KWANINI UPO SINGO (SINGLE)?

  • April 27, 2018
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 3 Comments






CAUTION/ TAHADHARI:

MPENZI MSOMAJI USOMAPO HADITHI HII JUA KUWA HII NI HADITHI TU KAMA HADITHI ZINGINE - NI MOJA KATI YA BURUDANI ZILIZOPO DUNIANI

TAFADHALI USICHUKULIE BINAFSI (PERSONAL)
______________________________________




KUWA SINGO SIO DHAMBI JAMANI, NI KWAMBA TUMESHAZOEAGA RUTINI ZA MAISHA, UKIZALIWA LAZIMA UENDE SHULE LAZIMA UPATE KAZI LAZIMA UOE/UOLEWE, LAZIMA UPATE WATOTO LAZIMA ULEE WATOTO NA MAJUKUMU MENGI LAZIMA UZEEKE NA MWISHOWE URUDI MAVUMBINI!

HAYA MAZOEA YAMELETEA SHIDA MBALI MABLI KWENYE JAMII NA BAADHI YA WANA JAMII KUTOELEWEKA VIZURI AU KUONEKANA WABAYA, WANA MAPUNGUVU, WACHAWI, WADHAMBI ETC ETC ETC

SIPO HAPA KUTETEA USIOE AU USIOLEWE, NIPO HAPA KUHADITHIA BAADHI YA MAISHA YA WATU WALIOKO SINGO (SINGLE) NA MAISHA YAO YANAENDELEA

LAKINI, KAMA UNAPENDA KUOA/KUOLEWA ENDELEA MBELE, KAMA HAUPENDI ENDELEA MBELE MWISHO WA SIKU HAYA NI MAISHA YAKO NA MUNGU ALIEKUUMBA SISI NI NANI KUKUHUKUMU?!

MAANA HATA VITABU VYA DINI VINATUAMBIA:

A. BIBLIA, "KAMA UNAWEZA KUKAA MWENYEWE BILA KUMTENDA MUNGU DHAMBI NA KUWAKA TAMAA, NI BORA KUKAA MWENYEWE KULIKO KUOA AU KUOLEWA UKAMTENDA MUNGU DHAMBI- 1KORINTHO 7:9-10"

B. MSAAFU - "SIJUI CHENYEWE KINASEMAJE"

KWA HADITHI KAMILI TUONANE TAR 15 MAY 2018 SAA 10 JIONI YA TANZANIA

_____________________________


CHAPTER 1



A. MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU





Kila mwisho wa mwezi mimi na marafiki zangu tunakutanaga kwa ajili ya kupata chakula, inaweza ikawa chakula cha jioni au mchana.. kwa Mwezi Maramoja, inaweza ikawa mwisho wa mwezi au mwanzo wa Mwezi 



Nina marafiki 3 wote tumeajiriwa, wote tulisoma pamoja kuanzia form 1 mpaka chuo lakini tofauti kati ya marafiki zangu na mimi ni kwamba wao wameolewa mimi sijaolewa 



Kila tunapokutana huwa wananipa wakati mzuri sana, hawanihukumu kwanini nipo singo, hawaniseki vibaya kwakweli wananitia moyo sana kuwa usijali haujachelewa, hakuna kuwahi wala kuchelewa kwenye ndoa, Kila mtu ni Mungu alivyompangia usijiskia vibaya, muda bado unao n.k wa kadhalika 



Siku moja rafiki yetu mmoja akawa anasafiri kukazi miezi 3, wakapanga tumuage kwa kupata chakula cha pamoja tukitoka Kanisani, tukapanga kuonana Hotel ya Kempinski Mjini saa 6 mchana 



Cha ajabu ni kwamba nilipofika pale, hatukuwa 4 kama tunavyokutanaga yule rafiki yetu aliekuwa anasafiri alikuwa na ndugu yake mmoja ambae nae alikuwa anataka kumuaga... jumla tukawa wa5



Baada ya kusalimiana na kujuliana hali na utambulisho wa ndugu yake na maongezi ya hapa na pale na kupata chakula na vinywaji; ndugu wa rafiki yangu ambaye anasafiri akagundua kuwa mimi sijaolewa akaanza kunihoji maswali Mengi ambayo kwa mtu ambaye sijamzoea sikujskia kujieleza kwake ila kwa kuwa alikuwa amenikazania ikabidi nimjibu 


Ndugu wa rafiki: una miaka mingapi

Mimi: 33 

Ndugu wa rafiki: una bwana au mchumba au boyfriend

Mimi: bado nipo singo 


Ndugu wa rafiki: kwanini upo singo miaka 33? Au unatembea na mume wa mtu wewe ni kimada?!

Mimi: kwani lazima kuwa kwenye mahusiano?!

Ndugu wa rafiki: kwahiyo wewe ni kimada wa mtu?!

Marafiki: wote wapo kimya wananiskiliza wala hawanitetei, nikahisi dunia imesimama 

Mimi: hapana sina mtu kabisa 

Ndugu wa rafiki: kwahiyo wewe ni bikra?!

Mimi: hapana sio bikra

Ndugu wa rafiki: ukiwa na hamu  (genye) unafanyaje sasa? ! Au unatumia dildo (midoli feki iliotengenezwa kama orijino dyu dyu ya mwanaume)

Mimi: Tz hii natoa wapi Dildo?!

Ndugu wa Rafiki: kwahiyo ukiwa na hamu unajikimuje?! Au una rafiki anaekusaidia ukizidiwa?!

Mimi: sina kitu wala mtu wala rafiki wa kunisaidia 

Ndugu wa rafiki: unauhakika wewe ni mzima kweli? ! 
Maana sio bikra sio nini,  au na wewe umeokoka Yesu anakusaidia? !

Mimi: hapana sijaokoka ni mkristo wa kawaida 

Ndugu wa rafiki: sasa kwanini upo singo mrembo kama wewe una kazi yako, hela zako, ila mamii kuvaa haujui embu ona hii minywele yani upo rafu?! 
Mwanaume gani Atakusogelea?! 
Kwanini unajiweka rafu my dia? !

Alafu nyie marafiki zake mko vizuri mmependeza mwenzenu kama ameamkia kwenye banda la ng'ombe kwanini hamumfundishi kuvaa akapendeza akawa fresh safi, 

Yani mrembo kama wewe umeshindwa kujipeleka Saloon ukajisopusopu ukapendeza, unakuja kula chakula cha laki 1 Kempinski wakati saloon kuosha na kutengeneza nywele ni elfu 20 

Nguo mpaka elfu 20 unapata mlimani city kwa hadhi yako basi 

Ivi nyie kwanini mnamwacha mwenzenu anakaa rafu?! Ndio urafiki gani mlionao

Wa kinafiki namna hii?!

Marafiki zangu: wakanyamaza kimya; lakini Mimi nilimpenda sana huyu ndugu wa rafiki yangu, Kwanzaa alikuwa smart sana sana sana, Alafu hakuwa ameolewa lakini alikuwa kwenye mahusiano, alionekana ana huruma na roho nzuri na upendo nilitamani angekuwa rafiki yangu; akaendelea tena kuongea 

Ndugu wa rafiki yangu: ahahahaha haki ya Mungu, my dia, haya ni maisha, sijui hawa mabwege unaowaita marafiki wanakufundisha nini?! 
Kama upo na hawa watu kuanzia form 1 mpaka sasa mnafanya kazi Alafu hawana hata mchango wa kawaida kukusaidia sielewi unafanya nini kwenye maisha yao, ondoka katafute marafiki wengine ina maana hawa ni wanafiki kwako hawakuelezi ukweli, rafiki wa kweli anakueleza ukweli, 

Mimi nimeingia hapana nimekuangalia sana nikajua labda ni house girl wa mmoja wa hawa wadada kumbe rafiki tena una ajira yako nzuri kwanini lakini umejikatia tamaa namna hii?! 

Kwanini umekuja mchafu mchafu kichwani Nguo hujanyoosha angalia majani kichwani kwani hapa hotelini umeingiaje Kwanzaa? ! 
Hawajakuuliza kama umekosea njia?!

Mimi: kimya

Ndugu wa rafiki: my dia, hawa sio marafiki zako,  hawa ni ma-free mason

Marafiki: wee! ushindwe, wakaanza kugomba hapo na kulalamikiana

Ndugu wa rafiki: ndio nyie ni wachawi wanyonya damu na waiba nyota, mnakuwaje mmerembeka namna hio lakini mwenzenu kakaa kama dada wa kazi?  Alafu anapataje mwanaume kwa staili hii?

Au mnafurahia mwenzenu anavyoteseka?!

Marafiki: hapana si tumemwambia lakini hasikii, labda umwulize kwanini kawa hivi maana zamani hakuwa hivi

Sikuhizi ndio kabadilika kawa hivi hana miezi 6 anavaa kiajabu ukimwuliza hasemi na sisi huwa tunamwachaga hivyo 

Ndugu wa rafiki: my dia, what happen?! Imekuwaje unakaa kama fundi gereji za magari? !

Mimi: hamna bwana mbona nipo sawa 

Ndugu wa rafiki: umetokea kanisani hivi Au umetokea nyumbani?!

Mimi: nikadanganya kuwa nimetoka nyumbani

Ndugu wa rafiki: OK labda uliamka ukasahau kuoga ukaja 

My dia ningependa kukusaidia sana, Mimi nimesoma Saikolojia na naweza msoma mtu sana kabla hajaongea na wewe unaonekana una mateso ya moyo sana, yanayokupelekea kukata tamaa, akaingiza mkono kwenye pochi akatoa business kafi yake akanipa 

Ndugu wa rafiki: unitafute kwa wakati wako kama unaona aibu kuongea mbele ya marafiki zako nitakusaidia lakini namna hii ulivyo hapana ukiendelea namna hii utazeeka mwenyewe kama sio kufa siku sio zako... akanyanyuka akaaga anawahi mahali akaondoka 

Mimi: nikampenda sana yule mwana psychology  (saikolojia) nikatamani tuonane siku hio hio tuongee 

Baada ya wiki 1 nikampigia simu yule mwana saikolojia nikamwambia nipo tayari kuongea nae, akaniambia uwa ana darasa la wadada ambao wapo single, kama anataka aniingize huko maana litanisaidia kuchangamka na wezangu, na kufunguka kwa urahisi 

Mimi nikakubali, akaniambia darasa kwa wiki mara 1, kila jumamosi, akanipa na bei ya hio programme na itachukua muda fulani wa miezi 10 na malipo yake natakiwa niwe nimemaliza kabla ya miezi 2 kuisha maana mbeleni kunakuwa na programme za kutoka out, kusafiri, yeye atakuwa analipia Hotel, Vyakula, Vinywaji, Usafiri,  

Ndio hela yake ilikuwa ndefu sana sana sana, lakini sikujali, niliona bora nitoke nikutane na watu,  nitengeneze marafiki wapya, nipate connection za maisha, nisafiri,  nipanue akili sikujali maana nilikuwa haba na haba lazima nitajaza kibaba hata kama nitabakia kuwa singo

Siku ya siku ikatimia nikaenda kwenye hicho kipindi,  nikapokelewana mtu wa mapokezi nikajaza form nikapelekwa sehemu ya kulipia nikalipa mil 8 cash ya Kitanzania sikutaka kuigawanya Au kuilipa kwa mafungu maana hela bwana Leo ipo kesho hamna 

Baada ya kupewa risiti nikapelekwa kwenye chumba ambacho nilikutana na wadada 6 na Mimi wa 7 sote tunamsubiria mwana saikolojia aje tuanze shoo 

Mwana saikolojia akaingia akatusalimia kwa kutukumbatia na kutubusu kwa furaha tukakaa kwenye masofa mazuri mazuri nakwambia wakaja wahudumu wakauliza mnataka vinywaji gani kila mtu anataja chake hapo saa 10 jioni ya Jumamosi

Baadae tukaanza kikao, mwana saikolojia akajieleza kwa ufupi kuhusu kazi yake na maisha yake kwa ufupi sana na watu aliowasaidia na lile lilikuwa darasa lake la 3

Amesaidia wadada 20 na wakaka 10 waliokuwa singo kama sisi na sasa wameolewa na kuoa na wanafamilia zao wengine ndoa miaka 5 wengine 10

Mimi: nikashangaa huyu dada alikuwa wapi sikuzote sijamwona?!

Mwana saikolojia akaongea sana mpaka alipohakikisha wote tumekuwa relaxed akaanza kutuuliza kila mmoja ajitambulishe kwa majina na kazi (shughuli) anayofanya na kama anawatoto au mtoto
Basi ilikuwa raha sana

Kwakuwa kipindi kilikuwa ni masaa 3 tu

Na hapo tulishaangusha Lisa 1 nanusu mwana saikolojia akaomba mdada m1 aanze kujielezea kwanini yupo singo

Yule mdada aliitwa Kokutona, mwenyeji wa Kagera, Mhaya kwa kifupi anaitwa Koku ... Mfanya biashara mzuri, hana bwana, hana mtoto,  hana mume yupo singo, mrembo sana,  ana figa namba nane, bonge la shepu,  wema sepetu atasubiria miaka 100.. ana weusi flani unateleza...Black Beauty, Mzuri vijana wa kileo wangemwita kisu balaa

Akaulizwa kwanini upo single mrembo

Koku: mimi naomba niwe muwazi na msema kweli, maana msema ni mpenzi wa Mungu 

Mimi kila mwanaume ninayempata ananiangusha 

Mwana Saikolojia: Kivipi?!

Koku: kila mwanaume ninayempata anakuwa na dyudyu ndogo, size ya bamia ndogo (machine ndogo) 

Sasa sijui nina laana au nimelogwa 
Mwaka wa 2 huu napata Vibamia tuuu; ah! nikaamuaga nikae mwenyewe kwa muda

Mtu unakuwa umejiandaa kila kitu wakifungua mlango unakutana na kidole cha mwisho, Sasa na hili zigo nililo nalo nachokaa 

Wengine nawahairishia kuwa naumwa nimepatwa na tumbo la kubana, Wengine nawaambia naumwa tumbo la mwezi, wengine najidai simu imepigwa nina dharura basi inaisha 

Nimeshapata wanaume kama 20 wana machine ndogo, wanene,  wembamba, warefu, wafupi, weupe, weusi, vijana, Ben 10, watu wazima ...eh kila mtu me sichaguagi, nikaona nikae mwenyewe huenda sio riski nikaamua kununua Dildo  (dudu ya kiume ya mpira) ndio inanisaidia kujikimu ila sio sawa kama ukiwa na mwanaume wa ukweli


Mwana Saikolojia: lakini tatizo sio machine ndogo kama anajua kuitumia Koku

Koku: hamnaaa hata matumizi yenyewe hawajui wala nini kuchoshana ujinga mtupu 

Wote: tukacheka huku tunamshangaa Koku maana sio kwa maelezo yale!


Tuonane kesho Tar 17 May 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA kwa Muendelezo mwingine

   

_________________________________________________________________________________ 

B. WACHUNGAJI WAMENIFUKUZIA WANAUME WOTE NILIOWAPELEKA KWAO, NDIO MAANA NIPO SINGO!



Tukaja tena siku nyingine kwa ajili ya darasa letu la wadada single, sikuile tuliacha patamu baada ya kuona kuwa KOKU anachangua chagua midushe ya akina kaka zetu

kweli niajabu, huyu Koku huyu haangalii tabia ya mwanaume haangalii kabila, haangalii dini, haangalii utaifa yeye ni kanyaga twende tu, na anakanyanga kweli kweli maana kuna maneno aliyaongea pale mpaka nikarudi nyumbani kichwa kinauma

hili darasa nimelipenda sana, watu wapo open, wanajiachia hawana aibu wala nini alafu limechangamka mpaka sisi tulio wapole tunachangamka tena

sikuile tulimaliza vizuri, tukapigwa na picha na selfie kibao, tukatamani jumamosi ifike haraka lakini kama unavyojua hamna jumamosi bila kuikanyaga j3 mpaka ijumaa

sikuhio kila mtu alitaka kuongea wa kwanza ajielezee kwanini yupo Singo, Koku katufungulia mlango wa nguvu, basi Mwana saikolojia kufika tu kila mtu anataka kuongea, darasa letu lina makelele sio kitoto, akawa anashindwa amchague nani, mimi hapo nipo kimyaaaaa

Mwana saikolojia: akaamua basi mimi naomba tuongee tu leo mimi nitawajibu mwishoni maswali yenu, kwa sasa naomba nimchague bibi hapa ambae ni mimi niongee maana nimekaa kimya sana, akaomba aanze na mimi na anajua nikiongea nitachangamka maana mimi ni mpole sana,

nikakubali kuongea nikaanza kwa kujitambulisha

Mimi: Kwa jina naitwa Mwelu, ni mwenyeji wa Singida, Mnyaturu, nina miaka 33, nimeajiriwa kwenye kampuni ya ... Meneja Masoko

Mwana Saikolojia: oh! jamani kazi nzuri hio na kampuni nzuri sana, hongera sana

Mwelu: asante
Mwana Saikolojia: enhe! endelea mami,
Mwelu: Nimefanya kazi kwa miaka 5 sasa, ila sielewi kwanini nipo singo mpaka sasa najua huu sio mpango wa Mungu mimi kukaa peke yangu, alisema atanitafutia wa kufanana nae lakini mpaka sasa sijamuona na umri unaenda, mbaya zaidi kinachonichanganya naumwa sana Fibroid!

Wote: oh! jamani pole sana mami, pole rafiki utapona, pole pole,

Mwana Saikolojia: kwahiyo wewe ni mlokole umeokoka?

Mwelu: ndio, nimeokoka nampenda Yesu sana sana

Mwana Saikolojia: Hospital umeenda wakakwambiaje kuhusu ugonjwa wako? wanakufanyia opereshen au? lini?

Mwelu: nimeenda, wakasema nikitoa Fibroid lazima nizae, nazaaje sasa wakati sina mchumba wala mume wa kuzaa nae?
Nikaenda kwenye maombi nikaombewa lakini wapii! bado zinakuaaaa, nikafunga mwenyewe namwomba Mungu aziondoe lakini wapi hazitoki, nimeshaenda kwa Manabii lakini wapiii bado zimekomaa nimefika sehemu nakaaga kama bumbu wazi, sijui shida iko wapi? sidhani kama nimelogwa asee!
Huu ni mwaka wa 7 sasa nimeishi nazo hizi Fibroid lakini hazitokii! doh nachanganyikiwa sana, nimekuwa singo kwa miaka 33!

Wote: uuuuwi ina maana wewe bikra? hujawahi kuwa na boyfriend?

Mwelu: Boyfrienda Kanisani wanakataza

Wote: Yesu JE? Anakataza pia au?

Mwelu: well, labda, ndio, sina uhakika!

Wote: haujawahi kumwuliza Yesu kuhusu kukupa hata Bwana wa kukufurahisha au akuzalishe kama ameshindwa kuleta Mume akuwowe uzae ndani ya ndoa kama anavyotaka?

Mwelu: kwakweli Yesu hashindwagi

Wote: Mbona Fibroid hajaziondoa miaka 7 sasa, Yesu gani huyo unamwomba usiku na mchana hakujibu? Yesu hana roho mbaya kama wachungaji wako hao, hawakuombei mpaka upeleke sadaka ndio anakuombea vizuri
na umebinuka na hizo Fibroid kwenye maombi miaka 7 lakini bado unazo?

Mwelu: hata sijui huenda ni jaribu langu

Wote: wanacheka kwanguvu sana, wengine walicheka mpaka wakatambaa chini

Mwana Saikolojia: Jamani naomba utulivu tafadhali, naomba aongee muhusika sisi tuwe wasikilizaji maswali nitauliza mimi!

Wote: pole sana mpendwa, hahahahaha, pole! pole! pole!

Koku: samahani Mwelu, unauhakika umeokoka sawa sawa? like asilimia 100? au unachakachua?

Mwelu: sijawahi kuchakachua hata siku 1

Koku: mimi nilivyokuwaga sina bwana kabla sijanunua doli la kiume, nilikuwa najisaga vibaya mno, unauhakika wewe haujichui kweli hata kwa kidole!

Mwelu: hata sijui hayo mambo, sijawahi kufanya hayo, maana Mungu hapendi! na mimi sipendi kumchukiza Mungu

Mwana Saikolojia: Mwelu my dia, sisi tunakupenda mno lakini hatuwezi kumfikia Yesu na Mungu kwa jinsi wanavyokupenda, lakini Mwelu, hii elimu ulio nayo ni degree au masters au diploma au certificate ya Masoko?

Mwelu: nina Masters!

Wote: ahahahahha wanacheka kweli kweli, wengine wakauliza hiyo Master uliipata kwa nguvu ya Chupi au Yesu?

Mwelu: Mungu alinisaidia akanipatia

Wote: wakacheka sana sana sana, doh walokole ni mwisho wa Matatizo! ahahahaha wengine wakasema Yesu akyanani ana kazi kweli kweli

Mwana Saikolojia: jamani naomba utulivu muda unaenda na Mwelu hajamaliza kuongea

Wote: leo tunamwachia uwanja Koku mwalimu acha amalize masaa 3 maana anashida kuliko sisi

Mwana Saikolojia: Mwelu mama achana na hawa bwana vichaa we endelea mimi nakusikiliza

Koku: lakini mwalimu huyu alisema alipata wanaume au hajasema embu atuambie walikuwa wanamtongozaje anawakubalije huenda kuna mbinu mpya ya kutongoza kwa Yesu tuijue na sisi tukikutana nayo tuishinde!

Mwelu: mimi nimewaambiwa kuwa sijawahi kuwa na mume, sijaolewa, sijawahi kuwa na bwana

Koku: kwahiyo wewe hautongozwi au? hata wa kukuchumbia hayupo?

Mwelu: wapo niliwapata

Koku: uliwapataje ndio tunataka kujua na walienda wapi mpaka sasa unabeba ma fibroid si ungewakubalia?

Mwelu: kwakweli, niseme ukweli kama Koku alivyosema ukweli, Koku mimi nakupenda hata kama una maswali kama Polisi,

Wanaume nawapata ofisini kwangu, nikienda kutafuta wateja, nikisafiri kikazi, kanisani pia nawapata, tukienda kwenye makanisa mengine kufanya huduma nawapata!

Koku: wanakutongozaje ndio tunataka kujua mama!

Mwelu: wananiambia tu 

Wale wa Kanisani: Bwana Asifiwe, naomba kuongea na wewe, nikiwasikiliza wengine wananiambia Mungu amesema na mimi wewe ni mke wangu, wengine wanasema nimekupenda nataka kukuwowa, wengine wanaogopa kusema wanaenda kumwambia Mchungaji, alafu Mchungaji anakuja kuniambia ofisini kuwa kijana amekuja kunichumbia anataka kunioa

Wote Pamoja na Mwana saikolojia: ahahahahahahha, uuuuwi Yeeesu leo ni siku ya kucheka na kuongeza Maisha! walicheka sana wote

Koku: alafu unamjibuje mzee baba mchungaji?

Mwelu: nakubaliana kuonana na huyo kijana niongee nae nakuta sijampenda

Koku: enheee1 hapo hapo ndio nimekupata! hujampenda! kumbe kutompenda mtu sio dhambi ee?

Mwelu: sijakwambia uchukie watu sasa Koku

Koku: aaah! si umesema hujampenda kwanini usimkubalie sasa si mlokole mwenzio bwana!

Mwelu: hapana sijampenda

Koku: au hana gari na maisha ya kukupa unaogopa kutembea kwa miguu?!

Mwelu: mimi gari ninalo tutaendesha langu

Wote: ahahahahahah ya leo kali, uuuwi ahahahahahha

Mwana Saikolojia: sasa kwanini upo singo Mwelu jamani kumbe vijana unawapata

Mwelu: hao ni wa Kanisani

Kuna wa Ofisini: hao wanakutongoza leo, wanakutoa out kesho, kesho hio hio wanataka kulala na wewe, na ukiwaambia umeokoka hauzini wanaondoka hawarudi wanaenda kukutangaza kwa watu yule mlokole msiende pale hafungui miguu

Kuna wale nawapata nikisafiri Kikazi: ndio hao hao wanafosi walale na mimi kabla ya ndoa!

Kuna wale nawapata nikienda kwenye Kwaya: wanakubali tunaoana lakini mwisho wa zote wanakuwa wahuni tu wanataka kile kile walichokuwa wanataka wa ofisini

Wote: wakacheka sana! doh leo Mwelu umeliamsha dude! ahahahahaha... Mwelu tunaomba uolewe na Yesu yaishe ahahahaha!
hawa raia wa Kazini hawatakuelewa mpaka unakufa!



Mwana Saikolojia: Sasa Mwelu hamna uliofanikiwa kuwapenda mkakubaliana kwenda kwa Kanisa ukamtambulisha?

Mwelu: kusema kweli napataga wachumba

Koku: sio wachumba bwana Boyfriend kwani wamekuvisha pete we nawe!

Mwelu: haya napataga wakaka tunapendana, wa nje ya Kanisa, wanakubali kabisa, wanakubaliana na Imani yangu wanakuwa wamenipenda kabisa

Koku: umewapata wangapi?

Mwelu: nilishawapata kama 5 hivi, nikawapeleka Kanisani, nikamwambia Mchungaji kuwa nimepata mwenzangu wa kuanza nae maisha, na wale wanaume wanakubali kweli kwenda kanisani kuonana na mchungaji na kuongea nae, lakini wakishatoka pale kwa mchungaji hawarudi kwangu tena

nilishawauliza wa 3 wakakata mawasiliano na mimi, nikamwuliza na kwingine wa 4 akaniambia ameshindwa masharti ya hapo kanisani kwako, na hawezi kupangiwa ndoa na kuishi na mimi kwa Masharti ya Mchungaji ambae hamjui

Nikamwuliza na mwingine wa 5 aliniamulia kwa hasira maana nilikaa nae kwenye mahusiano miezi 6 na hakuwahi kunigusa; akaniambia Mama bora tu huyo mchungaji akuoe mke wa Pili tu maana sio kwa vigezo alivyoweka kukuoa wewe! kama unataka kuendelea na mimi ambae sijaokoka twende ila kama unawasikiliza hao maboya we endelea nao wakutafutie mume au wakuoe wewe

wote: ahahahahaha! Mwelu weee utakufa na Bikra zako kama kweli unazo shenzi kabisa

Mwana Saikolojia: kwahiyo hao wanaume ukawaacha waende:

Mwelu: ndio

Mwana Saikolojia: kwahiyo walivyoondoka, ushawahi kuwasiliana nao tena au kujua labda walishaoa au?

Mwelu: ndio wote walishaoa wana maisha mazuri sana, sana sana na wana watoto

Mwana Saikolojia: na wewe unajiskiaje kuona wao wana maisha mazuri na watoto?

Mwelu: sawa tu! huenda hawakuwa wa kwangu, wangekuwa wangu wangeshanioa wakakubali masharti ya mchungaji

Koku: ivi hawa wanaume wanaoa wachungaji wanamuoa Mwelu? ushawapeleka hata nyumbani?

Mwelu: hapana bado, naanza kwanza kanisani ndio kwa wazazi

Koku: kwa mfano kanisani wakamkubali alafu wazazi wakakataa utaolewa?

Mwelu: ndio

Wote: ahahahahah kweli Yesu aje achukue vilaza wake sio kwa upuuzi huu ahahahaha

Mwana Saikolojia: kwahiyo Mwelu wewe Baraka za wazazi hauzitilii maanani kama baraka za Wachungaji wako sio?

Mwelu: Mchungaji ndio anatoa baraka za kwanza alafu wazazi baadae

Wote na Mwana Saikolojia: tobaaaa, ahahahahahah uuuuwi

Koku: unasali Kanisa gani hilo mama?

Mwelu: akalitaja

Wote: wakacheka sana doh akyanani Yesu ana kazi sio kitoto!

Koku: my dia Mwelu, naomba uniskilize kabla boss wetu mwana saikolojia hajakushauri, 
Kwanza hilo Kanisa mpo wasomi wangapi wanaoendesha magari wenye Degree na Masters?

Mwelu: tupo 5

Wote: uuuwi hamaaaaa hamaaa!


Koku: mami sikufundishi ukazini au umtende Mungu wako dhambi, hapana ila kaa ujue kuwa 

1. Mungu amekupa akili mamitooo, embu zitumie zile akili ulizopewa na Mungu za kuzaliwa

2. hivi hapo Kanisani kwanini usihame lakini? au wamekuloga maana Biblia ilishasema kuwa siku za mwisho watakuwa manabii wa uongo wengi tu sasa ona Mungu amekuletea wanaume weeengi na akakuongezea 5 umewafukuza mwenyewe kwa jinga wako wa kuwasikiliza wachungaji, embu hama nenda hata Lutheran au Katholic rudi kwenye dini ya wazazi wako si ushapata neno la kutosha kwa hilo Kanisa embu rudi kwa Kanisa ulilozaliwa unapoteza Muda my dia

3. Miaka 7 umekaa na Fibroid wakati Mungu ameweka hospitali kwa ajili ya matibabu? unataka kufa au hautaki watoto?
unajua Fibroid ukikaa nazo sana unatolewa kizazi mami? maana zinakula kizazi hatari mpendwa wangu

Mwelu: kweli ee jamaan sikujua

Koku: hukujua au haukutaka kusikiliza madokta ukaweka imani mbele ukaona Madaktari ni mashetani wa kuzimu? unafanya vibaya unaleta ujinga kwenye jamii asee wewe, kumbe ungeshaolewaga muda sasa hivi una familia yako kiroho safi, ona hao majingas wako wachungaji wanakuharibia maisha!

4. Wazazi Mwelu ndio Mungu wetu hapa Duniani Mungu amewaweka Mwelu, ina maana kwa maelezo yako wewe Mwelu unawatumikia sana wachungaji hata wazazi wako huwaangalii uongo?

Mwana Saikolojia: kwani Mwelu kwenu umezaliwa wa ngapi?

Mwelu: mimi wa mwisho

Mwana Saikolojia: Mwelu unawaangaliaga wazazi kweli?

Mwelu: sijaenda kwetu nina miaka 3, wazazi wapo Singida kijijini

Wote: tobaaa, laaana hio Mwelu una shida wewe una laana!

Mwana Saikolojia: pesa za matumizi unawapelekeaga? kuwa mkweli utueleze sisi ni zaidi ya marafiki tumeshakuwa ndugu sasa

Mwelu: sijapeleka nina miaka 3, dadangu yupo na kakaz wanawaangalia inatosha

Mwana Saikolojia: hao ndugu zako wanaishi kijijini au?

Mwelu: wapo hapa mjini

Wote: Mweeeeeluuu! we mbona una roho mbaya hivyo? miaka 3 wazazi hawajala hela yako, hawajaona sura yako?

Koku: unawasiliana nao hao wazazi wako au?

Mwelu: sijawasiliana nao nina miezi 6 sasa, wanaendelea vizuri bwana

Mwana Saikolojia: Kanisani hamfundishwi kuangalia wazazi? maana Biblia ukisoma au zile amri 10 za Mungu, kwenye amri ya 4 inasema waheshimu Baba na Mama yako upate heri na miaka migi hapa Duniani, wewe Heri unaitoa wapi?
Hivi inakuwaje una ajira nzuri wakati wazazi wanateseka kijijini?

Mwelu: Kimya!

Koku: ina maana tatizo lingine lipo kwa Mwelu, tusiwalaumu wachungaji wake huenda wanamfundisha lakini hasikii, huyu Mwelu ana roho mbaya jamani miaka 3 hujaona sura ya wazazi wako? we kweli Mafia, bora Fibroid zikuue tu

Mwelu: weee ushindwe kwa jina la Yesu

Koku: sishindwi, ushindwe mwenyewe paka weeee washakufanya msukule hapo kanisani utaisoma namba, lazima utakufa tu wewe mjaa laana mshenzi mkubwa

Mwelu akaanza kugombana na Koku hapo wee Koku akaonekana amejaa hasira sana sana, akamtukana sana Mwelu, we mlokole Fala kabisa huna hata aibu! mshenzi mkubwa wewe nenda Baharini wakakuogeshe, yani inakuwaje una Masters lakini kujumlisha moja na moja upate 2 unashindwa?

wewe Mwelu shida sio hao wachungaji au huenda wana shida, ila wewe una roho mbayaaaaa, na Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi, yani wewe hauna tofauti na mimi nyau wewe kenge mkubwa!
Yani mimi navyochagua madudu ya kiume na wewe mfunga miguu hatuna tofauti ni bora ungekuwa unapigwa na hao wanaume upate mimba kluliko kujidai unafunga miguu sijui bikra mshenzi mkubwa hao wachungaji wako wanakukula tu wewe boyaaaa usitufanye sisi matahira

Koku akaanza kulia, ningekuwa na wazazi mimi wangeishi kama Mbinguni, Mwelu una wazazi unashindwa kuwaangalia eti dada yupo ulikuja na Dada Duniani?

Ikabidi kila mtu sasa ambembeleze Koku, Koku maskini amewakumbuka wazazi wake analia sana kwa uchungu mpaka makamasi huku anamtukana Mwelu mshenzi kabisa wewe toka huko usituletee magundu humu ndani sisi tunaupendo we pekeyako shetani akamfukuza kwa kumpiga magumu ya mgongo toka bwana hata kama kipindi sio changu toka roho mbaya wewe kafie mbele na ma fibroid yako very stupid na masters yako ya chupi! huna maana

Wewe sio mlokole wa kweli utakuwa umetumwa makanisani, snitch mkubwa Wewe 
Usipobadilika hautakaa uolewe kenge wewe

Ikabidi Mwana Saikolojia ahairishe kipindi, Darasa limeingia mafuriko, Mwelu akainuka huyoo akaondoka na mkoba wake mkuuubwa kama Boti, wakabakia waliobaki wanamtuliza Koku alieonekana mwenye jazba kubwa kuhusu Matendo ya Mwelu!


TUONANE TAR 19 MAY 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA 

______________________________________________________

C. MATESO YA WANAUME YAWMENIFANYA NIWE SINGO 




Baada ya darasa la mwisho kuingia maji, wiki iliofuata tukaonana tena kwa ajili ya darasa lingine

Kwa mshangao nikaona Mwelu amekuja sikutegemea nilijua ataacha kweli Mwelu Mafia

Wanafunzi wote walikuwepo na siku ya leo hakuna aliekuwa tayar kuanza kwasababu ya fujo za sikuile 

Koku bila kukosa alikuwepo ila alikaa nyuma na Mwelu mbele

Mwana saikolojia akaamua kuukata mzizi wa fitina akamchagua Theresia 

Theresia kwa kifupi Tereza, Mwenyeji wa Musoma, Mgita, miaka 34, Mhasibu Mwenyeji Post Graduate, anafanya kazi kwenye kampuni ya simu 

Dada mzuriiii, ana mguu kama wa tembo honge la guu, mweupe maji ya kunde, mfupi, ana kishepu chake kizuri zuri kidogodogo 

Mwana Saikolojia: Tereza, Leo naomba uongee wewe Leo maana kwa maisha ulionieleza nadhani utaweka heshima leo

Tereza akasalimia pale na nini, akaanza kudondoka 

Tereza: mimi sipo mbali na aliyoelezea Mwelu wiki iliopita, Mwelu ndugu yangu mimi nakuelewa sana maana nimepitia huko huko lkn nikaamuaga kukaa pembeni

Kama nilivyowaambia nimesoma chuo hapa mjini Dar es Salaam, nimezaliwa Dar nimekulia Dar, michezo yote ya Dar naijua kifupi mimi ni mtoto wa mjini kwa sasa tunajulikana kama wadada wa mjini ila mimi sio Dada wa mjini zoba

Kwetu nimezaliwa mwanamke pekeyangu na kaka zangu 3 wamenitangulia jumla wa 4 kwahiyo unaweza elewa nimekuwa spoiled kwa namna gani kama mtoto wa mwisho 

Nilipomaliza degree ya Kwanzaa,  nilitoka chuo na Bikra yangu, mimi sikuwa mtoto wa gate kali ila sikupenda kujichanganya kwenye Makundi sikupenda na darasani nilipataga 1st class chuoni,  div 1 form 4 na form 6, form 1 mpaka 4 nilisoma St.Francis kifupi Kwetu tuna akili sana lkn sijui ngoja niongee Mwana saikolojia utanisaidia 

Kufaulu kwangu sana kwenye masomo kuliniwekea umaarufu mkubwa sana mpaka wanaume wakawa wananiogopa 

Nilipokuwa chuo nikaokokaga kwahiyo yale maisha ya ujana kwenda club nikawa sina 

Kiukweli sikuwahi kuwa na boyfriend maisha yangu yalikuwa kama Mwelu 

Nilipokuja kukumbuka shuka kumekucha ni pale nilipopata Post Graduate na kuona kila niliesoma nae ameolewa anawatoto, woooo hapo ndio mashetani yalinipanda 

Watu wooote niliosomaga nao wana maisha, familia, watoto nikiangalia mimi sikuelewa kwanini sipati mume wa kunioa

Kaka zangu walikuwa na marafiki waliokuwa wananipendaga nikawa nawakataa kwasababu ya wokovu 

Tatizo jamani sio Wokovu wala Yesu, Tatizo sijui kwa kweli ngoja niongee labda mtanielewa 

Kanisani ni kweli haturuhusiwi kuolewa na wanaume ambao hawajaokoka 

Koku: amen sister, mtasanda Duniani mpaka mkome 

Tereza: kwahiyo sio kwamba ofisini nilikuwa sipati wanaume lkn nikiwapata leo kesho wanataka walale na mimi kwa mtu alieokoka sawa sawa hawezi kukubaliana na haya labda akina Koku ndio watakubali sio walokole waliookoka kikweli kweli 

Uzuri wangu sikuwa najitangaza kazini wala kwa ndugu kuwa nimeokoka nilikuwa naulokole wa kimya kimya... nadhani unaweza niita mlokole wa chinichini 

Kuona wenzangu wameshaolewa wote na mimi wanaume wanaonifuata wananiimbia nyimbo za ngono kwanza


Sikuona haja hata ya kuwapeleka kwa wachunga alafu mimi sikuwahi kuwa mtu wa wachungaji, nikiingia kanisani hautajua nikitoka hautajua, gari naacha ofisini naenda Kanisani kwa taxi, nikikaribia ananishusha mbali natembea mpaka Kanisani 

Koku: at least wewe haukuwa mlokole zoba 

Tereza: wanaume wakaja kukata wale wa mtaani, nikawa nawapata wa Kanisani 
Tatizo la wa Kanisani walikuwa wavivu sanaa, wanakaa wanasubiria muujiza hawataki kufanya kazi

Koku: uhuhuhuhuuu! Hehehehehehe Preeeeach! sister Preeeeach! 

Tereza: mnaanza vizuri ukija kumfuatilia analala kwa kanisa analala kwa ndugu nilipataga wanaume 10 wote hawakujua naishi wapi nilikodisha hata nyumba uswazi nikawa nawadanganya naishi pale basi tu lakini walokole wa kiume wavivu jamani loh

Basi nikaachaga kudate wapendwa 

Koku: hahahaha eti wapendwa mxiuuui ndio mnajiitaga ivo ee?!

Mwana saikolojia: Koku tafadhali tupe utulivu muda sio rafiki 

Tereza: nikapataga bwana mchungaji, doh jamaaa ni muhunii, anatembea na waimba kwaya nje ya pale, kunasiku nilienda kwake nikamfumania kabisa anazini na mwimba nyimbo za injili maarufu nikawasha taa kwani unadhani waliacha? ! Ndio kwanza akaniambia nisubirie hapo sebuleni nimhudumie huyu nakuja 

Sikurudi tena kwenye maisha yake,  na ile nyumba ya uswaz nikahama nikapanga uswaz kwengine 

Basi siku moja tumeenda seminar ya vijana huko kanisa la Tabata akanifuata kaka mzuri mwenyewe anaonekana mtanashati, tukaongea akaniomba namba nikampa 

Kuja kuwasiliana nae ni mtoto  wa Mchungaji, alikuwa Malaya 

Hatari, yani akitoka shetani anaingia yeye 

Hapo nina miaka 29 nagonga 30, nazidi kuchanganyikiwa sijaolewa 

Yule mtoto wa mchungaji akawa ananifosi nilale nae kinyume na ninavyotaka, mjinga sana kwanza Kanisani ukimwona anavyopiga gitaa utasema Daudi wa kwenye Biblia katika kitabu cha Agano la Kale 

Fosi za hapa na pale kwenye geto lake nikamponyokaa nikaondoka nimeacha viatu ndani, maana Biblia inasema ikimbieni Zinaa nikakimbia kutoka nakutana na Dada mwimba kwaya anafungua mlango na funguo wala hakushtuka waswahili wanasema kisu chenye makali ndio kinaua mnyama 

Toka hapo nikasema wokovu baaaass kama usanii ndio huu staki tena kuskia wokovu 

Nikaanzaga kwenda Disco nina miaka 30, naenda Baa nakunywa ovyo narudi nyumbani usiku wa manane Uzuri nilishahama home nikapanga appartment Oysterbay, yani nikawa mtoto wa Yesu mwenye maumivu tele moyoni sikuwa na wa kunisaidia

Nikaanzaga kulia mwenye natafuta wanaume wanibake mara waniue naona kama nimeonewa kwanini maisha hayaendi?!

Ofisini nikapandishwa cheo nikaanza kusafiri na ma boss, tukasafirigi kwenda Kenya nikakutana na libaba limoja likanichangamkia ndio likanibikiri, toka hapo sikumwona tena

Toka nimebikiriwa na miaka yangu 31 sikuwahi kutulia utadhani shetani alifunguliwa huku chini ya kitovu changu, yani zile one night stand nilioigwa sanaaaa, kila mwanajme naekutana nae napugwaaa tena kavuuu nilipigwaaa midusheee nilipigwa machineeé mpaka akili ikakaa sawa nikaanza kuwa mjanja

Nikaenda kupima ukimwi sinaaa, mimba sinaa, nikajiambia kuanzia Leo mimi sitaki wanaume bora mradi nataka mabonge ya bwana

Basi toka hapo mimi nakaaga mahoteli makubwa,  nikipata mzungu hayaaa, mwamerika mweusi twendee,  mreno twendee, mchina twendee, mbongo twendee ila kwa nkingaa

Nilipigwa machine mpaka nikasahau Yesu anatamkwaje tena 

Maisha yangu yalikuwa mabaya sana sana lakini sio kazini 

Nikajaga kupata bwana wa kikurya jamani nilijutaaa yule bwana tulianza vizuuuri akanifanya nituliee kutulia kumbe yeye ni malayaaa, nikimfumania ananipigaaa, alafu alivyo mshenzi yule mjinga hakuwahi kutahiriwa Basi mechi ilikuwa mbayaaa yani doh kama una bwana wa kikurya achana nae mapema kabla hamjapiga shoo 

Kwasababu alikuwa ananipiga sana, nikaamua kuachana nae akaanza kunifuatilia ilimuuumaa hajawahi kuachwaaa akaanza kunichania tairi za gari anakuja nyumbani anapiga kioo cha nyumba nikaamua kuhama kumbe kamuweka mtu anifuatilie akajua napoishi Basi akija ni ugomviii anapiga kioo cha gari anapigana na mlinzi nikaamua kwenda Polisi,  Polisi wakaniambia huyu Bwana ana mtu wake juu tukimfunga kesho anatokaa na hizi kesi za kupiga wanawake anazo nyingi sana, cha kufanya hama mji au fanya chochote 

Nikaenda kuomba transfer nikahamishiwa Arusha,
Nikabadilisha simu na namba naanza maisha yangu upyaaa, nikaanza kazi wiki ya 1 ya 2 ya 3 nipo supermarket akaja kijana mmoja akanipenda ananisalimia vizuri mimi nampotezea sitaki kumjua wala anijue 

Akawa ananifuatilia akajua napofanya kazi, kila nikitoka kazini yupo getini, alikuwa gentlemen flani hivi ah mwisho wa siku Nikaamua kumsikiliza,

Tukawa marafiki mwezi 1 hajaomba chiu,  wa pili hajaomba mechi, mwezi wa 3 akaomba kunioa nikasema eh huenda huyu ni Mungu nikakubali

Nikampeleka nyumbani mwezi wa 4, mwezi wa 5  harusi ikafungiwa Arusha, ndoa ikaanza, Tukawa tunaishi vizuri mwezi wa 1 mapenzi moto moto.. mwezi wa 2, wa 3, wa 4 nikashika Mimba, niliposhika Mimba tu yule bwana sijui alikuwa ameficha makucha, jamani nilikoma, nilikuwa napigwaaa kila akinywa pombe napigwaa nikavumilia vumilia ndoa changa ya miezi 5 na Mimba miezi 2, Mmasai alikuwa ananipigaaa akaniambia acha kazi kwa mana Yeye anahela za kunitunza, nikakataa, basi kila akirudi nikipigooo kasoro jumamosi na j2

Mimba ikakua miezi 8 ikafikia, kazini sikuacha kwenda nikazoea kipigo cha Mmasai akaja mama mkwe kusikia ninakaribia kujifungua,  akaishi pale akajua kuwa mume ananipigaaa akamuonyaa akaacha wiki 3... Mimba ikaingia miezi 9 sasa muda wowote najifungua 

Sikuhio mama mkwe amelala ndani anaskia tunagombana, jamani nilipigwaaa Nilipigwa miteke ya tumbo nilikumbuka majina yote ya Mungu wa Yesu Kristo 

Namimi nikawa mbishi sasa akinipiga na mimi narudisha mechi, nachukua chupa nampiga anakwepa, nachukua meza namrushia anakwepa, nachukua kiti nampiga anakwepa akanikamata akanibana shingo sasa ananikaba kaba na wewe mpaka nashindwa kupumua akaja mamake anaachanisha hawezi mimi huku damu zimeshaanza kunichuruzika 

Huku nakabwa huku ananipigaaa mateke ya tumbo Sikuhio nadhani nilipigwa kuliko siku zote nilizowahi kukaa kwenye ndoa 
Mamake akachukua Fimbo akampiga mgongoni akaanguka chini,  nikaachiwa na mimi chini sikukumbuka kitu najikuta hospital nimelala mama mkwe pembeni kalala, afande pembeni amekaa sikuelewa nikarudi kulala 

Asbh nikaamka mama mkwe akaja anachekacheka nikamsalimia afande nae akanisalimia akanieleza kilichotokea kuwa mume wamemkamata yupo kituoni amewekwa ndani kwa kosa la kuua 

Tereza: kamuua nani?

Mama mkwe: analia pembeni

Afande: mwanao umempoteza kwa kipigo cha jana kama sio mama mkwe na wewe ungepoteza maisha mshukuru sana Mungu wako 

Tereza: nikalia wee mpaka wakaja kunichoma sindano nikalala 

Baada ya siku 2 nikatoka hospital, watu wa ofisini wakaja kunisalimia nikawaeleza kila kitu boss akasema basi nikuhamishie Mwanza ukaanze maisha huko nikakataa

Mama mkwe akaja kurudi kwake Umasaini baada ya wiki 1

Baada ya wiki 2 akaja mwanasheria akanisainisha talaka nikasaini akaipeleka jela mume akasaini nikawa huru sasa nimerudi nilipotoka sina mume kafungwa maisha, sina mtoto amekufa,  nikafanya kazi wiki 2 nikaona Arusha pachungu, nikaomba kurudishwa Dar maana mwaka na nusu umeshapita tangu nitoke Dar

Boss akanirudisha Dar nikapewa nyumba Mikocheni nikawa naishi hapo na kazini sio mbali 

Yule mchumba aliekuwa ananipiga mpaka nikaomba uhamisho alikuja kufungwa maana alimpiga mtoto wa Chief mmoja hapa nchini wakamweka ndani ndio ikawa pona yangu kwa maisha ya Dar

Tangu hapo na sasa nina miaka 34, sijawahi kutaka mahusiano tenaaa, nipo singo sitaki kusikia wanaume wala mapenzi 
Mimi nipo singo kwa kupenda 

Kanisani sijataka kurudi tena kwa Walokole nasali Lutheran kwa Dini ya wazazi wangu

Huenda wokovu umewasaidia wengi ila sio mimi kwakweli 

Nampenda Mungu sana na nasali sana, namtumikia Mungu kwenye huduma ya Mwalimu Mwakasege, hio inatosha kwa sasa 

Wanaume kwa sasa hapana ngoja Kwanzaa nipone kidonda 



Tuonane Jumatatu tar 21 May 2018 saa 1 usiku ya Tz

--------------------------------------------------------------- 

D. Nipo sing'o kwasababu Ng'ombe hawazeeki maini 

Ashakumsi matusi Kwa Mwalimu na wanafunzi wote 

Wote: ahahahahaha 

Kwajina naitwa Kulthum, sina kifupi wala nini, kama mnavyoniona mimi ni kibonge, mfupi, mtu wa Tanga, Mdigo Baby! Ndio je mimi mfupi wadigo sio wafupi ila mimi ni mfupi

Mfupi na kibonge, nimeishia kidato cha 4, ila sikufaulu nilipata divishen 0 lakini divishen 0 ya shule sio ya maisha 

Kwa sasa nina miaka 35, sina mtoto, sijaolewa, nimejiriwa kwenye hotel moja kariakoo kwenye mapokezi. .. Mimi nipo singo Kwa sababu moja tu, kwanza staking kuolewaa, pili staki watoto, tatu nipo singo kwasababu ng'ombe(wanaume) hawazeeki Maini... kwangu mimi kuwa singo ni kama ajira... unajua kwanini?!

