_________________________________________________________________________________
CAUTION/ TAHADHARI:
TAFADHALI USICHUKULIE BINAFSI (PERSONAL)
______________________________________
SEHEMU YA 1
A.PUNDA MWANA PUNDA
Juzi nilipigiwa simu na shoga yangu Harrieth akaniambia mume wa shoga yetu anamtakaa Kimapenzi…. Yaani awe mchepuko wake ….. amemsumbua miezi 3 sasa na anapanga amkubalie…. Nikamwomba tuonane anieleze vizuri!
Tulipoonana akanieleza kila kitu na kunionyesha sms za bwashemeji wetu… na hela anazomtumiaka kwa tigopesa nikachoka… Kumwuliza kama shoga yetu anajua hili akasema hapana, bimdashi hajui kitu.. ila bwanake anahela mbaya… anatawanya hela kama nini!
Harrieth: sasa wewe unyamaze maana nawe una huruma sana… huyu bwana nataka nimtengenezee show time ya kibabe… juzi nimemwomba anipe hela ya mtaji nifungue biashara milioni 50 akasema sawa.. ila hio sawa ilikuja na Emoji bikao za kimapenzi si unajua mambo ya whatsapp tena?
Ndo hivyo me pale nataka nitengeneze maisha…vp wewe ameshakutaka huyu bwana?
Mimi: hapana hajawahi atanionea wapi?
Harrieth: kwahiyo hajawahi kukutia machoni kabisa?
Mimi: hapana hajawahi!
Harrieth: akaniangalia sana…anyway, ikitokea akakutaka wewe nenda, ila usicheze mechi pekupeku jamaa ni Kipusa wa kumwaga nahisi ana ukimwi… embu ngoja tumwite mkewe tumsikie Madame Boss Leide atakavyokuja na mashauzi!
Tukapanga kumwita shoga yetu kumweleza ukweli kuhusu mumewe akaja pale Best Bite … kapaki Lexus yake akashuka amevaa skin jeans hataree, viatu vya Christian Louboutin, handbag na miwani ya Gucci… Le Madam Boss Leide!
Ulumbi: hey you, akatukumbatia na kutubusu mashavuni (ana mambo yake ya kizungu flani utamtaka)?!
Enhe kuna nini tunafungua Bank au Microfinanceu?
Wote: tukamwangalia kama hatujamsikia
Harrieth alikuwa amejaa sana hasira, hataki hata kuongea .. alikuwa na mipango yake kabambe kamwita Ulumbi kumsoma upepo wake upoje! nachompendeaga Harrieth hajawahi kuwa mnafiki tangu namfahamu!
Ulumbi akaketi, akaita waiter huku anajipepea joto utadhani hatujakaa kwenye a/c ….mademu wa kibongo na kujiongeza wamekuwa too much… hasa bibie Ulumbi… anyway hili silo lililotuleta hapa ngoja kwanza tuongee na Ulumbi
Ulumbi: Mbona hamuongei unajua nimeacha mume anajiandaa na safiri kwenda London!
Harrieth: London ee!
Ulumbi: yah, anasafiri kikazi leo usiku!
Harrieth: unaenda nae?
Ulumbi: Hapana nimechoka sana, si unajua ndio nimerudi toka Paris… ndege zinachosha sana sitaenda nae… enhe nambieni, kunanini?
Harrieth: unauhakika unataka kujua?
Ulumbi: nataka kujua nini? (Hapo uso umeshambadilika, anawasiwasi)
Harrieth: kuhusu Mu….
Mimi: Nikamstopisha!
Wote: wakanishangaa!
Mimi: Ala! Mtu hata hajanywa kinywaji chake unataka kumbutua we vepe?
Ulumbi: eh nyie mna nini leo au mmelewa kwa mvinyo jumapili hii? Kanisani hamjaenda?
Mimi: Tumeenda na tumemwomba Mungu sana ndio maana tumepata ujasiri wa kukuita!
