyumba.
Wakwe: Sawa, mali ni za kwako sio zetu tena mumeo amekukabidthi kisheria zote na za watoto wako ni zako hatuwezi ingilia hata moja.
Carrie: akashukuru akaaga ngoja niende naenda kufuatilia dalali wa nyumba.
Akasepea kwa dalali akampata wakamwambia kuuza nyumba ndani ya wiki moja ni ngumu labda utuachie mtu unaemwamini ambae akipatikana mteja anaweza kuja kutufungulia.
Akampigia Baba Mkwe akaongea nae akakubali akaacha kila kitu kwake na mawasiliano ya dalali akaondoka huyooooo kwa Chris.
Mauno mauno na hivi wamekaa siku 2 hawajaonana wakaona kama wamekaa miaka. Kesho yake usiku haoooo switzerland.
  HUKO BONGO:
Baada ya wiki kuisha Chanel akaruhusiwa kurudi nyumbani amebeba mtoto mzuuuuuri kweli kweli! Kabonge kama Babake, afu maji ya kunde kama Mama yake.
Wanamsifia Chanel anafurahi baadae simu ya Doreen ikapigwa akapewa Chanel wakaongea na Pedeshee kwa muda mrefu Pedeshee anafurahi akamdanganya mkewe anarudi baada ya miezi 2 ila hakumwambia kuwa hana mguu.
Lucifer: Anajiandaa kurudi Bongo maana walishamkamata mbaya wao na KARAKACHA alishafungwa kiRusi kwa kukatwa shingo. Ikambidi arudi haraka Bongo pamoja na timu yake. Akaomba apewe wiki hiyo amalizie matibabu wiki ijayo atarudi akakubaliwa.
Wiki ikapita kama mwaka kwa Doreen na Adrienne na Chanel, wakapata simu ya Carrie akiwa Switzerland. Wanashangaa imekuwaje akamwaambia ni hadithi ndefu jamani ila nimempata mtu, shemeji yenu mpya anaitwa Chris, ni mzungu nimekuja nae kwao huku.
Wenzake wanashangaa huyu mjane mbona mwendo kasi hivoo! Wakampongeza na kuongea kwa kirefu simu ikakatwa
       
KUTOKA ULAYA:

Watemi wameingia Bongo kimya kimya.
Stan, Don Lucifer, Pedeshee kwenye Wheel Chair na Shawn wakapokelewa Kishujaa na boss Mzee wakaenda kujificha kwenye nyumba ya Boss Mzee!
Mpaka mambo yao yatakapokaa vizuri…Stan akatambulishwa kama mfanyakazi mpya, wakamweleza kuwa Safaree na Peteroo wanatakiwa kufungwa nay eye anatakiwa atoe ushahidi wa maovu ya Safaree, Stan akakubali; mbele ya cheo kipya akatae?.
Wakawa buzy na kumalizia kesi ya Safaree na ushahidi kila kitu wakakiweka sawa.
Boss Mzee: akawaruhusu warudi makwao.
Wote wakafurahi kasoro Lucifer!
LUCIFER: Shawn msiseme kuwa nimerudi.
Pedeshee: akasema ngoja na nibaki nitarudi baada ya Shawn , Shawn upeleke ujumbe wangu kwa mke wangu nisikie atasemaje akaandika barua ndeefu akampa shawn.
     MTAA WA 3:
Ilikuwa siku ya jumamosi mchana, warembo wakiwa wamekaa wakaskia geti linafunguliwa, wapo buzy wanaangalia TV, mara wakaona mtu anafungua mlango, kuangalia ni Shawn!
Adrienne: hakuamini akakimbia kwenda kumkumbatia, jamani mume wangu umerudi analia na kamrukia kama kitoto.
Shawn anacheka anafurahi
Adrienne: Karibu Mume wangu Nakupenda sana, tumekumiss, matwins wamekuwa wanatembea.
Mishen ya miezi 10 imeisha kwa wakati wakaingia ndani,
Shawn: akasalimia.
Chanel: akamkumbatia karibu shemeji, pole na safari, anatumaini labda Pedeshee yupo nyuma yake, wote na Doreen.
Shawn: Lucifer na Pedeshee hawajarudi bado nimewaacha.
Shawn akatoa zawadi, akawapa mastori ya huko baadae akatoa barua ya Pedeshee akampa Chanel.
Chanel: haelewi akawa anaisoma fasta fasta kabla mtoto hajaamka, akaisoma kwanguvu wote wakanyamaza kumsikiliza:
BARUA:
“Mpenzi wangu Chanel Nakupenda sana, wewe pamoja na mtoto wetu.
Nimetamani sana kurudi lakini nimeshindwa, hali yangu ni mbaya sana! Nilipata ajali ya Treni wakati navuka nikavunjika miguu yote miwili, bado nipo hospitali Napata matibabu.
Nimetamani kurudi nyumbani nikafikiria na ulemavu wangu huu sijui kama utanipenda tena”…
Chanel akanyamaza: akaanza kulia, akina Doreen na Adrienne wanaangaliana wakaamua kwenda kumbembeleza ili amalizie kuisoma, lakini hakuisoma tena ile barua, wakawa wanafanya kazi ya kumbembeleza,
Shawn akaichukua ile barua akarudia kuisoma, ndipo Chanel akanyamaza,…
Shawn akaendelea... “Sitopenda wewe na mtoto wangu mnikute na hali hii, bora ninywe sumu nife kuliko kuwatesa, maana sina msaada tena kwenu na huu ulemavu sipendi kuwachosha na kuwasumbua!
Ulemavu Huu nitaenda wapi? Sitaki kuwa mzigo mara mbili kwako na mtoto wetu na kwasababu ninakupenda sana sitaki uteseke na mimi!
Mtoto wangu ataitwa Marion junior labda kama hautolipenda unaweza muita jina la Marehemu Baba yako.
Ikipita miezi 2 sijarudi, tafadhali naomba unisahau kabisaa ujue nimekufa, nitakuwa nimekufa kwa amani… nakuruhusu uwe na mwanaume mwengine yoyote hapa Duniani atakae kupenda na kukujali maisha yake yote, hata kama itakuwa ni Mark sina neno nimeruhusu.
Wako Mpenzi
Marion (Pedeshee)”
Chanel: alilia, aliliaaaa mpaka akakaa chini wenzake wakaenda kumshika wakamweka kwenye kochi Chanel hasikii
Chanel: Kwanini ananifanyia hivi, mbona anampenda tu kwani miguu kitu gani!?
Mbona hata ya bandia atawekwa jamani…
Wenzake wanamshikilia , wanamtuliza Chanel nyamaza tafadhali, unajua wewe ni mgonjwa unatakiwa utulie utawaamsha watoto, wamtuliza hasikii ikabidi wamchome  dawa ya usingizi baada ya dk 15 akalala.
Kumbe vituko vyote vinarekodiwa nyumbani kwa Lucifer. 
Baada ya Chakula cha usiku, wote wakaingia kulala, lakini Shawn na Adrienne hawakulala, usiku kucha ulikuwa ni uzinduzi wa Album ya Shawn na Adrienne.
Mechi non stop watu hawalali, mpaka asubuhi, uzuri kesho yake ilikuwa Jumapili.
Asubuhi Shawn akaipeleka ile video ya Chanel kwa Pedeshee, alimuaga mkewe anaenda kununua gazeti na kufuatilia ile nyumba waliokuwa wanakaa wapangishe wao wahamie kwengine.
Alipoiona ile video Pedeshee alishangaa, kumbe mke wake bado anampenda, maskini hana la kufanya akatamani arudi siku hio hio lakini bado roho inasita akajua tu mwezi ukiisha Chanel atakata tamaa ataenda kwa Mario lakini wapi, kila siku analetewa video Chanel anazidi kuwa Chizi.
Na akimwita mtoto Marion Junior ndio kabisaa analia tuu washamchoma misindano wamechoka sasa wanataka ahame pale.
Lucifer:Pedeshee utamuua huyu mkeo acha ujinga au Urusia imekufundisha ukatili!?
Rudi kwa mkeo haraka, akijiua mtoto atabakia na nani?! Kitu gani unaangalia wiki 2.
Pedeshee: Wewe mbona hauendi kwa Doreen?!
Lucifer: Umeona nimeandika barua kwake?
Embu ondoka nenda kwa mkeo hii nyumba ingekuwa yangu usinge kaa hapa.
Wakawa wanataniana hapo huku wanacheka



TUONANE KESHO J2 SAA 8 MCHANA YA TANZANIA  

_________________________________________________________________________________



E. ASALI YA MUME NA HUKUMU YA HAKI 
  
Malumbano ya hoja kati ya Lucifer na Pedeshee yakaendelea kwa muda wa dk 20, akaja boss mzee
Boss Mzee: vijana tuna kazi ya kufanya, kama hamtaki kwenda makwenu mniambie niwasafirishe tena mwaka mzima.
Vijana: ah hapana boss! tulikuwa tunataniana.
Boss Mzee: Mje huku tumalizie hii kazi kuna ripoti ya kupeleka
Baada ya wiki 2 Mahakama inaskiliza kesi ya Safaree na Peteroo, naamini watoa shuhuda wapo.
Lucifer: Wapo Boss.
Boss Mzee: Kesho kuna mazishi ya James, mtapenda kuhuduria wenyewe au na wake zenu?!
Pedeshee: Mwenyewe.
Lucifer: Bado sijaoa, nitakwenda mwenyewe.
Shawn: akaingia akawasalimia, akarudi kwa Pedeshee asee mke wako atamuua mtoto sasa hata kunyonyesha hataki washaanza kumpa mtoto maziwa ya ng'ombe mtoto analia hataki na mama ndio wa kuchomwa sindano ili alale sasa sindano na mama anaenyonyesha tunaogopa, embu rudi utawakosa wote ujue.
Juzi alitala kunywa sumu ya panya maana alishakoroga ile anaweka mdomoni bodyguard akaja akamputa ikamwagika.
Akaanza kumpiga kaka wa watu bila kosa, kwanini unamtesa mke wako ivyo!?
Boss Mzee: Wewe Pedeshee embu ondoka kwangu sitaki kukuona unaleta mzaha na familia hauoni wenzio na Lucifer tunavyohangaika?!
Unataka kuwa kama Carrie sio?!
Carrie familia yote iliuwawa na Peteroo mfuasi wa Safaree, acheni ujinga tokeni hapa nendeni makwenu.