Kama mtu ukiwa singo unakula kila kitu na kupata kila kitu bila stress kwanini nikaolewe?!

Ndio mimi kwetu wa kwanza na wadogo zangu washaolewa kwahiyo?! Ina who?! Hai-who babu wee! Habari ndo hio

Nawashangaa hawa waliotangulia wanavyochanganyikiwa kwasababu wapo singo! 

Mwana saikolijia: kwanini upo kwenye hili darasa sasa?!

Kuluthum: kusema ukweli, nimekuja Kwa ajili ya hizo safari unazosema baada zitakuwaepo, as hivi sina bwana nategemea kupata bwana kama tutasafiri, hela yangu haiendi bure, nilipolipa ada nilijua nalipa kwa ajili ya nini

Inawa watu wananisema nimepagawa na machine za kiume lakini me najiona nipo sawa, sijapagawa

Nyie hamjui tu, wanaume muwatumie mkiwa na shida tuu au mna hamu tuuu, mambo ya kujigandisha Kwa wanaume weee ndio mana mnalizwa

Mimi hakuna mwanaume ananisumbua kichwa, sina muda wa kupendaa

Mimi napendwa tu, na nikiona unanipenda sana nakuachaaa 

Watu wanapenda kuniita Mdangaji, ila mimi siamini kama ni mdangaji kwasababu zifuatazo:

1. Wanaume siwafuati wananifuata wenyewee na najua jinsi ya kuwapata bila kutumia nguvu

Mfano: najua wanaume wanapopatikana, nikitaka mwanaume wa aina flani labda matajiri, naenda sehemu za matajiri tuuu, kama Masaki, Mbezi  Beach, Kunduchi, Zanzibar, Arusha, Mwanza yani kwenye mahotel makubwa makubwa tu sio hotel zenu mavi mavi alafu unamlaumu Mungu hakupendi wakati wewe hujui kuzitumia hela na uchumi ambao Mungu kakupa 

Disco vumbi sijui maisha basement siendi, wala mende baa siendi kwanza ukinikuta ntaumwaa bora nilale nyumbani

2. Najua kujitoa ufahamu
Nikitoka out kwenda kudanga kwanza sivai chupi, ya nini, pili lazima nivae kivazi cha kutega cha kumwita mwanaume njoo, tatu akija lazima nijinatishe nanata kiduuuuchu ili nione ana uwezo kiasi gani sio unajirahisiiiisha mpaka anakuona njaa hapanaaa

Akikubali kukaa na mimi kula na kunywa lazima alipe yeye, akishakipa labda lakini 2 au 3 maana mimi vinywaji vya pombe za mataputapu sinywi ..bili zangu zote nikiamua kutoka kima cha chini ni laki 2 au 3

Lazima uizoee baa yako na uwe na urafiki na ma baa attendant, maana wateja wengine wakorofi, akikataa kulipa bili mliotumia unaongea na baa maid anakusaidia unaondoka zako, anakamatwa yeye

Nikiona mwanaume anazuga hataki kulipa najua huyu njaa, namwita baa medi namwambia bili atalipa huyu naacha pochi hapa naenda toilet aniangalizie (ndani ya pochi naacha condom 5 na elfu 1 na kitambaa cha kujifuta jasho) akiiba pochi imekula Kwake


Pia inamrahisishia baa medi kudai hela kwa huyo bwana aliejidai kunifuata na kama ataondoka na pochi yangu ndani atakutana na condom na mazagazaga yaliosalia

3. Mapenzi hayana kinyaa
Ukishakubalu kwenda na mwanaume hotel ( sio ghetto lake wala kichumba mbuzi) ... akikwambia weka mguu pande unaweka, mguu sawa unaweka, nenda kushoto unaenda, kulia unaenda 
Ukiambiwa kula koni unakula kweli kweli mpaka anapagawa 

Tatizo lenu nyie maspinsta watarajiwa mkiwekwa mechini mkabinuliwa mnaanza mapozi me siwezi, me sijui, me siendi, naskia kinyaa, hiki sifanyi, hiki nafanya... unaleta mambo ya kuboa boa unamboa mtu na pombe zake anaona alale tu mwisho wa siku kesjo hakutafuti tena 

Mwanaume lazima umchanganye mechini umpagawishe mpaka akiamka asbh anachokumbuka ni jana usiku

Sio unaleta ulokole ulokole Yesu kazema mkazae na kuijaza nchi, kitandani ni malazini lazima ujimwage kama shangingi mmesikia we Teresa na nyau Mwelu?!

Koku: ahahahaha watakuelewa baadae sana hao labda kama ataongea Mwalimu Mwakasege au Mchungaji wa Kanisa Lao ndio watafanya we endelea na somo hili la leo nimeliewa sana 

4. Mwanaume akikuita tena nenda kwani shida nini, ukienda mara ya 2 akataka ufanye kama jana au juzi we kubali, akimaliza hapo lazima akupongeze. .. mimi mwenzenu ninaishi kwangu nimejenga kwasababu ya chiu, nimenunua magari 2 kwasababu ya chiu, nina shamba kwasababu ya chiu, kazini nimepandishwa cheo kwasababu  ya chiu, chiu imenipeleka ulaya nimesafiri nchi 20 mpaka navyoongea kila nchi haijirudiii nawashangaa nyie


Walokole mnavyokalia chiu utadhani kuna medali mtapewa siku za mwisho woi!



5. Usiombe ombe wanaume hela, yani wewe ukikutana na mwanaume unamtangazia shiiidaaa utadhani umekutana na Mungu, woi! 

Kwani wewe mlemavu au?! Si una ajira yako?!



Wanawake sisi tungekuwa na mindset  (mtazamo) kama wangu kuwa mwanaume hata akinitumia vipi sitamwomba hela tungefika mbali 



Kwanzaa wanaume hawatutumii, tunatumiana, kwani yeye raha hapati au?!

Si wote mnapata?! Sasa unalalamika nini kuwa unatumiwa vibaya na wanaume wanakuzeesha kwani ukikaa mwenyewe hautazeeka?! Tena ndio utalongoroka kwa magonjwa na siku zako za kuishi zitakuwa chache, bora ujitahidi utimize alichokisema Mungu kuwa zaeni mkaongezeke mkaijaze Dunia yaishe 



Muache kusingizia wanaume kuwa wanawatumia wote mnatumika sema tu labda mnakuwa hamjapendana 



Mimi siwaelewagi wale wanaosema mwanaume kanipotezea Muda, amekupotezeaje kama wewe mwenyewe haujataka kupotezewa?! Kama haukutaka kupotezewa Muda Si ungeondoka kwani alikushika?!



Mwanamke unakuwaje zoba kiasi cha kupotezewa Muda? !



Mimi sipendi watoto nahakikisha siku za hatari najituliza ndani akiniita nasema naumwa au sipokei simu,  mahusiano ya kugandana na mwanaume sinaga 



Mwana saikolojia: my dia Kuluthum, unaongea kama Mwanamke mwenye maumivu na alievurugwa, skia mami hakuna binadamu alieletwa duniani awe kuwa kisiwa cha watu kupita na kuondoka unauhakika haujawahi kupenda?



Kuluthum: kupenda wanapenda watoto wadogo sio mimi, kwani hamjasikia watu wanasema Wanawake ni Dunia? ! Maanake  



Tumeletwa Duniani kutumiwa tu na wanaume

Mwana saikolojia: ukisema hivyo utakuwa umekosea na unajikosesha haki yako ya msingi

Kuluthum: haki za msingi zote nazipata, hizo zako ni zipi?!

Mwana saikolojia: Kuluthum mami, mapenzi sio utumwa mapenzi sio ndoo kiasi kwamba ukinge tuuu maji yawekwe yakatumiwe

wooote hapa tunawazazi waliopendana na kukubaliana wakaoana wakapata watoto tukazaliwa kwa ajili ya mapenzi ya wazazi wetu 

Kuluthum: kwahiyo mwl unakata kusema watoto wote wanaozaliwa wanazaliwa kwa sababu ya baba na mama kupendana? ! Je wanaobakwa?! Watoto wanaotelekezwa?!

Mwana saikolojia: naongelea upendo unachokosa ni upendo

Kuluthum: mimi napendwa ndio Maana kila napoenda napata Bwana, sio kama hawa majinga jinga, wanapata mabwana wanaleta pozi wao wanalalamika hamna wanaume

Mwana saikolojia: wewe haupendi wewe hauna tofauti na mtu anayejiuza na sijui kwanini unajiuza kwanini usitafute mtu mkapendana mkaanzisha familia mkapata watoto mkasonga mbele kwanini unachukia sana watoto na wewe ni mzaliwa wa kwanza?! Shida ipo wapi?! Kitu gani kilikutokea mpaka haupendi watoto, ndoa, unatumiwa unaona sawa? ! 

Kwanini unajidharau namna hii hata thamani yako kuwa Mwanamke hauijui?!

Kila mwanadamu ana thamani, Wanawake wanaume wote wana thamani, sijaelewa kwanini umejidharau kiasi hiki 

Kuluthum: love ni Bullshit hamna love Duniani... wanadamu wote nawapenda ila mpaka Sasa sijapata wa kunipenda kunifanya nitulie nianze maisha ya familia naona usanii mwingi tu mtaani

Si unaona mwalimu mwenyewe



Hawa mademu wanalia kuhusu wanaume walivyo wabaya. . Bora tu ufanye yako mengine mbele kwa mbele 

Kama ulivyoniuliza kwanini nipo singo na mimi nimekujibu nipo singo kwasababu ng'ombe hazeeki maini, na ng'ombe naowapata mimi hawana stress na mimi, wananitunza, wananilisha,  wananivisha, kila kitu napewa, nikisafiri haja kubwa naenda, haja ndogo naenda, hakuna nachokosa kwahiyo mimi kuwa singo hainisumbui kabisa,  haya ndio maisha yangu mpaka nitakaporudisha namba kwa Muumba hata kama mtanihukumu

Mwana saikolojia: akachokaa! Akaamua kuweka pozi baadae akaendelea
Ambacho mnanishangaza wote mliosema hapo awali ni kwamba wanaume wote wabaya Je mmeshawahi kujiuliza wenyewe kama nyie mnaowashutumu wanaume kama ni wazuri?

Kama wewe ni mbaya au una tabia mbaya au unaroho mbaya kwanini upate mwanaume mzuri?! 

Hamjawahi kusikia kizuri kinavuta kizuri chenzake?! Hata sikumoja Mungu hawezi kukupa Kitu tofauti na ulivyo, anakupa wa kufanana nawe 

Leo ninawapa homework mkifika nyumbani andikeni kwenye makaratasi  ma5 tofauti

Karatasi la:
1. Andika wanaume wooote uliowahi kuwa nao kimapenzi tangu unakua mpaka sasa ... Hata kama bwana wako alikuwa mchungaji au sheikh mimi sitahukumu

2. Andika mazuri yooote ya hao wanaume uliokutana nao

3. Andika mabaya ya hao wanaume wooote uliokuwa nao

4. Andika mazuri yako yoooote unayohisi na kujua unayo 

5. Andika mabaya yoote unayohisi  (unayojua) unayo


Alafu kila mtu aniletee darasa lijalo 

Najua tumebakia watu 2 kujielezea na Najua wote hatutokuwa mbali na ukweli watakaouelezea lakini naomba muandike na mniwekee kwenye bahasha za A4 juu ya bahasha muandike majina yenu 3 mniletee kila mtu kwa wakati wake. .. sawa

Wote: sawa mwalimu 


Tuonane Kesho tar 22 May 2018 saa 1 usiku ya Tz kuona nini kitafuata 








-----------------------------------------------------------------------


E. NILITAPELIWA KIMAPENZI NDIO MAANA NIPO SINGO 

Naitwa Rebecca ni mzaliwa wa Dodoma, nina miaka 32 nimfanya biashara wa nguo za kiume na kike nina duka kariakoo 

Nimefahamiana na mwana saikolojia kwasababu ni mteja wangu, sikumoja alikuja dukani kwangu kwa mara ya kwanza akanipenda nilivyovaa akaniambia anataka nguo kama yangu,  lakini wakati namtafutia nguo, akaniambia anti mbona hauna raha, unaonekana hauna raha kabisa kwanini nikatabasamu tu na kumpotezea

Basi kila mwezi akawa anakuja kununua nguo mpaka akajenga urafiki na mimi, tukawa marafiki ndani ya miezi 6 akajua tatizo langu ndio kuniambia kazi anayoifanya akanialika mahali hapa nipate kukutana na watu na marafiki mbali mbali 

Mimi sijawa singo kwa kupenda,  nilikuwa na mpenzi wangu tuliesomaga nae chuoni, tulianza urafiki wetu tukiwa mwaka wa 2, tukawa tunapendana sana, ila hatukutaka watu wajue tukawa tumeweka uhusiano wetu kwa siri 

Mpaka tunamaliza shule yeye akapata kazi kwenye kampuni ya simu lakini mimi sikufanikiwa kupata ajira nikaendelea na masomo ya masters, 

Mapenzi yakazidi kukolea mimi naishi na wazazi yeye anaishi kwake kuonana weekend lakini lazima nilale nyumbani kwa wazazi 

Wakati nasoma masters nikawa napata wakaka wananipenda mimi kama wanawake wengi wanaoamini true love nikawa nawakatalia nikilinda penzi langu na Crispin! 

Alikuwa anaitwa Crispin, sikujua hili wala lile kumbe mwenzangu alishaanzisha mahusiano ofisini na dada mwingine bila mimi kujua, na hivi nilikuwa naishi nyumbani kwa wazee, ilikuwa ngumu kumfumania

Uzuri wangu mimi nilikuwa nina ulimi mzuri kwa maana ya kaulu, mtu yeyote aliekuwa karibu yangu akiongea na mimi lazima atanipenda sikuwa najigamba 

Ajabu ya Crispin ni kwamba hakuwahi kunionyesha kwa sms wala simu kuwa Alikuwa na mwanamke mwengine hata kwake sijawahi kumfumania 

Nikawa napata wakaka wazuri wazuri shuleni nawakataa kisa nampenda Crispin

Shule ya miaka 2 ikaisha tukatawanyika kila nikiomba ajira nakosa, sipati, nikaenda kwenye maombi naombewa lkn wapi, kazi sipati, nimeshaombewa weee na kutabiriwa weee nishafunga sana na kumwomba Mungu lakini wapi, hapo nina miaka 3 sina ajira, miaka 4 kwenye mahusiano... nimechanganyikiwa sina cha kushikika

Nikaamua labda nifanye biashara huenda itanilipa, nikaomba sapoti nyumbani nikapata frem kariakoo nikaanza kununua vitu kwa wakinga kwa bei ya jumla nauza rejareja, nikakutana na wauzaji wenzangu wakaniambia machimbo ya huko China, nikajipanga na familia ikanisapoti kwa kunipa mtaji, nikadondoka kuingia China na wadada 2 wafanya biashara, nipo buzy mgogo natafuta hela kama mchaga, 

unajua watu wanasema wagogo ni omba omba lakini kwetu hatuna tabia ya uomba omba tunaamini kwenye kufanya kazi.

Nikafundishwa machimbo yote ya china, baadae tukaambiwa kuwa kuna machimbo ya Thailand na Uturuki tukiwa China, tukaamua tudondoke Thailand wakati tumeshaisafirisha mizigo kwenda Tz,

Tukafanikiwa kupata chimbo zuri la mavazi ya kike na kiume Thailand, muda wa kukaa ukaisha ikabidi tuondoke kurudi Tz


Nipo buzy na maisha sina hili wala lile  Nafanya biashara natangaza kwenye WhatsApp kwenye Facebook biashara zangu, nikijua kuwa mchumba yupo tu, tena wakati mwingine nikiishiwa hela ananipa hela nyingi tu nachukua Mali nauza

Sikumoja akaingia mteja dukani kwangu, kama kawaida mimi na lugha nzuri ya biashara akanipenda alafu akaniuliza samahani nahisi nakufananisha au nimekuona mahali, basi tukaongea kwa kirefu sana akajua niliposoma chuo kumbe tulisoma chuo kimoja ila madarasa tofauti, tukaanza kupiga stori za watu wa shuleni, yule vepe yupo wapi, ameoa au ameolewa anafanya wapi, ana watoto wangapi, katika ongea ongea akaniambia na yeye anaolewa wiki ijayo, nikamtamania sana, dada Alikuwa mrembo, mweupe, mpare kafupi kenyewe kamejaliwa shape mrembo kweli 

Akaniomba nimsaidie kupata gauni la sendoff nikamwomba arudi baada ya siku 3 nitakuwa nimempa jibu,

Baada ya siku 3 kweli akaja, akashuka kwenye gari gari ikawa inanguruma namwuliza mami kwenye gari kuna mtu!? 

Akajibu ndio nimemwacha bwana harusi anashikilia parking asifungiwe, tukaendelea na yetu,

Akajaribisha nguo akaipenda sana akaona amshirikishe bwana harusi wake akampigia aje ndani akamwomba dada wa dukani akamwangalizie gari 

Wakati bwana harusi anakuja yule demu wa kipare akatoa kwenye pochi kadi akaniambia nashukuru sana umenisaidia kupata nguo naomba nikualike kwenye sendoff yangu nikakubali 

Bwana harusi kuingia tobaa ni Crispin, nilihisi kufaa, Crispin mwenyewe kuniona hakuamini, unajua Crispin hakuwahi kuja kwenye duka langu kabisa, kila akipanga kuja anasema ana dharura  Dharura hizo zikawa nyingi mpaka nikaja kumkamata mwizi 

Aliponiona akakosa raha akanifanyia kidole ssshhhh Kwanzaa sikumwelewa nikapanga nimfanyie fujo pale pale dukani kwa kumwitia mwizi nikasema hii kariakoo navyoijua nitafungiwa duka kama sio kuporwa Mali, akaingia mwenyewe wanaitana Bebi Bebi yule demu wake anamtambulisha kwangu huyu ndio bwana harusi wangu anambusu mimi natamani kuzimia sizimii, nikashikwa na hasira nikamwuliza yule demu walikutana wapi walifahamiana 

Demu: tunafanya nae kazi kampuni moja lakini ofisi tofauti tulikutana kwenye seminar za kiofisi mwaka huu miezi 4 iliopita 

Rebecca: nikachokaa! Nikipiga mahesabu ndio ule mwezi nilienda China na Thailand jamaa akaamua kulipa mahari nikiwa sipo nikachukua kiti nikakaa huku Crispin suruali imembana mana hajui kitakachofuata si unajua hasira za kigogo ni kuua na kula nyama uliochinja! 

Demu alipomaliza kuongea nikamwambia demu 

Rebecca: mami badilisha nguo uje ulipie utanielezea ukiwa unalipia 

Kweli akaenda kubadilisha nguo mimi namwangalia Crispin ananiomba plz plz nisilianzishe plz 

Demu alipotoka nikaichukua ile nguo, nikamwomba akae kwenye kiti,

Nikamweleza A to Z ya Crispin, demu anashangaa, how imekuwaje!?

Nikamwambia huyu bwana nimekuwa nae tangu chuoni mpaka sasa ni mwaka wa 4, nimekataa wanaume wengi sana kwa ajili yake, ningekuwa nimeshaolewa nimeshapata watoto ila kwasababu nilimpenda sana nikijua nae ananipenda kama ninavyompenda nikawA nawakataa wale wanaume 

Leo hii mlangoni mwa duka na nyumba yangu unaniletea  Mwanamke unaetaka kumuoa wiki 2 zijazo?!

Naomba wewe na huyu chaufupi wako kama kigoda mtoke haraka kabla sijawaitia mwizi, we chaufupi achia nguo yangu na mtoke kabla sijawaitia mwizi matapeli wa mapenzi wakubwa

Na tena nitahakikisha hii harusi haifungwi mpaka unilipie fidia za kunipitezea muda mjinga mkubwa wewe tokAaaa tokeni mara watu wakajaa kidogo niwaitie mwizi 

Siku hio nguvu ziliisha nikaamua kufunga biashara mapema,  nikaenda kwa mwanasheria Nikamweleza kuhusu shida yangu akaniambia anaweza kunisaidia kwa kupotezewa muda kuna fidia natakiwa nilipwe na pia wanauwezo wa kusimamisha ndoa 

Nikapewa karatasi ya kumpelekea Crispin ya kuitwa aje ajieleze, nikaipeleka ofisini kwake, baada ya Siku 3 akaja kwenye ofisi na mwanasheria wake tukakaa tukaongea mwanasheria wake akamwelewesha tatizo lililopo na ninaweza simamisha harusi isifungwe kwahiyo kama nataka kuendelea na harusi anilipe fidia kwa kunipotezea muda kama hataki kesi ipelekwe mahakamani 

Mara ya Kwanzaa alikataa akifikiri ni utani yule mwanasheria wake akamwelezea kuwa ikienda mahakamani watahakikisha hataweza kufunga ndoa Tz hii na watamuandika vibaya kwenye magazeti inaweza ikamharibia ajira yake mana atatangazwA kama tapeli wa mapenzi na kufanya hata wakwe wamkatalie kuoa kwao 

Akayapima akayaona ni Kweli,  kazi anaitaka na demu wake anamtaka akakubali kulipa fidia 

Wakajumlisha na kutoa na kugawanya, mwanasheria wangu akasema nilipwe mil 30, Crispin akakataa, mwanasheria wa Crispin akasema watalipa mil 5

Mwanasheria wangu akasema  Kama mil 30 hataki waende mahakamani hata mil 50 itatoka mpaka mil 80, huyu ni mwanamke mmempotezea muda biologically psychologically ameshaumizwa na fidia yake ni kubwaa 

Mwanasheria wa Crispin akajaribu kumwelewesha Crispin kakataa sina hela bora yaende mahakamani akaondoka tukatawanyika 

Baada ya wiki, mwanasheria wangu akaniambia niende ofisini Siku hio hio, mimi nikijua naenda kuambiwa kuhusu mambo ya mahakamani kufika naambiwa Crispin amelipa mil 30 zote na amesaini na ameandika barua hii hapa ya kuomba msamaha anaoa kesho 

Rebecca: nikachokaa, nikajiskia mjinga Nikamweleza mwanasheria wangu? milion 30 za nini? ! Mil 30 zitanisaidia nini?! Mil 30 zitalipia muda niliopotezewa?! Je kupenda?!

Mwanasheria: mami chukua pesa, kuna watu wanaachwa kwenye ndoa kwenye mahusiano zaidi ya miaka 5 wengine 8 wengine 9 wengine 11 na wanaachwa hawaji kudai haki zao 

Kweli nakusifu kuwa na akili ya kwenda kwa mwanasheria na kulalamika wengine hawana 

Jipeleke vacation, jisafirishe uka relax huwezi jua utapata mwanaume mwengine mkapendana achana na huyu boya hakuwa wa kwako, 

Nikamshukuru mwanasheria nikamlipa chake nikaondoka kwenda bank moja kwa moja nikaziweka hela nikarudi nyumbani, nikalia wee ndio namkumbuka Mwanasaikolojia nikaomba kuonana nae akaniambia nije kwenye darasa sijui nini, ndio nipo hapa 

Nipo singo kwasababu mwanaume niliempenda amenitapeli kimapenzi bila kuniambia 

Wote: wakabaki wanashangaa hawaelewi jinsi gani mgogo ametumia akili kudai chake na kupata fidia ya tatizo lake 


Tuonane kesho tar 24 May 2018 saa 1 usiku ya Tz
------------------------------------------------------------------------ 
F. NIPO SINGO KWASABABU NIMEUMWA UKICHAA 

Mwana Saikolojia: leo naomba utulivu wa hali ya juu maana ndugu yetu anayejielezea kidogo hayupo sawa kama sisi ndio anapona heshima kubwa iwepo tafadhali 

Wote: sawa mwalimu 

Mwana saikolojia: Karibu rafiki yangu Aminata 

Aminata: asante mpendwa wangu?  Habari zenu wote

Wote: nzuri 

Mwana saikolojia: Aminata najua umeshapona mimi naamini umepona kabisa, na najua unaweza kujielezea vizuri sana ... embu tuelezee kwanini upo SINGO? !

Aminata:  NIPO SINGO kwasababu ninaumwa kichaa 

Mwana saikolojia: hapana kichaa umeshapona bwana wewe tuambie kwanini upo SINGO,  tuelezee maisha yako ya zamani ulivyokuwa kwenye mapenzi mpaka sasa 

Aminata: sawa Mwalimu 

Kwajina naitwa Aminata, kwakweli, kilichonifanya niwe SINGO,  ahiiiiiiiiiii  (akaanza kulia kwa uchungu) mpaka akagalagala ikabidi wamshike wambembeleze, hapo ni nusu saa ishakata ndio kaka sawa 

Akapewa tena nafasi ya kujieleza 

Aminata alikuwa mrembo sana, mzuri shape namba 8, maji ya kunde classic miaka 34, anafanya kazi kwenye shule za wazungu huko Masaki kama receptionist msaidizi 

Kwani ukiambiwa kichaa utaamini?! Huwezi alafu huku darasani alikuwa anakaa siti za nyuma hafanyi fujo mpolee anatabasamu tu hagombani haongei Mrembo pia mtu wa Iringa 

Aminata: zamani nilikuwa na mpenzi wangu, tunapendana sana aliitwa Ahmed, tulikutanaga kwenye school bash za vyuo tofauti tofauti tukapendana sana, mpaka tunamaliza chuo, huyu anapambana huku na yule kule 

Yani mapenzi moto moto ni kama romeo na Julieth Yeye ndio alikuwa mwanaume wangu wa kwanza, tulipendana sana 

Mimi nilikuwa nimeajiriwa kwenye kampuni ya Simu Yeye kaajiriwa kampuni ya Cement, kila tukitoka kazini anakuja kunipitia na kunirudisha nyumbani,  au tunaenda kula dinner ananirudisha, asbh ananipitia ananipeleka kazini kwangu ndio anaenda kwake, mchana anakuja kunipitia twende kula lunch kama sipo free au hayupo free ananiambia hatuonani mchana 

Tukawa tupo pazuri sana, mwisho wa mwezi ananipeleka shopping Mlimani city, Yani maisha flani ya exposure, kila kitu chake kilikuwa changu na changu chake, hakutaka nirubuniwe nje wala kuzuzuliwa na mwanaume yeyote ndio alikuwa analipwa mshahara mkubwa kuliko mimi, mwisho wa mwezi ananionyesha mshahara wake, kila week ananiwekea vocha kifupi mshahara wangu ni kama ulikuwa unasimama na hajawahi kunikopa wala kuniazima hela, tumekaa kwenye mahusiano miaka 2, na kwa dalili tulizokuwa tunaenda nazo nilijua muda wowote ananioa 

Mapenzi mapenzi na wewe akapelekwa kikazi mkoa kwa muda wa miezi 6 kila siku kila saa ananipigia simu akaanza kunipa na ahadi ya kunioa nikirudi Dar nitaleta wazee maana nahisi hii kazi watanileta mkoa moja kwa zote 

Sikumoja natoka kazini nasubiria lift ya mfanyakazi mwenzetu maana foleni zilikuwa kali kweli kweli 

Akaja kaka mmoja na gari yake landcruiser akaniambia twende nikupe lift, nikakataa, akaniambia twende nimetumwa na bwanawako mimi rafkiake nafanya nae mkoa nimekuja maramoja 

Nikataka kukubali nikasita, akachukua simu yake akanionyesha picha ya mchumba wangu  

Wamepiga pamoja, mmh moyo unasita lkn akili inakubali

Akanieleza mpaka na jina la utani ambalo Ahmed ananiita nikaanza kuamini, nikampigia simu Ahmed hapatikani, nikimpigia simu shosti yangu wa ofisini ananiambia amebanwa na bosi wewe nenda nitachelewa sana

Yule kaka alinifosi mpaka nikaona sasa nimkubalie tu nikapanda kwenye gari huku nimemwachia Ahmed sms kuwa nimepanda gari ya kaka mmoja namba ni... anasema ni rafiki yako

Basi nikapewa lift mpaka nyumbani, tukiwa njiani ananiambia kesho pia nakuja kukuchukua nikupeleke ofisini, nikamwambia hapana nikaingia nyumbani, usiku huo namtafuta mpenzi wangu hapatikani ambavyo sio kawaida yake ah basi nikalala.... kesho asbh kweli saa 12 nanusu yupo getini, doh nikachoka

Huyu kijana alikuwa mchangamfu sana, sana zaidi ya Ahmed, mcheshi, mstaarabu alikuwa na tabia tofauti na Ahmed na vitu vingi aliongea kuhusu Ahmed vilikuwa vya kweli nikajua ni kweli rafiki yake

Basi wiki nzima anaifanya kazi hio ya kunichukua na kunirudisha, weekend ikafika anapiga simu kama chizi nikimwuliza Ahmed yupo wapi anasema amesafiri nje ya nchi ghafla sikuhio wamesafirishwa usiku usiku ndio maana ameniomba nije kukuchukua kwa niaba yake nikajua kweli maana wiki nzima sikumpata Ahmed wangu

Wiki ya 1 ya 2 ya 3 mwezi, miezi 2, miezi 3 hakuna cha Ahmed wala simu na huku Huyu kaka mwengine ameshaniteka kiakili na keshajieleza kuwa ananipenda anataka kunioa

Mara ya mwisho nimeongea na Huyu kaka aliniambia kuwa Ahmed ananidanganya yupo na wanawake wengine mkoa anakula nao bata

Akanipa namba ya Ahmed ya 2 ambayo sikuwa naijua, akaniambia mpigie nayo kwa kupitia namba ya ofisini au mtu mwengine utaniambia au nenda mkoa Akanieleza mpaka na nyumba anayoishi utamkuta na mwanamke anaishi nae

Sikutaka kumwamini yule kaka nikaona niombe likizo niende mwenyewe mkoa nikashuhudie kufika Mkoa mpaka nyumbani kwa Ahmed kumbe kweli yule kaka alikuwa anasema ukweli, Ahmed ana mwanamke kweli tena wanaishi wote tena nimewakuta wana Do!

Doh nilichokaaa nguvu ziliniisha nikaanguka Chini kuja kuzinduka napepewa  na Ahmed na mwanamke wake
Nilipokaa sawa ananiambia sio kama unavyodhani na maelezo kibao mimi hamu imeniisha nikaanza kumkumbuka yule kaka nikachukua simu nimpigie akapokea namwuliza yupo wapi ananiambia nipo mkoa huo nilipo nikamwomba aje anichukue akaja baada ya dk 20 nikaondoka nae njiani nzima ananibembeleza njiani nzima nalia nilichanganyikiwa wala sikujua Dar nimefikaje lakini nilirudi na likizo nikamalizia kwa kulia huku yule kaka ananibembeleza ivyo ivyo mpaka nikaanza kumwelewa yule kaka, basi kazi ikaanza nikaendelea na maisha kila siku namuwaza Ahmed mpaka miezi 3 ikaisha ndio nikaanza kufungua moyo wangu kwa Huyu Kaka mgeni, nikaanza kumsikiliza nikaanza kumpenda na yeye akawa ananipenda...kwa muda wa miezi 6 mbele mapenzi yetu yakiwa mubashara kabisa, yule kaka akapotea

Mwana saikolojia: akapotea?! Akapoteaje? !

Aminata: sikumpata kwenye simu,  sikumwona akija kunichukua, alipokuwa anaishi alihama,  ooo nilichokaaa nilichanganyikiwaaa, ah baadae nikaona bwana basi

Huenda alitumwa
Nikaendelea na maisha baada ya mwezi m1 akarudi kwa nguvu zaidi ya zamani, mapenzi mara 2 ya zamani, akaniambia simu iliibiwa akakosa kila kitu kwenda kurudisha mawasiliano hakuwa na namba yangu alafu alisafiri kikazi, ila ndio alirudi kwa fujo na mapenzi mara 2, nikasahau hata kwa alinikimbia miezi yote aliokimbia

Tukakaa kwenye mahusiano miezi 6 tena akaja akapotea tena kama kawaida baada ya mwezi anarudi nikaanza kuzoea

Mwana saikolojia: sasa ukichaa uliupata wapi mama?!

Aminata: baada ya kupotea na kurudi na Kupotea tena kwa Huyu kaka, nikaja kuonana na Ahmed akaniomba sana ajieleze, akajieleza nikamwambia lkn mimi sihitaji mwanaume mwingine tena nimeshapata mpenzi wangu mpya akaniuliza nani nikamuonyesha akacheka sana

Ahmed: Huyu umemjua wapi?!

Aminata: si rafiki yako?!

Ahmed: sio rafiki yangu wala ila tulikuwa tunafanya wote kazi Dar, tuligombanaga sana ofisini ndio kisa basi kunihamisha mkoa nikaona poa sikujua ana revenge

Aminata: kurevenge kivipi tena?!

Ahmed: my dia mimi sasa nimeshaoa nina mke wangu, ndio yule ambae ulitufumania mkoa, lkn Huyu kaka alishaoa atakuoaje wewe? !

Aminata: nikalowaa nikaanza kusikia presha, kivipi?! Huyu si anaitwa Sadiki

Ahmed: Ahahaha Sadiki?! Si bora angekuwa Sadiki my Dia, Huyu anaitwa Andrew, ameoa muda ana watoto 3 wanaishi Arusha

Aminata: nikachoka na kuzimia kuja kuzinduka nipo hospital, dokta akaja na majibu nina ujauzito wa miezi 2 nikachoka mara 2 mana sikutegemea

Nikapeea ushauri pale baada ya kufanya malipo natoka Hospital, nakutana na yule kaka amemshika kiuno mwanamke mwengine

Nikamfuata ili kuongea nae, ananiambia hanijui, we nani yule mwanamke aliekuwa nae anamwuliza mume wangu Huyu nani?! Mara akaja mtoto wa kiume anakimbia anaita mama mama nisubirie, yule kaka akamkumbatia akambeba ananiambia anti naona umenichanganya mimi sikujui pole wakaondoka

Nikarudi nyumbani nikaanza kulia natukana watu napiga vitu nalia nalia weee nikapelekwa hospital wakanireport nina kichaa

Nikakaa huko milembe na mimba yangu lkn sikufanikiwa kujifungua mimba ilitoka maana sikunyingine nikipata kitu cha ncha kali najichoma mwenyewe najipigiza dah basi mimba ikatoka

Baada ya Miaka 3 nikaonekana nimepona ndio nikaletwa kwenye hili darasa la madam hapa

Tangu miaka 3 ipite sijawahi kuwasikia tena Ahmed na yule kaka, nimepoteza Kazi, maisha, mtoto, nipo nipo tu sasa naanza maisha sifuri tena

Lakini nam-miss sana Ahmed sijawahi kuwa mpweke kama nilivyo sasa

Hii ndio sababu ya kwanini nipo singo, nipo singo kwasababu nilitapeliwa kimapenzi kwa kumpenda mtu alieoa


Tuonane Tar 25 May 2018 saa 1 usiku ya Tanzania Kujionea Sehemu ya 2 ya kwanini Upo singo
------------------------------------------------------------------------
SEHEMU YA 2
A. NIPO SINGO TANGU BEAUTY AONDOKE KWENYE MAISHA YANGU 



Baada ya kuongea na warembo, nikaletewa tena wateja wengine na taasisi fulani kwa ajili ya kuwasaidia kisaikolojia

Sio kwamba nilikuwa nimemalizana na warembo hapana bali muda na warembo ulikuwa haujafika wao Walikuwa wanakuja kila jumamosi hawa wengine wakawa wanakuja katikati ya wiki

Wageni hawa walikuwa wa jinsia ya kiume, wanaume 5. Kama mnavyojua wanaume walivyo, hawapendi kuwekwa pamoja kwa grup waongee pamoja wao wanafanyaga mambo yao kivyao vyao kwahiyo kila mmoja alitaka nimsikilize pekeyake

Nikaanza na kijana mmoja ambae alikuwa na tatizo la pombe na kupiga wanawake... ingawa ameacha pombe na kupiga wanawake walimleta ili nimsaidie kurejea kwenye maisha yake ya kupata mkate wa kila siku, mana hata ajira alikuwa hana, alikuwa bado hajatoka rehab. .. alikuwa analetwa saa 4 anakuja kuchukuliwa saa 7

Mgeni huyu alikuwa anaitwa Fredrick, kabila la wamasai, mrefu, mweusi, miaka 40

Mazungumzo yetu yalikuwa ifuatavyo:

Mwana saikolojia: karibu Fredrick, karibu ukae ujiskie upo nyumbani, ukitaka kukaa au kulala sawa tu ila unatakiwa ujue kuwa chochote tunachoongea kinarekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu za ripoti yako, nataka uwe huru kujielezea

Fredrick: asante
Akalala kwenye kiti kirefu huku anakunywa maji kwahiyo dokta unataka kujua kuhusu nini? !

Mwana saikolojia: ripoti yako inasema kuwa unalewa ovyo na kupiga wanawake, kwanini unafanya hivyo wakati wewe ni mtu mzima sana? ! Miaka 40 nikiangalia hapa kwenye report yako, ulitakiwa uwe na familia sasa na watoto wapo shule ya msingi

Kwanini umejiharibia maisha yaliokufanya ukae rehabilitation kwa miaka 5?! Na ukawa umerepotiwa kama chizi?!

Fredrick: dokta mimi Sio chizi, mimi mzima, hayo niliofanya zamani nilishajisamehe na kuyasahau

Mwana saikolojia: sasa unataka tukuaminije?! Tukuwekee chupa ya bia au tukupe wanawake ushinde nao wiki nzima tuone utaishije nao? !  Kwanini uliamua kujipeleka jela ya maisha yako?! Miaka 5 kwa mwanaume ni mingi tena wewe ulikuwa na maisha mazuri sana

Labda uanze kuelezea kuhusu maisha yako ya utoto, je ulizaliwa na kuishi na baba na mama yako?!

Fredrick: OK, nitakueleza ila usipaniki
Kwetu nilizaliwa pekeyangu na mama yangu alikuwa anaishi na baba yangu, nilipofika miaka 10 baba yangu akabadilika akawa anarudi nyumbani usiku wa manane amelewa, wanagombana ikafikia kipindi akawa anampiga mpaka mama yangu,

Maisha yakaendelea hivyo hivyo kwa muda wa miaka 5, sikunyingine akawa harudi nyumbani wiki au mwezi nikawa nimeshazoea tunaishi na mama yangu tu

Mama akawa anahangaika kunisomesha, nikafaulu darasa la 7 nikaenda sekondari, nalelewa na mama tu, nilipomaliza form 4 baba yangu akafariki, aliokotwa kwenye mtaro alipigwa na majambazi akatupwa huko, tukaletewa maiti tukazika maisha yakawa yanaendelea

Sikuwahi kujua kwanini Baba alikuwa anampiga mama na Sikuwahi kuona upendo kati ya baba na mama. .. maisha yangu nimekua nikiona wazazi wanapigana tu, wanagombana ni fujo, ni vita nikiwa shuleni Sikuwahi kuwa na girlfriend, wala mpenzi, mpaka namaliza chuo sikuwahi kuwa na msichana maana msichana  Kwanini umejiharibia maisha yaliokufanya ukae rehabilitation kwa miaka 5?! Na ukawa umerepotiwa kama chizi?!

Fredrick: dokta mimi Sio chizi, mimi mzima, hayo niliofanya zamani nilishajisamehe na kuyasahau

Mwana saikolojia: sasa unataka tukuaminije?! Tukuwekee chupa ya bia au tukupe wanawake ushinde nao wiki nzima tuone utaishije nao? !  Kwanini uliamua kujipeleka jela ya maisha yako?! Miaka 5 kwa mwanaume ni mingi tena wewe ulikuwa na maisha mazuri sana

Labda uanze kuelezea kuhusu maisha yako ya utoto, je ulizaliwa na kuishi na baba na mama yako?!

Fredrick: OK, nitakueleza ila usipaniki
Kwetu nilizaliwa pekeyangu na mama yangu alikuwa anaishi na baba yangu, nilipofika miaka 10 baba yangu akabadilika akawa anarudi nyumbani usiku wa manane amelewa, wanagombana ikafikia kipindi akawa anampiga mpaka mama yangu,

Maisha yakaendelea hivyo hivyo kwa muda wa miaka 5, sikunyingine akawa harudi nyumbani wiki au mwezi nikawa nimeshazoea tunaishi na mama yangu tu

Mama akawa anahangaika kunisomesha, nikafaulu darasa la 7 nikaenda sekondari, nalelewa na mama tu, nilipomaliza form 4 baba yangu akafariki, aliokotwa kwenye mtaro alipigwa na majambazi akatupwa huko, tukaletewa maiti tukazika maisha yakawa yanaendelea

Sikuwahi kujua kwanini Baba alikuwa anampiga mama na Sikuwahi kuona upendo kati ya baba na mama. .. maisha yangu nimekua nikiona wazazi wanapigana tu, wanagombana ni fujo, ni vita nikiwa shuleni Sikuwahi kuwa na girlfriend, wala mpenzi, mpaka namaliza chuo sikuwahi kuwa na msichana maana msichana Kwanini umejiharibia maisha yaliokufanya ukae rehabilitation kwa miaka 5?! Na ukawa umerepotiwa kama chizi?!

Fredrick: dokta mimi Sio chizi, mimi mzima, hayo niliofanya zamani nilishajisamehe na kuyasahau

Mwana saikolojia: sasa unataka tukuaminije?! Tukuwekee chupa ya bia au tukupe wanawake ushinde nao wiki nzima tuone utaishije nao? !  Kwanini uliamua kujipeleka jela ya maisha yako?! Miaka 5 kwa mwanaume ni mingi tena wewe ulikuwa na maisha mazuri sana

Labda uanze kuelezea kuhusu maisha yako ya utoto, je ulizaliwa na kuishi na baba na mama yako?!

Fredrick: OK, nitakueleza ila usipaniki
Kwetu nilizaliwa pekeyangu na mama yangu alikuwa anaishi na baba yangu, nilipofika miaka 10 baba yangu akabadilika akawa anarudi nyumbani usiku wa manane amelewa, wanagombana ikafikia kipindi akawa anampiga mpaka mama yangu,

Maisha yakaendelea hivyo hivyo kwa muda wa miaka 5, sikunyingine akawa harudi nyumbani wiki au mwezi nikawa nimeshazoea tunaishi na mama yangu tu

Mama akawa anahangaika kunisomesha, nikafaulu darasa la 7 nikaenda sekondari, nalelewa na mama tu, nilipomaliza form 4 baba yangu akafariki, aliokotwa kwenye mtaro alipigwa na majambazi akatupwa huko, tukaletewa maiti tukazika maisha yakawa yanaendelea

Sikuwahi kujua kwanini Baba alikuwa anampiga mama na Sikuwahi kuona upendo kati ya baba na mama. .. maisha yangu nimekua nikiona wazazi wanapigana tu, wanagombana ni fujo, ni vita nikiwa shuleni Sikuwahi kuwa na girlfriend, wala mpenzi, mpaka namaliza chuo sikuwahi kuwa na msichana maana msichana  Ni wa nini sasa?!
Kupenda sikujua nampendaje?!
Ndio mama yangu alikuwa ananipenda lakini mimi sikuwahi kujua Kupenda,  najua watu wanasema wanaume wanatakiwa wapende wake zao lakini sisi wanaume hatujaumbiwa Kupenda sisi tupo vizuri kwenye kutii, ukiambiwa nenda unaenda, rudi unarudi, Usiende handicap hapo ndio tupo vizuri,

Nilipoanza kazi ofisini sasa wakawa wanaongelea kuhusu wanawake na jinsi ya kuwa pata na kuwachezea ni kama mchezo flan,  wakawa wanatoa na sheria ya jinsi ya kumpata mwanamke kumchezea na kumkimbia

Michezo hio ikaenda kwa muda wa miaka 3 na mimi nikajipatia wa kuwaunguza na kuwakimbia

Nikalowea kwenye mchezo huo nikasahau kuwa muda Sio rafiki, kukuta wenzangu wote walishaoa nimebakia pekeyangu jigolo  (kipusa)

Nikaamua sasa nitafute mwanamke nioe na mimi nionekane nimeoa nikampata dada m1 alikuwa mzuri sana, yeye ndio aliebadilisha maisha yangu, alikuwa mzaliwa wa Kwanzaa,  wazaliwa wa Kwanzaa wanapenda vibaya sana, alikuwa anaitwa Irene, mweupe, mrefu kiasi Sio kama mimi, mchaga, ana shape balaa mpaka unaweza kataa kama Sio mchaga, ni mzuri balaa

Sikuwahi kumpenda Dokta lakini nilikuwa nafanya nioe tu, jinsi ya kuishi na mwanamke huko ndani hata sijui nilikuwa naiga, nafata mkumbo,  bila kujua kuwa nimeathirika kisaikolojia Ndoa haikuwa suluhisho langu

Tukaingia kwenye mahusiano, Irene alikuwa ana akili sana, hakutaka Ndoa ya chap chap kama nilivyotaka, Alitaka tufahamiane, tukae kwenye mahusiano kwa muda Labda Mwana au miaka 2 ndio tuoane nikamkubalia

Miezi 6 ya Kwanzaa Tukaenda poa, vizuri sana, lakini za mwizi huwa ni 40, mwezi wa 9 makucha yangu yakaanza kufunguka, doh, nikaanza sikunyingine simpigii simu, simtafuti wiki nzima au mwezi nipo na wanawake wengine,  ananifumania namwomba msamaha ananisamehe tunaendelea

Mwezi mwingine ananikuta nimepigana baa wanampigia simu njoo mchukue bwanako anakuja anashangaa mbona Fredrick hanywi

Siku za ibada tushazoea kwenda wote kanisani nikawa siendi tena akawa anagomba kuna siku tuligombana nyumbani kwangu, nikamshika shingo nikamrusha upande wa pili uzuri aliangukia kwenye kochi sikumwona tena kwa muda wa Miezi 3, nikajiskia vibaya nikamtafuta nikamwomba anisamehe nimem-miss akakataa, nikalia na kulia Dokta akakataa, nikaomba mama akaongee nae lakini wapi, akakataa, nikaita marafiki zake wakaongee nae lkn wapi nikaamua kumuacha, tukakaa Miezi 3 tena hatujaongea nikaja kumkuta yupo na kaka mwingine wameanzisha mahusiano, nilimpiga yule kaka mpakaa wakaja walinzi wa lile eneo kuniachanisha maana nikiwa na hasira nakuwa kama linyama fulani sishikiki

Akaondoka na bwana wake baada ya wiki 2 nikamfuata kazini kwake na maua nikaenda kumwomba msamaha mbele ya wafanya kazi wake maana ilikuwa Siku ya Valentines day, wenzake wanashangilia wanampigia makofi yeye ananiangalia amekasirika sana... akapokea zawadi akanisindikiza mpaka getini akarudi ofisini kwake

Jioni nikaenda kumpitia kwao nikamwomba sana tutoke out, akakubali, tukaenda kula chakula cha usiku alafu tukarudi nyumbani kwangu kumalizia shoo!

Sikuhio nilimpiga shoo Mchaga wa watu kisawa sawa ili asahau wajinga wote waliokuwa wanamsumbua

Asbubuhi tulipoamka nikamvisha Pete akafurahi tukasameheana akakaa kwangu weekend nzima j3  nikampeleka kazini

Mapenzi yakawa mubashara... Irene akanifundisha kupenda tena, nikawa najitahidi kujifunza kupenda lakini ndani yangu najijua kuwa ni mtu ambae ameumizwa, amevunjika, kupenda ni msamiati, nawezaje kupenda ikiwa ndani nimeharibika?!