Ulumbi: haya nimekuja what’s up?
Mara waiter akaleta Juice ya Embe, Ulumbi akaichukua haraka haraka anakunywa! Sisi tunamwangalia!
Ulumbi: kama hamwongei nikimaliza Juice nasepa!
Harrieth: Shogaetu tunakueleza ukichukia haituhusu maana tumechoka!
Wote: Ukweli ni kwamba Mumeo ni Malaya! Kipusa! Tumemchoka!
Ulumbi: Eeeee?!
Harrieth: Anatusumbuaa ….anatutaka Kimapenzi…
Ulumbi: Akacheka kwa nguvu hahahahhahahahhahahahahah! Ahahahahahahhaha
Ulumbi: Akacheka kwa nguvu hahahahhahahahhahahahahah! Ahahahahahahhaha
Wateja wa Best Bite: Wote wakageuka wanamwangalia anavyovyocheka kama jini!
Ulumbi: akaendelea kucheka kwa muda
Harrieth: nampa dk 3 asiponyamaza namwagia hilo lijuisi lake usoni!
Ulumbi: akanyamaza baada ya kusikia anamwagiwa juice!
Ulumbi: Enhe! sasa mume wangu mmemkubalia ombi lake?
Wote: Tukashangaa! Tumkubalie? Noooo waaay!
Ulumbi: Mhy haya bwana nashukuru
Wote: Unashukuru?
Ulumbi: yah nashukuru kwa kunipenda na Kuniheshimu!
Wote: Kwahiyo haushangai Mumeo anatutaka?
Ulumbi: sio kwamba sishangai, namjuaaa! Ndio tabia yake… ndio maana akawa mume wa Ulumbi! Kwani ameitwa mume wenu?
Huyu ni mume wangu!
Na Mume wangu namjua vizuri sana… Ni Malaya wa kutupwaaa!
Na vile mnamwona pale hana hana hata chembe ya VVU wala UKIMWI labda awe ameupata Jana au leo
Wote: Tukaangaliana kwa mshangao jinsi gani tumezodoka! Huku Ulumbi anakunywa Juice yake kwa raha na kucheka, alipomaliza kunywa juice akaendelea…
Ulumbi: Mume wangu mimi namjua …na ningetamani sana mmoja wenu atembee nae ili nimwulize swali langu!
Ulumbi: Mume wangu mimi namjua …na ningetamani sana mmoja wenu atembee nae ili nimwulize swali langu!
Wote: Swali gani?
Ulumbi: Mume wangu Yule mmaemuona pale anabonge la Machine, zaidi ya inch 15… huku anakunywa juice!
Harrieth: Jesus Christ akaweka mikono juu
Ulumbi: Yeye na Punda hawachekani!
Wote: tobaaaaa!
Ulumbi: Na najua kwanini anatembea nje!
Wote: Kwanini?
Ulumbi: Yule akiniudhi namnyimaa unyumbaa!
Sasa yeye anajifanyaga kidume nikimnyima anaenda kupiga nje!....
Akifika huko nje anaumiza watoto wa watu na wake za watu mbayaaa(huku anakunywa juice yake ya Embe)….
Najua wanawake wengi hawawezi kuhenya kwenye ile kambi… wanamkimbia …. Na Mume akikosa pa kupoozeka anakuja kwangu mikono nyuma (Huku anamalizia Juice yake)
….Mimi ndio Kiboko yakeee! Mimi ndio namlizaga.
Hajawahi kutokea Msichana au Mwanamke wa kumliza tangu tumeoana huu mwaka wa 18 sasa ……Maana angepatikana asingekuwa anakuja kwangu mikono nyuma amejaaa!
Hajawahi kutokea Msichana au Mwanamke wa kumliza tangu tumeoana huu mwaka wa 18 sasa ……Maana angepatikana asingekuwa anakuja kwangu mikono nyuma amejaaa!