Lucifer: Boss nikienda kwetu ujue naenda kuoa kama vipi niende fasta sa hivi.
Boss Mzee:  ah! hapana mpaka tumalize kesi ya Safaree ndio utarudi.
Lucifer: akamwambia Pedeshee, unaona mimi namtamani Doreen sana lakini wewe unachezea bahati.
Wakaendelea na maongezi yao ya kikazi walipomaliza, Pedeshee akaondoka na Shawn maana Shawn nae alikuwa anakaa kwa Lucifer mpaka watakapopata nyumba.
Kufika Shawn akaingia ndani Pedeshee akabaki nje, Shawn akaenda kumwangalia Chanel alipo, akamkuta amekaa kwenye bustani amelalia hammock analia huku body guard anamlinda, akapita mlango wa nyuma akaenda kumtoa Pedeshee kwenye gari anamsukuma, alipofika karibu na Chanel akamuacha Shawn akaondoka.
Pedeshee: Anamwangalia Chanel amelala amegeukia upande mwengine akawa anajivuta na kigari chake akaenda akamshika Chanel mkono.
Chanel: akadhani ni body guard akamwambia niache bwana mimi sili chakula, akarudia kumshika tena mkono Chanel akajinyofoa, akamshika kwenye tako, Chanel akainuka anasema ivi we kaka kabla hajamalizia kuangalia ni Pedeshee, OMG, Marion?! Is this you Au naota? Akajipiga vibao mashavuni aamke anafikicha macho, kumbe ni yeye.
Akamshika mikono mara shingo mara uso mara mashavu mara macho huku analia, Marion my love, umerudi! Akamkumbatia mume wake huku analia, na Pedeshee analia kwa furaha kumwona mke wake, wakaanza mabusu, Chanel kamkalia Pedeshee kwenye wheel chair, dah hajaangalia hata hiyo miguu, mabusu mabusu na wewe dk 10 nzima.
Shawn: anawaangalia kwa dirishani anacheka. Akashuka chini kwenda kumtafuta mke wake akakuta amekaa na Doreen akawasalimia, Adrienne akainuka kwenda kumletea mumewe chakula.
Huku nyuma Shawn akamwambia shemeji sijui ulisikia lolote au?!
Doreen: hapana shemeji kuna nini?!
Shawn: unajua kule tulipoenda mambo yalikuwa mabaya sana, sasa katika kazi zetu bwana James akatutoka.
Doreen: akashtuka ghafla?! Ha?! Nini? What happend?! 
Shawn: kulikuwa na majambazi wanatoka benki wanafukuzana na mapolisi sasa wakarusha risasi ikampata James kifuani na shingoni, mpaka ambulance inakuja hamna James tena.
Pole sana Shemeji sikukwambia maana tulikuwa tunahangaika na Chanel nikasahau kabisaa.
Pia kuna hiki kitambaa alikuwa amekishika wakati amepata matatizo akakitoa kile kitambaa ambacho alipewa na James kutoka kwa Doreen, kuangalia kimejaa damu.
Doreen alilia jamani, akaanguka chini amekishikilia kile kitambaa analia haelewi, James amekufa uuuwi, rafkiangu James jamani, akawa anambembeleza usilie bwana tafadhali shemeji pole, jikaze sasa wewe na Chanel mkilia atabakia nani huku ndani?!
Kesho kuna mazishi yake nitakuiba twende wote ila usilie tafadhali.
Adrienne akaleta chakula akakuta Doreen anajifuta machozi akauliza kuna nini?
Doreen: akazuga nimefurahi Pedeshee amekuja nimemwona, na Chanel full kumrukia maskini.
Adrienne: yuko wapi embu nimwangalie, kuangalia chini anamwona Pedeshee kakaliwa na Chanel wanakiss akafurahi, anasema makelele ndani yameisha na huyu mtoto atapona sasa akarudi kukaa na mume wake.
Doreen akaondoka akaenda chumbani kwake akawa analia anakumbuka James walivyokutana alivyokuwa anamfukuzia, walivyopendana, alivyomtoa bikira, basi afanyaje ni kulia mpaka kalala usingizi hapo hapo.

Chanel:Pedeshee twende nikupeleke ukamwone mtoto wetu.
Pedeshee: Nimeambiwa hata chakula huli unalia tu mtoto atakula wapi sasa?!
Chanel: We acha tu maisha bila wewe hayasogei, hayaendi, nisamehe mume wangu kwa kuwa selfish kwa mtoto wetu.
Pedeshee: akanyamaza
Chanel: anamsukuma kwenye kigari haoo wakaenda chumbani. Kufika mtoto amelala, Chanel akamchukua mtoto akamkabishi kwa Pedeshee.
Marion unamwona mtoto wetu alivyo mzuri kama Baba yake, very handsome.
Pedeshee: anafurahi anacheka huku machozi yanamtoka, anambusu mtoto mzuuri, ila anaonekana anaanza kupungua lakini hakujali.Wakakaa wanaongea baadae akamrudisha mtoto kulala.
Chanel: akamwinua Pedeshee ili akamwogeshe, kweli ajira mara 2, kumwinua Pedeshee ni fresh kwenda kuoga ni mbinde, akamwekea stuli awe anamwogesha akiwa amekaa, kweli Chanel kakua, sio kwa maraha yale alokuwa anayapata Pedeshee. Walipomaliza akamwinua akamkausha na taulo, akamuweka kitandani ili achukue nguo amvalishe!
Pedeshee kama kawa bingwa akamdaka Chanel kwa mabusu,Chanel akiangalia mechi ya mguu mmoja anaona kama anamtonesha kidonda akawa anaipiga mechi with care.
Pedeshee hajawahi gusa mwanamke mwengine tangu ameenda kikazi, uzinduzi ulikuwa wa nguvu! Pedeshee kamfunga Chanel goal 3 bila wakalala
Usiku wa manane wakaamsha popo tena, Chanel akachukua ushindi mbili bila, alfajiri saa 12 mechi ya kuanzia siku, Pedeshee kajikakamua kamfunga Chanel goal 3 bila.Chanel akafurahi maana alijua baaàaaaaaass! Anajiambia mbona Marion amekuwa mtamu ghafla? Alafu mechi yake imeenda next level kuliko zamani au kwasababu haja-do muda mrefu?
Kulipokucha wakaondoka Shawn Adrienne na Doreen kwenda kwenye msiba wa James.
Watu kibao wanaagwa kishujaa, Lucifer akawa anajificha asionwe na Doreen, Doreen yupo buzy anaangalia msiba, wakati wa kuaga Doreen akaenda kuweka ua huku analia, Lucifer anamwangalia anatamani awe super man apae akamdake mkewe lakini ndio kazi hawezi.
Baada ya mazishi Adrienne na Doreen wakaondoka wamekumbatiana Doreen analia Shawn akabakia.
Lucifer: akatamani arudi nyumbani lakini wapi.
Shawn: umemwona mke wako?!
Lucifer: Nimemwona anazidi kuwa mzuri namshukuru Mungu miezi 10 hii amenitunzia, yupo mzuri zaidi ya nilivyomuacha, nimemwona na shem nae noumer sana, hongera bwana best!
Shawn: anacheka asante Boss wangu haoo wakaendelea na kazi.
                            