Aliporudi nyumbani kesho yake kaenda kumweleza mama yake kuwa nataka kuleta wazee kwa ajili ya mahari na mimi nikaandaa wazee kwa ajili ya mahari

Nikalipa mahari vizuri kabisa, sherehe ya mahari haikuwa kubwa saana maana Irene hakupenda umati wa watu, tulikuwa kama 25 tu wa upande wangu na wake

Mahusiano mazuri yakaendelea, tukapanga tukioana tutakuwa tunaishi pale kwangu mpaka tutakapopata nyumba yetu nyingine nzuri zaidi maana pale nilikuwa nimepanga

Irene alikuwa ni mwanamke wa shoka, jembe, kuna vitu alikuwa anafanya mpaka mimi mwanaume naona aibu, ukiachilia mbali alikuwa ameajiriwa pia alikuwa anafanya vibiashara vyake pembeni, alifungua vioski 3, kimoja cha msosi mgahawa, kingine cha nguo za kike, kiume na watoto, kingine cha spea za Bajaj na Magari

Sikunyingine anaomba likizo
Ofisini anaenda China, Thailand na India kuleta mali... yule Mchaga alikuwa kichwa, mambo ya wanaume sikuwahi kumkamata nayo ingawa sikumkuta bikra kwangu haikujalisha sana lakini Mchaga yule alikuwa ananifurahisha sana

Alafu alikuwa mchangamfu, ukikaa nae hauwezi kuboreka ila alikuwa akitaka kitu chake Lazima akipate, haangalii kama ni muda / wakati sahihi yeye hajali kama mazingira yanaruhusu au la ndio vitu alikuwa ananistress navyo

Kuna siku tuligombana  wakati tupo kwenye maandalizi ya Harusi sasa, nilimpiga sana Irene nae amezidi hasikii, akitaka chake ndio hicho tufanye kwani yeye ni mwanaume au?!

Nilimpiga mpaka akalala chini nikaendelea kumpiga mateke ya mgongo na wowowo akazimia nikaondoka nikaenda kwenye kibanda chake cha nguo nikachoma moto nikaondoka nikaenda nikachoma moto banda lake la spea za magari nikaondoka nikawa naelekea kuchoma banda lake la msosi nikapigiwa simu na babake kuwa Irene amelazwa ICU nikaenda fasta kumwona naulizwa imekuwaje mbona mnataka kuuana mpaka mimba zinatoka?!

Frederick: nikachokaa!  Mimba tena!?
Baba Irene: ndio alikuwa na mimba ya miezi 3 imekuwaje mpaka inatoka?!

Ikabidi nimwelezee Baba mkwe ukweli, aliogopa sana kwa jinsi nilivyomwona angekuwa na bastola angenimaliza akakaa chini na mimi nikapiga magoti huku nalia namwomba msamaha

Baba Irene: kijana natumaini mahari yako ilikuwa milion 4, akaingiza mkono mfukoni akatoa mil 5 akanipa, akachukua note book akaandika akachana katarasi akaikunja akaandika jina la mjomba akanipa,  mpelekee mjomba au mama yako waambie waje wachukue barua yao ya zamani mahari nimerudisha mtamuua mwanangu,  naomba uondoke kwenye macho yangu na ya familia nikikuona kwa mara ya 2 nitakufunga jela na kuhakikisha utatoka ukiwa na miaka 80

Frederick: nikanyanyuka kimya mkono mmoja umeshikilia mil 5 mwingine barua nikarudi nyumbani nikalala,  asbh kumbe wajomba walishapigiwa simu kuwa mahari imerudishwa na Baba Irene na Barua ipo kwangu wakaja kuuliza kwanini nimempiga Irene

Mama yangu mzazi analia tu lkn mimi najua kwanini analia, namkumbusha babangu alivyokuwa anampiga

Kikao kile kilivyoisha kuwa wamepokea mahari iliorudishwa nikaendelea na maisha yangu, lkn amani wala furaha hamna tena, nazidi tu kuumia, nazidi tu kuteseka hamna mwanamke anaenitaka kumbe nilishaandikwa kwenye magazeti kuwa napiga wanawake ni tapeli kama nisingekuwa mfanyakazi bora ofisini ningeshafukuzwa kazi muda

Nikakaa mwenyewe bila mtu, mama yangu nae anaimba anataka wajukuu kabla hajafa, hapo sijui nampata wapi mwanamke, nikimkumbuka Irene naumia zaidi, baada ya mwaka 1 Mama yangu akafariki

Hapo ndio niliiona dunia kwa rangi zote
Nikaanza kunywa pombe nikawa kama nimechanganyikiwa, nalia ovyo nalala barabarani,  napiga watu natukana, nikafukuzwa kazi nikafukuzwa napoishi nikarudi kwa mjomba akanipokea nikawa nakaa kwake

Baada ya mwezi m1 Nikakaa Irene anaolewa kanisa flani,  alikuja rafiki wa mjomba akawa anamwadithi maana alikuwa mshenga wangu Alimwadithia wakiwa kwenye maongezi yao wakidhani mimi nimelala kumbe nawaskiza

Nilipojua kanisa analofungia harusi nikaamua siku hio kwenda

Siku ya harusi kufika wakaondoka nyumbani wote wakanifungia mlango,  kufungua nashindwa, nikapiga mlango wapi, nikaupiga mpaka nikaubomoa nikatoka na mlango wa jikoni maana ulikuwa haufungi,

Nikakimbia mpaka kwenye hilo Kanisa kufika kweli Harusi ishafungwa, maharusi wapo nje wanapiga picha

Nikaenda mpaka nikamfikia kumshika bi harusi nampigia magoti nakupenda nakupenda kwanini umeolewa wakati mimi nakupenda, nikamshika kwa nguvu mpaka nikamchania gauni yake yake, wakaja ndugu zake wakanishika kwa nguvu wakanitupa kwa mlinzi... Ikabidi waitwe walinzi wanishike maharusi wakaondoka, nikaingizwa kanisani nikawa naongea na mchungaji, akawa amefahamu mjomba ninayeishi nae akampigia simu akaja mjomba na mapolisi nikafungwa nikapelekwa hospital kuwa nina matatizo ya akili. . Nikakaa hospital kama mtu aliechanganyikiwa

Mwanasaikolojia: kwanini ulihisi umechanganyikiwa?!

Frederick: sina mama Irene nae hayupo!

Mwanasaikolojia: kwani Irene wa nini wakati ulisema unashida ya kupenda

Frederick: hata sijui  Lakini nahisi kuondoka kwa Irene kuliniharibu akili vibaya sana

Nikakaa milembe na wagonjwa wa ukweli mimi najiona mzima nikawa napewa dawa nalala tu na kula

Miaka 5 ndio juzi wameniachia baada ya kuniona nipo sawa, ndio wakaniambia watanileta huku niwe naongea na wewe Lakini dokta mimi sio chizi kama nilivyokuelezea chanzo na mpaka sasa

Ningekuwa  na uwezo wa kurudishaga muda, wakati na miaka ningefanya hivyo ningemuoa Irene ningeenda kupata msaada kwa wajomba mama yangu angeshika watoto wangu na angeishi maisha mrefu sana ya furaha

Sikujua niliruhusu Baba yangu aharibu maisha na fyucha yangu. .. nikipewa nafasi nyingine na Mungu ya kuishi Uraiani ningefurahi sana wala nisingerudia makosa tena dokta

Mwana saikolojia: akamwangalia Frederick kwa huruma akawa anapanga mbinu za kumsaidia


Tuonane Kesh Tar 28 May 2018 saa 1 jioni ya Tanzania

------------------------------------------------------------------------

B. NIPO SINGO KWASABABU NILIEMPENDA ALINISALITI



Mwana Saikolojia: Karibu Kaka Dula, kama tulivyoongea kwenye simu nataka uwe huru, uniambie nini kilikupata mpaka ukawa kwenye haya matatizo ya kuzuiliwa kutoka nje ya nchi yako?!

Dula: ah dokta we Acha tu hawa wanawake watu wabaya sana

Mwana saikolojia: imekuwaje mbona unatuita watu wabaya?!

Dula: dokta me nisikufiche, kwasababu nipo hapa nipate msaada nirudi kwenye hali yangu ya kawaida, niendelee na maisha yangu

Mwana saikolojia: ndio Baba tuongee sasa kama marafiki niweze kukusaidia

Dula: dokta bwana mimi nipo hivi kwasababu ya mapenzi, kuna mwanamke mmoja nilimpenda sana, sana sana sana kwa kifupi nilihisi tunapendana, lakini naomba niongelee upande wangu kuwa mimi nilimpenda sana yule mwanamke,

Sasa sijui alijua au hakujua kuwa nampenda sana, akawa ananizunguka

Nilikuwa na best yangu sana anaitwa Hussein, best yangu kinyama sana, tangu utotoni tumeshakuwa kama ndugu sasa  familia yangu na yao imeshakuwa marafiki sababu ya urafiki wetu unaona dokta

Mwana saikolojia: ni kweli Dula: sasa dokta wakati namfukuzia huyo demu mpaka nampata nilimweleza rafkiangu kwa furaha kuwa huyu ndio shemeji yake kwa upendo tu dokta lakini sikujua kama huyu mwanamke atanizunguka

Rafiki yangu namfahamu sana hana tabia za mademu, tulipanga tusome shule, tusake maisha, tupate kazi na hela ndio tuoe na kweli Mungu si Athumani akatusikia tukafanikiwa katika nyanja za shule, elimu, kazi ikawa imebakia hatua za mwisho za ndoa

Hussein alifanikiwa kupata demu wake kabla yangu mimi, wakawa kwenye mipango ya kufunga ndoa ya mwisho mwisho, basi na mimi nikaja kupata mrembo wangu anaitwa Naima

Naima nilimpenda sana ingawa yeye kielimu nilimzidi alikuwa na Advance Diploma mimi nina Master's

Tukapenda sana na nilihakikisha simpeleki kwa best yangu nikafanya mahusiano yetu ya sirini

Tukakaa kwenye mahusiano mwaka nanusu nikajiridhisha nae kwa vigezo vyangu mimi, ndio nikaamua kumtambulisha kwa rafkiangu Hussein

Siku namtambulisha kwa Hussein, mpenzi wa Hussein alikuwa hayupo alisafiri kikazi mkoani, Hussein akamfurahia shem shem si unajua tena mambo yetu kibongobongo sikujua kuwa ni ile ya hainaga ushemeji

Tangu tumetoka kuonana pale na Hussein nikapata safari ya kikazi mkoa nikakaa miezi 2, Kurudi naona Naima ameshanibadilikia kitabia, unajua mpenzi wako mkiwa mnapendana na ukamfahamu vizuri akibadilika unajua tu na mimi Dokta nilijua kuwa huyu kabadilika kilichombadilisha sikujua kwasababu kila siku tulikuwa tunawasiliana kwa siku mara 2 mpaka 3

Nikamwuliza shida nini akaniambia hamna mara
Shangazi anaumwa akaondoka sikunyingine hapokei simu nikimtumia msg Leo anajibu kesho kuwa yupo msibani, nikimfuata nyumbani kwao naambiwa hayupo, dah kuna siku ikapita wiki hatujawasiliana nikimtumia ama hajibu nikampigia kimya dah nilichanganyikiwa dokta, mtu wa kwanza nilieenda kuongea alikuwa best yangu Hussein, kufika nikakuta viatu kama vyake, nilipomwuliza Hussein kuwa shem yupo anasema hapana viatu vya nani ananiambia ah vya shem wako alikuwa hapa jana ah nikapotezea si unajua tena wanawake hufanana viatu tukaendelea na maongezi yetu lakini roho ikawa inaniuma sana kiasi kwamba nikabadilisha topic ya maongezi yalionileta

Baada ya nusu saa nikaaga naondoka nikaondoka Kurudi nyumbani alafu nikarudi na taxi usiku saa 2 nimevaa miwani na kofia nimekaa kwenye kiduka pembeni nakunywa pombe yangu huku naiangalia ile nyumba ya Rafiki yangu Hussein

Nikakaa sana mpaka saa 3 usiku ndio naona Naima anatoka na Hussein wamekumbatiana wanapigana mabusu dah nilichoka dokta,  nikaangusha ile chupa ya bia uzuri pale nilipo palikuwa mchanga Kwanzaa sikuamini,  nilijua labda nimelewa nikawafuata mpaka wanapoenda kumbe Hussein alikuwa anamrudisha Naima nyumbani kwao

Doh nilichoka dokta, nililia sana,  sio kwa fumanizi lile

Nikaamua kufanya uchunguzi tena nikiwa sijalewa kesho yake nikaenda eneo lile lile la tukio wakati wa giza, kweli namwona mpenzi wangu Naima anaingia kwa Hussein kwa raha zake, nikawa nawapiga picha kila wakikutana napiga nao picha

Kumbe walikuwa wanachukuana ofisini asbh anamrudisha usiku
Nyumbani kwa akina Naina, weekend mitoko beach lakini najiuliza huyu Hussein anaoa wiki 2 mbele inakuwaje sasa?!

Nikamtafuta mke mtarajiwa wa Hussein nikamweleza ukweli kuhusu Hussein nikamwonyesha na picha alihuzunika sana alilia mpaka nikaogopa watu walijaa nikambembeleza sana akanyamaza ilibidi tuhame pale tukahamia sehemu nyingine karibu na nyumbani kwangu, kufika tukaamua kupanga sasa tuwafumanie wakiwa wote,

Mchumba wa Hussein alikuwa anaitwa Warda akaniambia kuwa yeye huwa anafunguo wa nyumba ya Hussein, Leo Leo usiku twende tukafumanie, tukuchue na mwandishi wa habari mmoja twende nae

Basi usiku kama kawaida tukajibanza kwenye kibanda cha nje ya nyumba, tupo 3 mimi, Warda na Mwandishi wa Habari rafiki wa Warda

Tukawaona wanavyoingia kwenye nyumba ya Hussein, Warda akasema twende sasa hivi nikamwambia, hapana ngoja wazime taa tutaenda

Tukasubiria kama lisaa 1 wakazima taa tukanyata hao na mwenye duka sasa akaita na majirani kuwa kunafumanizi si unajua mambo ya uswazi,

Warda Mbele mimi nyuma, mwandishi wa Habari Katikati

Kufika tukakuta wapo buzy wanapiga mechi dokta mpaka Warda anawasha taa mijamaa ipo buzy mechini haiskii mpaka mwandishi wa habari anawapiga picha eti hawasikii nikaanza kuwa nawasiwasi huenda nyumba tumechanganya

Warda: akamwita mpenzi wake Hussein kwa nguvu, Hussein unafanya nini lakini?! Ndio wanashtuka majirani washajaa,   mwandishi wa habari buzy na camera anarekodi, majirani nao makelele, mwenyeduka haelewi, doh ni sheedah

Wakaomba msamaha mimi sikuongea kabisa

Niliinuka nikampiga Naima mpaka wakaita majirani wa kiume wengine waje wanishike mana wakinamama walikuwa wanawashika wakina Warda na Hussein

Ngumi na wewe kama nampiga mwanaume mwenzangu,  doh kumbe ni Mpenzi wangu, sikujua saa ngapi wanaume wa sungusungu wakaja wakanishika, wakamshika na Hussein mara mjumbe huyooo mtaa umejaa

Mjumbe kuskiza kesi, akaona sasa hii kesi ya familia,  akaomba waitwe wazee usiku ule ule mana ilikuwa ni uchumba unaoelekea kwenye ndoa,
Baada ya lisaa li1 wazee wakaja wote wa Hussein wa Warda wa kwangu tukakaa pamoja na mjumbe hapo saa 5 usiku

Yakaongelewa ya kuongelewa Warda akagoma hataki ndoa tena na Hussein amemdhalilisha sana ikabidi iandikwe barua ya kurudisha mahari ya Warda kwa wazazi wa Hussein Mbele ya Mjumbe kama Mshenga wa Dharura na kesho watarudisha pesa mbele ya mjumbe mana ishakuwa usiku

Basi na mimi nikaombwa tusameheane na Hussein nikawaambia nimeshamsamehe lakini huyu Naima simtaki tena kumwona, maana Naima nimemsomesha Degree nimelipa ada ya mwaka nanusu Ndio ameamua kunibadilikia na nilikuwa nataka tuoane ili shule yake ya degree amalizie ndani ya ndoa lakini amekosa uvumilivu na uaminifu kwangu mpaka kutembea na best yangu Ndio sielewi kwa nini

Wazee wakamwuliza Hussein kwanini umemtenda ubaya rafikio, na nyie ni kama ndugu mmetufanya sisi wazazi wenu kuwa ndugu kwanini ulikuwa na tamaa kiasi hichi? !

Hussein: kimya

Akaamriwa aongee

Hussein: hana cha kuongea

Akaulizwa Naima kwanini umeamua kumfanyia ubaya mwanaume aliekupenda kwa kuwa

Kuwakosanisha urafiki hawa vijana?!

Naima: mimi sijawahi kumpenda Dula kabisa

Nilipokutana na Hussein ilikuwa mwaka nanusu ushaisha

Wazee wanamshangaa Naima

Naima: Ndio hivyo shule sikumlazimisha anilipie alitaka mwenyewe mimi nilipokutana na Hussein tukaendana kabisa na Ndio mwanaume nimeamua kuishi nae na ndie mwanaume nina ujauzito wake sasa

Wazee & Mjumbe & Majirani: tobaaaa majanga!

Dula: sikuongea nikamdunda magumi Naima, hata sijui nilipata wapi ujasiri huo lakini nilimpiga sana mpaka akazimia nikapelekwa polisi

Nikakaa siku 2 nikatoka kwa dhamana, kusikia kuwa ujauzito wa Naima umeharibika na amenifungulia mashtaka kunishitaki nimeua mwanae

Kesi ikaenda mahakamani Nikajitetea upande wangu na prove nilikuwa nazo na yeye akajitetea na Warda akaongea yake, mjumbe, wazazi, majirani waliokuwepo eneo la tukio, kila mtu akaelezea

Nikaonekana mimi ninamakosa nikalipa faini kubwa kwa Naima na nikaambiwa nipate msaada wa kisaikolojia sitaruhusiwa kutoka nchini mpaka niwe nimepona nimemaliza kozi zako zote dokta

Dokta wewe Ndio tiket yangu ya mimi kutoka nje ya Nchi maana naiona chungu Dar jamaa

Mwana Saikolojia: Hussein alimuoa Naima?! Warda je?

Dulla: Hussein alimuoa Naima kweli, ila ndoa haikukaa Naima akamkimbia akaenda kwa Boss wa Hussein

Warda alienda kuishi Uingereza kwa Dadake akaolewa na Mzungu

Na mimi nipo hapa na wewe nachukia sana wanawake

Wanawake nyie mmeniharibia maisha, nimewapenda lakini hamkunipenda

Wanawake Ndio wamenifanya niwe singo maana hawajielewi



Tuonane Tar 31 May 2018 saa 1 usiku ya Tz
------------------------------------------------------------------------


C. Nipo Singo Kwasababu Niliharibiwa Kimaumbile

Mwanasaikolojia: karibu Shaibu, kama nilivyokueleza uwe huru na mimi kunieleza kwanini unahisi una matatizo na kwanini unasema unashida ya kupata mke wa kumuoa?!

Shaibu: well doctor, kama unavyoniona nilivyoo sidhani kama unadhani ni mwanaume wa kawaida

Kusema kweli mimi natafuta mwanamke wa kuoa huu mwaka wa 5 sasa, nina miaka 35 na sina mke, pia kama mwanaume napata sana shida,  hata kutafuta mwanamke wa pembeni ni ngumu mana wananitania kuwa mimi shoga

Mimi sioni kama ni shoga, najiona sawa, huenda labda jinsi navyoongea ni kwasababu marafiki zangu wengi ni wa kike na wanaume nikifanya urafiki nao hawataki wananikimbia wanasema nimekaa kama shoga

Mwanasaikolojia: kwanini wewe unaamini ni shoga?

Shaibu: hapana dokta, Kusema ukweli mimi nilizaliwa mzima kabisa
Ila kuna vitu nilikuwa nafanyiwa na mjomba wangu, kaka yake na mama ambae alikuwa anaishi kwetu nadhani alikuwa ananifanyia tangu alipokuja kuishi na sisi

Mwanasaikolojia: alikuja lini kuishi na ninyi?! Mkiwa na miaka mingapi?!

Shaibu: nikiwa darasa la 3, akaja mwenyewe toka kijijini mama akampa kazi ya kutuangalia akiwa anaenda kazini. .. akawa anatupikia mana dada wa kazi alikuwa hayupo

Mwanasaikolojia: anawapikia wewe na nani?!

Shaibu: mimi na mdogowangu wa kike

Lakini mdogowangu wa kike alikuwa darasa la kwanza na akawa anawahi kutoka shuleni saa 7 yupo nyumbani mimi mpaka saa 10 ndio narudi nyumbani

Nikirudi namkuta analia sana nikimwuliza akitaka kuniambia mjomba anatokea

Anamnyamazisha mdomo anamwambia ameumia
Sasa kila siku anaumia yeye tu ah nikapotezea

Mama akirudi akimwadithia mjomba anamwambia huyu anaota ndoto mbaya mchana akiamka anaongea ovyo mama akawa anapotezea

Akajaga mama mdogo nyumbani na mwanae wa kike, mjomba akaanza kumwaribu na mtoto wa mama mdogo akaachana na mdogowangu

Yule mtoto akawa akimweleza mama yake mamake hamwelewi basi wakawa wanaongea na yule mdogowangu, wanaelewana

Sikunyingine mamdogo ametoka amewaacha wote 2 mjomba anapata skukuu anawatishia mkisema naenda kuwaitia mbwa maana wadogozangu walikuwa wanaogopa sana mbwa wakawa wananyamaza

Mwanasaikolojia: sasa wewe haya yote ulikuja kuyajuaje wakati ulikuwa mdogo?!

Shaibu: tulia dokta nitakueleza si tuna masaa 3 au? Ngoja Acha papara

Basi wadogozangu wakawa wakienda kucheza wanachora chini dudu ya mwanaume ukiwapa karatasi wanachora dudu ya mwanaume inavyoingia kwa mtoto wa kike wanachora mwanaume anavyowakaba yani Acha tu alafu zile picha wanazificha chini ya kitanda changu

Sikumoja shule ikafungwa, mama mdogo akamwambie mama yangu kuwa aende na mdogowangu kijijini wakacheze na mwenzake, mama akafurahi sana wakaondoka wakaniacha mimi na mjomba

Tukakaa wiki moja ndio nikajua mchezo wa mjomba

Akaja usiku tumelala ananishika kwanguvu ananigeuza mara ya kwanza nikapiga kelele mama akaja nikamweleza akakataa akasema anaota, akanitishia nikisema atanichinja mama akiondoka na mimi nilikuwa naogopa kichinjwa sana nikakaa chini

Mama akiwepo kazini Nikirudi shuleni nataka chakula

Ananiambia sikupi mpaka nimpe kwanza raha ashibe nikawa sina jinsi, nashindwa kwenda kwa majirani maana majirani wapo mbali na mimi

Mchezo ndio ukawa huo huo sina wa kumweleza mpaka mdogowangu akaja mimi ndio nilikuwa chakula cha mjomba

Mdogo wangu alipokuja akaacha kabisa mchezo wake kwangu,

Akaendeleza huo mchezo kwa miaka 2 mbele kwa wote mimi na mdogowangu...
Sikumoja nikakuta mdogowangu analia nikawa nambembeleza mjomba alikuwa ametoka kwenda sokoni na mama hayupo ndio akanieleza kila kitu nikaelewa

Akatoa picha chini ya godoro langu akanionyesha ndio nikaelewa sasa mchezo ulivyo nikasubiria j2 mama yupo na mjomba kaenda kanisani nikamueleza mama tukamtolea zile picha ndio akaamini akaenda kwa mwanasheria akamweleza nikaona Sikumoja jioni mama amewahi kurudi mdogowangu amelala hapo mjomba keshamchezea mdogowangu mpaka kalala wakaingia mapolisi 2, mwanasheria na mama wakamweka kikao mjomba doh mjomba alikanushaa picha zikatolewa akakanushaa

Wakamwambia tunakuweka ndani kwa kubaka watoto mdogowangu akasema yote sasa ameshakuwa mkubwA anajua kumweleza wakaenda kumpima kweli wakanipima na me kweli nimeharibiwa doh ndio ilikuwa mwisho wa mjomba kuwa huru akafungwa kwa kubaka

Mpaka Leo sijawahi kumwona mjomba, mdogowangu alikuwa akaolewa na sasa ana watoto na ndoa yake, shule alimaliza mpaka chuo kikuu ana masters sasa alishasahau ya utotoni maana alitafutiwa mwana saikolojia mapema

Mimi pia nilitafutiwa Mwanasaikolojia kunisaidia lkn sasa ndio aliniharibu sana, kutembea nikawa natembea kama Nimepinda, kama nyoka, yani ni sheedah kuongea naongea kama mwanamke ah aliniharibu mjomba

Hii ndio sababu hata kuoa nashindwa

Marafiki zangu wengi ni watoto wakike, nikipata mwanamke naempenda anaishia kunicheka tunaishia kuwa Marafiki

Sijajua kutongoza najifunza kwa nani?! Babangu alishakufaga tukiwa wadogo na mjomba ndio huyo alituharibu

Kwahiyo ndio nipo nipo tu natamani kuoa lkn nashindwa

Mwanasaikolojia: ulipokuwa mkubwA mtu mzima ulishawahi kutembea na mwanaume au kupenda mwanaume au kuwa na mahusiano na mwanaume?!

Shaibu: mmmh hapana ila wanaume wengi wakija wanataka kutembea na mimi huwa tunagombana sana wanaishia kuniambia kwani wewe haujioni ulivyo?! Unalipa kabisa wengine wananiambia watanilipa hela nyingi kama nitakubali tunaishia kugombana kunasiku tulipigana kabisa wakaja watu kuamulia

Mwanasaikolojia : unafanya kazi wapi?!

Shaibu: sijaajiriwa kabisa, kila nikiomba kazi nanyimwa nadhani ni kwa jinsi nilivyo

Mwanasaikolojia: Kwahiyo unapataje hela ya kuishi au mama anakupa!?

Shaibu: oh nooo!  Nafanya biashara zangu, nina maduka kariakoo na mwenge na sinza nauza urembo wa kike,  nguo za kike, watoto na kiume na napata sana wateja sana sana sana kwa akina mama na dada

Naenda China, Thailand kuchukua mzigo narudi kuuza Tz

Hela ya mtaji nilipewa na mama nilipofanikisha biashara nikamrudishia hela ya mtaji

Mwanasaikolojia: nikachokaa! Nikawa natafuta maneno mazuri ya kumsaidia Shaibu ambae alikuwa desperate kupata  mke lakini yupo singo!



Tuonane Tar 3 June 2018 saa 1 usiku
------------------------------------------------------------------------

D. NIPO SINGO KWASABABU MIMI NI PIMP

 

Karibu Calvin

Calvin: Asante Doctor doh ilo jina sasa 

Mwanasaikolojia: Calvin sio jina lako au?!

Calvin: ah langu la kwenye cheti ila mtaani siitwi hivyo wananiita Pimp K

Mwanasaikolojia: Pimp?! Kwa maana gani?!

Calvin: nilikuwa sio tena, nilikuwa naendesha danguro la wanawake, nawatafutia wateja wakishamaliza kutoa huduma nachukua percent yangu nawapa chao

Mwanasaikolojia: humu humu nchini kwetu au ulaya?!

Calvin: we acha tu hapa hapa unapoishi na nikafungua mpaka branch Africa nzima 

Mwanasaikolojia: ilikuwaje ikapelekea ukafanya hivyo?! Nini kilikupelekea kuwa muuza watu na unajua kuuza watu ni kosa la jinai 

Ah, ndio umeletwa kwangu nikusaidie maana ulikamatwa 

Niambie chanzo cha wewe kuwa pimp ni nini?! Ulikuwa na maisha mazuri, umezaliwa kwenye familia nzuri, una wazazi wana maisha mazuri, Dadake ana maisha mazuri, kwanini unajiharibia maisha?!

Calvin: kusema kweli doctor nipo hapa kufanya hii programme nikimaliza nioe nipate mali ya mzee

Mwanasaikolojia: mali ya mzee tena!?

Calvin: mzee kaandika urithi muda wowote akisepa kwa Mungu atakae kuwa na maisha ya usawa (sane) atapewa urithi kama anamaisha hayaeleweki dada atachukua zote

Mzee ana mali kweli kweli na sidhani kama nataka kuzikosa 

Mzee katoa urithi kabla hajafa atakaekuwa ameoa na watoto ndani ya ndoa ndio atapewa mali 

Dadangu kaolewa naskia ana mimba changa, mimi ndio kama unavyoniona hata demu sina wa maana wa kuoa maana mtaani nimeshaharibu sana sijui napata wapi demu wa kuoa nikamate urithi 

Mwanasaikolojia: unajua Unayoongea yanarekodiwa sio?!

Calvin: dah doctor unaua bendi, unanirekodi tena!? Basi utaniedit haina noma nakuaminia, nikishapewa changu ntakukatia kidogo au unasemaje?!

Mwanasaikolojia: 
I don't know what u hear abt  me, 
but Calvin can't get a bribe out of me, 
no Cardilac no Porche you can give, 
that am a mother f*** psychologist! 

Calvin: aahahahahahha uuuwi Doctor we noma, mpaka huo wimbo unaujua ahahahahah we ni nomaaa aahahahahahha Calvin akacheka sana hakuamini Mwanasaikolojia ataujua wimbo wa kitaa kama huo

Mwanasaikolojia: aahahahahahha 
Basi wakacheka hapo weee dokta mwenyewe mweleeewa down to earth wazungu wanasema 

Mwanasaikolojia: haya turudi kazini, akafuta recorder akaanza upya,  niambie kilichokuleta hapa kwangu unataka nikusaidie nini?!

Calvin: nataka maisha yangu ya mwanzo tena 
Nataka nirudi kuwa raia wa kawaida niwe mwanaume wa kawaida nioe nipate familia nilee familia lakini sasa nashindwa kazi yangu ya upimp imenilevya naomba unisaidie 

Mwanasaikolojia: kwanini wapi na lini ulianza biashara ya u-pimp?!

Calvin: dokta zamani nilikuwa kwenye mahusiano na dada mmoja tukiwa chuoni, tulikuwa tunapendana sana, mimi nafanya masters mwaka wa mwisho yeye anafanya degree mwaka wa mwisho lakini nchi mbili tofauti

Alikuwa anaitwa Linda 

Linda nilimpenda sana sana kuliko mama yangu wa kunizaa mimi nilikuwa Uingereza napanda ndege kwenda Marekani Alikuwa anasoma nakaa kwake wiki nageuka imagine wote wanafunzi lakini mimi nikawa najiongeza kimapenzi 

Sasa sijui ilikuwaje kule Marekani


Yule demu na marafiki zake wa mikumbo sijui akawa anawafuatisha wanavyofanya kumbe mchana wanafunzi usiku wanajiuza

Nikawa natonywa na marafiki zangu Marekani bwana tumemkuta shem anajiuza nikawakatalia Linda hakujua kuwa nina marafiki kule Marekani nilimficha unajua hawa wanawake sio wa kuwaambia kila kitu

Sikunyingine nikatumiwa picha kabisa anafanya udanguro kwenye hoteli na ananunuliwa na wanigeria nilikataa mpaka wakaniambia maliza pepa uje Marekani ujionee

Kweli pepa dokta nikamaliza shule ya masters ikawa imeisha nikaenda zangu mpaka Marekani nikafikia kwa masela, nikapelekwa sasa huko kwa Linda Alikuwa anajiuza doh Dokta nilihisi nguvu zimeniisha mwilini nilimfuata na masela kwenda kuongea na kumwuliza vipi Alikuwa na jibaba jimoja la kinigeria lile zee lilikuwa ni kama Don fulani hivi

Nikaenda kumtoa Linda anakataa hanijui ananikatalia lile Don likawa linalindwa na ma bodyguard dah nikaangalia lile picha pale linavyoenda na marafikizangu nikasema anhaa kumbe Linda anapenda ma pimp ee?

Sikuhio sikulala nililia marafikizangu wananibembeleza we dokta ushawahi kuona mwanaume analia? ! Mimi nililia kwa uchungu kama mwanamke anaetaka kuzaa nililia mpaka marafiki wakaita polisi wakihisi nimechanganyikiwa

Nikaja zolewa mpaka hospitali nikapelekwa rehab nachomwa masindano dah lile tukio sasa liliniumiza mara 2

Mpaka kuja kutolewa wiki imeishaisha wazazi waliitwa toka nyumbani wanashangaa nimefikaje Marekani wakati nasoma Uingereza

Wakaelezewa kila kitu basi turudi UK mana kiuhalali

Nilitakiwa kuwa UK mpaka graduation ipite, UK wakasema graduation mpaka miezi 2 mbele tukarudi Tz roho inaniuma mbayaa wanawake Nawaona kama chapati maji hawana ladha

Nikaanza kunywa pombe Mimi sikuwa mnywa pombe kabisa na sigara Nikaanza kuvuta kwa kujificha sikutafuta kazi mpaka nilipoenda graduation na kurudi Tena nikapata kazi hapa nyumbani

Nikapiga kazi miaka 5 nikakusanya Nikaanza kazi ya u-pimp!

Mwanasaikolojia: ulianzaje labda? !

Calvin: wale marafikizangu waliopo Marekani ndio walianza wakaniambia tukupe connection uwe dealer wa nyumbani mana wazungu na watalii wanakuja sana nyumbani watahitaji kituo cha kupumzikia  (watahitaji wadada) nikakubali

Nikaanza kutafuta wadada machangu, machangu wa ohio street, baadae nikaona hailipi nikatafuta wale wadada mapepe unajua nimefanya masters ya Marketing kwahiyo kwenye marketing  (masoko) nipo vizuri sana

Nikapataga wadada 10 tukaanza nao, mchana wengine ni wafanyakazi waajiriwa wengine wanafunzi wa vyuo wanaopenda maisha ya pesa Za chap chap wengine wafanya biashara wadogo usiku ni wanajiuza kwa siri kubwa

Tukafanya ile biashara kwa miaka 4 mbele Nikawa Don kwa soko la nyumbani, Nikaanza kufungua branch nchi Za jirani Za Africa, dah nikapata wateja balaa nikakua mpaka Nikawa naenda Marekani kusoma kozi ya u-pimp kwa ma-taicoon wengine wakubwa

Nikawa nafanya kazi Marekani hapo napata hela mwanamke kitu gani,  naweza pata mwanamke yeyote nikamfanya nachotaka kwanza wananifuata wenyewe siwafuati Tena nagombaniwa

Nikawa Marekani kwenye nyumba Ya Don mmoja Pimp na yeye, nikaletewa mrembo nimpe raha kuangalia ni Linda kachokaaa kachakaaaa anasukumwa kama mavi dah sikuhio kumwona hamu ya kula, kunywa ikaisha siamini Linda bado yupo kwenye danguro? !

Alikuwa mzuri yule demu wa kichaga doh, mzuri sana anashape nzuri mweupe sasahivi kakonda mabega juu juu kama breki ya Honda, weupe umeisha mifupa imemsimama sijui kawaje jamani kachokaaa nikamchukua nikaenda nae hotel namwuliza nini analia tuuu, hasemi analia ananiomba msamaha tu doh huruma

Kumbe baada ya kuachana nae usiku ule, aliendelea na udanguro kwa yule bwana akamchakaza anamfanyisha kazi hamlipi akakamata passport yake akaificha sasa wenzake badala ya kumshauri aende ubalozini au polisi akashitaki wakamtisha akisema atauawa ndio akaozea kwa huyo baba miaka 4 anamtumikia

Akaniambia ana ukimwi kesho anataka akaseme ukweli waje wamrudishe nyumbani akafie nyumbani doh dokta nilichokaa nilihisi moyo kusimama Linda sio Linda yule wa zamani tena kaisha kweli wanadamu sisi ni mavumbi

Asbh nikamsindikiza ubalozini akasema kila kitu baada ya siku 3 akarudi Tz akapokelewa Na wazazi wake waliomtafuta miaka 4 bila kufanikiwa mana kwenye simu hakupatikana

Akaja akauguzwa nyumbani afya ikarudi sasa hivi yupo anafanya kazi kabisa kaajiriwa ila ndio anaishi kwa matumaini vidonge kila siku nini kanenepa kapendeza ukimwona utataka umwoe lkn siri yake naijua Mimi na wazazi wake

Basi Mimi maisha yakaendelea ya u-pimp kwa mwaka wa mwisho wa 5 hapo nina miaka 35 buzy na kazi yangu na kuingiza hela wazee


Wakaniita wananiuliza vp kuhusu ndoa mana hatuoni hata dalili tunajua unaishi kwako lakini hatujasikia chochote toka kwako unaoa lini? !

Sikuwa na jibu, nikaambiwa mdogowangu sister kaleta mchumba anataka kuolewa nimtoe kwenye send off basi nikafanya yangu na nini  baada ya miezi 2 sister akaolewa akaenda kwake

Nikaendelea na kazi ya u pimp mwaka wa 6 ukatimia hapo ndio nilikamatwaa nikatiwa nguvuni nikaambiwa makosa yangu nitakataaje wakati wameshanikamata na vidhibiti wanavyo, nikapelekwa mbele ya sheria nikaambiwa nilipe faini au jela, wazazi wakasikitishwa sana na mwenendo wangu,  hapo nina miaka 36 nipo nipo na bangi nimeshakuwa mvutaji mzuri

Wazazi wakakubali kunilipia fine kama nitakubali kupata msaada wa madaktari wa kiakili la sivyo nikaozee jela nikakubali wakalipa faini pesa nyingi hata sikuwahi kujua kama wazazi walikuwa na hizo hela
Maana ni wastaafu wa sikunyingi, ndio nikaletwa hapa kwako

Juzi ndio wameniambia kuhusu urithi kabla sijaja hapa walimwita sister wakatueleza kuhusu urithi utakavyotolewa na mwanasheria alikuwepo

Sister yeye kesha olewa na anamimba changa nimebakia mimi nipo nipo tu naona wenge

Ndio dokta nataka msaada mana yale maisha Kwanzaa nilishayachoka natamani kuwa na familia yangu na mimi lakini siwezi

Maisha yote dokta nimeyaishi ila kuna kuchoka na namshukuru Mungu alinitia nguvuni sio kwamba nilikuwa napenda kufanya ile biashara inafika sehemu mpaka roho inaniuma kuuza watoto wa watu na sikunyingine siwalipi nawadhurumu dah asee kama Mungu atakuja kunisamehe aanze kunisamehe kwa hapo Kwanzaa

Niliyachoka hayo maisha na Mungu aliona ndio maana akaniweka nguvuni, za mwizi 40 ila nimechoka na maisha ya u-pimp

Misha ya show business (show biz) yanachosha sana dokta usipime

Kingine napenda nipewe urithi kama wazazi walivyopanga mana ndio furaha yao. .. ni hayo tu dokta, nipo singo kwasababu nilikuwa Pimp

Mwanasaikolojia: akamwangalia Calvin akampenda bure mana kila alichokieleza kilikuwa na kweli lakini je ni kweli Calvin alitaka kubadilika?!



Tuonane Tar 5 May 2018 saa 1 usiku ya Tz
_________________________________________________

 D. NIPO SINGO KWASABABU KAZI HAIKUNIRUHUSU KUWA KWENYE MAHUSIANO 


Mwanasaikolojia: karibu Mr Piggy?!

Mr Piggy: ndio jina langu

Mwanasaikolojia: haya Mr Piggy tuambie kwanini upo hapa!?

Mr Piggy: ah me hata sielewi kwanini NIPO hapa nadhani boss wangu ameniambia nitafute msaada kwa watu kama wewe kwahiyo nipo hapa unisaidie sasa

Mwanasaikolojia: unaweza kunieleza tatizo ni nini Mr Piggy?!

Mr piggy: mimi hata sina tatizo, najiona nipo sawa

Mwanasaikolojia: OK lkn record yako inasema una piga watu ovyo, hasa wanawake, hauna huruma na binaadam wenzio, mtu akikuongelesha vizuri unakasirika na umekaa mwenyewe kwa miaka 45 bila mke na watoto (yaani haujaoa) kwanini?!

Mr Piggy: nilikwambia KAZI yangu haikuniruhusu kuoa, sasa ndio wameamua kuniruhusu nioe labda itasaidia lakini sioni sababu ya kwanini nioe au niwe kwenye mahusiano na mwanamke hapa nilipo. .. wanawake wamewaumiza sana wanaume sitaki na mimi kukimbizwa

Mwanasaikolojia: lakini sio wanaume wote walioumizwa na wanawake
Pia kuna wanawake wengi walioumizwa na wanaume na hawataki kusikia habari za wanaume

Nikuulize, ushawahi kuwa na mahusiano au urafiki na watoto wa kike?! Kabla haujaanza kazi? !

Mr Piggy: ndio

Mwanasaikolojia: ikawaje?!

Mr Piggy: nilipoanza kazi nikaambiwa niachane nae, sijamwona wala kuwasiliana nae tena,  atakuwa ameshaolewa ni miaka 20 imeshapita sasa haijalishi

Mwanasaikolojia: ushawahi kuwa na mahusiano na wanaume wenzio ya kimapenzi?!

Mr Piggy: ah hapana asee, hahahaha never doctor

Mwanasaikolojia: kwahiyo ukiwa na hamu unafanyaje? !

Mr Piggy: dokta mimi kazi yangu kulala kwenyewe nalala sio zaidi ya masaa 3 hio hamu naipata wapi?! Nikilala nalala kama gunia

Mwanasaikolojia: my dia, sisi wote ni watu wazima hapa,  kuwa mkweli uongo hautakusaidia si unataka nikusaidie au?!

Mr Piggy: nalala nikiskia hamu

Mwanasaikolojia: miaka 20 unalala tu? ! Au unanunua wanawake

Mr Piggy: swali lingine?!

Mwanasaikolojia: unavutiwaga na jinsia ya kike?!

Mr piggy: nikiwa na muda navutiwaga

Mwanasaikolojia: unaonekana ni mtu wa hasira sana na wa kutoa oda

Mr Piggy: mimi nibosi kazini ndio kazi yangu

Mwanasaikolojia: unapenda watoto? !

Mr Piggy: nilikuwa napenda sana, ila muda umenitupa mkono sidhani kama nitaweza kuwalea

Mwanasaikolojia: ninae rafiki wa kike, hajaolewa, hana mchumba, hana mtoto yupo singo unaonaje nikakuunganisha nae huenda mkapendana mkaoana, ana miaka 35

Mr Piggy: miaka 35 kwanini hajaolewa?! Kwanini hakuzaa?! Au anashida au alitoa mimba?!

Mwanasaikolojia: wewe una miaka 45, mbona Huna watoto, mbona hujaoa?! Una shida gani? ! Au wewe ni hanithi?!

Mr Piggy: hahahahahaah dokta unakaba mpaka penati? !

Mwanasaikolojia: unasemaje?!

Mr Piggy: siamini kwenye kutafutiwa mchumba, kabisa kabisa

Mwanasaikolojia: unadhani una chaguo kwa sasa?! Mwanamke yeyote utakaemfuata sasa hivi ukamwambia umuoe ukamtajia jina atajua lazima umeoa unamke hatokuchukulia serious kabisaa sana sana atakupiga hela zako, hatokupenda utaishia kuwachukia wanawake wote. .. my dia Piggy, ur finished kubali nikusaidie

Mr Piggy: hahahahahaah dokta bwana au nianze na wewe?!

Mwanasaikolojia: unaanzaje na mimi?!

Mr piggy: nikuoe wewe

Mwanasaikolojia: kwamfano, huku anafungua kifungo cha blouse yake, anang'ata modomo yake, si unajua tena mambo ya kujiseksisha

Mr Piggy: akaganda ohoo kumekuchaa!
Kama mbwa alieona kitoweo

Mwanasaikolojia: wewe amkaa,

Mr Piggy: doh Dokta! Utaniua mgonjwa ooo!

Mwanasaikolojia: nakukubalije wakati haujanitongoza?!

Mr Piggy: unataka nikutongoze?!

Mwanasaikolojia: ndio je

Mr Piggy: kimyaa!

Mwanasaikolojia: vp kutongoza hujui?!

Mr Piggy: ah mimi nishakwambia nataka kukuoa sasa wakubwa tuanze kutongozana wewe nipe ramani ya kwenu nilete mahari tufanye harusi ya watu 10 yaishe

Mwanasaikolojia: ndio umemaliza hapo au?!

Mr Piggy: ndio je

Mwanasaikolojia: ungenikuta nimekaa kwenye hotel napata kinywaji ungenitongozaje?!

Mr Piggy: wala nisingekuja

Mwanasaikolojia: eh sasa ungefanyaje!?

Mr Piggy: ningemtuma kijana wangu akakuangalie kwanza upoje akiridhika mimi nitakuja, na lazima nihakikishe amekuumiza ili nikija nisiwe na kazi ya kukutongoza, nikija tu unakubali fasta mana kwanza muda utakuwa umeenda lazima utakuwa desperate

Mwanasaikolojia: doh! Sasa naelewa kwanini upo singo, kumbe kutongozana hata haujui? !
Ahahahahahaha my dia utakufa ukiwa single

Mr Piggy: kazi ya kutongoza sio yangu kuna vijana nawapa hio kazi

Mwanasaikolojia: kwahiyo hata kumpa raha mkeo utawapa vijana wako wakuingizie mbegu ukishaoa?!

Mr Piggy: hapo nimeshakuoa kazi ya vijana inakuwa imeisha

Mwanasaikolojia: doh hapa kazi ipo sio ndogo, sasa nimeshajua tatizo lako,  unaonaje tuanze na kukusaidia jinsi ya kutongoza Mwanamke bila kutumia vijana wako na jinsi ya wewe kuwa gentlemen

Najua umesoma saikolojia kama mimi, ambayo itakusaidia kujua Mwanamke yupi mkweli na yupi jambazi na yupi wife material

Na yupi mpenda raha

Ukimaliza hapo tutaenda mtaani mimi na wewe nione unavyo approach msichana

Ukimaliza hio nitakupeleka kwenye sherehe nione upo vipi na watu unaishije nao

Mwisho kabisa tutaenda vacation nione jinsi gani una-behave kwa watu wote

Najua wamekupa miezi 3 likizo, kwa kazi yako sidhani kama watakuwa wanatania ingawa wengi mkiwa likizo mnakuwa hampo likizo lkn aliekuleta namwaminia

Nakushauria ufuate masharti yangu mimi kama unataka kusaidikika Mwisho wa siku mimi ndio nakupa uhuru wa kurudi kazini kwako

Mr Piggy: sawa boss

Mwanasaikolojia: naomba uwe serious na pia nimegundua kuwa una tabia ya kutoa oda na ku-command watu, kwa wanawake hio ni mbaya tukishaona upo hivyo tunapiga pochi yako tunalala mbele. .. wanawake ni viume laini sio kama wanaume wanataka wapetiwe wapendwe maneno matamu sio amri amri kama tuko vitani

Mr Piggy: sawa Dokta

Mwanasaikolojia: unao wazazi?!

Mr Piggy: walisha tangulia mbele ya haki

Mwanasaikolojia: ndio mana unamoyo mkavu, unahitaji Mwanamke atakaekupenda na wewe umpende hasaa maana kwa umri wako unatakiwa upate Mwanamke umri kuanzia 32 mpaka 40 na wengi wamekuwa wameumizwa sana kwenye mahusiano watoto miaka 20 hautawezana nao watakuliza wengi wao akili zao hawajakomaa ila ukibahatika sawa

Mwanasaikolojia akaendelea na maneno na ushauri mwingi juu ya wanawake wapoje, ni nani, wanataka nini

Jumamosi asbh tukutane hotel. .. saa 7 mchana mimi utanikuta nataka nikuone jinsi gani unavyotongoza wadada

Mr Piggy: sawa Dokta hamna neno nashukuru sana



Tuonane Kesho tar 6 June 2018 saa 1 usiku ya Tz
--------------------------------------------------------------------------------------

E. NIPO SING KWASABABU MIMI NI GIGOLO 



Mwanasaikolojia: karibu Benjamin

Benjamin: asante doctor

Mwanasaikolojia: uwe huru kujielezea usiwe na wasiwasi na mimi

Benjamin: sina cha kujielezea

Mwanasaikolojia: kwanini unajiita Gigolo unajua maanake? !

Benjamin: hata sijui

Mwanasaikolojia: kwanini unahisi umeletwa hapa!?