Ndio mana nasema namjua …acheni atembeze mimi siumii mana mimi ndio saizi yake aliyopewa na Mungu.
Ndio mana nikawauliza nani katembea nae kati yenu ili nijue kama mmeumizwa au nimepata mkali wangu!
Mume akitoka nje ya ndoa (akicheat) siumizi kichwa mana najua ni yeye pekee ninayemwezea na kumtosheleza, I make him feel like a MAN, A REAL MAN
Mume akitoka nje ya ndoa (akicheat) siumizi kichwa mana najua ni yeye pekee ninayemwezea na kumtosheleza, I make him feel like a MAN, A REAL MAN
Harrieth: Amen sister!
Ulumbi: akamalizia juice yake akaweka Glass chini, akatoa elfu 20, akaweka mezani! Akatuuliza!
kuna kingine?
Wote: tukatikisa vichwa kwa ishara ya hapana!
Ulumbi: ila hamjachelewa, nendeni mkatoboe vizazi …. siwatishi ila mtanipigia simu!
Alafu hakuna mwanaume muoga kama mume wangu!
Anaogopa kufa utadhani alijiumba, hawezi kutembea nje peku lazima avae viatu!
Ni hayo tu kwa leo… mtanipigia kunijulisha kikao kijacho!
Akainuka akaondoka!
Sisi: tunamshangaa hatummalizi! Doh Ulumbi huyu au?
Harrieth: shenzi kabisa huyu mwanamke anajishaua sana… unajua huyu rafkiako anajishaua sana!
Inch 15 ya wapi bwana anatutisha tu.
Huyu rafkiako anatuletea michezo ya Boarding School michezo ya kutema mate kwenye maji ya kunywa wenzio wasinywe… au kupaka mate kwenye nyama mwenzio asile, ila kwangu hatonipata!
Nina Plan ya kumkomesha Ulumbi… amejaa mashauzi sana, nataka nizinyofoe hela za mumewe mpaka aje aniombe msamaha… ajue kuwa Mungu hakumuumba mwanamke pekeyake!
Inch 15 kitu gani bwana, watu tunazaa watoto kilo 10 na bado tunaishi itakuwa Inch 15? We ngoja tu … London hio naenda kukomeshea!
Embu ngoja!
Akanyanyua simu akampigia Mume wa Ulumbi… akaweka Loud speaker!
Simu ikaita wee ikaita wee ikaita na kuitaaa… haikupokelewa!
Akasubiria kama dk 2 akataka kupiga akapigiwa, kweli aliempigia ni Mume wa Ulumbi.
Mume wa Ulumbi anaitwaga JITU!
JITU: Sema mpenzi
Harrieth: Baby uko wapi nina hamu na wewe
JITU: nipo kwangu, uko wapi?
Harrieth: Nipo Best Bite… nimekuja kutuliza akili lakini hazituliziki
JITU: pole sana mpenzi ngoja nije
Harrieth: karibu
SIMU IKAKATWA!
Harrieth: Sasa skia mami, huyu bwana usiku wa leo naanguka nae London, alishanikatia visa na kila kitu!
Mimi: Tobaaa unasafiri nae tena? We bwana mwongo sana!
Harrieth: Mimi sio mwongo, leo nakuita hotel uje uone visa na toketi!
Hapa nataka nikampe show ya kichokoraaa! Kwa mara ya kwanza nakubali maumivu, nataka nikalione hilo lipunda kabla hatujasafiri! Alafu nilimwomba hela sijui ataniletea… akiniletea nakupigia uje!
Nikamuaga Harrieth maana sitaki shida za waandishi wahabari, akaniomba sana nibakie, ili nisome alama za nyakati!
Mimi nilie na Harrieth naitwa Grace, nimeolewa na Mtoto 1 …ndoa ya miaka 10… Mume wangu anaishi Mkoa mimi naishi Dar.