HUKO ULAYA:
Bibie Zungu wakatua Switzerlamd, pazurije!
Walipofika hotelini mechi ikaanza, CHRIS alimkamua Carrie mpaka si unajua mechi ya nyumbani lazima ukomae upate ushindi!? Ukiwa ugenini kamba za mguuni nyingi nini, woga woga flani wa kiboya, ila Carrie alinyooshwa sio kitoto, alihisi papuchi inatoka!
Baadae wakatoka hotelini akampeleka nyumbani kwake, doh! Hilo Jumba sasa kama white house ya Marekani?!
Carrie: Samahani unaishi na nani?!
Chris: Nipo mwenyewe, nilikuwa naishi na mdogo wangu wa kiume lakini nae kapata kwake, sasa nimebaki mwenyewe.
Jumba kama Mbingu bwana nzuuuri!
Carrie: anatoa macho huku anazunguka chumba hadi chumba mchaga anahesabu kila kitu, kweli mchaga ni noumer!
Akapelekwa chumba cha Chris ambacho watakuwa wanalala huko, yeeewooooniii ni kufuruu!
Ile bedroom utadhani Presidential Suite ya 7 star Hotel!
Carrie: huyu Chris usikute alikuwa anatuibia mbona nyumba nzuri namna hii…baadae ya mshangao mrefu Carrie akaenda kuoga, Chris akamfuata huko huko wakapeana mambo, walipotoka Chris akamwinua Carre kambeba mpaka kitandani.
Carrie: we Chris umemeza Viagra nini?! Mbona mechi kila saa?
Chris: akacheka!ni kwamba u-turn me on kila nikikuangalia naishia kujaa! 
                              MAHAKAMANI:
Ikaisha wiki ya 1 na ya 2 ikaingia …Kesi ya Safaree na Petero ikawadia wakapandishwa kizimbani!
Wote wawili wakasomewa mashtaka. Adrienne, Shawn, Pedeshee na Chanel lakini Doreen hakwenda, mjomba wa Safaree nae alikuwepo.
Lucifer kama hawa anajifiiicha hataki kuonekana.
Kesi ikasomwa, washtakiwa kama kawaida yao wakakataa hawayatambui yale mashutumu.
Wakaitwa mashahidi, sema sema na wewe, Safaree anashangaa leo Stan nanisaliti?! Kweli sio mchezo, haya wakaja na wengine na Boss Mzee wakaongea yao na akina Pedeshee na vidhibiti vikaonyeshwa.
Safaree na Peteroo nao wakaambiwa wajitetee wakaongea yao lakini hamna wa kuwatetea ni wao tu.
Ikafuata kipindi cha Break ya nusu saa.
Baada ya nusu saa kuisha ukafika wakati wa Hukumu kutolewa, watuhumiwa wakasimama huku wanasomewa hukumu.
                                         NO 1:
Peteroo: unatuhumiwa kuua kwa kukusudia, ulilipua familia ya George pale Bondeni, utafungwa kifungo cha maisha bila dhamana na kasha kunyongwa!
Tobaaaaa Peteroo aliliiaaa anapiga makelele anaomba asamehewe anajidai anafamilia, lakini akakataliwa!
Chanel na Adrienne wanafurahia haki ya Carrie, Marehemu George na watoto wake imepatikana.
                                        NO 2:
Safaree: unatuhumiwa kwa kuwa jambazi sugu wa kimataifa ukishirikiana na Taicoon KARAKACHA ambae ameshahukumiwa Nchi Urusi, wewe kama supplier mkubwa hapa nchini na kuendesha genge la ujambazi
Unahukumiwa kifungo cha Maisha bila dhamana na mwisho kunyongwa!
Uncle: tobaa jamani Stanslaus umefanya nini sasa mwanangu?
Watu wanamshangaa mzee analia.
Uncle: jamani mwanangu nani atanisaidia na uzee huu, Stanslaus nitaenda wapi mimi, ikabdi walinzi wamtoe nje Uncle akiwa analia.
Kesi ikaisha Jaji akagonga meza yake mara 3 akasimama akaondoka, akina Peterooo ndani, Safaree akageuka nyuma akamuangalia Shawn hayupo akamwona Adrienne akaamwangalia kwa hasira kweli kweli. Wakaondoka kuelekea Segereea!
Chanel: akamkumbatia Adrienne hongera sana, maisha yako Mungu ameshakutetea wewe na Carrie hamtamwona tena Safaree wala Peteroo.
Wakaondoka wote kurudi nyumbani
                        
HUKO JELA:Safaree na Peteroo wakaingia Segerea, wakaingizwa Celo kila mtu na kwake.
Usiku baada ya msosi wakati Safaree amejilaza kitandani mara anaona tatoo zake zooote zinawaka taa nyekundu, akajua hapa naondoka kudadeki mganga ameniita hapa Bagamoyo!
Kumbe hamna cha kunyakuliwa wala nini, mganga huyoo katia timu ndani ya Celo la Safaree!


TUONANE LEO J2 SAA 1 JIONI YA TANZANIA.  
__________________________________

F. ASALI YA WOKOVU NA KUWEKWA HURU
Mganga ndani ya Segerea. Akajidharau sasa alipoona mganga kaja.
Mganga: akamsalimia mbele yake akamwambia nilikwambia safari zako 3 hukunielewa.
Safaree: nilitaka kuja lakini ulinikataza mpaka uniite.
Mganga: hata nikikutoa itabidi ukae na mimi nikufundishe uwe mchawi kama unataka kesho nije kukuchukua tuhame makazi. Ila kwangu ni pagumu ikikosea masharti utajikuta humu humu ndani.
Safaree: Hamna neno nitakuja tu mganga!
Mganga: akaondoka zake
Safaree: akajua kesho atapata freedom yake akawa anatembea kitemi jela, ma taicoon wanamwangalia anawaambia mimi kesho asubuhi hamnikuti wala nini; wenzake wanamcheka.

Siku hio hio walioamka akapita Mchugaji jela, anahubiri, watu kimya Safaree anamwambia Peteroo watu wengine Bwana kazi za kubipu hizi wanatafuta Kiki kwa Sir God wakifika watelezee Mbinguni wakati ndio walaji wakubwa wakina Mama, wajane na madada ya Kanisani hapa mjini hawana lolote; embu waone walivyojaa maupwiru Yesu Yesu! Yesu kitu gani, wamevaa mwamvuli wa Yesu hawana lolote, wakaendelea kusikiliza injili, baadae maombi yakaanza Safaree na wenzie wanaona anavyoombea watu wanaanguka na kutetemeka kama wamenaswa na umeme.

Uuuwi anashangaa si unajua tena Safaree anapenda mambo ya ndumba sasa mambo ya kuangusha watu yakampa mshangao kidogo, anataka kujua Pastor ana nini nae apewe mgao wa kuangusha watu maana sio kwa kuonewa kule na Mataikuni akiwa Jela, Safaree alikuwa na hasira kugeuzwa Bibi ya Taicoon!

Maombi ombi na wewe Petero kushikwa mkono na Pastor akaanguka chiniii.
Safaree: anacheka oya Peteroo acha usanii bwana, amka nini mnampa bichwa huyu jinga.
Peteroo hakuamka wala nini. Safaree akajua Pastor kaua sasa anafungwa aje amfundishe maujanja ya Superman kurusha watu akiwashika.

Mara Peteroo akaamka baada ya Pastor kuomba sana.
Safaree: akanyoosha mikono juu anasema roja mila umerudi, karibu Duniani bwana.
Pastor akamwuliza Safaree, wewe ni nani?
Safaree: Naitwa Safaree vepee kwani?!
Pastor: akataka kumshika mkono
Safaree: akamkimbia
Pastor: akamfuata Safaree akakimbia, akatokea Taicoon na watu wake wakamkamata Safaree wanamwambia huyu hapa mwizi wako Pastor, njoo umrushe huku wanacheka.
Pastor akaja akamwekea mikono Safaree akaanguka chini akaendelea kumwombea baadae akazinduka.
Pastor: akaongea nae anamwuliza haya matatoo sio mazuri, yana uhusiano na mchawi na leo usiku anakuja kukutorosha, nimekuombea Mungu asikudhuru kabisaa na hauta toroka, yeye akija atashindwa hata kukushika atakuwa anakuona kama unang'ara atashindwa kukukaribia.
Nakupa dawa akija mwambia Ushindwe kwa jina la Yesu rudi kuzimu nakuchoma kwa moto wa Roho Mtakatifu.
Safaree: anashangaa! Anawaza kimoyomoyo kwahiyo mimi leo siondoki jela? Kweli huyu Pastor nuksi sana!
Pastor: kesho narudi, uje unipe ushuhuda.
Safaree: akamwangalia anatamani kumpiga anashindwa!
Pastor: akafunga ibada huyoo akasepa.
Usiku Mganga akatia timu kama kawaida kufika heeee! Anaona hawezi kumshika Safaree, akajaribu mandumba yooote lakini wapi akamwuliza Safaree umefanya nini!? Umeenda kwa watu wa Nuru na huyo jamaa namwona hata sasa anakuombea anang'aa sana, amekuambukiza mauchawi yake.
Akajaribu kumchukua ndio Safaree anakumbuka dawa ya Pastor akaanza kuongea Ushindwe kwa jina la Yesu!
Mganga kaanguka chini kwa bonge la kishindo wenzake wakaamka.
Safaree: nakuchoma kwa Moto wa Roho Mtakatifu! mganga anapiga mikelele kama anazaa.
Safaree: toka kwa jina la Yesu,
Mganga: huyoo akatoweka.
Safaree: akasema hii dozi kali pakuche, Pasta aje niongee nae ushuhuda anipe tena maujanja ya kupambana na huyu Tycoon wa Jela anaenionea.

