MTU CHAKE...PART 1

  • September 13, 2018
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 2 Comments



_________________________________________________________________________________

                   CAUTION/ TAHADHARI:

MPENZI MSOMAJI USOMAPO HADITHI HII JUA KUWA HII NI HADITHI TU KAMA HADITHI ZINGINE - NI MOJA KATI YA BURUDANI ZILIZOPO DUNIANI

TAFADHALI USICHUKULIE BINAFSI (PERSONAL) 

______________________________________



SEHEMU YA 1


A.PUNDA MWANA PUNDA              


Juzi nilipigiwa simu na shoga yangu Harrieth akaniambia mume wa shoga yetu anamtakaa Kimapenzi…. Yaani awe mchepuko wake ….. amemsumbua miezi 3 sasa na anapanga amkubalie…. Nikamwomba tuonane anieleze vizuri!

Tulipoonana akanieleza kila kitu na kunionyesha sms za bwashemeji wetu… na hela anazomtumiaka kwa tigopesa nikachoka… Kumwuliza kama shoga yetu anajua hili akasema hapana, bimdashi hajui kitu.. ila bwanake anahela mbaya… anatawanya hela kama nini!
Harrieth: sasa wewe unyamaze maana nawe una huruma sana… huyu bwana nataka nimtengenezee show time ya kibabe… juzi nimemwomba anipe hela ya mtaji nifungue biashara milioni 50 akasema sawa.. ila hio sawa ilikuja na Emoji bikao za kimapenzi si unajua mambo ya whatsapp tena?

Ndo hivyo me pale nataka nitengeneze maisha…vp wewe ameshakutaka huyu bwana?

Mimi: hapana hajawahi atanionea wapi?
Harrieth: kwahiyo hajawahi kukutia machoni kabisa?
Mimi: hapana hajawahi!
Harrieth: akaniangalia sana…anyway, ikitokea akakutaka wewe nenda, ila usicheze mechi pekupeku jamaa ni Kipusa wa kumwaga nahisi ana ukimwi… embu ngoja tumwite mkewe tumsikie Madame Boss Leide atakavyokuja na mashauzi!

Tukapanga kumwita shoga yetu kumweleza ukweli kuhusu mumewe akaja pale Best Bite … kapaki Lexus yake akashuka amevaa skin jeans hataree, viatu vya Christian Louboutin, handbag na miwani ya Gucci… Le Madam Boss Leide!

Ulumbi: hey you, akatukumbatia na kutubusu mashavuni (ana mambo yake ya kizungu flani utamtaka)?!
Enhe kuna nini tunafungua Bank au Microfinanceu?

Wote: tukamwangalia kama hatujamsikia

Harrieth alikuwa amejaa sana hasira, hataki hata kuongea .. alikuwa na mipango yake kabambe kamwita Ulumbi kumsoma upepo wake upoje!  nachompendeaga Harrieth hajawahi kuwa mnafiki tangu namfahamu!

Ulumbi akaketi, akaita waiter huku anajipepea joto utadhani hatujakaa kwenye a/c ….mademu wa kibongo na kujiongeza wamekuwa too much… hasa bibie Ulumbi… anyway hili silo lililotuleta hapa ngoja kwanza tuongee na Ulumbi

Ulumbi: Mbona hamuongei unajua nimeacha mume anajiandaa na safiri kwenda London!

Harrieth: London ee!

Ulumbi: yah, anasafiri kikazi leo usiku!

Harrieth: unaenda nae?

Ulumbi: Hapana nimechoka sana, si unajua ndio nimerudi toka Paris… ndege zinachosha sana sitaenda nae… enhe nambieni, kunanini?

Harrieth: unauhakika unataka kujua?

Ulumbi: nataka kujua nini? (Hapo uso umeshambadilika, anawasiwasi)

Harrieth: kuhusu Mu….

Mimi: Nikamstopisha!

Wote: wakanishangaa!

Mimi: Ala! Mtu hata hajanywa kinywaji chake unataka kumbutua we vepe?

Ulumbi: eh nyie mna nini leo au mmelewa kwa mvinyo jumapili hii? Kanisani hamjaenda?

Mimi: Tumeenda na tumemwomba Mungu sana ndio maana tumepata ujasiri wa kukuita!

Ulumbi: haya nimekuja what’s up?

Mara waiter akaleta Juice ya Embe, Ulumbi akaichukua haraka haraka anakunywa! Sisi tunamwangalia!
Ulumbi: kama hamwongei nikimaliza Juice nasepa!

Harrieth: Shogaetu tunakueleza ukichukia haituhusu maana tumechoka!

Wote: Ukweli ni kwamba Mumeo ni Malaya! Kipusa! Tumemchoka!

Ulumbi: Eeeee?!

Harrieth: Anatusumbuaa ….anatutaka Kimapenzi…

Ulumbi: Akacheka kwa nguvu hahahahhahahahhahahahahah! Ahahahahahahhaha

Wateja wa Best Bite: Wote wakageuka wanamwangalia anavyovyocheka kama jini!

Ulumbi: akaendelea kucheka kwa muda

Harrieth: nampa dk 3 asiponyamaza namwagia hilo lijuisi lake usoni!

Ulumbi: akanyamaza baada ya kusikia anamwagiwa juice!

Ulumbi: Enhe! sasa mume wangu mmemkubalia ombi lake?

Wote: Tukashangaa! Tumkubalie? Noooo waaay!
 
Ulumbi: Mhy haya bwana nashukuru

Wote: Unashukuru?

Ulumbi: yah nashukuru kwa kunipenda na Kuniheshimu!

Wote: Kwahiyo haushangai Mumeo anatutaka?

Ulumbi: sio kwamba sishangai, namjuaaa! Ndio tabia yake… ndio maana akawa mume wa Ulumbi! Kwani ameitwa mume wenu?
Huyu ni mume wangu!
Na Mume wangu namjua vizuri sana… Ni Malaya wa kutupwaaa!
Na vile mnamwona pale hana hana hata chembe ya VVU wala UKIMWI labda awe ameupata Jana au leo

Wote: Tukaangaliana kwa mshangao jinsi gani tumezodoka! Huku Ulumbi anakunywa Juice yake kwa raha na kucheka, alipomaliza kunywa juice akaendelea…

Ulumbi: Mume wangu mimi namjua …na ningetamani sana mmoja wenu atembee nae ili nimwulize swali langu!

Wote: Swali gani?

Ulumbi: Mume wangu Yule mmaemuona pale anabonge la Machine, zaidi ya inch 15… huku anakunywa juice!

Harrieth: Jesus Christ akaweka mikono juu

Ulumbi: Yeye na Punda hawachekani!

Wote: tobaaaaa!

Ulumbi: Na najua kwanini anatembea nje!

Wote: Kwanini?

Ulumbi:  Yule akiniudhi namnyimaa unyumbaa!
Sasa yeye anajifanyaga kidume nikimnyima anaenda kupiga nje!....
Akifika huko nje anaumiza watoto wa watu na wake za watu mbayaaa(huku anakunywa juice yake ya Embe)….
Najua wanawake wengi hawawezi kuhenya kwenye ile kambi… wanamkimbia …. Na Mume akikosa pa kupoozeka anakuja kwangu mikono nyuma (Huku anamalizia Juice yake)

….Mimi ndio Kiboko yakeee! Mimi ndio namlizaga.
Hajawahi kutokea Msichana au Mwanamke wa kumliza tangu tumeoana huu mwaka wa 18 sasa ……Maana angepatikana asingekuwa anakuja kwangu mikono nyuma amejaaa!

Ndio mana nasema namjua …acheni atembeze mimi siumii mana mimi ndio saizi yake aliyopewa na Mungu.

Ndio mana nikawauliza nani katembea nae kati yenu ili nijue kama mmeumizwa au nimepata mkali wangu!

Mume akitoka nje ya ndoa (akicheat) siumizi kichwa mana najua ni yeye pekee ninayemwezea na kumtosheleza, I make him feel like a MAN, A REAL MAN

Harrieth: Amen sister!

Ulumbi: akamalizia juice yake akaweka Glass chini, akatoa elfu 20, akaweka mezani! Akatuuliza!
kuna kingine?

Wote: tukatikisa vichwa kwa ishara ya hapana!

Ulumbi: ila hamjachelewa, nendeni mkatoboe vizazi …. siwatishi ila mtanipigia simu!
Alafu hakuna mwanaume muoga kama mume wangu!
Anaogopa kufa utadhani alijiumba, hawezi kutembea nje peku lazima avae viatu!

Ni hayo tu kwa leo… mtanipigia kunijulisha kikao kijacho!

Akainuka akaondoka!

Sisi: tunamshangaa hatummalizi! Doh Ulumbi huyu au?

Harrieth: shenzi kabisa huyu mwanamke anajishaua sana… unajua huyu rafkiako anajishaua sana!
Inch 15 ya wapi bwana anatutisha tu.

Huyu rafkiako anatuletea michezo ya Boarding School michezo ya kutema mate kwenye maji ya kunywa wenzio wasinywe… au kupaka mate kwenye nyama mwenzio asile, ila kwangu hatonipata!

Nina Plan ya kumkomesha Ulumbi… amejaa mashauzi sana, nataka nizinyofoe hela za mumewe mpaka aje aniombe msamaha… ajue kuwa Mungu hakumuumba mwanamke pekeyake!

Inch 15 kitu gani bwana, watu tunazaa watoto kilo 10 na bado tunaishi itakuwa Inch 15? We ngoja tu … London hio naenda kukomeshea!
Embu ngoja!
Akanyanyua simu akampigia Mume wa Ulumbi… akaweka Loud speaker!

Simu ikaita wee ikaita wee ikaita na kuitaaa… haikupokelewa!

Akasubiria kama dk 2 akataka kupiga akapigiwa, kweli aliempigia ni Mume wa Ulumbi.

Mume wa Ulumbi anaitwaga JITU!

JITU: Sema mpenzi
Harrieth: Baby uko wapi nina hamu na wewe

JITU: nipo kwangu, uko wapi?
Harrieth: Nipo Best Bite… nimekuja kutuliza akili lakini hazituliziki

JITU: pole sana mpenzi ngoja nije
Harrieth: karibu
SIMU IKAKATWA!

Harrieth: Sasa skia mami, huyu bwana usiku wa leo naanguka nae London, alishanikatia visa na kila kitu!

Mimi: Tobaaa unasafiri nae tena? We bwana mwongo sana!

Harrieth: Mimi sio mwongo, leo nakuita hotel uje uone visa na toketi!
Hapa nataka nikampe show ya kichokoraaa! Kwa mara ya kwanza nakubali maumivu, nataka nikalione hilo lipunda kabla hatujasafiri! Alafu nilimwomba hela sijui ataniletea… akiniletea nakupigia uje!


Nikamuaga Harrieth maana sitaki shida za waandishi wahabari, akaniomba sana nibakie, ili nisome alama za nyakati!

Mimi nilie na Harrieth naitwa Grace, nimeolewa na Mtoto 1 …ndoa ya miaka 10… Mume wangu anaishi Mkoa mimi naishi Dar.

Najua unajiuliza kwanini mume anaishi mkoa na mimi nipo Dar.. hio ni stori nyingine kwa wakati mwingine… kwa leo tulimalize hili sakata la Harrieth na Mume wa Ulumbi..

Harrieth akapanga na kupangua hapo… Mara JITU akaingia, kaja na uso mkavu kama hajawahi kututaka sisi sote!

UKWELI NI KWAMBA:
Jitu hata mimi alishawahi kunitaka, kuna siku nilienda kwa Ulumbi kumsaidia kumwangalia mwanae, yeye alienda kwenye sherehe na mume alikuwa amesafiri.

Nikiwa buzy nacheza na mwanae, mume akaingia, nikamlaza mwanae nikabakia kumsubiria Ulumbi.

Masaa yanaenda Ulumbi haji mumewe tukawa tunaongea akaanza kunitongoza, akachukua simu yangu akajibipu akasave namba yangu.. kanitongoza siku hio mpaka… uzuri wa JITU bwana hakufosi, anakuandalia mazingira yaw ewe kumfuata mwenyewe!

Sikuwahi kujua habari za hela wala nini, mimi nilimkataa kwasababu ni mume wa rafkiangu, nimeumbiwa haya!

Akanibeba juu juu mpaka chumba cha wageni, akanibwaga kitandani kimahaba zaidi, akaanza kunibusu busu nini kweli nikakolea, lakini alipotoa machine ndio nilikimbiaaaaaaa! Kha! Ile sio machine ni laana! Huyu kaka sijui Mghana au Mnigeria sijawahi kuuliza habari zake sana ila nikimwuliza Ulumbi ananiambia mtu wa Kagera lakini sidhani kama ni raia mwenzetu

Katika kimbia Mara geti likafunguliwa akakimbia chumbani kwake, mimi nikajitengeneza fasta mkewe akaingia akanishukuru nikaondoka!

Tangu sikuhio sijaonana tena na JITU, akawa akinipigia sipokei akituma sms sijibu, akawa ananitumia hela tigo pesa laki 5… mil 1.. mimi nazitoa nakauka, sijawahi kumjibu sms wala kupokea simu

Ndio leo namwona JITU live kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho kwake alipotaka kuniharibu… lakini hii ni siri yangu Mimi Grace mpenzi msomaji, ni siri yangu na Mungu na JITU… Sijawahi kumwambia mtu kabisa kuwa kila week JITU ananitumiaga hela… naanzaje kwanza? Ukila na kipofu usimshike mkono, kama anahela za kumwaga ni yeye hainihusu!

Alipofika pale Best Bite kaja mkavuu ananisalimia kama hanijui!

Harrieth: Babe huyu ni rafkiangu anaitwa Grace!

JITU: Oh! Grace! Nimefurahi kukufahamu akanipa mkono huku ananitekenya katikati ya mkono!

Grace: nashukuru pia… nikajinasua mkono

JITU: eh niwaagizie nini?

Harrieth: Oh! hapana Babe tumekaa sana hapa zaidi ya masaa 2… nanihii ile ishu ya ile nyumba ulioniambia ya Posta Mpya (huku ananikanyaga kiatu- ishara ya kwamba sisi tunadondoka kwa Hotel), nimeshaongea na dalali amesema tukamwone leo na mwenye nyumba ana nafasi leo..
JITU: Sawa hamna shida basi twende!
Akaaga akatoka, Harrieth anamwambia nisubirie kwenye gari nakuja…

Harrieth: Grace embu nipe mipira

Grace: kwani mimi nauza duka la dawa?

Harrieth: we acha mambo za kihuni, unataka nikafe

Grace: Na wewe ni mbishi! Sasa unaenda kwa Punda kufanyaje… utakufa ujue!
Ahahahahhaha

Harrieth: Punda my foot! Lete mipira
Akaninyang’anya pochi akachukua mipira yangu yote… we ngoja niende nikamhakikishe huyo Punda nione kama ni Punda aliempanda Yesu au kuna mwingine!

Grace: Kwani wewe unataka nini hasa kwa JITU? Kama ana ukimwi je?

Harrieth: Ukimwi kama Malaria tu, tunakunywa Dawa tunaishi, kufa kila mtu atakufa, ingekuwa Kansa nisingekanyaga pale maana Kansa ni mwisho wa Ukimwi, Kansa unakufa unajiona Ukimwi unaishi mpaka unachoka!
Nitakupigia jioni usijali … tunaingia Sheraton!
Grace mimi huwa ni mpole sina maneno sana, nikarudi nyumbani kwangu nikalala nimeacha simu kwenye chaji nimeweka vibration… hapo saa 10 jioni!

Nikaamka saa 1 usiku naskia uvivu kwenda kupika njaa inaniuma kweli… nikadondoka jikoni nitafune angalau tunda!
Nimebakia mwenyewe nyumbani mwanangu yupo Likizo nimempeleka kwa Baba yake Mkoa akahangaike nae kumlea!

Nikarudi chumbani nakuta simu inaita, nataka kunyanyua ikakata!
Kuangalia nakuta missed calls 20 zote za Harrieth!
Nikampigia nimsikie Mwana Punda amefika wapi!

Grace: Halo?

Harrieth: Mama nakuomba tafwadhali uje Sheraton!

Grace: vp umefumaniwa nije na maafande wakuokoe?

Harrieth: we acha ujinga njoo… utakuja kula huku na kulala huku ukipenda maana kesho ni sikukuu.

Grace: sawa! nikaondoka kufika Sheraton akaniambia nipande chumbani, kufika nakuta chumba kiko wazi hakijafungwa vizuri nikahisi fumanizi, kuingia naskia A/C kubwaa inawaka Kama Mochwari

Harrieth kuna nini huku mbona a/c kubwa… kusogea namwona Harrieth amelala chini!

Nikakimbia kwenda kumnyanyua, kumwangalia
Harrieth anahema juu juu

Grace: nikainuka kuangalia mazingira kwanza huenda kaporwa, kumbe hamna mtu wala mporaji … ngoja niwapigie reception waje kwanza … nikanyanyua simu nipige Harrieth akanitukana kwa nguvu nikaweka simu chini, nikachukua kiti nikakaa nimsikilize maana kanitukana tusi sio dogo, kaniudhi!

Harrieth: Grace, naomba ukachukue maji moto bafuni unikande?!

Grace: nikukande?

Harrieth: Bwana fanya nachokwambia muda unaenda nasafiri usiku saa 8…
Grace: nikadondoka nikafanya kama alivyotaka, nikamkanda, doh! Mpanda Punda, aliumizwa vibaya mno!

Baada ya kumkanda nusu saa akapata nguvu tukanyanyuana mpaka kitandani akalala….kwenye kumnyanyua ndio naona makaratasi ya Condom yamezagaa, katika okota okota nikahesabu na kukuta zilichanika condom zaidi ya 5 …kweli Mwana Punda kapatikana

Yeye akalala mimi nikaagiza msosi .. baada ya nusu saa Harrieth akaamka nikampa chakula akawa anakula …akafunguka:

Harrieth: Grace! Ulumbi ni msema kweli

Grace: ahahahahhahahahhaha… nikamcheka sana hapo Harrieth kanunaje

Haarieth: unaliona lile begi pale, embu lilete

Grace: nikainuka nikaenda kubeba begi, kufungua ndani kuna hela nyingi sana, kwanza sikuamini!

Harrieth: Hizo hela hizo, nimepewa na JITU leo leo! Zipo Milion 50

Grace: macho yamenitoka! Harrieth umemuua huyu baba au?
Harrieth: naanzaje? nina sura ya kuua? Mxiuuuuu embu acha utoto
Nilikwambia rafkiako Ulumbi ni mjinga hana lolote!
Na nilikwambia naenda London, fungua zipo ya mbele, utaona passport yangu na Jitu zimegongwa British Visa!

Kweli Grace nikafanya kama alivyonielekeza, nilichokaaaa! Macho yananitoka saa ngapi Harrieth amepiga tukio mpaka usiku huu anaanguka kwa Queen?!

Dah nikajiona jingas, nikarudi kuzichungulia zile hela kama ni Mil 50 kweli au la!

Harrieth: kama alikutaka JITU wewe nenda kapige helaaaa mama …. piga helaaa ila ndio ujue kumpanda Punda maumivu yake ndio haya…nimelala chini masaa 3 nakupigia haupokei! a/c imenisaidia mbaya

Grace: macho yananitoka nahesabu hela haziishi! Sasa JITU yupowapi asije akanikuta hapa!

Harrieth: Tulia wewe ameenda kwa mkewe tutakutana Airport! Hapa amelipa mpaka kesho saa 6 mchana wewe utabakia hapa mimi naondoka na gari ya hotel!
Kesho saa 6 urudishe funguo ya watu reception!

Dah, huku anashika tumbo, huyu baba ni zaidi ya Punda kudadeki, ameniumiza balaa na mimi niliingia kichwa kichwa, najua uongo mama! Oh! Jamani acheni huyu mwauame sijui waliumbwa saa wakati Mungu amekasirika au?

Nimejidai nampa mechi ya kichokoraaa, mechi ya kibishi nilikomaaa.. nimejikaza Grace nimejitutumuaaa… nimesali sala zote basi kumkomoa shogako Ulumbi kudadeki huyu Ulumbi ana CHIU au Bahari ya Shamu? Kha!

Grace: nacheka mbavu sina, kweli nikimwangalia Harrieth kaumizwa mbayaa! Yani kaumizwa kweli mpaka nimeenda kuomba first aid kit nikaja kumsafisha na kumpaka dawa!
Akome nae kazidi tamaa ya kudandia magari kwa mbele… na hivi anaenda London atakoma sijui nani atamkanda!

Harrieth: Mume wa Ulumbi wakati ananitongoza, mimi nikawa nalia njaa, njaa njaa kwasababu ya magari anayoendesha Ulumbi mkewe, sasa akawa ananiomba show time kila tukichat nikamwambia show time sitoi bongo kama vipi nipeleke ulaya nitakupa raha mpaka hutanisahau… kweli kaenda kunigongea visa, nikaitwa kujibu maswali, akaunt yangu akawa aningiza hela kila mwezi mil 10 kumi kwa muda wa miezi 6…kila wiki anaweka mil 2.5 Ndio leo kanipa Visa na Tiket za ndege nikaamini nikaona bora nimpe ahadi yake hapa hapa nyumbani lakini kwa maumivu haya nikirudi Bongo nitakuwa sifai!

Huyu mwanaume namwombea asife aishi miaka 100 walaahi, maana sijui kama nitapata habari kama yake tena! Doh! Huku analia maumivu, anameza panadol kama hana akili nzuri, mara diclofenac maumivu heavy mama!

Grace: Umemliza?

Harrieth: Nimemliza shoga, kwanza sikuamini kama analia, maana muda mwingi mimi ndo nalia! Finally akaanza kulia! acheni nilipwe hela nyingi nimemliza vibaya mno, Ulumbi atanitafuta kuchukua kozi kwangu!
  
Grace: hahahahahah mbavu sina na hivi napenda kucheka kweli kicheko kilipata mchekaji!

Harrieth: na nimeshajua udhaifu wake upo wapi! Mbaya zaidi hachoki ndio maana Ulumbi kakondeaaaana maskini… mpaka anaondoka hataki kuondoka!

Grace: nikamaliza kuhesabu hela kweli ni Mil 50 cash! Dah wanawake wengine njaaa…

Harrieth: Mimi nalala, ikifika saa 7 niamshe nianze safari… naona nimepoa poa maumivu sasa!

  
Grace: nikachoka hela ni nyingi sana… huyu baba anafanya wapi kazi mbona anatupa sana hela au free mason? Milion 50 kwa kununua uroda? Dah hapa kuna kitu sio bure!

Saa 7 ilipofika Bindada akaja kuchukuliwa, akaniomba nimsindikize Aiport nitarudi na gari ya hapa, akaniomba sana hizo hela nikae nazo kila week niwe naziweka bank milioni tano tano alafu risiti nimuwekee!

Grace: sinaga makuu nikamkubalia, tukadondoka Aiport kweli namwona JITU kaletwa na taxi pia, nikamuaga Harrieth sikutaka JITU anione, wakaondoka haooo wakaingia ndani ya Airport tayari kwa safari!

Nikarudishwa hotelini na gari ya Hoteli, nikapanda kulala hapo saa 8 kamili usiku, najiambia kweli mtu chake masikini Ulumbi!



ITAENDELEA KESHO TAR 14 SEPTEMBER 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
__________________________________________________________________

B. VYA BURE VINA GHARAMA 

Asubuhi nikashituka, kuamka ni simu inaita, nikaipokea haraka haraka nikidhani kuwa Harrieth karudi!

Kuangalia simu eh ni Shangazi, ananikumbushia kuwa kwake leo kuna sherehe, mjomba amechinja Wanyama anataka kufurahi na watoto wake wote na wajukuu, nikamwambia sawa najiandaa nitoke

Kucheki simu whatsapp hamna cha message ya Harrieth wala nani, hata simu ya Ulumbi haikuwepo!

Nikiangalia saa ni saa 5 asubuhi, nikaoga fasta nirudishe funguo ya watu saa 6 mchana, mara naskia hodi kufungua wameleta breakfast! Doh aibu mtu mzima nikala fasta nikakusanya hela na mikoba yangu nduki mpaka kwangu, njiani roho inanidunda nisije pokonywa maana hela za watu hizi! Nikafika salama nikawahi kuzifungia kwenye safe yangu, jamani Milion 50 sio ya kitoto, oneni tu watu wanaandika kwenye makaratasi lakini ukipewa mkononi unaweza ukafa ukachanganyikiwa!

Nikajiandaa kubadilisha nguo nikaanguka kwa mjomba kwenye sherehe! kufika baada ya kumsalimia Mjomba na shangazi ile nataka kuomba kazi nisafishe chochote au nisaidie chochote nikavutwa mkono na binamu;

Binamu: we jinga kweli Grace embu twende kuna umbea chumbani, hatujaitwa kupika tumeitwa kula na kunywa washapika waliolipwa

Haooo tukadondoka chumbani, doh chumba kikubwa cha binamu yetu wamejaa mabinamu huku utadhani kikao cha harusi cha wachaga!
Baada ya masalimiano na nene! Topiki ikaanza kuzungumzwa, si unajua tena mabinamu tukikutana, mnajazana habari za tangu mlipoachana mpaka leo!

Ila Mabinamu wangu ni wazuri jamani! Yani acha sina mfano wa kukuelezea! Ni Visu Balaaa! Yale matoto ya
Singida balaaa, si mnajua watoto wa Singida walivyoo eee, wako wamgawanyika flani hivi amaizing kama wale katuni wa kwenye magazeti ya SANI, kiuno dondolaaa, Chura Mashaalaah, Mahispi Don’t Lie akajiimbia Shakira!
Rangi zao sasa, wengine weupe ila maji ya kunde ndio wengi, ndio akina sisi!

Hawa ni ndugu zangu upande wa Mama yangu, Mama yangu mzazi ni Mtu wa Singida, Baba ni Mchaga, kwahiyo mimi Grace unaweza niita Halfcast wa Kichaga… ila hao mabinamu zangu ni watu wa Singida Pure … Nikisema Pure namaanisha Baba yao wa Singida na Mama yao wa Singida, okay?
Katika ongea ongea za hapa na pale, kila mtu kafunguka kuanzia tulipochana mpaka leo tumekutana na nini basi Binamu wa miaka 28 akaomba ushauri:
Binamu Miaka 28:
Samahani naomba niwe mkweli nina shida, naombeni mnisaidie kama ndugu yenu wala sijataka kuongea mnifikirie vibaya!
Jaman mimi nina tatizoo, mwenzenu kila nikipata bwana tunaenda vizuri tuuu ila tukifika kwenye michezo ya wakubwa a.k.a Mechi naogopaaaa! Nakimbiaaaa!
Mpaka sasa sijawahi hata kufanya kitu inaitwa Romance hata kukiss sijui! 
Mabinamu Wote:
lahaulaaa! … akyanani… Mukombi wa nene? ….Aiseee… ahahahhahahaha…. Majanga haya… Mungu weee… kwahiyo wewe ni Bikra?... Yeeessuuuu na Maria… Mwehu kabisa… unatuaibisha…. Fcku …stupid girl… shubatra …bitch… oh Lord….Jeesuuus criiipeers…Jinga sana wewe.,… huyu kazaliwa saa ngapi?...
Hapo kila binamu aliongea kwa staili yake mimi nikabakia namshangaa Binamu alivyo mzuri jamani Zari Mke wa Diamond Platnumz atasubiria miaka buku! Alafu anasema ni Bikra?! Hii ni mupyaaa!