Najua unajiuliza kwanini mume anaishi mkoa na mimi nipo Dar.. hio ni stori nyingine kwa wakati mwingine… kwa leo tulimalize hili sakata la Harrieth na Mume wa Ulumbi..
Harrieth akapanga na kupangua hapo… Mara JITU akaingia, kaja na uso mkavu kama hajawahi kututaka sisi sote!
UKWELI NI KWAMBA:
Jitu hata mimi alishawahi kunitaka, kuna siku nilienda kwa Ulumbi kumsaidia kumwangalia mwanae, yeye alienda kwenye sherehe na mume alikuwa amesafiri.
Nikiwa buzy nacheza na mwanae, mume akaingia, nikamlaza mwanae nikabakia kumsubiria Ulumbi.
Masaa yanaenda Ulumbi haji mumewe tukawa tunaongea akaanza kunitongoza, akachukua simu yangu akajibipu akasave namba yangu.. kanitongoza siku hio mpaka… uzuri wa JITU bwana hakufosi, anakuandalia mazingira yaw ewe kumfuata mwenyewe!
Sikuwahi kujua habari za hela wala nini, mimi nilimkataa kwasababu ni mume wa rafkiangu, nimeumbiwa haya!
Akanibeba juu juu mpaka chumba cha wageni, akanibwaga kitandani kimahaba zaidi, akaanza kunibusu busu nini kweli nikakolea, lakini alipotoa machine ndio nilikimbiaaaaaaa! Kha! Ile sio machine ni laana! Huyu kaka sijui Mghana au Mnigeria sijawahi kuuliza habari zake sana ila nikimwuliza Ulumbi ananiambia mtu wa Kagera lakini sidhani kama ni raia mwenzetu
Katika kimbia Mara geti likafunguliwa akakimbia chumbani kwake, mimi nikajitengeneza fasta mkewe akaingia akanishukuru nikaondoka!
Tangu sikuhio sijaonana tena na JITU, akawa akinipigia sipokei akituma sms sijibu, akawa ananitumia hela tigo pesa laki 5… mil 1.. mimi nazitoa nakauka, sijawahi kumjibu sms wala kupokea simu
Ndio leo namwona JITU live kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho kwake alipotaka kuniharibu… lakini hii ni siri yangu Mimi Grace mpenzi msomaji, ni siri yangu na Mungu na JITU… Sijawahi kumwambia mtu kabisa kuwa kila week JITU ananitumiaga hela… naanzaje kwanza? Ukila na kipofu usimshike mkono, kama anahela za kumwaga ni yeye hainihusu!
Alipofika pale Best Bite kaja mkavuu ananisalimia kama hanijui!
Harrieth: Babe huyu ni rafkiangu anaitwa Grace!
JITU: Oh! Grace! Nimefurahi kukufahamu akanipa mkono huku ananitekenya katikati ya mkono!
Grace: nashukuru pia… nikajinasua mkono
JITU: eh niwaagizie nini?
Harrieth: Oh! hapana Babe tumekaa sana hapa zaidi ya masaa 2… nanihii ile ishu ya ile nyumba ulioniambia ya Posta Mpya (huku ananikanyaga kiatu- ishara ya kwamba sisi tunadondoka kwa Hotel), nimeshaongea na dalali amesema tukamwone leo na mwenye nyumba ana nafasi leo..
JITU: Sawa hamna shida basi twende!
Akaaga akatoka, Harrieth anamwambia nisubirie kwenye gari nakuja…
Harrieth: Grace embu nipe mipira
Grace: kwani mimi nauza duka la dawa?
Harrieth: we acha mambo za kihuni, unataka nikafe
Grace: Na wewe ni mbishi! Sasa unaenda kwa Punda kufanyaje… utakufa ujue!
Ahahahahhaha
Harrieth: Punda my foot! Lete mipira
Akaninyang’anya pochi akachukua mipira yangu yote… we ngoja niende nikamhakikishe huyo Punda nione kama ni Punda aliempanda Yesu au kuna mwingine!