Kesho yake Pastor hakuja Safaree akamind kinyama, keshokutwa Pastor akaja bwana… ikabidi wasubiri muda wa maombezi na mahubiri Safaree anaona yanachelewa. Ibada ilipoisha akamfuata Pastor akampa ubuyu wote, akamwambia nataka hayo manpower na mimi nikomeshe waone wivu
Pastor: akacheka kha! SAFAREE hizi nguvu za Mungu lazima zitoke kwa Mungu sio kwangu. Akapigwa Injili hapo weeee Injili ikakolea kama maji ya kunywa rohoni mwa Safaree.
Pastor: akamfundisha safaree kusoma Biblia na kuomba Usiku.
Basi kila siku Safaree anaomba mwenyewe na kusoma Neno, muda ukapita akaanza kubadilika. Tycoon akija kuchukua mrejesho wa mechi ya Sodoma kwa Safaree, Safare anamkemea ushindwe kwa jina la Yesu na Ulegee, anaanguka chini anakosa nguvu, wakija wenzie kumshika anawakemea wanaanguka chini pwaaaah!
Safaree: doh! maujanja ya Pastor bwana sio mchezo, akaanza na yeye kuwa komandoo wa Jela na msaidizi wake Peteroo.
Siku Pastor kaja akampa ushuhuda, Pastor akafurahi akamwambia hizi nguvu usitumie vibaya kazana kusoma Neno la Mungu na Maombi, uwe unafunga pia, basi Safaree na Peteroo wanafuata mawaidha ya Pastor.

Siku Pastor hayupo, akina Safaree na Peteroo wakahubiri, akina Tycoon woote kimya wanawasikiliza wanashangaa hawa Paulo na Sila wametokea wapi tena?!
Juzi juzi wamekuja hapa mara ghafla wameshakuwa watemi, kila wakijitahidi kuwaumiza hawawezi mwisho wa siku wakawatungia majina Pastor Safaree na Pastor Peteroo.
Mwisho wa siku wakawa marafiki na Tycoons wa Jela, wanakula pamoja hamna tena michezo ya Mombasa, wanamtumikia Mungu wote wakaokoka kule Jela.
Yule Mchungaji aliekuwa anakuja jela kuwaombea hakutokea tena baada ya miezi 2 wakasikia yule Pastor aligongwa na gari akafa maskini!
Ah safaree na peteroo waliumia sio kitoto, lakini ndio wameachiwa kijiti; wakajiambia atapata thawabu kubwa kwa Mungu huyu Mchungaji aliekufa.

Shawn, mjomba na Adrienne wakaja kumtembelea Safaree, wakamwulizia wakaambiwa anaitwa Pastor Safaree sio Safaree tena wanashangaa.

Safaree akaja, wakamsalimia wanamwonea huruma, Adrienne hataki hata kumwangalia Pastor Safaree akamwomba sana Adrienne msamaha akamwambia Shawn nilimpenda sana mke wako kabla haujaja kwenye maisha yake lakini sasa sikujua itakuja kuwa hivi kisasi na hasira viliniponza sasa nashukuru Mungu amewaleta hapa niwaombe msamaha, naomba mnisamehe akapiga magoti huku analia.
Shawn na Adrienne wanashangaa.
Adrienne akainuka akamwinua Safaree akamwambia nimekusamehe wala usiwe na wasiwasi, kila mwenzi tutakuwa tunakuja kukuona kama familia na watoto wetu, Safaree akafurahi sana, wakaongea kwa muda wakasepa

Kwa Lucifer nako kumenoga. Ripoti ishapelekwa kwa Muhusika kuhusu ile mishen alioifanya, akapongezwa na kusifiwa!
Boss Mzee: sasa ni wakati wa kukupeleke kwa familia yako.
Lucifer: akakataa, hataki hata kwenda akamwomba yule boss wake azidi kukaa kwake kwa mwezi m1 tena, akampa Cheni iliokuwa ameivaa akamwambia nakuomba umpatie Doreen atajua cha kufanya akikuuliza mume wangu yupo wapi mwambie tu am sorry, uondoke usimwambie kama nipo hai au nimekufa.

Boss mzee akakubali, akaenda kwa Doreen.
Kufika akina Shawn hawapo wala Pedeshee. Akamkuta Doreen na Mama mkwe na dada wa kazi yule mama mzee. Wakasalimiana na kuongea kwa muda, alipokaribia kuondoka Doreen akashangaa mbona hamwongelei Lucifer akamwuulizia Lucifer yupo wapi?!
Boss Mzee: akaitoa ile Cheni akamwampatia.

Doreen kuiona Cheni roho ikamuua sana, akaanza kulia anamwambia we baba mume wangu yupo wapi aliniahidi anarudi sasa hii chain imekujaje bila mtu.
Boss mzee: Am sorry Doreen, ngoja niondoke nawahi kikao.
Doreen: akaliaaa kwa nguvu kama yupo leba, mama mkwe akaja kuna nini?
Doreen: Lucifer amekufa jamani ona, wakawa wanambembeleza bembeleza na wewe wapi.
Doreen kawa mbogo hasikii maneno ni kulia na kujitupa.
Boss mzee: akajiambia vijana wangu jamani ni wakatili jamani sasa namna hii kweli?
Alipofika akamwambia sasa Lucifer unakuwa kama Pedeshee unaleta ukatili mpaka kwa familia una akili sawa sawa?!
Lucifer: Kimyaaa!
Boss Mzee: Embu rudi kwa mkeo upesi kwangu staki kukuona.
Lucifer: akachukua kila kilicho chake akamshukuru Boss wake akaaga nduki akaingia hotelini Bagamooyooo! Simu akazima kabisaa hakutaka shida!

Wanarudi Adrienne na wenzake wanamkuta Doreen analia kama chizi, anatupa vitu anapasua Tv, uzuri watoto walikuwa shuleni wote.
Lia lia na wewe mama mkwe akachukua sindano ya usingizi akamchoma huku Shawn na Adrienne wanauliza kulikoni wanaambiwa Lucifer kafa. Wakimwangalia Mama Mkwe halii!
Shawn anajua ramani yote akanyamaza.
Adrienne: akamwuliza mumewe mbona hujatuambia siku zote hizi kama Lucifer amekufa?
Shawn: ah mimi nimemwacha Lucifer mzima tu.
Mama mkwe kusikia kwa Shawn akajua ya kweli akaanza nae kilio, lia lia na wewe, wakaanza kazi ya kumbembeleza lakini wapi.

Switzerland nako mambo supa miezi imepita, Carrie amezoea maisha ya huk,o Mrs Chris to be anatanua mbayaa huko ndani anazunguka na chupi na bra mara kiminj.
Usiku Mume akija anampokea akiwa mtupu na champaine kwenye glass ameiweka mgongoni!
Chris anazichizika sio kwa creativity ile ya Mchaga. Mechi mechi na wewe mechi nyingi zimepigwa kila koda ya nyumba ya Chris na bado hawajaimaliza.

Pedeshee na mkewe wakarudi kwenye nyumba yao ambayo mpangaji alikuwepo ila mkataba ulikuwa umeisha.
Wakahamia na mwanao. Chanel ameshazoea kumpiga mechi Pedeshee mwenye mguu mmoja. Pedeshee akawa hana raha jinsi gani mke wake anateseka akatamani kama angewekewa miguu bandia ila ni ghali na maisha ya ndoa ndio yameanza. Wakaendelea na maisha, Chanel ameitupa namba ya simu asiwasiliane na Mark, hataki tena ujinga maana amejifunza somo lake la kuchepuka kulimfanya mumewe apoteze mguu. 

Pedeshee, Shawn na Lucifer wakaitwa ofisini kwa Boss Mzee kila mtu kwa wakati wake. Alianza kwanza Shawn akapongezwa kwa kazi nzuri akaambiwa anahamishiwa Kikazi Marekani kwa muda wa miaka 10. Akapewa wiki 4 za maandalizi ya kuhama.
Akaja Pedeshee akaapongezwa kwa ujasiri na ushujaa aliouonyesha kutumiakia Taifa akaambiwa anahamishiwa kikazi Ujerumani kwa muda wa miaka 12 na atalipiwa matibabu yote kama atataka mguu wa bandia atalipiwa.
Pedeshee akafurahi sana, akaambiwa mmebakisha wiki 4 muondoke kwahiyo ajiandae na familia yake yote.
Akaingia Lucifer nae mziki ni ule ule akapongezwa baadae akaambiwa nasikia unataka kuoa, haya weee kaoe kwa amani zote.
Ila tumekupenda zaidi itakubidi ubaki hapa hapa mpaka utakapoambiwa vinginevyo.
Kha! Lucifer alifurahi finally anarudi nyumbani kwa mke wake anaenda kuoa.


TUONANE KESHO TAR 4 SEPTEMBA 2018 SAA 10 JIONI YA TANZANIA.  
__________________________________ 

   G. SOME LEMONADE FOR               YOU MADAM



Carrie akapigiwa simu na Adrienne kuwa mambo yameharibika zimebakia wiki 2 Birthday ya Doreen inakuja, plz njoo Bongo bwana tufanye maangamivu maana tunaanza kutawanyika na Doreen kawa chizi sasahivi.
Sasahivi tunamfunga kamba.