Binamu Miaka 28:
Mwanaume akitaka kunibusu nasingizia naumwa meno, anahama anahamia kwingine… ila akishatoa mgobole wake tu dooooh! Nikiliona tu nakimbiaaaa naachaga na viatu hapo hapo!

Mabinamu:
hahahahahahahah, oooooooooooooooooooooooo mamaaa ahahahahahhaha yani walicheka mpaka shangazi akaja kusema punguzeni makelele tafadhali.
Shangazi alipoondoka tukaendelea na mastori!
Grace:  Kwani shida ipo wapi kwa huyu kuwa bikra?
Kayaleta tumsaidie, kama nduguzake mnatakiwa mumsaidie, tujadiliane jinsi ya kumsaidia kumtukana haileti suluhu, hapa ana miaka 28..bado miaka 2 achungulie 30, hana mume, hana mtoto, wenzake wanaolewaaa wanazaaa yeye yupo

Binamu Miaka 28:
Tena napataga wanaume very potential, wealthy, rich, alafu wanakuwaga wakubwa kwangu kuanzia miaka 40 mpaka 45 ila wakisikia mimi bikra wanakimbiaaa!

Binamu Mchafu: Kwanza embu tueleze mwana wewe una bikra ipi labda?!

Binamu Miaka 28: Kwani kuna bikra ngapi si ipo moja tu?
Wote: wakacheka hawana mbavu… uuuwi kazi ipo hapa ndugu hatuna, muhahahahhahahahhahaha

Binamu Mkubwa: My dia Bikra zipo 6, nitafute kwea muda wako nitakutajia!
Binamu Miaka 28: heee?!
Binamu Mkubwa: umebakisha ngapi sasa tujue jinsi ya kukusaidia?
Binamua Miaka 28: Zote zipo!
MABINAMU WOTE: tunakusahuri uzitoe tu angalau toa 1 basi yaishe… ila ukiitoa moja automatically utakuwa umeshazitoa 5 jumla, utakuwa umebakisha moja ya nyuma! toa wewe, acha uboya toaaa.
Binamu Mchafu: kuna mangi mtaa wa 3 nikupe akutoe vzuuri?
Binamu Mkubwa: Mdogo wangu jamani, ujue wanaume watu wazima hawapendi mabikra sikuhizi, wanawasiwasi akishakutoa je utatulia au utamuacha hapo?! Labda akuoe akakutoe, watu wazima sikuhizi wanapenda wale waliotumika, ili wakapige show za kichokoraa na show zingine tofauti na wanazopiga kwa wakezao!
Yani watu wazima wanaona bora akachukue kuberu lililoshindikanaaa mtaani, limepiga round maishani weeeee na mielekaaa yakutosha likachoka maana wanajua Kuberu likiwekwa ndani litatuliaaa kuliko wewe! Wanakuwa na wasiwasi huooo tu mdogowangu! Dah ila bora umelileta tutakusaidia, damu nzito jamani kuliko maji! Lazima tumsaidie wa kwetu asijeakatuletea aibu!

Binamu Mchafu: Kwa kuanzia atafute mwanaume wa maana kuanzia miaka 37-39 amtoe bikra alafu ampige round weeeeee alafu baadae arudi kwa hao watu wazimaaa. Umri niliokutajia kidogo wanauwezo wa kukutunzia siri na kuwa na speed ya kuitoaa … lakini hapo watachukua kwa kukadiria kima cha chini siku 2.. ukiwapata wale wa 41 kuja juu wanaogopaaa maana speed yao ya kutoa malaika imeshapunguaaa, tena bikra ya miaka 28 mama sio mchezo kuimwagaaa, inahitajika mwanaume mwenye nguvu zakee hawa 40+ washachokaaa, goal 1 hoi, case yako anatakiwa bro aliejaaa akiisimamia masaa 3 inatoka yoteee tena ukafungie bagamoyoo maana maumivu yake utapiga yowe Dar es salaam yote tutaskia!
Alafu usikubali kwenda gesti uchwara sijui manzese sijui kariakoo, kariakoo yote watajuaaaa! lakini umri chini ya 35 watakutangazaa utaisoma nambaaa utachukia Mji unaoishi!

Hivi tukuulize kwanini umeamua kukaa na Bikra mpaka umri huu lakini?

Binamu Miaka 28: Nimeokoka Yesu anakataza kuzini kabla ya ndoa!

Binamu Mchafu: huko Kanisani hamna jamaa akuoe sasa?

Binamu Miaka 28: ah siwapendi hawana hela, wavivu na hawana focus ya maisha!

Binamu Mkubwa: ninachompendea Binamu yangu huyu ni mkeli kuliko maelezo sasa wewe vya Mungu unataka vya shetani unataka, Kanisani hamna wanaume wenye hela kusema ukweli na ukimkuta aliepo kila mwanamke anamtaka aolewe nae huku kwa shetani wamejaa kibao ila ndio wanamatatizo mwanzo mwisho!

Binamu Mchafu: Huku kwa shetani mami, huolewi bikra yani ukiolewa bikra una bahati sana, yani wewe Mungu akushukie mwanaume wako awe mwelewa sana msikae kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwezi ndio utaolewe bikra… la sivyo jiandae kubanjuliwa unapigwa puli mama utanyooshwa mieleka miaka nenda rudi, utalia wewe umeumizwa utalia wewe kwa Mungu mpaka uje umpate wa kukupenda atake kukuoa itakuwa kama huna mimba basi bahati yako imefika!
Kwa shetani pagumu ndugu bora ubakigi huko kwa Yesu .. najua hamuamini kubadilisha mwanaume unachoweza kufanya ni kumchukua mtaani na kumpeleka kwa Yesu ila wasanii nao kibao, anaweza kukuaktia akishakuoa anafungua mikucha!

Inabidi uwe mpole ukubali kubaki sehemu mmoja, naona hata Yesu hakupi wa kukuoa kwasababu bado huna maamuzi mazuri, akikupa aliefulia utamkimbia akikupa mwenye hela utakasirika! Anaona bora akuache tu.

Binamu Mpole: Ah mimi nakumbuka Bikra yangu nilitolewa kijijini kule mtoni, Malaika anachomolewa roho inamwagika inadondokea mtoni.. enzi hizo nilienda Arusha kwa shangazi, doh siwezi sahau, ila hongera sana umejitunza yangu ilitoka nikiwa na miaka 16

Binamu Mjeuri: eh 16? Yangu ilitoka miaka 13, kwenye michongoma kijijini, maumivu mara 3, maumivu ya bikira, maumivu ya mchongoma na maumivu ya machine!

Binamu Mchafu: Yangu nilitolewa kwenye holi la ng’ombe!

Wote: wakacheka ahahahhaha uuuwi Yesu alipozaliwa sio?

Binamu Mchafu: yani sikuhio mimi na ng’ombe tulikuwa tunapokezana zamu ya kulia uzuri mvua ilikuwa inanyesha alafu usiku wa manane! Ila bira imetoka, ningeishia kuwa mbululaz kama huyu bibie hapa! Amekaa kama makamasi yupo yupo tu kila siku anaota!

Enhe Grace tuambie yako ulitolewa ulikuwa wapi?

Grace: Mlima Kitonga kule njia ya kwenda Singida?

Wote: ahahahahhahahaha uuuuwi huyu mchawi huyu ahahahahhaha

Grace:  Ajali zilizidi kuwa nyingi nikaamua kwenda kuachilia tambiko pale, nikanyofolewa usiku wa saa 6.. ajali zikakata, so  Bikra yangu imeponyesha wazawa wengi, kweli nakwambia hamnaga ajali za kizembe tena tangu sikuhio mpaka leo

Wote: ahahahahahahahahah, tunaomba umpeleke na huyu bibie akafanye tambiko kwengine kwenye matatizo ahahhahahah

Shangazi akaingia haya twendeni mkale Mchungaji ameshakuja anataka aombee nyumba alafu tuingie kula mnapiga makelele sana, twendeni;

Basi kila mmoja akanyanyuka, mimi nikabakia nasubiria wote watoke, nikaona kama Binamu wa Miaka 28 amekasirika, nikamfuata kuongea nae,

Grace: Nambie mami mbona umekasirika, wala usijali, sasa kwanini unataka kuitoa labda nikiuliza? Unaharakia wapi?

Bikra miaka 28: Grace nimeshakuwa mkubwa sioni hata haja ya kukaa nayo!
Nimemaliza shule, nina Degree, Masters, nipo na kazi yangu nalipwa mil 3 Gross Salary, nina Gari, nina Kiwanja nataka kuanza kujenga, ninachomiss ni Mume na watoto!

Grace: sasa unataka nini? Mume au watoto? Unataka kuzaa kwanza ndio uolewe? Ujue kuna single mothers wengi wanahangaika mtaani.. leo una kazi kesho ukaachishwa kazi utamleaje mtoto? Unataka nini kwenye maisha yako?

Binamu Miaka 28: Napenda niolewe nipate watoto ndani ya ndoa!
Grace: Nikikushauri utanisikiliza au umeshaamua kufanya maamuzi yako? Achana na hawa machokoraa wanaokucheka wanakuonea wivu!
Ni kweli hamna mwanaume wa miaka kuanzia 40 atataka apate bikra, washakuwa na wake zao wakitoka nje wanatafuta pa kupoozea sasa hataki kuja kupooza kwenye mihangaiko tena!
Na kumpata mwanaume ambae hajaoa kuanzia miaka 40 ni wachache sanaaa!

Binamu Miaka 28: Kwahiyo unanishaurije nitakusikiliza, nisaidie Dadangu!

Grace: Kaa ujue mapema kuwa wanaume wote ni washenzi, tena hao watu wazima wako ndio balaa… na wewe umejitunza alafu uje umpate mshenzi best unaweza ukanywa sumu ukafa, nakushauri usitoe bikra yeyote kwanza zaidi ya akili, lazima ubadilishe akili yako kwanza, uache kuwa innocent sana, jifunze uchakaramu wa akali… nataka uwe chakaramu kama machangudoa, wanaume wanaogopaga wanawake machakaramu, ukiwa mchakaramu utajua na kumpata atakaekupenda, na ukimpata usikimbilie kulala nae, atakuumiza… mkazie kwanza mvute vute yani unamkazia mwanzo mwisho, akichoka ndio unajidai unataka kumpa lakini usimpe
Hio nakuachia Home work, ila uchakaramu usiwafanyie watu wazima, wanaume watu wazima kwa sasa wablock! Achana nao we kimbizana na hawa umri wako 30 mpaka 39 hao hao ukifanikiwa hapo niite nitakupa mrejesho!

Jinsi ya kuwa chakaramu:
Soma vitabu vya uchakaramu, angalia movies za kichakaramu lakini sio za ngono huko utachanganyikiwa, sikiliza audio za kichakaramu, plz usivae wala kukaa uchi sijui nini hapana, ila akili ya kuambiwa uchanganye na ya kwako best ila usiitoe kwanza nakushauri, mimi nina uhakika kwenye hao hao marafiki zako yupo kijana anaekupenda ni vile unatanguliza kusema wewe bikra

Basi tukaondoka kwenda kula tukanywa na kufurahi, sherehe ikaisha kila mtu akarudi makwao..

Baada ya wiki tatu nikapata simu ya binamu yangu yule wa miaka 28, akaja nyumbani kwangu, ananiambia amefanya yote niliyomfundisha na amepata bwana

Grace: nikakaa kitako nimjue mjanja anaetaka kumsakramenti mdogowangu ni nani, kupewa picha nikachoka! Kweli shetani ni Yule Yule lakini anatumia njia nyingi kumaliza watu wangu wa nguvu, huwezi amini ile Picha ilikuwa ya JITU!

Ndio, JITU mume wa Ulumbi bwana wa Harrieth!

Grace: wow! Huyu ni nani? (Hapo najifanya simjui)
Binamu Miaka 28: Nimempata juzi nilitoka out nilienda South Beach Kigamboni… nipo na marafiki zangu nakula good time na nini mara nashangaa mtu mrefu anakuja anaomba kuongea na mimi, nikajongea kumsikiliza maneno yale yale anaomba namba yangu, nikamkazia kama ulivyonifundisha, akanilazimisha sana, nikamwambia sawa nikampatia akaniomba twende kutembea ufukweni mwa bahari, akanitongoza mpaka, ananiambia atanibadilishia maisha ana hela sana, mimi nikamsikiliza tu lakini naona kwake akili imeganda!

Grace: akili imegandaje?

Binamu Miaka 28: ananipa attention mbayaa, sijawahi kupewa attention kiasi hiki, anapiga simu kutwa mara 10, hadi aibu ofisini, yani hizi wiki 3 zimekuwa amazing kwangu..

Grace: okay! So ushatembea nae?
Binamu Miaka 28: Hapana ulinikataza!
Grace: Umempenda?
Binamu Miaka 28: mmmh sijui kwakweli ila ameniambia yupo singo
Grace: umeshatoka nae Out tangu muonane Kigamboni?
Binamu Miaka 28: ndio kila siku tunaonana nikitoka kazini ananinunulia dinner, tuna kiss ananihug narudi kwangu, sikuhizi ananifuata asubuhi saa 12 nanusu ananipeleka kazini na kunirudisha usiku home baada ya kutoka kula dinner.. ananipenda ananijali wala hajawahi kunilazimisha kulala nae
Grace: ushamwambia wewe ni Bikira?
Binamu Miaka 28: Never sijawahi kumwambia
Grace: umemfanyia mavurugu kama nilivyokufundisha?
Binamu Miaka 28: Ndio
Grace: na akawa anasemaje ukimfanyia mavurugu?
Binamu Miaka 28: anayapenda mafujo yangu sana tu
Grace: kimoyomoyo nasema tobaaa, huyu mjinga anamlia bisi akimkamata mdogwangu atachukia wanaume milele dah sio kwa lile punda la JITU!

Mdogowangu unajua kuna wanaume wanatembeaga na ukimwi! Nadhani hilo bado sijakufundisha!

Sikiliza mdogowangu, huyu JITU namfahamu vizuri sana, ni mume wa rafiki yangu ana Ukimwi, sasa nakuongezea akili ya ziada, wewe mpige hela zake lakini usionane nae ana kwa ana tenaaa… yani upo steji ya mwisho mwisho kubakwa! Yule anakulia timing ahakikishe umekuwa comfortable nae huogopi kuonekana nae unamwamini kifupi ameshakujengea mazingira ya kujiaminisha kwako, Plz plz nakuomba kama huamini hautamaliza wiki huyu bwana atakubakua mpaka utaomba ufe na usiniite!

Kwanza umeharibu kumwonyesha unapofanya kazi na unapoishi, huwezi hamisha ofisi ya watu ila unaweza hama unapoishi, nakushauri hama unapoishi, usionane nae tena live plz plz plz, alafu pokea simu zake mtangazie njaa mwanzo mwisho, baada ya wiki 1 omba likizo mimi na wewe tutasafiri, kumbuka hela ya JITU ni kama ina mashetani, anaeila lazima anailipa na sidhani kwa hali yako kama utaweza malipo ya JITU!

Nakushauri vitu viwili:
1.  Mpige hela ndefu hata milioni 100 hata million 800 we mpige utapewa, akikupa hela nyingi hama namba, mimi na wewe tutasafiri kwa siku 28 hatutakaa hapa Bongo, plz fanya navyokwambia ukikosea umeisha!
2.  Achana nae yani kata mawasiliano nae usimpige hela zozote, yani kata tu mawasiliano nae akija kwako usifungue mlango mpotezee, akituma hela usimrudishie, akipiga simu usipokee, meseji usijibu akija ofisini kwako usitoke, mkwepe mwanzo mwisho ataacha, itachukua hata miezi 6 lkn ataacha!

Binamu Miaka 28: akaanza kuogopa nikamweka sawa akatulia

Nakushauri kwa mara ya mwisho kwa Jitu hama, yani kimbiaaa kama ulishawahi kukimbia pale paaaaa, paaa omba Mungu akupe mabawa!

Dogo akakubali fresh, akaondoka!

Baada ya wiki 3 nikapokea simu ya Harrieth ananiambia amerudi nimpelekee hela zake kwake, nikaondoka mdogo mdogo mpaka kwa Harrieth, kufika nikamkabithi akahesabu akashukuru, wakati tunataka kuanza stori za London simu yangu ikaita kuangalia ni Binamu wa Miaka 28, nikapokea haraka haraka ananiambia Grace njoo sehemu flani huku Sinza kumekucha kuna gesti yupo hapo amekwama
Tukaondoka na Harrieth mpaka Sinza kwenye hicho kihotel hapo najua binamu kaharibu mbaya
Kufika naona wasichana 2, wamelala wanalia kumwangalia Binamu wa 3 amekaa pembeni analia.. kuuliza kulikoni watu hawaongei nikataka kuita nguvu ya dola ije isaidie maana ni mikelele tu kama mapaka ya usiku

Harrie akafanya kazi ya kuwanyamazisha, wakanyamaza wakakaa sawa, wakaanza kuongea
Binamu wa miaka 28:
Grace dadangu huwezi amini, mimi nimetoka zangu kazini, napata simu ya shogangu ananiambia nije sinza nikaja hapa nakutana na bi shoga mwingine nae kapigiwa simu kaambiwa aje kuingia ndani tunamwuliza mwenzetu vepe uzuri mimi nilikuwa nimesimama mlangoni sijaufunga mara namwona JITU anatokea bafuni yupo mtupu doh kumwangalia na Punda lake nikahisi nakosa nguvu!

Jitu akawa anasema sisi wote tumemchezea na kula hela zake kwa muda mrefu ni siku ya kulipa leo, eh kusikia kulipa huyu mwenzangu akadakwa na Jitu mimi nikakimbia nje!
Nikawa nawaza niite Meneja nikajua tu huyu bwana atakuwa ameshajipanga na Meneja kalipwa asisumbuliwe, basi nikapanga kwenda kuita polisi lakini nikahisi na kule atakuwa anamtu ndio nimekupigia
Harrieth: imekuwaje? Mmebakwa au?
Grace: Bwana wako kaumiza watoto wa watu ona walivyochanika maskini!
Harrieth: ahahahahha! Uuuwi maskini ya Mungu jamani watoto mmezidi lakini mnalipia tama
Binamu Miaka 28: Mimi nimeponea chupuchupu ila kama wanaume wote Duniani wapo kama JITU, naghairi kuolewa bora nizae kwa kupandikiza!
Wote: tukacheka maskini huku watoto wa watu wamelala wanaskilizia maumivu
Tukaishia kuwazoa zoa warembo tukaondoka, nikamwambia Harrieth apitie polisi akawaandikishe wamebakwa ila ndio warembo wajiandae kukutana na waandishi wa habari
Warembo wakakataa katu katu hatutaki, tupeleke kwa rafkietu tukalale, rafkiao akakataa akasema bora twende kwa Dada Grace mimi pale nimeshahama na sitaki mtu ajue!
Baada ya kufika nyumbani kila mtu akiwa ameshatulia na kula chakula tukawauliza imekuwaje, wakaanza kutuhadithia kuwa walimfahamu JITU kupitia Binamu wa miaka 28, sikuile walipokuwa Soth Beach Hotel, Binamu alivyoondoka mmoja wa rafkiako alibakia, Jitu alipomwona akamfuata na kuanza kumtongoza akakubali
Rafiake mwingine na Binamu nae akasema sikuwahi kutongozwa na JITU lakini nashangaa niliona ananipigia simu wiki 3 zilizopita ananifuata kazini anakuja kunitoa out michezo kama aliofanyiwa Binamu lakini wao hawakujua kuwa Michezo ya JITU mwisho wake ni malipo!
Jitu aliwaosha kwa pesa na pesa kila siku anawapa pesa wakaona bwana wa kumchuna ndio huyu kumbe kuna siku yao ya kuchunwa!
Sasa hotelini alienda na mmoja wakawa wanajiandaa kwa mechi rafkiake Binamu alipoingia bafuni JITU akachukua simu akatuma sms kwa rafkiake mwingine na Binamu na Binamu pia kuwa waje guest house namba flani, haraka kuna mtu amemkamata, ndio wote wanakutana na kuingia kumkuta mwenzao amelala mtupu analia, walipomsogele JITU akatokea bafuni akamkamata mmoja na Binamu akakimbia

Watoto wa watu walipigwa Punda kwa kubadilishana alafu kawafungia na kuwarekodi! Anawaambia Pesa zangu mmekula, shopping nimewapeleka leo na mimi nataka mnipe raha.. wakiwa wanaongea simu zao zikaingia message whatsapp, kuangalia ni video toka kwa JITU, kawarekodi maskini walivyokuwa wanapigwa mechi watoto wa watu wanalia mbayaa, wanapiga mikelele Jitu unatuua mpaka wanamaliza na JITU anaondoka anawaacha wanalia na kupumulia mdomo na maskio
Nikaiangalia ile video nikaona jinsi gani shemji yangu JITU alivyo katili, huyu baba sijui free mason au sijaelewa alafu anarekodi watoto wa watu yeye amejificha sura amevaa mask, dah akaniachia mawazo huyu shemeji, sijui Harrieth huko London kulikuwaje..

Binamu Miaka 28: akanifuata akanikumbatia, ananiambia asante sana dada Grace nisingekusikiliza leo ningekuwa nakandwa kama wenzangu wanavyokandwa na Harrieth huku wanalia


ITAENDELEA KESHO TAR 15 SEPTEMBER 

2018 SAA 8 MCHANA 

YA TANZANIA
____________________________________________________________ 
C. MOON LIGHT LADY- 1985





Baada ya lile sakata la jana nikawaacha warembo wamelala, Harrieth kaondoka kaniacha kaenda kuongea na JITU anataka kumchamba kwanini amewarekodi watoto wa watu kwenye simu
Mimi nimemkataza lakini hajasikia.. nikaona usiku ni mwaka nikaamua kwenda kumalizia sikukuu yangu mjini, nikampigia simu shogangu aje anipe kampani;
Nikadondoka mpaka IT PLAZA, HIGH SPIRIT LOUNGE nikakaa zangu huku Napata wine na kusikiliza mziki mzuuuri huku napunguza stress.. wakati nimekaa nasikiliza Mziki huku namsubiria shogangu mara wakaingia wakaka kama 4 wakaja wakakaa nyuma ya kochi nililokaa, mimi nipo buzy nawaza na kuwazua jinsi JITU alivyowatenda watoto wa watu na jinsi gani Binamu yangu ameponea kwenye mdomo wa mamba, sijui alichukua pesa za JITU au alikataa kama nilivyomuelekeza, unajua hawa watoto bwana akili zao wanazijuaga wenyewe lakini!.. anaweza akasema hajachukua kumbe ameshakula hela kibao, na anaweza akasema ni bikra kumbe ameshabingirita mudaaa sasa anajikosha, nikiwa nawaza na kuwazua hawa watoto siwamalizi mara nikashtushwa na maongezi ya wakaka waliokaa nyuma ya kochi langu wakiwa wanabishana. Maongezi yao yalikuwa hivi;
MJEDA WA KWANZA
mwanamke mwenye ngozi nyeupe sio mtamu kama mwenye ngozi nyeusi
MJEDA WA PILI
Mwanamke mweusi sio mtamu kama mwanamke mweupe
MJEDA WA TATU
Mwanamke maji ya kunde ndio mwisho wa matatizo