Grace: Kwani wewe unataka nini hasa kwa JITU? Kama ana ukimwi je?
Harrieth: Ukimwi kama Malaria tu, tunakunywa Dawa tunaishi, kufa kila mtu atakufa, ingekuwa Kansa nisingekanyaga pale maana Kansa ni mwisho wa Ukimwi, Kansa unakufa unajiona Ukimwi unaishi mpaka unachoka!
Nitakupigia jioni usijali … tunaingia Sheraton!
Grace mimi huwa ni mpole sina maneno sana, nikarudi nyumbani kwangu nikalala nimeacha simu kwenye chaji nimeweka vibration… hapo saa 10 jioni!
Nikaamka saa 1 usiku naskia uvivu kwenda kupika njaa inaniuma kweli… nikadondoka jikoni nitafune angalau tunda!
Nimebakia mwenyewe nyumbani mwanangu yupo Likizo nimempeleka kwa Baba yake Mkoa akahangaike nae kumlea!
Nikarudi chumbani nakuta simu inaita, nataka kunyanyua ikakata!
Kuangalia nakuta missed calls 20 zote za Harrieth!
Nikampigia nimsikie Mwana Punda amefika wapi!
Grace: Halo?
Harrieth: Mama nakuomba tafwadhali uje Sheraton!
Grace: vp umefumaniwa nije na maafande wakuokoe?
Harrieth: we acha ujinga njoo… utakuja kula huku na kulala huku ukipenda maana kesho ni sikukuu.
Grace: sawa! nikaondoka kufika Sheraton akaniambia nipande chumbani, kufika nakuta chumba kiko wazi hakijafungwa vizuri nikahisi fumanizi, kuingia naskia A/C kubwaa inawaka Kama Mochwari
Harrieth kuna nini huku mbona a/c kubwa… kusogea namwona Harrieth amelala chini!
Nikakimbia kwenda kumnyanyua, kumwangalia
Harrieth anahema juu juu
Grace: nikainuka kuangalia mazingira kwanza huenda kaporwa, kumbe hamna mtu wala mporaji … ngoja niwapigie reception waje kwanza … nikanyanyua simu nipige Harrieth akanitukana kwa nguvu nikaweka simu chini, nikachukua kiti nikakaa nimsikilize maana kanitukana tusi sio dogo, kaniudhi!
Harrieth: Grace, naomba ukachukue maji moto bafuni unikande?!
Grace: nikukande?
Harrieth: Bwana fanya nachokwambia muda unaenda nasafiri usiku saa 8…
Grace: nikadondoka nikafanya kama alivyotaka, nikamkanda, doh! Mpanda Punda, aliumizwa vibaya mno!
Baada ya kumkanda nusu saa akapata nguvu tukanyanyuana mpaka kitandani akalala….kwenye kumnyanyua ndio naona makaratasi ya Condom yamezagaa, katika okota okota nikahesabu na kukuta zilichanika condom zaidi ya 5 …kweli Mwana Punda kapatikana
Yeye akalala mimi nikaagiza msosi .. baada ya nusu saa Harrieth akaamka nikampa chakula akawa anakula …akafunguka:
Harrieth: Grace! Ulumbi ni msema kweli
Grace: ahahahahhahahahhaha… nikamcheka sana hapo Harrieth kanunaje
Haarieth: unaliona lile begi pale, embu lilete
Grace: nikainuka nikaenda kubeba begi, kufungua ndani kuna hela nyingi sana, kwanza sikuamini!
Harrieth: Hizo hela hizo, nimepewa na JITU leo leo! Zipo Milion 50
Grace: macho yamenitoka! Harrieth umemuua huyu baba au?
Harrieth: naanzaje? nina sura ya kuua? Mxiuuuuu embu acha utoto
Nilikwambia rafkiako Ulumbi ni mjinga hana lolote!
Na nilikwambia naenda London, fungua zipo ya mbele, utaona passport yangu na Jitu zimegongwa British Visa!