Benjamin: uje unisaidie

Mwanasaikolojia: nikusaidie nini? ! Mimi nawasaidiaga watu mwenye matatizo ya akili je wewe ni kichaa?!

Benjamin: hapana sio kichaa

Mwanasaikolojia: my friend Mimi ni tiket yako ya kwenda mtaani ukiamua kuwa mjeuri na mkaidi utalala ndani, unataka kukaa ndani?! Haupendi uishi uraiani?!

Benjamin: kimya!

Mwanasaikolojia: kwenye riport yako umeandikiwa kuwa ulipigwa sana, kwa fumanizi ulizokamatwa nazo, ripoti inaonyesha ulipigwa sana mpaka ukawa kichaa, ukatupwa mlangoni mwa kituo cha polisi tangu hapo unakumbuka kilichotokea?!

Benjamin: hapana sikumbuki

Mwanasaikolojia: rafiki naomba nikurudishe ulipotoka nitaandika ripoti kuwa umeshindwa kushirikiana na mimi mpaka utakapokuwa tayari watakurudisha au kukutafutia Mwanasaikolojia mwingine

Mwanasaikolojia akapiga simu Benjamin akaja kuchukuliwa darasa likaisha

Mwanasaikolojia akapigiwa simu kuwa kuna kesi nyingine anatakiwa aishughulikie, mteja anakuja ndani ya dk 10 asiondoke

Kweli baada ya dk 10 akaja mteja, kapendeza mwenyewe yupo smart, Mwanasaikolojia anacheka akakaribishwa akakaa kwenye Kochi waliomleta wakasubiria nje

Mwanasaikolojia akajieleza yeye ni nani na mengine mengi kumweka sawa
Mteja
Akapitia file lake fasta fasta akakuta ni kama la Benjamin, akapumua Kwanzaa akamsemesha kama alivyomsemesha Benjamin. .. mteja anamwangalia tu baadae mteja akacheeeka sana akamwuliza

Mteja: dokta unauhakika unataka kuskiza mataptap yangu? !

Mwanasaikolojia: sina shida ndio kazi yangu. .. niambie Bwana Simon

Simon: ah me sijambo sijui wewe mtoto mzuri

Mwanasaikolojia: eh mtoto tena? !

Simon: ah kwani dokta wewe hujioni ulivyo totoz? ! Kwanzaa umeolewa? ! Kama haujaolewa tuongee vizuri?!

Mwanasaikolojia: embu tufanye kilichokuleta, kwanini wanakuita Gigolo?!
Je unajua maana ya Gigolo?

Simon: Gigolo ni mwanaume anaetembea na wake za watu, kwa kulipwa pesa
NI kama wewe uwe umeolewa mumeo yupo buzy na maisha hakupi mahitaji yako ya unyumba, na mimi Simon kidume NIPO sina hela ila huduma ya ndoa naiweza kuliko mumeo, tunasaidiana tunafanya mabadilishano mimi nakupa huduma ya unyumba wewe unanipa pesa kunipongeza asante kwa huduma ... umeelewa mama?! Vp mumeo anakuonea niite mimi kazi nikuhudumie utamsahau

Mwanasaikolojia: umeifanya hii kazi miaka mingap sasa?!

Simon: mwaka wa 15 sasa

Mwanasaikolojia: sasa ikawaje ukatumbukia kwenye mtaro?! Ikawaje ndege mjanja ukanaswa kwenye tundu?!

Simon: sijawahi kuwa na kazi, sijawahi kuajiriwa nimetafuta kazi nimekosa, basi na huu u handsome wangu nikaamua kufanya biashara ktk zungukazunguka yangu na kuuza uza biashara wakina mama wakaanza kunipenda mara wananieleza matatizo yao ya ndoa waume zao hawawatimizii haja zao za ndoa wengine wana miaka 3

Wengine wana miaka 2 wengine mwaka 1, miezi 6 hawajakutana kimwili na waume zao

Ndio nikawa nabebwa bebwa na wa mama watu wazima, wamama wenye ndoa zao, wake za wakuu wa dini,  dah hii jamii nimeifaidi

Nilikuwa nalipwa sana mil 3, mil 5, milion 2, sijawahi kulipwa Chini ya mil 2

Miaka yote nilikuwa Gigolo na mfanya biashara maarufu ila umaarufu wangu ndio u-gigolo

Za mwizi kama wanavyosema waswahili ni 40, na 40 ilinifikia walikuja kushtuka waume za watu kwa kutonywa na marafiki za waume zao walituona tunatoka hotelini sasa wale matajiri wakaanza kuambiana wakaanza kuchunguza wakakuta wote wake zao nawagongea mimi mtoto mdogo

Wakaamua kuungana na kunitafuta wakanikamata NIPO zangu baa nakunywa walinitandika vbaya mno walipomaliza wakaita ma-body guard wao wakanibonda wakanitupa baharini

Sikumbuki niliokotwa saa ngapi nakumbuka nilikuwa hospital nimetundikiwa mguu juu ulikuwa umekatwa mguu wa kulia haupo nililia mpaka nikawa kama kichaa dokta ndio kupelekwa milembe lkn sijawahi kuwa kichaa ila ni uchungu wa kwanini nimekuwa mlemavu ghafla?! Lazima uchanganyikiwe dokta

Mwanasaikolojia: akamwangalia akamhurumia akamwuliza, ulipotoka milembe ukaenda wapi?!

Simon: nikarudishwa nyumbani kwa sharti la mimi kuja kupata msaada kwa Mwanasaikolojia kama wewe vinginevyo nirudi milembe nyingine ya wanaojielewa lkn zinarukaga nikachagua nirudi kwa wazazi

Inauma sana jamani wale jamaa sio watu kuniweka ulemavu namna hii kwa kosa gani dokta nahangaika nateseka umri unaenda nashindwa kutongoza mwanamke

Nikiwa na hamu zangu nashindwa kusaidiwa dah jamani Mungu amenichagulia adhabu mbaya sana jamani,

Mwanasaikolojia: umejifunza nini ktk hili sasa

Simon: mke wa mtu ni sumu

Mwanasaikolojia: hela ulizokuwa unalipwa zilienda wapi?!

Simon: zipo kwenye akaunt yangu bado japo nyingine nilitumia ila ndio zinanisaidia kusukuma maisha, nataka nikitoka hapa nikawekewe mguu wa chuma angalau niweze kutembea ndio napanga nikitoka kwenye darasa lako niende kutibiwa India

Mwanasaikolojia: mbona kama sikuelewi, umekatwa mguu ukatupwa baharini ukajikuta hospitali? !  Ukikatwa mguu ukaendelea kutoka damu baharini ungekuwa umekufa

Simon: dokta nielewe,  walinipiga sana wakanitupa baharini baada ya hapo nimejikuta hospital sina mguu wa kulia umekatwa mpaka kwenye goti hapa kwa Chini si unaona?!

Mwanasaikolojia: akaangalia akamhurumia Simon wa watu handsome kweli kweli, Mnyamwezi, mtanashati, hajui maisha yake baada ya hapo yatakuwaje na hivi ana miaka 38 hana mke, watoto, yupo singo!



Tuonane Tar 8 June saa 10 jioni ya Tz kujionea sehemu ya 3 na ya mwisho ya mahisha ya vijana hawa walioenda kupata msaada kwa Mwanasaikolojia 

Je wataendelea kuwa  singo maisha yao yote?!

_________________________________________________

SEHEMU YA 3
A. UKWELI MTUPU 




Baada ya kumalizana na session ya kwanza ya wanaume nikarudi KWA warembo ambao hatukuonana nao KWA wiki 2 sasa

Tukafurahi kuwaona nikaongea nao kwa korefu kuwaona sote tumeshakuwa marafiki na kama ndugu nikawauliza kama niwasomee yale majibu yao niliowaambia wakaandike waniletee wakasema sawa tu hamna shida

Nikaanza kumsoma mmoja mmoja kulingana na walivyojibu

Haya naanza na swali la 1

Swali 1:
"Wanaume wangapi uliwahi kuwa nao kimapenzi tangu unakua mpaka sasa"

A. Kuluthum:  wanaume 100

Wote: wakacheka uuuwi Kuluthum we noma

B. Koku: wanaume 90

Wote: wakacheka

C. Mwelu: wanaume 3

Wote: wakaguna

D. Tereza: wanaume 15

Koku: duh mbona kidogo ivo

E. Aminata: wanaume 2

Wote: mmmh! Wakaguna

F. Rebecca: mwanaume 1

Wote: aaaah uongo huo bwana uongo we boya tu Rebecca unatudanganya we boya tu

Wengine wanasema anatakiwa apate mwanaume kipusa amkimbize Wengine wanasema hamna huyo malaya tu basi makelele matupu

Mwanasaikolojia: basi basi tuwe na utulivu naomba tusikilizane mimi naendelea kuokoa muda maana mbele nina mengi ya kuongelea

Wote wakanyamaza kimya wanamsikiliza dokta

Swali la 2:
"Andika mazuri ya wanaume uliowahi kuwa nao"

1. Kuluthum- wana mashine za kunifanya nisiolewe wala kutaka ndoa

2. KOKU - Wana Pesa

Wote: wakacheka

3. Rebecca - sijaona zuri lake, hana

4. Aminata - sijaona mazuri hawana

5. Mwelu - hawana Mazuri

6. Teresa - hawana mazuri

Swali la 3:
" Andika Mabaya ya wapenzi wako uliokuwa nao"

1. Kuluthum - hawana ubaya Wote


2. Koku- wana machine kubwa uuuwi

3. Mwelu - waongo, matapeli, hawajaokoka

4. Tereza - Vichaa, hawajaokoka, wabaya Wote

5. Rebecca - Tapeli

6. Aminata - wanaume Wote Malaya

Mwanasaikolojia: nimemaliza

Sasa nimeskiliza malalamiko yenu mniambie nini mnataka baada ya hapa maana tunaingia mtaani sasa

Wote: wakashangilia finally

Mwanasaikolojia: ila hatutaingia mtaani mpaka nijue mnachotaka, nataka niulize mmoja mmoja aseme nijue nini cha kumsaidia

NA pia napenda kuwapa pole sana sana kwa yote mliopitia kwenye maisha yenu, hapa nikiwaangalia mpaka naogopa maana naona mashujaa, wafanya biashara wakubwa, mabosi wakubwa wa baadae,  matajiri wakubwa hapa nchini, eh yani nyie mnatisha sana hii nchi yenu ipo tayari kuwafahamu maana mateso yenu yamefika mwisho yamefika kileleni

Haya yote mmepitia ni darasa tosha mmepitishwa na Mungu, kabla haujaingia kwenye ndoa lazima upitie majibu ili ukiingia ndani ya ndoa ujue kutulia na kumheshimu Mume

Najua pia kuna wanaume wamepitia maisha mliopitia na wamechoka sana na maisha ya ubachela wanataka kuoa lkn mimi siwajui wala nyie hamuwajui lakini Mungu anawajua

Wote: amen dokta amen

Mwanasaikolojia: na pia hamna haja ya kukata tamaa kwasababu waliopita wamekupiku kimaisha wapo mbali wana watoto wameolewa hio sio hesabu na kipimo cha maisha, maisha yako lazima yaendelee, lazima uamke asbh uende ofisini ufanye maendeleo ni lazima kama Mungu amekupa kuamka asubuhi lazima maisha yako yaendelee, maisha yako hayasimami kwasababu mapenzi yameondoka sio kweli

Kwani kabla hawa wanaume hawajaja kwenye maisha yenu si mlikuwa na maisha lakini?!

Wote: ndio

Mwanasaikolojia: nawashauri kama ndugu, marafiki,  maisha yenu lazima yaendelee na lazima muyafanye maisha kuwa mazuri na ya ushindi na lazima muwe na maisha ya kuwapita wale waliowaacha ili muwatie wivu wakiwaona wajute kwanini waliowaacha

Koku: hilo nalo neno

Mwanasaikolojia: pia hata kama itatokea hamtaolewa au mkaolewa

Kwa wale ambao labda hawatataka ndoa sio dhambi, sio kila mtu kaandikiwa ndoa na Mungu, sio lazima wapo wanawake duniani wanaishi bila ndoa, usikubali mtu akakufanya ujione duni kwasababu haujaolewa au Huna ndoa sio kweli. .. Kila mtu ana saa yake ya ndoa na mwingine hajapewa ndoa kwahiyo msijiskie vibaya

Kama Mungu amekuandikia ndoa basi ukiipata ithamini ndoa aliokupa Mungu maana umeshaona kuna wenzio kama wewe wanataka na wanamwomba Mungu masaa 24 na umri umeenda hawajapata iyo neema msichezee baraka aliowapa Mungu maana walioolewa ndani nao wanataka kutoka; talaka zimekuwa kama karanga sikuhizi msikubali nyie mmeshajua maisha mliopitia na wala msikubali marafiki wawaharibie ndoa maana mnajua mlivyoipata

Ni kama kuomba kazi na ukaipata alafu mtu aje akuharibie hajui ulivyohangaika masomoni  (kwenye usichana) hajui kazi umeifanyiaje interview  (uchumba) na hajui hao waliokuajiri (mume) walikuchukua kwa vigezo gani ukaipata kazi (ndoa)

Sawa wapendwa wangu?

Ndoa kama unaitaka usichezee ukiipata ukavumilie ukamwombe Mungu aliekupa kuianza safari akakusaidie kuimalizia unakomaa Mpaka mwisho hamna kulemaa kinyongenyonge

Nimefurahia sana maisha mliopitia naamini mtakuwa wa mama wazuri kwa watoto, mabibi wazuri kwa wajukuu wenu na vitukuu

Wote: wakanyamaza wanamshangaa Mwanasaikolojia anaongea nini?

Na wale ambao hamtabahatika kuolewa au hampendi ndoa, jitengenezeeni maisha kiasi kwamba hata walioolewa wawatamanie uhuru wenu,  maisha yenu, asiwepo wa kukubabaisha milele

Uhai na maisha lazima pia uvishikilie na kumshukuru Mungu sana, kuna watu wanatamani kuishi lkn hawawezi, wamelala vitandani wanaumwa, wanatamani kuwa na kazi biashara wanashindwa wanawatamania nyie mlichonacho Ni kizuri na kikubwa msikubali kukatishwa tamaa na mtu au mwanaume yeyote mkataka kuwafanya mchukie maisha mtake kujiua sio kweli, maisha ni mazuri sana, ukifa unaenda kufukiwa Chini usubirie hukumu ya Mungu baadae sana sasa unataka kujiua unajipeleka wapi ?!

Embu niambie kama ungetaka kujia Leo ungekutana wapi na wenzio hapa ukaona na kusikiza matatizo yao?! Si mmeona kuwa ya wenzenu ni makubwa kuliko yenu sio?!

Wote: ndio dokta

Na kwenu Wote mnaotaka kuolewa na msiotaka kuolewa:

Lazima mtafute amani ya ndani, amani yako kwanza, uwe na amani ndani

Maana sababu mmeletwa huku kwangu inaonyesha jinsi gani kule uraiani wamewashindwa kuwapiga hawawezi maana wanawapenda kuwaweka jela hawawezi wanawapenda, wameamua kuwaleta mpate msaada

Ukiwa na amani wewe Kwanzaa hata mume,  familia yako, biashara na kazi zako zitakuwa na amani na baraka

Mama mwenye nyumba ukiwa Huna amani taa ya nyumba yako Inadorora inakuwa giza wanawake sisi ndio kila kitu, ndio tunatengeneza mafanikio, tunatengeneza ndoa, tunatengeneza maendeleo tunatengeneza watoto na familia yenye furaha sio mwanaume, mwanaume hata akiwa kimya amenuna mwanamke anafuraha nyumba inakuwa na amani tele na hakuna atakaejua

Si mnaona nyie mmeonekana mnashida mtaani wamewaleta mpate msaada maana wanajua wanawake ndio kila kitu huku duniani

Sasa nataka tufanye zoezi la kutafuta amani, amani hailetwi na vitu kama pesa,  mali, inakuwepo ndani yako, nataka mkiondoka hapa, muwe na mawazo na fikra chanya  ( positive mind and thoughts) sio mawazo mabaya

Nataka kuwafundisha jinsi ya kuwa na mawazo chanya

Mfano
1. Rebecca unajulikana umeachwa ukatembea njiani ukakutana na marafikizako wanasemeshana ukaona wanakusema

Usijiskie vibaya kama wanakusema au last? ! Au kama marafikizako wameolewa wewe Huna hata mchumba

Cha kufanya usiwafuate ukaanza kugombana nao, jiambie mbona wananiangalia sana nimezidi kupendeza nini au sikuhizi nimekuwa mzuri nini au labda kiatu changu, ah hata sijui Bwana watajaza wasinichoshe yani wapotezee hata kama wamekuita kikundi wanakusema wasikilize ukimaliza waambie sawa asante nashukuru Mungu atanisaidia maana anaetoa Mume na watoto ni Mungu

Uwe na majibu chanya usianze tena kulialia ndio hapo utakonda na mawazo maisha yatasimama utaanza kupungua na kupata mapresha ya nini?!

Tena kama mimi ni Rebecca naiboresha biashara yangu nafungua biashara mikoani najiweka sopusopu hata watu wakikuona wanajiuliza Rebecca Yupo kapata na shemeji au?! Eh unajiweka bomba mbaya unajisafirisha unajipeleka vacation unapanda ndege 1st class unakutana na wafanya biashara wakubwa unaongea nao unapata channel ya biashara na maisha, au unajisomesha shule kuongeza kipato bila kusahau kumwomba Mungu akupe mumeo kama unataka kuolewa usikose ibada unaenda kusali unamtolea Mungu sadaka ya shukrani kabisa buzy unafuraha utaniambia mwaka hautaisha utaolewa

Lk ukikaa unalialiA utalia mpaka kurudi kwa Yesu,  Kwanzaa hamnaga mwanaume anaetaka mwanamke alienuna nuna analialia ni mzigo changamkaa Acha kukaa kinyonge nimeshasema mwanaume asikufanye uone maisha mabaya yeye sio Mungu bwana. ..

Wote hahahaha kweli dokta

Mfano wa 2 : tumchukue Koku na Kulthum

Lazima mpate amani Lazima,  amani hailetwi kwa Kuchukua waume za watu, hata Mungu hapendi kuiba mume wa mtu, Lazima muwe na class na dignity mjiheshimu ndio watu watawaheshimu

La sivyo jamii itawachukulia poa, hata akitokea mwanaume anakupenda anataka afanye maisha na wewe jamii ikimwambia pale usiende hasogei

Usikubali kujiharibia maisha mana huko mbeleni ni pagumu kuliko usichanani

Mfano Leo umekuwa mtu mzima na wameshakujua wewe ni mwiba waume za watu, ukadondoka au ukaumwa paaa, nani atakusaidia?! Sana sanaa Serikali itakuzika tu ila kuumwa kama Huna mtoto hakuna wa kukuangalia mana umeumiza wanajamii wenzenu, haya nayowaambia ni maisha halisi niliyoyaona kwa watu, wasichana wanadhani maisha ya usichana ndio ya milele hapana kuna Leo na kesho tena mema nenda zako, ishi vizuri na watu uvae viatu milele

Nimesema kikubwa ni amani ya moyo wako, hata kama ukapata mume ana mashie ndogo lakini anajua kuitumia inatosha huwezi kwenda huku na huku ukawaita wanaume za watu vibamia kwasababu kuna maisha ya mbeleni

Umemwita baba au kaka za watu vibamia Leo,  umesogeza matatizo mbeleni,  kuna siku utadondoka kwa mtaro  (utakuwa na hamu zako za kimwili) utatamani hata mwenye kibamia aje hautampata na hata ukimpata Lazima atakulipizia vibaya mlishawahi kusikia watu wanarekodiwaga na video zinarushwa kwenye mitandao sio?!

Wote: ndio

Mwanasaikolojia: hao walikuwa na tabia kama zenu na zaidi, usiombee mzazi wako akute au jamii ikute video zako za utupu utadhalilika Milele mpaka kwa wajukuu wataitwa majina ulioitwa

Wewe kama unataka bwana mwenye machine kubwa ukimkuta na ndogo usimseme uchune, maliza ulichokuwa unakifanya nae jikaushe ondoka kwenye maisha yake kama simu zake mblock au usipokee basi tunatafuta amani sio vita

Na kama mmeshatembea na waume za watu wake zao wakajua nawaomba mkawaombe msamaha myamalize mapemaa nawaambia bora nusu shari kuliko shari kamili, kama mliita mtu kibamia mkaombe msamaha basi si mnatafuta amani, akatae akubali wewe ushafanya yako haina shida

Wote: sawa

Mfano wa 3: Aminata na Teresa

Naelewa Sana mmekuwa abused na wanaume na wala hamtaki kuwasikia lkn wanaume Wote hawapo abusive!  Sio wanaume Wote wahuni na matapeli kuna wanaume wazuri tu sasa kwakuwa mmeumizwa sa ajabu walishakuja mkawafukuza kwa kuumizwa kwenu

Mimi nawaomba kwanza mjifunze kusamehe, muwasamehe Wote waliowakosea, maana hata sisi tunamwomba Mungu msamaha kila Leo na tunasamehewa sio?!

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: anzeni kwa kuwasamehe waliowakosea kupotezewa mtoto sio mchezo kuachwa sio mchezo inauma Sana hayo maisha usipime lakini kusamehe ni kit cha kwanza

Wote Lazima msamaha na Lazima muwe na mawazo change kuwasamehe Mungu atawapa watoto na Mungu atawapa wanaume wazuri wa kuwapenda lakini kwanza Lazima msamehe usiposamehe Leo kwenye ndogo mwanaume akakuudhi kidogo au ukimfumania hautamsamehe milele, kila siku utakuwa unamkumbushia makosa yake na kumfananisha na aliepita ndio ndoa inapasuka unakuwa umeolewa mara 2
Umeachika mara 2

Mfano wa 4: Mwelu

Nimekubakisha wa mwisho kwasababu 

Ulisema umeokoka nakushauri kama ndugu yangu,  wanaume wengi sikuhizi wanachukia kuoa wanawake waliookoka, nakwambia ukweli sikuhizi zamani za enzi za mababu kuoa mlokole ilikuwa unaoa Gold, sasa hivi kuoa mlokole ni sawa na kuoa shetani au changudoa au dada poa uwanja wa fisi Tandale ndani ndani 

Kama kweli umeokoka kaa nayo moyoni isiwe ni kama defensive mechanism  ( kujizuia na ngao) basi watu wakikushauri hapana nimeokoka twende sehemu hapana nimeokoka vaa hivi hapana nimeokoka my dia,  ulimwengu aliotuweka Mungu uwa unaendelea hausimami miaka inaenda na imebadilika hakuna mwanaume atao mwanaume amekaa kama katuni haujulikani hii nywele ya mwaka 47 au ya 2018

Unabeba kikapu mama unaita pochi hahahahaha unatuvalia malemba wewe kwani mfuasi wa kakobe au bibi wa miaka 80?! 

Sidhani kama Mungu amekuokoa uwe mjinga kiasi hichi bali mwerevu sio?!

Mwelu: ndio

Mwanasaikolojia: alafu kitu umenishangaza ni wewe kutoangalia wazazi wako hakuna dhambi mbaya Duniani kama kutoangalia waliokuangalia wakati Huna akili, ina maana unataka kuwa kichaa au?!lakini naona ushaanza kuwa kichaa maana hizo nywele na mavazi yako Huna tofauti 

My dia wazazi wetu ni miungu yetu duniani ukifeli hapo ukifeli maisha nakushauri kama wanakufundisha kanisani hivyo hamaaa, kama hawakufundishi ni wewe tu mkaidi badilika, nakuomba ubadilike haraka sana Sana Sana maana ni tabia mbaya

utakuwa kupata mawifi na mama mkwe utakumbuka hili darasa halitakuwepo mama 

Wazazi na wakwe ndio baraka zetu Duniani kama hamkuwa mnajua, bora hii mil 8 msingelipa mkapelekea wazazi kuliko kulipa alafu wazazi wapo vibaya ni mbaya mmesikia nyie wa mama wa kesho? 

Kupata moyo wa mwanaume ni kwa njia 3:
Pendezesha tumbo lake
Wapende wazazi wake
Kitandani uwe mzuri 
Hapo mwanaume utamkamata milele 

Mwelu badilika kabla hujaendelea kujiita mlokole, wanaume wanaambiana mama, wakijua una roho mbaya hawarudi plz badilikaa 

Pia Mungu aliweka hospitali, nenda hospital kaondolewe hizo fibroid, zinauaga watu na watu wanaondolewaga kizazi kwasababu ya fibroid miaka 7 unajisifia mama utakuwa salama kweli?!

Nakushauri uende kwa wazazi alafu uende kwa hospitali yaishe ukitoka hapo utaniambia Mume Mungu atakupaa sawa mama?!

Mwelu: sawa dokta

Mwanasaikolojia: najua mambo ya amani ya moyo Mwelu hauna shida nayo ila mengine badilika na wote mmesikia sio Mwelu tu wote muwaheshimu wazazi wenu na wakwe Mungu atakaowapa mpaka mwisho

Wote: sawa dokta 

Mwanasaikolojia: darasa la leo litaishia hapa,  nimewapa kazi ya kutafuta amani moyoni mioyoni na nimeshawafundisha cha kufanya  plz ifanyieni kazi mpaka wakati mwingine tutakapoonana 

Pia nataka mniandikie kwenye karatasi kama mnataka kuolewa na watoto wangapi mnataka, na kama hautaki ndoa uandike na kama unataka watoto bila ndoa uandike tukionana mniletee nitazipitia

Wote: sawa Dokta asante sana

Darasa likaisha kwa siku hio



Tuonane kesho tar 9 June 2018 saa 1 usiku ya Tz
------------------------------------------------------------------------ 

B. I WILL SURVIVE 


Mwanasaikolojia akakutana na Dula na Frederick kwa pamoja akaongea nao vizuri sana kama wale wadada wa jana, akawatia moyo wao ndio wanaume wasikate tamaa maisha lazima yaendelee wao ndio vichwa vya familia,  lazima wajikaze wamepitia hayo kwasababu Mungu amewapitisha kwenye darasa la maisha wao ni washindi, wao ndio vidume watakuja kusaidia jamii kama sio watoto wao basi ni ndugu, jamii, au taifa kwa ujumla

Wakawekwa sawa sakawa sawa

Dula:
Akaambiwa hamna sababu ya kichukia wanawake maana wanawake wapo wengi sana kama yule aliondoka ina maana hakuna wa kwake lazima ajifunze kusamehe lazima maisha yaendelee ndio uanaume unavumilia yote

Pia anatakiwa amsamehe rafiki yake hata kama hawatakuwa marafiki tena kwasababu kusamehe sio kwa ajili ya best yake bali ni kwa ajili ya uponyaji wa dula kwani tayari Mungu ameshamlipia kwa kukimbiwa na mwanamke aliemchukulia na amejifunza toka na makosa na nyie ni ndugu msiharibu undugu kwa ajili ya mwanamke ... ikatokea best yake akarudi amsamehe ingawa ni ngumu kuwa kama zamani lakini best yake hatokaa amchezee tena Dula maana alishaweka historia

Pia wanaume sio watu wa kununiana na kuwekeana vinyongo hio ni tabia ya wanawake na akina mama akamsihi sana amsamehe aendelee na maisha akikutana nae amsalimie akiitikia asipoitikia hilo isiwe shauri ya Dula

Dula: sawa dokta nitalifanyia kazi maana maisha yangu bado yanaendelea

Mwanasaikolojia: Pia ajifunze tena kusamehe wanawake wooote Duniani na awapende kama anavyompenda mama yake mzazi Ni hatua anatakiwa kuichukia hata kama ni ngumu sana na Mungu atamsaidia

Dula: sawa dokta

Fredrick:
Najua umeumizwa sana na baba yako ila narudia tena maisha yako hayasimamishwi na baba yako, najua haukupata msaada wa haraka mwanzoni lakini sidhani kama umechelewa wakati wa kurudisha maisha yako ni sasa,  hata kama itachukua miaka au mwaka au miezi lakini ni sasa, hauwezi ukajifungia ndani tu unajitesa
Ndio jamii ilishuhudia ulichofanya lakini miaka 5 ishapita wameshasahau kama unaona shida kuishi Dar nenda kaishi mkoa nenda kaishi Kenya au Uganda nenda sehemu mbali na nyumbani kwake katengeneze maisha yako upya lazima usonge mbele

Fredrick: lkn dokta sijui nafanyaje nimekaa ndani miaka 5 ni sawa na kukaa jela dokta

Mwanasaikolojia: nitakusaidia kuanzia sasa mpaka hapo nitakapoona umekaa sawa, kila siku wewe na dula na wengine tutakuwa tunatoka nje tunajifungia kwenye nyumba tunafundishana cha kufanya mpaka tunamaliza mtakuwa mmeshajifunza mengi sana, tutaenda sokoni, baharini, mashambani, maporini kwenye nyumba za starehe, kwenye nyumba za ibada, kote nitawapeleka mpaka mtakapokaa sawa ndio nitawaruhusu kuingia mtaani wenyewe

Frederick & Dula: sawa dokta tunashukuru

Mwanasaikolojia: najua hatujaonana kwa wiki mbili naomba niwape kazi mkitoka hapa muandike kwenye karatasi je mnataka kuoa au hamtaki tena?

Mnataka watoto ndani ya ndoa na kama ndio wangapi?

Mnataka watoto nje ya ndoa kwa kusaidia jamii kulea watoto yatima, kama ndio wangapi?!

Frederick & Dula: sawa dokta

Darasa likaahirishwa

Shaibu & Calvin:
Nao wakaja kwenye wakati wao kwa pamoja wakatambulishwa wakasalimiana Mwanasaikolojia akaongea nao kama alivyoongea na akina Dula na Fredrick

Shaibu:
Wewe ni mwanaume na bado utaitwa mwanaume hata kama umeharibiwa kimaumbile Mimi nimekupenda kwasababu katika yote ulioyapata umeweza kutoboa kimaisha huo ndio moyo wa mwanaume ulivyo

Wewe so shoga wewe ni mwanaume kama wanaume wengine na unaweza ukapenda mwanamke ukapata familia kama wanaume wengine na wajukuu na vitukuu

Shaibu: ndio dokta lakini Mimi sijui kutongoza

Calvin: akamwangalia akacheka sana

Mwanasaikolojia: najua ndio maana nimekuweka na Calvin hapa kuna vitu vingi atakufundisha na kuna vitu vitu vingi utamfundisha sawa Shaibu?!

Shaibu: sawa dokta

Mwanasaikolojia: Calvin najua wewe umeishi maisha yote mabaya lakini shaibu ameishi maisha mazuri na mabaya na najua wote ni wafanya biasharA wazuri sana lakini biashara uliokuwa unafanya Calvin sidhani kama utataka kuirudia

Calvin: sitaki hata kuisikia

Mwanasaikolojia: Shaibu hapa anafanya biashara nzuri na analipa kodi zake zote atakusaidia jinsi ya kurudi mtaani na kuanza maisha ya biashara kuanzia chini sawa?

Calvin: sawa

Mwanasaikolojia: na pia Calvin nataka umsaidie Shaibu sio kumcheka jinsi ya kutongoza wanawake kwa uzuri sio kwa ubaya, nataka muwe marafiki msaidiane tukija kuonana tena nataka nione jinsi Shaibu anavyotongoza pia msaidie kutembea kama wanaume kwa imara na nini wewe unaelewa sio?!

Calvin: hamna shida dokta

Mwanasaikolojia: najua Calvin

Ameniambia anataka kuoa, ila hauwezi kuoa kama hauna kipato chako mwenyewe hauwezi kutegemea wazazi unatakiwa uwe na vyako vya halali,  usimwibie mtu wala kumdhulumu mtu sasa hivi umeshakuwa mtu nzuri unatakiwa utende mambo Mema

Sehemu za ibada lazima muudhurie wote kila mmoja kwa imani yake msiache kusali na kumwomba Mungu mtafanikiwa umri mlionao wala hamjachelewa nyie ni wanaume sio kama wanawake nyie mnaoa hamuolewi ukitaka mwanamke yeyote sasa unampata unaoa lakini kwa wanawake ni ngumu

Nataka mkija tena mniandikie kwenye karatasi kama
1. Mnataka kuoa au hapana

2. Mnapenda watoto?! Na kama Mnapenda watoto Mnataka muwapate ndani ya ndoa au hapana?! na kama ni ndio je watoto mnataka wangapi?!

3. Kama hautaki kuoa je unapenda watoto? ! Unataka kuisaidia jamii uwalee watoto yatima kama ndio je ni wangapi? !

Darasa likaisha sikuhio ikaisha, wakaondoka wamekuwa marafiki tena

Asbh yake wakaja tena kwa Mwanasaikolojia Simon na Mr Piggy kwa pamoja

Mwanasaikolojia akawakaribisha kama kawaida yake na lekcha ya nguvu akawaweka sawa maana alimjua Mr Piggy hapendi makundi lakini akamweka sawa

Akawatia moyo kila mtu na mwenzake kwa kadiri ya waliopitia

Mwanasaikolojia :
Maisha ya kutembea na wake za watu kwa pesa natumaini umeacha na hautarudi tena huko sio?!

Simon: ndio dokta nimejifunza kwa makosa

Mwanasaikolojia: lazima ujue kuwa maisha yako bado hayajaisha na wewe ni mwanaume na bado una nafasi ya kuanzisha familia na maisha yakasonga mbele sawa?!

Umri wenu usiwavuruge nyie bado ni wanaume Bado vijana bado mnanguvu zenu wala msiogope kurudi uraiani kama raia wema hata kama mtasemwa mtanyooshewa vidole ninyi ni watu wapya sasa atakaewasema mfuteni vichwani mwenu mpotezeeni

Pia lazima muwe na mawazo chanya  (positive thoughts) kila saaa kila wakati kila dakika hio ndio itawasaidia kusukuma gurudumu lenu la maisha

Simon ulemavu usikufanye ukajiona wewe ndio basi wapo walemavu wanaendesha maisha yao na WanA familia na wajukuu na vitukuu na vilembwe wala usiwe na wasiwasi

Wanawake wapo wengi wazuri wanazaliwa kila siku, ni jinsi ya kuongea nao tu  kwa upole na heshima na upendo

Najua wanaume kupenda ni mtihani hasa kwa Mr Piggy hapa upendo kwako lazima utawale lazima ujifunze kupenda kama kweli Unataka kusaidikika

Wanawake sisi hatujui kutii ila tunajifunza kutii na hivyo kwa wanaume lazima ujifunze kupenda tena hata kama imepita miaka 20

Wanawake Mr Piggy sio wa kufosiwa na kusukumwa na kuambiwa njoo leta sitaki kwenda maneno makali kwa wanawake hayafai kabisa wanawake wote ukitaka kuwapata lazima uwe na lugha ya mvuto nzuri ya mapenzi sawa Mr Piggy?!

Kutoa oda au kuwa boss ni ofisini tu sio nyumbani kwa mkeo

Na mkifanikiwa kupata watoto msiwatolee oda kama mesenja mnatakiwa muwapende sana wasije wakakua wakiwachukia maisha yao yote

Nyie ndio vichwa lazima mtengeneze maisha yenu lazima mpange familia kama wanaume

Mr Piggy wanawake au mwanamke hapigwi ngumi mateke unatakiwa umpige mabusu, mazawadi, umpe kauli laini, ukiweza hapo umeukamata moyo wa mwanamke

Najua kujifunza kupenda kunachukua muda na siwashauri mkurupuke muda tunao mwingi wa kujifunza

Kwa Leo nataka mkienda nyumbani mniandikie yafuatayo

1 . Mnataka kuoa au hapana? !

2. Mnapenda kuwa na watoto kwenye ndoa?! Kama Mnapenda wangapi?!

3. Kama hampendi kuoa je Mnapenda watoto?!je mnapenda kuisaidia jamii kwa kulea watoto yatima mkiwa mnaishi nao nyumbani kwenu au wakiwa kwenye vituo vyao?!

Mniletee majibu alafu tuanze kujifunza mambo mengine yanayowasumbua kwa vitendo

Pia nataka mfahamiane muwe marafiki msaidiane kwa kila kitu kizuri msifundishane mabaya tafadhali

Mr Piggy & Simon: sawa dokta asante



Tuonane Kesho j2 tar 10 June 2018 saa 8 mchana ya Tz
------------------------------------------------------------------------

C. SHUKRANI  (THANKFUL)



Karibuni tena warembo,  nimeona majibu yenu yote mlioniletea
Je ni sawa nikisoma wote tukashirikishana?

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: haya

Swali la 1:
" Je unapenda kuolewa?!"

Koku - Ndio

Mwelu - Ndio

Teresa - Sijui lakini sawa tu

Kuluthum - hapana

Rebecca - Ndio ila sitaki watz

Aminata - ndio

Swali la 2:
" kama unapenda kuolewa unapenda kuwa na watoto wangapi?!"

Koku - watoto 3

Mwelu - watoto 3

Teresa - watoto 2

Kuluthum - staki kuzaa

Rebecca - mapacha

Aminata - watoto 2

Swali la 3
"Kama haupendi kuzaa watoto ungependa kuisaidia jamii kwa kulea watoto yatima? !"

Koku - hapana

Mwelu - hapana

Teresa - hapana

Kuluthum - ndio nataka nilee watoto mapacha yatima

Rebecca - hapana labda baadae

Aminata - hapana

Well hayo ndio yaliokuwa majibu yenu na mimi nayaheshimu sitaki kumhukumu mtu lakini nikiwauliza kwanini hamtaki kuisaidia jamii kulea watoto yatima mnaweza kuniambia kwanini?!

Koku - mmmh mtoto yatima nitamsaidia akiwa kituoni sio kumchukua kwangu

Mwelu - mimi ni kama alivyosema Koku

Rebecca  - kama alivyosema Koku

Aminata - kama alivyosema Koku

Teresa - kama alivyosema Koku mana Sijui mwanaume atakaenioa kama anapenda nitawachukua

Mwanasaikolojia : Kuluthum kwanini hautaki kuzaa watoto wako mwenyewe?!

Kuluthum - madam mimi nina miaka 35 nipate bwana saa ngapi anioe, nizae saa ngapi, nikuze saa ngapi?! Nilee saa ngapi? By the time nina miaka 60 nimechoka mtoto yupo chuoni sina hata hela ya kumlipia ada nimeshastaafu hapana asee ngoja nisaidie jamii

Mwanasaikolojia: OK najua niliongea nanyi kuhusu kutafuta amani mioyoni mwenu na kuongea na kuwaz positive mmefikia wapi mpaka sasa? ! Kuna shida gani mmekutana nazo mpaka sasa tangu tulipoonana?!

Nianze na Mwelu:

Mwelu: dokta nilifanyia kazi ushauri wako, nikaenda nyumbani kuwaona wazee

Wote: wakampigia makofi

Mwelu: wakafurahi sana,  nikawapelekea hela mama nikampa mil 5 baba mil 6, nikawapelekea na simu mpya nikawabadilishia nikawapa hizi simu za smart phone

Wote: doh wanamshaangaa Mwelu ana hela!

Mwelu: tukaongea siku hio mama hakulala tunapiga stori, wakanieleza matatizo ya pale asbh tukapanga na wazazi baba akaenda kuleta fundi wakarekebisha mambo madogo madogo
Mzee akaongelea kuhusu biashara anataka kufanya tukapanga jinsi ya kufanya biashara toka kijijini Singida kuja Dar tukakubaliana akaenda kunionyesha mashamba yake tukapanga kulima ufuta, mafuta ya alizeti, mahindi, maharage, karanga, njugu, pamba nikamwambia atafute vijana mwaminifu wawili awalete Dar tufungue maduka ya jumla ya chakula basi ikawa imebakia siku 1 kurudi Dar maana kazi ilikuwa inaniita

Nikawa naongea na Mama ananiuliza umepata mchumba nikamwambia hapana hata sina

Akaniuliza naskia umeokoka, nikamwambia ndio

Akauliza huko kanisani haujapata mchumba?! Nikamwambia hapana anashangaa kwanini na nakosaje mchumba nilivyo mzuri?!

Nikamwambia kuhusu kuumwa kwangu kwa fibroids zangu akashangaa akaniambia niende hospital atakuja kuniuguza nikiwa Dar
Tukaongea sana kirefu tukalala asbh nikaamka kutengeneza chai ya asbh

Walipoamka wakafurahi kukuta kila kitu kipo tayari,
Tukanywa chai nikaingia ndani kujiandaa na safari maana bus lilikuwa linaondoka saa 4 asbh

Kabla sijaondoka wakaniita nipige magoti wakaniombea sana sana baraka kwa Mungu, wakamkemea shetani

Koku: yeah ashindwee

Mwelu: wakaniombea nipate mume na watoto wakike na kiume wakaniombea nipone fibroids na kama nitafanyiwa opereshen iende salama nitoke salama

Nikasindikizwa mpaka kwenye bus nikakumbatiwa wazazi wanafuraha kweli kweli Kwanzaa hawakuamini

Nikarudi Dar kuingia kazini nikapata barua naitwa na boss nikaambiwa na boss nimepandishwa cheo nimekuwa COO  (Chief Operations Officer) wa ile kampuni niliokuwa nafanyia kazi na mshahara umeongezeka mara 10 ya pale nilipokuwa nikaona kama muujiza kweli dokta uliposema wazazi ndio Mungu wa Duniani tuliopewa

Nikaenda kupima hospital kwa mara ya kwanza nikakutwa na Fibroids zipo bado natakiwa nizitoe haraka, nikaweka appointment ya dokta nikaambiwa dokta mzuri amesafiri mpaka miezi 3 ipite ndio natafuta dokta mpya

Koku: kama una hela kwanini usiende India ukatibiwe? Sijaelewa kwanini unataka kutibiwa kwetu, mtafutie mama Passport mpandishe ndege akakuuguze

Teresa - ndio India wanatibu vizuri haitafika hata mil 10 labda mil 4 au 5 lakini wapo vizuri

Mwanasaikolojia: ndio Mwelu kama una hela nenda kutibiwa India wako vizuri kimatibabu huwezi jua kwanini Dokta uliemtaka hayupo, huenda Mungu amekuepushia kitu,

Mwelu: ivyo ee,  haya basi nitaenda ngoja nimhangaikie mama aje Dar nimtafutie Passport

Wote : wakampigia makofi Mwelu kwa hatua aliochukua

Mwelu: pia tangu niwaone wazazi Wangu nimekuwa na amani ya ajabu sana nina amani kila wakati na lile kanisa nimehama nasali Lutheran sasa nimerudi kanisa la wazazi Wangu staki shobo tena

Wote: wakampigia makofi na kumpongeza hongera sana hongera mno

Mwanasaikolojia: nimefurahi sana Mwelu ila usiache imani uliokuwa nayo huwezi jua kwa imani yako utapona

Mwelu: amen sister

Mwanasaikolojia: haya naomba nisikie kutoka kwa Kuluthum

Kuluthum: well dokta, tangu tulipoongea skuile nikaifanyia kazi somo la amani na positive thoughts  (fikra chanya)

Nikaanza kuitendea kazi ninapoishi nilikuwa sisalimii majirani na wale walinzi Nikaanza kuwasalimia kwa smile kubwa mpaka wakashangaa

Ofisini nikawa naskiliza mahubiri ya TD Jakes na Joel Osteen ya positive thoughts nikawa na amani muda Wote

Nikawatafuta watu wote niliowaokosea nikawaomba msamaha wanAshangaa mimi ni wa kuomba msamaha maana nilikuwa mafia hatari

Ofisini wanashangaa nimekuwa mtu wa amani ukinisema nakuangalia sikujibishi sijibishani

Nikaamua kwenda kujiunga na chuo, nisome certificate ya public relations kwa mwana mmoja maana mimi hesabu sijui
Nimeanza shule darasa la jioni jana na enjoy mpaka mwisho kusali siachi kila siku nasali, ijumaa nipo msikitini ni raha nina amani mbaya

Wote: wakampigia makofi na kumpongeza

Mwanasaikolojia: hongera sana Kuluthum, Mungu akufanikishe kama alivyomfanikisha Mwelu

Haya mwingine nataka atuelezee ni Tereza

Tereza: kwakweli dokta somo la  Kutafuta amani moyoni nalijua maana walokole ndio somo letu, nimelifanyia kazi nimewasamehe wote walionikosea amani ninayo ila naitendea kazi swala la kujithamini na kujipenda ndio inanipa shida ila muda upo nitakaa vizuri

Nikajaribu kujitoa out mwenyewe kwenye mahotel ya kisasa nikakutana na wanaume wazuri wazuri nimepata marafiki wa kiume sasa ajabu ni kwamba wananiona mdada mrembo wanadhania nina miaka 26 kumbe nina miaka 34, nimetengeneza marafiki nikiwa natoka out na office mates na haijanibadilisha I mani yangu maana najijua mimi ninani kabla ya mtu kutaka kunibadilisha

Nimesamehe wanaume wote na sasa natamani kweli kuolewa

Wote: wakampigia makofi

Mwanasaikolojia: hongera sana Teresa naona hata kuvaa kwako umebadilika mpaka ma lace wig ma Peruvian hair unaweka that's nice kitu ambacho Mwelu bado anakifanyia kazi si ndio Mwelu ee?!

Mwelu: dokta mimi kuvaa sijui itabidi mnifundishe asee sijui kabisa

Koku: sawa mdogowake Yesu tutakufundisha na ukubali kufundishika lkn wewe sio kilaza

Wote: wakacheka

Mwanasaikolojia: hongera sana Tereza naamini hili somo halitaishia hapa kwa wote liwepo maishani mwenu wote siku zote mpaka mtakapoitwa na Muumba
Amani ya moyo kwa mwanamke inawasha taa na mwanga mzuri kwenye maisha yake sikuzote msikubali negative thoughts kabisa hata kwenye ndoa hata mkiwa na watoto

Sasa tumsikie bibie Rebecca

Rebecca - Dokta ushauri wako nimeufanyia kazi sana nimejitahidi sana kusamehe na kusahau nimejitahidi kuwa na mawazo chanya kama ulivyotushauri nimeifanyia kazi

Wiki mbili najinenea mambo mazuri mema nikakutana na watu wananiambia am glowing usoni nina nuru ninang'ara nimependeza wanauliza nimepata bwana nini? !

Hata sijui ni kweli au uchawi hata sielewi lakini nimetendea kazi nilichofundishwa

Wateja wangu wote nawahudumia vizuri kwa furaha na amani na lugha nzuri kuliko zamani, biashara inafanya vizuri sasa kuliko zamani Wateja wanaongezeka nimeongeza bei ya bidhaa lakini wanazidi kuja

Kesho nasafiri naenda Uturuki kuchukua mzigo wa biashara kwasababu umeisha kabla ya wakati, I hope nitawahi darasa lijalo nisipokuwepo Dokta ujue nimesafiri

Wote: wakampigia makofi na kumpongeza

Mwanasaikolojia: oh hongera sana Rebecca, Mungu Akuzidishie na kukubariki, positive thoughts  ( fikra chanya) inaleta baraka na inaondoa mabaya yote

Rebecca: Amen

Mwanasaikolojia: haya sasa tusikie toka kwa mrembo Aminata

Aminata: asante sana Mwanasaikolojia nimefurahi sana wenzangu wamefanikiwa

Na mimi nimefanyia kazi ulichotuambia kila siku nawaza mazuri naongea mazuri, nikawa najiambia nitapata kazi tu nitapata kazi nikawa na apply kwenye magazeti natuma maombi kila siku, huku najifunza kila kuwa na mawazo chanya na kutabasamu na kucheka kama kazi zetu zinavyotaka, juzi nikaitwa kwenye interview ubalozi wa Africa Kusini nikaenda nusu saa kabla ya muda sikujua kama walikuwa wanaangalia nikatulia nikawa nasubiria zamu yangu nikafanyiwa interview nipo poa kabisa nafurahia interview toka ndani
Nikamaliza interview nikarudi nyumbani unajua naishi na wazazi kwa sasa tangu yanikute Leo wakati nakuja huku wakati nashuka kwenye gari nikapigiwa simu na ubalozi kuwa nimepata kazi ya receptionist natakiwa nianze kazi j3 kwenye probation  (maangalizi)

Wote: wooooow wakampigia makofi akina Koku wamesimama wanampongeza hongera sana wanamkumbatia Tereza mpaka analia Kulutum anamtania Twin wangu Receptionist mwenzangu umetisher hongera sana

Mwanasaikolojia: akamsifu sana Aminata akamshauri aendelee hivyo hivyo akiwa na swali ampigie atamsaidia masaa 24 yeyote atakaekuwa na shida ampigie simu

Haya sasa nimebakisha mjanja chautundu wetu wa darasa cha fujo Koku

Tukusikie na wewe umeitendeaje kazi niliokuagiza?!