Wakabishana hapoo mara shogangu akaingia, shoga kapendeza kaulamba mbayaa! Walipomwona shogangu wote wakageuka wanamtizana maskini shogangu kidogo aanguke maana sio kwa ile minjicho!
Shoga: niaje we mnyama!
Grace: nikacheka maana shogangu ana fujo balaa, nakuona sikuhizi umekuwa mswahili ukiitwa unachelewa lisaa li1
Shoga: yani we acha tu nilikuwa nampa utamu shemeji wako si unajua mpaka nikombeleze utamu ndio naweza kutoka, nimemwacha amelala anahemea pua mdomo na masikio… vp wewe mumeo umemtupa wapi mbona simwoni?
Grace: yani wewe hujaacha tu, huku wale wakaka wanamwangalia bado shogangu.. nikamsogelea shoga nimamwambia hawa wakaka wamekuelewa kweli unaonaje ukiwaalika waje wakae hapa walikuwa na topiki yao walikuwa wanadiscuss wewe ndio umekuja kuwavurugia!
Shoga: akageuka, hello Boys! Hw are you?
MIJEDA: hi, hey, mambo, niaje mrembo
Shoga: Mnaonaje mkija kukaa na sisi tukaendeleza ile topic mliokuwa mnadiscuss kabla sijaja?
MIJEDA: wakashangaa, mmoja akainuka na mwingine na mwingine wakaisha!
Tukasalimiana pale wanaume wakajitambulisha
MJEDA WA 1: Naitwa Moses
MJEDA WA 2: Naitwa Hassan
MJEDA WA 3: Naitwa Baraka
Grace: oh jaman nashukuru kuwafahamu, naitwa Grace na huyu ni best yangu sana anaitwa Money Stars!
WAJEDA: Money Stars?!
Shoga: Yes ndio jina langu, kwahiyo mlikuwa mnaongelea utamu wa rangi za wadada mmeishia wapi sasa?
Moses: Mimi naona wadada rangi yako watamu sana
Hassan: we si ulisema weupe ndio watamu huyu dada sio mweupe ni maji ya kunde
Moses:  Na wewe Hassan ulisema weusi ndio wazuri sasa kwa Money Stars unatafuta nini?
Baraka: Mimi pekeyangu nilisema rangu ya Money Stars hapa ndio tamu au sio my dia?
Money Stars: ahahahahahaha! Kwahiyo nyie wote mabikra au?
MIJEDA: hapana
Money Stars: nyie wote mmetembea na wanawake wangapi mpaka sasa?
Moses: 15
Hassan: 35
Baraka: 20
Money Stars: na mna umri gani?
Moses: 29
Hassan: 32
Baraka: 35
Money Stars: ndio maana mna maongezi ya kitoto! So nyie wote mmeoa au?
MIJEDA: noooo bado
Baraka: wanawake wa sikuhizi pasua kichwa hatuwezi kuoa kabisa,
Money Stars: kwahiyo nyie wote hamna mademu mnapiga na kukimbia sio?
MIJEDA: hapana, ila wanawak wa sikuhizi wanatupa mazingira ya kuwapiga na kuondoka… hatujawahi kuwapata wale wife material, hawapo!
Money Stars: mnadhani mimi ni wife material au?
MIJEDA: wewe ni zaidi ya Wife material
Hassa: Money kwani wewe umeshaolewa?
Money Stars: nimeolewa mama watoto 3 na wajukuu 5
MIJEDA: NOOOOOOO WAAAAAAY, unadanganya!
Money Stars: nina miaka 48
MIJEDA: huo uongo sasa
Money Stars: hii hapa driving licence yangu angalieni
MIJEDA: wakaidaka fasta fasta, wakaangalia kweli kazaliwa mwaka 70, duuu! Mbona mzuri hivi… dah wajanja wanajua kuwahi na kutunza
Money Stars: Mnadhani mkipata mwanamke mnaweza kuwapenda na kuwatunza wakifika 48 wafanane kama mimi au mnaongea tu? Tatizo lenu nyie mnaonekana waoga hata nikiwapa mdogowangu mtampiga mtakimbia
MIJEDA: Hapana Dada, tupe tu! Lakini Dah shemeji huyo tunaomba ututambulishe maana sio kwa uzuri huu utadhani una miaka 25?
Money Stars: ahahahahahha, ila kwa kujibu Maswali yenu ni kwamba hakuna uzuri wa mtu kumzidi mwingine kila mwanamke Mungu kamuumba Mzuri na ana utamu wake! Ni kwamba nyie wote hamjakutana na wake zenu, mkiwapata hata akiwa albino mtasema ni mtamu kuliko mwenzake!
Ni muda tu ukifika hamtaongea kama mnavyoongea sasa!
Mwisho wa siku mtaendelea kubadilisha mabucha wakati nyama ni ile ile!
MIJEDA: basi tunaomba utusaidie namba ya wadogo zako kama hutojali maana kama dada mtu yupo hivi hao wadogo sijui itakuwaje!
Wote: tukacheka, na kuendelea kuongea pale, Money Stars akawaahidi kuwapa wadogo zake ambao hana kama wataonana tena, wote wakabadilishana namba na Money Stars, wakarudi kukaa kwenye kochi zao wakiamini kabisa atawapa wadogo zake.. sisi tukaendelea na maongezi yetu!
Money Stars: mama mbona waonekana umechoka au shem karudi nini?
Grace: goooooooooooooooooorl, goooooooooorul! Acha tu nipo na wadogo zako hapo nyumbani kwangu natamani hata kuhama mtaa, nikamweleza A to Z za yaliotokea… nikamwelezea kuhusu Shogangu Ulumbi… nikamwelezea kuhusu Harrieth… nikaja kumwelezea kuhusu shemeji yangu pasua kichwa anaitwa JITU!
Money Stars: JITU MANYANGA?
Grace: Yes unamjua?
Money Stars: kakutaka au?
Grace: of course nikamkataa
Money Stars: Unakataa hela?
Grace: hey! Embu nambie kwanza umemjuaje JITU
Money Stars: hakuna asiemjua JITU, we mwulize JITU kuhusu Money Stars atakueleza nilichomfanya!
Grace: ulichomfanya?
Money Stars: nishakula hela zake sana hakuna bwege kama Yule! Kabla hajamuoa huyo shogako ULUMBI, Yule bwanake alikuwa anataka kunioa mimi
Grace: oh nooo! Kwahiyo na wewe ushapita kwa JITU
Money Stars: unataka niongee au utaongea wewe?
Grace: basi endelea mama
Money Stars: Yes nilishmdate JITU miaka ya zamani kabla sijaolewa, kwao wazazi wake wanahela chafuu, Jitu kwao wana hela mbayaaa,  Bikra ya kwanza JITU nimetoa mimi upoo?
Grace: Money staaaars! Wewe wa kumtoa JITU BIKRA si amekuharibu?
Money Stars: kaniharibu?
Grace: ina maana wewe una bwawa?
Money Stars: skuelewi unaongea nini anti bwawa ndo kivipi?
Grace: kwani hujui kuwa JITU ana machine kama ya PUNDA? Ameliza kila mtu kuanzia mkewe, Harrieth mpaka marafiki za binamu yangu!
Money Stars: ahahahhaha kumbe ni JITU makubwa! JITU katoa wapi dude kubwa?
Grace: kwani zamani alikuwa na bamia?
Money Stars: ndio tulichoachania nacho!
Grace: heee!
Money Stars: habari ndo hiyo!
Grace: nimechanganyikiwa jamani embu rudia tena
Money Stars: bwana unanichosha! Unanilipa au ujue me nina uchaga nusu!
Grace: how much unataka?
Money Stars: unauhakika unaweza kunilipa?
Grace: taja bei
Money Stars: Milion 5
Grace: unakichaa
Money Stars: unataka ukweli?
Grace: sina hela
Money Stars: kachukue kwa jitu
Grace: nooo sio kwa lile punda
Money Stars: akanipokonya simu yangu, ukitaka nimfanye JITU aache kutesa watoto wa watu nahitaji Milion 5 nitakusaidia, akaanza kutafuta namba ya JITU akasevu kwake, akatuma sms kwa JITU akahakikisha imeenda akanirudishia, ole wako utume kingine nasubiria jibu ndio nikuhadithie
Grace: nikachoka huyu mwanamke sijui vepe ananiharibia, kucheki nikakuta kaandika - MoonLight Lady – 1985
Nikiwa katika kushangaa, mara simu ikapigwa nikaitupa kwa Money Stars, haya sasa ongea nae anapiga
Money Stars: akapokea,
JITU: Money is this you?
Money Stars: I miss you!
JITU: what? How? Si umekufa wewe?
Money Stars: Sijafa!
JITU: haiwezekani na kaburi lako wamenionyesha
Money Stars: kwani huyu unayeongea nae ni nani?
JITU: Grace unanichezea akili au?
Money Stars: wala huhitaji kujichetua,
JITU: Siamini Money Stars kama upo live
Money Stars: nipo
JITU: nataka kukuona!
Money Stars: haiwezekani
JITU: Kivipi?
Money Stars: Dola laki 1 kuniona
JITU: Sielewi
Money Stars: unakumbuka ile joint akaunt tulifunguaga pamoja?
JITU: ndio
Money Stars: kaniwekee dola account yake ninayo unabadilisha tu pale kwenye…. Kila week weka dola 5000 zikishafika dola laki 1 nakupigia kwa namba yangu uje kuniona.. nikakata simu
Grace: macho yanamtoka, JITU akapiga tena, Money stars akachukua simu yangu akaiblock ile namba,
Money stars: hama namba kesho sawa?
Grace: siwezi hama namba
Mone Stars: tena hama namba andikisha jina la mwanao Yule wakike usiandike lako huyu mjinga ataenda kukufuatilia
Grace: unajua umeniudhi leo umeniletea makesi ya kijinga mimi nina matatizo ya kunitosha
Money Stars: hayanihusu matatizo unayalea mwenyewe na ukiendelea kukaa na hio namba huyu mjinga atakusumbua mpaka kwanza ataanza kukutrack simu yako kila ukienda anajua hama namba nakuambia yani kama mimi wewe leo leo ningechomoa nikaitupa kwenye sinki la chooni hapa hapa
Grace: unajua nimekasirika
Money Srats: dola kai 1 kwa rate ya leo inasoma tsh 2200 kwahiyo nitapata million 220,000,000.
Grace: hawezi kuweka!
Money Stars: umemzaa au?
Grace: hapana
Money Stars: Mbona unamsemea?
Grace: hela nyingi sana
Money Stars: hela zangu au zake? We inakuhusu nini?
Grace: unajua Yule ni free mason, kila mtu anaeshika hela yake lazima ailipe!
Money Stars: na mimi ni Free Jesus, aje na makorokocho yake name nakuja na Damu ya Yesu
Grace: Damu ya Yesu haifanyi kazi kwa wapiga panga kama wewe
Money Stars: Yesu mwenyewe alisema muwe wajanja kuliko nyoka! Sasa kama JITU ni nyoka mimi zaidi ya nyoka!
Grace: sasa nikishachomoa line
Money Stars: kwanini hujampiga hela zake lkn?
Grace: sina tama
Money Stars: ndio maana umebakia na shida zako, doh, kazi huna, hela huna, umeachika, upo upo tu
Grace: sasa unavuka mipaka
Money Stars: nisipovuka mipaka utakuja kuhamia kwangu, wewe una miaka 33 hujisomi unajidai umeokoka umekuwa fala kabla hujaokoka! Si bora urudi kuwa wa zamani? Alafu unaokokaje hauishi na mumeo wa ndoa
Grace: haya hayakuhusu
Money Stars: alafu mwisho leo kuniomba hela ya rent kama unaniambia hayanihusu
Grace: poa
Money Stars: Ngoja niondoke nirudi kwa mume wangu, wengine tunachunga ndoa zetu maam nakushauri uchunge na yako.. akaondoka ameniachia matatizo juu ya matatizo hata kurudi nyumbani naogopa!

Nikakaa pale kama lisaa limoja natafakari maneno yake, akaja waiter nikalipa hela yangu nipo tayari kuondoka mara namwona JITU huyo anaingia mwenyewe kama anatafuta mtu!

Doh Grace kidogo ninye, nikainama, akapita akaenda chooni nikakimbia nikatoka, nipo kwenye lift nikakumbuka kuchomoa like, dah nikachukua peni fasta nikajiandika namba ya simu ya mume, mama na baba nikazima simu nikachomoa line lift ikafunguka nikaitupa line ndani ya lift nduki, nikaingia kwenye gari, ile natoka namwona JITU anashuka kwenye lift ameshikilia sim card anacheka doh Money Stars noma, pa kwenda sina naona kama atanikamata JITU, nikaenda moja kwa zote kwa Money Stars, kufika mumewe anashangaa vepe Grace mbona umetujia usiku wa saa 7 kuna nini?
Grace: namtafuta mkeo
Money Stars: mama umekuja kunitukana na kwangu?
Grace: amenifuata Yule mtu
Money Stars Mume: nani anakufuata?
Money Stars: mmh! Haya twende ukalale, huyu amelewa mume wangu twende huku
Nikapelekwa chumba cha kulala, Money Stars ananivuta na kunifinya ole wako uongee chochote kwa mume wangu ntakuchinja stupid girl! Kufika chumba cha wageni nikatupwa kwenye kitanda kama gunia, asubuhi mume akiondoka tutaongea lala, akachukua simu yangu akaondoka nayo!
Grace: sikujua saa ngapi nililala lakini asbh niliamshwa kama nipo jeshini nimemwagiwa maji ya bariiidi dah na zile hangover za jana nilitamani kulia… bibie amesimama mbele yangu ameshikilia Panadol
Money Stars: Meza hizi dawa, una masaa 3 kukaa kwangu uondoke
Grace: nikafanya kama alivyotaka, nikaingia kuoga kurudi nakuta ameniwekea mfuko, gauni na kikoti, nikavaa nikakusanya virango vyangu huyo nikajongea sebuleni
Money Stars: chai hii kunywa uondoke!
Grace: nikakaa kunywa chai maskini
Money Stars: simu yako nimeitupa, hii simu nyingine na line kanunue kwa jina la mwanao, umeniingiza kwenye matatizo mimi nilishakufaga mwaka 90 sasa ole wako ukaongee kwa mtu yeyote…
Grace: macho yananitoka kuangalia ni Iphone6s.. simu ambayo nimeitamanije, sijawahi kuwaza kuimiliki na hizi ni Milion5,
Money Stars: Pale ulipo umeshahama. Taxi ikija itakupeleka… ukifika mwulizie… mwambie nimekuja kwa ajili ya nyumba… utakaa hapo mpaka nikwambie uhame… Yule JITU ameshaweka dola 5000 kwenye akaunt leo asubuhi.
Binamu yako nimeshaongea nae leo asubuhi nimemwambia umesafiri simu umepoteza kama kuna chochote ongea na mimi, virago vyako vipo kwenye gari yangu taxi ikija utahamishia, hamna kuwasiliana na mtu zaidi ya mumeo, wazazi, mtoto na mimi.. Harrieth mpotezee kwa sasa na Ulumbi..Ukiharibu usikanyage kwangu nitakufukuza kama mbwa hunijui ee?
Grace: macho yananitoka najiuliza bado naota au nimeamka!



MWAKA 1985
Nikiwa na miaka 15, nilikutana na JITU akiwa na miaka 20
Tulipendana sana, tukakaa kwenye mahusiano miaka 2 mechi zote tumepigana lakini hakuwa na PUNDA nashangaa umenionyesha kituko jana kwenye simu sijaelewa katoa wapi, nikajua tutaoana, sikumoja akanikaribisha kwao nikapokelewa vizuri na Mama yake akanipenda sana ila Baba yake sikumwona niliambiwa amesafiri kikazi.. kwao kulikuwa kuzuri mno kama ulaya ndogo!
Tukawa kwenye mahusiano yeye yupo Chuo Kikuu Mlimani mimi namalizia form 6 Tambaza High School,
Shule ilipoisha na kumaliza mitihani mimi na mashosti zangu tukaenda kujirusha Mziki mambo ya Happy time, usiku wa Ijumaa tunaenjoy groove night na nini tunajikumbushia miziki ya kikwetu kwetu old school Fulani hivi amaizing… Mara akaja Baba m1, akakaa pembeni anatuangalia tunavyoserebuka! Mimi sikumwona na siku hio JITU hakuwa na mimi nilijiiba na marafiki zangu tukatoka, JITU alikuwa na pepa ya j3 yake nikaona nisimsumbue!
Lile libaba likaja moja kwa moja kwangu, 
Baba: hey you 

Money Stars: Hi (Ya Mkato)

Baba: naomba nicheze na wewe, maana katika wadada wote hapa mimi nimekuona wewe tu, 

Mashosti: aaaaah embu kwenda zakoo 

Baba wa watu haogopi wala nini, kaning'ang'ania mpaka nikaenda kucheza nae 

Nikiwa nainuka Yule Baba akawaambia she's my moonlight lady, hata sijali mtakachosema:

Mashosti wakawa wanacheka

Hapo nimevaa bonge la umini, baba amekolea anacheza mara anishike kiuno basi vurugu. Tukacheza mziki wa Moon Light Lady wa JULIO IGLESIAS 

Tukiwa tunacheza akaniambia jina lake Mr Manyanga! Sikuelewa hilo jina maana sikuwahi kujua kuwa jina la JITU ni Manyanga, aliniambia anaitwa JITU Peters!

Nikamwambia nashukuru kukufahamu Mr Manyanga,

Mr Manyanga: wewe ni msichana mzuri sana, nimekuona tu nimekupenda, una miaka 15 tu au?
Money Stars: nikashangaa huyu baba kajuaje umri wangu?
Mr Manyanga: nataka kukupa ofa nzuri sana itakayobadilisha maisha yako!
Nataka uachane na mwanangu JITU
Money Stars: nikasimama kucheza, unasemaje we baba?
Mr Manyanga: umeniskia sana, narudia nataka uachane na mwanangu JITU
Money Stars: kwanini?
Mr Manyanga: Mwanangu hawezi oa kwenu! Ndoa yake ilishapangwa mud asana akimaliza shule nampeka Uingereza anaenda kufundishwa kitajiri, wewe ndio unamzibia bahati yake
Money Stars: Nikataka kuondoka akanishika mkono kwa nguvu, kama unataka kubaki mjini nifuate!

Money Stars: kuangalia pembeni naona ma-body guard wanamsubiria nikajua leo nafwa maana hata nikipiga kelele haisaidii kuna mziki mnene!

Nikaongozana na Yule mzee mpaka alipokaa, akachukua kitabu chake cha benki akaniuliza ulishatamani kuwa na hela kiasi gani kwenye maisha yako?

Money Stars: mbona sikuelewi baba kuna sehemu nimekukosea au?
Mr Manyanga: Taja au unataka nikuondoe bila malipo sina muda wa kupoteza! Huyu ni mwanangu wa pekee wa kiume na hakuna kitu kitakachoingilia na mipango yangu!

Money Stars: Nataka
Mr Manyanga: Yes ngapi?
Money Stars: nampenda sana mtoto wako siwezi kuondolewa kwake kwa pesa, upendo wetu hauwezi kununuliwa kwa pesa wala mali
Mr Manyanga: Jitu anajua upo hapa na mimi?
Money Stars: hapana
Mr Manyanga: kwahiyo umemdanganya? Ina maana humpendi mwanangu
Money Stars: ana mitihani j3
Mr Manyanga: milioni ngapi kuondoka kwenye maisha ya mwanangu?
Money Stars: Milion 800 (Niliitaja nikijua hana)
Mr Manyanga: akaandika cheki 10, kila moja ina million 80 nikajua huyu anazingua haya makaratasi tu na mimi najuaje kuhusu pesa ndio kwaaanza nimemaliza form 6 cheki hizi sijui kutumia
Mr Manyanga: akaunt namba yako mpya ni hii, kila baada ya miezi 6 peleka cheki moja moja watauliza waambie nimetumwa na Mr Manyanga

Money Stars: kama ya uongo je?
Mr Manyanga: uje nyumbani kwangu unishitaki kwa mke na mwanangu, sijawahi kuwa mwongo ni vile hunijui
Hizi hela ukizitumia vizuri utasoma kokote Duniani na utafanya biashara yeyote Duniani
Na ukitaka niwe referee wako maishani mwako niambie
Ila kaa na mwanangu mbali
Money Stars: plz naomba basi niwe nae mwisho mwisho amalize mitihani yake tafadhali
Mr Manyanga: sawa, na ukijibebesha Mimba utaniona kwa rangi nyingine
Money Stars: ivi namuachaje mtu nimependana nae?
Mr Manyanga: akimaliza mitihani, mwambie aje Hotel Kilimanjaro, chumba namba… tutakuwa wote, atatufumania, atakasirika atakuacha na wewe utaondoka
Money Stars: kuna msamaha Mr Manyanga
Mr Manyanga: Binti yangu hujawahi kutana na fumanizi, maandalizi yake nitakusaidia!

Tangu hapo sijawahi kumwona tena Mr Manyanga, nachojua nilipoenda kuweka cheki ya 1 ikakubali na ile akaunt ya benki alinifungulia ilikuwa ya kweli maskini, nikawekewa hela zangu za kwanza mil 80 zikaingia ndani ya miezi 2… sikuamini, nikaenda kutoa laki 2 sikuamini.. kweli kuna MaDON sikuwahi kuamini!

Nikarudi nyumbani kumweleza sista wangu akaniambia hapo hapo kwani Tsh ngapi?
Usiku wa Tukio la kufumania ukafika bwana, hapo kweli ndio niliona rangi nyeusi ya Mr Manyanga!
Kweli JITU akaja kweli akatufumani kama Baba yake alivyopanga, JITU alikasirika sana, akaniuliza kwanini baba yangu? Nikamwambia hauniridhishi kama Baba yako, Baba yako ana Machine kubwa wewe una ndogo siwezi tena,
Jitu alikasirika, akaanza kupiga vitu anatupa meza, anarusha chupa, mimi nalia maskini JITU, Baba yake akavaa pensi akashuka kumshika,  anambembeleza, mimi nikanyata nikavaa nguo fasta, ile nataka kutoka nikashikwa na JITUu nikapigwaa Baba yake amekaa pembeni anavuta sigara, nilipigwaa mpaka nikazimia, ndio babake akainuka, akamzuia, kunishika akamwambia hapumui mwanangu umeua!

JITU: akachanganyikiwa hakuamini, mimi nimekaza roho sipumui si moja ya mpango, Baba yake akamtoa haraka, nenda kaite mabodi gadi, wakaja JITU kachanganyikiwa, Mabodi gadi wakanitoa fasta kama napelekwa hospitali, JITU na Babake haooo wakaondoka.. mimi nikashushwa kwa sista, yeye na babake wakaenda kwao!

Mr Manyanga akatengeneza msiba feki uswazi akamwonyesha mwanae, mwanae akaenda kutoa pole zake akaondoka, baada ya mwezi mmoja JITU akaonyeshwa kaburi na babake pale Kisutu kwa nyuma makaburi ya Upanga! Kaburi feki limetengeneza na jina langu kabisa!
Ndio JITU akaamini nimekufa, shule yake iliisha akaondoka kwenda kufanya Masters Uingereza na mimi nikaenda kusoma Marekani kwa Dada yangu!
Aliesimamia Visa ya Marekani ni Mr Manyanga na Bank statement alitoa Baba Yake JITU!

Stori ya alimuoaje Ulumbe anayo mwenyewe JITU, utafuatilia kwa muda wako..

Na hilo dudu atakuwa ameongezea alipoenda kusoma Masters nina uhakika, nadhani ameongeza kwa kunikumbuka! Ahahahahah JITU BWANA! Ameenda extra mile kuwakomesha watoto wa watu! Akijua sikufa anaweza akaua mtu asee!
Yule bwana bado ananipenda mpaka leo kaweka hela natamani sana kuonana nae ila ndio mume asijue!

Sasa wewe unataka kuniharibia kuwa nimefufuka, unataka kuua wazee wa watu au?


Grace: JITU amejuaje akaunt namba yako?

Money Stars: Baba yake alifungua hio akaunt alifungua zinafanana

Grace: Moon Light Lady maanake nini? Kwanini umeandika Moon Light 1985 Akakumbuka na kupiga?

Money Stars: Tulifahamiana 1985 na kupendana na huo wimbo ndio ulikuwa wimbo wetu tunaupenda, tulionana wakati huo wimbo unapigwa mziki!


Baba yake alifanya kukopi … sijui Yule Mzee Manyanga bado yupo au amekufa sijamwona miaka 30 sasa!


Taxi imeshakuja mama tutawasiliana ukishapata namba nipigie!

Grace: nikaondoka nimejaa stori za ajabu kichwani nimechanganyikiwa naona dah mbona kama ni uongo lakini kama ukweli!


 

TUONANE KESHO TAR 27 SEPTEMBER 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
_______________________________________________________ 


D. KUTAPELIWA KIMAPENZI

Grace mimi nikakaa benchi kwenye nyumba nisioijua miezi 6, Kazi yangu ni kuangalia Tv, kusikiliza Redio na kulala…kila week Money Stars anakuja ananichungulia naendeleaje analeta msosi anarudi kwake.. sijakanyaga kwenye nyumba ya ibada nina miezi 6, uzuri kila siku nawasiliana na mtoto wangu.

Kazi mkataba umeisha, Ile hela aliokuwa anawekewa Money Stars na JITU ndio nilikuwa nalipwa mshahara mimi na kuzidi ijapokuwa sikuwa napewa hela yote kwahiyo muda mwingi nilikuwa nakaa ndani kama mwali.

Ijumaa moja jioni nikapata simu toka kwa Money Stars kuwa nijiandae kuna nguo ameiweka Kabatini, hata sikujua ameiweka saa ngapi, kwenda kucheki ipo kiwalo kizuri nakwambia, akaniambia nijiandae nichukue Taxi tuonane Samaki Samaki Mbezi Beach.. nikafanya kama alivyonielekeza, nikatua Samaki Samaki natetemeka sijui kuna nini… nikiwa nashangaa shangaa gari ikaja miguuni mwangu ikasimama, mara simu ikaita, kupokea naona ni Money Stars, ananiambia Ingia ndani ya gari!... mmh nikasita sana akaanza kunitukana kama kawaida yake, nikaingia ndani kuangalia ni yeye kaka siti ya abaria ya mbele
Money Stars: sasa unaogopa ogopa nini, huniamini au?
Grace: Kimya!
Mara simu ya Money Stars ikaita akapokea akaweka Loud Speaker
Money Stars: enhe?
Simu:  We Mchawi ipo wapi?
Money Stars: shida?
Simu: Tupo Serena njoo,
Money Stars: poa
Tukadondoka mpaka Serena Hotel, gari ikaondoka tukaingia ndani, kufika nakutana na wadada, wadada visuuu balaaa, doh! Hawa wadada nawaonaga kwenye TV kama sio magazeti yale ya SANI! Wazurije! Mimi mwenyewe nasubiria sanaaa, nikawapenda bure, tukasalimiana alafu tukakaa

Wakaongea na Money Stars weeeeee, yani huwezi amini maongezi yao, wana majeraha mtindo mmoja, topiki iliokuwa inaongelewa ni matatizo ya wanaume!

Dada wa 1: wanaume hata siwaelewi Money Stars, nipo na mume wa mtu ni wapenzi wangu tuna kama miaka 3 sasa, amenipangia nyumba hapo Mikocheni, yeye anaishi Upanga na mke wake na watoto 4… ameninunulia gari, analipa kodi ya nyumba,  ndio nina kazi yangu lakini kila mwezi nawekewa hela kwenye akaunt yangu sio chini ya million 3…
Money Stars: du! Sasa shida iko wapi mke wa pili? Au unataka ndoa?
Dada wa 1: Sitaki ndoa mimi, sio kwa hizi stress…
Siku 1 akaja kuniambia anataka nimpe michezo ya Sodoma na Gomora! Hapo ndio niliona Dunia imebadilika rangi na jua limekuwa jeusi, miaka 3 hajaniomba michezo ya kipuuzi leo hii ameamkia wapi na kutaka kuniharibu?  
Yani nimechoka mazimaaa! Nimekataaa wanaume weeengi kisa upendo wangu kwake na kukubali kuwa Mchepuko wake (Side Chick) alafu ananiletea habari za kiduwanzi kaniudhii!

Money Stars: ahahahahahha ukamfanyaje baada ya kuudhika?
                                                         
Dada wa 1: Nikamfukuza nikamwambia akiendelea kuniletea habari za kishetani naondoka kwenye maisha yake… hapa nina stress akiondoka life style yangu ya maisha inabadilikaje! Sijui nafanyaje unanisharije Money Stars?!
Money Stars: Du! Hapo pagumu! Ngoja nisikilize wengine nitakujibuni wote!

Dada wa 2: Mimi matatizo yangu kama ya bishouger! Lakini natofautiana kiduchu sana, Hapa nilipo nipo na waume za watu 2,

Wote: wakamuangalia kwa mshangao!
Dada wa 2: Mtanisamehe wamejileta wenyewe sijawafuata, mmoja wa mahitaji yangu ya kila siku mwingine wa maisha yangu ya ziada ya hali ya juu (exclusive life)... Nikawapanga hawajuani wote !
Sasa juzi kati nikaja kufumaniwa na wote wawiliii, 
Haikuwa kasheshe kama mnavyodhani, tukaongeaaa kikubwaaa nikawaambia ukweliii, wote wakataka walale na mimi ili waniaonyeshe nani mkali halafu ataniachia nichague mojaaa, katika mechi heeee nashangaa nataka kuliwa Sodoma, weeee nilicharuka na mashetani yangu ya kichaga hakuna mfano ... 

