A. KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI
Mwaka 2013 dada yangu alitualika kwenye sherehe yake ya kuzaliwa ambayo aliamua kuifanya kwa watoto yatima wa Mbezi ya Kimara wa kituo cha Watoto wetu
Birthday nyingi nilizowahi kuhudhuria hii ilikuwa ya kwanza niliyoiona imefanyika kwa watoto wa Mungu! Sherehe ilikuwa nzuri sana, na watoto walikuwa wazurije, watoto wa kila umri, miaka 2 mpaka miak 18, wakatueleza historia ya kituo jinsi ilivyoanza na mpaka sasa walipofikia, walikuwa na watoto wangapi na walioanza nao wapo wapi, nk wa kadhalika
Tangu siku hio, moyoni mwangu nikasukumwa kuwatumikia watoto hawa, nikaanza kwenda kuwaona kila baada ya miezi 3, ina maana kwa mwaka mara 4... kwa kile kidogo nilicho nacho nakipeleka, sio lazima uwe na viiingi ndio utoe!
Mwaka 2015, nikawashirikisha wafanyakazi wenzangu pale nilipoambiwa nitoe mchango wa maendeleo ya kampuni, moja wapo niliwaomba tuwe tunatoa kwa wahitaji, wakakubaliana nami kwa mwaka tuwe tunaenda kuwatembelea mara 1 kwa kuanzia... siku ya siku kweli tukaenda kuwatembelea nikawapeleka pale pale aliponipeleka dada yangu alipofanyia sherehe yake ya kuzaliwa, Mbezi ya Kimara kituo cha Watoto Wetu... tangu siku hio walipoamua kutoa pale kazini, mambo ya ofisini yalikwenda vizuri, kampuni ilifanya vizuri sana na mpaka leo maisha ya wale watu yalibadilika sana, ingawa nimeavha kazi kwenye ile kampuni ila kuna wengine bado huwa wanaenda kuwatembelea wale watoto wa Mungu, na wengine bado wananiuliza lini utatupeleka Money Penny Jamaani tumepapenda sana
Sikunyingine nikapata tena nafasi ya kumshirikisha rafiki yangu, alikuwa anasema mambo hayaendi kwenye maisha yake na ofisini, nikamshauri tenga sadaka yako kwa ajili ya watoto wa Mungu, alafu utaniambia, kweli akafanya yake tukanunua mahitaji ya watoto tukaenda kuwaona, tangu siku hio mambo yake ya ofisini yanalindwa na Mungu, hapati tena shida, wenzake wengi wamepunguzwa kazini yeye bado yupo, mpaka uwa ananiulizaga lini tena Penny tunaenda kwa wale watoto wetu kuwasalimia?!
Mwaka 2015 huo huo, kutokana na kero zilizokuwa zikisemwa na shule za Kayumba, na watu wengi walikuwa wakizilalamikia nikaongea na Familia yangu tuwa support kwa kuwasomesha watoto 2 kwenye shule za kidhungu, za English Medium, wakakubali, tukawasomesha watoto 2 wa jinsia ya kike na kiume (Gender Balance)
Wale watoto walianza Nursery mpaka kufikia mwaka 2017, mmoja yupo darasa la 1 na mwingine yupo darasa la 2, ingawa walikuwa level moja lakini mmoja alirukishwa kwa sababu alikuwa na akili nyingi sana. wale watoto wa Mungu hawajawahi kufeli darasani, wanashika namba ya 1 tu wakiteleza ni ya 2, wana akili sana
Tangu siku hio Mungu amebadilisha maisha yangu na ya familia yangu! Maisha yangu hayajawahi kuwa kama zamani, sijawahi kupungukiwa namshukuru Mungu ni kwasababu nilijifunza kumtolea na kumtumikia Mungu kwa kidogo nilichokuwa nacho!
Mwakani Mungu akinipa uzima na neema nina hamu na shauku ya kuongeza tena watoto 2 niwasomesha shule za kidhungu!
Napenda sana kumshukuru Dada yangu alienitambulisha kwa watoto hawa wa Mungu, yeye alifanyika njia ya mimi kufanyika baraka kwa watoto hawa! Popote ulipo Dada yangu unayesoma wakala huu Mungu Akubariki, akuzidishie, usipungukiwe, usitindikiwe, akuzaje kwa kipimo cha kujaa, kushukwasukwa na Kushindiliwa mpaka Kumwagika!
Hata wewe mpenzi mmsomaji unaweza kuwa baraka kwa watoto wa Mungu, nafasi bado zipo za wewe kumtolea na kumtumikia Mungu,
Kituo cha Watoto wetu kipo MBEZI YA KIMARA, unaweza kuwapata kwa njia za mawasiliano haya:
SIMU: 0712439124/0713225267/0767225267
WHATSAPP NO: 0712439124
Website yao: http://wwtz.org/about-wwt/
Karibuni Sana, Bado Haujachelewa!
KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI
GIVE & IT WILL COME BACK TO YOU, GOOD MEASURE PRESS DOWN SHAKEN TOGETHER & RUNETH OVER, WHEN YOU GIVE, GIVE TO UNTO THE LORD!
------------------------------ x---------------------