Koku: well Dokta,  mimi ni kama Rebecca wote wafanyabiashara nilipotoka hapa nikaenda kuifanyia kazi kila siku najirekodi kwa simu Wateja wakija nawaongelesha vizuri kwa furaha

Wale watu wote niliowakosea nilienda kuwaomba msamaha wakashangaa mana hawakutegemea

Wengine niliwaita vibamia nikawaomba msamaha wakashangaa Wengine wananitania nikupe uone kama nina kibamia tena basi tu tunacheka tunafurahi tukawa marafiki tena ila sio urafiki wa mapenzi, wakanipa oda kubwa toka kwangu nikawapelekea mzigo wakanipa hela ya kuzidi na chenji wakaniambia nichukue

Wakawa wananiletea Wateja doh biashara yangu imeongezeka imepanuka nafikiria kufungua branch mikoani sasa

Nikawatafuta wake za wanaume niliokuwa natembea nao nikawaomba msamaha wengi walishangaa wakakubali nikawahakikishia haitarudia tena

Wengine walinitukana na kunifukuza lakini kama ulivyosema msamaha ni kwaajili yangu sio Yao, basi ilimradi nimefanya yangu sina neno na mtu tena

Sasa majuzi kati nikajitoa out hotel moja mjini baada ya mikiki mikiki yote ya kuomba msamaha na kutafuta amani

Nimekaa nakunywa zangu wine sina habari na mtu nipo na ipad yangu mara naona kaka mmoja ananiuliza hii siti inamtu?!

Kumwangalia kaka mrefu handsome mmmh nikachokaa!

Wote: wakacheka

Koku: nikamjibu hapana haina,

Akakaa akajitambulisha anaitwa William

Wote: uuuuh! William!

Koku: akaanza kuniongelesha mwenyewe yup charming mimi nimekaa kimya namchora si unajua mapepe nimepunguza tangu Dokta anichambe

Mwanasaikolojia: hapana sijakuchamba nimekushauri

Koku: poteto potato Dokta!
Anywho!
Tukaongeaa eh kuangalia ni saa 6 usiku
Sikujua saa ngapi muda ulienda maana nilikuwa nacheka muda wote ninafurahi tu

Nilipoona muda unaenda nikaaga, nikaondoka akanifuata mpaka kwenye gari akanipa kitambaa nilikuwa nimekiacha ananiambia naona umesahau nimeona nikuletee je unaweza kunipa namba yako ya simu ili sikunyingine ukisahau chochote nijue pa kukuletea!?

Dah huyu jamaa alinichanganya kidogo nimrukie nikachukua simu yake nikamuandikia namba yangu ya simu nikaondoka

Tangu sikuhio tumekuwa tukiwasiliana asubuhi mchana usiku kama dozi ya Panadol

He makes me so happy, nacheka kila saa so usiku wa Leo anataka kunitoa out kwa mara ya kwanza

Unaonaje Dokta, nilale nae au nimkazie  (nimbanie)

Wote: mkazie

Mwanasaikolojia: usimpe, siku ya kwanza unafungua miguu atakuona mrahisi, mkazie mpaka mwezi uishe

Koku: eh Dokta mwezi?! Utaniua mimi  So bikra ujue

Mwanasaikolojia: si umeomba ushauri wangu?! Usimpe kabisa, ila unaweza kumtega ili aje sikunyingine na sikunyingine na sikunyingine akimaliza mwezi bado yupo na wewe ndio umpe

Ukifanya vinginevyo darasa linalokuja utakuja kuniambia hatokutafuta na ukimbania asipokutafuta usimtafute
Kumbuka wewe unadate nae hampo kwenye mahusiano

Koku: Sasa nitajuaje kama ana mashine kubwa?! We Dokta unataka kuniingiza kwenye mtaro

Mwanasaikolojia: wewe niamini mimi mama fanya tunayokushauri sijawahi kukosea na Mungu ananisaidiaga sawa? !

Koku: sawa Dokta

Mwanasaikolojia: nimefurahi sana kusikia watu wangu wa nguvu mnaendelea vizuri Mungu mkubwa kwakweli hongereni sana sana

Ila msiache amani ya moyoni na mawazo chanya mpaka mwisho

Nataka muendelee na hilo zoezi ila Nataka mtoke nje muwe mnatembea mnajitoa out kama Koku na Rebecca mkutane na watu mjue jinsi ya kuongea nao kutengeneza marafiki kutengeneza mawasiliano ila muwe na mawazo chanya kila siku kila wakati kila saa

Na Rebecca nakutakia safari njema huko unakoenda mwendo ule ule kama nilivyosema



Tuonane Leo J3 tar 11 June 2018 saa 8 mchana ya Tz
------------------------------------------------------------------------

D. MAMBO YAMEKUBALI


Baada ya lile darasa la warembo ikaingia wiki ya kuonana na wanaume kila siku kila mtu na siku yake, kama kawaida nachukua wawili wawili ili kuokoa muda

Karibuni tena , Shaibu na Calvin, nimefurahi kuwaona tena naamini mmekuwa marafiki wakudumu

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: nimepata majibu yenu yote mmeniletea
Je ni sawa nikisoma wote tukashirikishana?

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: haya

Swali la 1:
" Je unapenda kuoa?!"

Calvin - Ndio

Shaibu - Ndio

Swali la 2:
" kama unapenda kuoa unapenda kuwa na watoto wangapi?!"

Calvin - watoto 3

Shaibu - watoto 3

Swali la 3
"Kama haupendi kuzaa watoto wako mwenyewe je ungependa kuisaidia jamii kwa kulea watoto yatima? !"

Calvin - hapana

Shaibu - ndio nataka nilee watoto yatima napenda sana

Well hayo ndio yaliokuwa majibu yenu na mimi nayaheshimu sitaki kumhukumu mtu lakini nikiwauliza kwanini Calvin hautaki kuisaidia jamii kulea watoto yatima unaweza kuniambia?!

Calvin - mmmh watoto yatima nitamsaidia akiwa kituoni sio kumchukua aje kwangu

Mwanasaikolojia: okay asante kwa kuwa mkweli

Haya mmelifanyia kazi somo langu la kuwa na mtazamo na fikra chanya? !

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: je kuna mafanikio yeyote mliopata?!

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: okay, mnaweza kunieleza kila mtu kwa nafasi yake?! Nianze na Shaibu

Shaibu:
Kwakweli dokta nisikufiche, nimejitahidi sana kuwa na fikra chanya ingawa ni ngumu lakini imenisaidia sana kwenye kazi zangu, mpaka wafanyakazi wangu wananishangaa nimetoa wapi imani

Wateja wakija nawasemesha kwa confidence na kwa upendo na kauli nzuri wanashangaa wale wanaonishangaa nipo kama mwanamke nawachekesha wale wanaoniuliza we ni shoga au rijali nawatania wanipe niwaonyeshe mwisho wa mchezo watajua tunacheka

kusema kweli imenisaidia sana hii fikra chanya sii ya level hii mambo yamekuwa fire kwangu

Biashara inaenda vizuri nashukuru sana dokta

Pia bwana Calvin amenisaidia kunifundisha kuwa mgumu, doh mwalimu Calvin anaupendo hajakata tamaa na mimi,  kanifundisha kufikiria kama wanaume wanavyofikiria, kanifundisha kutembea kama wanaume wanavyotembea kuwa mgumu, tukaenda out ananifundisha kutongoza mademu hahaha ha anawatongoza yeye alafu mimi nipo pembeni namwangalia... akanifundisha kujua wife material na mwanamke wa maraha, akaniambia enzi zake alikuwaga pimp, hahaha ha uuuwi

Wote: wakacheka jinsi anavyoadithia

Shaibu: dokta nakushukuru sana sijui nitakulipa nini Darasa likiisha umenisaidia asilimia 50 najua mpaka Darasa linaisha asilimia 100 nitakuwa mgumu kama Calvin

Mwanasaikolojia: hongera sana Shaibu hivyo hivyo mwendo ni huo huo kwahiyo sass hivi unajua kutongoza wanawake? !

Shaibu: bado naifanyia kazi ila naamini naweza

Mwanasaikolojia: usijali utaoa very soon

Haya turudi kwa bingwa Calvin, mambo nasikia ni fire kwa Shaibu hongera ila kwako mambo yakoje

Calvin: nashukuru sana dokta ila kwangu nimeifanyia kazi ile fikra chanya,  imenisaidia Shaibu hapa kanifundisha kuhusu Biashara kama malipo yake kumfundisha kuwa mwanaume rijali anakuwaje

Kanieleza jinsi alivyoanza Biashara akiwa na mtaji wa elfu 20, nikashangaa akanieleza na njia alizotumia kupata Wateja, mpaka amekuwa kibiashara akaenda huko China kununua mzigo doh nilikuwa nakudharau China ila sasa napaangalia kwa macho 3

Kanielekeza mambo mengi na baadae nikakaa nikaandika mambo nayoyataka kufanya kwenye Biashara nikagundua ninao ujuzi mkubwa kwenye sekta ya biashara ni kwamba sikuwa na ujasiri ya kufanya yote hayo kwasababu nilivurugwa

Sasa ujasiri ninao nimepanga nitengeneza Brand yangu ya chakula hapa hapa nchini kwetu, niwe nauza nje ya nchini,  natafuta masoko napeleka kama export nataka nianze Africa Mashariki na Congo na Mafia nasikia Demand ipo

Mwanasaikolojia: oh safi sana kwahiyo umeshapata mashamba ya kulima?!

Calvin: bado natafuta dokta kama unamjua mtu anauza mashamba au anauza mazao niambie

Mwanasaikolojia: well ninae mmoja nitakupa mawasiliano yake utaongea nae ikishindikana nitakutafutia kwengine

Pia kwanini usifikirie kusambaza vyakula vya nafaka kwenye mahotelini makubwa na mashuleni?

Au ufungue hotel yako ya vyakula tu?! Si unajua wewe ni mwanaume, usitegemee sehemu moja tu... ukifungua mgahawa wa chakula au restaurant unaweza ukawa unawauzia watu wa maofisini vyakula nini inalipa

Calvin: yah ni kweli dokta ngoja nifanye hivyo asante sana

Mwanasaikolojia: nimefurahi kuwa Wote mnaendelea vizuri

Pia Shaibu kuna uhitaji wa bidhaa unazouza mikoani unaonaje ukiwa unauzia watu wa mikoani?!

Shaibu: kweli dokta tulikuwa tunapanga na Calvin hapa nitafanya hivyo

Mwanasaikolojia: nataka muwe buzy na maisha mambo yataenda vizuri tu wapendwa wangu, yakale yamepita sasa hivi nyie ni watu wapya

Haya Calvin chukua namba ya huyu dada anaitwa Mwelu anamashamba singida wanalima ongea nae Biashara tu na sio mapenzi

Wote: wakacheka

Calvin: dokta bwana usijali strictly business poa asante sana

Mwanasaikolojia: Haya wapendwa tuonane tena keshokutwa ila nataka nije sehemu zenu za biashara nione mnavyofanya kazi zenu

Wote: sawa dokta hamna shida

Darasa likiisha kwa siku hio

Mwanasaikolojia akawa amekaa anasubiria Wateja wake wengine waliokuwa na Darasa baada ya Lisa li1

Akiwa anasubiria akaingia Aminata akashangaa hee Aminata umekuja Leo kwani tunaonana leo? !

Aminata: hapana nilikuwa jirani nikaona nije kukusalimia kuna maswali nilikuwa yananisumbua naomba unisaidie

Wakaongea weee lisaa limoja likaisha Mwanasaikolojia akamwambia Aminata kuwa anadarasa na watu Aminata akaaga

Aminata alipotoka nje ya ofisi akamkuta Dula amekaa anasubiria wakasalimiana

Aminata mwenyewe amepeendeeza kapata kazi utamjua na alivyo mrembo Dula kachizika kajisahau mpaka kamwomba namba ya simu Aminata akamkazia kamnyima akaondoka Dula akamfuata kwa nyuma akaona ameingia kwenye gari akaandika plate no ya gari ya Aminata mara akamwona Frederick anaingia wakasalimiana wakaingia kwa Mwanasaikolojia

Mwanasaikolojia: Leo naona mmechelewa karibuni sana

Dula: dokta Leo ulikuwa na totoz mmoja anaitwa nani? ! Niunganishie basi?

Mwanasaikolojia: my dia Dula, kwani upo tayari kuingia kwenye mapenzi kwa sasa?!
Kazi ya kuunganishia watu kimapenzi sio yangu Haya nipeni karatasi za majibu ya maswali niliowapa mniletee tukionana

Wakatoa majibu wakakaa Mwanasaikolojia: nimesoma majibu yenu yote mazuri sana,
Je ni sawa nikisoma wote tukashirikishana?

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: haya

Swali la 1:
" Je unapenda kuoa?!"

Dula - Ndio

Fredrick - Ndio

Swali la 2:
" kama unapenda kuoa unapenda kuwa na watoto wangapi?!"

Dula - watoto 2 mpaka 6

Fresrick - watoto 2

Swali la 3
"Kama haupendi kuzaa watoto wako mwenyewe je ungependa kuisaidia jamii kwa kulea watoto yatima? !"

Frederick - hapana

Dula - hapana

Well hayo ndio yaliokuwa majibu yenu na mimi nayaheshimu sitaki kumhukumu mtu lakini nikiwauliza kwanini hamtaki kuisaidia jamii kulea watoto yatima mnaweza kuniambia?!

Frederick & Dula - dokta tunawapenda sana watoto yatima ila tutawasaidia wakiwa vituoni mwao inatosha

Mwanasaikolojia: okay asante kwa kuwa wakweli

Haya mmelifanyia kazi somo langu la kuwa na mtazamo na fikra chanya? !

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: je kuna mafanikio yeyote mliopata?!

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: okay, mnaweza kunieleza kila mtu kwa nafasi yake?! Nianze na Dula

Dula:
Kwakweli dokta nimefurahi sana kwa lile somo, kuwa na fikra chanya imenisaidia sana kwenye kazi zangu, mpaka wafanyakazi wenzangu wananishangaa

Pia nilikutana na yule best yang mjini sikumoja nilikuwa nafuatilia mambo ya kikazi nikamsalimia hakuamini nikamwambia nimemsamehe yale yote amenitendea nimeshasahau nimemsamehe bure tunaweza kuwa marafiki yale yamepita

Akanishukuru sana Kwanzaa hakuamini mana alihisi tutapigana sikuhio

Nikamtoa lunch akafurahi tukabadilishana namba za simu akaniambia kuwa weekend hii alikuwa anaoa akanialika kwenye harusi akanipa kadi nyingine niwape wazazi wangu nikamshukuru

Weekend ikafika kweli tukaenda kwa harusi yake akaoa wazazi wake wanashangaa kutuona wakafurahi tukarudisha undugu

Amepata mwanadada mzuri naamini atatulia nae kwenye ndoa

Hayo ndio yaliotokea na huyu Bwana Fredrick tumekuwa marafiki ila tatizo tunashindwa kwenda nae nje mana amefungiwa huku kwenu ni sheedah sijui mtamsaidiaje

Mwanasaikolojia: hongera sana sana Dula, nimefurahi mambo yako yanaenda vizuri, na usiache kuwa na fikra chanya hata ukioa ukipata watoto ukipandishwa cheo, ukiwa na wajukuu mwendo ni ule ule
Kuhusu Fredrick atatoka tu nje labda keshokutwa tutakuwa wengi tutaanza kwenda nje

Dula: sawa dokta

Mwanasaikolojia: Kuhusu wanawake umepata mchumba?!

Dula: mmh sijafuatilia habari za wanawake ila nimempata mrembo mmoja ametoka hapa ofisini kwako nipe basi contact zake dokta

Mwanasaikolojia: NO

Haya Frederick najua ulikuwa ndani tuuu,  mambo yanaendaje maana huku ndani nako kuna maisha

Fredrick: nimetoka juzi ni kitu ambacho Dula alikuwa hajui ila sikuwa na mawasiliano yake kumweleza ila naishi na mjomba

Sijapewa simu ila muda mwingi nakaa ndani

Somo lako dokta nimelifanyia kazi, naongea vizuri na watu pale nyumbani, nawasiliananna watu vizuri pale nyumbani, nimeanza kuongea na majirani jana wakija nyumbani kuulizia nawasaidia na wapi Keane vizuri

Ni mwendo mdogo mdogo lakini naendelea vizuri Mungu ni mwema nitakaa vizuri siku za usoni

Kila siku mchungaji anakuja nyumbani pale ananifundisha neno la Mungu mjomba amemleta na j2 naenda kanisani kama kawaida mambo ni supa

Mwanasaikolojia: wow hongera sana Fredrick wala usijali safari ya kuwa sawa inachukua muda au unaweza kuchukua muda mfupi haijalishi utachukua muda gani sisi tunataka upone tu

Frederick: sawa dokta nashukuru

Mwanasaikolojia: haya wapendwa wangu tutaonana tena keshokutwa ila darasa litawahi saa 5 asbh kwahiyo Fredrick umwambie Mjomba akulete mapema

Frederick: sawa dokta

Mwanasaikolojia: Pia Dula napenda kukushauri kwenye maisha yako hata wewe Fredrick ukipenda kitu chochote, kazi, biashara, gari,  nyumba, aina ya maisha,  kiasi cha mshahara, mwanamke, mke, usikubali kutafutiwa tafuta mwenyewe, kipiganie mwenyewe huku ukimwomba Mungu akusaidie na kukuwezesha kukipata, lazima upiganie mwenyewe unachokitaka sio kwa kupigana ngumi hapana kwa jitihana kwa kutumia akili na busara na hekima Mungu akiokupa

Kumbuka mwanamke yeyote hapigwi ngumi wala mateke na mwanaume maisha yote usimpige mwanamke lakini mpiganie mwanamke haijalishi amekuudhi haijalishi mazingira mwanamke hapigwi

Tunataka kurudisha maisha yenu na tabia njema zenu naombeni msiharibu huko mlipo la sivyo kazi mliofanya ya kuja hapa itakuwa sifuri

Mwanamke umsemeshe kwa maneno mazuri sikuzote lazima uhakikishe unamfurahisha mwanamke unaempenda haumkosei hata kama hauna hela jitahidi ufanye kazi kwa bidii na sio kuiba au kuua ili upate hela ukamfurahishe mwanamke hapana

Unamtoa out, unamnunulia zawadi sio lazima kitu kikubwa hata zawadi ndogo, ukijua anachopenda unampa hicho hicho na kuzidi kadri ya uchumi uliokuwa nao usijiumize

Pia usijilinganishe na wanaume wenzako kuwa mbona anacho mimi sina ukajiskia upo duni hapana kila mtu Mungu humpa kwa wakati yeye amejaliwa akapewa vingi mshukuru Mungu kwa niaba yake, siku za Mbeleni Mungu nae anakuja kukupa vyako Pia usimdharau mtu asiekuwa nacho bali muwasaidie kwa Hali na Mali na kwa mchango wa mawazo kwa hekima yote Mungu aliokupa

Wote: sawa dokta

Darasa likaisha siku ikaisha

Ikawa jioni Ikawa usiku Ikawa asbh darasa lingine likaja

Hello karibuni sana wapendwa wangu,

Simon akasukumwa mpaka kwenye kiti wakamsaidia wakamwinua wakamweka kwenye kiti

Mr Piggy akaingia akakaa pembeni ya Simon

Mwanasaikolojia: akakusanya majibu ya maswali aliowapa akawa anayasoma akamaliza

nimesoma majibu yenu yote mazuri sana,
Je ni sawa nikisoma wote tukashirikishana?

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: haya

Swali la 1:
" Je unapenda kuoa?!"

Mr Piggy- Ndio

Simon - Ndio

Swali la 2:
" kama unapenda kuoa unapenda kuwa na watoto wangapi?!"

Mr Piggy - Mtoto 1

Simon - watoto 3

Swali la 3
"Kama haupendi kuzaa watoto wako mwenyewe je ungependa kuisaidia jamii kwa kulea watoto yatima? !"

Mr Piggy - hapana

Simon - hapana

Well hayo ndio yaliokuwa majibu yenu na mimi nayaheshimu sitaki kumhukumu mtu lakini nikiwauliza kwanini hamtaki kuisaidia jamii kulea watoto yatima mnaweza kuniambia?!

Mr Piggy & Simon - dokta tunawapenda sana watoto yatima ila tutawasaidia wakiwa vituoni mwao inatosha

Mwanasaikolojia: okay asante kwa kuwa wakweli

Haya mmelifanyia kazi somo langu la kuwa na mtazamo na fikra chanya? !

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: je kuna mafanikio yeyote mliopata?!

Wote: ndio dokta

Mwanasaikolojia: okay, mnaweza kunieleza kila mtu kwa nafasi yake?! Nianze na Simon

Simon:
Lile somo lako dokta nimelifanyia kazi sana tu kwa kuwa sasa naishi na wazazi nikatafutiwa kaka wa kazi kwa ajili ya kunihudumia na kunisaidia hapa na pale

Nakumbuka nilipopata ulemavu nilikuwa mkorofi sana Na mkali sana kila kitu naona naonewa sio kwamba ndio nilivyo hapana lakini ile hasira nilionayo ya kwanini nimekuwa mlemavu?! Inauma basi kila siku namgombeza kaka yangu aliekuwa ananisaidia hapa na pale nagombana na wazazi hasa mama nagomba chakula kibaya yani nilikuwa vibaya sana

Lakini tangu nimelifanyia kazi somo lako la kuwa na fikra chanya doh mambo yamebadilika Kwanzaa nilimwomba msamaha yule kijana wangu ananisaidia pale nyumbani akashangaa nikamshukuru kwa kazi anayonisaidia kila siku namwambia Mungu akubariki kugomba gomba nyumbani kukatoweka nawashukuru wazazi wangu kila siku kwa kunipa fursa ya kukaa nyumbani kwao

Nikakwaeleza ule mpango wangu wa kutaka kwenda kuwekewa mguu bandia India wakakubaliana nami Mama akasema atanisindikiza kuniuguza yeye mwenyewe kwahiyo ndio tupo kwenye maandalizi

Kanisani sikosi dokta nahudhuria kila j2 najenga imani yangu Pia nimesoma mchungaji awe anakuja kila j5 nyumbani anifundishe somo la kusamehe na kusahau

Ndio nipo kwenye hilo somo nafanya na Mr Piggy hapa anakujaga kila j5 kujifunza pamoja nami tumekuwa wanafunzi wa Yesu sasa

Mwanasaikolojia: wooow hongereni sana nimefurahi hata kusikia kuwa mnashirikiana hongereni sana

Hongera sana Simon usijali naamini matibabu ya mguu yataenda vizuri sana utasahau

Simon asante dokta nashukuru

Mwanasaikolojia: haya napenda kusikia Mr Piggy una mapya yapi au habari njema mpendwa? !

Mr Piggy: asante dokta ni kweli somo lako nimejitahidi kuliwekwa kwenye matendo na jinsi ya kuja control na hasira na kutuma tuma watu ingawa ni kazi yangu lakini naweka na ubinaadamu kidogo

Nimekuwa mtu wa kuwa na mawazo chanya kwangu mimi binafsi jinsi ya kujiamini mimi Kwanzaa kujifahamu mimi Kwanzaa na yote kuhusu mimi kabla sijamfahamu mtu mwengine yeyote nataka nijijue mimi Kwanzaa

Kwahiyo nimefanyia kazi ndio bwana Simon akanishirikisha kuhusu Mchungaji anaemhudumia akanikaribisha nikaenda kujifunza neno la Mungu nikawa namwuliza maswali mengi nikaona kama namkwaza Simon nikaomba muda wangu kwahiyo mchungaji wa Simon akawa anakuja kunifundisha siku ya ijumaa pekeyangu amenisaidia vitu vingi ambavyo nilikuwa sivijui na nilivyokuwa navijua nimevielewa zaidi

Hii imenisaidia kuwa na amani ya Moyo ni Mungu pekee anaetoa amani ya Moyo na akili

Mwanasaikolojia: wow Hongera sana Mr Piggy

Mr Piggy : bado sijamaliza dokta

Sikumoja nilitoka out nikaenda kutembea bagamoyo kwa mara ya Kwanzaa nikaamua kulala huko siku 2 ili niinjoi mazingira nje ya kazi yangu doh niliienjoy sana nikapata marafiki wakike na kiume

Nikatoka hapo nikarudi nyumbani, Sikumoja nikatoka kwenda hotel moja mjini nikamwona mrembo mmoja nikampenda sana kwenda naona aibu nikawa nashangaa namshangaa tu

Nikajikaza nikaweka imani ya kwenda kumsalimia nikapiga hatua maana alikuwa amekaa pekeyake nikafanikiwa nikaweza

Tukaongea akawa anacheka sana anasema nachekesha nikamnunulia chakula kwa mara ya Kwanzaa nimemnunulia mwanamke chakula kwa pesa zangu

Akaaga anaondoka akasahau kitambaa nikamkimbilia kumpatia nikamwona namba yake ya simu kama ulivyonifundisha sikuwa na hasira wala maneno ya kuamrisha

Tangu hapo huwa tunaongea kila siku kutwa mara 3 nimempenda Bure hana mapepe ametulia kwa jinsi nilivyomwona sijui lakini

Juzi nimemtoa dinner  (chakula cha usiku) nilipomrudisha kwake nikawa natamani anikaribishe kwake akakataa Juzi tena akaja nyumbani kwangu mchana kwa mara ya Kwanzaa nimemkaribisha mwanamke nyumbani kwangu hata sijui ndio nimempenda au nimeanza kuwa boya sielewi

Tukashinda akanipikia tukaangalia TV movies mara tamthilia ikafika saa 1 akaaga nikawa najishangaa sijamgusa hata busu sikumpa

Mwanasaikolojia: duh! Unasema u kweli au?!

Mr Piggy: ndio dokta

Mwanasaikolojia: huyu mrembo uliempata anaitwaje

Mr Piggy: anaitwa Koku mzaliwa wa Kagera

Mwanasaikolojia: akachokaa Darasa limeota nyasi mapema

Kwanini haukutaka kulala nae?!

Mr Piggy: hata sijui nadhani nimempenda na sikutaka kumtisha au kumfukuza kwa kutaka kulala nae mapema asijeona nataka kumchezea

Mwanasaikolojia: na yeye hakuonyesha kukutega kwa aina yeyote

Mr Piggy: hapana asee alikuwa mtulivu tu

Mwanasaikolojia: unauhakika na hisia zake kwako usijekuwa unafosi mambo?!

Mr Piggy: ninauhakika ananipenda ila jinsi ya kunieleza hajui
Na mimi natamani kumwambia nashindwa Dokta haya mambo ya vijana mimi nishakuwa mzee nampenda kiasi cha kusubiri na kumfanya mke

Mwanasaikolojia: lini unataka kumuoa

Mr Piggy: nikimaliza tu Darasa

Mwanasaikolojia: umemweleza Boss akasemaje

Mr Piggy: bado sijamweleza nashindwa asije akamkataa Bure

Mwanasaikolojia: ni kweli mwanamke unaempenda hautataka kumchezea haraka nakushauri usubirie hata miezi 3 ndio utembee nae ili ujue kama hisia zako ni za kweli au la na za mwenzako zikoje usije ukawa unajisumbua kumbe mwenzako hayupo na wewe

Pia mnaweza wote mkawa pamoja kihisia akaona unachelewa akapata mwanaume mwengine makusudi au kwa bahati nzuri akaambatana nae

Sikushauri cha kufanya kwa kuwa wewe unajua jema na baya

Mapenzi hayapangiwi cha kusema amani ya moyo yako itaamua

Napenda kuwashauri wote haya yafuatayo:

Ukipenda kitu chochote, kazi, biashara, gari,  nyumba, aina ya maisha,  kiasi cha mshahara, mwanamke, mke, usikubali kutafutiwa tafuta mwenyewe, kipiganie mwenyewe huku ukimwomba Mungu akusaidie na kukuwezesha kukipata, lazima upiganie mwenyewe unachokitaka sio kwa kupigana ngumi hapana kwa jitihana kwa kutumia akili na busara na hekima Mungu akiokupa

Kumbuka mwanamke yeyote hapigwi ngumi wala mateke na mwanaume maisha yote usimpige mwanamke lakini mpiganie mwanamke haijalishi amekuudhi haijalishi mazingira mwanamke hapigwi

Tunataka kurudisha maisha yenu na tabia njema zenu naombeni msiharibu huko mlipo la sivyo kazi mliofanya ya kuja hapa itakuwa sifuri

Mwanamke umsemeshe kwa maneno mazuri sikuzote lazima uhakikishe unamfurahisha mwanamke unaempenda haumkosei hata kama hauna hela jitahidi ufanye kazi kwa bidii na sio kuiba au kuua ili upate hela ukamfurahishe mwanamke hapana

Unamtoa out, unamnunulia zawadi sio lazima kitu kikubwa hata zawadi ndogo, ukijua anachopenda unampa hicho hicho na kuzidi kadri ya uchumi uliokuwa nao usijiumize

Pia usijilinganishe na wanaume wenzako kuwa mbona anacho mimi sina ukajiskia upo duni hapana kila mtu Mungu humpa kwa wakati yeye amejaliwa akapewa vingi mshukuru Mungu kwa niaba yake, siku za Mbeleni Mungu nae anakuja kukupa vyako Pia usimdharau mtu asiekuwa nacho bali muwasaidie kwa Hekima yote Mungu aliowapa na kwa upendo mana kuna kesho hatujui kesho kutakuwa na nini

Kwa Leo Darasa limeishia hapa tuonane kesho kutwa saa 5 asbh muda umebadilika


Wacha Movie iendelee tuonane tar 12 June 2018 saa 10 jioni ya Tz
-----------------------------------------------------------------------

E. UPENDO HAUHESABU MABAYA 


Mwanasaikolojia: Karibuni wapendwa Leo najua kwa mara ya Kwanzaa tumekusanyika wanaume wote 6

Napenda kuwakaribisha sana, kwasababau darasa letu linaelekea katikati na mwisho napenda tufahamiane kila mtu ajitambulishe

Wakajitambulishabpale kila mmoja kwa majina yake mawili na kazi / biashara anayofanya

Mwanasaikolojia: asanteni naaamini tutasaidiana katika mengi hasa kwenye gurudumu letu la maendeleo na kutengeneza marafiki

Leo nimewaita kwasababu kipindi chetu cha darasani kinaisha, sasa tunaanza kuingia mtaani, kwasababu tupo 6 napenda tugawanyike kwenye makundi 2 yaani watatu watatu kwahiyo siku za kwenda mtaani tutaenda kwa makundi

Tutaanza na session ya asubuhi, alafu mchana, alafu usiku, alafu za weekend alafu za sherehe alafu za misiba alafu za watoto yatima, masokoni, nyumba za ibada, mwisho tutasafiri kwenda zanzibar alafu darasa litakuwa limeisha

Kila mahali tutakapoenda ni kwa ajili ya kujifunza maana mkitoka hapa mnaenda kuingia kwenye maisha halisi na kupambana na maisha halisi

Mtakuwa mnavaa hivi vifungo, hivi ni speaker kwa ajili ya kuongea na pia Mtakuwa mnavaa hizi saa kwa ajili kuongea pia kuna chain na kuna contact lenses kwa ajili ya macho kwa wasipenda kuvaa miwani

Wote: wanashangaa

Mwanasaikolojia: najua ni lazima nisikilize mazungumzo yenu nijue wapi mnakosea turekebishane na pia mazungumzo yote yatakuwa yanarekodiwa

Siku zote nitakuwa naenda na nyie lakini nakaa mbali na nyie

Naomba tena msisababishe magomvi wala kutaka kugombana mkiwa mtaani mjizuie sana kukimbizana na magomvi

Pia lazima mjizuie tamaa za mwili, sio ruhusa kumbaka mwanamke au kumpiga mwanaume mwenzako kwasababu labda amekataa kitu fulani

Ukiwa mkaidi mtaani utaandikiwa report mbaya ina maana itabidi uanze tena kozi upya na kuna mambo mtazuiliwa kufanya mkiwa uraiani na mnaweza kurudishwa mlipotoka mwanzo, naaamini mmenielewa

Wote: sawa dokta

Mwanasaikolojia: kabla hatujaingia mtaani, nataka mniulize maswali yeyote mlionayo ya nyuma ya sasa ya baadae

Basi kila mtu akauliza maswali kulingana na kutoelewa na sintofahamu zake, Mwanasaikolojia kama kawaida akayajibu tena

Akauliza kama kuna mwenye swali wote wakanyamaza

Akawaita wasaidizi wake wa 4 atakaokuwa nao kila anapoenda mtaani akawatambulisha wakatoka nje kusubiria

Wakati wanataka kuanza safari Dula akaomba aulize aeleze kinachomsumbua dokta akakubali kumsikiliza

Dula: dokta nataka nilitoe dukuduku langu moyoni, ili nisaidikike maana naona kama nakwama

Unamkumbuka yule mrembo niliekutana nae juzi hapa kwako, kabla sijaingia ndani huku nilimfuata nikachukua plate no ya gari lake nilipotoka darasani nikaanza kumfuatilia nikaongea na rafkiangu akaniambia mmiliki wa ile gari jina akanipatia na namba ya simu nikampigia siku ya Kwanzaa nikijidai mimi mfanyakazi wa kampuni ya simu huduma kwa wateja nikajua ni sauti yake na jina lake

Tulipomaliza kuongea baada ya massa 3 nikaanza kumtumia sms za kawaida namsalimia mwisho naweka secret admirer

Tutaanza kuwasiliana kwa kuchat kila siku namtumia sms na ananijibu vizuri tu na tunachat tatizo ni kwamba sasa anataka tuonane kama kweli mimi ni mtu aside akawa anachat na jini

Anataka tuonane leo jioni na mimi naona aibu itakuwaje?!

Mwanasaikolojia: doh Dula sijawahi kukufahamu kuwa mwenye aibu nakuonaga mjanja kila siku kwanza hongera kwa hatua uliochukua ya kufanya jitihada ya kumfuatilia huyo mrembo

Pia usikate tamaa nenda tu kaonane nae na ufanye kama nilivyowafundisha majuzi, msome anapenda na anataka nini, usimfosi kwa kitu chochote jitahidi kumfanya awe na Wakati mzuri atake tena kuonana na wewe sikunyingine

Jitahidi usiharibu sasa hivi, yakale yamepita sasa yamekuwa mapya,  akikuuliza baadae au huko mbeleni mlulishawahi kuwa kwenye mahusiano mwambie ndio, ikawaje mwambie hatuweza kuendelea aliolewa na mwanaume mwengine usiseme kuhusu kumfumania na best yako itakufanya uwe na hasira zaidi utaanza kuchanganyikiwa tena

NA wala usilazimishe kujua mambo yake ya zamani hayakuhusu na asipokuuliza mambo yako ya zamani usijielezee kwani amekuuliza? !

Nakuaminia jembe hautaniangusha, Ukiwa na swali nipigie nitakusaidia

Dula: sawa Dokta asante

Mwanasaikolojia: mwengine anaetaka kuuliza kabla hatujaondoka, ndio Shaibu karibu

Shaibu: je nikitaka nikaombe kulea watoto yatima kwa Wakati huu ambao bado naendelea na kozi nitakubaliwa au?

Mwanasaikolojia: hapana ngoja kwanza umalize kozi kuna mambo mengi ya kujifunza subiri kwanza usiwe na haraka

Shaibu: sawa dokta

Mwanasaikolojia: mwingine mwenye swali?!

Enhe Calvin tuambie

Calvin: dokta nashukuru kwa msaada wako umenipatia juzi kati,  nikampigia yule dada kumwulizia kuhusu mashamba akanielezea vizuri akasema kama itawezekana tukaonana anielezee zaidi na kama nitapenda tuende mkoani eneo la tukio nikamkubalia

Kwahiyo Kesh ndio tutaonana na huyu dada tuongee ila nitakuwa na mwenzangu Shaibu ili anisaidie jinsi ya kuongea kibiashara zaidi

Mwanasaikolojia: wow hongera sana Calvin, nakutakia mafanikio mema ya maendeleo ya biashara zako zote utafanikiwa tu utakaa sawa usijali

Mwingine mwenye swali aulize

Mr Piggy: dokta mimi kesi yangu ni pasua kichwa

Mwanasaikolojia: kivipi tena best

Mr Piggy: Unakumbuka nilikueleza kuhusu yule binti niliekutana nae, tunaanza safari ya urafiki na nikamkaribisha kwangu na nini, dah kumbe yule mrembo ni malaya wa kutupwa

Mwanasaikolojia: eh! malaya tena umejuaje?! Imekuwaje?!

Mr Piggy: Basi Boss aliniita, nikaenda kumsikiliza akanisifu kuwa naendelea vizuri kwenye programme yako, akaniambia nikimaliza kuna kazi nitaifanya alafu nitapewa kazi ya nje ya nchi,

Tukaongea mambo mengi nikaona nimgusie Boss swala la huyo mrembo nikamweleza akaniambia nimpe contact zake na majina yake nikampatia

Jana akanifuata nyumbani akanieleza kuwa yule Koku ni Malaya alishawahi kutembea nae sana tu, ndio kipoozeo chake hata sasa akimwita atakuja tu, anapenda sana hela...akaniambia niachane nae hanifai dah niliumia sana Dokta, sielewi nafanyaje Wakati bado nampenda na hata sijamwelezea hisia zangu kwake kuwa nampenda leo naambiwa niachane nae

Na boss akiongea achana nae unatakiwa uache

Nafanyaje dokta akili imenasa na Koku nampenda kweli

Mwanasaikolojia: haikukusumbua kuwa ametembea na boss wako?!

Mr Piggy: iliniuma sana na sijajua kama ameacha au bado anatembea nae sijui nafanyaje nyie wanawake ndio maana tunawapiga

Hizi vitu nilikwambia bora ningewapa vijana Wangu wapige shoo kwanza sasa na mimi nimeingia mazima mazima ni sheedah kabisa naumia mwenyewe

Mwanasaikolojia: umewasiliana na Koku lini?

Mr Piggy: yangu juzi sijaongea nae jana yote na sio tabia yangu kabisa kila siku tunaongea

Jana amenipigia sikupokea leo kanipigia sijapokea

Mwanasaikolojia: pole sana Mr Piggy, nikuulize swali je kweli unampenda huyu Koku au?!

Mr Piggy: sana dokta ila ndio kanichosha kwa habari nilizozipata

Mwanasaikolojia: labda niwasaidie wote na nashukuru umeongelea hili swala

Kwa umri wenu nyie wote mliopo hapa mkibahatika kupata mwanamke Bikra ni kwa nadra sana labda mkaoe kijijini ndani ndani tena wa miaka 18

Pili kila mtu ana maisha yake ya nyuma hata nyie mnayo,  maisha yenu ya nyuma yasikufanye ukashindwa kuendelea mbele na maisha yako. .. maisha yako ya nyuma yatakuharibia maisha yako ya mbeleni kama utaruhusu wewe mwenyewe

Msikubali mtu yeyote, wazazi, bosi, majirani, jamii kukuzuilia kupata kitu unachokitaka au ulichokipenda

Msihukumu mtu au watu kwa maisha yao ya nyuma walioishi kwenye maisha Mungu hutoa nafasi ya Pili kwa ajili ya kutubu, kutengeneza, kusawazisha na kufanya upya
Tungekuwa tunahukumiana kila siku tusingesogea kimaisha, kimaendeleo

Mngekuwa mmehukumiwa huko mtaani msingepewa nafasi nyingine na familia,  jamii, wazazi ya kutengeneza na kubadilika na msingekuwa hapa mlipo sasa hivi

Mr Piggy: usimhukumu Koku kwa maisha alioishi zamani haujui kwanini aliishi hivyo, kilichompelekea aishi hivyo hata Koku bado anayo nafasi ya Pili ya kutengeneza na kupendwa na wewe

Unatakiwa uwe na msimamo wako kama mwanaume kama kweli umempenda Koku ongea na boss mpaka mwisho uone kama atakuzuilia

Koku angefukua majalada yako ya nyuma unadhani angekubali uwe rafiki yako?!

Je Ukiwa nae anakupigaga vibomu vya pesa?! Kuna umalaya wowote ameuonyesha kwako tangu mmekuwa marafiki

Mr Piggy: hapana

Mwanasaikolojia: ulisema kuwa mchungaji anakuja kila ijumaa kukufundisha dini sio?!

Mr Piggy: ndio dokta

Mwanasaikolojia: kuna mstari agano jipya la Biblia unasema

UPENDO - Uvumilia, hauhusudu, haujivuni, hau-hesabu mabaya, hautoi toi kasoro

Kama kweli unampenda Koku usimhesabie mabaya

Pia kama haumtaki mtoto wa watu kwa ajili ya kazi ulionayo ni bora umwambie mapema kuliko kumpotezea Muda

Huo ndio ushauri Wangu kwako Mr Piggy natumaini utafanya chaguo sahihi ...labda kama una swali lingine

Mr Piggy : asante Dokta hapana sina nashukuru

Mwanasaikolojia: haya sasa naomba tuvae hivi vifaa eh tupo viongozi wa 5 tugawanyike makundi 2 kila kundi na kiongozi 1 na mimi nitakuwa nafuatilia maendeleo yenu

Msivue mlioyavaa na mkimaliza tutarudi hapa hapa kurudisha vifaa na Kesho tutakutana hapa Muda na Wakati kama wa leo

Tunaelekea sokoni tukimaliza tutaenda nyumba za ibada kila mmoja kwa imani yake

Safari ikawiva watu wanaelekea maeneo ya tukio kwa mara ya kwanza wakisimamiwa na viongozi wao wenyewe wanafurahia wanacheka kwenye gari wanafuraha doh kweli kwenye maisha hatufanani ni kama walikuwa hawapo sasa wamerudi tena


Tuonane Kesho tar 14 June 2018 saa 10 jioni ya Tanzania
------------------------------------------------------------------------

F.  BOYS BOYS!

 


Baada ya lile zoezi la sikuile la kwenda sokoni kesho yake vijana wakaja tena kwenye darasa na furaha wamechangamka sana

Mwanasaikolojia kama kawaida akawapokea wamechangamka wanamtania dokta jana ni kama tumeenda peponi, tumejifunza vitu vingi sana tumefurahi sana

Wakaongea wakacheka wote wanafurahi darasa limewaka taa

Dula: dah dokta jana show ilikuwa ya kibabee tumeenda kule sokoni dah tumejifunza kila kit,  mimi siendagi sokoni  kuna dada namwagizaga dada pale ofisini ananiletea ofisini au naenda super market doh mambo yalikuwa bam bam nimefurahi sana tukaenda na sehemu za ibada ah nimefurahi sana mimi msikitini hata siendagi ila kwa jinsi tulivyoenda jana nimeazimia kuwa naenda kila siku na kila ijumaa sikosi kwenda kuswali

Mwanasaikolojia: ah hongera sana Dula nimeupenda moto wako hivyo hivyo usiachie ngazi

Dula: pia dokta nilikutana na Aminata jana usiku kwa chakula cha usiku, dah yule mrembo ni noma kwanza sikuamini kama angekuja

Tukaongea sana mcheshi kweli kweli, tumeongea mambo mengi ananiambia anafanya kazi ubalozi wa Africa Kusini doh si atakuwa na hela kuliko mimi nitamweza kweli?

Mwanasaikolojia: kumuweza kwenye nini tena?!

Dula: si ana hela zake atakuwa anatala wanaume wenye pesa kama yeye

Mwanasaikolojia: kwakweli hayo sijajua kwa mana hajaniambia ila hana ulimbukeni namfahamu na hiyo kazi kaipata kimiujiza juzi ni Mungu kampatia wewe siamini kama mwanaume wa kweli rijali kamili pesa zipo Leo kesho hazipo cha muhimu ni upendo kati yako na yeye je mnaweza kuishi pamoja?  Je anakupenda kama wewe unavyompenda?!

Dula: kweli dokta, haya ngoja niendelee tuone mwisho wake utakuwaje

Fredrick: dokta hata mimi nilifurahi sana kwenda sokoni mana nyumbani nafungiwaga kama nipo jela

Jana ni kama nimepata uhuru nimejifunza vitu vingi sana, na kanisani kwa kuwa naendaga sijaona mabadiliko sana mana kanisani ndio kwangu

Ila nikiendaga kanisani kuna karembo kamoja nimekaelewa kanaitwa Mary, dah yule dada sijui ni mfanyakazi wa kanisani kila siku nikiendaga namwona alafu anapendezaje sasa, doh

Jana sasa nilimwona nikamfuata wakati msimamizi wangu alienda msalani. .. nikamsalimia akaniitikia vizuri mwenyewe ana lugha nzuri kweli, doh Dokta unasemaje nimchukue huyu mtoto au

Mwanasaikolojia: mmmh hapana sio kwa sasa tafadhali, usijiingize kwenye mapenzi sasa hivi

Fredrick: kwanini? ! Mbona akina Dula na Mr Piggy umewaruhusu?!

Mwanasaikolojia: sijaruhusu mtu yeyote kuingia kwenye mapenzi au nasema uongo jamani?

Wote: kweli dokta ni sisi na viherehere vyetu tuliamua kwenda wenyewe ndio mana tunajisalimishaga kwa pilato tunamwambiaga dokta ili ajue cha kutusaidia

Mwanasaikoloji: Fredrick kila mtu aliepo hamfanani matatizo yenu kabisa kila mtu na matatizo yake na mimi nankufahamu wewe na Calvin mlipotoka ni kama mpo sawa hata Simon pia

Nawashauri wote msijiingize kwanza kwenye mahusiano ya mapenzi, na nyoe Mr Piggy na Dula mlioingia huko lazima mnisikilize kwa makini kabla hamjaharibu kabisa

Wote: sawa dokta

Mwanasaikolojia: kwahiyo ukafanyaje na Mary wewe Fredrick

Fredrick: tukasalimiana nikagundua kuwa yeye sio Mtz ni Mganda kiswahili hajui vizuri anaongea kizungu zaidi uzuri na mimi nilisomaga somaga kinapanda kizungu kidogo nikamwomba namba yake ya simu akaniambia haikumbuki ndio ameingia Tz ana wiki 3 ngoja akachukue simu aniandikie akaenda kuchua kurudi akakuta nimeondoka mana muda ulikuwa umeisha na supervisor akaja kunichukua tuondoke, tukiwa kwenye gari tunaondoka namwona anaingia kanisani kuniangalia hajanikuta

Mwanasaikolojia: oh pole sana!  Ila nakushauri hata ukienda kanisani ukimkuta hayupo au ukimwona usimkumbushe namba ya simu
Jaribu kuongea nae kwanza uwe rafiki kwake kwanza, utengeneze urafiki nae kwanza baadae utajua kama umempenda kweli au ulimtamani

Kumbuka baharini kuna samaki wengi na wengi wanafanana kama Mungu amekuandikia yeye utakuwa nae usifosi mambo, mambo yanajipaga yenyewe
Na pia umepata wapi simu?!

Fredrick: mjomba amenipa akaniambia kwa kuwa ninashinda nyumbani muda mwingi kukiwa nandharura au namwitaji dereva anilete huku ndio nimpigie

Mwanasaikolojia: OK hongera sana unaona mjomba anakuamini sasa usijali uaminifu utaendelea kujengwa kwenye familia yako ila jitahidi usiharibu wewe ni mtu mzuri,  mtu wa maana, kaka wa maana, handsome, una akili sana, usijali maisha yako yatakaa vizuri sana

Fredrick: asante sana dokta

Mwanasaikolojia: na nyie wengine safari ya jana mliionaje

Calvin: ah dokta poa tu kama alivyosema Fredrick ni nzuri sana tunasubiria kwenda Beach huko tuone warembo

Wote: hahaha ha ndio dokta beach lini tunaomba twende weekend

Mwanasaikolojia: ah baharini tutaenda mara 2 kesho na weekend jumamosi saa 5 asbh lkn lazima turudi mapema maana saa 11 jioni nina watu wengine wa kuwahudumia

Simon: dokta na kumbi za sinema usisahau pia, twende na huko na disko!

Mwanasaikolojia: hahaha we Simon unataka kwenda na disco utachezaje sasa? !