Tulivyoishia hakuna hata m1 aliepata huduma mpaka leo nakuadithia sina mawasiliano na wale watuuu, nina wiki 1 ila hapa nishapanikiii... sijui shetani gani wa sodoma amepita huku Bongo mbona wanaume wanaudhi hivi?
Money Stars: hao wanaume zako wameoa? Au mabachela sugu?
Dada wa 2: Wote waume za watu
Money Stars: ahahahahha, sawa nitarudi na kwako usijali enhe na wewe mwana yapi yanakusibu?!

Dada wa 3: Mimi nipo na huyu alieachana na Baby mama wake, lakini ni Kipusaaaaaa (Pervert) ibilisi atarudi kwa shetani kuchukua darasa.. Tuna miezi 2 anadai azame Sodoma bila Sodoma haoni raaaahaaa ... Nimemweleza ukweli lakini bado anang’ang’ania
Ndio kanipangia nyumba na nini, gari kaninunulia naishi appartment Masaki, kazi kaweka mkono yeye nipo NG'O nalipwa mil 4 kwa mwezi, lakini all my life hajawahi kuniambia habari za Sodoma wala nini, nilichooooka, hapa nime-give up ujana wangu kuwa na hili bwana alafu mwisho wa siku linataka - mavi? This is disgusting!
Money Stars: kwahiyo hapo ndio mmekwaaama wenyewe!
Wadada: kumbe je! Au ulitaka tutii maagizo yao
Money Stars: me sioni tatizo hapo kabisa!
Wadada: kwahiyo unataka tufanyaje?
Money Stars: nyie mnataka mfanyaje?
Wadada: wakaangaliana, hatuwezi kutoa huduma ya mavi
Money Stars: achaneni nao basi
Wadada: Itatucost
Money Stars: miaka yooote hio mmekaa nao hao majinga bado tu hamkuwa na akili ya kusevu pesa?
Wadada: kimyaa!
Money Stars: kama hamkutumia akili za kuzaliwa poleni, ila mimi kama dada yenu siwashauri mfanye kitu ambacho hampendi, na msiruhusu mwanaume yeyote awaharibu! Mnaharibiwa alafu hata hamjazaa watoto, mkija kuharibiwa huko kuzaa mtapata shida nyie, labda mtumie C-Section lakini siwashauri, kuzaa kawaida kuna raha yake asiwadanganye mtu!
Kwanza hawa wanaume wanataka kuwaoa au?
Dada wa 2 & 3: hawana hata mpango
Money Stars: na nyie mnataka kuolewa au ndio mmejitoa sadaka kwao kuishi bila kuwa na ndoa maisha yenu yote?
Dada wa 2& 3: tunataka ndoa na watoto
Dada wa 1: sitaki kusikia ndoa ila watoto nataka
Money Stars: Achaneni na hao majingas, kwanza haweawapendi, mimi nipo na Mume wangu na ndoa miaka 30 sasa … mume wangu hajawahi kuniomba mavi hata siku moja!
Mwanaume anaekupenda hawezi kukuomba michezo michafu ya Sodoma!..
Angalieni maisha yenu.. fanyeni yenu mbeleni mtapata mabwana wa kuwapenda, ingawa itawacost ukiachana na mtu umemtegemea asilimia 100 ujiandae kushuka chini na kuishi maisha ya kawaida.. hao wanaume wanawapotezea muda, yani kwanza ningekuwa mimi ningewavutia hela ndefu ya kuwapotezea muda alafu ningesepa!

Wazuri wanazaliwa kila siku, wanawanyonya damu hao kesho mtakuta wamewapangia nyumba vimwana wengine wazuri zaidi yenu, msibweteke kwa uzuri mlio nao wazuri wanazaliwa kila siku, najua hamtapata shida ya kupata watu wa kuwapenda, ila hapo mnapoishi kodi ikiisha tafuteni sehemu zenu muhame, hao majamaa wapigeni chini, kwani wamewaumba mpaka wawaumize vichwa?!
Sawa?
Wote: sawa
Money Stars: huo ndio ushauri wangu, ila kama bado mnawaza kuaibika shaurienu nendeni mkatumbukizwe Sodoma muone mbeleni mtakuwaje!..
Akili za kuambiwa changanyeni na zenu za kuzaliwa jamaa, eh haya!
Wadada: Sawa dadaetu tunashukuru
Money Stars: wakirudia kuwaomba tena sodoma waambieni waende maji taka, mavi yanapatikana mengi tu pale Msasani kuna Maji taka!
Wadada: wakacheka sana, maana hawakuamini kama ataongea hivyo!
Basi wale mabinti wakashukuru wakaaga wanarudi makwao maana wamekaa pale muda mrefu sana, Grace macho yananitoka doh, warembo kama wale wanafanyiwa unyama sie wenye sura kama za mamba itakuwaje?

Walipoondoka tukawa tumekaa tunaskiliza mziki, tukaagiza chakula tukala, baada ya msosi Money Stars akaanza kuniuliza maswali:
Money Stars: Anti nimechoka kuwa dada wa kazi wako.. muda umefika uanze kutoka, ila kabla hujatoka lazima uelewe Yule JITU ameshaweka hela zote kwenye ile akaunt, lakini sasa hapa usikae nataka ukakae kwa mumeo huko Mkoa, kwani yupo mkoa gani?
Grace: anaishi Mbeya!
Money Stars: huko hata JITU akiota hawezi kufikiria kukupata
Grace: huko siwezi kwenda mume wangu tumeacha
Money Stars: eh! We mbona unakuwa mzembe wa kufikiria? kwani nimekwambia ukaishi nae nyumba moja? Kapange kwengine lakini mkoa mmoja!
Grace: nataka kuishi dar staki kwenda huko
Money Stars: mmmh! Ivi wewe na bwashemeji mliachanaje.. ah ngoja kwanza niambie mlifahamianaje?
Grace: kimya!
Money Stars: usipoongea hautasaidiwa mama, usiri unakuumiza bora uongee tu tusaidiane! Vitu vingine nashindwa kukusaidia kwasababu sijui!
Hivi haum-miss mumeo kweli Grace?
Grace: not a bit
Money Stars: una bwana mwingine zaidi ya JITU?
Grace: sina
Money Stars: haja zako unamalizia wapi?
Grace: nafanya mazoezi!
Money Stars: aisee! Hata mimi unanidanganyia mazoezi? Au ndio mnapunguzana na Yule demu anaitwaje sijui Harrieth sijui nani?
Grace: sijawahi kuwa changudoa wa wanawake
Money Stars: unasema umeokoka, unaokokaje unamwacha mume? Yesu anapenda kuachana?
Grace: hapo ndio mimi tunaishia kugombana



Money Stars: nambie ilikuwaje? Walokole tunaowajua walokole wa kweli hawaachanagi wanavumiliana mpaka Yesu anarudi au kifo kiwatenganishe sasa wewe mbona unatuchanganya mama? Embu kuwa mkweli usaidikike, si umeona hawa wadogo zako na matatizo ya wanaume hayaishi, lazima upambane… kwani wewe mwana wa Mungu roho ya Uvumilivu hujapewa na Roho Mtakatifu? Sasa si ungemvumilia mumeo tu yaishe?
Grace: akaanza kulia.. kalia kwa nguvu kwa sauti watu wote wanageuka kumshangaa… du kweli starehe imeingia mchanga!
Money Stars: ohooo! mambo ya kubembelezana nyumba za starehe tena bwana mimi sipendi jamaa si ungelia nyumbani Grace, aya nyamaza basi! Nikambembeleza hapo mara akaja waiter kuleta vinywaji, Grace akajifuta haraka asionekane analia, Yule waiter akamuangalia anaona kama anamjua
Waiter: Grace?
Grace: akamwangalia, ah Mary mambo?
Waiter: poa upooo?!
Grace: yah nipo kwanini?                            
Waiter: sijakuona nina mwaka au ulienda mkoani kwa mumeo?
Grace: hapana nipo buzy tu na kazi
Money Stars: Grace unamjua huyu
Grace: namjua
Waiter: mtoto wa Babangu Mkubwa huyu
Money Stars: oh nashukuru kukufahamu mpendwa, naona Grace hajiskii vizuri, karibu ukae mpenzi
Waiter: hapana nipo kazini
Money Stars: hamna neon kaa tu umsalimie ndugu yako mimi naenda msalani mara moja nakuja!
Waiter: akakaa wakawa wanaongea na Grace
Money Stars: nikaondoka moja kwa moja mpaka kwa waiter mwingine, nikaongea nae nikamwulizia yule dada anaeongea na Grace anafanya kazi hapa?
Nikajibiwa ndio tena ni dada wa muda mrefu ana miaka zaidi ya 3
Nikamwomba sana kama nitaweza kupata namba yake ya simu, Yule waiter akawa kama ana sita nikamdanganga nikamwambia Yule dada anaelia babake amefariki, sasa nataka namba ya Yule bindada, nimpigie wakati shogangu hayupo tupange tunamwekaje sawa mfiwa! Akakubaliana na ombi langu akanipa namba ya Yule ndugu wa Grace, nikaisave nikamshukuru nikampa laki 1 mwenyewe anashangaaa tip ya leo vipi?
Nikaenda msalani uongo na kweli nikarudi kumchukua Grace maana pale hapafai tena! Tukaondoka nikamwacha Grace kwake bado analia nikaingia kwangu… Kesho asubuhi nikampigia Yule waiter ndugu wa Grace kwa kutumia namba ya Land Line, nikamwomba tuonane maana kuna dharura akajua labda ya kumhusu Grace
Tukaonana Samaki Samaki Mbezi Beach, mwenyewe kaja na Boda Boda ananiwahi, doh!
Money  Stars: Pole mpenzi naona nakuchosha
Waiter: Hamna vipi kuna nini mami?
Money  Stars: Grace nduguyo
Waiter: Hee amefanyaje?
Money  Stars: Yupo poa ameamka poa, usijali
Waiter: oh nimeshtuka alafu Yule kaka ulimwomba namba yangu jana aliniambia baba yake Grace amekufa ndio maana nimekuja fasta fasta!
Money  Stars: oh! Hamna bwana nilitaka tu kuipata namba yako
Waiter: Enhe kuna nini?
Money  Stars: Kazini unaingia saa ngapi?
Waiter: usiku saa 3
Money  Stars: ok samahani nimekusumbua maana jana ulionekana kushtuka kumwona Grace
Waiter: Yah Grace bwana, hahah yani Yule mwanamke msiri sana
Money  Stars: eti ee? Jamaan, yupo hivyo tangu zamani au sikuhizi
Waiter: Tangu tupo wadogo, na usiri wake ndio umemponza
Money  Stars: Umemponzaje?
Waiter: wewe ni rafiki yake?
Money  Stars: hapana Grace nilisomaga nae Sekondari tu, tumekuja kuonana ukubwani nilikutana nae anasubiria daladala nikamsalimia nikampa lift maana mabasi yenyewe yalionekana hamna katika kuongea ongea nikahisi ana shida, nikaenda nae hotelini nikanunua chakula, tukala, tukaanza kuongea mambo ya zamani tangu tumeachana yupo wapi anafanya wapi
Akanieleza tangu tumeachana mpaka pale, tumekutana, akasema anamtoto m1 ila mume waliachana sikuelewa kwanini, wakati tunamaliza kula nikamwuliza anpoishi akaniambia anaishi mwana nyamala amepanga, doh nilijiskia vibaya sana, nikampeleka mpaka kwake ile nyumba yenyewe sasa anayoishi gari kwanza haifiki ilibidi nipaki petrol station ashuke atembee!
Nikatoa kwenye pochi mil 1 nikampa na namba yangu ya simu nikampatia nikamwambia ukiwa na shida tutafutane me nipo tu
Tangu siku hio Grace akiwa na shida ananitafuta,
Waiter: oh jamaan we dada una roho nzuri! Usawa huu unampa mtu mil 1 tu kisa umesoma nae?
Money  Stars: Hamna Bwana Grace tulipotezana baada ya kumaliza Form 4 ila hatujaonana tena alikuwa rafiki yangu mzuri sana ingawa kwao aliniambia ni mkoa
Waiter: mkoaaa? Du!
Money  Stars: anaishi wapi kwani?
Waiter: wazazi wake wanaishi Magomeni, pale Mapipa! Grace Mtoto wa Dar ujue!
Money  Stars: oh sasa kwanini alidanganya?!
Waiter: Grace Msiri mama
Money  Stars: Mume wake kwanini waliachana?
Waiter: wameachana? Hahahaha ndio kakwambia
Money  Stars: ndio amesema walizaa nae mtoto mmoja yupo huko Mbeya
Waiter: Mbeya? Ahahahah ivi Grace unamjua au unamsikia? Unajua nashindwa sasa kuongea ila kwasababu unaonekana hujui kitu ngoja nikusaidie tu ila usije niletea matatizo Yule ni ndugu yangu kabisaa!
Money  Stars: Hamna neno sitamweleza
Waiter: Grace stori yake ndefu sana, ila dah naona aibu kukueleza
Money  Stars: niambie bwana nimsaidie:
Waiter: ok ngoja nikueleze ili na wewe umjue rafiki yako!
MWAKA 1995:
Grace alimaliza chuo, kwanzaa Grace kwao kama nimekueleza ni Magomeni Mapipa, wazazi wake wote wapo hai, kwao walizaliwa 5, wote walishaoa na kuolewa, Grace ndo mtoto wa mwisho pale… Grace mtoto wa Dar ujue, asikudanganye haijui Dar ni mwongo
Grace kama unavyomwona ni mzuri sana, alipomaliza Chuo pale Magomeni akapataga wanaume 3 wanataka kumwoa, Grace akawakataa, Grace anapenda mambo makubwa pale akawa anangojea apate bonge la bwana (Bwana mwenye hela), basi kwa kuwa wale mabwana 3 walikuwa watu wa kawaida hawana hela kama anazozitaka Grace na sijawahi kuelewa walimsomaje Grace sijui nae yule alikuwa anawaambia hata simwelewi!
Mwisho wa siku wale majamaa wa3 wakaja kujuana kijiweni kuwa wote walimchumbiaga Grace wakakataliwa wakawa wanajiuliza kwa nini wakati Grace hakuonekana wa maringo!
Wakajiambia labda kwasababu ya hali zao ndio maana wamekataliwa, wakaamua kumpanga mtu mwenye hela, wakamchangia kweli akaenda Yule jamaa, kufika kwa Grace kuongea nae na lile Gari la Benzi Grace akaona hapa hapa, akamkubalia, wakaenda kwenye mahusiano Yule bwana kweli akamtafutia ajira, Grace akaona haya ndio maisha!
Yule jamaa akawa anarudisha mrejesho kila week kwa wale waliomtuma, Yule jamaa alipoona Grace anataka kuolewa jamaa akachomolewa aondoke! Jamaa hakuonekana tenaaa!
Kati ya wale wanaume 3 waliotaka kumuoa mmoja akarudi bwana, akamtafuta Grace hapo kachanganyikiwa kweli kweli, akaja kuongea na Grace
Yule kaka alierudi anaitwa Haji!
Akamdanganya Grace anaitwa Innocent, lakini alirudi ana helaaa! Akaongea na Grace kambembeleza wee Grace kweli kaona hela na magari mazuri kaka anaishi Kijitonyama akaona eh Mungu kanikumbuka, kumbe shetani amemuandama mwanzo mwisho
Wakaendelea na mahusiano weee, mpaka Yule jamaa kaleta tena barua nyumbani kwa Baba Mkubwa Grace kuulizwa akakubali, wazazi wa Grace wakamwuliza mara 3 tatu Grace akasema sawa nimekubali!
Basi harusi ikafungwa Kanisani Kubwaaa ukumbini tunashangaa kweli Grace Mungu kamjibu maombi, Upo mama?
Sisi tukaserebuka nakwambia Grace anaolewa na Bonge la Bwana! Na wazazi wa Innocent walikuwepo!
Mahusiano ya miezi 2 ndoa ikafungwa wakaenda Honey Moon Kenya!
Kurudi wakafikia nyumba ya Sinza, Grace kuuliza kule kwa mwanzo akaambiwa ile nyumba haitoshi kukaa na familia akiangalia ile ya Sinza ni nzuri kuliko ya Kijitonyama!
Wakaishi mwezi wa kwanza, maisha mazuri, sisi tunaenda kumsalimia Grace kanunuliwa Gari nakwambia Toyota Prado zile za kwanza kwanza sio hizi za sasa, maisha mazuri … mwezi wa 2…mwezi wa 3… mwezi wa 4 mume akaaga anasafiri kwenda kikazi Nairobi, hapo Grace teyari ana kamimba kachanga cha miezi 3… upo mama?

Mwanaume akaenda akakaa miezi 3 akarudi Grace ana mimba ya miezi 6
Akaaga anasafiri tena anaenda Uganda kikazi atarudi baada ya miezi 2 akaenda kurudi, Grace ana mimba miezi 8.. akirudi uzuri anakaa mwezi anasafiri
Mwanaume akaaga anasafiri mwezi m1 awahi pale Grace kabla hajajifungua!
Kweli kaenda mwezi kurudi Grace akajifungua mtoto wa kike! Wakaishi miezi 2 ndio miezi ya mwisho Yule mwanaume akaaga naenda Afrika Kusini atarudi baada ya wiki 1 lakini hakurudi!

Grace akipiga simu namba aliopewa feki haipo! Akaita wazazi akawaeleza wakaenda kucheki kunakohusika, kumbe jina la Innocent aliloambiwa ni la marehemu alishakufaga miaka 5 nyuma na hawana undugu wowote na mwanaume aliemuoa Grace
Kupigia wazazi wa Innocent hamna kitu kumbe walinunuliwa tu!
Dah babake na Grace alipaniki, mpaka akaumwa Stroke, ndio Grace kuhama pale Sinza maana kodi ya nyumba ilishaisha kabisa, akarudi akawa analea mwanae na wazazi wake
Kazini kule mkataba ukaisha akatemwaaa, upoo? Baba ana Stroke, mama hana ajira Grace chali ndio kikao cha familia kikakaliwa na ndugu zake wakawa wanamchangia Grace kumlea mwanae na Grace akapewa kazi ya kumwangalia Baba Mkubwa na Mama Mkubwa!
Baada ya miaka 10 kupita, Grace akiwa anatoka sokoni akamwona mtu kama Innocent, akamfuatilia huku anajificha, akaona anaenda kuingia nyumba ya Tandale ndani ndani..
Sikunyingine akarudi tena pale pale akamkuta Yule Innocent, akachukua simu anataka kupiga nyumbani anashindwa!
Ndio akanipigia mimi, nikaja fasta, kweli kumcheki ndo mwenyewe, tukamfuatilia tukajua anapoishi tukaenda kuleta afande raia!
Akaja akaangalia, akacheka sana baadae akasema tutakuja kumkamata huyu Innocent tukamwulize maswali kwa muda wetu alafu tutawapigia!
Kweli Yule afande akafanya yake baada ya wiki tukapigiwa simu!.. kwenda tunamwona Innocent yupo ndani, tulikusanyana kikundi, familia ya Grace yote kasoro baba yake walimficha, Mchungaji aliewafungisha ndoa yani palijaa!
Wakamhoji Innocent unamjua huyu dada anakataa!
Wakaanza kumtishia akaongea ukweli wote:

Innocent: Mimi naitwa Haji, ni Dalali pale Tandale, maisha yangu ni ya kuzurura na kuhangaika tu! Sio tajiri kama nilivyoonekana, ila nilichangiwa na wale marafiki zangu 2 tuliokuja kulipia mahari ili tumpate Grace maana alituringia kwa hali zetu duni, tukaamua kujiongeza!
Wanafamilia: hawana hamu kila mtu analaani kivyake!
Akaulizwa kwahiyo utaenda na huyu mama mkalee mtoto? Maana ulishamuoa tena Kanisani kwanza umefanya uhalifu wa hali ya juu sana ina maana wewe sio tu tapeli wa mapenzi bali ni jambazi wa kutupwa wewe na wenzako.
Innocent: kimyaaa!
Grace hapo analia hali hana… ameumbukaje aibu! Aibu my dia aibu! Ameharibiwa maisha kijinga!
Basi wakaongea pale wazazi wakalaumiwa imekuwaje mnaoza mtoto hata kumchunguza huyu bwana mpaka anawafanyia utapeli na nyie mpo hapa hapa Dar
Kaka zake: wakasema kuwa walimwuliza Grace mara 3 tatu na Baba wa Grace alimwuliza Grace akasema huyo huyo anamtaka kwa hiyo wao hawakuona haja ya kwenda kumchunguza kokote!

Basi Maongezi na lawama na maushauri yakatolewa pale wakamaliza, Grace akaamua kumshitaki kwa makosa 2:
1. Kutumia jina la Marehemu wa watu kumuolea
2. Kumtapeli kimapenzi
Money Stars: du! Maskini Grace! Alikubali kuishi nae baada ya kumtoa Jela sasa?
Waiter: Wapi? Grace unamjua unamsikia?! Yule Haji alifungwaga ujue, mpaka leo yupo jela maana hela ya kumlipia fidia hana na wale wenzake 2 walienda kukamatwa wakafungwa pamoja na yule Haji! Ndio Grace akatulia!

Baadae ndugu za Grace walichanga akapatikana mwana sheria akamtalaka Yule Haji akiwa Jela, ndio sasa hivi Grace yupo huru kuolewa na mtu yeyote!
Money Stars: na mtoto je?
Waiter: anaishi kwa mama yake Grace Magomeni, ndio alimchangamshaga Babake Grace mpaka kapona stroke!
Money Stars: ivi maneno umenieleza ni ya kweli?
Waiter: sijakudanganya kama hauamini nakupa address ya nyumbani kwao magomeni mapipa… akachukua karatasi akaandika akanipa
Mama chonde chonde naomba usinitaje huko we utaangalia jinsi ya kumsaidia ila Grace yupo Frustrated! Kwanza namba yake ya simu alibadilisha tu pale alipotalakiana na Yule Haji!

Pili kwenye sherehe za familia hajagi… nilishangaa kumwona juzi alikuja kwa mjomba, hajagi ana miaka 7 sasa mwaka huu ametu-surprise alafu akawa yupo buzy na dogo mmoja sijui wanaongea nini?!
Nikamsalimia nikasepa zangu maana kazini nako kulikuwa kunanisubiria!
Money Stars: asante sana ndugu.. Ubarikiwe sasa kazi hana?
Waiter: alitafutiwa na kakake mkataba ukaisha miezi 6 iliopita!
Sijui labda kama amepata upya hakutaka kuendelea kufanya pale walikuwa wanamnyanyasa nyanyasa akaamua kuondoka mkataba ulipoisha!
Money Stars: Doh! Maskini ya Mungu, dah naumia kusikia mwenzangu amefanyiwa unyama
Na wewe sasa umeolewa?
Waiter: ndio mimi niliolewa na maskini mwenzangu zamani kabla ya Grace tena Grace alinicheka sana, sasa hivi Mume wangu ni Meneja Benki na mimi nafanya hapo Hotelini, mkataba ukiisha naacha kazi nataka nirudi kwenye biashara ambazo nazifanya wakati nimeajiriwa, nazifanya nje ya ajira hamna anaejua zaidi ya wazazi wangu na mume wangu.. Grace hajui plz usimwambie maana atazidi kuumia, unajua mimi na mume wangu tumeanzia chinii, mimi nilikuwa housegirl kwenye majumba ya watu, na mume wangu alikuwa ameishia form 6 wazazi wake wakafariki, akahangaika anagusa hapa na pale akapata hela akaenda kusoma Cartificate mpaka Degree na sasa ana Masters… tulioana Baada ya miaka 3 akiwa anafanya kazi dukani kwa mhindi anatumwa tumwa usiku anaingia Darasani, Grace akawa ananicheka unaolewaje na mtu hana maisha lakini sisi tulikuwa na malengo yetu na tunapendana!
Money Stars: nikamshukuru ndugu ya Grace, nikampa laki 3 akaondoka anafurahi mwenyewe

Waiter: Tuwasiliane jamani tumeshakuwa ndugu tujue jinsi ya kumsaidia Grace maana jana alikataa kabisa kuongea na mimi kwanini alikuwa analia

Yule waiter akaniachia mawazo sijui namsaidiaje Grace masikini na sikuelewa kwanini alikuwa anamtaka JITU!

Kweli baada ya mwezi mmoja wa kufuatilia Grace alipozaliwa na kuishi nikakuta kweli taarifa za Yule Dada waiter ni za kweli, kweli alizaliwa na kuishi Magomeni; na wazazi wake wanaishi pale pale bado!
Doh kweli kwenye maisha hatufanani!



ITAENDELEA TAR 5 OKTOBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
_____________________________________________________________________________________________


E. MIPANGO NA UKOSEFU WA MAPENZI YA KWELI…




“Baada ya lile sakata la kufanya usnichi juu ya Grace nikaamua kuchanja ramani mpya kumsaidia Grace.
                                       
Lakini Grace bwana mimi mbona namwona kama anajua anachokifanya kwenye maisha yake? Huu mchezo wa anti huruma naotaka kuuanzisha sidhani kama utaniacha salama lazima kuna mjinga ataumia na Mungu anisadiei naomba isiwe mimi, nikijikuta naumia lazima wote tuumie tu!

… unajua mtoto wa kike usimhurumie sana, hawa watoto wa kike wanakuwaga na akili nyingi sana, unaweza kudhani unamsaidia kumbe anasubiri kukupandia kichwani akupiku akae juu yake sidhani kama Grace pale ana penda maisha yangu wala ya Ulumbi shogake, ngoja kwanza nipange mipango yangu.


Aku kwani Napata kitu gani kumsaidia Grace mtu tu ambae nilisomaga naaae zamaaaan ya nini, ila huyu demu bwana ameniingilia sekta moja tu ambayo hata mimi nataka kujua yalikuwaje?
Sekta yenyewe ni JITU!
JITU bwana nataka kufahamu tangu kuondoka amekuwa na maisha gani? Na kusikia anaongeza machine yake hapo ndio nazidi kushangaa, why why waaaaaaaai?

Nikaendelea kuumiza kichwa na kupanga na kupangua nikaishia kupanga Mbinu A… B… C… D… E… F...na G ya mwisho, shughuli ya kupanga mchujo na mchekecho sio wa kitoto, ikanichukua siku 3 mpaka 5 kupanga na kupangua!