Carrie: uuuuwi kwa muda gani?
Akaambiwa miezi 2 sasa, akaambiwa kuwa Lucifer na James wamekufa.
Carrie: tobaaa nakujaaaaa nakuja poleni sana!
Carrie roho inamuuma kwanini rafkiake yamemkuta hayo!
Akamuaga Chris kuwa anarudi Bongo maramoja atarudi mambo yakikaa sawa. Rafkiangu kawa chizi.
Chris: akamwomba amsindikize, Carrie akakataa acha niende mwenyewe nisikusumbue.
Chris: kalazimisha anaona kama Carrie akienda mwenyewe ataibwaaaa.
Carrie: akamweleza jinsi urafiki wao ulivyo, wanapenda kukaa pekeyao na kuongea anaogopa asijejiskia isolated akiomba wakae pekeyao

Chris: akakubali. akabook tiketi ya ndege, haooo Bongo mojaaa.
Adrienne na Shawn wameshachoka hawajui wamfanyaje Doreen,
Adrienne: tumpeleke milembe?
Shawn: hapana, akijua kuwa Lucifer yupo atakuja tu ila lini hajui. Sasa mke wangu nimehamishiwa kikazi Marekani kwa muda wa miaka 10. Na siwezi kukataa maana ni Amri.
Adrienne: akashtuka Mungu wangu, nitafanyaje unaniacha na watoto?
Shawn: tunatakiwa twende wote nimeambiwa nichukue familia yangu yote.
Adrienne: akapumua lakini sijui nafanyaje unajua nimeajiriwa, sijawahi kufikiria kuiacha kazi.

Shawn: Mwombe uhamisho Boss wako, sidhani kama watakataa.
Adrienne: Imebakia muda gani uondoke?

Shawn: Imebakia wiki 1 tu.
Adrienne: wiki 1? Ndio unaniambia sasa hivi?
Shawn: nimetoka kuambiwa jana,
Adrienne: siwezi kupata ruhusa ndani ya wiki 1 unawajua watu wa UN walivyo Shawn hizi kazi za watu kama ilivyo yako, kuomba uhamisho inaweza chukua hata miezi 6!
Shawn: naelewa mpenzi sasa kukueleza imekuwa kosa? Anyway mimi naweza kwenda nikaandaa makao alafu nyie mkaja polepole.
Adrienne: sawa akawa amepata bonge la shock!
 Kesho yake akaenda ofisini akaongea na Boss wake kuhusu uhamisho, Mume wangu amehamishiwa kikazi Marekani na mimi sijui nafanyaje kulea watoto wadogo pekeyangu kwa miaka 10 sioni kama nitaweza.
Boss: Ma cho yanaamtoka, doh pole sana Adrienne, sawa basi ngoja tuone issue yako nitakujibu baada ya wiki 1.
MTAA WA 3:
Pedeshee akamweleza mkewe kuwa anahamishiwa Ujerumani.
Chanel: lini Tunaondoka?
Pedeshee: eh Mama! umepachoka bongo mara hii?
Chanel: ah bwana! tusepe tu... huku anampa hongera nyingi wakawa wanapanga mambo ya Visa, Cheti cha kuzaliwa cha mtoto.

Chanel: akaambiwa kuna birthday ya Doreen wanataka wamfanyie na Carrie ameshakuja. Tutaifanya nyumbani kwake weekend hii tukiwa sisi tu bila waume zetu na watoto kwaiyo ajiandae.

Chanel akafurahi lakini hakuelewa birthday ya chizi itafanyikaje!
MTAA WA 4:
Lucifer kila akitaka kurudi roho yake inasita, Shawn akampigia simu Don weekend kuna Birthday ya Baby Mama wako, je utakuja kwa kumfanyia surprise au?!
Lucifer: sitakuwepo naenda Kenya kikazi kwa mwaka mmoja.
Shawn: akachoka! kweli Lucifer ni level nyingine ya matatizo, akamuaga akakata simu.
MTAA WA 5:
Carrie na Chris ndani ya Bongo, wakafikia Hyatt Regency Hotel, mechi kama kawa mechi ya nyumbani ushindi anachukua Carrie!
Mzungu hoi.
Chris: nataka nikatoe mahari kwenu, naomba unipeleke kwa wazazi wako.
Carrie: macho yanamtoka kweli zali la mentali! akamjibu ngoja nikamwone Doreen kwanza alafu tutaenda maana weekend kuna Birthday ya Doreen.
Chris: Naomba twende wote kwa Doreen!
Mzungu noumer! anamganda mchaga wa watu anakaba mpaka penati!

Kufika kwa Doreen, Carrie akaanza kulia baada ya kumwona Doreen nauliza hali hii kweli amekuwa chizi Doreen imekuwaje mbona ameharibika namna hii?
Doreen: alipomwona Carrie akainuka kumkumbatia kama sio chizi anamwambia nimekumiss rafkiangu umepotea sana pole na matatizo.
Kabla Carrie hajajibu anamwuliza huyu nani?

Carrie: Anaitwa Chris anaishi Switzerland Geneva, akamshika mkono akamwambia ni Mume wangu mtarajiwa, ameshanivisha Pete hii hapa!

Doreen: akaiangalia pete nzuri kuliko yake, anashangaa doh Carrie maana hakutegemea! Akamsalimia Chris kama mtu wa kawaida ambae sio chizi.
Wakaongea sana, Chris anashangaa chizi gani huyu mbona yupo Normal au dawa zinamfanya azidi kuwa chizi wanampa dawa mbaya?!

Wakaongea sana mambo mengi na Mahari ambayo Chris anataka kwenda kumlipia Carrie Moshi kabla hawajarudi Geneva!
Stori na stori basi Carrie alipotaja tu Lucifer akawa kama ameharibu.
Doreen: Kichaa kikaanza
Carrie: akajuta kwanini alimtaja Lucifer sio kwa ile mikekele iliotoka,
Chris akaziba maskio Kha! Mbona majanga!
Wakaamua kuondoka na Chris wamemwacha Doreen ameshikwa na ma body guard anatulizwa.
Njiani Chris amekosa hata pozi la kumwuliza Carrie anamwambia i feel sorry for your friend Doreen ila atapona tu usiwe na wasiwasi.
Carrie: akaitikia lakini hakuelewa lile tukio, akahisi labda Doreen anajifanya!

 


Kesho asubuhi yake Carrie na Bwana wake Chris wakaamsha kuelekea Kilimanjaro Machame.

Wazazi wa Carrie wakavamiwa, walipoambiwa anataka kuolewa wakachoka!
Mama Carrie: wewe mtoto! hata mwaka haujaisha unataka kuolewa? Kivipi? Mbona msiba umeupeleka kijeshi sana?!

Carrie: Mama, we only live once! hata George asingependa kuniona nalia kila siku, ninaamini Chris ameletwa na Mungu, na ni furaha yangu wakati wa mateso.

Basi wazazi wakakosa cha kufanya wakaamua kupokea mahari, wakauliza harusi lini wakaambiwa watajulishwa. 

Wakaishi Moshi siku 3 Baba wa Carrie anamfundisha Chris kunywa Mbege, Kwenda Buchani na kununua nyama, kukata ndizi na kukatia migomba ng'ombe na mbuzi.
Chris mwenyewe ana enjoy si unajua wazungu wanapenda kujifunza vitu vipya kila siku anaona raha kweli.
Mkwe akapendwa ghafla, wakapata amani na mkwewe, maana hajibakizi anajitoa mazima mazima, usiku anawanunulia pombe wanakunywa.

                       SIKU YA MAHARI:
Siku ya mahari alishusha kreti 100 za Bia, ng'ombe wa 4 mbuzi wa 5, Mbege debe 20, Soda Kreti 30, iyo ilikuwa tofauti na mahari aliolipia.
Wanakijiji wakaalikwa wooote mpaka mwenye kiti na katibu kata na familia zao.
Kweli Carrie ana nyota kali, kafiwa juzi mara hii kaopoa zigo kubwa zaidi ya awali. Bonge la sherehe likafanyika, wakaamua kuongeza siku 2 kurudi Dar kwa ajili ya Birthday ya Doreen.
                            
                 HAPPY BIRTHDAY DOREEN:
Ilipofikia sherehe ya siku ya Kuzaliwa Doreen, wakamuandaa mapema, wakamvalisha nguo zake vizuri kapendeza mwenyewe Doreen, wakaamua kuhamishia Sherehe nje ya nyumba yao kwenye Gardeg karibu na Bahari!
Carrie, Adrienne na Chanel wanamwangalia Doreen amelalia hammock.
Carrie:Butler embu mpelekee Juice ya Limao huyu kichaa wenu maana sijui hii sherehe inafanyikaje sasa!
Butler akakubalia akaondoka na juice ya Doreen mpaka alipokuwa amelala, akamsalimia, akaweka meza na Glass na Chupa ya Juice ya Limao! Akawa anamwangalia Doreen aliegeukia upande mwingine, anatamani kumsemesha anashindwa!

“Butler: Some Lemonade for you Madame,
Doreen:akamwangalia Butler,
Butler akajua anapigwa muda sio muda akawa anajiadhari na magumi ya Doreen!
Doreen: No i Don't want”.
Butler: akaondoka akaacha kila kitu pale mezani!

Carrie: anamwangalia Doreen akawaambia akina Chanel jaman mimi e nameona Doreen anadeka tu hata haumwi, huyu anajifanya!
Kwanini mnamlea lea huyu? Mpaka kawa hivi , embu ngioja we Butler hii Birthday itafanyika hapo nje, kila kitu leta nje, embu twendeni nje kukaa nae tukikaa ndani haisaidii.