Simon: ah we dokta achana na mimi, mimi nacheza kuliko maelezo au nikuonyeshe?! Akainuka anataka kucheza hawezi basi ni shida tu ikabidi wen zake wamsaidie akae

Basi dokta kama disko itashindikana twende kwenye mahoteli makubwa

Mwanasaikolojia: sawa Simon tutaenda kote usijali kumbe na wewe umo kwenye kucheza mziki ee hongera sana

Shaibu: dokta tunakushukuru sana kwa ajili ya jana kama alivyosema Dula mimi Msikitini ilikuwa ni kama kituo cha polisi nashukuru jana tumeenda umetukumbusha mambo mengi kwahiyo nimepata Imamu mwalimu atakuwa ananifundisha mambo ya dini kwa muda wa miezi 3
Pia sokoni umetupeleka nafurahi sana ingawa sokoni mimi naendaga ila jana nimejifunza lugha za biashara nilikuwa nikiendaga siombi kupunguziwa bei kumbe bwana wale jamaa wanapataga sana hela ee?!

Doh asante sana lile soko nimelipenda sana sikuwahi kwenda ila nitakuwa naenda

Mwanasaikolojia: wow hongera sana Shaibu nimefurahi kusikia hivyo

Mr Piggy: Dokta mimi ni kama hawa wote wengine walivyosema nashukuru sana, Kanisani ni pale naposali, Sokoni sijawahi kwenda kabisa nashukuru sana pia natazamia pa kwenda siku ya Leo sijui kutakuwa wapi?!

MwanSaikolojia: Leo tutaenda sokoni kwa wazungu kunaitwa Super market kufanya shopping mtapewa tsh 20,000 msinunue kitu zaidi ya elfu 20, na lazima ununue kitu cha muhimu tu somo letu la leo linahusisha mahitaji ya Binaadamu  tumeanza jana na Chakula ( Cha kimwili na Kiroho)
Leo tutaendelea na chakula pia kwenye masoko na majumba ya kidhungu kwa maana ya hotel kubwa kubwa

Alafu tutarudi hapa kila mtu atarudi nyumbani kwake akitokea hapa

Kesho hatutakuwa na darasa mpaka kesho kutwa muda wa asubuhi

Wote: sawa dokta wenyewe wamefurahije sasa wapo tayari kwenda huko lkn sio Mr Piggy hakuwa na furaha kabisa

Wanasaikolojia: Mr Piggy Leo hauna furaha au unahisi utakutana na koku huko?! Kuna nini Mbona umekasirika namna hii?!

Mr Piggy: ah dokta Acha tu kwa sasa twende tukija tena kwenye Darasa nitaelezea

Mwanasaikolojia: ila sio vizuri kwenda na mtu alienuna nieleze tatizo lako nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia

Mr Piggy: Dokta hamna bwana mimi nipo sawa ngoja kwanza niangalie siku 2 hizi maana nilioyaona jana sikuamini alafu keshokutwa nitakuja tutaongea kwa marefu na mapana

Mwanasaikolojia: ikabidi aridhie,  wakaja wasaidizi wake wakagawa pesa kwa kila mtu, wakaambiwa wanunue mahitaji muhimu tu ya kila siku hatowaambia ni nini lakini yeye anawaaminia wanajua

Pia akawafundisha somo la kutotumia pesa vibaya, na kutonunua vitu visivyokuwa na lazima, na jinsi ya kutunza pesa kama akiba kwa muda wa nusu saa

Hivyo ndivyo darasa lao leo lilivyoenda



Tuonane Tar 18 June 2018 saa 8 mchana ya Tanzania
------------------------------------------------------------------------

G. ALL IN MY GRILL  (LAZIMA NI ISHI )

 


Mwanasaikolojia: Baada ya matembezi ya jana asubuhi asubuhi nilipata simu ya Koku kuwa anataka kuniona haraka ana dharura 

Nikamwambia aje asbh maana saa 5 nina kipindi na watu

Saa 1 asbh akaja hata chai hajanywa chai itadhani amelala baa kaja amecharuka nywele, mswaki hajapiga ikabidi nimpeleke bafuni akaoga kwanza akapiga mswaki akaosha na nywele akawa yupo sawa, nikamuazima nguo zangu akavaa nikamfanyia makeup doh hatari 

Kazi kama yangu hauhitaji kujiweka juu juu lazima ujishushe mpaka tunamaliza ni saa 2 nanusu asbh 

Nikampatia kikombe cha chai na maandazi akanywa ndio kukaa sawa anaongea

Koku: madam mimi kuolewa baaass

Mwanasaikolojia: eh kwanini?! Kuna nini tenaa

Koku: unakumbuka nilikwambia nilimpataga this guy anaitwa Mr William 

Mwanasaikolojia: ndio nakumbuka imekuwaje?!

Koku: basi tukaenda vizuri ikafika sehemu akanichunia nikiwasiliana nae kwa njia ya sms hajibu simu hapokei sikuelewa 

Nikampigia  kama siku 2 lakini kimya Baada nikajiona mjinga woi nikamchunia 
Tukamaliza wiki sijamwongelesha akaja akanipigia sikupokea akapiga sana sikupokea 

Weekend moja nikasikia hodi, kufungua namwona bwana wangu wa zamani anaitwa Julius

Julius bwana nisikufiche na ndio maana nipo hapa kuja kuongea nawe sikutaka wale wenzangu wajue

Julius ndio kanileta kanipa maisha mjini ndio kanitoa bikra yeye ndio kila kitu kwangu lakini kuoa hataki ana miaka 50 lakini hataki 

Yule jamaa ni noma, ila anaweza akaja Leo kesho au akamaliza wiki akapotea mwezi, miezi 3, 6 haonekani na mimi nina mahitaji kama mwanamke, nikachoka 

Nikaendelea na maisha yangu huyu Julius ana karaha moja akishajua nimepata mwanaume mwengine tu na tunapendana anarudi fasta na Nikamwambia anasema aliekwambia mimi nimeachana na wewe nani?!

Na atahakikisha anamtoa huyo mtu niliekuwa nae kwa fujo zote mpaka ataondoka narudi naanza moja 

Mwanasaikolojia: huyo Julius anafanya kazi wapi?! Kwanini usibadilishe namba yako ya simu ukahama unapoishi

Koku: nimeshafanya yote hayo, Julius nipo nae mwaka wa 10 sasa, mambo yake sijui kama mchawi

Nilishabadilishaga namba ya simu mimi kesho yake akanipigia nikachoka, nilishahama nyumba kama 3 anatokea anakuja anagonga mlango au sikunyingine namkuta ndani yani kama pepo sijui ovyo kabisa 

Mwanasaikolojia:  kwahiyo sasa ikawaje?

Koku: mara ya mwisho kuondoka ilikuwa miaka 2 iliopita nikajua hapa harudi

Julius ndio ameniweka mjini,  akaunt zangu za bank hazijawahi hazijawahi kupungua hata 100
Kama nina milion 800 nikitoa 10 Leo nikienda kucheki Baada ya wiki nakuta mil 800 kama kawaida 

Nyumba naishi Masaki nimenunuliwa
Gari naendesha ndio hill Discovery 4 evogue 

Nasafiri nchi nazotaka Madam hakuba nchi sijasafiri nimesafiri Dunia yote nahisi nimemaliza

Ila jamaa hataki kunioa hataki tuzae

Kuna siku nilijilengesha dokta nikashika mimba yani niliitoa bila kupenda alininyanyasa, alinichukua akanirudisha kijijini, akatoa hela zote kwenye bank yangu, nikawa maskini upyaa akaniachia lake 1 akaniambia ukishaitoa mimba nipigie akaniachia simu tochi Nokia nikasota kijijini ni kama Yesu ametoka Mbinguni kaja ahera nilisota nikaitoa mimba mwenyewe nilipomwambia nimetoa akatuma mtu akaja kunichukua nikapandishwa ndege za kukodi zile ndogo mwenyewe na dereva na mimi mpaka Dar nikapokelewa na Ambulance nikaenda kusafishwa Hospital akaja kunichukua mpaka kwake makao mengine mapya ya Masaki ndipo napoishi 

Sasa aliondoka kwa muda mrefu ukimpigia hapokei mara namba haipo sms hajibu basi majanga tupu 

Ndio nampata sasa Mr William woi, na Mr William tumependana mambo yanaenda vizuri namwona kabisa anataka kunioa ingawa hatujatembea wote wala nini, lakini ananipenda 

Kwa Julius mimi ni kama Mtumwa wake hata akinifanya unaona kabisa hamna upendo kama anamfanya changudoa 

Wakati tunaendelea na Mr William, akaja tena Julius yani kama jini anasubiria nikiwa nimeshaanza kumpenda mwanaume linakuja kama jini oh nakupenda na nini, nikamwambia nimeshapata bwana mwengine tunapendana naondoka kwenye maisha yako sasa akanijibu huondoki, nikamwambia ukirudi hautanikuta akasema hautakaa uondoke kwenye maisha yangu

Ndio Mr William akakata mawasiliano sasa sijui aliikamata namba yake akaenda kuongea nae hata sielewi


Mwanasaikolojia: kati ya Mr William na Julius nani unampenda sana

Koku: nampenda William ila sielewi kwanini ananikimbia 

Basi aliporudi Tena William nikahakikisha tumeonana nikajilengesha siku ambazo naweza kupata mimba, tukakutana nyumbani kwa Mr William tukapigana mechi kwa mara ya Kwanzaa dooooh! Mr William ana machine balaaa utadhani Mghana!

Woi lile limnara sio la nchi hii jamani,  Kwanzaa sikuamini alafu wa moto inaelekea hajapiga nje muda yule, alafu anajua mechi nimefungwa magoli kiboya boya seriously Mr William kanivuruga vibaya mno

Julius hana machine kama William

Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye machine kama William madam, wengine wote vibamia kasoro huyu William sijawahi kuinjoy mechi kama ya William kwa miaka 5 sasa doh!

Mwanasaikolojia: sasa utafanyaje?! 

Koku: Baada ya mechi nikaamua kumweleza ukweli wa maisha yangu Mr William, akachokaa, nikamwonyesha picha ya Julius akachokaa, anashangaa nikamwambia nimechanganyikiwa kwenye maisha yangu kiasi kwamba sasa natafuta msaada kwa Mwanasaikolojia ndio kidogo napata unafuu na naogopa huyu bwana Julius anaweza akamfuata akamfanya kitu mbaya nimeona nikuambie tu

William hakuongea aliondoka akaenda kuoga,  akavaa akaondoka sikumwona tena William

Nikakaa pale siku nzima hakuja nyumbani, kesho yake hakuja, kurudi kwangu sitaki maana najua ni makelele tu

Simu nampigia akawa hapokei sms hajibu sijui nimekosea wapi?!

Nikarudi nyumbani kwangu sasa, namkuta Julius ananisubiria nyumba ipo tupu hamna kitu naona masanduku yangu tu, namwuliza umehamisha vitu wapi ananiambia kuanzia Leo mimi na wewe basi, nimechukua kila kilicho changu naondoka kwenye maisha yako tafuta mwanaume atakaekupenda na kukupa familiar mimi siwezi nisamehe kukupotezea muda na kukutolea Mimba, Mungu akuzidishie akupe watoto dhambi Yako naomba niibebe mimi

Pesa kwenye bank nimechukua zote nimekubakishia mil 150 tu ya kuanzia maisha nenda katafute maisha yako, nimekusubiria tangu jana haupo unatakiwa uondoke nirudishe funguo

Biashara nimekuachia mbili zingine zote 3 nimechukua
Gari langu nalitaka nipe funguo

Sikuamini, ni kama mfungwa amewekwa huru haamini kama ameachiwa nikamkumbatia, nikambusu kwenye mashavu na mdomoni, nikamwambia nimekusamehe asante sana Mungu Akubariki nikampa funguo wa gari nikaondoka kutafuta  hotel nikaenda sea cliff

Sea cliff na hela ndio hizo nikaongea na dalali anitafutie nyumba kuanzia upanga mpaka mikocheni, akaniambia Kuna nyumba Mikocheni B wanapangisha kama utawezs kodi ndio nipo naishi hapo 

Mwanasaikolojia: hongera sana kwa kuwa huru na kwa kuwa na msimamo, sasa utafanyaje na maisha yako ya sasa?! Biashara ni kweli kakuachia 2 na Pesa ni kweli kakuachia alizosema?!

Koku: ninkweli nilienda kwenye Biashara zote nikafukuzwa 3 nikapewa barua kuwa sio mmiliki tena wa Biashara zile Nikarudi kwenye mbili nikakuta barua ya umiliki wa zile Biashara nikashukuru

Biashara ya hotel za watu kulala kariakoo na Biashara ya mgahawa wa chakula Upanga nashukuru Mungu kwa kweli

Pesa kama alizosema ni hizo hizo kaniachia bado nashukuru

Madam tangu nimeondoka kwenye maisha ya Julius nina amani ya ajabu lakini pia naumia 
Nampenda sana William lkn naona nae anakuwa kama Julius ni kama nimeruka majivu nimekanyaga moto 

Nae anatokea kama malaika na kupotea ni sheedah hata sijielewi nina shida gani au kaoa?! Ila anasema hajaoa sielewi tatizo nini 

Mwanasaikolojia: mara ya mwisho kumuona William ilikuwa nini?!

Koku: wiki 5 zimeisha sasa 

Mwanasaikolojia: na Julius mlipoonana ulitembea nae?

Koku: hapana ndio kilichomfanya afikirie mara 2 na kunifukuza kwake kila akija namnyima simpi nakimbia nalala nje ilikuwa shughuli nimelala hotelini mara zote nimelala nje na kwa William ndio akanibana nimweleze nikamweleza ukweli naona kama nimemfukuza doh majanga 

Nifanyaje Dokta?!

Mwanasaikolojia: nakushauri usimtafute tena William atakutafuta mwenyewe maana ameshafanya hivyo tena we mpotezee akija usitembee nae tena ila safari hii mkaribishe kwako na akitaka mechi mwambie hapana maana sielewi na sikuelewi unataka nini kwangu akueleze kwanini anatokea na kuondoka mimi sijui kwanini anatokea na kukimbia 

Hio ndio kazi nakuachia mpendwa wangu, tutaonana kesho nina darasa na nyie utanielezea yaliojiri 

Koku: sawa Madam asante sana 

Koku akaondoka zake amekuwa mwepesiii sio mzito na mwenye majonzi kama alivyokuja 




Tuonane Kesho tar 20 June 2018 saa 1 usiku ya Tz

☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆

H. MTOTO WA MAMA


Mwanasaikolojia: karibuni wapendwa wangu kwenye darasa letu

Najua mlifurahia sana mtoko wa jana

Wote: ndio

Mwanasaikolojia: nataka chenji yangu plz haya kill mtu anirudishie pamoja na karatasi ya vitu vya muhimu alivyonunua na chenji Najua mliambiwa muandike

Mwanasaikolojia akapita akakusanya makaratasi na chenji akawa anasoma akarudi kwa watu wake

Calvin, Dula & Shaibu
Niliwaambia Jana mnunue vitu muhimu mmeenda kununua dawa ya mswaki, mswaki, machine ya kunyolea ndevu, taulo na sabuni ya kuogea kwanini?

Wote 3:hivyo ndio vitu muhimu kwetu kwa sasa kila tukiamka na kurudi kulala

Mwanasaikolojia: je mkiwa na familia sio muhimu kwenu au?!
Chakula je?!

Wote 3: hapo basses kwa sasa hivyo ndio muhimu

Hotel zimejaa kwa ajili ya Chakula

Mwanasaikolojia: akacheka doh! Kwahiyo kupika nyie hamtaki? !

Wote 3: wanawake ndio wapike sisi tutafute

Mwanasaikolojia: kila siku mtakula nje?!kupika inapunguza stress mjue

Wote 3: sisi ndio wanaume bwana tuache

Mwanasaikolojia: okay, na nimesoma mmebakisha hela nyingi hii kweli hongereni

Wote 3: iliobaki tungeenda kula hotelini kama usingesema turudishe

Simon, Frederick & Mr Piggy:

Mmebakisha chenji ndogo,  mmenunua mahitaji Mengi na Chakula

Waliobaki 3: ndio, mahitaji muhimu ya mwanadamu ni Chakula malazi mavazi

Mwanasaikolojia: sasa hamtaki ku save kwanini?

Waliobaki 3: dokta wazungu wanasema tumia fedha ikuzoee, tumia fedha ujue jinsi ya kuitafuta ... unatumia zaidi utafute zaidi, upate zaidi utumie zaidi

Mwanasaikolojia: akacheka akaanza kuwafundisha kuhusu mambo ya afya na kuweka akiba kwa muda wa lisaa limoja

Baadae akawaelekeza safari waliokuwa wanaiendea siku hio na kesho asubuhi safari ya kwenda beach wanafurahia kweli wenyewe

Kabla ya kuondoka kuingia mtaani akawauliza kuhusu mahusiano yao walio na mahusiano

Kila mmoja alikuwa na jibu lake

Fredrick: mimi sijamwona tena Maria kanisani

Dula: Mrembo wangu kwa kweli tupo nae vizuri tunaendelea vizuri nahamu ya kumuoa hata kesho

Mwanasaikolojia: mmmh hapana kuoana wakati hujamaliza kozi sio suluhu subiri umalize alafu utaangalia

Dula: sawa dokta

Mr Piggy: akaongea yote ambayo hakuongea na Mengi alikuwa ameshaelezea Koku jana yanafanana akamwambia mwanasaikolojia kuwa amemchunia sana Koku hajui tena jinsi ya kurudi

Kule boss ameniambia niende nae tu, ameona jinsi gani ambavyo Koku anampenda sana Piggy, hatoingilia mahusiano yao tena na wakitaka kuoana waoane

Mr Piggy akawa ameshangazwa sana na jibu la boss wake akahisi anamtega sijui mana hakuelewa ile ruhusa ilikuwa mapema sana

Mwanasaikolojia: Kwahiyo umeamuaje sasa?!

Mr Piggy: nimeamua kukaa kimya sidhani kama nitarudi kwa Koku ule ni mtego nimewekewa Boss wangu namjua haachi chombo chake anschokipenda kirahisi

Mwanasaikolojia: unajua mimi siwaelewi nyie watu, kwanini mnachezea maisha ya watu alafu mnakimbia kama hamumtaki mtu si mumwambie

Unajua mnachokifanya mnafanya wanawake wengi wawachukie wanaume Wote na ndio shida inapoanzia mtu anaamua kujizalia watoto bila ndoa, kwasababu mmempotezea muda na umri wake umeshaenda sana na ndio mana wanaume kama ninyi mpo hapana sababu ya watu kama Piggy wanaochezea wanawake na kuwaacha na kuwafanya wanawake wengi kuwa wapigaji na wapenda hela Kwanzaa utu baadae

Wanaume wa sikuhizi wanasifika kwa tabia ya kupenda pesa Kwanzaa alafu utu baadae ni kwasababu wanaume kama Mr Piggy hapa waliwachezea akili wakakimbia na wanaolipia makosa na madhambi yaliofanywa na Mr Piggy na nduguze ndio wanaolipia akina Dula, Simon, Calvin

Wote: kimya

Mwanasaikolojia: Kwahiyo kwako Mr Piggy tumefunga ukurasa wa mapenzi sio?!

Mr Piggy: mimi nimemaliza sitamtafuta tena Koku aendelee tu na maisha yake huko aliko

Wote: wakashangaa doh wanaume kama Piggy wangekuwa milion 1 nchini hakuna mwanamke angetamani kuolewa tena sio kwa ukatili na roho mbaya ile


Wakajiandaa na safari yao mara wakasikia hodi

Mwanasaikolojia: karibuni,  wewe ni mgeni wangu au?!

Mgeni: ndio mimi mgeni wako madam Naitwa Masumbuko nimepewa hii barua nimeambiwa uje kuisoma ni mtu wako mpya

Mwanasaikolojia: akachukua barua akaisoma, akaisoma wateja wake wakae chini amsikilize Masumbuko

Akamkaribisha Masumbuko akakaa, akawasalimia wenzake 6 walioko pale,

Kuwa hurt,  jisikie upo nyumbani akamweleza kwa ufupi kuhusu kila mmoja aliekuwa pale na shida yake ili ajiskie vizuri

Masumbuko akajiskia vizuri akaanza kuongea

Masumbuko: Naitwa Masumbuko, mzaliwa wa Dar, ninafanya kazi kama mwl wa chuo kikuu kimoja Dar, nina miaka 35, Mkristo, Mchaga, nimefanya kazi miaka 3 sasa nafundisha wanafunzi wa Diploma, nimepewa hapa nipate msaada

Ninakunywa sana pombe lakini pombe nimekunywa hivi karibuni, kwasababu ya mpenzi wangu Nancy ameniacha

Mwanasaikolojia: kwanini Nancy amekuacha? !

Masumbuko: ameniacha kwasababu ya kutoelewana sijui alikuwa hajanielewa yeye au mimi sikuwa naeleweka

Mwanasaikolojia: Nancy hakukuelewa nini? !

Masumbuko: Nancy tulienda nae vizuri na tulioana kabisa, lakini analalamika kila mawazo na mipango tukipanga lazima nimshirikishe mama yangu mzazi kwanza ndio tuje tufanye mipango

Mama akikataa hakifanyiki kitu

Mama akikubali tutafanya

Mwanasaikolojia: umeoa kwa muda gani?!

Masumbuko: ndoa mwaka sasa

Mwanasaikolojia: kwanini mipango yako ya maisha umshirikishe mama tu na mpaka mama akubali ndio mpange? ! Kwani hauna Baba?! Kwani wewe hujiamini?!

Masumbuko: baba yangu alifariki wakati nimemaliza degree yangu, mimi ni mtoto wa mwisho kuzaliwa, mama yangu ndio kila kitu kwangu

Mwanasaikolojia: unajua kuwa ulimwengu wa sasa umeenda mbele sana, unapoamua kuwafanya mama ndio mwamuzi wa maisha, mipango na maendeleo yako kwenye maisha yako ya kila siku?! Ikatokea Mungu akachukua utafanyaje! Na wewe utakufa nae au?!

Masumbuko: akakaa kimya, akanyamaza kama hakusikia swali

Wote: wanamshangaa Masumbuko Hawaelewi kalogwa na nani? ! Mamake au nduguze? !

Calvin: dokta mimi nimeelewa tatizo la Masumbuko ni Mama's Boy mtoto wa Mama kila kitu anafanyiwa na mama wanapenda wanaume wa mwisho wanawadekeeza kweli kweli

Hapa umeletewa Mtoto wa Mama kazi sio ndogo dokta ila sisi tunakuaminia utamsaidia tunataka kwenda mtaani sasa

Mwanasaikolojia: sawa, Masumbuko naomba unione j3 asbh saa 3 tutaendelea na swala lako nitakushauri? Leo ni kama UMeCHELEwa kuja na sisi tulikuwa tunatoka

Masumbuko: sawa dokta nashukuru

Wakainuka Wote wakatoka tayari kwa safari yao



Tuonane Tar 28 June 2018 saa 1 jioni ya Tz
-------------------------------------------------------------------------
SEHEMU YA 4

A. MAISHA MPYA

Baada ya ule mtoko wa sikuile kesho yake asubuhi tukakutana ilikuwa weekend saa 3 asbh watu wamewahi, maana tulipanga kwenda beach

Usiku wa jana tulishindwa kwenda mziki kulingana na outing ya jana na watu kuchoka tukaona tuahirishe tuweke siku spesho kwa ajili ya muziki

Asubuhi vijana wamewahi wamevaa Kaptura, utadhani kuogelea wanajua basi tu midadi

Safari ikaanza kuelekea Kigamboni kwenye hotel moja hivi ilikuwa siku ya sikukuu

Foleni sasa ni sheddah kuvuka kivuko,

Kufika tukawekana sawa, jinsi ya kuenenda
Watu Kufika wakakimbilia kwenye kuogelea swimming pool akina Calvin, Shaibu, Dula, Fredrick, wana dive kama kawaida

Simon anaijua hali yake  akakaa pembeni anaangalia Mr Piggy akakaa na Simon wakawa wanaongea

Ikapita nusu saa, nikaona wadada wameingia si unajua tena mambo ya beach, vichupi nene wale waliokuwa kwenye swimming wote wakatoka wakaja kukaa wanakunywa soda wanaangalia vichupi

Kuangalia kwa mbali nikamwona dada




Mmoja ameingia na time zake, nikamsogelea Mr Piggy nikamwambia kuna mrembo pale, unaweza kwenda kumpa kampani au?!

Mr Piggy: akamuangalia, doh ngoja niangalie akamuangalia tena akaniambia haya ngoja niende mama

Akainuka akaenda, huku tumemvisha mike aina ya kifungo

Akaenda pale anamsalimia doh nikafurahi sana, Mr Piggy ni wale ma Gentlemen flani hivi ila sijui hajijui au hajielewi au sijui ndio ajira yake hio

Alifika akamsalimia vizuri dada wa watu kamnunulia na kinywaji wakapotelea kwenye ufukwe wa bahari, dada wa watu anatabasamu na kucheka tu nikajua hapa KOKU vepe?!

Nikamwachia supervisor wangu aendelee kumsikiliza Mr Piggy mara namwona  Simon ameshakamatia beibe mwingine aliekuwa amekaa nje ya swimming pool doh, vijana wana moto utadhani wamefungwa mota

Kuangalia kushoto kwangu kila mtu na demu wake, si Calvin si Shaibu, si Dula tena nilishangaa kuona Dula yupo na demu mwingine wakati ameniambia mambo yake na Aminata yapo vizuri

Fredrick nae ameshasahau kuwa Mary wa Kanisa anafananaje maana amekaba mpaka penati totoz moja matata amefungasha hataree hahahahah kweli wanaume shikamoo marahaba!

Tukakaa Beach hapo mimi nipo buzy na kusikiliza Receivers za watu wote kwenye gari  sasa
Akikosea unamsahihisha ukiona anaharibu unamsahihisha

Darasa limeiva, vijana wamejielewa, vijana wapo vizuri utadhani wanataka kuchomba dawa skuhio hio

Mpaka tunaondoka kila Mmoja amekamata mawasiliano ya kila demu (mrembo) aliekutana nae Beach

Tukazama Darasani kwetu baada ya msosi wa mchana na movement zote nawauliza sasa mtamuoa nani

Wote wanacheka, cha kushangaza zaidi kila Mmoja anasifia kuwa wale wanawake hawajagundua kama wao ni wagonjwa au walikuwa wagonjwa wa akili

Shaibu hakuonekana kama shoga alidanganya alipata ajali akaanza kutembea kama mwanamke na huyo demu akakubali

Kweli njaa njaa tu,

Huyu Dula nae akamdanganya demu wa watu kuwa ni Mkristo akaiba jina la Fredrick akampatia Huyu mrembo alikuwa nae na akaamini tena kamdanganya ameokoka akaanza na kumhubiria
Na kesho kanisani ameshaalikwa aende na amekubali, doh Dula Mungu anakuooooonaa!

Calvin kama unavyomjua, alitoka na mawasiliano ya mademu 3, si unajua tena Calvin alikuwaga pimp anajua njia ya kumkamatia mwanamke akakamatika usiku huo walishapanga watoke out na mmoja leo; kesho usiku na mwingine na j3 usiku na mwingine sasa sijui akigonganisha magari itakuwaje nimemshauri asifanye huo mchezo maana yaliomkuta Simon yanaweza kumkuta mara 3 kaniahidi hatagonganisha magari lakini hajaniahidi kutoonana nao

Simon na hali yake ya ulemavu alifanikiwa kupata mrembo matata sana tabu ya huyo mrembo ni ufupi, sasa sijui safari ya matumaini ya mapenzi itakuwaje lakini mimi nipo hapa kumsaidiia

Mr Piggy tayari alishapendana na huyo dada Darasa likiisha wanaonana kwa Hotel, anasema akitoka pale anaenda kununua condom maana lazima achinje kuku siku hio

Nimemwuliza vipi kuhusu KOKU akanijibu KOKU ndio nani? !

Fredrick nae anasema Mary hajisomi lakini bado anampenda sana, kwa sasa ataenda Kwanzaa na Huyu demu amempata beach afanye kama twishen ya kutongozea ili aone ufanisi wake umefikia wapi na wapi kapungua

Kweli wanaume shikamooni Marahaba!

Baada ya Mirejesho hio nishauri ya kushauri lakini kushauri watu waliojipanga kufanya matukio inakuwaga ngumu nikaamua kugawa zawadi ya Condom kwao wasije kupata Ukimwi

Naamini wamenisikia na watayafanyia kazi lakini sidhani!

Baada ya hapo wakaondoka, jumamosi saa 11 jioni, saa 1 usiku nina Darasa na warembo, nikaamua kujilaza kwenye kitanda kwa masaa 2 mpaka 3 nipunguze uchovu

Kuja kushtuka naona wanafunzi wanagonga, doh warembo nimewamiss kweli kweli wamependeza wana nuru usoni, nikatamani nisikie kutoka kwako

Baada ya dk 20 tukaanza Darasa let

Kila mtu yupo na good news kila mtu anatabasamu kuongea lakini KOKU hakuwa na furaha kama siku za mwanzoni

Nikatamani nianze na KOKU nikaona hapa Darasa litaingia mafuriko

Nikaanza na Mwelu

Mwelu:
Madam nashukuru Mungu nilienda India na Mama nikafanyiwa upasuaji wa njia ya kisasa mambo ya kidhungu inaitwa Robotic Surgery kule mjini Bangalore, hospital ya Manipal nikaondolewa Fibroids pazurije sasa

Woi hospital kubwa gharama zipo chini doh tulienjoy, nimefanyiwa upasuaji baada ya siku 5 nipo mzima natembea fresh tukaongezea siku 3 tukarudi

Na leo nilijua sitakuja nimekuja ila nimeendeshwa na dereva wangu

Wote: wakampigia makofi hapo wanampongeza Hongera Mwelu umetoka Mali,  Mungu Akubariki

Koku: ulivyompandisha Mama ndege alijiskiaje!?

Mwelu: Kwanzaa hakuamini Koku, aliliaa ile tunapaa nakwambia ananishikilia anaogopa, anasema Yesu Yesu kumbe ndivyo ulipaaga kwenda Mbinguni, tisa kumi nikamweka siti ya dirishani weee Acha kabisa

Mama nimemdondoshea 1st class utamjua, ahahahaha akajua kufunga na kufungua mlango basi kila Saa anabonyeza namcheka mama utaaribu

Vyakula sasa anakula kila kitu mpaka tumbo ikamwuuma akaharisha masaa kibao anakaa chooni hatoki hajui ku flash, anataka kuchamba namwambia tumia toilet pepa hajazoea basi ni vituko tu kweli tuli enjoy sana

Vyakula vyenye pilipili anakula kwa fujo ulimi akaungua hajazoea akaweka soda ikawa shida ya coca zaidi acha apige makelele wale flight attendant wakaja anawaonyesha ulimi si kizungu hajui

Wote: ahahahahahahahha

Mwelu: Ni vile hatukukaa sana kazini walinipa siku 10 tu sasa nikaona nizitumie ipasavyo

Kule India sasa hajui kingereza yeye anajua kusema yes, no, yes, no sasa kuna vitu anatakiwa aseme no anasema Yes
Pale airport wanamwuliza hili jina lako anasema No basi vurugu mwanzo mwisho

Koku: ulijiskiaje kuona mama anafurahi namna hii?!

Mwelu: ah ni amani koku, amani mwanzo mwisho, rahaa unapara raha nafsini mwako

Wote: hongera Mwelu,  Mungu akubariki Mwelu

Mwelu: asanteni sana na Mwanasaikolojia pia nashukuru sana, mmeniambia ukweli mmenikemea nimewapenda Bure, Koku nakupenda Bure asante kwa kunisuta na kunisema vibaya ... mama karudi kila siku Ubarikiwe Ubarikiwe doh, akiongea na watu vijijini anasema mwanangu amenipandisha ndege abarikiwe sana doh hadi raha

Naombewa ofisini,  Naombewa nikitoka asbh nikirudi, nikila chakula doh utadhani naishi na Mchungaji ndani rahaa

Koku: no problem my dia tupo hapa kusiadiana

Mwelu: nilimcheki pia mama afya yake, ameonekana ana tatizo la mifupa nitatafuta likizo niende nae akatibiwe mgongo unamsumbua sana

Mwanasaikolojia: hongera sana Mwelu, tunafurahi unavyoangalia wazazi na sikunyingine umchukue na Baba na Mama wote 3

Mwelu: sawa dokta

Mwanasaikolojia: enhe na taka kuskia toka kwa mfanyabiashara wetu maarufu Madam Rebecca

Rebecca: asanteni unajua sikujua kama nitawahi hili Darasa nashukuru Mungu nilifika salama niliwahi kwenda niwahi kurudi maana Visa ilikuwa bado haijaisha

Basi siku naenda Airport njiani nikakutana na baba mmoja mzungu amesimama na mabegi, nikamwambia Dereva embu simama,  akasimamisha gari nikashuka nikaenda kumsikiliza

Akaniambia anaelekea airport, taxi aliochukua imeharibika sasa amesimama pale kwa muda mrefu anasubiria labda taci nyingine itapita, ameshasimamisha magari mengi hayasimami, anashangaa mimi kwanini nimesimama

Nikamwambia nami naelekea airport kama vipi twende wote tukaongozana mpaka Airport, tukiwa kwenye gari akaniambia anaelekea mji huo huo ninaoenda, yeye ni mwenyeji kule, nikashukuru kuwa tunaenda safari moja

Uzuri wote tumelipia business class, tukakaa Business Class lakini sio seat moja,

Tukasafiri tukaja kukutana tena Transit, tukabadilisha wote tukaja kuwekwa seat moja

Doh  tukaongea mastori sasa na mimi nimezoea kwenda hio nchi lakini yeye alinieleza huo mji kwa namna ya tofauti,  akanielekeza nguo na viatu kwa bei ya jumla, akaniandikia na maduka, akanipa namba yake ya huko nikiwa na shida nimpigie

Kufika tukaagana kila mtu na safari zake,



Nikaendelea na hamsini zangu siku ya kwenda kutembelea yale maduka nikapotea nikarudi hotelini nampigia kumwuliza maana nimepotea akaniambia nakuja nikupeleke

Kesho yake nikapelekwa doh, nilifurahije vitu vizuri sana bei nafuu na rafiki yani faida mara 10 ya zamani niliokuwa napata

Nikazungushwa huko mimi kazi yangu kuandika tu naandika tu majina ya hizo sehemu

Kurudi saa 2 usiku kila mtu kachoka

Tukaonana kama siku 3 zaidi, siku ya kununua mzigo yule baba kanipeleka, kanitambulisha kwa wabeba mzigo wa bei nafuu ni nduguzake, nikapewaje discount sasa dah kweli kusiadia mtu usiemjua iliniponyesha

Nikapakia sasa kesho kutwa nirudi zangu Tz, akaniomba niende nae out kule nae dinner kesho yake, nikaenda nyumbani kwako kuzurije sasa doh kama Mbingu ndogo, nikagundua huku ninaemwita baba hajaoa hana hata watoto hakuwahi kuoa aliona muda ushapita kila mtu kaoa akaendelea na maisha yake hajali keshapotezea habari za kuoa

Koku: weuweee enhe tupe ubuyu mama tunaskiza

Rebecca: shoga nikataka nijirahisi nikaona sasa nitaboa dinner ikawa dinner baba wa watu anaonyesha movement mimi nimejikausha kama mti mkavu najifanya sielewi

Akaniambia basi ukiwa Tz tuwe tunawasiliana nikampa namba yangu ya Tz nikamshukuru sana, nilinunua saa moja matata sana designer kwa ajili ya kumshukuru nikampatia mwenyewe hakutegemea anashangaa na kushukuru

Mwisho wa siku hamna cha shoo wala mechi iliopigwa niliamua kubana miguu mwanzo Mwisho,  ni kukumbatiwa basi

Akaniuliza umeolewa nikamwambia hapana, watoto sina

Nikamwuliza una umri gani akaniambia miaka 45 doh! Sheedah!

Koku: enhe 45 huyo anaitwaje

Rebecca: anaitwa Johnson

Wote: uhuuuu! Johnsooon!

Rebecca: basi nikarudi zangu hotelini baada ya chakula cha usiku, kwa Uber, kesho asbh nasafiri

Kurudi Tz simu ya kwanza nimeipata ya kwake anauliza kama nimefika salama,

Basi tangu hapo mawasiliano ni simu na whatsapp

Simu - WhatsApp

Kama hajapiga leo kesho atapiga

Mzigo yangu imefika salama sijawahi uza kama nilivyouza wiki hii doh,

Koku: mbona haukuniita nije kukuungisha shogari? !

Rebecca: oh jaman sikujua ila hujachelewa karibu tena

Koku: hukujua au ulikuwa buzy na Johnson

Wote: wakacheka

Tuonane Kesho Tar 29 June 2018 saa 1 usiku ya Tz kuona sehemu B ya Kwanini Upo Singo!

 

_____________________________________________


B. NIPO SINGO KWASABABU NIMEHARIBU MBAYA 



Aminata: hongera sana Rebecca, uliokota embe dodo Chini ya muembe
Sasa usijishatue kitchen pati inakuhusu msumbue sana dokta hapa ukikwama tu unampigia usiharibu

Wanaume watu wazima ukiwaletea mapicha mapicha haueleweki wanaondoka kimya kimya mami

Wanaujua kwa umri wao wanaweza kamata jike aina yeyote popote pale walipo ni vile tu umeonyesha ubinaadam kwake kakupendea hiko

Umri unaenda ivo 32 ni umri mzuri wa kuolewa ukifika 34 unachanganyikiwa mara 3 maana unaiona 35 inapiga hodi alafu uwe hujaolewa haujazaa weee unawakened jiua

Rebecca: Sawa somo nitakuwa nakupigia na wewe pia

Aminata: dokta me sina mrejesho kwa wiki hii nachosubiria ni hizo trip za Zanzibar alafu na hilo disko pati mwisho wa siku tuzame kwa watoto yatima nikachukue changu nilee nimeshajikubalia kuwa kuolewa mimi baaas nimeshachelewa, nina miaka 34 mwakan 35 nani anataka wazee?! Kuzaa staki staki hata kuskia ngoja nisaidie watoto wa Mungu niwalee

Kikazi nipo vizuri sana kazini nimepelekwa training nimefuzu, wiki nzima ndio j3 naendelea na kazi ya u-receptionist

Mwanasaikolojia: mmmh kwahiyo kuolewa baas hutaki kuskia, Sawa na hakuna mwanaume yeyote amaekusumbua hata huko kazini, hata wa kukuchokoza chokoza!?

Koku: ndio embu tuambie ukweli bwana kazini hapo hata wa kukupigia miluzi hamna maana kukumgeni sikuzote anakuwa kama nyuki kila mtu anamfuatilia

Aminata: ofisini nimeweka uso wa Mbuzi (serious face) kuna mtu anahangaika na mimi Sasa alafu majibu yangu ni shot shot staki uendeleze maongezi na mimi

Koku: kwa namna hio mama utaendelea kuchina kwenye jiji la wazaramo

Tereza: kwahiyo wewe ukiwa na hamu zako unafanyaje au ndio unamwomba Mungu

Koku: heheheeeee Bwana Yesu ameuliza Leo swali la Kidunia, patamu hapoo!

Aminata: hahaha ha niachee me sijaokoka ujue niachee nikikuambia ukweli utaishia kufunga na kuniombea bora nikae kimya nisikukoseshe amani bure

But since mmenishambulia kuna huyu kijana sijamwelewaga mpaka Leo amepataje mawasiliano yangu, alinisumbua kwenye simu nimemblock kaongezea tena namba nyingine kunitafuta nikamblock akanifuata ofisini dah nilichoka

Anatuma maua kila siku mara kadi zimeandikwa mtu asiejulikana alafu jioni namkuta ananisubiria anipe lift wakati gari ninayo doh!

Kanisumbua sana nikaamua kumwonyesha mimi sio level za chini akazidi kujiongeza nikakubali kuonana nae

Tukatoka out siku moja anaonekana ni kijana mzuri sijui bwana me nimevurugwa wanaume wote sawa kwahiyo sijui

Tunawasiliana kila siku na wala staki kumweka moyoni kifupi staki kufungua moyoni wangu kwa wanaume

Namhurumia ila kwakua ameamua mwenyewe kuweka kambi nikimhama asinilaumu

Huku anatabasamu

Koku: huyu bwashee anaekusumbua anaitwaje

Aminata: anaitwa Dula
Huku anatabasamu

Koku: asee madam msaikolojia huyu teyari

Mwanasaikolojia: teyari kivipi

Koku: hawa walishakulana muda sana

Mwanasaikolojia: kulana kivipi tenaa tumia kiswahili sanifu

Koku: ah we nawe kama kilaza,  washatembea tena sio mara 1 wala 2 hata mara 5 asitupotezee muda. .. We Aminata hii shoo ya ulokole waachie akina Mwelu na Tereza we mwenyedhambi kama sisi kama hutaki kutueleza ukweli pisha wengine waongee

Wote: wakamwangalia aminata Huku Koku anakunywa soda yake ya Coca

Aminata: ndio ni kweli

Wote: ohoooo, mbona mapema sana mamaaa
Wengine wanasema tobaaa ushaachwaa
Kila mtu anamlaumu kasoro Mwanasaikolojia

Mwanasaikolojia: mmefahamiana kwa muda gani na Dula

Aminata: wiki 3

Wot: wiki 3?! Doh pole

Koku: msimlaumu alikuwa na kiu na njaa kali hahahahahaha, acheni anywe maji ya uzima ya Dula ahahahaha

Wote: wakaishia kucheka

Walicheka sio kwamba kinachekesha lkn hawakutegemea Koku angeongea yale maneno

Mwanasaikolojia: mlipomalizana mechi 5 amekutafuta

Aminata: mechi 3 bwana achana na Koku,  mmmh tangu juzi sijamsikia sijui kumekuwaje maana sio kawaida yake kila siku ananipigia

Mwanasaikolojia: ulimpigia siku hizi 3 akasemaje

Aminata: hajapokea nikituma sms hanijibu

Koku: asee tafuta bwana mwengine na ujifunze skunyingine kuwa mafia
Mtu wiki 3 unafungua miguu we jinga sana

Aminata: akawa mnyonge ghafla maskini

Mwanasaikolojia: usijali aminata kama ni wako atarudi tu kama si wako Mungu ni wa kwetu sote atakupa mwingine mzuri zaidi atakaekupenda na kukujali zaidi

Aminata: sawa dokta nashukuru



YAJAYO YANAFURAHISHA UPO TAYARI?!

USIKOSE KESHO TAR 30 JUNE 2018 SAA 10 JIONI YA TZ
________________________________________________

C. NIPO SINGO KWASABABU WANAUME HAWAELEWEKI


Tereza:
Madam mimi sina cha kuongea maisha yangu yanaendelea nipo na furaha amani, ingawa nilitamani niwe tajiri kwa umri wangu lakini wap nipo hapa hapa

Koku: tobaaa! Dillusional people wameamka
Embu tuambie kivipi?!

Tereza: nilijipangia mambo mengi,  nikasoma kwa bidii nipate elimu zote zinazotakiwa nchini elimu ya kutosha, kazi Mungu alinipa, nilipanga kwa umri huu niwe na familia yangu,  watoto wawili lakini sielewi shida iko wap, sijui wap nakosea

Koku: labda utueleze tangu uanze kuja hapa na ukapata marafiki huko uliko mana ulituambia unatengeneza marafiki, tuambie hujapata hata ka bwana kanakobipu bipu huko kwako? !

Tereza: kubipu hakuna me sibipiwagi

Koku: we nawe unachelewa sana kufikiria namaanisha hamna kijana anaeonyesha anakutaka kimapenzi akupe dudu labda

Kuluthum: ahahahahahaha akyanani Koku nimekushindwa nakugawa bure

Tereza: mmmh sijaona

Koku: ukiwa na hao wanaume marafiki uwa mnafanyaje?!

Tereza: tunatokaga kiofisi

Koku: enhe?!

Tereza: basis tunakaa kwenye meza tunaongea tunakula tunakunywa

Koku: nawe unakunywa maji au divai? !

Tereza: soda

Koku: endelea me Leo ni monita wenu mana spidi yako ya ngama hatutafika

Tereza: ndio hivyo

Koku: ushawahi kujitahidi ukatoka hata sikumoja ukaenda out mwenyewe tu

Tereza: mmmh hapana naogopa

Koku: ungemchukua hata Kuluthum au Rebecca au Aminata hapo ungeenda na mmoja tu yeye akae upande wa kushoto wewe kulia muwe mnatumiana sms mnachat mnajifanya buzy na simu kumbe hamna kitu hata kumcheka jirani yenu mwenye sura mbaya ee?!

Tereza: sijawahi kuwaza kwa upande huo

Koku: unawazaga nini sasa?!

Tereza: lakini kujitoa out ili kutafuta bwana ni kama kudanga na kufanya uchangudoa

Koku: sasa hapo ndio unafeli, tofauti yako wewe unatoka na marafiki zako na mwenyewe ni nini?!

Tereza: tunatokaga wengi kujiuza kunakuwa hamna

Koku: naomba nimsaidie kazi Mwalimu Mwakasege mama ukitoka out mwenyewe haimaanishi kuwa unajiuza, na hakuna mtu anaeanza kukufikiria unajiuza labda kama umeamulia ndani ya moyo wako kuwa unajiuza

Usituletee ushamba wa kijijini, ndio umesoma na una elimu ya kidunia ila elimu ya maisha wewe ni boya sana

Nakushauri uchukue likizo uende hata hapo bondeni kwa Mrehemu Mandela ukaondoe ka ushamba kako hata kwa wiki 1 ukirudi akili itakaa sawa la sivyo utakuwa na maisha magumu sana hata ukija kuzaa watoto utawaumiza vbaya mno

Maana mitoko ya watoto wake itakuwa beach, kanisani, shuleni, sokoni,  mlimani city, mbuga za wanyama
hata shul naona watasoma za serikali kisa unasevu hela kwa ajili ya baadae

Mama una 34 changamka una mwaka m1 kuwa 35 kama alivyosema Aminata jana

Alafu huu ufupi wako sasa doh uache ubishi Maana wanawake wafupi mnashida sana na wabishi mno, eh! Mwanaume akikuangalia anaona matatizo sasa ujirekebishege ivoo usimpe nafasi ya mwanaume kusema nilijua tu Maana kafupi kanaonekana shida shauriako

Pia WANAUME wengi hawapendagi kumfuata demu ambae yupo kwenye makundi

Hata kama amekupenda haji, ukiwa pekeyako inakuwa rahisi kwake

Ni WANAUME wachache sana wanaweza mfuata mwanamke aliekaa kwenye magrup, wachache kama kwenye kumi wapo 2 tu

Sasa endelea kukaa na makundi wenzio wataoa na kuolewa utabakia unatoa macho

Una kingine kipya tuokoe muda?!

Tereza: hapana kwa Leo inatosha (akajibu kwa unyonge masking doh)

Koku: haya mwingine nani anafuata?