Nilipomaliza nikalala, kuja kushtuliwa na simu ya shostisto wangu flani hivi tulikuwaga tunaishigi wote Upanga miaka ya zamaani za kale! Nikawa nasita kupokea maana hawa watoto wakipiga simu buana hawamalizi simu itakuwa ya moto utaweka kwenye chaji huku bado wanataka kuongea
Simu ikaita ikakata, ikaita tena ikakata, ikaita tena kwa mara ya 3 ikakata mara ya 4 nikaipokea;

Simu: We Mwali umefungiwa wapi? Mwingine anaongea nyuma ya simu njoo hapa we chizi wee kalewa mbayaa, nikaona ohooo hapa kushakuja wakaniita niende huko wameweka hema huko Sinza ndani ndani dah hapo nina usingizi balaa,

Baada ya masaa 2 nikajongea Sinza kuniona wanalaumu wanatukana unatuweka masaa 2 kwani sisi tupo leba tunasubiria uchungu, wanatukana dah mademu wanatukana wale utadhani walizaliwa Kuzimu!

Sikuongea si unanijua mimi Money Stars, kuniita unite alafu unitukane, nikawa nawaangalia wanavyoongea wanalalamika;

Mashosti: Oh!, hamna mapenzi ya kweli sikuhizi, wanaume wanapiga bubaaa na kuondoka, wanatupiga mijeledi wanasepa, wanapiga Sodoma wanacheua, wanakupiga round 3, 4 mpaka 7 wanahakikisha wamekuweka sawa kuja kushituka wameshasepaaa unaachwa kwenye mataa ukiwa na matumaini upo kwenye mahusiano, kwani wanaume wamekuwaje lakini?

Mwanaume akianza na wewe anaanza kwa moto mkali anakufukuzia mpaka unanyegeka, mkishakuwa kwenye pick season yani honemoon stage, love on cloud 9, na akishajua tu unampenda anaanza kupunguza mapenzi mdogo mdogo mpaka anapotea. Hamna real love anymore ni drama all the way, natamani ningezaliwa miaka ya 60' or 70's kule angalau wanaume walikuwa wakweli sio mijambazi ya miaka hii.. yani wanaume wa Kibongo matatizo mwanzo mwisho.

Shoga Naive: Lakini Mapenzi ya kweli yapo jamaa, yapo hata sasa..
Shoga Alievurugwa: Mapenzi ya kweli yapo kwenye sinema tuu, Kweli nakwambia hamnaga Mapenzi ya kweli tena hata Yesu alisema siku za mwisho Upendo wa wengi utapoaaa, sikuhizi mambo ni ku-compromise na kuhemeana tu!
Wanaume wanaangalia wapi pa kuhemea, pa kutulia, wapi kuna ganda la ndizi wanahemea hapo hapo, wanaume sikuhizi wanalenga kwanza, wanatafuta mwanamke ambae kwao ana heeeeela au mwanamke mwenye helaaaa anajibanza hapo hata kama mwanamke anasura mbaya hajali

Shoga mwenye Hasira: Naive Shoga embu twambie, unamjua nani ambae mahusiano yake yamebadilika kwa usiku mmoja?
Nani?!
Hapo shoga mwenye hasira kanuuuuuna, kaviiimba usoni kafura hasiraje? uuuwi!

Naive Shoga: kweli Mapenzi ya kweli yapo unajua imetokea kwa shoga yake shogangu Kelly, wanaishi happy ever after ….kweli jaman kweli

Shoha Mwenye Hasira: yah ni kweli kweli kabisa, yani sikuzote ukisikia kuna mapenzi ya kweli utaambiwa ilitokea kwa rafiki wa rafiki ya rafiki unaemjua!

Nakwambia hapo utaambiwa walikutana kwenye mvua wakapendana waka-kiss, sikunyingine wakakutana kwa maua wakafanya na picnic wakala, wakanywa, jua lilipozama wakakimbia kuelekea jua linapozamia.. hizo ni stories kama sio movie …. Kwenye maisha ya kweli hamnaga kitu kama hichoo … ukitaka tukuamini tuambie nani mahusiano yake yalibadilika mara moja!

Naive Shoga: Money Stars hapa!

Money Stars: Nikashtuka! Mimi? Kwanini mimi?

Naive shoga: Angalieni maisha ya Money Stars na Bwana wake Handsome!
Wote: wakanyamaza kimya wananiangalia Money Stars!

Mimi nipo buzy nawaza, je ni kweli hamna Mapenzi ya kweli tena?




Money Stars: Bwana embu niacheni na ndoa yangu, mnavyoiona kwa nje ndio ivyo ivyo hamuijui, kwahiyo mimi sina cha kuwaeleza, tatizo lenu nyie mnapaniki sana, yani akili zenu zinatafuta, zipo kwenye mawindo ya kupata mapenzi ya kweli, kwanini msijikite kwenye maendeleo?
Maendeleo ya Binafsi maendeleo ya jamii maendeleo ya familia maendeleo ya ukoo, kuweni buzy na mambo tofauti na mapenzi muone kama mtawakagua wanaume na tabia zao…, mimi nipo buuuzy na kazi zangu, nikirudi nyumbani nimechoka, au nisipotoka nipo buzy nafanya kazi zangu nyumbani..

Kwanza nyie wote hapa mna AJIRA, kama ajira zenu mmezizoea si mtafute kazi zingine ambazo zinawapatia changamoto zaidi kwenye makampuni mengine?

Au kama kupata kazi nyingine ni shida, basi fungueni vioski vyenu ambavyo vitakuja kuwasaidia baadae mkiacha kazi au mkistaafu.. mtumie huo muda wa bure mlionao kazini kupanga maendeleo yenu.

Sasa kama muda wooote mnakuwa na stress za wanaume, wanaume, wanaume kila saa wanaume wamekwenda mbele wamerudi nyuma huko kwenye ajira mnafanya kazi za watu vizuri kweli au ndio mnalipua?
Sidhani kama mtu akiwa na stress za mapenzi hata kazi zinafanyika, mimi naona kama mnawaibia waajiri wenu mnaenda ofisini kuweka saini ili mwisho wa mwezi mlipwe mshahara namna hii mtaishia kuwa na performance mbaya ofisini na kufukuzwa kazi.. sasa ufukuzwe kazi alafu na stress za mapenzi juu si mtajiua nyie? Acheni ujinga, nyie ni watu wazima wote hapa endesheni maisha yenu kiutu uzima!

Wote: Kimyaa!

Money Stars: Huo ndio ushauri wangu kwenu!

Wote:  Lakini hatujui kuhusu Biashara sisi akili zetu zote zimeshalala kwenye ajira!

Money Stars: kwahiyo mnasemaje sasa?

Wote: labda utusaidie cha kufanya utupe aidia ya Biashara!

Money Stars: Nikawauliza wanapenda kufanya kitu gani nje ya ajira, kila mtu akataja yake, nikawashauri wafanye biashara ya vitu wanavyovipenda itawasaidia kuifanya kwa moyo zaidi hata kama wakikutana na changamoto watajua kuikabili maana ni biashara wanayoipenda!
Wote: sawa shoga, lakini sasa hela hatuna

Money Stars: Hee?! Mmekaa kwenye ajira mnakula mshahara wote mnatumbua tu hamsevu hela?

Wote: Kimyaa!

Money Stars: ndio maana basi hao wanaume wanawakimbia, yani nyie majinga kweli, mkipokea hela tu mnaweka kwenye tumbo, hamjui cha kulipa kodi ya nyumba, umeme, maji, mafuta kwenye gari si ndio?

Wote: ndio maana wanaume wapo!

Money Stars: sasa kama wanaume wapo hizo hela zenu mnapeleka wapi? Au mnajenga makwenu?

Wote: hatujajenga!
Money Stars: kwahiyo nyie hamna tofauti na magoli kipa sio?
Wote: sasa unatutukana sisi tuna kazi zenu
Money Stars: mmekaa kazini miaka mingapi
Wote: zaidi ya 5
Money Stars: na hamna hata 100?
Wote: kimya!
Money Stars: kwahiyo mnataka mimi niwasaidiaje maana nondo nilizowapa mpaka sasa mlitakiwa mnilipe!
Wote: aaah we nae, si unatusaidia shogaetu
Money Stars: kwani nyie shule mlisoma mpaka wapi?
Wote: chuo tulimaliza
Money Stars: kwahiyo nyie wote mna Degree au certificate au Diploma au?
Wote: tuna Diploma
Money Stars: kweli kazi ipo!
Mnaonaje mkijisomesha? Mkajiendeleza na elimu
Wote: oh! hapana bwana akili zetu zimeshazeeka sisi tunawaza machine na burudani kusubiria kufa
Money Stars: kwahiyo sasa mnataka nini kwangu maana kila kitu naona mmeshajipangia… kama ajira mnazo na machine mnapata.. subirini kufa msiwalalamikie wanaume
Wote: sasa unasusa Aunty?
Money Stars: mimi naona mnacheza na akili yangu hampo serious na maisha yenu, ngoja mimi niondoke niende kwangu; hapa mnanifilisi na kuninyonya damu kimaarifa na kucheza na akili yangu, mkiwa serious na maisha yenu mtanitafuta tena mnilipe kwa kila ushauri laki 3 kwa kila mmoja tena hapo nimewapunguzia ningewafanyia laki 5…. La sivyo endeleeni kulalamikia wanaume mpaka mfe… mkitaka kuishi mnajua pa kunipata!
nawaambia mkiamua kufunga milango ya wanaume mkawa buzy na kazi zenu na maendeleo yenu mtashangaa wanaume wa maana wasio-pasua kichwa watakuja tu
Mkiendelea kuweka vichwa vyenu kwenye mambo ya wanaume sijui wamefanyaje mtakufa mkiwa hai mnajiona, huo ndio ushauri wangu…
Wazungu wanasema the Opposite Attracts, unataka Mume mwema mwombe Mungu alafu jishughulishe na mambo mengine tofauti na mapenzi, ukijikita kwenye mambo mengine tofauti na mapenzi buzy na mambo yako mambo ya Mapenzi yatavutika kwako ndio maana ya Opposite Attracts!
Anywho nawahi kwangu nikaangalie familia…

Mashoga: Oh Penny baki tafadhali tutakulipaa…utupe maujanja ya biashara na mambo mengine ya maendeleo plz plz plz….

Money Stars: Nikibakia hapa wekeni laki 6 mezani ndio nabaki.. na elfu 30 ya fuel na chakula nakula hapa na vinywaji mnaninunulia hapa…

Mashoga: wakashauriana hapo wee wakateta amimi nipo buzy na simu, mara naona wanaingiza mkono mfukoni, wanatoa hela, wakakusanya mmoja wao akanipatia laki 6 cash! Mwingine anaita waiter njoo msikilize taajiri yetu hapa, mwingine anasema enhe shoga tupe nondo mama tukawatese wanaume wametusumbua sana!

Money Stars: Nikapokea laki 6, na elfu 30 juu ya mafuta ya gari, nikahesabu si unanijua halfa cast wa kichaga mimi, kweli laki 6 na elfu 30 nikaweka kwenye mfuko wangu wa Jeans, Kinywaji kikaja nikaanza kunywa taratibu, mashoga wamefungua ma-Ipad zao wanasubiria kuandika

Nikawapiga darasa pale, warembo wakakolea, pombe zote zikaisha kichwani walizokuwa wanakunywa wakahamia kwenye maji ya kunywa!

Darasa nikaliendesha pale kiroho safi, tena kwa pozi na kuku choma ikaja nikaitafuna vzuri sana, haina kuremba, naanzaje kuremba labda? Fursa ikija lazima ujitoe kimaso maso!..

Mpaka masaa 2 yanaisha, watu wanaliaaaa, tulikuwa wapi, jamaaani, hatuelewi, hawa wanaume wametuloga, basi kila mtu analalamika kivyake!

Money Stars: hawajawaloga wanaume wala nini, mmejilogesha wenyewe kwa wanaume, kwani nyie si mnazo akili za kuzaliwa? Mwanaume ameishikiliaje akili zenu ni nyie mmewaruhusu wawaburute ndio maana mnateseaka

Mashoga: oh Bibie punguza basi maneno makali ujue pombe zishaisha akilini hata usingizi hamna, wakakubali kujisomesha, kuhama nyumba walizokuwa wamepangiwa na wanaume zao na kuanza maisha yao mapya na kufanya kazi kwa bidii maana walikuwa wanalalamika mishahara midogo kumbe utendaji kazi wao ni mbovu…

Money Stars: sasa wapendwa, mimi nina deal la hela, kwa nyie mnaotaka kufanya biashara hamna mtaji hili deal litawaingizia mamilioni ya hela mnaweza hata kuacha kazi, lakini sijasema muache kazi, nikiona unaniletea mambo ya kipuuzi mambo ya kijinga nakutoa fasta na ukiniharibia tu urafiki na wewe umeisha, je mnalitaka hili dili?

Wote: Leta Pesa hio tupe tupe tuchangamshe akili maana we mtoto una akili wewe mjinga una akili wewe embu tuamshe mama tumelala sana..

Money Stars: lakini hamna kuacha kazi, mkiacha kazi nawakata kwenye deal langu

Wote: eh tukale wapi? Hatuachi!

Money Stars: Nikawapa kiduchu cha mipango yangu juu ya JITU, Ulumbi, Harrieth na Grace!
Nikawaeleza kiduchu kuhusu JITU na jinsi alivyowatandika watoto wa watu na machine yake kubwa, anawaumiza vichwa wadada mjini kwa hela yake
Shoga mwenye Hasira: hio ndio nyama yangu naitaka salama nimpigeee nimalizie mahasira yangu yote juu ya wanaume
Shoga Naïve: Stars hii show kali nahisi ntaishia njiani sitaweza, Punda tena?
Shoga Alievurugwa: Mimi show yeyote napiga niambie nakaa mlango gani wala hutajuta! Ila mshahara ngapi mama?
Money Stars: ELfu 30 kwa siku
Wote: Nini? Hata kazini hatulipwi hivyo
Money Stars: lakini sio kila siku maana mmeajiriwa hizi kazi zitafanyika usiku na weekend sana, sasa kama mnasoma hamtaweza!
Wote: hio ndio nzuri Overtime yetu!
Money Stars: lakini kuna jambo moja tu!, kila weekend kabla hamjaingia kwenye kazi lazima niwape brief
Wote: sawa hamna shida Boss
Money Stars: na tukianza hamna kuacha atakaeacha atanilipa! Hii safari sio rahisi kama mnavyodhani jamani kweli mtaweza?
Wote: Poa tunaweza na tutaifanya vizuri sana usijali hatutakuangusha…
Money Stars: ok tuonane kesho tusaini Mkataba maana nyie nahisi mtaniharibia mbaya hasa huyu Naïve! Kesho j2 tukutane … nitakuja na mwanasheria wangu … atawapa makaratasi mtasoma mkikubali msaini, mkikataa poa siwafosi…
Wote: Poa Boss wetu kesho saa ngapi
Money Stars: saa 8 mchana sharp ukichelewa ushafeli interview
Wote: asante sana
Money Stars: msinishukuru sasa, mnishukuru Baadae mambo yenu yakikaa sawa, plz alafu kama kazini hamfanyi vizuri nawatoa kwakweli sitaweza
Shoga Alievurugwa: kwahiyo kama ukitaka kufanya kila siku kazi kwako je tunaruhusiwa
Money Stars: yah lakini si umeajiriwa mama
Wote: Wakaangaliana,  wakamwambia bora useme ukweli mama
Shoga Alievurugwa: My dia, mimi kazi sina, nimefukuzwa jana
Money Stars: heeeee?!
Shoga Alievurugwa: mimi nimevurugwa hapa nina stress za mapenzi na kazi doh yani hapa ulipoongelea pesa nashukuru kweli… kwahiyo mimi nitakufanyia kazi full time…ndio hawa wakaamua kunitoa out wanipoze nipunguze stress
Money Stars: doh! Hii kazi lakini poa ila mimi silipi kodi yako ya nyumba wala hela ya usafiri, mshahara naokupa ukutoshe
Shoga Alievurugwa: embu ngoja, elfu 30 mara siku 30 ni Tsh laki 9 (Fair).. hamna shida nitafanya..
Money Stars: tutaonana kesho warembo, we bibie uliovurugwa hii hapa laki 2 yako itakusaidia nauli kuja kesho na safari zingine zote, malipo yenu ya kazi mwisho wa mwezi alafu sina huruma na kazi zangu, ukinizingua nakudunda kweli kweli..

Wote: sawa boss

Money Stars: tuonane kesho saa 8 mchana sawa?

Wote: Sawa Boss Lady!


ITAENDELEA KESHO TAR 20 OKTOBA 2018 SAA 12 JIONI YA TANZANIA.
_______________________________________________

F. GANG-SISTERS A.K.A 3L…


Kesho yake saa 7 dk 45 mchana warembo wakaja mhali tulipokubaliana… Shoga alievurugwa, shoga mwenye hasira na shoga Naïve wamependeza wenyewe wana hasiraje na wanaume.. ahahhaha utadhani wanakuja Beijin kupanga sheria za Haki za akina Mama na wanawake bwana au wanakuja kuonana na Muumba kuleta madai yao
Shoga alievurugwa: amefunga usongo utadhani Rambo anaenda vitani, hahahahaha
Shoga Naïve amevaa Miwani asije onekana na watu wanaomjua
Shoga mwenye hasira amevaa jeans na lipstic nyekundu! Si unajua tena rangi nyekundu inakuwa na maana gani, hahahah warembo wamejipangaje?! Wanasukuma masanduku yao kama wanaenda Ulaya kumbe hapa hapa kwetu…
Mimi na Mwanasheria wangu tulishatengeneza ramani yetu kuubwa tu, tukawa tunacheka kuwaona walivyopigilia, wameshasahau hatuishi vitani, hawa mademu wa wapi?

Wakaja tukasalimiana na kutambulishana nikaanza kuwatania, wenyewe wamenuna nyuso za mbuzi wapo serious wanasubiri kusaini mikataba! Mikataba hio vipi?

Baada ya Utambulisho mrefu, wakaanza kusoma makaratasi, kwani wanaelewa sasa? Kidhungu kitupu! Wakaomba watafsiriwe, wakatafsiriwa uongo mtupu mimi kicheko kimenibana haki nachekea tumboni, wao wapo makini jomooni elimu wakati mwingine usipo kuwa nayo unaumizwa vibaya mno!

Wakadanganywa hapo wakasaini kweli Mwanasheria wangu wa kuunda unda akaondoka,
Money Stars: hawa warembo bwana wanamajina yao,
Shoga alievurugwa anaitwa Lina
Shoga Naïve anaitwa Lola
Shoga Mwenye Hasira anaitwa Lila

Money Stars: Lina wewe unaondoka na mimi na masanduku yako, tunaenda kwenye nyumba moja ivi, utakuwa unaishi huko na Lola na dada mmoja anaitwa Grace… nyie wawili hamna kuwasiliana na mabwana zenu wa zamani, mkiwasiliana nawatoa mkataba wenu na mimi umeisha… nyie wawili namba zenu za simu ni hizi hapa na hizo simu zenu naziomba, nikapewa simu zao nikaweka mfukoni, nikawapa mamba zao na simu zao mpya za tochi.. wakaniangalia kama natania au nipo serious?! Kumbe mimi nimemaliza!

We Lila, funguo yako ya nyumba mpya hii hapa, utakuwa unaishi Kijitonyama ndani ndani huko, hamna kuwasiliana na mabwana wako wa zamani tena, alafu mambo ya kujishaua kujiongelesha ongelesha kwa majirani kama hauna akili nzuri, nikiskia nakutoa!
Lila kimyaaa! Baadae akajibu sawa madam boss leide!
Tukamsindikiza Lila mpaka kwenye nyumba yake mpya, akachoka, chumba kimoja kina choo ndani, hamna Tv hamna nini, kalalamika mwenyewe nikamwambia hela nayokulipa nunua Tv, nunua Gari, nunua masufuria hainihusu we si unataka ajira bwana, kwaheri, tukaondoka na Lola na Lina haooo mpaka kwa Grace

 

Grace anashangaa anagongewa mlango utadhani hajalipa kodi, kufungua nikamsukuma namwambia wasaidie ndugu zako hao wametoka chuo!
Wakasaidiana masanduku, kila mmoja akaonyeshwa anapolala,

Money Stars: oya! Mwisho wa mwezi nakuja kuchukua kodi, wewe Lola andaa laki 3, Lina andaa laki 3, we Grace andaa laki 3…

Grace: Mimi sina ajira

Money Stars: hawa unaowaona ni ndugu zako, wamepata ajira leo, na wewe kazi nimeshakutafutia, kuanzia kesho j3 unaanza kazi

Grace: akafuraaaahi mwenyewe, mshahara bei gani?
Money Stars: huyu anaitwa Lola na huyu anaitwa Lila ndio room mate zako, mkae kwa amani nisiskie mnaibiana mabwana sijui mnapigana mkipigana tu nawatoa sawa?

Wote: sawa Boss Lady

Money Stars: we Grace mshahara wako kwa siku elfu 10,

Grace: kazi nafanya lini mpaka lini? Likizo vepe?

Money Stars: we unataka kazi au unataka kurudi kwa wazazi wako? Mbona maswali kama polisi?

Grace: sawa madam nakusikiliza

Money Stars: Kesho mtafute shogako Ulumbi, mwambie unataka ajira, hata ya usafi nyumbani kwake mwombe
Grace: uuuwi Money Stars, unanipeleka kwa JITU tena?

Money Stars: usiponisikiliza huyo JITU utaishia kubakwa kiboya boya yani usiponiskiliza wewe utakuwa unaumizwa kila siku sasa wewe jifanye machi nooo, endelea kuongea kama hutaki hapa kwangu ondoka usituletee usiku sina huruma na wewe kabisa

Grace: sawa Boss Lady!

Money Stars: Kesho unaondoka na Lina muende kwa Ulumbi kesho saa 5 asubuhi anawasubiria pale The Slip Way, mkifika mwambie Lina ni mdogowako wa kijijini wote mnatafuta ajira hawezi kukunyimeni, ila lazima mlie lie mpaka mwisho mkijidai mmeshiba imekula kwenu na mkiondoka kwa Ulumbi hamna ajira tusijuane!
Lina utakuwa House Girl kwa Ulumbi na wewe Grace utawekwa kwenye ofisi ya Ulumbi,

Grace ukiulizwa unaishi wapi mwambie unaishi Sinza na Lina ukiulizwa unaishi wapi mwambie unaishi Mpwapwa kijijini!

Lola, nataka uongee na Grace, akueleze kuhusu Harrieth muwe ma best, mkishakuwa ma best nipigie nitakupa ramani

Lila ukishaenda nyumbani mwa Ulumbi kama tulivyoongea naomba umkatalie JITU, usitembee nae kabisa, ukitembea nae umeharibu, wewe fanya juu chini usitembee nae, kwanza Yule bwana ana ukimwi, sasa nenda kachizike na zile hela umeumia sawa mama?

Lila: Sawa boss!

Money Stars: Na hili Body lako, sema una miaka 58, bibi wajukuu 3, watoto wako wanaishi Arusha, mumeo alishafariki miaka 5 iliopita, mfanye JITU awe rafiki yako na sio mpenzi wako, mshauri kwa kila kitu, akishakuwa rafiki yako nipigie simu nitakuambia cha kufanya

Lila: sawa boss leide!

Money Stars: Lila, mama usiharibu tafadhali tafadhali! Nakujua akili zako zimechelewa kukua, mtu unaeenda ku-deal nae ni mwehu zaidi ya mwehu, alafu ana akili mbaya, kwahiyo wewe nenda nae mpwela mpwela hivyo hivyo jidai akili huna zinachelewa lakini nataka akili yako ipae, akikutukana wewe mpende, akikudharau wewe mpende, mwisho wa siku atakuona zoba, jinga, ataanza kukutumia, ukifika hapo nipigie simu akiwa hayupo nitakusaidia cha kufanya next!

Money Stars: nikawaaga nawaambia mwisho wa mwezi naja chukua change laki 9 staki ujinga asietoa laki 9 namtoa! Nikaondoka nikawaacha wanaongea wanafahamiana wanapeana majukumu. 


Kesho yake saa 4 asubuhi kweli nikadondoka The Slip Way, nikaenda kujibanza sehemu, namwona anaingia Ulumbi akakaa akaagiza kinywaji, mara akaingia Grace amevaa choka choka Fulani hivi kumwangalia Lina sikuamini, kama kibibi cha kijijini kila mtu anamwangalia huyu mama ametokea wapi?

Wakafika kweli wakaongea na Ulumbi, ulumbi anashikilia pua kuashiria Lina ananuka, anamwuliza Grace umemtoa wapi mimi mbavu sina!
Wakaongea kama lisaa limoja, wakaondoka wote wa-3, nikawa najiandaa kutoka niondoke mara namwona JITU na Harrieth wanaingia, wameshikana mikono wanacheka wanatembea, doh nilisikia moyo umesimama! Jitu akiniona hapa itakuwa msala mkubwaa, nikampigia simu Lola, akaniambia yupo maeneo ya Masaki,

Money Stars: Njoo fasta kama unajipenda,
Baada ya dk 20 Lola akaja, akakaa kwa pembeni akamcheki Harrieth anavyojishebedua na kujichekesha kwa JITU, akasoma ramani nzima ya pozi lao na waiter anaewahudumia, akasubiria waiter wao arudi tena, akamfu kwa nyuma, alipofika kwa akina JITU akamkuta waiter anamwekea kinywaji Harieth… akamsukuma waiter akamwagia Harrieth kinywaji chake na waiter akaanguka chini,

Harrieth: akapiga makelele nakwambia utadhania yupo labor!
Huo ugomvi wake sasa doh!
Harrieth anatukana mwanzo mwisho aibujeee!

Lola nae alishajiangusha chini, JITU akamwona akaamka haraka haraka akamwinua Lola, Harrieth kanuna anagombana na waiter watu wanawashangaa, baadae Lola akamwinua waiter akamwomba msamaha, Manager akaja pale anaulizia ulizia kuna nini, waiter akaombwa aondoke,
Manager anaomba msamaha pale na nini, wakabakia Lola, Harrieth na Jitu!
Jitu sasa anavyomwangalia Lola, utadhani sijui nini?
Lola: akaomba msamaha kwa Harrieth, akatoa kwneye pochi yake top nzuri nzuri, pole my dia, kama hautojali naona shirt yako imeharibika twende toilet ukabadilishe hii Top uvae yangu sio vizuri kukaa na nguo chafu,
Harrieth akamwangalia Lola, Jitu akamruhusu aende wabadilishe kweli ile nguo wakaondoka!