Wakatoka nje, wakawa wanamwangalia wakiwa wamesimama, wanamsikia anataja jina la Pilot huku anacheza blues.
Carrie: akauliza huyu pilot ndio nani sasa?!

Adrienne: Labda anamaanisha Lucifer, zamani  alikuwa pilot wake kwenye mechi!

Wote wakacheka sio kwa utani ule aliotoa Adrienne.

Carrie: Siamini tumempoteza rafkietu kwenye insane department (Uchizi).  Na yupo wapi huyu binti yake Sandra alisema ameenda kuleta keki!

Doreen: anaendelea kucheza blues huku anaelekea baharini.
Wenzake wanachoka! Ma Body Guard wakaenda kumkamata na kumrudisha walipo akina Carrie wakamkalisha chini walipokaa wenzake!

Carrie: Huyu Sandra sasa yupo wapi? anatuweka ujue mimi natakiwa kurudi Geneva usiku huu ivoo! Hapa sijapaki sijafanya chochote.

Mara Sandra huyoo akaja amebeba keki nakuja mama zangu samahanini sana nimechelewa. Shikamooni.
Wote: Marahaba Sandra.
Sandra: Akaweka Keki chini walipokaa, akazunguka kumkumbatia mama yake na kumbusu, shikamoo Mama
Doreen: Marahaba my Love!

Wote: wakamuimbia
Happy Birthday to you!
Happy Birthday to you!
Happy Birthday Dear Doreen
Happy Birthday to you!
Huraaaay! Hongera Doreen, Hongera sana, tunakupenda!
Doreen: akawaangalia machozi yanamtoka, akatabasamu, hata mimi nawapenda marafiki zangu wazuri na mwanangu Sandra nakupenda sana.
Akaambiwa apulize mishumaa akapuliza mishumaa aka-make-a-wish baada ya sekunde 30 za wishes akakata keki, akamlisha Sandra alafu akawalisha marafiki zake wote, alafu Sandra akamlisha mama yake.
wakakaa wanaongea wanakula keki na kunywa, wanapiga stori,
Carrie: Nimeshalipiwa mahari Moshi, hakutaka kuwasumbua ilifanyika juzi alivyoenda kwahiyo harusi ni muda wowote kuanzia sasa
Kwahiyo Doreen nataka unisimamie kwenye Harusi yangu sawa? Pamoja na Sandra na Kaka yake! Ujitahidi sasa ubadilike uache mavitu unayoyafanya!
Wote: wakampongeza Carrie, hongera
Doreen: sawa nitakusimamia hamna shida!
Adrienne na Chanel: wakawaeleza kuwa waume zao wamehamishwa kikazi wanasafiri wiki ijayo ina maana na wao watahama nchi
Doreen: anashangaa, jamaan mnaniacha pekeyangu lakini nitakuja kuwatembelea
Wote: wakawa wanamshangaa kumbe Doreen anasikia na anajibu vizuri wakamwangalia Carrie alichosema ni kweli Doreen anajifanya kweli haumwi!
Carrie: akaaga jamani muda umeenda Chris ananisubiri pale ndani kwa muda sasa, ndege inaondoka saa 8 usiku.
Mara akapata simu ya Chris anamwambia nime cancel flight, wewe endelea na sherehe tu. Wakaendelea kupiga stori zote Sandra akaingia ndani kwenda kukaa na Chris na Shawn.

Adrienne: Eh! Nimesahau kuwaambia, nina good news nimepata uhamisho kwenda Marekani kikazi, nimefurahije finally naenda kuungana na Mume wangu!

Wote: wakashangaa eh una bahati ndani ya wiki 1 umeshapata uhamisho? wakampigia makofi.

Doreen:Hongera rafkiangu, am happy for you unaondoka lini?

Adrienne: Baada ya week 3 ila Shawn atatangulia.
Doreen: akaona anabaki pekeyake akampongeza na Chanel      
                                 NYUMA YA PAZIA:
Wakati Birthday inaendelea, gari ikaingia akashuka kwenye gari Lucifer na Pedeshee

Lucifer: Finally nimefika nyumbani salama, akawa ananusa harufu ya nyumbani kwake huku anatabasamu!

Mama yake alipomwona alipiga makelele akidhania ni mzuka.
Lucifer: Mama shhhh huku anamkumbatia, hapana mama sijafa ni mimi mwanao Lucifer! Tafadhali usipige kelele nataka kumfanyia surprise mke wangu nasikia ana Birthday leo.

Sandra: akamwona Baba yake, akamrukia daddy daddy! Umeruuudi! Akamkumbatia huku anambusu kwnye mashavu!
Lucifer: akambusu mwanae, Sandra Shhhh! Mama yupo wapi?

Sandra: amekaa nje na akina Aunty wote
Lucifer: ahahahaha, sasa usipige kelele plz nataka kwenda kumfanyia surprise mama yako usiimwambie sawa.
Sandra: OK Daddy!
Lucifer: Kaka yako yupo wapi?
Sandra: yupo chumbani anafanya homework!
Lucifer: sasa wewe kaa hapa na bibi nataka kwenda kuongea na mama yako. akachungulia nje akamwona Doreen amekaa kwenye kitambaa na wenzake Helpless! Anaonekana ana maumivu mengi moyoni mpaka inaonyesha usoni amekoooonda dah akajilaumu kwanini hakuja mapema.
Akatoka nje kuelekea Doreen alipo.

Doreen: kumwona hakuamini akafikicha macho!
Lucifer?! Lucifer is that you?

Wote: wakageuka, kuangalia kweli, ni Lucifeeer!



TUONANE LEO SAA 1 USIKU YA TANZANIA, KUONA MWISHO WA HADITHI HII YA LIMAO NA ASALI...
JE HATIMA YA DOREEN NA WENZAKE NI IPI? 
__________________________________ 

     H. MWISHO WA MAMBO                           YOTE


Doreen akasimama akaelekea alipo Lucifer, kumkaribia tobaaa kweli ni yeye!
Doreen akamkimbilia akamrukia, imagine anamrukia na lile zigooooooooooo!

Lucifer: akambeba na kuanza kumbusu!
Sandra na Kakake wanachungulia dirishani wanacheka.
Mama mkwe wa Doreen: anamziba na macho eti anaona aibu hehe!
Shawn, Chris na Pedeshee: wanawaangalia wanacheka, walipoona watoto wanaangalia na kuwacheka wakawabeba juu juu wanawatekenya na kuwachokoza wakaondoka dirishani.
Carrie, Adrienne na Chanel: wanafurahi finally uchizi unamuisha Doreen, wakaangaliana wakacheka, wakaamua kuwapisha wakaingia ndani wamewaacha wanapeana raha!

Mama Yake Lucifer: akafunga milango, akaacha mmoja wa kuingilia, akafunga mapazia, akazima na taa za nje walipo akina Lucifer, Ma Body Guard ajira ya kumlinda Doreen imeishaisha, wakaingia ndani!

Doreen: anampapasa kila kona ya mwili wa Lucifer mpaka vidole anamchunguza shingo huku machozi yanamtoka!
kweli ndio yeye, akampapasa na Dyu Dyu ndio yenyewe!
Lucifer: anacheka!
Doreen: kila saa anafikicha macho aone kama anamuona au anaota.
Lucifer: ndio mimi mpenzi nimerudi nyumbani.
Doreen: akaanza kubadilika akachangamka, uchizi ukapotea ghafla!
Mpenzi wangu niliambiwa umekufa nikachanganyikiwa sana, nikatamani kufa tu na wewe! Sikutaka chochote tena.
Lucifer: I know I know!
Doreen: Umerudi umekuja na uponyaji, Nakupenda sana huku anambusu.
Lucifer: I know I know.
Doreen: You know?!
Lucifer: Ndio najua, na najua kwa kiasi gani umekuwa mwaminifu kwangu miezi yote 11 nilipoondoka!
Doreen: hakutaka kujua kilichompata Lucifer miezi yote 11, alikuwa wapi, kama alikuwa mwaminifu au la, akawa anamwangalia machoni na kumpenda, wakaanza kucheza blues, hamna mziki wapo gizani, taa kubwa ipo kwenye nyumba.

Doreen: Hakutaka maswali anainjoi blues aliobebwa na Lucifer, amefurahi sana

Walipoingia ndani wakakutana na waume zao, kila mtu akaenda kwa mume wake! Wakashikana mikono kila mtu na njia yake.