Mwanasaikolojia: ahahahahaha doh kazi ipo jamani mwingine, Tereza mzoee Koku bwana ingawa amenisaidia kushauri ila anasema ukweli
Usichukie bwana

Tereza: sawa madam, sijachukia nipo sawa

Kuluthum: me nataka Koku aongee Maana naona Leo anamoto  balaa sijui kapata bwana wa kizungu au hatuelewi

Koku: a hahaha ongea wewe mama yangu mengi na marefu sana hautayafikia

Kuluthum: doh haya me sina cha kusema nataka kumwambia Tereza me natokaga mwenyewe napataga wanaume ila show ikiisha nawahama sihangaiki nao

Ukitaka kampani niambie tutatoka mama usijali

Nimeshasema ndoa sitaki wala watoto sitaki shule yangu inaendelea vizuri naipenda kozi muzuri sana naifurahia
Ni hayo tu kwa Leo tumpishe bi Koku aongee maana Leo kitaeleweka sio kwa moto aliokuwa nao




Koku: haya haya mniache Leo nijimwage mdomo unawasha sana leo

Wote: karibu mama karibu umalizie dk 45 zilizobaki tucheke tukalale

Koku: sauwa
Si mnakumbuka niliwaambiaga kuhusu Mr William, yule mjinga me nimeachia yule bwana wangu was miaka yote kwa ajili yake alafu yeye ananiletea mambo ya kunata mambo za kijinga mapicha mapicha tu hata simwelewi

Nikaamua kuwaondoa Wote kichwani nikatoka kama Mungu nimetoka nikapata buaaana  (Bwana) heavy duty flani amazing, kapanda kajaa kama body guard wa Mwanamziki Diamond Platnumz

Tukazama kwa room, kabla hatujaanza show tuko zile steji za mwanzoni doh tunaskia mlango unagongwa, kwa hasira yule baunsa akaenda kufungua kuangalia mtu hamjui anamwambia mtoe mke wangu kabla sijakumaliza

Me nimekaa kitandani naskia wanagombana mara mlango ukafunguliwa kwa nguvu yule baunsa kapigwa chini tobaa kuangalia kumbe ni William kajaa na marafikizake 3 nao wamejaa eh kweli Hotel imevamiwa

Wakamwambia yule baunsa aondoke la sivyo watamgeuza demu wake wamle nyama
Baunsa kakataa ugomvi watu wakaanza kujaa, watu wamejaa mpaka wakaja security, kuwekana saw a wakaniuliza huyu mtu ni mumeo, kumwangalia William amelewa chakari nikamhurumia nikasema ndio basi wakamtoa baunsa nikamwomba msamaha akaondoka

Wakabakia hao mabaunsa wa William nikamwaomba wamweke kitandani wakaondoka

Nikamwangalia William anakoroma kalala nikamtoa nguo zote mana alikuwa anatoka jasho kweli a/c haifanyi kazi

Nikakuta simu yake, pekua pekua na wewe hamna contact hata 1 kuna namba yangu ya simu tu...yani simu yake haina namba zaidi yangu alafu kasevu jina Love nikachoka

Kama kawaida me mwenyewe mtoto wa mjini, nikamfunika nguo nikaondoka hotelini na simu yake hapo saa 6 usiku, nikazama kwa rafkiangu mmoja nikamkuta amelala,  nikamwamsha akaja anafoka nikamwambie we tulia kuna dharura hii simu ya jinga mjanja naomba tucheze nayo usiku huu huu nina massa 2 pombe itamtoka sitaki anikose kitandani nimemfunika lakini amelala mtupu

Cheza na hii simu unganisha na yangu akitembea kokote mimi namwona akiongea na mtu yeyote me najua

Mjanja akafanya yake akafeli

Nikamkomalia akasema hii simu ya mjanja mwenzangu, sa cha kukusaidia labda nikuwekee akipata simu za watu wa kawaida tu unajua ila simu zingine huku ngumu zaidi ya hapo sitaeza niache nilale mama

Koku nikapiga akili kwani Tsh ngapi?! Weka mjanja Weka
Mjanja akafanya yake ndani ya Lisa limoja nikarudi hotelini William hajafurukuta nikamvisha nguo zake na simu yake pale pale nikarudishia nikaingia kuoga nikapanda kulala

Saa 12 asbh nashtuka William hayupo eh Nikaamua kuondoka kurudi kwangu namkuta amelala kitandani kwangu kwenye nyumba yangu mpya nilishtuka skuelewa ameingiaje namwuliza mlinzi ananiambia amesema ni mpenzi wako na msg kanionyesha imetoka kwako nikamruhusu

Mlinzi akaaga nikaenda kumwamsha oya amka we umeingiaje huku

William: kwani vepe?! Mbona makelele unajua unaniumiza kichwa ujue dah niache Bwana

Nikaenda kuchukua maji nikamwagia we jingas amka upesi ulilipia hii nyumba au?! Nikavuta kiti unasemaje?!

William: njoo njoo nikamwambie nasemaje siwezi ongea kwa nguvu

Koku: kama lofa nikasogea Si akanibambia Tukazama mechini baada ya mechi kuisha ananiambia hicho ndicho nilitaka kukuambia yani huyu mwanaume anaboa sijawahi kuona

Nikalala kuamka hayupo, nikaendelea na mambo yangu kufungua laptop na simu naona alipo anapoenda anakutana na watu anapokaa nikajua anavyotongoza wanawake wengine najua nikahisi huyu boya ameshanifanyia maujanja hata simu yangu pia imekamatika

Nikanunua simu mpya ya tochi kubwa nikawa naiacha nyumbani naondoka na ndogo doh nilimvuruga vbaya mno alafu line ya simu nikaandika jina la bibi yangu marehemu patamuje line yenyewe ya kutengenezeshesha vibandani

Nimemsumbua wiki nikampiga misele na wanaume akija nyumbani ananikosa analala mpaka asbh hamna mtu akiangalia kwenye simu yake anaona nipo nyumbani

Ndio kupekua chumbani akaikuta akacheka sana akairudisha akaondoka

Siku na mimi nikamwibukia kwake bila taarifa kuna Siku alikuja akasahau funguo wake nikachongesha bila kujua

Kufika namkuta na mwanamke mwingine wanaanza ku-do!

Nikachukua kiti nikasogea karibu yule demu aliekuwa anamjigijigi anampa dozi akaniona akashtuka mimi nawaangalia huku natumia simu, William akaniona akashtuka, nikamwambia mkimaliza niambieni mimi nipo hapa nasubiria zamu yangu tena usimwibie raha yake mpe dozi kikamilifu ukimaliza uje na kwangu

Sasa ole wako usinipe yangu kwa staili ya kitemi ntakukata gololi hizo nikaning'inize mpakani mwa nchi yako endeleeni tu

William alichoka, akaacha akamwambia yule demu unajua huyu mke wangu namkosea sana nisamehe me nimeoa mke wangu alisafiri kwenda kwa wazazi nilijua atachelewa kurudi naona kawahi

Kaomba msamaha pale mimi nawaangalia tu yule dada akaamua kuondoka baada ya kuvaa nguo zake William akampa laki 3 akaondoka

Akarudi ananiomba msamaha mimi namwangalia tu, alipomaliza kuongea makorokocho yake nikamwambia kuanzia Leo sahau kuhusu mimi, usinitafute, usije kwangu usihangaike na mimi na ile simu ulioni-track hii hapa kaa nayo sitaki kufuatiliwa mimi sio mhalifu

Nikainuka nimemwacha amepiga magoti na kaptura lake kama muuza samaki wa feri

Tangu Siku hio sijamsikia tena William wala makamasi mpaka Leo hii simu Nikanunua nyingine lkn namba ina jina la marehemu bibiangu mpaka aje ajue atapata tabu sanaa

Wote: wakachoka wakaanza kuangaliana tu

Mwanasaikolojia: doh, Koku tunakuonaaa! Umekuwa James Bond wa kike au sio?!

Nyie Bwana mnapendana msituchoshe sisi kama vipi wekeni mambo yenu sawa tule pilau yaishe hizi vurugu zenu pelekeni Bongo Movie zitawasaidia kuingiza hela kama wataweza kutengeneza movie zako

Basi wiki ijayo tutaenda Zanzibar, ijumaa jioni saa 1 tutakutana hapa kwa ajili ya safari tutakaa mpaka j4 maana j4 ni sikukuu, naombeni muweke mambo yenu sawa nyumbani au sio?

Wote: wakafurahi wenyewe safari ya Zanzibar imewadia



Tuonane Kesho tar 3 July 2018 saa 1 jioni ya Tanzania
__________________________________________________

D. NIPO SINGO KWASABABU NILIMKOSA TEREZA




Mwanasaikolojia: karibu sana Masumbuko na hongera kwa kuwahi, jisikie upo nyumbano uwe huru na mimi maana tupo wawili na siri ni kati yangu na wewe

Masumbuko: asante Dokta

Mwanasaikolojia: haya niambie kuna sababu nyingine nyuma ya pazia kwanini unamsikiliza sana mama kuliko mwanamke uliempenda?!

Masumbuko: hapana dokta

Mwanasaikolojia: baba alifariki ukiwa na umri gani? !

Masumbuko: miaka 20, nikiwa najiunga na chuo 

Mwanasaikolojia: wazazi wako walikuwa wanapendana sana au walikuwa wanagombana kila siku? 

Masumbuko: walikuwa wanapendana sana sana mpaka nikatamani kuoa nikimaliza chuo tu

Mwanasaikolojia: sasa hii tabia ya utoto WA mama umeipata wapi?!

Masumbuko: mimi sioni kama ni mtoto WA mama najiona nipo sawa

Mwanasaikolojia: kwani huyu Nancy uliemuoa ulimpenda au ulioa kwasababu marafiki zako walikuwa wanaoa ukaona uoe

Masumbuko: kusema kweli dokta hapa nitakuwa mkweli, unajua mimi wazazi wangu walikuwa na hela sana, sasa wakati nasoma chuo mimi nikawa nakuja chuoni na gari zuri kwa kipindi kile kuwa na gari ya land rover ina maana una hela sana,

Sasa mimi sikuwahi kumpenda Nancy, unajua tena watoto wa mjini hawa watoto wa kizaramo sikumpenda kabisaa 

Mimi kuna dada m1 tu nilikuwa nampenda ila sijui yupo wapi, nitampata wap, nitamtoa wap yule nampenda mpaka Leo 

Mwanasaikoloji: huyo uliempenda ulisoma nae hapo chuo au?!

Masumbuko: ndio dokta, alikuwa anaitwa Tereza Albert alikuwa mfupi, ana bonge la guu tangu tumemaliza shule sijamwona tena

Sasa huyu Nancy alijua kuwa nampenda Tereza na alikuwa best na Tereza na nikawa namtumia kumwambia kuwa nampenda sana best yake kama vp aongee nae aninyooshee kumbe na yeye alikuwa amenipenda 

Doh akaniganda Dokta akawa ananiambia kwanza Tereza ana mwanaume mwingine ana hela sana anafanya kazi Kampuni ya wazungu, amekataa hakutaki basi nikarudi nyuma

Nikawa singo sina mtu ndio Nancy kunitongoza ananipenda kumbe hajanipenda kapenda Mali za nyumbani

Mwanasaikolojia: ulishawahi kuonana na Tereza Life akakataa kukuskiliza au uliogopa?

Masumbuko: hapana sijaweza kabisaa kumweleza na kila nikikutana nae ananisalimia vizuri sana, ndio baadae kuja kugundua kuwa Nancy hakunipenda ni pale nilipomuoa 

Mwanasaikoloji: sijakuelewa ulijuaje hakupendi?!

Masumbuko: alikuwa na bwana wake mmoja ambae niliskia alikuwa na ukimwi, baada ya kuoana na Nancy, akaja mke wa huyo Bwana ananitafuta pale kazini akanionya kuwa mkeo anatembea na mume wangu nakushauri ukapime maana mume wangu anaukimwi, nimemuonya mara nyingi lakini hasikii kabisaa nikaambiwa ameolewa na wewe nimeona nije nikutahadharishe kapime afya yako, kama utakuwa na ukimwi pole sana kama hautakutwa nao mkeo achana nae, akatoa picha za fumanizi la mumewe na Nancy wakiwa wanakutana kila siku ya ijumaa hotel moja Kinondoni 

Mpaka siku moja akaenda kumwitia waandishi wa habari, wakapigwa mapicha akamwambia mumewe ukiendelea na huyu demu aliekuletea ukimwi nitawaweka magazetini 

Ndio mume akaachana na Nancy ndio tukasikia umemuoa 

Dokta nilichokaa nilikuwa mdogo ghafla nikalowa jasho nikamwambia yule mama naomba twende hospital nikacheki afya maana hapa nguvu sina akakubali akachukua taxi mpaka hospital Posta tukapima tukasubiria majibu ni hapo hapo si unajua mambo ya kisasa 

Majibu kuja sina UKIMWI 
Yule mama hakuamini, tukahamia hospital ingine nikakutwa SINA 

Tukahamia hospital kama 4 tena jumla 6 zote sina doh ni kama nimeponea kwenye mdomo wa Mamba dokta 

Nikarudi nyumbani moja kwa zote nikarudi kwa mama nikamueleza uzuri sisi kwetu wazazi wangu walikuwa wasomi wote, kabla hatujaoana na Nancy tulienda kwa Mwanasheria tukaandikishana kitu kinaitwa Prenaptual agreement  (makubaliano ya Mali kabla ya ndoa) kwa maana ya Mali alizozikuta Nancy kabla hatujaoana zote ni zangu,  zile mali tutakazochuma baada ya ndoa ndio zetu hata tukiachana tunagawana zile tu tulizochuma ndani ya ndoa 

Basi hio ndio ilikuwa pona yangu

Nikamweleza mama akasema naita kikao cha familia, lkn uniambie kama unampenda Nancy na unataka kuendelea na Ndoa nikamwambia Nancy simpendi sijawahi kumpenda nahisi kwanza aliniloga maana sielewi nimemuoaje maana alinidanganya ana mimba yangu tumeoana ananiambia imetoka hata sijui ukimwi nimeponaje 

Mama akaniambia Leo utalala hapa mpaka Nancy akuje akija tutaongea 

Nikashinda kwa mama siku 2 sijapata simu wala sms toka kwa Nancy, nikajua tu yupo anachepuka 

Mama akaita kikao cha familia baadae akamdanganya Nancy aje ampeleke hospital maana anajiskia vibaya, Nancy kufika anaona wanafamilia wamejaa, na yule mama alienipeleka hospital alikuwepo akafichwa ndani, wazazi wa Nancy pia walikuwepo

Nancy akasomewa risala na baba Mkubwa akakataa, sio kweli anakataa, yule mama akaitwa akaeleza mkanda mzima, akatoa na vithibitishi kumbe zile siku 2 nililala kwa mama Nancy alikuwa na mume wa huyo mama

Nancy la Kusema hana

Mwanasheria alikuwa ameletwa ameshaandaa na talaka nikasaini talaka nikamwachia nyumba tulionunua tukawa tunaishi akae nayo mimi nitahamia nyumbani 


Wazazi wa Nancy nao wakaja juu, mnamnyanyapaa mtoto etu kwasababu ni mwathirika mnataka kumuacha, basi kwa ubinaadam nikakubali kuishi nyumba na Nancy, lakini hatulali chumba kimoja 

Tukaishi namna hio kwa miaka 3, yeye anaugua kivyake mimi nipo kivyangu,  chakula nakula kwa mam, kila kitu ni kwa mama, Nancy akitoa mchango wa Mawazo wa maendeleo namwambia ngoja kwanza mama akikubali tutafanya basi tu namkera na kumkaraisha 

Maisha yakaendelea namna hio mpaka mama yake Nancy akahamia pale nyumbani maana Nancy alikuwa anaumwa akawa anamhudumia mimi sikuhangaika 

Mama mkwe akamwuguza mwanae miezi 6 akahamia kwake akamwuguza miezi 6 mbele Nancy akafariki

Ikawa mwisho wa habari, na ile nyumba nikampatia mama yake mzazi afanye anachotaka

Sasa hivi naishi kwangu, mwaka wa 35, ndoa ilivunjika miaka 3 iliopita ndoa ilikaa miezi 8 tu kugundua Nancy anaukimwi tukaachana 

Nimekuwa singo kwa miaka 3 sasa, sina hamu na mwanamke nahisi sipo sawa nahisi nimekufa kimwili na kiroho, nipo nipo tu ndio maana nimekuja kwako kutafuta msaada naona kama sipo sawa dokta 

Mwanasaikolojia: ulishawahi kumtafuta Tereza? ! Ukaambiwaje?

Masumbuko: nilimfuatilia nikaambiwa anafanya kazi Kampuni ya simu ila ameolewa yupo na bwana wake
Alafu kuna siku nimekutana nae supa maketi nikamsalimia tukaongea sana nikamwuliza vp kuhusu ndoa watoto akalia hapo hapo, nikamtoa mahali pale nikampeleka mgahawani, akanieleza jinsi gani alivyokuwa abused 

Ndipo nilipojua kuwa Nancy hakuwahi kumweleza Tereza juu ya penzi langu kwake

Tukabadilishana namba za simu lkn ile namba sasa nikiipiga haipo kabisa, haipo hewani dah sijui

Na ile Kampuni ya simu nilienda nikaambiwa alihamishiwa mkoa ah basi bwana huenda sio riziki 

Mwanasaikolojia: akabakia ameshangaa, kweli Mungu ndio anapanga mambo yote, kama ni wako atakuja tu kwako hata wakimwiba atakuja tu kwako 




Tuonane Kesh tar 5 July 2018 saa 1 usiku ya Tanzania
_________________________________________________

E. NIPO SINGO KWASABABU BADO SIJAPONA

 

Mwanasaikolojia: nikaongea na Masumbuko nikamwelewesha na kumsaidia na kumtia moyo kuwa asonge mbele maisha yako hata kama hakumpata Teresa  Mungu atampa mke mwingine watakaependana 

Tukaongea kama Lisa Limoja namtia moyo namsomea vifungu vya dini, namwelewesha mpaka akaonekana kukaa sawa

Muda wa Darasa la wengine likawadia nikamshauri akae na wenzake wafahamiane najua atajifunza kitu toka kwao

Muda wa Darasa la pili ukawadia wakaingia ndani na makelele na mafujo kama kawaida yao wameshazoeana 

Safari ya uponyaji wa usongo wa mawazo haijawahi kuwa rahisi lakini hawa vijana wamejitahidi sana ndani ya miezi 3 wameonekana kupona haraka 

Lakini Calvin hakuonekana na furaha,  yani ni stori ndefu ngoja umsikilize mwenyewe 

Baada ya salamu nyingi na kuongea kila mtu alitaka kuongea hata Simon hata Mr Piggy lakini nikaamua kumpa nafasi Shaibu tumsikie anaendeleaje

Shaibu:
Dokta huezi amini skuile tulirudi hapa tukaachana nikatoka out na yule mrembo, usiku huo huo tukarudi gheto kwangu nikasimamisha show, mechi kwa mara ya Kwanzaa nimetembea na mwanamke

Wenzake: wakamshangilia oyooo nakwamboa Calvin anafurahi Darasa lake kwa Shaibu limefanya kazi mara wamtanie tunakuona bikra wa kiume umeivunja ukubwani ukiwa na miaka 35

Mwanasaikolojia: hahaha ha ulijiskiaje Boss?!

Shaibu: hauwezi kuamini ni kweli yule demu alinibikiri lakini sikupenda nilikuwa naona ajabu, ah labda sikunyingine 

Wote: du na minong'ono mingi

Mwanasaikolojia: kwahiyo mtaonana na huyo binti tena? !

Shaibu: alishinda kwangu mpaka Leo asbh wakati naenda kwenye shughuli zangu nikamshusha kwake ila mmh sijampenda 

Calvin: hujapenda huduma yake au hujapenda alivyo? !

Shaibu: sijampenda 

Mwanasaikolojia: usijali Shaibu Mungu atakupa mwanaume mwingine utakaempenda, maisha ni safari usifosi siku yako itakuja

Mr Piggy: sasa huyu dada akija kwako tena utamfanyaje?!

Shaibu: doh sidhani kama nitamfungulia 

Calvin: sikunyingine usipeleke mademu kwako chukua chumba mtaani mkayamalize huku kubeba akina mama kwako kesho atahamia na kwako mwisho wa siku anabeba mimba yako mnaishia kuoana hamjapendana mnakaa kwenye ndoa kwa ajili ya watoto, huo mchezo usifanye tena chief, achana nao kabisa

Shaibu: asante boss

Mwanasaikolojia: ni kweli Shaibu kama hauna uhakika na hisia zako juu ya mwanamke hasa uliemchukua tu barabarani humjui usimpeleke kwako kabisa, mtaani yaishe juu kwa juu mpaka uone kama umempenda au la

Shaibu: sawa Dokta nashukuru

Mwanasaikolojia: sawa Bikra wa zamani, naamini utaufanyia kazi ushauri, enhe mwingine nani au Shaibu Bado haujamaliza?!

Shaibu: nimemaliza Dokta asante

Simon: Dokta me nashukuru naendelea vizuri

Skuile wale mademu walikuwa wananihurumia sana kama mama zangu nikajiona kama sio mwanaume nahurumiwa tu ah inaboa! 

Bora nikatengenezeshe mguu bandia yaishe 

Calvin: kwahiyo ukawaacha waende zao?!

Simon: ah wa nini sasa?!

Calvin: dah kaka umechezea shilingi chooni kaka

Wote: wakacheka 

Calvin: ningepewa mimi hao mademu pangewaka moto 
Yani hamna wakati wa kumla mwanamke kama pale anapokuhurumia... hapo hapo unakamatia fursa na unamwomba namba yake kabisa skunyingine upo upo unamwita unamla tena oh hizi neema Dokta kwanini hazitukutagi?! Zinawakuta watu hawajui kuzitumia

Mwanasaikolojia: hahahaha, aya Calvin tumekusikia usimfanye Simon wangu ajiskie vibaya, Simon mwaya usijiskie vibaya, hicho ulichokifanya ni sawa, umewaachia wale mabinti somo watakutafuta tena baadae umetenda kama Gentlemen yeyote humu duniani utaniambia ukimpata utakaempenda utamheshimu na kumtunza 

Simon: sawa dokta





Mwanasaikolojia: Frederick vepe!? Na wewe ulitumbukia na kimwana majuzi mmefikia wapi?!

Fredrick: madam Acha tu, yule mwanamke nilienda nae kwa lodge tukayamaliza, tulikesha usiku mzima simu zikawa zinapigwa walijua nimepotea ikabidi niongee na mjomba kikubwa akanielewa 

Asbh natoka nikakutana nae ananisubiria nje ya lodge akatuchukua kwenye gari akamshusha yule mama akamwambia mwanangu anaumwa nimemkuja kumchukua twende hospital akaamini 

Tukarudi nyumbani hakugomba hakunisema aliniuliza tu umetumia condom nikamwambia ndio akaondoka zake 

Hio ndio iliokuwa siku yangu... sikwenda kanisani kabisa jana na leo nimeamkia hapa lakini yule mrembo tunaongea tu kwenye simu tunachat tu

Mwanasaikolojia: nimefurahi Fredrick, kwahiyo Mary na Huyu mrembo mpya nani Zaidi?!

Fredrick: Bado nafikiria unajua Mary sijamjua kabisa

Mwanasaikolojia: basi sawa lakini usifosi mapenzi hayafosiwi na usiokote tena wanawake barabarani ukijaribisha mapenzi, mapenzi ya kweli yanakuja tu bila hata kutembea na mwanaume unashangaa unampenda tu mwanamke na hauna haraka ya kutembea nae hata miezi 3...6 hata mwaka unaweza usimguse 

Wote: doh hataree dokta iyo zamani miaka ya sa hivi wiki tu ushamaliza kila kitu!

Mwanasaikolojia: haya mwingine nani anataka kuongea?!

Dula: mimi hapa 
Dokta najua nilizama na demu wa beach, lakini hayo uliomweleza Fredrick kuhusu mapenzi ya kweli yalinikuta jumamosi,

Si nikaondoka na yule demu kumchukua chumba mambo yakaenda tulipoanza kuzama mechini nikawa naona sura ya Aminata 

Wote: Aminata? ! Kakulogaa 

Mr Piggy: huyu Aminata ulishatembea nae?!

Dula: ndio,

Wote: oh ushaharibu 

Mwanasaikolojia: bwana mwacheni Dula aongee msimpangie, kwahiyo ukafanyaje sasa?

Dula, kila nikijaribu kwenda mbele nashindwa, nikitaka kwenda mbele nashindwa, eh nikaahirisha na nanilii akalala 

Wote: ahahahahaha kazi  kweli kweli

Dula; nikamwomba msamaha yule dada nikatoka nikakimbia nimemwacha ananishangaa yupo utupu 

Sijamwona tena yule dada 

Calvin: ulimwona nani tena, Aminata au?!

Dula: jana asbh Aminata akanitumia sms ananisalimia nikampigia tuonane nikaenda kwake kumuona hatukuwa na cha kuongea ni moja kwa moja mechini tena peku 

Wote: dooooooh! Aminata Kakulogaa ahahahahahah wakawa wanamcheka Dula 

Mwanasaikoloji: haya jaman yaishe tumeshajua kuwa Dula anampenda Aminata, hongera sana Dula kwa kufanya uamuzi sahihi

Dula: asante Dokta 

Mwanasaikolojia: mwingine nani au Dula Bado haujaliza?!

Dula: nimemaliza dokta 

Calvin: madam niongee au?!

Mwanasaikolojia: mmmh aya ongea Calvin umeniudhi sana lakini umeanza vizuri unaharibu mwishoni

Calvin: dokta mimi sijaharibu kitu, unajua kimetokea nini jaman,  skuile tulitoka na viwana usiku ule ule mimi na yule demu tukazama club mziki tukachezaa weee baadae nikaenda kuchukua vinywaji nikamwacha amekaa anajisubiria

Wote: enhe ikawaje?!

Calvin: kurudi namkuta yule demu anacheza kimahaba na mwanaume mwingine tena wana kiss, doh nilichanganyikiwa nikamfuata yule jamaa namuachanisha na yule demu wangu lakini akawa hataki, nikamwuliza yule demu vp tena mbona uko na jamaa mwingine yule jamaa akaingilia kati, ndio kuzozana tukapigana, pigana pigana na wewe wakaja ma bouncer kutuachanisha nikawekwa chumba flani nisubirie mapolisi waje 

Wakati nasubiria naona meneja wa club anaingia na dokta hapa, nikashangaa imekuwaje

Mwanasaikolojia: nilikuwa naenda mziki sikujua kama Calvin yupo pale kufika naona Calvin anapigana na kwenye report yako Calvin hutakiwi kabisa kufanya fujo nchini la sivyo unajua kitakachokupata! Umesahau au?!

Calvin: ndio nakumbuka 

Mwanasaikoloji: nikaachana na marafiki zangu nikaenda kuongea na Meneja kuwa namjua huyu ni mdogowangu, uzuri Meneja wa Club namfahamu miaka mingi akaniachia ndio tukaja kumtoa Calvin 

Nikamrudisha kwa wazazi wake ikabidi niongee nae, kwanza nashangaa hata leo umekuja nilijua utaacha darasa

Calvin: siachi madam labda uniachishe ila ulinisevu sana ningekuwa jela sasa hivi doh asante Madam 

Mwanasaikolojia: yule msichana mmewasiliana tena au?

Calvin: sijawasiliana nae kabisa wala sina namba yake

Mwanasaikoloji: ukipigana tena mtaani au mziki itakula kwako uache,  kifupi maishani mwako punguza fujo na kupigana, vurugu hazijengi zinabomoa

Calvin: sawa dokta nashukuru 

Tuonane Tar 7 July 2018 saa 8 Mchana ya Tanzania
_________________________________________________

F. NIPO SINGO KWASABABU NDIO NAANZA KUJIELEWA

Mwanasaikolojia: okay! Haya anaefuata nadhani atakuwa ni Mr Piggy

Mr Piggy: ah hapana asee mbona dogo hapana hajaongea

Mwanasaikolojia: huyo nimeshamalizana nae ash nimemwalika afahamiane nanyi baaas
Leo hatoongea labda sikunyingine

Pia nataka nimweke kwenye grup la akina Simon na wewe Mr Piggy

Naomba msimfundishe vbaya amepitia maisha magumu sana nataka awe rafkienu

Mr piggy& Simon: sawa madam hamna neno tutamlinda kijana wako

Mwanasaikolojia: haya Mr Piggy tufungie darasa tafadhali, yalikupata yapi tangu tumeachana?!

Mr Piggy: tulipoachana nikapata vimwana 2 mmoja anaitwa Sarah mwingine Delia

Sarah anaonekana mambo mengi siku hio hio tumeonana nimeshamla doh aibu! Alafu anajirahisi sana kwahiyo nimempotezea nimemtupa kule

Ila selina ndio naanza kumwelewa
Kwanza hana haraka na kulala na mimi, pili hana papara mtoto mzuri Selina amefundwa kwao

Mwanasaikolojia: oh afadhali,  now umeshampata mkali wako Selina hongera

Mr Piggy: mmh dokta sijamaliza, Selina bwana sijui kwanini kila tukikutana kwenda kula tukiwa tunaongea nakuwa naona sura ya KoKu

Wote: eh KoKu keshakuloga!

Mr Piggy: yani kama kuna kulogwa basi mimi Koku ameniloga, True love siamini kabisa

Basi tukachukuana sikuhio mpaka kwa Selina namshusha nirudi nyumbani akanikaribisha ndani kwake kumbe anaishi mwenyewe  doh!

Calvin: brother brother! Nalipenda movie lako linavyoendelea, tupe habari baba tukalale sie

Wote: aakacheka

Mr Piggy: hahahaah Calvin Bwana; basi kufika kwake tukaanza show za mwanzoni mwanzoni

Eh lakini hauamini, namwona tu KoKu dah ikanisumbua usiku mzima nikashindwa kumpiga mechi Selina kabisa huyu mhaya sijui kanilogaje usiku huo huo nikarudi kwangu

Leo asbh nimeamka naskia mtu anagonga kuangalia ni Selina amefuata mrejesho wa jana, tukazama kitandani doh hamna kitu, NI KoKu mtupu naona kama namsaliti

Shaibu: nyie haya mambo mnasema kweli au?!mimi mbona haijawahi kunitokea?!

Calvin: haujawahi kupenda kaka, haujawahi kumweka mtu moyoni Alafu ukampotezea kumbe unampenda mbaya

Me Piggy: basi nikamwomba radhi Selina haelewi kwanini namfanyia vituko, nikamweleza ukweli nipp na demu wangu anaitwa KoKu nahisi bado nampenda

Selina akalia maskini nadhani alijua mimi na yeye tutaenda mbele lakini imeshindikana

Nikamshukuru kwa kuwa mvumilivu, nikamkatia pochi kama milion 1 akaondoka ndio nimekuja Darasani

Mwanasaikolojia: pole sana Mr Piggy na hongera kwa kuwa mkweli kwa Selina, sasa utafanyaje na KoKu? !

Mr Piggy: nataka nikaongee nae Leo nikitoka hapa nadhani atanielewa asiponielewa basi

Mwanasaikolojia: nakushauri ukae kwanza siku 3 ndio umtafute, ili uwaze vizuri juu ya hisia zako kwa KoKu,

Mr Piggy: sawa Dokta

Mwanasaikolojia: haya naona leo darasa litakuwa limeishia hapa tutaonana tena keshokutwa, tunarudi tena kwenye ratiba yetu ya j3, j5 na ijumaa muda ule ule saa 5 asbh mpaka saa 8 mchana

Basi wakasalimiana pale wakatawanyika

Wiki hio darasa likaendelea kama kawiada yetu, ilipofika jumatano nikawatangazia hukusu safari ya Zanzibar ya jumamosi kwa wale ambao wanatakiwa kuomba ruhusa na waombe ruhusa

Wakafurahi kweli safari hii wanaenda Zanzibar lakini hawakujua kuwa Zanzibar watakutana na akina nani

Ila Mr Piggy alisema hakumfuata Koku, aliogopa maana KoKu nae mkali sana

Ijumaaa jioni nikawa buzy ofisini nafuatilia safari ya kesho ya Zanzibar, na kuweka mambo sawa mara Secretary wangu ananiambia kuna watu wanataka kuja kuonana na wewe nikauliza ni nani akasema kuna mteja wako basi nikamwambia aingie

Kuingia eh kumbe ni Rebecca kaja na mzungu doh kweli hii surprise

Nikawakaribisha tukasalimiana huku wanaketi mzungu anatema English kama maji
Tukaongea kama nusu saa wakaniambia kuna kitu wangependa  kunishirikisha kabla ya kesho safari ya Zanzibar

Rebecca akanyoosha mkono wake wa kushoto ananionyesha ona,  kuangalia bonge la pete inawakaje,

Rebecca: ni 20 Karat Diamond Ring, amenivisha leo asubuhi nikiwa naamka nikaikuta mkononi, sikuamini na yeye alikuwa jikoni,  nataka kutoka jikoni akaja na breakfast ameniletea ikabidi nirudi kukaa kitandani namwuliza vipi akapiga magoti baada ya kuweka trei lililokuwa na chai akasema

Mr Johnson: you are a very special woman, I couldn't stop thinking about you ever since you left Turkey,  you are everything I ever wanted and prayed for, am so happy that God brought you in my life, I love you, will you Marry me?!

Rebecca: Yes of course I will marry you! And the rest is history

Mwanasaikolojia: wow! Congratulations to both of you! Nikainuka kuwakumbatia, finally Rebecca wangu amepata wa kumpenda

Tukaongea sana na safari ya kesho wakaomba niongeze chumba maana Johnson nae anataka kwenda ndio maana wamekuja mapema

Nikafurahi nao na kwa ajili yao nikawauliza harusi lini? !

Johnson: nilitaka ifanyike Zanzibar lakini Rebecca anasema kuna mila za kufuata na wazazi wa kuwaheshimu kwahiyo nitasubiri

Rebecca: wazazi wangu unawajua dokta walivyo, nikiolewa juu juu haitakuwa poa, tukitoka hapa nataka nikawatambulishe kwao lakini nashindwa nikiingia nyumbani leo safari kesho nisahau tu

Mwanasaikolojia: my dia subiri urudi toka Zanzibar, Alafu tutapanga kwenda kwa wazazi kuwaeleza kwa sasa hapana na wala usimweleze mtu kwanza wa familia labda mpaka kesho utawaeleza

Tukaongea kama dk 20 wakasema wanaondoka wakapaki na kujiandaa na Kesho

Rebecca alikuwa na furaha kweli Mungu yupo jomoni! Rebecca wa miaka 32 anaolewa kama mchezo

Nikarudi kuendelea na kazi zangu na kuongeza vyumba kwenye hotel niliopanga kwenda na watu wangu Wote mara naskia tena hodi

Kuangalia ni Dula

Mwanasaikolojia: eh! Dula, karibu umesahau kitu tena boss?

Dula: hapana nimekuja kuongea na wewe kuhusu kitu flan
Akafunga mlango akaa kwenye kiti

Mwanasaikolojia: nambie boss shwari lakini?!

Dula: shwari
Kuna kitu nataka kukueleza kuhusu kesho

Mwanasaikolojia: vp tena umepata dharura au?!

Dula: nooo hapana, dokta najua tumeongea leo mambo mengi lakini sikutaka kuweka ya kwangu hewani labda mpaka kesho

Mwanasaikolojia: mambo gani haukutaka kuweka hewani tena Dula na wewe!

Dula: jana alhamisi nilimfuata Aminata baada ya kuelezea somo la mapenzi ya kweli nikagundua kweli nampenda Aminata

Mwanasaikolojia: doh! Enhe!

Dula: nikampigia simu Aminata nataka kuonana nae akakubali tuonane nae hotel karibu na ofisini kwake nikamwelezea kuhusu hisia zangu kwake akawa anacheka tu nikajua nimeharibu kumbe alishajua muda kuwa nampenda na yeye anampenda pia lakini sasa anaona haitawezekana kwa kuwa ana wiki 2 tu kukaa Tanzania
Amepewa nafasi ya kwenda kufanya kazi Africa kusini, kufanya kozi na kufanya kazi kwa muda wa miaka 3 haitawezekana

Dula: nikanyong'onyea nikajiona sina bahati mtoto wa watu, dah akili ikawa haizunguki imeganda ananiuliza maswali nimeduwaa kweli Aminata ndio nampoteza

Mwanasaikolojia: doh sasa ukafanyaje?

Dula: pale pale nikainama chini nikamwomba nimuoe

Mwanasaikolojia: eh?! Lini hii imetokea boss?

Dula: jana usiku

Mwanasaikolojia: Aminata akasemaje sasa? !

Dula: akakubali

Mwanasaikolojia: weuweee Dula Dula my brother! Dula umetisher sana!  Alafu sasa itakuwaje?
Harusi lini?!

Dula: ataenda Africa kusini na mimi nilimfuata baadae

Mwanasaikolojia: kwahiyo mtaoana lini sasa?!

Dula: tukitoka Zanzibar

Mwanasaikolojia: eh?! Wacha wee amejua unaenda Zanzibar kufanyaje?

Dula: nimemweleza kuhusu wewe akaniambia na yeye anakuwa kwa darasa lako, Tukaongea sana sana sana nikashangaa siku zote hizi kumbe unamjua Aminata mbona hukuniambia madam?!

Mwanasaikolojia: Tanzania yetu ina wadada Aminata maelfu kwa maelfu ningejuaje kama ndio huyu?!

Dula: najua ndio maana nimemleta nijue kama ndio huyu wa kwako,  akatoka nje akaingia ndani na Aminata yule yule mwananfunzi wangu nikacheka sana sana sana loh nyie watoto mmenishinda tabia

Tukaongea sana wakanieleza kila kitu kuhusu walipokutana mpaka kuja hapa leo wakaniomba niwatafutie chumba cha pekeyao ndio maana wamekuja leo

Wakasema wakiwa Zanzibar watawaeleza kila mtu kuhusu mahusiano yao

Mwanasaikolojia: nikawakubalia wakaondoka wakiwa wamefurahi wakitazamia safari ya Zanzibar Kesho

 

Nikarudi tena kazini kuwasiliana tena na hotel ya Zanzibar na kuomba upya chumba kingine 

Nilipomaliza nikasikia tena hodi doh nikatamani wasiwe wanafunzi wangu awe ni dereva amekuja kunichukua maana imeshakuwa usiku sana muda umesonga 

Kufungua ni Koku anafuraha... nikamfungulia kumkaribisha na kumsikiliza 

Koku akaniambia ana ujauzito, wa Mr William

Sikuamini, nikamweleza kama ameongea nae akasema hapana mara ya mwisho alienda kumfuata kumweleza akakuta yupo mwanamke kwake kama wana do!

Mwanasaikolojia: kweli darasa limeingia mafuriko upande mmoja upande mwingine jua linawaka 

Tukaongea sana na Koku tukahesabu miezi aliotembea na Mr William mpaka mimba inaonekana ni sawa

Nikamwuliza kama hajachakachua akasema ndio dokta me sijachakachua nasema ukweli

nikamwambia kama ataweza anipe namba ya Mr William nimpigie aje pale amweleze kieleweke 

Akanipa nikampigia akakubali kuja baada ya Lisa limoja, nikamficha Koku kwanza ili niongee na Mr William nijielezee 

Kweli baada ya Lisa Li 1 Mr William akaja nikaongea nae akashangaa sana namjuaje Koku 

Nikamwita Koku akatoka akasema kweli Koku ndio huyu namfaham lkn amenifahamuje 

Koku akamweleza kuwa anafanya Darasa na mimi akamweleza kila kitu Mr William akaamini 

Nikamwambia Koku mimi namfahamu huyu kaka kama Mr Piggy hilo la William umelitoa wap? !

Mr Piggy: jina langu la kwanza ni William na la mwisho ni Piggy ila maarufu sana ni William ndio maana sijataka kulitumia hapa

Akaanza kumlaumu Koku kwanini ameleta kesi kwangu kwanini asingemfuata mwenyewe nyumbani akamwambia

Koku akamweleza kila kitu Mr Piggy akazodoka 

Mwanasaikolojia: nikatoa kipimo cha kupimia mimba nikamwambia Mr Piggy ampime Koku tusubirie majibu wote wa 3 wakafanya hivyo

Baada ya muda kweli kipimo kinaonyesha Koku mjamzito, doh Mr Piggy alifurahije sijawahi mwona Mr Piggy akicheka maana kila siku yupo na uso wa Mbuzi

Anafuraha anasema siamini naenda kuwa baba jaman doh!

Wakakumbatiana na Koku hapo wee malavi davi kwenda mbele hata hawanionei haya 

Walipomaliza nikawauliza je kesho mtaenda Zanzibar au ndio mnalea mimba?!

Wakajibu kwa pamoja: ndio tutaenda Zanzibar tuwaeleze marafiki zetu wote kuhusu mahusiano yetu lakini tutahitaji chumba cha pekeyetu madam 

Wakaondoka wamekumbatiana sijawahi kumwona Koku akiwa mwenye furaha kama sikuile 

Nikarudi kupiga simu tena kwenye ile hotel kuomba waongeze chumba kingine cha watu wawili 

Huku nacheka maana sielewi safari ya Zanzibar itakuwaje kesho!




Tuonane Tar 9 July 2018 saa 2 usiku ya Tanzania kuona Sehemu ya 5 na ya mwisho ya Nani amebakia kuwa singo!
_________________________________________________

SEHEMU YA 5

A. ZANZIBAR NA MIUJIZA YAKE



Zanzibar Zanzibar kisiwa kilichounga Tanganyika kuwa Tanzania

Tukadondoka Zanzibar au wabongo wanaita Zenji

Nilienda na rafiki yangu kipenzi tumefahamiana Tangu utotoni tumeishi wote Upanga best yangu kinyama 

Kufika Zanzibar hotelini alfajiri maana sisi ndio waratibu safari, saa 7 mchana tukaonana kwa hotel wote kula 

Koku, Mwelu, Tereza, Kuluthum, Rebecca, Aminata, Fredrick, Shaibu, Simon, Masumbuko, Calvin, Dula & Mr Piggy

Watu Peeeeeeeepooooooo hadi raha meza kubwa tunakula tunafurahi 

Wasaidizi wangu wa kazi walikuwa pembeni wamekaa walikuwa 7

Mr Johnson hakuwepo maana tulitaka iwe surprise kwa watu wote 

Koku na Mr Piggy kama hawajuani,

Wasichana wanashangaa hawa wanaume akina nani maana hawajawahi kukutana nao na wanashangaa kwanini wapo pale 

Nikatoa utambulisho wa Nguvu, kwa wote wanaume na wanawake na Wasaidizi wangu wa kazi, lakini rafiki yangu kipenzi hakutaka kuwepo alilala tu na kula chumbani 

Tukaweka ratiba ya usiku na kesho asbh na mchana na usiku

Kutembelea na kuizunguka Zanzibar 

Usiku kukawa na "Bon fire" dah kiswahili chake sasa, ni ule moto wa kuni nyingi unaowekwa nje alafu watu wanakaa pembeni yake wanapunga upepo wa baharini, wanakula wanakunywa wanacheza 

Baada ya msosi kukawa hamna kitu cha kufanya kila mmoja akarudi chumbani kwake

Wasichana waliobaki walikuwa na chumba chao maajabu ni kwamba Koku hakurudi kwenye chumba nilichowapa na Mr Piggy, Rebecca pia kwahiyo hakukuwa na mtu aliejua 

Mimi Nikarudi kulala chumbani kwangu nipo na rafiki yangu kuja kushtuka saa 12 jioni, Bon fire inaanza saa 2 usiku, tukajiandaa fasta fasta rafiki akaniuliza kama ni sawa yeye kuhudhuria maana hawamjui 

Nikampa maelezo kwa ufupi kuhusu Watu wangu wa nguvu akawa anacheka tu



Bon fire tukajongea

Nikajitahidi sana kutumia sauti kubwa si unajua tena me na sauti ndogo kama sisimizi

Tukatambulishana upya kama kawaida wanaume kwa utani wao

Wanaume:
Dokta umetukusanya na warembo unataka tuanguke dhambini,

Mwanasaikolojia: nikacheka sana, asee hamna mtu kuhanguka dhambini hapa, alafu ujinga wa kutokomea na watoto wa watu kwenye giza spend

Nyie wanawake mjiheshimu, hawa wanaume hawana hela mkienda nao mjue mmeangukia pua

Na Nyie wanaume hawa wanawake wanaukimwi mtakuwa mmeangukia uso sio pua

Wanaume: ukimwi si kama Malaria madam kwan Tsh ngap? ! Tutatibia tu ugonjwa huo

Rafiki yangu: anacheeeka huku anakunywa juice yake

Calvin: Dokta huyo mrembo uliokaa nae hapo anacheka ni nani?!

Mwanasaikolojia: mdogowangu

Calvin: hana jina?!

Mwanasaikolojia: hana labda umbatize

Rafkiangu huyu jaman, wa miaka yote tumeshibana kuliko maelezi sijui ajitambulishe au nimtambulishie?!

Wanaume: ajitambulishe tumtathmini

Wanawake: ajitambulishe jomoon

Mwanasaikolojia: haya mama jitambulishe

Rafkiangu: za jioni mabibi na mabwana

Wote: nzuri, poa mrembo

Shaibu: samahani mrembo umeolewa au up singo? ! Nimekupenda ghafla

Rafkiangu: hahahahah jaman Nyie asanteni
Kwa jina naitwa Money Penny

Calvin: ah mtoto Penny huyoo jaman nan yupo singo me nataka kumchukua jumla, aliebakia singo anyooshe mikono juu

Wakanyoosha wanaume Wote hadi mzungu wa Rebecca sijui alielewa au alinyoosha kwasababu wanaume wenzie walinyoosha mana alinyoosha mwishoni

Money penny: asanteni wapendwa wangu, nawapenda wote... ila mimi ni mama watoto 3 na mume mmoja wa ndoa ya Kanisani Lutheran, ndoa ya miaka 15.

Calvin: doh we umekomaa lkn unauhakika hauchakachui?!

Money Penny: nina michepuko 10,000 sasa sioni wapi nitakuweka mchumbaangu Calvin

Wanawake: wakamcheka sana Calvin

Money Penny: haya ni hayo tu kwa Leo nimefurahi kuwafahamu ingawa siwajui majina zaidi ya Calvin ila Nimekupenda huyo kaka hapo pembeni

Calvin: nani? ! Huyu Shaibu? !

Wanaume: aaah Shaibu weee mrembo amekuelewa mbaya changamkia fursa ya majimama

Money Penny: Shaibu njoo tukae Wote huku zanzibar mchumbaangu atakuwa Shaibu sitaki maneno

Wanaume: ooooh! Ahahahahahaha Shaibu weee Shaibu umeopoa Cougar!

Shaibu akainuka akaenda kukaa na Money penny pembeni

Money Penny: nimefurahi kukuona Piggy, miaka mingi sijakuona

Mr Piggy: me too, akainuka akaenda kumkumbatia Money Penny

Wote: wanashangaa

Koku: mmejuanajae na huyu mama sasa?!

Mwanasaikoloji: anacheka mbavu hana

Mr Piggy: ni Rafkiangu wa miaka mingi,  alikuwaga mchumbaangu zamani ila mumewe akaniwahi, doh umenikumbusha mbali, sikujua unafahamiana na Mwanasaikolojia hapa, nisingechukua darasa kwake

Mwanasaikolojia: kumbe huyu ndio mchumba wa miaka 25 iliopita sikujua! Ahahahaha

MR Piggy: ndio huyu bwana alinifanya nisitamani tena mwanamke mwingine!

Wote: wakacheka kasoro Koku kama hajaskia vile!

Mwanasaikolojia: akamtambulisha Money Penny kwa wanawake na wanaume Wote waliobaki alafu akamtambulisha kipekee Mzungu Johnson akamwita mbele akamtambulisha kwa kila mmoja kila mtu akiwa amekaa anasikiliza

Baada ya utambulisho ndio wanawake wanashtuka mara wakaanza kupiga makelele  wanamshangilia Rebecca wanaume sasa hawaelewi

Mwanasaikolojia: Baada ya kutuliza fujo za akina dada

Akamtambulisha Rebecca kwa watu Wote akatangaza kuwa watafunga ndoa hivi karibuni

Doh hio fujo na mikelele sasa mzungu wa watu alikumbatiwa mpaka akaanguka chini

Nikamsogeza Rebecca pembeni maana sio kwa fujo zile mara waimbe mara wamchumu mashavuni wamtanie shemeji shemeji fujo kwa kwenda mbele si unajua tena wadada wa kibongo walivyo!

Baada ya Muda Mr Johnson akaenda kukaa na Rebecca wake wamekumbatiana, shilawadu wanapiga picha what a cute couple! Finally Rebecca amepata Bwana na hayupo singo tena

Mwanasaikolojia: baadae nikamnyanyua Mr Piggy nikamleta mbele nikamkumbatia kiuno, nikawatania huyu ndio ananioa mimi

Wanaume: ah madam Acha ujinga

Mwanasaikolojia: nikacheka pale Baadae nikamwelezea Mr Piggy kwa wanawake kuwa ndio Mr William

Wanawake: walipiga makelele doh wakambeba Koku juu juu wakamleta mbele dah wanaume wanashangaa Leo kuna nini? !

Mwanasaikolojia: nikawatangazia kuwa Koku ana ujauzito wa mwezi mmoja wa Mr William Piggy na tukitoka hapa anaenda kutoa mahari kwa akina Koku

Wote: wakashangilia nakwambia fujooo wanawake wa kibongo wana makelele doh utadhani wanazaa leba hio mifujo sasa eh Money Penny anawashangaa mdomo wazi hawa mademu vepee?!