Money Stars: baada ya kuona JITU amebakia mwenyewe nikasema sasa huu ndio muda wa kwenda kumfunga paka kengele, nikainuka na kofia yangu na miwani uzuri meza ya JITU ilikuwa mbele yangu kwa sana, nikaenda nikachukua kinywaji cha mtu mwingine nikatembea mpaka kwa JITU, nikasimama mbele yake hakuniona alikuwa buzy na simu

Money Stars: Manyanga mzima?
JITU: akainua shingo aangalie nani huyu? Aliponiona alishtukaa, nikachukua kile kinywaji nikammwagia machoni akaanza kuhangaika kufikicha macho mimi ndukiii, akaja Meneja nadhani aliona, akaanza kumsaidia mimi nishafika mbali namchungulia JITU anavyohangaika na macho!
Alipokaa sawa anamwuliza Meneja kuna demu alikuwa hapa amenimwagia kinywaji yupo wapi?

Meneja: ameondoka Yule, JITU akainuka anikimbilia Meneja akamtegeshea mguu akaanguka chini Meneja akaondoka, mara akina Harrieth na Lola haooo wakarudi wanacheeka wenyewe wanafurahi, walishapatana Chooni walipoenda wanashangaa kumkuta JITU ameanguka chini anahangaika kuamka!

Harrieth: akamzoa zoa pamoja na Lola, wakamweka kwenye kiti wanashangaa mbona Macho ya JITU yamekuwa mwekundu, hapo hamna tena cha kusubiria Harrieth anataka JITU aende hospital, Lola akamwambia Harrieth mimi nitaendesha gari yangu twendehi Hospital, wakawahi kwenye gari ya Lola, hao mpaka Hospital

Baada ya masaa 2 namwona Ulumbi nae anakuja fasta, mimi nipo kwenye Parking na dereva naona kama movie vile!

Nikakaa Parking masaa 4 ndio naona Lola anaondoka na Harrieth wanakimbia!

Baada ya Nusu saa namwona Ulumbi anatoka na mumewe JITU, amevaa miwani! Ameshikiliwa haoni!

Money Stars: nikashika midomo nasema Mungu weee nimeuaaaa! Baba wa watu masikini, wakaingia kwenye gari na mkewe Ulumbi haooo mpaka kwao, nikarudi zangu kwangu!

Baada ya wiki 3 nikapigiwa simu na Lola, kuwa yeye na Harrieth walishakuwa mabest

Baada ya wiki 4 nikapigiwa simu na Grace kuwa amepata kazi kwenye kampuni ya JITU, kama Secretary Msaidizi wa JITU…

Lina anafanya kazi kwa JITU kama House Girl Incharge anapika, anafua, anapeleka mtoto shuleni, ila usafi wanakuja kampuni ya usafi inafanya usafi!

Money Stars: nikasema safii.. kila kitu kinaenda kama nilivyopanga, nashukuru Mungu kwa ajili ya hawa warembo akina Lina, Lola na Lila - a.k.a 3L.


TUONANE KESHO J2 TAR 21 OKTOBA 2018 

 SAA 10 JIONI YA TANZANIA..

_______________________________________________ 
G. HUJAFA HUJAUMBIKA...

Money Stars:
Baada ya Sakata la Jana, dah roho iliniuma, nikajiambia hii sasa tushafika mbali pabaya, hii kesi ishakuwa sasa!

Nikampigia simu Grace kumwuliza yaliojiri baada ya wiki 10 kupita na kudai hela yangu ya kodi ya nyumba:
Grace: Jioni uje uchukue nyumbani sasa hivi nimebanwa na kazi nitakupa habari zote za JITU!

Money Stars: nikampigia na Lina, kusikia mrejesho wa JITU na mkewake
Lina: JITU tumeshakuwa rafiki, ila kama unavyojua mamcho yake haoni vizuri, huu ndio muda mzuri wa kuja kuongea nae
Money Stars: mke wake yupo wapi? Naanzake kwanza kuja?
Lina: nimewaambia nina binti mkubwa anaishi Arusha, wewe utakuwa binti yangu, mkewe ameenda mkoa kumchukua baba yake na JITU, huu ndio muda wa wewe kuja wanarudi baada ya siku 3
Money Stars: sawa nitakuja usiku saa 3, hakikisha hizo CCTV zimezimwa staki matatizo mimi…nikakata simu roho inaniumaje!
Nikamcheki Lola na Harrieth wamefikia wapi,

Lola: tupo pazuri Boss lady usiwe na wasiwasi, hawajaonana na JITU tena, sasa hivi Harrieth yupo na Bwana Mwingine
Money Stars: utanipa feedback, jitahidi asijue unapoishi
Lola: sawa madam!

USIKU SAA 3:
Nikaingia kwa kupitia geti la nyuma nyumbani kwa JITU, mtoto ameshalala, Ulumbi hayupo, walinzi wapo upande wa pili anakula, nyumba iko kimyaaaa!
Nikapelekwa chumba cha JITU alikuwa amekaa kwenye kiti anaangalia dirishani

Lina: Fanya haraka madam, mlinzi akimaliza kula anarudi getini itakuwa shida kukutoa na CCTV hazizimwi zaidi ya lisaa limoja kampuni itaanza kupiga imu, una dk 20 tu…

Money Stars: nikamsogelea JITU, nikamshika mgongoni,
JITU: akashtuka, haoni kweli anauliza nani wewe ni Lina?
Money Stars: Manyanga nimefurahi kukuona! Pole sana na kuumwa
JITU: Money Stars? Ni wewe?
Money Stars: Akanishika mkono kwa nguvu hataki kuniachia, nikapiga magoti nikaweka mikono yake kwenye uso wangu, akawa ananipapasa masikio, macho, mashavu… ndio ni mimi
JITU: noooo, haiwezekani, wewe ulishakufa miaka 30 iliopita
Money Stars: Manyanga bwana hauachi,
JITU: kweli sauti kama ya Money Stars, umefufuka? Haiwezekani akaanza kutoa machozi, kweli ni wewe!
Money Stars: nikapapaswa mpaka kusikopapasiwa na mtu asie mumeo wako, tobaaa!
JITU: ni kweli ni wewe, ingawa sioni lakini ni wewe, imekuwaje nimeambiwa umekufa,
Money Stars: nikainuka nikamkalia kwenye mapaja, imekuwaje unatesa watoto wa watu, imekuwaje umekuwa kipofu Manyanga?!
JITU: hata mimi sielewi nimekuwaje kipofu, kuna mdada alikuja pale slip way akaniita jina akanimwagiwa wine usoni, lakini huyo dada alikuwa kama wewe, ana sauti yako
Money Stars: una maana mimi ndio nimekuweka ulemavu?.. nakuweka ulemavu wakati mimi nimeshakufa?
JITU: lakini uko hapa nakushika nakusikia
Money Stars: hilo ndio tatizo, mimi nilishakufa miaka 30 iliopita,
JITU: haiwezekani, wewe ni nani mbona unaongea kama money stars?
Money Stars: inabidi uwe na imani na maneno yangu na uwe mwangalifu na unayoyasema la sivyo sitakuja tena kwenye maisha yako!
JITU: kweli wewe ni Money Stars, nimekumiss mpenzi wangu… ulienda wapi?
Money Stars: shhhh! Nikamkumbatia, baada ya muda nikamwinua, tukaanza kucheza blues, huku naimba wimbo wa Moon light lady, nikimwangalia JITU anatoka machozi haamini….. nitakuja kukutembelea kwa masharti tu, kama hautasema kwa mtu kuwa nimekuja kukuona….
JITU: usiondoke tafadhali mke wangu hayupo
Money Stars: inabidi niondoke ikifika saa 6 usiku, na sasa ni saa 5 dk 55.. nina dk 5 tu
JITU: kwanini ulikufa mpenzi wangu
Money Stars: kwanini umeongeza sehemu zako za siri Manyanga? Ina maana bado haujanisahau?
JITU: akanyamaza kwa muda… baadae akajibu ni kwa sababu yako, nilikupenda sana ukaenda kulala na baba yangu, ukaniambia nina kibamia
Money Stars: Maisha yameshaenda miaka 30 bado haujanisahau? Una mke na mtoto mmoja kwanini unawatesa namna hii?
JITU: Huyo sio mtoto wangu
Money Stars: ina maana mke wako amechepuka ukiwa kipofu?
JITU: Mke wangu amezaa na baba yangu mzazi, niliempenda alitembea na baba yangu mzazi, sina maisha tena.. nipo nipo.. hata ingekuwa ni wewe lazima ungechanganyikiwa kama mimi…
Money Stars: kimoyomoyo nasema tobaaa! Kweli Mzee Manyanga Senior ni noma ana-njaa kweli na ulafi na vitoto vidogo vidogo du! huyu mzee habadiliki?!…
JITU: tangu nimuoe Ulumbi, sijawahi kutembea nae, nilimwoa siku hio hio ya Honey Moon amelala na mimi usiku akachomoka akaenda asipokujua, kumfuatilia kumbe yupo chumba cha pili na baba yangu mzazi….Na wewe Ulikufa…hapa nilipo nilishafeli kabisa kwenye suala la kukusahau.. kama haujafa kweli turudiane tafadhali sina raha sina amani nipo nipo tu…
Money Stars: Nikamwangalia JITU analia hana raha, kwanini usiachane na Mkeo mambo yote hayo mmefumaniana kwanini mnakaa pamoja kama hampendani?
JITU: acha tu! Nikiachana nae tunapasuana mali nusu kwa nusu…na nikiachana nae ataenda kwa Baba yangu kuvunja ndoa ya mama yangu na kuwa mke wa pili…
Money Stars: Manyanga, pole sana lakini ndoa yako ilishakufa kabla hamjaoana!... mali kitu gani achana nae, utakuja kufa mapema kabla siku si zako!...Muda wangu wa kurudi nilipotoka umefika, tutaonana tena siku nyingine…
JITU: plz usiondoke tafadhali, nasikia raha kukaa na wewe!
Money Stars: nitakuja kukuona kwa masharti kama hautamwambia mtu yeyote…
JITU: sitomwambia mtu tafadhali usiondoke… baki na mimi
Money Stars: kama kweli bado unanipenda, usiumize watoto wa watu kwa machine yako ulioiongeza, plz
JITU: sawa… tafadhali ukae
Money Stars: utanisubiria na utakuwa mwaminifu kweli?
JITU: kweli nitakusubiria mpenzi,
Money Stars: Nitakuwa nakuangalia kutoka juu, ukitembea na mwanamke nje ya ndoa sitakuja tena..
JITU: nakuahidi sitatembea na mwanamke mwingine mpaka urudi
Money Stars: chukua hii dawa, uwe unapaka, asubuhi ukishaamka na usiku ukiwa unaenda kulala, kwa muda wa mwezi mmoja, alafu…
Lina: akaingia, Boss mbona umesimama unaongea na nani?
JITU: nani wewe? Nani kakuita (kwa ukali)
Money Stars: nikamwachia mikono fasta nikakimbia
Lina: nimeskia kama unaniita
JITU: sijakuitaaa tokaaa,
Lina: akamsogelea, boss umesimama ngoja nikusaidie ukae
JITU: kanuna anatafuta tafuta hakumpata anaemtafuta, akaishia kupanda kitandani, Lina akamfunika shuka, huku ameishikilia ile dawa kwa uaminifu akalala
Lina: akatoka na mimi, kuangalia mlinzi nae anakuja kurudisha sahani ya msosi, kaa hapa nyuma ya mlango, akishapita wewe toka
Mlinzi: mamaa, asante kwa chakula,
Lina: Kaka ingia naomba uje unisaidie boss ameanguka njoo
Mlinzi: akaingia fasta anapanda ngazi kuelekea chumba cha JITU,
Money Stars: nikatoka nduki mlango wa nyuma huyoooo, hapo saa 4 kasoro usiku, nikaenda kukutana na dereva wangu mbelee tukarudi nyumbani…

Baada ya mwezi 1, Lina akanipigia simu kuwa tangu niondoke, JITU amekuwa na furahaaa, akipelekwa Hospital maendeleo yake mazuri, anakula, anacheza na mtoto, amebadilika kweli kwani umempa nini Boss Lady?

Money Stars: wewe fanya kazi yako, baba mkwe ameshakuja hapo

Lina: yupo, kuna makubwa huku yanaendelea Money Stars hata sielewi nikuelezeje

Money Stars: enhe kuna nini?

Lina: kwani huyu Mke wa JITU anatembea na baba mkwe wake?

Money Stars: weeee! Usiniambia! Umewaona wapi?

Lina: kila siku usiku huyu bin Ulumbi anaingia chumbani kwa baba mkwe saa 6 usiku anatoka saa 11 alfajiri

Money Stars: weeee! Sasa best embu nipatie izo video au picha basi za huyo mama kuingia kwa baba mkwe, na mama mkwe yu wapi?

Lina: Mama mkwe aligoma kuja akadai JITU aende kijijini yeye hawezi kuja hapa.. hata hivyo Ulumbi alishafukuzwa kijinini aliishia mjini, akamsubiria baba mkwe wake aje mjini wakaja nae huku

Money Stars: nakuomba sana kama itakuwa kwenye uwezo wako, nitafutie picha za huyu ulumbi na baba mkwe wamelala pamoja, unadhani utaweza?

Lina: nitajitahidi

Money Stars: ukizipata niambie tuonane

Lina: Madam kesho tunaenda hospital na JITU na dereva, utataka muonane?

Money Stars: nitakuja hospital, nipe jina la Dokta wa JITU kwa sms le oleo kesho tutaonana huko hakikisha dereva haji

Lina: sawa Madam!
Baada ya nusu saa Lina akanitumia jina la Dokta wa JITU nikaanza kuhangaika nae,

Kesho yake, nikajiwahisha kabla ya Muda, wakaingia JITU na Lina na dereva, Lina akamwambia Dereva asubirie nje kwenye gari, wakaingia kwa Dokta baada ya Dk 10 dokta akaja kunichukua tukaingia wote, akaongea na JITU maendeleo yake ya macho na nini akaambiwa kuhusu opereshen JITU akakataa anataka akafanyiwe opereshen nje ya Africa, Dokta akamsihi wamfanyie hapa lakini wapi

JITU: nina wiki 2 zimebaki nimeshabook appointment na dokta wangu nje nikafanyiwe opereshen

Dokta: sawa Bwana JITU, nisubirie hapa nikaprint barua yako nije kukupa tayari … dokta akatoka akabakia Lina, Jitu na mimi

Money Stars: nikasogeza kiti, nikamshika mkono Jitu, Manyanga mzima? Usishituke hamna mtu anaeniona dada yako ametoka na dokta

JITU: Money umerudi

Money Stars: nimefurahishwa na maendeleo yako tangu tumeachana

JITU: Nilikuahidi mimi ni mtu wa ahadi

Money Stars: unaenda wapi kufanyiwa opereshen ya macho?

JITU: naenda Uingereza,

Money Stars: nani anakusindikiza?

JITU: naenda na Lina na Mama yangu Mzazi

Money Stars: pole sana, ukirudi mambo yatakuwa yamekaa sawa

JITU: nikirudi nitakuona Money wangu

Money Stars: nitakuwepo kwenye opereshen yako usijali

JITU: akafurahi mwenyewe

Money Stars: ila sitokaa sana, muda wangu wa kukaa kwako umeshaisha

JITU: usiondoke mpenzi kaa tu si umesema hamna anaekuona

Money Stars: na Ulumbi nae haendi Uingereza?

JITU: sitaki hata kumwona kila siku anatembea na baba yangu mzazi

Money Stars: huu ndio ulikuwa wakati wa kumkamata Ulumbi, umejuaje anatembea nae wakati wewe hauoni?

JITU: halali kitandani kwangu, usiku anaondoka anarudi kumeshapambazuka, namsikia anavyoondoka na anavyorudi ijapokuwa najidai nimelala

Money Stars: JITU tutaonana, nikainuka nikaondoka, ile nimetoka tu nimeshasogea mbele namwona Baba yake mzazi JITU anaingia na Ulumbi, dah bado kidogo nikamatwe huo ungekuwa msala mkubwa haujawahi kutokea!
Sikuonana na JITU tena tangu siku ile ya Hospital, mpaka anaondoka Airport kwenda kwenye matibabu Uingereza, kweli alipelekwa na mama yake mzazi na Lina baasi… nilimhurumia JITU sio kwa yale mateso, doh wanawake wengine wana roho ngumu, unatembea na baba mkwe wako mpaka unazaa nae kabisa na bado mume hakuachi?!
Shikamoo Ndoa za Kikristo!

Baada ya wiki 1 Lina akanitumia email ya picha za Baba yake JITU na Ulumbi wanatembea pamoja na videos whatsapp, … aibu mpenzi msomaji aibu huyu ULUMBI kama Jezebel wa siku za mwisho, hajali analenga sana, ila nani wa kumfunga paka kengele kama sio rafikiwa Ulumbi?!

Ngoja JITU arudi anaona tuanze kumchezea Ulumbi akili mpaka aachane na JITU, JITU ameteseka vya kutosha miaka 30 mtu anateseka tu, ila wanaume wana-moyo! Huyu JITU akifika miaka 50 na akaendelea kukaa kwenye mateso atakufa na umri mdogo kwa stress…

Baada ya wiki 1 nikaambiwa na Lina kuwa Opereshen imeenda vizuri na JITU anaanza kupona anaanza kuona kwa mbali sana…

Nikakwea pipa nikadondoka Uingereza moujaaaa!


Tuonane KESHO Tar 23 OKTOBA 2018, Saa 1 usiku ya Tanzania

_______________________________________________


SEHEMU YA 2
A.   PLAN A – KALALA TAJIRI, KAAMKA MASKINI



Kufika Uingereza, najiandaa sasa niende Hospital hapo nimechoooka kweli kweli (Jet Lagged) … nguvu zikaniishia nikaamua kujituka kitandani na kulala..
Baada ya masaa 3 nikaamka, nikajiandaa, naangalia whatsapp nakuta missed call kibao toka kwa Lawyer wangu…
Kumpigia hapatikani, kufungua sms nakuta sms kibao… kilichonichosha ni jumbe nilizozikuta huko kwa whatsapp na picha na video kibao zilinichanganya nikataka kurudi kwetu siku hio hio lakini dah!
Huwezi amini nimetumiwa picha za Baba yake JITU na Ulumbi waki-DO!

Nimetumiwa Picha za Lina na JITU waki-DO pia!

Nimetumiwa picha ya Lola na Harrieth wakisagana!

Yeeeesu nilichanganyikiwa, nikiwa katika hali ya kuchanganyikiwa Lawyer wangu akanipigia kunielezea mkanda mzima,

Lawyer: Best, hawa madada 3 wanakuzunguka, Ni Mashangingi walioshindikana mjini, kama unataka kuendelea nao lazima uangalie akili ya ziada, ukienda nao kama unavyoenda lazima kuna sehemu utaangukia pua, kumbuka ni JITU pekee anayefahamu kuwa wewe ni marehemu, ni muda wa kuendelea na Plan A kwa haraka umefika.…hakikisha unakuwa rafiki na Mama wa JITU bila JITU wala Lina kujua…

Money Stars: Akyanani, ku-deal na mashangingi wa mjini ni shida …maana ni pasua kichwa, umezipata wapi hizi habari wewe?

Lawyer: kuna mlinzi pale anafanya kazi kwenye kampuni ya rafiki yangu… nikaongea na rafkiangu aongee na mlinzi anisaidie maana sijawaamini wale masister tangu siku ya kwanza tumekutana wanaonekana wengi sana wa akili na wajanja wajanja na wana njaa sana, yani masister wa kupiga na kubabua… sasa pale sijui utafanyaje ikiwezekana tukae pembeni kwa muda, au tuendelee kujifanya kama hatujui?

Money Stars: na Grace je?

Lawyer: huyo nitakuelezea bado sijakamilisha file lake lakini jua wewe hapo uko pekeyako na kama JITU ataenda kuona sio vizuri ukaonekana kwake, utaharibu kila kitu!

Money Stars: haina noma mtu wangu, we kwa sasa nitafutie ex wa Ulumbi na Grace anamdogowake anaitwa Suzzane, nitafutie habari zao mpaka sasa wako wapi, huku mimi siondoki mpaka kieleweke, tuwasiliane ukishapata habari zote 3…

Lawyer: sawa boss lady!
Money Stars: Siku hio nikawaza na kuwazua, nakuwaza na kuwazua mwanzo mwisho nikaona huu ndio mwafaka wa kuanza na Plan A nikiwa huku kwa Queen…

Usiku wa manane nikaondoka kuelekea hospital aliolazwa JITU, kufika namwona JITU anatembea tembea toka kitandani kwenda dirishani na kurudi, Lina amelala kwa pembeni maana ilikuwa saa 8 usiku; kuangalia pembeni simwoni Mama yake JITU, nikaondoka kwenda kumtafuta nikamkuta amekaa cafeteria wanapouza chakula, nikaenda kununua chai, nikamsogelea nikamsalimia

Money Stars: sorry is this seat taken?

Mama JITU: Nooo,

Money Stars: Nikajisogeza fasta nikakaa na Mama JITU, alionekana ana mawaza mia kidogo…nikamkaribisha chai wala habari hana
Mama are you alright?

Mama JITU: Yes am fine

Money Stars: You look so worried, what’s wrong?

Mama JITU: ah we mama embu niache, matatizo yangu ni mengi niache, hautanielewa

Money Stars: what? I don’t understand you!

Mama JITU: nimekwambia niache ah we nawe mbona mbea hivi?

Money Stars: Kimyaa! Kama sijui Kiswahili vile

Mama JITU: akaongea hapo Kiswahili wee analalamika na kutukana, analia na kunyamaza

Money Stars: namwangalia kama sisikii kumbe nasikia.. nikamaliza chai yangu fasta, nikamuaga kwa kidhungu

Mama JITU: wewe nenda tu mama, wasalimie

Money Stars: nikaondoka kurudi wodini na kukuta kweli Lina na JITU wana-do! Hapo ndipo nilipomwelewa Lawyer wangu, kama kawa kama dawa saa 9 usiku hapo nikachukua video camera yangu nikawarekodi wapendanao wawili..
Dah kweli Lina ni binti alievurugwa, ila amesahau mimi nimevurugwa mara 100 yake, lazima nimnyoshe akikutana na mimi lazima aniamkie mara 100.. Ila Lina ni noma na ule mjoka wa JITU mtu amesimamia kabisa ukucha?! Kha!
Embu mwangalie JITU, nina uhakika asilimia 100 kichwani kwake nimemjaa!.. Lina anadhani anamchanganya JITU kumbe anajichanganya mwenyewe, nikakiangalia chumba weee kina CCTV za wenyewe.. nikasikia watu wanaongea kuja nikazima camera nikaondoka fasta, nikarudi reception nikakaa, kuangalia mchongo mzima wa ile hospital, masaa 3 nasoma ramani ya pale reception, kweli ULAYA ULAYA tu, naanzaje sasa kukamata file la JITU? Nikiwa katika kuwaza na kuwazua mara namwona mama mkwe anapita kuelekea wodini, nikaamua kumsindikiza, kufika anachungulia ndani anashindwa kuingia akatikisa kichwa akaondoka zake… nikaamua kwenda kuchungulia nakukuta JITU na Lina wamelala pamoja.. yani hawa watu wanajisahau sana…
Kumfuata Mama JITU, namkuta yupo chooni analia, kweli maisha magumu jamaa, mama huyu hana raha, nikaingia chooni hakuniona nikaanza kumwongelesha kizungu kumwuliza analia nini?

Mama JITU: kimyaaa!.. Mama amebeba siri nyingi sana za familia yake, akilia inamsaidia kuondoa stress

Money Stars: Nikajifanya naendelea na shughuli zangu za chooni nikatoka namwacha amekaa chini kabisa kwenye sakafu,
Nikarudi wodini kwa JITU na Lina, bado wamelala, uzuri taa ilikuwa imezimwa, nikajifunga shungi nisionekane na miwani, nikaingia nikachukua pochi ya Lina na Wallet ya JITU, wakati naondoka nikabonyeza kengele ya kumwita nesi nikakimbia hakuna alieona wapo buzy wamelala
Nesi kufika anakutana na watu wamelaliana kama hotel, akaenda kuita boss wake wakaanza kuamsha amsha, amsha na wewe ishakuwa kesi mara Mama JITU nae huyo akarudi, ikabidi Lina afukuzwe, katika fukuzwa fukuzwa Lina anaangalia pochi yake haioni, wakaanza kugombana na nesi.. nesi anasema sijachukua Lina anasema umechukua
Wakati huo mimi nipo zangu nje ya Hospital nakagua pochi ya Lina, nikakutana na Passport, tiketi ya ndege, wallet ya JITU kuna hela nyingi… nikaondoka zangu kurudi Hotelini maana pale Hospital kumeshanuka!
Baada ya siku 3, nikampigia simu Lina aje Aiport, afunge virago vyake vyote atanikuta airport,.. kweli akaja na sanduku lake kuubwa mshamba wa Uingereza sijui kajaza nini, macho mekunduuu namwuliza vepe mama kulikoni JITU kafa au?

Lina: hapana nimepoteza Passport yangu hata sijui nafanyaje

Money Stars: Tiket yako hii hapa na Passport yako hii hapa, ndege yako inaondoka baada ya dk 20, safari njema tunaonana Nyumbani

Lina: Akashangaa anatoa macho kwanza hakujua nimekuja saa ngapi Uingereza, kwani kuna nini Madam mbona ghafla ghafla ivyo? Au kuna mahali nimekukosea?
Money Stars: tutaongea nyumbani, ukifika Airport kesho kuna mtu atakuja kukupokea …atakupeleka kwenye nyumba yako mpya utaishi hapo mpaka nitakaporudi, kule unapoishi hama wala usiwasiliane na wale watu uliokuwa unaishi nao tena..
Lina: Madam kwani kuna nini?
Money Stars: Hamna kitu mbaya, kuna kazi ya haraka ya kufanya kule nyumbani, naomba uwe mwaminifu na maelekezo unayopewa ukifika sawa?
Lina: sawa madam, nashukuru sana
Money Stars: nikahakikisha kuwa Lina anapanda ndege anaondoka Uingereza, maana janamke kama lile halichelewi likawa likimbizi ghafla, alipoondoka nikaamsha hema mpaka hotel aliokuwa anakaa JITU na mama yake mzazi… nikamtumia sms Lawyer kwa whatsapp kumkumbusha ampokee Lina ampeleke kule tulipokubaliana…
Kufika Hotelini na kuulizia nikaambiwa JITU na Mama yake wamekaa Restaurant wanapata Lunch, nikazama huko huko waliko, nikakuta JITU amenipa Mgongo na mama yake ananiangalia kwa mbali
Nikasogea mpaka kwenye meza yao, nikawasalimia nikasogeza kiti nikakaa nikiwaangalia wote 2
Mama JITU: samahani we nani?
JITU: Money Stars?! Haiwezekani! Wewe si umekufa?
Money Stars: Shikamoo Mama
Mama JITU: marahaba wewe nani mbona unavamia meza za watu?
Money Stars: Mama kwani haunikumbuki?
Mama JITU: akaniangalia, hapati picha,
Money Stars: Nikamkumbusha kuhusu siku 3 zilizopita hospital,
Mama JITU: oh yah! Nimekukumbuka, hujambo binti?
Money Stars: Sijambo, umeacha kulia sasa?