Mama Lucifer akawachukua watoto wakaenda kujiandaa na chakula na kuoga. Walipomaliza kula akawalaza, akarudi chumbani kwake kuchungulia kwa dirishani haamini kama Yule ni mtoto wake, alifurahi sana wako na mkewake wanacheza.
               HUKO KWA WENGINE:
Carrie na Chris wapo kwenye gari,
Chris: Rafiki yako amefurahi sana ee? Naona amechangamka ghafla.
Carrie: Ndio, maana walimwambia yule Lucifer amekufa kumbe ni uongo!
Am so happy for her, wakafika Coco Beach wakapaki gari.
Hamna cha mihogo wala mishkaki 40, Chris akaanza kumdandia Carrie kwenye gari aliokodi, mechi mechini, tobaaaaaa!
Gari inanesa nesa na hivi usiku na zile kwichi kwichi, uzuri walipaki ule upande wa sinema ya Coco Beach!
Walipomaliza Chris akamwambia kesho nina surprise yako ufike sehemu fulani saa 10 jioni utaiona, mimi nitatangulia!
Carrie: akashangaa okay, lakini si uniambie tu maana naogopa kupata heart attack na hizi surprise!
Chris: Napenda uvae nguo unayoipenda, nzuri!
Carrie akashanga, akajibu sawa!
Chanel na Pedeshee nao walispotiwa hotelini wanakatika mayenu kwa miguu 3, woyoooooooo! Tena bora Mechi ya miguu 3 kuliko 4 maana hio mitatu tu ni hataree, sasa ukiweka wa 4 inakuwa  patashika nguo kuchanika.
Baada ya world cup, wakiwa wanahemea maskio, pua na midomo;
Pedeshee: Kesho nina surprise yako, naomba ukife sehemu fulani saa 10 jioni … mimi nitaondoka asubuhi mapema nitakuja kuchukuliwa na gari ya ofisini ila saa 10 uje mwenyewe utanikuta!
Chanel: oh! Another surprise, jamaan asante sana huku anashangaa!
Adrienne na Shawn nao wakaingia Sea Cliff kufanya uzinduzi, uzinduzi na wewe!
Inaitwa hakuna kulala… baada ya mechi Shawn akafunguka;
Shawn: Kesho nina surprise yako, naomba ufike sehemu…. saa 10 jioni ..,. asubuhi nimeitwa kazini nitakuja kuchukuliwa ila saa kumi jioni ukija utanikuta!
Nataka upendeze uvae moja ya kivazi nachokipenda!
Adrienne: oh! Okay! Huku anacheka! Sawa mpenzi nitakuja!    
                      HUKO KWA WENYEWE:
 
Lucifer na Doreen wakacheza blues weee, baadae Lucifer akafunguka;

Lucifer: Kesho naomba tuonane sehemu …. Saa 10 jioni… asubuhi nitaondoka nimeitwa na Boss kuna kazi naenda kumalizia, lakini uje umevaa nguo nzuri unayoipenda ambayo unahisi nitaipenda! Nimekuandalia surprise ya sisi wawili tu.
Doreen: hapana mimi hata sikuachii, nisije kuambiwa umekufa kweli nilikuwa naota bure!

Lucifer: Niamini tafadhali, akambeba juu juu akampeleka chumbani kwao, ikapigwa mechi moja kali sana na hivi Doreen hajaguswa zaidi ya miezi 10, mpaka buibui walishajenga neti zao!
Anakaribia kuitwa bikra mama mtoto m1…

Lucifer ndio usiseme, maupwiru ya miezi 10 yalimjaa mpaka kichwani … Mechi iliopigwa mpaka watoto waliamka wakadhani ni mwizi, kumbe Mama na Baba wanaliana!
Hawakulala usiku kucha, kuja kushtuka ni alfajiri 

Doreen: akashtuka, eh kumbe nilikuwa naota?! Akainuka kwenda chooni akamkuta Lucifer anaoga akapumua, akamsindikiza na mechi ya kudumu bafuni, akamfunga Lucifer goal 3 bila, akajisemea kimoyo moyo afadhali sioti asante Mungu!
Baada ya mechi Lucifer akawa anavaa haraka haraka, Doreen bado anaoga, akampigia simu Boss Mzee, wakaongea sana Lucifer akamjibu sawa.
Doreen akatoka bafuni Lucifer hayupo akajua atamkuta sebuleni, hapo ni saa 5 asubuhi wakaingia Ivan na Sandra chumbani kwake,

Sandra & Ivan: mommy! Mommy!  tumemwona Daddy anakunywa chai, tukaongea nae akatubusu akasema jioni mje na mommy! kwani kunanini?!
Doreen: Baba yenu yupo wapi?!
Watoto: ameondoka na ma body guard amesema saa 10 twende wote… Mara akaingia mama mkwe anasema ni kweli hata mimi ameniambia nije na nyie kwani kuna nini?
Doreen: akanyamaza, maana aliambiwa aje mwenyewe sasa imekuwa kikundi cha watu wengi!
Mchana wa saa 7 wakaingia Adrienne, Carrie na Chanel kwa Doreen, shouger tumekuja kukusabahi tunataka kujua hali yako kwa sasa maana hali yako ya jana haikuwa hali!
Nahisi jana ulidhania unaota!
Wakashangaa kumkuta Doreen amechangamka, kaponaa anaandaa watoto wale chakula,

Doreen: akacheka, naendelea vizuri, asanteni kwa kuja karibuni chakula!
Wakakaa wakawa wanakula wote.. walipomaliza msosi wakaenda kukaa Library wanaongea!
Doreen: saa 10 Lucifer ameniambia niende mahali flani …. Niende na Mama Mkwe na watoto, anataka kuonana nasi!

Wenzake: Hata sisi tumeambiwa hivyo hivyo! Ndio tumekuja kwako tuzuge basi kama ndio hivyo basi twende wote!
Wakapia mastori Doreen anawahadithia ya jana usiku ambavyo hakulala na jinsi amechoka anatamani alale kidogo, wenzake nao wakafunguka kila mmoja kwa nafasi yake wakabaki wanacheka

Carrie: jamani mimi namshukuru sana Mungu, we are soo Lucky kuwa na hawa waume!
Mungu ametujibu ingawa ni kwa mateso na maumivu Mengi lakini nimeshasahau maumivu nilioyapata kuondokewa na Mume na watoto wote!
Baada ya maongezi ya muda mrefu wakaingia kuvaa kila mmoja na kivazi chake!
Doreen: akatoka amependeza kuliko wote, wakaanza kumsifia na kumtengeneza tengeneza

Watoto nao wakaja na Mama Mkwe… Mara dereva akaja wakaingia kwenye gari haooo wakaondoka kuelekea eneo la tukio.
Kufika kumbe ni White Sands Hotel, wakaingia ndani wakapelekwa kwenye garden!



Wanashangaa kulivyopambwa, maua mazuri, na mziki na watu wamejaaa wamekaa kwenye viti, wanashangaa kumwona Boss wa Lucifer, wanashangaa kumwona Mchungaji ameandaliwa na wanaume wote wapo mbele, Lucifer amepiga suit nyeupe kapendeezaa!

Wakiwa katika kushangaa shangaa akaja mtu mmoja akawachukua watoto, akawapa maua na Ivan akapewa kijiti

Akaja mtu mwingine akawachukua warembo akawaambia hii ni harusi, Doreen hoi heee ya nani anauliza!
Mtu: ya kwako, kwahiyo wataanza akina Carrie alafu Adrienne alafu Chanel ndio utakuja wewe na Baba yako Mzazi!
Doreen: Baba yangu mzazi? Akiwa katika kushangaa Babake kweli akatokea kapendeza bonge la suit, Doreen akaomba kiti akae!

Baba Doreen: najua una maswali mengi imekuwaje na nini, lakini Lucifer alikuja kijijini na wajomba zake na Yule Boss wake wakalipa mahari, wakasema wanataka kukufanyia surprise, tukaletwa Dar, tukawekwa kwenye hii Hotel, ona hata mama yako Yule pale

Doreen: hoi maana taarifa ilikuwa kubwa kwake!

Mara mziki wa kuingia Bi harusi ukapigwa, kaanza kuingia Ivan na Sandra wenyewe wanacheka
Baadae akaingia bibie Carrie, akafuata Adrienne alafu bibie Chanel, akamwamngalia mume wake amekaa mbele kwenye wheel chair anamkonyeza, Chanel akacheka kwa nguvu kila mtu anamwangalia huku anatembea kwenda mbele kusimama na wenzake!

Baadae akaingia Doreen na Baba yake mzazi anamsindikiza,
Mchungaji: nani anaehusika kumtoa binti huyu?
Baba Doreen: akamvuta Mama Doreen wakajibu, sisi tunamtoa Binti yetu kuolewa na Bwana LucifWakaingia pale watoto wa Lucifer B. Kipara!

Doreen: akakabidhiwa kwa Bwana Lucifer amependezaje kafunikwa shela kimtindo cha kikofia amaizing!
Baadae akasogea Chris, akamshika Carrie wakasogea pembeni ya Lucifer na Doreen wakafungishwa Joint Wedding!

Carrie: hakuamini alijua ni harusi ya Doreen na Lucifer tu!
Kumbe wanaume walishapanga matukio mudaa! Shawn ndio mwenye kiti wa harusi zote mbili!

Harusi ilifungwa na Yule Yule Mchungaji aliowaambia kuwa wataolewa, Yule wa Kanisa la Doreen aliewaombea Mkesha wakiwa bado wapo singo (Kama hukusoma soma Part 1 utamwona)!
Doreen: alipomwona akacheka sana hakuamini, anamwuliza Lucifer umempata wapi Mchungaji wangu jamani?!
Lucifer: akacheka!
Baada ya kuhubiri na kila kitu, ukaja muda wa kufungisha ndoa!
Pastor: Akauliza kama kuna pingamizi lolote?
Wote: kimya
Pastor: akaendelea kufungisha ndoa, akawaombea Baraka… alipomaliza akawaambia you may now Kiss them brides!
Doh! Kila mtu utadhani anakunywa Soda, boooonge la kiss utadhani hawajazaa!
Pastor: anajuta kwanini aliwaambia wa kiss.
Ivan na Sandra: wakafunga macho wanaona aibu!
Wazazi wa Carrie, Doreen wanaangaliana wanacheka!
Mama Lucifer: akaangalia chini maskini analia, akaja Boss wa Lucifer akaanza kumbembeleza!