Baada ya zile fujo tukatulia Wote maana hakukuwa na wapendanao wengine waliotangazwa

Baada ya fujo kuisha Money penny akawafuata Me Piggy na Koku akawakukbatia akawaponyeza, anamwambia Koku utulie huyu jamaa atatulia wewe ukitulia

Hongera sana Mr Piggy nimefurahi umepata barafu ya moyo wako

Tukala tukanywa tukacheza miziki yote, bongo fleva,  R&B, Gospel, Rumba, Chacha n.k wa kadhalika, watu walikula na kunywa mpaka, sikujua saa ngap Koku aliondoka na Mr Piggy,  wala Rebecca na Mzungu wake na wala sikujua saa ngapi watu Wote waliondokaje kurudi vyumba vyao lakini mimi niliondoka mwenyewe kufika chumbani namkuta Penny amelala

Tuonane kesho tar 12 July 2018 saa 1 jioni ya Tanzania
_________________________________________________

B. ZANZIBAR NA MAPENZI TELE



Kulipokucha tukakutana na warembo chumbani kwa warembo,
Nikawaamsha Baada ya kujiandaa huku tunakunywa breakfast chumbani, akaingia Koku, kama mkimbizi kaja na kichupi na kitopu 

Mara akaja Rebecca wote wakampigia makofi

Nikauliza Tereza leo kaenda wapi?!

Kila mtu anaangaliana hawajui, basi tukaendelea na kipindi chetu maana kila mtu alikuwa anataka kuongea

Mara tunamwona Kulthum anaingia, kila mtu anashangaa 

Mwanasaikolojia: haya mama wewe umetokea wap?!

Kulthun: my dia long story

Wote: wakamwangalia na kumwambia tunasuburia

Kulthum: jana wakati tunacheza mziki pale nikamwona Frederick amekaa kaa tu kihasara nikaenda kumsalimia, mmmh Frederick ni noma, 

Rebecca: kafanyaje mama?!

Kulthum: tumeongea nikamwambia nifuate, akanifuata tukatokomea huko pembezoni mwa bahari, tukazama kwenye mahaba ya nguvu, Frederick yule dah sijawahi kukutana na dizaini yake, mtu anachemka kama ametoka kuchemshwa jikoni! 

Koku: kama ana ukimwi je?

Kulthum: ajali kazini 

Wote: hahaha haha

Kulthum: usijali nilitembea na kinga

Mwanasaikolojia: ndio umechelewea baharini kama nguva umelala ufukweni au?!

Kulthum: ndio tumeshtuliwa na mlinzi aibuje

Koku: mkiwa watupu?!

Kulthum: tena ametuamsha kwa kuturushia nguo

Wote: tobaaa! 🙆🏼‍♂

Mwanasaikolojia: kwahiyo itakuwaje sasa na huyu mwanaume?!

Kulthum: wala sina mpango nae!

Wote: abee? !

Kulthum: leo nataka niende na Shaibu!

Koku: Money Penny atakumaliza

Kulthu: hahahahaha 

Wakati tunacheka akaingia Tereza huku ananyata

Mwanasaikolojia: haya na wewe umetokea wap mama etu?!
Ulisahau Leo tunakikao au?!

Tereza: akaingia akakaa kimya 

Koku: kikao hakisogei mpaka useme ulitumbukia wap sie tunawasiwasi ndio tulikuwa tunajipanga tukakutafute

Tereza: mmmh me siwezi hata kuongea

Koku: nakurahisishia ulilala na nani jana maana hukulala hapa jana

Tereza: long story anger mwingine labda nitapata nguvu ya kuongea ngoja ninywe chai Kwanzaa

Koku: naona ulienae amekunyonya damu,  mpaka unakosa pumzi?! 😂😂😂

Koku akaelezea yake weee baadae akasema kama ataolewa ataomba wote tumsimamie harusi yake 

Tukafurahi doh harusi ya 2 tunacheza sasa 

Rebecca: nae akasema kitu chicho chicho, Koku ukiolewa Kwanzaa mimi nasimamia yako kama maid, na mimi nikiolewa kabla yako wewe usimamie kama maid pia na mumeo

Mwanasaikolojia: nani atakuwa matron wako wa ndoa Koku

Koku: nataka uniombee kwa shogako Penny anisimamie 

Mwanasaikolojia: ahahahaha wala usiende huko mama, usitake kufukua makaburi, yule ni mwenda wa zimu zaidi yako mamito anaweza akakukubalia siku ya harusi ukajikuta mwenyewe 

Koku; basi nitamwambia William atafute mwenyewe maana lazima awe ameolewa

Tukaongea kama kawaida yetu, Rebecca akaongea yake,

Mwelu: akaelezea kuwa jana alikuwa na muda mwingi na Calvin

Mwanasaikolojia: akachoka! CALVIN tena?

Mwelu: ndio tulikuwa tunaongelea kuhusu kilimo, wakaongea sana leo tena wataendelea 

Mwanasaikolojia: mmmh! Ila uwe mwangalifu na Calvin!

Koku: ana nini kwani?!

Mwanasaikolojia: ni kama wewe Koku, Ila hayupo hivyo tena Ila sijui nenda nae mdogo mdogo 

Mwelu: sawa dokta 

Aminata akaelezea jinsi gani amefurahi kuja Zanzibar na Dula, wame enjoy kweli kweli utadhani wapo Honey Moon, akaomba pia tushiriki kwenye shughuli yake ya harusi kikamilifu 

Wote: wakamkubalia 

Mwanasaikolojia: haya Mama Tereza upo tayar kuongea maana tu nataka kutoka kwenda kutembelea historical sites (makumbusho)

Tereza: jana nimekutana na rafiki yangu wa miaka mingi nilisomaga nae anaitwa Masumbuko 

Tukaongea wakati nyie mnacheza mziki, Tukaongea sana akaniambia kila kitu ambacho sikuwa na jua, sikujua kuwa alikuwa ananipenda na sikujua kama best yangu Nancy alinidhulum na amekufa na ukimwi 

Tumeongea sana mambo mengi, mengi na hakutegemea kunikuta pale 

Baada ya watu wote kuondoka tukaenda kukaa juu kule kibarazani tukalala hapo hapo tunaangalia bahari 

Koku: stori yako inatufundisha nini?!

Tereza: hamna kitu si mmesema niongee ndio tumeshtuka nikakimbilia hapa 

Koku: umeingia hapa saa 5 umeshikilia vista na nywele timutimu

Tereza: nimemaliza madam 

Mwanasaikolojia: tumpe muda Tereza ndio ameanza mapenzi bado anaushamba akikua ataongea tumsaidie 

Tukafunga kipindi kila mtu akajiandaa tukaenda kula lunch saa 8 wote tukazama makumbusho wote wanaume na wanawake basi raha mapicha sasa kupigana woi 

Kutoka huko saa 12 tukazama Forodhani kwenye mishkaki ya kuku, ilikuwa raha sana

Akina Dulla wakaanza kuimba na Shaibu, wote tukawa tunaitikia basi ni kula na kunywa na kuimba tu

Wakati tunaimba pamoja Mr William Piggy akatunyamazisha 

Tukamsikiliza akaongea hapo wee Mara akapiga goti akamshika mkono wa kushoto Koku, anaomba akubali amuoe, watu wote wanapiga picha Koku kaganda 

Kulthum akamfinya Koku we mama amka, eh akatuangalia wote alafu akamwangalia money penny 

Money Penny: me nishamtupa miaka 25 iliopita we nenda nae kwa baraka zote 

Ndio Koku akakubali,

Tukashangilia na wapiga picha wapo kazini watu wamejaaje wanashangaa hawa wabongo mafujo wamevamia Forodhani, 

Baada ya engagement tukaimba tukacheza huku tunawapongeza Akina Koku na Mr Piggy, wakiwa wenye furaha,

Mimi na Money Penny tumekaa pembeni tunawaangalia Akina Koku na Bwanake Piggy, namwuliza Penny hii safari ya Heri au maumivu?!

Money Penny: sasa hivi William ameshakuwa sidhani kama atakubali kuchezea shilling kwenye tundu la choo

Ila nawasiwasi na Koku, Koku ndio unaemjua wewe 

Kumbuka Mr Piggy ana boss wake ambae nahisi alikuwa na Koku, huyu jamaa ni mshenzi wa tabia atakubali William amuoe Koku?!

Alinifanyiaga mimi kitu mbaya sitasahau kama sio kumpata mume nilienae akampiga biti nadhani ningekuwa nimechanganyikiwa kama Koku, 

Mwanasaikolojia: nikamwangalia Money penny; nikawaangalia Koku na Mr piggy walikuokuwa wamekumbatiana kwa furaha 






Tuonane Kesho Tar 16 July 2018 saa 1 usiku ya Tz
_________________________________________________ 
C. NANI AMEBAKIA KUWA SINGO



Baada ya kuburudika na Forodhani, kesho yake tukaenda kuwaona watoto yatima 

Watu wanafurahi hasa Shaibu, tulikaa masaa 2 kwasababu ya Shaibu anataka awachukue siku hio hio, Kulthum nae mwenzake na Shaibu, wamekutana mpaka wanalia,

Tulipeleka mahitaji mengi sana watu walijitoaje hata sikutegemea kama watakuwa na ushirikiano mkubwa namna hii

Shaibu na Kulthum na maswali yao mengi, ikabidi tusubirie wapewe utaratibu dk zingine 45, tukamaliza tukaondoka 

Kufika hotelini kila mtu akawa buzy kupaki maana muda wa kurudi Dar ulikuwa umefika 

Tulipofika Dar tukaagana kwa taarifa ya kuwa tumebakisha madarasa 2 tu alafu kumaliza kozi 

Baada ya wiki moja kuisha, tukakutana na warembo Kwanzaa kila mtu alikuwa na cha kuongea
Ila nitaandika maelezo yao kwa ufupi maana so unajua tena wanawake

Kulthum:
Baada ya kuwaona watoto wale nikaamua toka moyoni kwenda kuomba niwalee watoto 2 wakike na kiume, nimekubaliwa kwahiyo weekend hii naenda kuwachukua, huwezi amini naenda kuwa mama sasa, mama watoto 2 mapacha! 

Wote: wakampigia makofi hongera sana

Kuluthum: nachotakiwa ni kupewa certificate yangu hapa na dokta kuwa nimemaliza masomo, niweze kuipeleka nikabidhiwe

Mwanasaikolojia: hongera sana Kulthum naamini upo strong enough kulea watoto mapacha ukiwalea vibaya unanyang'anywa mimi na kituo tutakufuatilia maana safari yako na mimi imeisha kwa kitambo kidogo tu..

Haya mwingine nani?!

Aminata:
Taratibu zote za ndoa zimekamilika, Dula ameshalipia mahari, ndoa ni wiki ijayo baada ya ndoa nasafiri kwenda kuanza maisha Afrika Kusini

Wote: wakamshangilia wengine wakamkumbatia basi full shangwe 

Mwanasaikolojia: Haya mwingine nani?!

Rebecca:
Nimeshalipiwa mahari wazazi wamemkubali Johnson, harusi yangu baada ya wiki 2, Wote lazima muwepo kasoro Aminata sijui utakuwepo 

Wote: wakamshangilia kama kawaida mafujo amaizing nini 

Mwelu:
Mimi bado nipo sing,  kwahiyo nitakuja kwenye sherehe zenu wote

Wote: usijali utapata Mungu mwema wanamtia moyo dah hataree 

Mwanasaikolojia: haina haraka Mwelu mambo mazuri huwapata Wote wanaosubiria. .. wakati wako utafika na utapata wa kukupenda kiasi cha kukufanya uwe mke wake

Haya mwingine nani najua mmebakia wawili

Tereza: 
Tangu tumetoka Zanzibar mimi na masumbuko tumekuwa watu wa karibu sana, tunatoka out tunaongea kiila siku, doh sijui huyu mwanaume alikuwa wapi, amekuwa kila kitu ambacho nimemwomba Mungu

Wote: wow hongera sana Tereza

Tereza: huwezi amini wiki iliopita amenitoa out  tulivyomaliza kula akapiga goti, akaomba anioe,  hakuwa na muda wa kupoteza maana amenisubiria miaka mingi na hajanipata na sasa amenipata hajaona kwanini akubali kunipoteza 
Nikakubali, sikujua ameita ndugu na wazazi wangu wakatokeza wanapiga makofi wengine wanachukua video doh nilishtuka 

Juzi ameenda kulipa mahari nyumbani na harusi ni ndani ya mwezi huu

Wote: mafujo nakwambia wanashangilia uuuuwi Darasa kama la shule ya msingi hataree, Tereza Finally anaolewa na Masumbuko Mchaga!

Mwanasaikolojia: hongera sana Tereza, najua nimebakisha Mwelu na Kulthum mtapata tu na wewe Kulthum kichaa Chao cha kuchukia ndoa kishindwe 

Kulthum: na kilegee kwa jina la Yesu, ahahahaha uuuuwi me siolewi madam sahau!

Mwanasaikolojia: Haya mwingine aliebakia ni cha utundu wangu Koku!

Koku:
Ndio Ndio sterring mwenyewe nimeingia

Wote: wanacheka! 

Koku:
Baada ya ile engagement yangu Forodhani, nikampeleka Mr Piggy kwa wazazi wangu,  wakamkubali wamempenda nakwambia doh sikuamini, kwanza walijua sitaolewa kabisa maana waliuliza mpaka wakachoka 

Mama nakwambia mpaka analia,  Mr Piggy kumbe alishawatonya ndugu zake wakaja na mahari ikalipwa 

Kila kit kipo saawa kwangu na harusi ni mwezi ujao

Wote: hongera Koku cha utundu wetu, umetisher!

Koku:
Oh! Bado sijawaadithia kilichotokea baada ya mahari

Wote: nini tena jamaa kaingia mitini au?!

Koku:
Basi baada ya mahari tukarudi kwa Mr Piggy, nikaamua kumpa shoo ya kivuruge!

Tumeingia tu ndani, tunamwona mtu amekaa gizani anavuta sigara,  kuwasha taa tobaa ni boss wa Mr Piggy, ex wangu wa zamani Julius

Mwanasaikolojia: toba!  Enhe mkayamalizaje? !

Koku: amesema ndoa haifungwi dokta nimechoka 

Tukamwuliza kwanini?!

Julius: nyie mnadanganyana hamuambiani ukweli we Koku me sijawahi kukupenda maisha?! Siwezi mwacha Koku yeye ndo mwanamke wangu wa kwanza Ndio niliemtoa malaika wake nashangaa mnapotezeana muda sijui mnaenda kuchanganya wazazi mnalipa mahari mahari hio vepe!?

We William Koku alikwambia alishawahi kuwa na mwanaume mimi?!

William: Ndio 

Julius: na unampenda? !

William: sana 

Julius: unauhakika hatokusaliti?! Huyu so mwanamke wa kuoa, alafu anapenda pesa wewe tukikuweka kwenye umaskini sasa hivi unadhani Koku atakaa na wewe?

William: kimyaa  (si unajua tena Julius Ndio boss wake)

Julius: hamna ndoa inayofungwa kuna kazi utatakiwa ukaifanye maana nimeshaambiwa kozi imeisha ntakupeleka kijijini ndani ndani miaka 5 kama Koku atakubali mtaoana kama hatokubali ukarudishiwe mahari yako umwache mtoto wa watu 

Koku: niliskia kuumia, kwanini nihukumiwe kwa kitu sicho? !

Tereza: lkn Koku tuwe wakweli huyo William akipelekwa kijijini awe katibu kata wewe utalima kweli?!

Koku: akamwangalia Tereza; ah niache bwana!

Nikaongea na Julius nikamweleza Kuwa hizi vurugu zote analeta sio kabisa yeye mbona hataki kuoa anaharibia wenzake maisha kwanini?!

Nikamchamba pale nikaishia kumwambia Ndio maana Money penny alikunyoosha mjinga wa mwisho wewe 

Nilipigwa ngumi sikujua saa ngap nilianguka kushtuka naona mtu na boss wake wanapigana, kwa yale maumivu nikaamua kulia chini pale sikujua saa ngapi nimepanda kitandani Ila niliposhtuka sikumwona mtu na ilikuwa asubuhi 

Mpaka Leo naongea na wewe sijaonana na Mr William Piggy siku ya 2, sijui kaenda wapi? Simu yake aliangusha pale nyumbani sina wa kumpigia nimwulizie, ndugu zake nao hawajui walipo, nimechanganyikiwa sio kitoto Dokta 

Wote: kimyaa!  Wanashangaa

Mwanasaikolojia: pole sana Koku kwahiyo umejaribu kwenda polisi? ! Ukamwulizia labda maana siku 2 ni masaa 24 hujaona mtu umekaa kimyaa unatakiwa uende polisi jamaa 

Koku: nimeeenda wameniambia mwisho kesho watajua cha kufanya 

Lkn nilikuwa naomba unisaidie kitu

Mwanasaikolojia: nini tena?!

Koku: naomba unisaidie namba ya simu ya Money Penny, sijui kwanini lakini najua yeye anajua William alipo na Julius Alipo 

Mwanasaikolojia: eh kwani yeye ni mama yao hao watu au?!

Koku: sio mama yao lkn naomba unisaidie tu tafadhali plz madam plz 

Mwanasaikolojia: nikamwangalia Koku kwa huruma maskini, huyu money penny kama mwanga alichoongea Zanzibar Ndio kilichotokea kwa Koku, hapa kazi sio kitoto na bora harusi yao ni mwezi ujayo ingekuwa wiki ijayo sijui ingekuwaje 



Tuonane kesho Tar 18 July 2018 Saa 1 usiku ya Tanzania kuona Nani amebakia kuwa singo

_________________________________________________ 

D. SISSY BUSINESS 

 

Hodi Hodi Hodi. .. jamani Hodii fungua na wewe unalala sana amkaa 

Mwanasaikolojia: eh jaman nan tena saa 6 usiku tunaamshana

Kufungua namwona Money Penny na Koku

Mwanasaikolojia: eh vepe?!

Money Penny: habari za kugawa namba zangu bila taarifa sipendi
Sasa nimeacha mume kwa kitanda nipo hapa kuwaskiza maujinga yenu

Mwanasaikolojia: Koku nini mama?!

Koku: sijamwona William siku ya 5

Mwanasaikolojia: polisi wamesemaje

Koku: wanazuga zuga tu mara we nani kwake kama sio mkewe ondoka basi mapicha picha tu naletewa 

Nikampigia shogako anisaidie labda atajua William alipo anisaidie 

Money Penny: mini ni me wa William au Mamake Mzazi?!
Huyu mteja wako ni mwenda wa zimu au?!kaja kutuamsha na mumewangu kanikera kweli 

Anaulizwa unashida gan asaidiwe anasema William kapotea Sasa mimi na mumewangu tumekuwa kituo cha polisi au?!

Kweli baada ya dk 15 tukafika eneo la tukio kweli tumewakuta chai imeisha tukamshauri Koku aende na Money Penny wakalimalize ila asilete vurugu 

Kufika Julius na William wanashangaa hawa wamama vepe 

Penny akamtuliza Koku; mama tulia me naongea ukiharibu imekula kwako 

Wakaongea sana muda mwingi alikuwa anaongea penny Julius anatikisa kichwa

Money Penny: Julius wakati umefika Sasa ukue basi, haya mambo unafanyiwa watoto wa watu utaacha lini? !

Julius: tena nashukuru Mmekuja wote, Huyu mwanamke hana shukrani, nimemtoa kwenye umaskini mpaka hapa alipo anaishia kusema hanipendi

Nimemvumilia anatembea na wanaume wengine

Koku: we Mbona unatembea na wanawake wengine sijaongea

Penny: Koku nikiinua mguu hili utalimaliza mwenyewe embu nyamaza

Julius: William yupo chini yangu, hana usemi zaidi yang, mimi ndio naamua kila kitu na imeshapitishwa 

Penny: unajua William ameshatoa mahari kwa akina Koku Sasa Mbona unataka kumtia mwenzio gundu lakini?!

Julius: Penny wewe angalau unaelewa kazi zetu zilivyo William ana chaguo mbili ngoja niwaeleweshe

Moja: kama atamuoa Koku ataenda kukaa kijijini ndani ndani maisha yake yote atakuwa mkulima 

Pili: kama hatomuoa Koku ataenda kukaa Ulaya miaka yake yote 

Mimi sio Mbaya Penny, sijawahi kuwa mbaya ni wewe tu uliniponyoka 

Penny: Tafadhali Julius Huyu mtoto wa watu unamwachaje na wameshapendana usifanye hivyo

Julius: kwa sauti ya ukali, Penny mimi sipangi kazi wanapanga wengine usinilaumu 

Penny: hauwezi kabisa kumsaidia Huyu dada imeshindikana

Julius: naweza lkn anatakiwa anioe mimi, ndio msaada wake mkubwa 

Penny: Koku umeskia, je utakubali kukaa kijijini umpate William?!

William unapenda kwenda Kijijini?!

William: akamwangalia Koku, Koku nakupenda sana nipo radhi hata nikae juu ya dari kwa ajili yako, kijijini nitaenda kwa ajili yako ni wewe tu kuamua 

Koku: akawa anatoa machozi maskini utamhurumia akaanza kulia Penny akamkumbatia pole sana Koku lkn haya ndio maisha ya mwenzako hana jinsi

Koku: akamwangalia Julius akamwangalia na William, haina shida nenda tu Ulaya 

William & Julius: wakashangaa eeh?! 

Julius: ina maana umekubali kuolewa na mimi?!

Koku: sitaki kuolewa na wewe najua William hawezi maisha ya kijijini siwezi kumtesa kwa ajili ya mapenzi nenda tu Ulaya mimi naendelea na maisha yangu 

Wote: wakashangaa na jibu la koku 

Penny: na hio mimba utatoa au utamzaa mtoto?!

Julius: kwani Koku ana mimba ya William

William: ndio miezi 4 sasa inaenda

Julius: sikujua nisamehe Koku 

Penny: Sasa umeshajua unawasaidiaje?!

Julius: siwezi tena wangesema mapema Sasa hivi wameshachelewa

Koku: akamshukuru Julius na kumtakia maisha mema William, akavua Pete akamrudishia William akaondoka

Penny akafuata nyuma hao wakaingia kwenye gari




Mwanasaikoloji: enhe imekuwaje Mbona bi dada analia? ! Kwanini William na Julius wameonekana wanakula pamoja wakati mara ya mwisho walikuwa wanapigana

Koku: siwezi kuongea dokta niache nyumbani 

Money Penny: akaongea yote yaliotokea Mwanasaikolojia anashangaa kwa uamuzi wa Koku 

Wakamshusha nyumbani kwake penny, akamshusha na Koku Mwanasaikolojia akarudi ofisini kwake kuendelea na kazi 

Darasa la mwisho la wanaume likawadia,

Wanaume wakaendelea na Darasa lao la mwisho na William pia alikuwepo

Shaibu akasema yeye amefuatilia watoto yatima kuishi nao ameshapata 3, ndoa anaoa sio chaguo langu kwa sasa, labda baada akitokea mtu

Wote: wakampigia makofi na kumpongeza 

Dula: akatualika kwenye harusi yake wiki inayofuata akasema anaenda kuishi na mke wake Africa kusini, kazi ameshaacha

Wote: wakampongeza

Frederick: akatueleza maendeleo yake na mapenzi wake dada wa kanisani Mary na anafikiria kumuoa 

Akasema amepata kazi kwenye supermarket anafanya huko Mlimani City, mshahara sio mkubwa sana ila anamshukuru Mungu anaendelea vizuri

Wote: wakampongeza 

Masumbuko: akatueleza kuhusu mahari yake kwa Tereza ilivyoenda na Mungu akijalia wataoana mwezi ujao

Wote: wakampongeza 

Simon: akatueleza juu ya uhusiano wake na mrembo wake mpya walionana kwenye lift alipokuwa anaenda kufuatilia tenda ya biashara anaitwa Nancy

Wamekuwa kwenye mahusiano ya wiki 2 na wapo vizuri, kwa mara ya Kwanzaa Simon amekuwa Gentlemen hataki kukosea katika hili na Nancy anampenda balaa ijapokuwa hawajacheza mechi! 

Calvin: yupo buzy na biashara zake za uuzaji kilimo na mazao, bado yupo singo na hana haraka 

Anamshukuru sana Mwelu kwa kumsaidia katika maisha yake ya biashara pia anamshukuru Shaibu wamekuwa marafiki wakubwa sana akashukuru na watu wote waliokuwa pale kwenye Darasa akafurahi amepata ndugu wengi wa kudumu 

Wote: wakashangilia na kumpigia makofi

William Piggy: akashukuru watu wote wamekuwa marafiki zake, akaomba undugu uendelee usiishie pale

Japokuwa yeye ana siku 5 nchini ataondoka kikazi kwenda Ulaya, akaweka wazi mawasiliano yake ya barua pepe 

Swala la kuoa kwake halipo tena wataangalia jinsi ya kumlea mtoto na Koku 

Wote: wakampigia makofi wakamkumbatia kwa ujasiri ule aliokuwa nao

Mwanasaikolojia: akawapongeza wote akawashukuru sana kwa kuwa pamoja nao

Akawashauri mahari yote katika maisha wasikate tamaa maisha lazima yaende mbele na yaendelee

akawatangazia hukusu party itakayofanyika keshokutwa hapo hapo mjengoni akawa pa na muda watakuwepo wasanii mbali mbali na warembo pia,ikiwezekana Frederick amlete Mary na Simon amlete Nancy 

Watapewa vyeti vyao na mgeni mualikwa sikuhio kwahiyo wasikose waje wamependeza party ya kula na kunywa

Darasa likaahirishwa wote wakamshukuru sana Mwanasaikoloji kila mtu akatawanyika kasoro Mr William Piggy 

Mwanasaikolojia: nambie boss Mbona umegoma kuondoka 

Mr Piggy: huezi amini maisha yangu hayana raha bila Koku

Mwanasaikolojia: hamna unachoweza kufanya kabisa?! Me nadhani ipo namna, unaenda nchi gani kwani?!

Mr Piggy: akagoma kusema maana haruhusiwi 

Mwanasaikolojia: hamna neno, unaonaje ukimtafutia shule Koku  nchi unayoenda maana mimba haionyeshi kwa sasa akafika huko akasoma na ikiwezekana akajifungulia mtoto huko mtoto akapata uraia yeye akaweza kuishi huko kwa ajili ya mtoto na mkawa mnaonana 

Mr Piggy: hata mimi nimefikiria lkn siwezi kumwambia tangu tuonane sikuile walikuja na Penny sijamwona tena Koku, simu hapokeo, sms hajibu kwake hapatikani kwenye vioski vyake hayupo basi taaabu kweli kweli 

Mwanasaikolojia: we niachie endelea na kazi zako usikose kwenye sherehe lazima atakuwepo mtayamaliza usijali 

Mr Piggy: sawa madam hamna shida asante sana 

Mwanasaikolojia: karibu 

Siku zikasonga, maisha yakaendelea ikawa usiku ikawa asubuhi ikawa mchana ikawa jioni siku ya sherehe ya kuhitimu wanafunzi


Tuonane leo tar 19 July 2018 saa 12 jioni kusoma sehemu ya mwisho ya Hadithi hii ya Kwanini upo singo!
_________________________________________________ 

E. SEHEMU YA MWISHO
Baada ya risala na hotuba ndefu toka kwa mgeni mwalikwa, Mwanasaikolojia alisimama kwa ajili ya kutoa utaratibu

Mwanasaikolojia:
Asante mgeni rasmi napenda kutoa utaratibu wa kukabithi vyeti vyenu, wanafunzi mpo 50 kwahiyo naomba utulivu wa hali ya juu

Nitaita majina ya kila mmoja mmoja kumkabithi cheti chake

Wapiga picha naombeni mkae upande mmoja mpishe njia wahitimu waweze kupita 

Ndugu na jamaa na marafiki wote mtasimama upande wa pili kwa ajili ya kuvishana mashada 

Nikiita jina utapita hapa utamshika mkono Director wa kituo alafu utakuja kumshika mkono Mgeni Rasmi utapigwa picha na mpiga picha wetu kwa ajili ya kumbukumbu alafu mtatokea upande wa pili 

Naanza kuita majina ya kila mmoja mmoja

1. Shaibu Mohammed - akapewa cheti
Wenzake na familia yake wanamshangilia

2. Calvin Lyamuya - akapewa cheti wazazi wake wanafurahia

3. Simon Urasa - akakabidhiwa cheti mwenyewe anafuraha anasukumwa kwenye kiti chake na mamake

4. Frederick Samon - akakabidhiwa cheti mjombake na nduguzake wanashangilia

5. Abdul Mohammed -akapewa cheti chake mwenyewe ana tabasamu kweli kweli 

6. William Maganga Piggy - akakabithiwa cheti chake huyo akashuka 

7. Masumbuko Laswai - akakabithiwa cheti chake akaondoka

8. Aminata Bakari - akakabidhiwa cheti chake

9. Rebecca Peter - akakabithiwa cheti chake huku nduguzake wanamshangilia 

10. Kulthum Kitumbua - akakabithiwa cheti chake

11. Tereza Albert - akakabithiwa cheti chake akaondoka 

12. Kokutonwa Mushumbusi - akakabithiwa cheti chake huku Ndugu zake wengi wakimshangilia 

13. Mwelu Mkumbo - akakabithiwa cheti chake huku wazazi wake toka kijijini wanamshangilia na nduguzake

List ya vyeti ikaendelea mpaka walipoisha 

Mwanasaikolojia akatoa risala zake za shukrani, akawatakia maisha mema akawaambia mkiwa na tatizo lilite wasikose kumfuata 

Baada ya sherehe ya kukabidhiana vyeti ukatolewa utaratibu wa kwenda kwenye chakula, Diamond Jubilee VIP Hall 

Watu wakala wakanywa, wakapiga mapicha wacheza mziki ilikuwa siku nzuri yenye furaha 

Mgeni rasmi alipoondika mziki ukapigwa mpaka saa 6 usiku

Wapendanao wanacheza blues utadhani wapo kitandani, doh ilikuwa hatari, kuja kufunga mziki saa 8 usiku 

Baada ya wiki 1 nikaalikwa kwenye harusi ya Aminata na Dula ilifanyia Upanga ukumbi wa Pathenon Hall karibu na Nyumba ya sanaa kituo cha Aghakan kama unaelekea Posta 

Baada ya wiki 2 nikaalikwa kwenye harusi ya Tereza na Masumbuko doh ilikuwa nzuri jamaani ilifanyika ukumbi wa Sunset Mbezi Beach Makonde 

Baada ya mwezi mmoja nikaalikwa kwenye Sendoff ya Rebecca na Mzungu wake Johnso, harudi ikafanyika Uturuki, ingawa nilialikwa lakini sikuweza kwenda mana nililetewa wagonjwa wengi sana wa kuwasaidia, nilipata wagonjwa 150 kazi ilikuwa sio ndogo 

Baada ya miezi 2 nikaalikwa kwenye harusi ya Frederick na Mrembo wake Mary, ilikuwa nzuri sana, Watu walikula na kunywa walicheza kimasai mwanzo mwisho

Baada ya miezi 6 nikaalikwa kwenye harusi ya Simon na Mrembo wake Nancy, huwezi amini Simon sasahivi anatembea nikamtania nikamwuliza vp umepata muujiza nini wa Yesu naona unatembea akasema nilienda kuwekewa mguu wa Bandia India ndio mana unaniona naweza kucheza na mke wangu 

Baada ya Mwaka mmoja nikaalikwa kwenye harusi ya Mwelu na Calvin Kwanzaa sikuamini lkn ndio imetokea, kwenye sendoff nyimbo za Yesu harusi nyimbo za kidunia

Nilifurahi sana kuona Mwelu na Calvin wameoana 

Mwelu aliolewa akiwa na miaka 34, 

Tereza aliolewa akiwa na miaka 35

Rebecca aliolewa akiwa na miaka 33

Aminata aliolewa akiwa na miaka 34

Kulthum hakuolewa kabisa aliendelea kulea watoto wake 

Shaibu pia hakuoa alikuwa analea watoto yatima 3

Mr Piggy na Koku sikuwasikia tena Baada ya Mwaka na nusu nikapata email imeandikwa Asante 

Kufungua nikakuta email ya Mr Piggy inasema hivi;

" Dear Madam!
Najua imepita muda haujaniskia, nashukuru Mungu nilisafiri salama nikafika salama huku nilipoletwa

Nashukuru sana umenisaidia wakati wa Kozi yangu, ninaendelea vema sana 

Koku sikuonana nae tena tangu tulipokuja kwenye graduation, Baada ya Graduation tukarudi nyumbani kwangu na Koku, tukafanya yetu, akakaa kwangu miezi 2 kabla sijasafiri, tukakubaliana kwamba nimtafutie chuo aje huku nilipo akakubali 

 Nilipoondoka kuja huku, Koku akaanza kuumwa aliumwa sana akarudi kwa mamake mkubwa kuuguzwa, akakaa wiki 1 mimba ikatoka 

Wakampeleka Hospital akafanyiwa matibabu akarudi nyumbani, process za kufasiri zikatimia nikamtumia aende ubalozi akaombe visa, kila akienda kuomba visa anakataliwa, akajibu tena na tena na tena ikashindikana 

Tukakaa miezi 6 kujaribu visa inakataa

Tukakaa Mwaka mmoja visa akakataliwa 

Hatukuelewa tatizo ni nini, akatoka akamfuata Julius maana alihisi ni yeye anamzibia, Julius akamwambia hautatoka kwenda kokote Najua unataka kumfuata William nitahakikisha hautoki 

Tulidhani ni masihara kumbe ni kweli 
Nadhani Julius alifuatilia sana kile alichokisema ikamfanya Koku kuwa frustrated na hii habari 

Kadri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda Koku akazidi kuchanganyikiwa akajaribu kwenda Kenya aondokee hule ikashindikana,

Akazidi kuchanganyikiwa baada ya mwaka wa 1, mama yake Mkubwa Koku akanipigia simu maana alikuwa na namba yangu akaniambia Koku amechanganyikiwa usihangaike tena kumpigia tumempeleka Milembe kabisa ni kichaa anapiga watu

Nilichoka sana nikampigia Julius kumweleza alichofanya sio kizuri akanijiby Fuata kilichokupeleka huko fanya kazi achana na wanawake, kama unataka wanawake jipatie ukiwa huko 

Mpaka navyokuandikia email Koku hatunae tena alijiua aliokota mkasi akajichoma shingoni 

Nililia sana Dokta, Money Penny nilimpenda lkn Koku nilimpenda Zaidi, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina.

Mimi nipo naendelea vizuri nilitaka tu nikupe taarifa kuwa Koku hatunaye tena 

Nimeoa Mzungu wa huku tumebahatika kupata watoto 2 wakike mapacha, mmoja nimemwita jina la Koku mwingine nimemwita jina la mamayangu Kaitlin 

Naendelea vizuri sana na familia yangu hatujambo pia



Mwanasaikolojia; nikashangaa sana Koku kujiua sikuelewa kwanini lakini mapenzi ni daraja lingine ambalo Mungu tu ndio anaweza kumshindia mwanadamu

Koku alimpenda sana Mr Piggy kiasi kwamba aliona hawezi kuishi nae na Kumbukumbu ya Mtoto ambayo ingemsaidia kumkumbusha William haipo

Koku ameniangusha sana katika wanafunzi wangu wote nilimwamini sana kuwa yupo imara na shupavu lkn kumbe ndani alikuwa amekufa nje anajikaza

Mungu ailaze Roho ya Koku Mahali Pema Peponi Amina.

Nikamtumia email Mr Piggy kumshukuru kwa taarifa, kumpa pole na hongera na kumtia moyo asonge mbele asiangalie nyuma kamwe, sisi tulimpenda Koku lkn Mungu alimpenda Zaidi.

Baada ya Miaka 5 kupita, nikapata email toka kwa wanafunzi wangu wote wakitoa shukrani tele kwa msaada niliowapatia

1. Calvin & Mwelu walipata watoto 3, wakiume 2 wakike 1, wanaishi Arusha Tanzani, Calvin alikuwa kupewa urithi mkubwa toka kwa wazazi wake lkn waligawanyishwa nusu kwa nusu na dadake, sasa hivi ni mfanya biashara mkubwa na Mwelu bado ni mwajiriwa na sikuhizi a Najua kupendeza huyo utamjua?! Mobile mpaka makeup anapaka sikuhizi na ma-weaving ya laki 3 laki 5 anavaa. .. hapana chezea

2. Tereza na Masumbuko walipata watoto 2, wakike na kiume wanaishi Rwanda ndipo alipopata kazi Masumbuko

3. Kulthum hakuolewa ila analea watoto wake aliowachukua, wamekuwa wakubwa wanasoma primary sasa akanitumia na picha zao, alikuwa na furaha sana

4. Rebecca na Mzungu Johnson walipata watoto mapacha wakike na kiume bado wanaishi Uturuki, Rebecca aliiuza biashara yake kwa mtu akaondoka Tanzania, wanaishi maisha mazuri wanafanya biashara zao huko huko


5. Aminata na Dula wanaishi Africa Kusini na watoto wao wazuri hao doh hadi raha

6. Frederick na Mary walibahatika kupata watoto 2, wanaishi Gongo la Mboto Dar es salaam
Frederick anafanya biashara zake mwenyewe na mkewe anafanya biashara za mapishi anapika kwenye maharusi

7. Shaibu hakuoa aliendelea kulea watoto wake aliopewa na Jamii, anaishi Dar es Salaam, Tanzania

8. Simon & Nacy walihamia Nchini Kenya, Simon alipata kazi huko, wana watoto 3, wakike na kiume

Nafurahi sana kuona watu niliowasaidia wanaendelea vizuri, wakati mwingine nawaomba waje wawatie moyo hawa wanafunzi wapya wanakuja wanaongea nao wanaondoka

Sijasafiri kuwa na Darasa zuri kama la akina Mwelu mpaka sasa haijawahi kutokea



Sikumoja wakati najiandaa na Darasa la waliojiunga upya nusu saa kabla ya Darasa nikaskia mtu anagonga mlango, alipoingia nikahisi hii sura kama naijua lkn sikumbuki nimeiona wapi

Akaingia akakaa alikuwa mwanamume mmefu mweupe handsome mzuri sana doh ukimwona tu hivi unavutika nae.

Nikawa nawaza anatafuta nini ofisini kwangu

Handsome boy: habari madam

Mwanasaikolojia: nzuri za kwako? !

Handsome Boy: salama

Mwanasaikolojia: karibu nikusaidie na nini?!

Handsome boy: nimekuja nina shida nahitaji msaada wako, nikipata msaada wa kisaikolojia nahisi nitakaa sawa

Mwanasaikolojia: karibu sana
Umeleta risiti ya malipo?!

Handosme boy: ndio akatoa mfukoni akanipa, imeandikwa milion 10

Mwanasaikolojia: mbona hela nyingi sana kwanini?ada yangu ni mil 5 tu kwa sasa au mpo wawili mnataka ushauri?!

Handsome boy: kesi yangu kubwa sana ndio mana nimekulipa mara 2

Mwanasaikolojia: karibu sana unaweza ongea nakuskiza

Handsome Boy: shida yangu sijui kama utaielewa, nilikuwa na mpenzi wangu mmoja tulipendana sana, Miaka 10 iliopita

Nilimpenda sana maana nilimtoa mbali, nilimgaramikia kwa kila kitu, mimi nilikuwa mwanaume wake wa Kwanza, Baada ya Miaka 5 akaanza kuota mapembe mara anatembea na wanaume wengine ananidharau nikaamua kukaa pembeni

Lkn kwakuwa nilikuwa nampenda sana Nikawa narudi kila Baada ya mwezi mmoja kumcheki namkuta habadiliki

Tukawa tunaendelea hivyo hivyo na mapenzi ya kugombana nikaamua nikae pembeni nimwone jeuri yake iko wap

Akaja akapata bwana wakapendana sana ambae nilikuwa nafanya nae kazi, nikajaribu kila njia kuwatenganisha kwasababu nilikuwa nampenda sana Koku lkn wapi sikufanikiwa

Baada ya Miaka 5 kupita nikasikia mpenzi wangu alipata kichaa akajiua ... sikuamini, lakini shida yangu kuu sio hio

Mwanasaikolojia: shida ni nini?!

Handsome boy: shida yangu ni kwamba namwona kila siku,

Mwanasaikolojia: unamwona? Unamwona mtu aliekufa? !

Handsome Boy: ndio kila siku namwona anakuja amevaa nguo nyeupe ina damu kwenye Bega na kifuani, lakini akija haongei ananiangalia analia tu

Miaka yote 5 amekuwa anakuja kila siku, sikunyingine anakuja anavunja vitu, TV,  radio, anapasua vioo nikimwuliza kwanini unafanya hivi ananijibu unavuna ulichopanda

Mwanasaikolojia: eh hatari hii kesi ngumu sana! Umeshaenda kanisani kuombewa au wewe ni mwislamu? !

Handsome Boy: mimi ni mkristo pure, nimeenda kanisani kuombewa lkn anarudi

Nikiingia kanisani wakianza maombi anaondoka nikitoka nje ya mlango wa kanisani Nikiingia kwenye gari namkuta amekaa seat ya mbele au nyuma

Mwanasaikolojia: doh pole sana ndugu, huyu anaekutokea ulimfanyaje?!

Handsome boy: sikumfanya kitu wala sikumdhuru sijui kwanini ananitokea, Leo asbh amenitokea kitandani akawa ananikaba shingo nikapambana nae nikachomoka nikaenda kwa rafkiangu ndio akaniambia unahitaji msaada wa kisaikolojia maana tunahisi unakichaa!

Mwanasaikolojia: eh pole mno! Sijawahi kukutana na kesi kama take ila nitajaribu kukusaidia lkn usiwe mkaidi ukishauriwa

Handsome boy: sawa dokta hamna shida

Mwanasaikolojia: ah! Embu nambie, sijajua jina lako,  wewe unaitwa nani nani anaekutokea anaitwaje?!

Handsome Boy: Kwajina naitwa Julius, Mwenyeji wa Musoma, nina Miaka 50 sasa nafanya biashara zangu

Mwanamke ananitokea anaitwa Marehemu Koku, alikuwa mhaya. .. Kokutonwa Mushumbusi

Tena huyo hapo nyuma yako amekushika bega mkono mmoja, ananiangalia kwa hasira sana, mkono mwingine ameshikilia tumbo lake analia

Madam nisaidie nimechoka kuonana na wafu nimechanganyikiwa sijui nafanyaje

Mwanasaikolojia: akageuka nyuma hakuoa mtu, akainuka akaangalia hamna mtu akarudi kukaa akatikisa kichwa akamjibu Julius
Ndugu yangu kuna usemi unasema malipo ni hapana hapa Duniani, hukumu ni Mbinguni unaujua?!

Julius: ndio naujua

Mwanasaikolojia: sasa wewe unavuna ulichopanda kwa marehemu pole sana

Kesi yako ngumu siwezi kukusaidia, nakuandikia cheque ukachukue hela yako kesi yako imenishinda, nenda kwa walokole wakusaidie hizi  ndizo kesi zao utapata nafuu haraka ndio uje nikusaidie

Julius: akalia sana kwa uchungu alilia mpaka wafanyakazi wangu wakaja kumwondoa kwa kumbeba na kumpeleka hospital

Tangu sikuhio sikumwona tena Julius ila niliskia alijiua akiwa milembe kwa kujichoma na kiwembe alichokificha

Alijichomachoma shingoni mpaka watu kuja kumwona anavuja damu hatari na anakata roho

Sikuwahi kumwona tena Koku lakini nilipeleka maua ya shada kwenye kaburi lake nikalia sana kwa uchungu Koku nimekukumbuka sana mdogowangu Mungu akuruhusu upumzike kwa amani sasa, watesi wako wamelala pia,nikalibusu kaburi nikainuka nikaondoka

THE END - MWISHO!

Tuonane kwenye sehemu ya 2 ya kwanini Upo Singo mwakani 30th June 2019

Usisahu kununua kitabu chake kupata orijino stori

Asante sana kwa kusoma hadithi hii naamini umejifunza kitu, Mungu Akubariki Sana.



HADITHI INAYOFUATA: SOME LEMONADE FOR YOU

IPO HAPA HAPA ANGALIA PAGE YA MWANZO

You Might Also Like

3 comments

  1. Baada ya miaka 5 katika ndoa na mume wangu na watoto 2, mume wangu alianza kufanya tesa na kutoka nje na wanawake wengine na akanionyesha mapenzi baridi, kwa mara kadhaa anatishia kunitukana ikiwa nitathubutu kumuuliza juu ya uhusiano wake na wanawake wengine, mimi iliharibiwa kabisa na kuchanganyikiwa hadi rafiki yangu wa zamani akaniambia juu ya simulizi ya spell kwenye wavuti inayoitwa Dr.Wealthy ambao husaidia watu walio na uhusiano na shida ya ndoa na nguvu za miiko ya upendo, mwanzoni nilitilia shaka ikiwa jambo kama hilo litakuwapo lakini aliamua kujaribu, nilipowasiliana naye, alinisaidia kutoa upendo na ndani ya masaa 48 mume wangu alirudi kwangu na kuanza kuomba msamaha, sasa ameacha kwenda nje na wanawake wengine na wake pamoja nami kwa uzuri na kwa kweli . Wasiliana na cell hii kubwa ya upendo kwa uhusiano wako au shida ya ndoa kutatuliwa leo kupitia: wealthylovespell@gmail.com au moja kwa moja WhatsApp: +2348105150446.

    ReplyDelete
  2. Hey, I'm so excited that my broken marriage has been restored and my husband is back after leaving me and our 2 children for another woman. After 8 years of marriage, my husband and I argued until he finally left me and moved to California to be with another woman. I felt that my life was over and my children thought they would never see their father again. I tried to be strong only for the children, but I could not control the pain that tortured my heart. My heart was full of worry and pain because I was really in love with my husband. I think of him every day and night and always wish he would come back to me. I was very upset and needed help. So I looked for help online and came across a website that says whitemagicmaster. , So I felt like I should try. I contacted him and he told me what to do and I did it, then he made one (love spell) for me. 28 hours later my husband really called me and said he missed me and the children so much. So incredible !! So he came back with love and joy on the same day and apologized for his mistake and for the pain he had inflicted on me and the children. Then, from that day on, our marriage was now stronger than before, all thanks to whitemagicmaster. He is so powerful and I decided to share my story online that whitemagicmaster is a real and powerful magician. I will always praythat he lives a long time to help his children in difficult times when you are here and need your ex or your husband has moved to another woman, or you want Herb's to get pregnant.stop crying, contact this powerful wizard now. Here is his contact: Email to: wightmagicmaster@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Haya, nimefurahi sana kuwa ndoa yangu iliyovunjika imerejeshwa na mume wangu amerudi baada ya kuniacha mimi na watoto wetu 2 kwa mwanamke mwingine. Baada ya miaka 8 ya ndoa, mimi na mume wangu tulibishana hadi mwishowe aliniacha na kuhamia California kuwa na mwanamke mwingine. Nilihisi kwamba maisha yangu yamekwisha na watoto wangu walifikiria hawatamuona baba yao tena. Nilijaribu kuwa na nguvu kwa watoto tu, lakini sikuweza kudhibiti maumivu ambayo yalitesa moyo wangu. Moyo wangu ulijaa wasiwasi na maumivu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana mume wangu. Ninamfikiria kila siku na usiku na siku zote natamani anirudi kwangu. Nilikasirika sana na nilihitaji msaada. Kwa hivyo nilitafuta msaada mkondoni na nikapata wavuti inayosema whitemagicmaster. , Kwa hivyo nilihisi kama ninafaa kujaribu. Niliwasiliana naye na akaniambia nifanye na nikafanya, kisha akanitengenezea moja (upendo spell) kwa ajili yangu. Masaa 28 baadaye mume wangu alinipigia kweli na kusema ananikosa sana na watoto. Ajabu sana !! Kwa hivyo alirudi kwa upendo na shangwe siku ile ile na akaomba msamaha kwa kosa lake na kwa maumivu aliyonipata mimi na watoto. Basi, tangu siku hiyo kuendelea, ndoa yetu ilikuwa na nguvu kuliko hapo awali, shukrani zote kwa mzungu. Yeye ni mwenye nguvu sana na niliamua kushiriki hadithi yangu mkondoni kwamba whitemagicmaster ni mchawi wa kweli na mwenye nguvu. Nitawaombea kila wakati kuwa anaishi muda mrefu kuwasaidia watoto wake katika wakati mgumu wakati mko hapa na unahitaji baba yako wa zamani au mumeo amehamia kwa mwanamke mwingine, au unataka Herb apate ujauzito.stop kulia, wasiliana na huyu mchawi mwenye nguvu sasa. Hapa ni mawasiliano yake: Barua pepe kwa: wightmagicmaster@gmail.com

    ReplyDelete

all rights reserved - OFFICIAL MONEY STARS | Designed by ARACK