Mama JITU: akacheka sana, unaitwa nani mrembo

JITU: anaitwa Money Stars, Money ni wewe kweli?

Money Stars: Mama kwani unaongea na mtu au jinni
Mama JITU: naongea na wewe hapo si unaona ni mtu akaanza kumshika Money Stars, kwani vipi mwanangu mnafahamiana na huyu dada?
JITU: kimyaa!

Money Stars: haya mama nashukuru umeacha kulia … nimefurahi kukuona unafuraha sasa, pole sana kwa matatizo

Mama JITU: asante sana Binti yangu

Money Stars: nikainuka niondoke nilikamatwaje Kiuno na JITU

JITU: plz usiondoke, haiwezekani ukawa hai

Mama JITU: kwani mwanangu kuna nini mbona unamtabiria mtoto wa watu mauti unamjua au?

JITU: Money tafadhali usiondoke

Mama JITU: we JITU unashida gani na mtoto wa watu

Money Stars: we JITU nini hiki kwenye kifua chako

JITU: akageuka.. alipogeuka tu Money Stars nikamponyoka fasta! Kugeuka nishafika mlangoni alichokaaa! Anamwuliza Mama yake ninaota au? Kuna dada alikuwa hapa mzuri mzuri ee?

Mama JITU: kwani shida iko wapi JITU mnajuana na huyu dada?

JITU: sio tu namjua, nikimpata lazima nimuoe huku huku uingereza!

Mama JITU: akacheka sana, leo umejua kunichekesha mwanangu sijacheka muda sana

JITU: mama ukikutana na huyu dada naomba mkamate kwa maneno na kila kitu mpaka nije ikiwezekana mlete mpaka nilipo.. huyu ni furaha yangu ya miaka 30 iliopita, akaanza kumwelezea kuhusu Money Stars, Mama yake akakumbuka alikuwa na girlf friend akiitwa Moon Light Lady!
JITU: ndio huyu sasa

Money Stars: sasa mbona unamwita Money Stars?

JITU: yani mama stori ni ndefu, natakiwa nimpate huyu binti, dah! Akitokea akakufuata Mama nakuomba usimwache aondoke zake, sawa mama?!... huyo ndio tiket yangu ya furaha ya milele, kwingine napita tu Mama wala usijali

Mama JITU: Sawa Mwanangu… hahaha leo nimecheka sijawahi kukuona ukiwa hivi Mwanangu kwa muda sasa, am happy for you


HUKO BONGO:
Lina alipofika, alipokelewa na Lawyer akajiona wa Muhimu kweli hakujua anapopelekwa, baada ya dk 45 za kutoka Aiport mpaka alipotakiwa aende, alijikutwa amebwagwa Manzese ndani ndani uswazi, hakuelewa kwanini akaambiwa akae pale pale mpaka Money Stars atakaporudi atapigiwa simu
Lina alichoka, hakujua cha kufanya, maana alirudi Bongo simu hana si aliibiwa!
Baada ya kusota wiki nzima ya maisha ya uswahilini, Lina akaletewa simu ya touch na Lawyer, akaonekana kuchangamka, alipoambiwa kuna msg zako whatsapp akachangamka zaidi, kufungua anakuta video na picha zake na JITU wanapeana raha, sura ikaanza kubadilika ghafla.. alipoanza kulia Lawyer alishaondoka muda wananchi wakajaa wanamshangaa aunt analia nini tena?
Hapo hana mia hana nini, nyumba yenyewe imepangishwa hajui inalipwaje, akiangalia kwenye akaunt yake ya bank hafikishi laki 3… kweli kulala tajiri na kuamka maskini hakujawahi kumwacha mtu salama…
Baada ya wiki 3 kupita nikarudi Bongo, sikuonana tena na JITU wala Mama yake kama walivyodhania itakuwa, kufika nyumbani kwangu Lawyer akaja kunipa mkanda mzima wa Grace, Harrieth, Bwana wa Harrieth, Lola na ndugu wa Grace Suzzane

PICHA LIPO HIVI:
1.  Baada ya kugundulika kuwa Lola na Harrieth wanasagana, Lawyer akaenda kumtifua Bwana wake Harrieth wa zamani ambae walipendana sana, Harrieth alipompata JITU akambwaga ex wake… Lawyer akaongea kikubwa na ex wa Harrieth akamweleza kila kitu kuhusu mahusiano yake na demu mwenzake na kuwa kama anataka kumlipiza kisasi Harrieth ni sasa, anatakiwa amfuatilie sana Lola amfukuzie mpaka amkubali alafu awe mpenzi wake, Jitihada zikafanyika mpaka Ex wa Harrieth akampata Lola, maana alikuwa anampa attention za level ya kizungu Lola akachizika.. siku moja Lola na Ex wa Harrieth wakalewa wakarudi nyumbani anapoishi Lola, wakaingia kulala, kulala na wewe Harrieth akiwa amesafiri, ndio ikawa tabia yao mpaka siku Harrieth anawafumania wana-do kitandani kwa Harrieth, ugomvi ukawaka usio na mwisho, ikabidi Lola ahame nyumbani kwa Harrieth akaishi kwa Ex wa Harrieth, haya yote yalitokea na kumfanya Harrieth kuchanganyikiwa zaidi maana aliporudi kwa JITU, JITU alimkataa… akili ya JITU bado inamtafuta Money Stars kwa udi na uvumba..
Baada ya Mizei 3 ya mahusiano kati ya Ex wa Harrieth na Lola, Ex wa Harrieth akaaga anasafiri kikazi kwenda Ethiopia, akamwambia akae pale kwani ile nyumba ni yake hakuna wa kumsumbua…
Lola alivyo na akili kama upepo akaamini, baada ya wiki 1 ya kuishi pale mwenyewe akaja mwenye nyumba na kumtoa kwa nguvu, alivyompigia simu Ex wa Harrieth hapatikani na namba haipo hewani wakati ni jana yake tu waliongea kwenye hio hio namba ya simu aliompigia… Lola akarudi kumtafuta Money Stars hapatikani kwenye simu.. kurudi kwa Harrieth hawezi, akafukuzwa kwenye nyumba asioijua na mtu asiemjua akidai ni mwenye nyumba akarudi kupanga Sinza… uzuri alikuwa na ajira yake ndio kilichomsaidia, mpaka sasa anamtafuta Money Stars ambae bado hapatikani!

2.  Grace bado anafanya kazi kwenye kampuni ya JITU, siku JITU alipomwona ofisini kwake alimwangalia tu kama mahindi ya kuchoma ingawa Grace alijua atasumbuliwa, ikapita wiki, mwezi, miezi JITU haangaiki nae.. hakuelewa kwa nini… sikumoja akaamua kumfuata ofisini na kumsalimia kimahaba, JITU hamu hana wala hamtaki akaamua kumfukuza ofisini kwake kabisa akamwambia nikikuona nakuweka ndani … Grace akaondoka kurudi kwenye ile nyumba aliopangiwa na Money Stars, akakuta nyumba haipo, imechukuliwa na mwenye nyumba, macho yakamtoka, akimpigia Lola na Lina hawapatikani, akarudi kwa Ulumbi kumwelezea matatizo yake, Ulumbi akamwambia hatoweza kumsaidia tena, akamtafuta Money Stars hayupo kwenye simu hapatikani…Grace akaamua kurudi nyumbani kwao magomeni kuishi na wazazi wake..

3.   Bikra wetu Suzanne, ndugu wa Grace ndio ambae amebakia, mpaka sasa yupo kwenye mahusiano na Lawyer, Lawyer ameamua kumweka sawa kwanza, anampa attention za kufa mtu ili akija kumbwaga anataka aangukie miguuni mwa JITU, … ila Lawyer nae ana roho mbaya! Mara ya mwisho nilipoongea na Lawyer akaniambia Suzzane Bikra alishaiondoa muda sana, kwa sasa ana bikra moja tu Mungu mwenyewe ndio anaijua!...

Lawyer: Best imebakia miezi 3 sasa tuingie kwenye Plan B maana wale mashangingi sidhani kama watakuachia tu wakae kwenye umasikini wakati walishaonja Mbingu kabla ya hapo.. lazima watarudi kukumaliza ushike adabu yako… hapo walipo wamechoka best utadhani wametoka kijijini leo, fanya tuingie Plan B watakuheshimu wakitoka hapo
Money Stars: bado tusogezi mpaka mwaka na miezi 6 upite na hela zao zote ziishe kwenye miliki yao…hawajajifunza wakishika adabu watanitafuta hata kuzimu.. kwa sasa waendelee kupata taabu sana!





TUONANE JUMAMOSI TAR 27 OKTOBA 

2018 SAA 6 MCHANA YA TANZANIA..
_______________________________________________

B. PLAN B – TUWACHANGANYE AKILI ZAO KWA MUDA



Baada ya miezi 6 kuisha, tukapanga kuonana na Lawyer mjini kupata Lunch na kuongelea mikakati yetu ya sasa

Money Stars: Mwana Mwana! Lawyer ni wewe lakini kuchelewa unajua kweli kweli!
Lawyer: we acha tu, ushukuru Mungu nimefika
Money Stars: Mara ya mwisho kuongea na wewe umenipa maneno magumu sana..
Lawyer: hahahahahaha, Star bwana!
Money Stars: kwahiyo amebakiwa na bikra 1 tu Mungu mwenyewe ndio anaijua? Hayo sio makubaliano yetu ujue! Ushafeli hapo!
Lawyer: unajua ndio maana tumeonana, mambo haya ya simu sio mazuri, nilihisi simu yangu imehakiwa ndio maana nikakujibu vile… ila usikonde mambo yapo vizuri, isingekuwa ni kazi mimi ningeshamuoa Yule binti Suzzane… unajua aliumia sana pale nilipomkimbia, nikambwaga nikarudi baada ya mwezi tukakaa miezi 2 nikambwaga tena nikarudi baada ya miezi 3 na juzi nimembwaga kikubwa, nikamwambia nimeoa!
Ila Stars bwana unajua kunidatishaga na vimwana wako, nitaoa kweli?
Money Stars: Kwanini umemfumua mtoto wa watu?!
Lawyer: ndio nachojaribu kukueleza Yule binti bado sijamgusa
Money Stars: Miezi 8?! Hujamgusa? Hajakuhisi wewe sio mzima?
Lawyer: Kazi ulionipa ni ngumu sana Star, ni vile tunaheshimiana ila muda sana ningeshakula tunda
Money Stars: Kwahiyo?
Lawyer: Kila siku nampa excuse nampiga kalenda mtoto wa watu mpaka naona aibu ndio maana namkimbia naibuka, mtoto Yule mchumba ujue! Mzuri sana Yule binti, yani kukaa na demu mzuri kama Yule alafu unamwangalia kama Picha ya Yesu inahitaji imani sana ujue?! Mnanitia majaribuni buana!
Alafu uache mambo zako za sizitaki mbichi hizi, unaniwekea ndizi mbaaali unanifanya sungura nizifikie!
Money Stars: hahahahahha, usijali nitakuozesha yale mashangingi mengine yale ndio mazuri
Lawyer: oh! Wale tena,. Alafu ushawasiliana na warembo wako?
Money Stars: wapi?! Kimyaa! Habari sina! Kwani wapo wapi hawajanitafuta kwenye simu maana namba ya simu nilishabadilisha kipindi kile tumemaliza kuongea nikaitupa chooni nikaflush!
Lawyer: dah! We mwana wewe! Ila poa tu Lawyer wako nipo kukudaka usianguke
Money Stars: Vp kwani nini kimetokea?!
Lawyer: Mengi yameytokea Star kwanza sijaamini kama tunaoana leo, wale majinga yamekuzunguka mbayaa!
Money Stars: aaa?! Imekuwaje tena?
Lawyer: una muda?!
Money Stars: siku hii ni kwa ajili yako!
Lawyer: dah yametokea makubwa na madogo pia!
Money Stars: Am all Ears!
Lawyer: Tulipoachana nikaendelea kuwafuatilia wale mamama wa mjini,
Money Stars: Enhee!
Lawyer: wote walirudi kwa JITU kila mtu kwa kalenda yake
A.  Harrieth aliomba appointment kwa JITU akaambiwa aende nyumbani kwa JITU kumbe alikuwa na mpango wa kumrubuni alale nae, hakujua kuwa ULUMBI yupo mule mule ndani
Harrieth akafanya yake kamrubuni JITU wakaingia chumbani kwa JITU, wakawa wanafanya yao weee mara Ulumbi akaingia, akawafumania, vurugu zikaanza
Ulumbi anadai chake, Harrieth nae anatema chehe zake anazozijua
Wakagombana kwa maneno wakaingia kwenye ngumi.. wakadundana wee JITU anawachukua video camera, walipomaliza JITU akainuka akawala wote 2 kila mmoja kwa wakati wake, mambo ya three sum nene kwa mara ya kwanza ULUMBI ametembea na mume wake!
Money Stars: acha kusema uongo bwana unajua unaniudhi
Lawyer: akatoa flash, hii falsh ina kila kitu, akafungua laptop yake akaniambia angalia kama nakudanganya, doh kucheki kweli JITU kafanya three sum alafu kawaacha wote hoi!
Money Stars: ivi Lawyer unatoaga wapi haya maigizo?
Lawyer: Mil 5 niandalie sijafanya hii kazi kwa bure
Money Stars: usijali, enhe kwahiyo ikaishiaje
Lawyer: Baada ya lile zoezi Ulumbi na Harrieth hawaongei, Ulumbi akaishia kugombana na mumewe kuwa amemcheat anataka talaka na talaka ikipita ni nusu mali tunapasua, JITU akamwambia nenda kashitaki kokote hata mimi nimekuchoka, ila hautapata hata Tsh 10 yangu
Money Stars: kwahiyo sasa?
Lawyer: Ulumbi akakasirika akaenda kukaa hotelini, JITU anakaa pale na mtoto, siku moja akamchukua mtoto akampeleka kufanya DNA test Afrika Kusini, akaondoka na nywele na kucha za Baba yake mzazi.. kweli akakuta mtoto sio wake ni wa baba yake mzazi!
Money Stars: Kudadeki! Baada ya hapo
Lawyer: akarudi zake mjini, akampeleka mtoto kwa mama yake hotelini alipokuwa anakaa na barua ya DNA akamwambia subiria talaka na kwangu usikanyage mpeleke mtoto kwa baba yake!
Ulumbi kachanganyikiwa akapanda ndege mpaka kwa Baba yake JITU akaenda kumweleza kila kitu, kikao kikaletwa mjini nyumbani kwa JITU
Wazazi wakaongea Mama ake mzazi JITU analia tu, kujua mumewe ana mtoto mdogo na umri ushaenda ana miaka 75 baba JITU, ataleaje anamtegemea JITU ndio awasaidie
Wakaita mwanasheria wa familia kuamua kesi, ULUMBI akajua hapa lazima napewa change naendelea kuwa taajiri!
Mwanasheria wa familia akamwambia ULUMBI talaka yako hii hapa, JITU ameshakutalaka kwa sababu ya kutembea nje ya ndoa tena na baba yake mzazi, ana haki ya kukushitaki kwahiyo kwenye ndoa hii hauna chako
Ulumbi akalia lia lakini mtoto wangu ni mtoto wa familia
Mwanasheria akamwambia mali zote za Mzee Manyanga alishamkabidhi mwanae JITU miaka 15 iliopita kwasababu ya uzee wake na katika urithi wake hakuwa amemwandika mwanao kabisa na huyu mtoto ana miaka 10, urithi ulishakabithiwa kwa JITU miaka 5 kabla ya mtoto kuzaliwa… kama anataka mwanao aangaliwe ni makubaliano yako na mzee Manyanga, mali za familia zipo mikononi mwa JITU tu kwa sasa!
Itabidi wewe na mwanao mkalelewe na Mzee Manyanga huko kijijini awalishe awavishe ndio uwezo wake ulipo..
Ulumbi akalia sana maana alijua maisha yatamwendea mteremkoni!
Mama JITU na JITU wakakumbatiana, Ulumbi akaondoka kwa hasira akisema ataenda mahakamani kushitaki, mtoto wake apate haki zake kwa Mzee Manyanga!

Money Stars: Maskini Ulumbi, sijawahi kuonana nae lakini simpatii picha na hopes zake maskini!

Lawyer: baada ya mwezi m1 wakaenda mahakamani, kesi ikasikilizwa, ikapaishwa mbele, mwezi wa 2, kesi ikapaishwa, mwezi wa 3 kesi ikapaishwa, mpaka kufikia mwezi wa 5 Ulumbi hana hela ya kumlipa Lawyer! Mpaka kuja kusomewa hukumu, ikaamuliwa mtoto alelewe na baba yake mzazi na mama yake na sio kaka wa mtoto!
Na mali alizonazo Mzee Manyanga ni shamba 1 analolimia kijijini alilolinunua hivi karibuni, ndio anaweza pewa huyu mtoto
Ulumbi hakuamini, anaenda kijijini, akakataa, akaleta jeuri hataki hata hilo shamba, mwisho wa siku Mzee Manyanga akafariki huko kijijini, wamezika wiki 3 zilizopita!

Money Stars: weee! Mzee Manyanga amekufa hata sijazungumza nae?

Lawyer: ulikuwa kimya mimi nakutafuta kwenye simu haupatikani

Baada ya Mazishi, Mwanasheria wa Familia akaja kuandika lile shamba la mzee Manyanga jina la MAMA JITU na kama Mama JITU atafariki atapewa JITU!

Money Stars: makuuubwaa! Ina maana ULUMBI kweli kakataa hata kashamba mjinga kweli… sasa Ulumbi yupo wapi na Harrieth yupo wapi?

Lawyer: Ulumbi hajulikani hayupo na mwanae, Harrieth yupo mjini anadanga!

Money Stars: anamdangia nani sasa? Nani anataka wazee!

Lawyer: ameokota lizee limoja limestaafu ndio yupo nae na Zungu moja hivi, anatoa huduma kwa zamu, wiki hii yupo kwa zungu wiki ijayo yupo kwa mstaafu, hataree angalau anaishi hela ya kodi ya nyumba, mahitaji ya kila siku anapata lakini sio life la zamani kwa JITU hatopata!

Money Stars: JITU je?!

Lawyer: mpaka jana nimeambiwa JITU yupo Arusha ameenda kujipumzisha kuondoa stress za kufiwa na baba yake, Mama yake anaishi nae hapa hapa mjini ameondoka kijijini ndio anamkazania aoe tena ila yeye anasema anakutafuta wewe stars hakupati
Inabidi uende Arusha ukaongee na JITU, hana raha hataki kitu anakutafuta, kaongee nae sasa hivi hamna ishu sana yupo huru!

Money Stars: Suzzane ana ishu gani wiki hii?

Lawyer: yupo tu amechukua likizo kazini, vp unataka kuonana nae?

Money Stars: nataka nipande nae Arusha akanisaidie kuonana na JITU!

Lawyer: na mimi je?

Money Stars: kama tulivyopanga, niandalie vijana wako 4 waliovimba kifua, nipande nao, JITU mjinga sana asije akanibaka, panda nao na Suzzane pia, tuonane ARUSHA kesho tumalizane na Plan C yetu!
Lawyer: sawa Boss!

Money Stars: kuhusu wale manyambizi tutaongea sikunyingine natakiwa kumuwahi JITU asije akajidhuru!

Lawyer: sawa boss lady!

Money Stars: nitakulipa tukirudi Mjini ngoja tukamalizane na Arusha kwanza!

Lawyer: sawa boss wangu!
Tukaagana tukaondoka, nikaenda kuwazungukia akina Grace… Lola…. Lila… Lina!
Kweli wanatia huruma afadhali na Lila ana kazi yake lakini hao wengine wa3 wanatia huruma! Anyway hicho ni kiporo cha baadae, angalau wapo!
Ila acha waendelee kuumia wakiniona wajue kuniheshimu, wanaonekana wamechanganyikiwa sio kitoto, manyambizi kama yale kuangukia uswaz mchezo?!
Usiku huo huo nikaaga kwa mume nasafiri naenda Arusha kufuatilia biashara flani hivi, Mume akaingia line kweli, Alfajiri nikapelekwa Airport nikapanda ndege asubuhi ya kwenda Arusha… baada ya masaa kadhaa nikatua Arusha, Arusha kuna baridi jamaaani, uuuwi!

Nishazoea kwetu jotoooo, nimekutana na Baridiii! Nikamwa nawaza kwa sauti nah ii baridi nikikutana na PUNDA ya JITU si nafwaaa?!

Uuuuuuuwi, Kiru! Half-Cast wa kichaga nimeingia Arusha!


TUONANE TAR 5 NOVEMBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
________________________ 

C. PLAN C ~ KUONANA NA JITU NA KUTOLEWA MAHARI



Half cast wa Kichaga nikatua

 Arusha, sikufikia hotelini

 nilifikia kwa somo yangu 

mmoja ivi alinifundishaga 

kitchen pati wakati naolewa 

Somo huyo ni noma, 

amefundisha wadada wengi 

mjini na asilimia 80 ya 

aliowafunda wana ndoa zisizopungua miaka 15

Sikumoja nikiwa ulaya nikamkumbuka kumsalimia akaniambia ameshaolewa na yeye alipataga mzee mwenzake. .. huyo mzee alifiwa na mke akabakia mwenyewe kulea hawezi ndio wakakutana na somo yangu

Nikisema Somo kwangu mimi namaanisha mfundaji wangu wa Kitchen Pati cha ndani... 

huyu Mama alinifundishaga miezi 2 mafundisho ya ndoa yote mpaka ya enzi za kale, kabla hatujatoka kitchen pati cha ukumbi ni noma asikwambie mtu ni vile ameacha hio kazi ila sikuhizi amefungua grup lake la WhatsApp amewaweka watu wote aliowafundaga ingawa wengine walishafariki lakini tuliohai tupo WhatsApp tunakula good time 

So nikaaga kwa mume nikamwambia nafikia kwa Somo yangu akapata utulivu wa moyo 

Kufika kwa somo mumewe alikuwa amesafiri nikampa mkanda wote wa JITU 

Somo: My dia hapo usiingie kabisa ni sawa na kuchezea waya wa Tanesco ukasema haurushwi huyo atakuharibu mbaya ni bora nikodishe nyumba umwite muyajenge kwenye hio nyumba nikiwepo ajue kweli umefikia kwangu maana najua ukimwonyesha hapa atakuja anisumbue

Basi tukapanga na kupangua, akaenda kutafuta nyumba huko Mushono nyumba kapata mbaya mbaya nakwambia alafu kuna bonge la shamba na mazao kibao ah sikuamini 

Tukakaa hapo siku 5 tukazoea na mazingira kabisa ili asishituke, nikaja nikampigia

Lawyer nikamwambia mambo yamekaa poa ampelekee barua JITU amwelekeze pakuja

Kweli Lawyer akafanya yake kama kawaida akamuagiza kijana wake akaipeleka barua hotel aliokuwepo JITU, JITU akaipokea akaiweka pembeni, kijana wake alipoona hatilii maanani akamwambia imetoka kwa Moonlight Lady, ndio JITU anashituka akataka kumshika kijana akamponyoka akakimbia

JITU: akaichukua ile barua akaisoma maelekezo yote ya kuonana. .. siku hio hio akachukua gari yake na ma body guard 3 wakaja kule Mushono Arusha ndani ndani huko wakafika na Land Rover yao nzurije,

Wakashuka wakapokelewa na Somo, Somo kwani utamjua amekaa kama bibi wa kijijini, hapo keshalipwa Milioni zake 5 anaitumikiaje hela sasa? !

Wakapokelewa wakakaribishwa ndani wakakataa, JITU anataka kuonana na Moonlight Lady,

Somo: yupo ndani, lakini utaingia pekeyako, hawa hapana
JITU: akawaambia ma body guard zake waingie ndani kukagua kwanza wakafanya yao wakatoka kumwambia pako sawa kuna Mama amelala ndani 

JITU: akaingia ndani fasta akijua Leo anamzimua mpenzi wake wa miaka mingi kwa mahaba makubwa, akashangaa kukutana na Bibi amelala
Akamsogelea labda hajaona vizuri, bibi akamnyooshea kidole dirishani, JITU kuangalia dirishani akaona mdada amekaa shambani 

Akatoka fasta fasta kukimbilia shambani huku wafuasi wake mabodigadi wanamfuata Kufika akanikuta nimekaa sina papara wala sikugeuka kumwangalia 

Money Stars: umekuja kunidhuru au kwa amani? ! Naona aumenijia na vijana wa ulinzi

JITU: money stars?! Ni wewe? ! Siamini

Akasogea kuaniangalia kweli

Mpenzi Ni wewe?!
Akanikumbatia mwenyewe anatoa machozi ananiangalia hanimalizi

Akawaambia Body Guard wake, mkanisumbirie kule kwenye ile nyumba na muhakikishe hakuna mtu anakuja huku shambani, kama mtakula pale kuleni msije mpaka nije mwenyewe 

Mijemba ikaondoka kwa oda chezea pesa wewe hata ukisema waning'inie kwenye miti kama masokwe wataning'inia tu

JITU: Bebi, nimekumiss sana... huku ananipapasa mikono, macho, mashavu, shingo dah ukaguzi sio wa nchi hii mwisho wa siku akajua kweli mimi ndio mimi sio mzuka au jini anaetembea, 
Kukumbatiwa sasa kiru utadhani nitamponyoka anakumbatia kwa nguvu utadhani bikra wa kiume bwana!

Money Stars: unaniumiza JITU bwana acha ujinga,
Nikajinyofoa kwa JITU, hivii hukui tu na mambo yako ya kitoto?!

JITU: sio hivyo mpenzi mimi nakupenda sana na nimefurahi kukuona upo hai, niliambiwa umekufa na tangu niambiwe umekufa ulikufa na mimi mpenzi

Money Stars: well, sijafa kama unavyoniona na acha kunishika shika bwana unanichosha we vipi?! Embu niachie

JITU: akaniachia kwa woga huku ananiangalia, basi naomba nikushike mkono basi

Money Stars: JITU, hivi unataka nini kwangu?!

JITU: nakupenda, nataka tuoane 

Money Stars: JITU si unafahamu kuwa mimi Ni mkristo?!