Baada ya kufungiwa ndoa wakaingia ukumbini, kwa ajili ya chakula na kunywa!
Carrie: anashangaa kuwaona wazazi wake hajaelewa saa ngapi wamekuja akamwuliza mumewe Chris!
Chris: walikuja na wazazi wa Doreen, Lucifer alinisaidia!

Kwenye sherehe MC ni  MC Makasi Junior na Bendi yake ….ilipendeza nakwambia double wedding ya nguvu!
Carrie na Doreen wanashangaa hawa watu walipanga lini sherehe kubwa namna hii?! Imagine hata dada na wadogo zake Carrie walikuwepo.
Kabla ya msosi MC akafungua mziki watu wakaingia walichezaaa walicheeezaaa doh mpaka kuwatoa ilikuwa ni shida sijui walikuwa wamepania?!

Baadae wakaenda kula MC na Bendi yake wakawa wanapiga MC anaimba!

Baada ya Msosi, MC akaomba maharusi wafungue kwa Blues!
Wakaweka wimbo wanaoupenda wa I say a little prayer for you…

Ilikuwa raha sana, maharusi wanaimba huku wanacheza na wapenzi wao;
Doreen anafuraha, anamwangalia Lucifer machoni anamwambia siamini, finally tumeoana! Thank You my Love!
Lucifer: I Love you my wife now and forever am yours! I will make you the happiest wife here on earth until the kingdom come!
MC akabadilisha mziki wakaweka mziki wa kuchangamka, ah Chris utamjua sasa anavyoyarudi utadhani kazaliwa Bongo! Anavyourudi huo mziki wa Ngwasuma anakatika watu wanacheka maana hawezi lakini anajitutumuaje maskini ahahahhahaha… wakwe wanacheka mbavu hana!

Kipindi cha Zawadi hakikuwepo, wageni waliacha zawadi nje lakini wazazi walitaka kutoa zawadi zao wakapewa muda wa kuongea!
Kila mzazi akatoa Baraka zake
Wazazi wa Doreen wakatoa zao na kumkaribisha Lucifer ukweni Singida kwa Wanyisanzu!
Mama Lucifer akatoa zake na kumkaribisha Doreen kwake
Wazazi wa Carrie wakatoa Baraka zao za uchagani wakamkaribisha Chris uchagani…
MC akaingilia kati kabla wazazi wa Carrie hawajamaliza kuongea akaweka mziki wa kichana wa otetereee tereee tereeree! Ule mziki mnashikama mikono wote alafu mnarusha mguu! Ahahahhaha wachaga oyeeee, maharusi wakaunga tela wanacheza, akina Adrienne na Chanel na waume zao wakaunga tela wakawa wanacheza!

Baadae MC akaunganisha mziki wa twist, doh wachaga walicheza, Lucifer anapenda twist anaiwezeaje sasa akawa anamfundisha Chris kucheza Twist! Woyoooooooo!

Baadae MC akafunga sherehe na mziki wa Diana King ambao Mabwana harusi waliuchagua wa Say a little Prayer for you

Carrie na Doreen wakakaa kwenye kiti akina Lucifer na Chris wakawa wanawaimbia:

From the moment I wake up
Before I put on my makeup
I say a little prayer for you..
While combing my hair now
And wondering what dress to wear now
I say a little prayer for you...
Doreen na Carrie wakaitikia:Forever, and ever, you'll stay in my heart, and I'll love you
Forever, and ever, we never will part, oh I love you
Together, together, that's how it should be
Living without you
Would only mean heartbreak for me...
Chris:
I run for the bus dear, while riding I think of us dear,

I say a lil prayer for you
Lucifer:
At work I just take time, and all through my coffee break time
I say a lil prayer for you...
WOTE:Forever, and ever, you'll stay in my heart, and I'll love you
Forever, and ever, we never will part, oh I love you
Together, forever, that's how it should be
Living without you
Would only mean heartbreak for me...
LUCIFER:My darling believe me
For me there is no one but you
CHRIS:
Say you love me too...
DOREEN & LUCIFER:Forever, and ever, you'll stay in my heart, and I'll love you
Forever, and ever, we never will part, oh I love you
Together, forever, that's how it should be
Living without you
Would only mean heartbreak for me...

Wakainuka maharusi wakawakumbatia waume zao wakaanza kucheza, ivan na Sandra na watoto wa Adrienne wakainuka na familia zao huku wanaimba na kucheza.
Boss Mzee akaenda kumwinua Mfanyakazi wa Adriene Yule mama mzee wakaenda kucheza mbele, akina Adrienne na Shawn wanashangaa, mh mbona haya makubwa sasa?!

Mama mkwe akaenda kucheza na mtoto wa Chanel, aaah ilikuwa rahaa Doreen alifurahi lakini Lucifer alifurahi zaidi kwa kutimiza ahadi ya ndoa kwa Doreen.

Carrie alifurahi akajiona kama Kim Kardashian hahahahahha… maana sio kwa kuolewa mara 2 kule alafu ndani ya mwaka mmoja wa msiba.

Chris: akafurahi kwa kumpata Carrie wake, Carrie alimchanganya mauno mbayaaa! Akiamini wataenda kuishi maisha yao milele, ndani ya happily ever after.

Baadae maharusi haoo wakaondoka kila mtu na gari lake, nyuma limefungwa makopo na kikaratasi kimeandikwa JUST MARRIED!

Maids na waume zao na watoto zao wakarudi zao makwao, wazazi wakarudi hotelini, Mama Lucifer na wajukuu zake akina Ivan na Sandra wakadondoka kwao..


                   MIAKA 10 BAADAE:1. CARRIE:
Anaishi Geneva Switzerland na mumewe Chris, wana watoto 2, wa kike na kime wana miaka 5 na 7 kwa mwaka 2014.
Afrika kusini alihama na nyumba aliipangisha kila mwezi anapata kodi, hakutaka kuajiriwa tena, wana Mahoteli Matatu Makubwa ambazo zimekuwa ranked as 5stars Hotek
Wazazi wa Carrie walipata neema ya kuishi Geneva kwa miaka 3 sasa sijui ng’ombe na mbuzi wanakatiwa na nani majani?
Mdogo wa Carrie alishamaliza shule akaenda kusomesha Degree na Master Geneva, sasa anafanya kazi Bongo!
2. CHANEL:
Chanel na Pedeshee wanaishi Ujerumani, wana watoto 3, wakiume wawili, wakike mmoja, Baadae Pedeshee aliwekewa mguu bandia .. Ambao ulimsaidia kumpiga Chanel Mechi kama zamani ambavyo hakuwa mlemavu!

3. ADRIENNE:
Adrienne na Shawn wanaishi Marekani, Adrienne alipata transfer kazini ya miaka 10 pia, wana watoto 5 mapacha wakike 2 na wakiume 3, mpaka mwaka 2014 watoto wa kiume wana miaka 5

4. SAFAREE & PETEROO
Safaree anatembelewa na mjomba wake jela, bado ni Mchungaji, ameshakuwa mzee ana miaka 52 sasa, sio mtemi tena jela ila ni Mchungaji wa watemi jela, Peteroo alifariki, aliumwa sana akafa.
5. DOREEN:
Doreen na Lucifer wanaishi Dar es salaam, Oysterbay, wana watoto 5, waliongezeka wakiume 2 na msichana mmoja, wale watoto waliozaliwa mwishoni wana miaka 2 kwa mwaka 2014.
6. BOSS MZEE:
Boss Mzee alimuoa Dada wa kazi wa Adrienne, Yule Mama Mzee kabla Adrienne na wanae hawajaenda Marekani! Ilikuwa harusi ya watu 10 tu… Lucifer na Doreen walikuwepo! Kwa Yule Mama Mzee ilikuwa zali la mentali kwake!
7. MAMA LUCIFER:Mama Mkwe wa Doreen bado anaishi na mwanae Lucifer, nina miaka 80 kwa mwaka huu wa 2014 ndio niliekuletea hadithi hii! 
ASANTE Money Penny kwa kunisumbua kukuhadithia, I hope you will get paid and remember me.

THE END
PART  2 YA HADITHI HII YA SOME LEMONADE FOR YOU ITALETWA KWENU KWA NJIA YA KITABU … 
MAISHA YAO BADO YALIENDELEA NA WATOTO WAO WALIKUA..

UNAWEZA KUTOA FEEDBACK / MAONI / PONGEZI YA HADITHI HII KWA NAMBA YANGU YA WHATSAPP +255621950631

MONEY STARS ATARUDI TENA KWENYE HADITHI YA: MTU CHAKE! USIKOSE


You Might Also Like

0 comments

all rights reserved - OFFICIAL MONEY STARS | Designed by ARACK