JITU: ndio mpenzi

Money Stars: na wakristo hatunaga ndoa 2 sio?!

JITU: ndio lakini mimi sijaoa 

Money Stars: najua ulishaoa na umeacha, lakini mimi Ni mke wa mtu, mama watoto 3, unachokitafuta kwangu Ni ngumu kukipata 

JITU: oh jamaan Ni kweli ulishaolewa mpenzi, hapana usiseme hivyo kunifukuza mpenzi


Huku ananichum kwenye shingo mara shavuni machozi yanamtoka, siwezi kukukosa kwa mara ya 2 haitawezekana bora nife nikalale na baba zangu kuliko kuishi bila wewe

Money Stars: bado una akili za kitoto umeghairi kukua sio?!

JITU: sio utoto nakupenda mpenzi, 

Money Stars: JITU akanisogelea akakaa kwa mbele yangu ananikumbatia mambo ya 0 distance nene, huku ananichum kwenye shingo dah, nguvu zikaanza kuniisha nikasema Leo nabakwa mana mtu ameshakuwa wamotoooo na machine imesimama mbayaa suruali itatoboka sasa hivi, nikaamua kuyamaliza kiutu uzima alafu nimkimbia 

Nikaamua kumchum, ikawa kosa na yeye akazidisha dozi ya mabusu... mabusu yalipozidi akainuka akanibeba kuelekea shambani ndani ndani ambapo hatuonekani 

Kweli JITU alikuwa amenimiss, kusika na kufika katoa nguo zake zote kabakia na boxa, doh kuangalia machine yake nje ya boxa nikasema Leo nakufaaa uuuuwi halfcast wa kichaga natobolewa kizazi leo

Tukiwa tumezama kwenye Hot Romance nikakumbuka miaka ya zamani ndio tumeanza ki-do, JITU anakupa raha mpaka tone la mwisho, mjinga yupo vizuri kwenye sekta ya Romance

Utamu kolea Money Stara nikaishiwa na nguvu, namwona kabisa hapa huyu mjinga anataka kuniingia na mjini nimeacha ndoa alafu JITU hana hata mpira... mambo ya kuja kutafuta mimba za uzeeni sitaki Nikajinyofoa kama kawaida

 yangu lakini JITU alikuwa na nguvu sana

Huwezi amini alipovua Boxer lake ndio nilijionea miujiza. .. doh bonge la machine jamaan 
khaaaa nikamstopisha 

namwuliza, we JITU nini hiki sasa

JITU: anachekelea utadhani mazuri

Money Stars: nikawa najiweka sawa narudishia nguo za juu, JITU nae yupo buzy kunivua na mie nakataa kuvuliwa...kha!
Nani anataka kubakwa na JOKA?!

Money Stars: we JITU nini hiki tena? !

JITU: kwani vipi mpenzi wangu 

Money Stars: he?! Saa ngapi umepata hii kitu? !

JITU: usijali bwana haina shida hii haiumizi usijali 

Money Stars: nikaruka, heee embu niache tafadhali kha unataka kunitoboa utumbo na mapafu yangu au?!

JITU: anakazana kunipetipeti kimahaba, Money bwana Acha utoto 

Money Stars: ukitaka usinione tena nidumbukizie ujinga wako kwenye mwili wangu 

JITU: ah usiseme hivyo bwana dah yani unamwona anavyohangaika sasa hapo machine imesimama balaa, anahangaika hana pa kuiweka

Money Stars: mimi nimekuwa mbogo balaa, nampiga kwa mazao yaliokuwepo yeye anazuia na kukwepa Mengine yanampiga vurugu mechi mtindo mmoja

Nikaona hapa nitabakwa vibaya sana alafu litakuja kutubu baadae, nikakimbia kuelekea kwenye nyumba, akanikimbiza mara ya Kwanzaa akanikosa mana hana nguo, akarudi kuchukua nguo zake, akavaa mimi nikakimbia kwenda kwenye kile kijumba chetu nikaingia ndani Somo akanifuata mabody guard wakamkimbilia boss wao 

Baada ya dk 15 JITU akaja anagonga anataka kuonana nami, nikakataa akafosi akaingia ndani dah padogo na yule bibi pale kuongea anashindwa akaniomba sana tuongelee hata kwenye gari 

Money stars: nitaongea na wewe kesho,  leo niko na mshituko na bibiyangu hapa anaumwa naomba uondoke 

JITU: mpenzi mimi siondoki, nalala hapa hapa kwako,  kesho ukiamka utanikuta..

Money Stars: sikuhio sikutoka ndani, Somo alitoka akapika, nikasikia wanaongea nje na JITU, 

Baada ya muda wakina JITU na Body Guard wakala, mimi na yule bibi tukaletewa msosi ndani tukala tukalala,

Usiku wa Saa 7 Somo akaniamsha 

Somo: huyu kaka bado amelala nje ya mlango wale mabody guard wake wamelala kwenye gari...amekataa kula chakula mpaka wewe ulipomaliza kula ndio akala. .. JITU anakupenda sana ungekuwa hujaolewa na hauna familia ningekuambia uende nae

Money Stars: Somo hujakutana na wasanii bado ila tutayamaliza yote hapa hapa, tulale 

Asubuhi nikaamka Saa 12 kufungua mlango namwona kweli kalala mlangoni hamna pa kupita, nikachukua maji ya baridi na lile baridi la Arusha nikamwagia 

JITU: ah bebi ni wewe?!

Money Stars: nifuate 

Tukaongozana mpaka shambani,  

JITU: umeamkaje mpenzi naona upo na nguvu alfajiri hii

Money Stars: ukitaka niachane na Mume wangu niambatane na wewe hio kitu yako ulioongeza uirudishe kama zamani

JITU: nini?!

Money stars: umeniskia vizuri na najua umenielewa 

JITU: haitawezekana 

Money Stars: hio sio shida yangu ni yako

JITU: money tafadhali, siwezi kuwa na mwanamke mwingine zaidi yako

Money Stars: nikamgeukia, nikamkumbatia, nikamwangalia machoni kwa macho ya huruma, nikamwambia najua na ndio mana nataka unisaidie na kitu kimoja tafadhali 

JITU: chochote mpenzi nitafanya kwa ajili yako 

Money Stars: kweli Mpenzi?!

JITU: kweli si unajua nakupenda sana

Money Stars: nataka uoe 

JITU: kuoa? ! Nakuoa wewe au?!

Money Stars: kwasababu mimi na wewe


Imeshindikana, nataka umuoe mwanangu mtoto wa dadangu

JITU: sielewi unanichanganya me nilidhani kwenu mpo wasichana 2 tu

Money Stars: kwa hali ulionayo ambayo huwezi kuirudisha nyuma ukabadilika ukarudi kama nilivyokuacha, na kwa hali ambayo nipo nayo ya ndoa ambayo haiwezi kubadilika, lazima tukubaliane kusaidiana na kufikia muafaka kuliko kuumizana 

JITU: nakuskiliza 

Money Stars: kama ambayo unanipenda mimi, naomba umpende zaidi mtoto wa Dada yangu ninaekupatia tafadhali... hauna mwanaume anaetaka kukaa pekeyake JITU utakufa na stress mpenzi, usijiharibie maisha kwasababu yangu, maisha ya mateso uliopitia yanatosha kwa sasa, tafadhali nakuomba unikubalie ombi langu

JITU: hapana bwana mimi nakupenda wewe 

Money Stars: najua unanipenda ndio mana nimekuomba plz plz JITU, kama unanipenda niamini na huyu binti hana shida na hautakuja kujuta nakuahidi plz, huku namchumu kwenye shavu 

JITU: sasa natafutiwaje mke kwani mimi siwezi kutafuta?!

Money Stars: tumeshayaona kwa Ulumbi 

JITU: hujui chochote kuhusu Ulumbi, akaanza kujawa na hasira 

Money Stars: nikamkumbatia, tafadhali rusirudi Misri tumeshavuka bahari ya shamu tunaelekea Caanani... plz

JITU: akatulia na hasira ikaanza kushuka, akaniangalia machoni, navyotia huruma maskini kwa muda ... mwone Kwanzaa ulivyo mzuri, hapa una watoto 3 uko hivi, ila huyu mumeo kakunenepesha kwanini lakini 

Money Stars: Yes or No?!

JITU: nikisema No?!

Money Stars: then mimi na wewe tumeshamalizana hautaniona tena narudi kwa Mume wangu Uingereza


JITU: kumbe ilikuwa ni wewe Uingereza?

Money Stars: hapana malaika wangu, plz huku namrembulia macho

JITU: akacheka sana, unajua kuninyong'onyeza unavyonirembulia ... si bora nikafanyiwe opereshen nikarudishiwa machine yangu ya zamani je?!

Money Stars: najaribu kukusaidia naona hatuelewani, nampenda sana Mume wangu na watoto wangu siwezi kuwaacha kwa kitu chochote

JITU: kama unampenda sana mumeo kwanini upo hapa na mimi?! Ina maana hata mimi unanipenda vile vile na mimi pia namasharti yangu nataka kukuoa wewe

Money Stars: No

JITU: Yes

Money Stars: Ndege yangu inaondoka kesho saa 10 jioni kwenda Uingereza, utanipa jibu kama hapana hautaniona tena kama ndio tupange yanayofuata 

Nikaondoka toka shambani kurudi ndani nimemuacha JITU shambani anawaza na kuwazua...ilipofika saa 3 asubuhi nikamwona Body Guard ananiita kuwa Boss wake anataka kuongea nami shambani 

Kufika Kwanzaa nikapokelewa na mabusu motomoto nikabebwa juu juu kama kigunia, nikaenda kuwekwa kwenye mahindi buana... doh! Salala, nilipigwa Romance ya kibabe hakuna mfano

Ambacho umesahau mpenzi msomaji ni kwamba mwanaume anaekupenda sana hawezi kukufanyia kitu ambacho wewe uliependwa haukipendi ... sikupenda anipe machine yake hakunipa machine yake

Ila unamwona mtu kabisa anavyokupa raha ya romance unaona ni kiasi gan anaumia kukukosa... lakini atafanyaje ndoa ya mtu lazima uiheshimu 

JITU: Aliopomaliza akaniambia nimeishiwa na nguvu juu yako, kukupata siwezi kukufaidi siwezi, kukupenda naweza,  sawa nionyeshe mtoto wa dadako nitamuoa 


Money Stars: nikafurahi lakini sikuwa na uhakika kama ni ya kweli anayoyaongea JITU au hapana!

Nikamkumbatia na kumshukuru kwa yote, nikamwomba tafadhali muangalie vizuri mtoto wangu, nampenda sana na hajui mwanaume wewe utakuwa wa Kwanzaa 

JITU: Akaniangalia kwa mshangao, we Money unaniletea Bikra?

Money Stars: hata sijui wewe ndio utaniambia 

Tukaondoka kurudi ndani, akaomba chai ya pili akapewa akanywa kwa furaha mpaka yule bibi anamshangaa alivyo na furaha

Somo akajua tumedo maana sio kwa ile furaha aliokuwa nayo JITU

Jioni yake akaomba tuondoke wote twende Arusha mjini nikamtambulishe kwa mtoto wa Dadangu, atanirudisha Dar kwa Ndege, tukaondoka na Somo na JITU na ma body Guard wake wote tumeshamwita mwenye nyumba aje akae na bibi tutarudi wiki ijayo 

Tukaingia hotelini Somo kakodiwa chumba chake, mimi nikaambiwa nitalala na JITU nikakataa nikagoma,
Baada ya muda nikampigia Lawyer amlete Suzanne mishen imeshatiki upande wangu

Tukiwa kwenye kumsubiria Mwali akuje na JITU akiwa chumbani kwake na sisi kwetu, Somo akaniuliza yaliojiri nikamweleza 

Somo: nyie hamja-do kweli?

Money Stars: hapana, ameniheshimu kwa hilo, tena amejikaza kweli ni sawa na kumsusia Mwili mwanaume anaekupenda alafu akatae kula chakula

Somo: du hii mpya, Ila sio bure,  huyu mwanaume atafanya unachotaka kukuridhisha Ila lazima sikumoja atakukamata tu kwenye ango yake ... usikubali tena kuonana nae mkiwa wawili

Money Stars: sawa Somo yangu nashukuru sana kwa msaada wako

Baada ya Lisaa limoja akaingia mwali Suzzane kapendeza kweli kweli utadhania sio Bikra, 

Tukaongea nae akaelewa, tukamwita JITU tumtambulishe kwa Suzanne akaja akamwona akamfurahia JITU nae ni mchangamfu Bala,  akamfanya Suzanne asijiskie aibu 

Money Stars: namwangalia JITU namwangalia na Suzanne nacheka kimoyomoyo mbayaa doh siamini naona kama naota jamani kweli JITU ndio anaenda na Suzanne? !

Uuuuwi PLAN C ndio umeniendea sawa sawia,  nashukuru Mungu kwa yote

Kesho yake mimi, Suzanne,  JITU tukarudi jijini kwa Ndege, nikafikia Hotelini na JITU, Suzanne akaenda kwao, akaenda kuwaeleza wazazi wake kwa amepata mchumba anataka kumleta nyumbani kumtambulisha 

Wazazi wakakubali, aje tutampokea

Wiki iliofuata JITU akaingia nyumbani kwa akina Suzanne na washenga akapeleka barua, ikapokelewa Baada ya siku 3 ikajibiwa,

Siku ya kuleta Mahari, Grace alikuwepo lakini mimi sikuwepo, naskia alipojua ni JITU anamuoa nduguyake Suzanne alizimia kwa mshutuko!

Chezea Punda wewe?!



Tuonane Kesho Tar 8 Novemba 2018 saa 1 usiku ya Tanzania
-----------------------------------

 


D. KUWEKWA HURU NA HARUSI YA PILI 

Baada ya sakata la Arusha na Dar na mahari ya Suzanne bado nilikuwa naishi hotelini kwa malipo ya JITU nikaambiwa Grace amelazwa hospital moja hapa mjini 

Nikaamua kuuvaa ubinaadam nikaona niende kumchungulia bila yeye kujijua, kufika wamejaa ndugu kibao na mama yake anamwuguza
Akiulizwa vepe mbona ulizimia anasema alikuwa amechoka na sikuhio hakula kabisa kabla ya kuja kwenye mahari si unamjua Grace alivyo msanii kama kawaida yake lazima adanganye 

Nikaondoka kwenda kumtafuta Lawyer

Money Stars: mwana mwana! 

Lawyer: ah boss wangu niaje?!

Money stars: Leo mkono wangu wa kulia unaniwasha mbaya

Lawyer: sawa taajiri nakuja nakuja

Baada ya nusu saa tukaonana kijiweni kwetu Mbagalaa, ndio Mbagalaa kwani Mbagalaa kuna nini?!

Tukaongea kwa muda wa lisaa limoja tunapanga na kupangua

Money Stars: hivi Lawyer una mpango wa kuoa lini? !

Lawyer: doh Boss Lady ulisema mkono upi unakuwasha!?

Money stars: wa kulia

Lawyer: hivi pesa inamtokaga mtu mkono gani ukiwasha?

Money Stars: we bwana unaoa lini?!

Lawyer: ah sina wa kumuoa, sijapata binti wa kupenda nae we si umeninyakulia mtoto Suzanne bwana

Money Stars: nipo serious bwana

Lawyer: na mimi pia

Money Stars: unamwonaje Grace

Lawyer: sipendagi baby mamas nataka mabikra

Money Stars: we unayo?!

Lawyer: ah bwana me sijampenda huyo Grace wako Kwanzaa anaonekana ana roho mbaya

Money Stars: Ulumbi je?!

Lawyer: khaaa! Uyo aliekuwa anahemewa na wazee... staki laana mimi 

Money stars: yale manyambizi hujayaelewa?!

Lawyer: ah bwana ngoja nipate wangu

Money Stars: sawa hivi Ulumbi yupo location gan kwa sasa?!

Lawyer: yupo mkoa, bado naendelea kumtafuta kuna mikoa 2 nimebakisha nahisi yupo huko 

Money Stars: usisahau kunifahamisha sasa nipelekee hizi barua kwa Lola,  Linda na Lila
Hakikisha naonana na kila mmoja kwa siku niliowaandikia na wasichelewe, wakichelewa utawalipia

Lawyer: sawa boss

Money Stars: hela zao za kuwatoa kwenye uchafu hizi hapa na walipie kodi zao wanazodaiwa na wenye nyumba was

Lawyer: sawa boss

Money Stars: saa 1usiku nataka kuonana na Lina nadhani yeye ndio anafanana na mimi zaidi kiumbo 

Lawyer: kweli boss umejuaje?!

Basi kikako kikaisha tukarudi town, kurudi hotelini namkuta JITU amekaa kitandani kwangu ananisubiria 

Money Stars: samahani nimekosea chumba 

JITU: hapana ni chako

Money Stars: huku umeingiaje? !

JITU: usijali, tunahitaji kuongea, 

Money Stars: sawa, lakini tunaongelea pale nje restaurant humu sitarudi tena

JITU: doh! Sawa Mama watatu 

Baada ya muda wa kushuka restaurant malumbano yaliendelea kwa chini chini maana JITU sijui alikuwa amekunywa pombe au amelewa mvinyo sikuelewa alipandwa na nini sikuhio

Anasema eti hataki kumuoa Suzanne hajampenda ananipenda mimi, nikaendelea kumsihi afanye kama tulivyokubaliana lakini si unajua mwanaume aliekunywa pombe anavyokuwa nikaona hapa napoteza nguvu zangu bure 

Tukaendelea kuongea baadae JITU akaanza kutoa masharti yake:

JITU: sawa nitamuoa kama unavyotaka lakini jua simpendi ila nitampenda sababu yako 

Money Stars: ukitaka kuiona hii sura yangu tena 

Nataka ufanye kama tulivyoongea... umpende kama ambavyo ungenipenda mimi,
Umlinde kama ambavyo ungenilinda mimi
Umthamini kama vile ambavyo ungenithamini mimi
Umtumikie na kumheshimu kama ambavyo ungeniheshimu, ungejitoa na kunitumikia mimi na mama yako mzazi
Wewe sio mtoto tena na hauna miaka 18 tena 
Pamoja mtazaa watoto wa kike na kiume kadri ya Mungu atakavyowajalia nawaombea 

Siku utakayomtesa au kumpiga Suzanne utakuwa umenitesa na kunipiga mimi

Siku utakayochepuka kwa Suzanne ni siku ambavyo utakuwa umenichepukia mimi 
JITU: mbona masharti magumu kama jini mtoa roho 

Money stars: kama hautaki me na wewe tuachane utajiju na maisha yako

JITU: doh hapo pagumu

Money Stars: ukitaka urafiki na mimi tuwe family friends na nini, we nikubalie ombi langu
mara simu yangu ikaita,
Samahani napokea simu maramoja 

Nikasogea pembeni nikaskiliza simu kumbe Lawyer ameshamleta Lina 

Sawa mpeleke chumbani na mwambie asikosee..  akiharibu hapa tusijuane... simu ikakatwa 

Nikarudi kwa JITU, sasa mimi naondoka na harusi yako ni kesho, ngoja nikalale nimechoka sana... usiharibu plz tumeipanga hii harusi kwa muda wa miezi 2 na wala mume hajui narudi lini Uingereza usiniangushe 

JITU: sawa Basi angalau niachie usiku huu niwe na wewe basi

Money Stars: usiku mwema Bwana harusi, tuonane kesho ukumbini... usisahau mimi ni mtoto wa Baba Mkubwa wako sawa?!

Huyoo nikapanda juu kufika namkuta Bimdashi Lina ameshafanya yake, nikakusanya kila kilicho changu nduki, ile nakaribia kwenye lift namwona JITU anapanda 
Ngazi kuja kulala, nikacheka sana

Nikaondoka kulala hotel nyingine kabisa 

Usiku wa saa 6 napigiwa simu na Lawyer kuwa Lola na Lila wamekubaliana na ule mpango wetu kesho watafika saloon na Suzanne amewakubali pia 

Money Stars: Grace vipi?!

Lawyer: bado yupo hospital amesema hatoenda kwenye harusi 

Money Stars: usiku mwema taajiri yangu simu ikakatwa

Asubuhi nikaamshwa na simu ya Lawyer;

Lawyer: mama amka wee tuna harusi ya kwenda 

Money Stars: Lina je?!

Lawyer: anasema JITU hajagundua chochote alikuja pale chumbani kwako akidhania umelala, akaingia mazima mazima akafanya yake na Lina akafanya kama alivyoelekezwa alfajiri kabla JITU hajaamka akawa ameshaondoka mahala pale 

Money Stars: utanisindikiza kwenye harusi kama mume wangu... Jiandae

Lawyer: poa boss kubwa shukrani 

Baada ya masaa kadhaa tukadondoka kwenda kanisani na Lawyer kushuhudia ndoa ya JITU na Suzzane Bikra, kama kawaida maids ndio hao hao mashosti Lola na Lila... baadae wakaingia maharusi kanisani ibada ikaanza na litrugia tele kikaingia kipindi cha kufungishwa ndoa 

Mchungaji akauliza kama kuna mtu yeyote mwenye kupinga ndoa hii aseme sasa au akae kimya milele 

Watu wote kimya, tukasubiri kama dk moja mara tukasikia Mimi hapa napinga, kuangalia ni Grace 

Watu wote hoi, Grace?!

Grace: akasogea mbele kuelezea kwanini anapinga akasema kuwa anamfahamu sana bwana harusi na bi harusi ni mdogowake 

Bwana harusi atamtesa mdogowake mana Bwana harusi ana machine kubwa sana na bi harusi ni Bikra

Watu: wakaanza kuning'ona aibuje

Mimi nipo na Lawyer nyuma tunacheka mbavu hatuna

Mchungaji: unajuaje kuwa bwana harusi ana machine kubwa?!

Grace: nilishatembea nae sio chini ya mara 5

Wageni: wananong'ona aibu,

Mamake JITU: anaona aibu mpaka anaangalia chini 

Money Stars: aisee embu kamtoe Grace bwana ameshajiaibisha vya kutosha kwa nduguze 

Mchungaji: binti mnahamhusiano na bwana harusi?!

Grace: ndio... hapana 

Mchungaji: kipi ni jibu sahihi?! Mbona majibu yako hayajitoshelezi?!

Grace: nilikuwa baadae nilipojua ameoa tukaachana 

Mchungaji: bwana harusi umeoa?!

JITU: nimeshatalakiana na mkewangu kwasababu alizaa na Marehemu Baba yangu na talaka yangu hii hapa

Wageni: kimyaaa na mishangao juu 

Mchungaji: binti una lingine la kuzuia ndoa hii?! Maana kama ni machine kubwa ya bwana harusi naona umetushangaza wengi lakini sio sababu ya kufanya ndoa isifungwe ... hawa wawili ni watu wazima mpaka kuchukua hatua ya kuoana ina maana wameshafahamiana na kuja huku kufunga ndoa

Grace: akanyamaza kimya huku akiwaangalia JITU na Suzzane mdogowake... akamjibu mchungaji hapana akarudi kukaa kwenye kiti cha kanisa 
Mara wakaja mabaunsa wa JITU kumtoa Grace nje, Lawyer akawafuata nje.. mimi nikabakia ndani kushuhudia harusi ya JITU na SUZZANE kama ilivyopangwa!

Mchungaji: akarudia swali tena kama yupo wa kupinga ndoa aseme sasa akiwa na sababu za muhimu zaidi ya hii alioitaja Binti aliepita

Wageni: kimyaaa 

Baada ya muda kupita hakuna aliejitokeza, Mchungaji akafungisha ndoa Baada ya madakika machache mbele JITU na Suzzane wakawa 
Mr & Mrs JITU MANYANGA

Wamama: vigelegele nene kwa sana 

Money Stars: nilipoona wameshasaini vyeti vyao vya ndoa na kuonyesha umati nikatoka nje kumtafuta Lawyer hayupo Kumpigia simu haipatikani

Kumpigia simu hapatikani, nikaona huu msala sasa nikikaa hapa wakatoka mambo yangu mengi yataharibika nikachukua taxi mpaka hotelini kwangu, namkuta Lawyer na Grace wanaongea 

Money Stars: simu umeibiwa au?! He Grace upo? ! Sikujua kama mnafahamiana na huyu kaka

Grace: analia machozi Acha! 

Money Stars: kulikoni Mbona mnalia lia?!

Lawyer: mambo yameharibika Money,

Money Stars: nini tena?

Lawyer: Grace ni mjamzito wa miezi 2 na anasema mimba ni ya JITU 

Money stars: nikashtuka lakini nikajikaza kisabuni, nikajibu mmmh tutajuaje kama ni ya JITU?! 
Najua Grace sio Muhuni ila nina miezi mingi sijamwona kwahiyo sijui huko alipokuwa

Grace hii mimba ya JITU kweli?!

Grace: ndio 

Money Stars: ina maana umelala nae miezi 3-2 iliopita?!

Grace: ndio

Money Stars: nikiwaza hio miezi ndio JITU Alifiwa na Baba yake inawezekanaje?! Mmmh huenda kweli au la lakini sidhani kama mimba ni ya JITU na ingekuwa kweli ya JITU Grace angeongea pale Kanisani kwanini alinyamaza?!
Grace yupo very selfish asingenyamaza nakwambia ila haya yote tutayajua siku Za usoni, 

Grace, nakushauri rudi nyumbani ukapumzike nitakutafuta tutafanya DNA test kama mimba ni ya JITU nakuhakikishia haki za mwanao zitapatikana usijali sawa? !

Grace: sawa 

Money Stars: wala usikasirike, JITU sio mara ya Kwanzaa anaoa,  hii hapa namba yangu

Tutawasiliana sawa mami?!

Grace: sawa

Akakubali kurudi kwa wazazi wake magomeni kupumzika 

Mimi na Lawyer tukarudi ukumbini kuendelea na sherehe, harusi ilikuwa nzuri sana, kubwaaaa nzuri kagharamia mwenyewe JITU kila kitu 

Alivyomjinga katika utambulisho akasahau kunitambulisha kabisaa doh basi nikawa buzy na Lawyer tunakunywa wines nakucheka hapo tunamshukuru Mungu dili tulilojitahidi kulipanga limefanikiwa doh nilipumuaje sikuhio mpaka kunywa wine sio mchezo ati. ..

Nilijiona nimetua mzigo mkubwa saanaaa roho yangu ilipumuaa huuuu nikaanza kupata raha moyoni mwangu 

Nikiwaangalia Suzanne na JITU wanavyocheza Blues naskia raha sana na kumshukuru Mungu, hatimaye Imekuwa. .. asante sana Mungu




TUONANE TAR 13 NOVEMBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
-----------------------------------




You Might Also Like

2 comments

all rights reserved - OFFICIAL MONEY STARS | Designed by ARACK