Kweli Grace nikafanya kama alivyonielekeza, nilichokaaaa! Macho yananitoka saa ngapi Harrieth amepiga tukio mpaka usiku huu anaanguka kwa Queen?!
Dah nikajiona jingas, nikarudi kuzichungulia zile hela kama ni Mil 50 kweli au la!
Harrieth: kama alikutaka JITU wewe nenda kapige helaaaa mama …. piga helaaa ila ndio ujue kumpanda Punda maumivu yake ndio haya…nimelala chini masaa 3 nakupigia haupokei! a/c imenisaidia mbaya
Grace: macho yananitoka nahesabu hela haziishi! Sasa JITU yupowapi asije akanikuta hapa!
Harrieth: Tulia wewe ameenda kwa mkewe tutakutana Airport! Hapa amelipa mpaka kesho saa 6 mchana wewe utabakia hapa mimi naondoka na gari ya hotel!
Kesho saa 6 urudishe funguo ya watu reception!
Dah, huku anashika tumbo, huyu baba ni zaidi ya Punda kudadeki, ameniumiza balaa na mimi niliingia kichwa kichwa, najua uongo mama! Oh! Jamani acheni huyu mwauame sijui waliumbwa saa wakati Mungu amekasirika au?
Nimejidai nampa mechi ya kichokoraaa, mechi ya kibishi nilikomaaa.. nimejikaza Grace nimejitutumuaaa… nimesali sala zote basi kumkomoa shogako Ulumbi kudadeki huyu Ulumbi ana CHIU au Bahari ya Shamu? Kha!
Grace: nacheka mbavu sina, kweli nikimwangalia Harrieth kaumizwa mbayaa! Yani kaumizwa kweli mpaka nimeenda kuomba first aid kit nikaja kumsafisha na kumpaka dawa!
Akome nae kazidi tamaa ya kudandia magari kwa mbele… na hivi anaenda London atakoma sijui nani atamkanda!
Harrieth: Mume wa Ulumbi wakati ananitongoza, mimi nikawa nalia njaa, njaa njaa kwasababu ya magari anayoendesha Ulumbi mkewe, sasa akawa ananiomba show time kila tukichat nikamwambia show time sitoi bongo kama vipi nipeleke ulaya nitakupa raha mpaka hutanisahau… kweli kaenda kunigongea visa, nikaitwa kujibu maswali, akaunt yangu akawa aningiza hela kila mwezi mil 10 kumi kwa muda wa miezi 6…kila wiki anaweka mil 2.5 Ndio leo kanipa Visa na Tiket za ndege nikaamini nikaona bora nimpe ahadi yake hapa hapa nyumbani lakini kwa maumivu haya nikirudi Bongo nitakuwa sifai!
Huyu mwanaume namwombea asife aishi miaka 100 walaahi, maana sijui kama nitapata habari kama yake tena! Doh! Huku analia maumivu, anameza panadol kama hana akili nzuri, mara diclofenac maumivu heavy mama!
Grace: Umemliza?
Harrieth: Nimemliza shoga, kwanza sikuamini kama analia, maana muda mwingi mimi ndo nalia! Finally akaanza kulia! acheni nilipwe hela nyingi nimemliza vibaya mno, Ulumbi atanitafuta kuchukua kozi kwangu!
Grace: hahahahahah mbavu sina na hivi napenda kucheka kweli kicheko kilipata mchekaji!
Harrieth: na nimeshajua udhaifu wake upo wapi! Mbaya zaidi hachoki ndio maana Ulumbi kakondeaaaana maskini… mpaka anaondoka hataki kuondoka!
Grace: nikamaliza kuhesabu hela kweli ni Mil 50 cash! Dah wanawake wengine njaaa…
Harrieth: Mimi nalala, ikifika saa 7 niamshe nianze safari… naona nimepoa poa maumivu sasa!
Grace: nikachoka hela ni nyingi sana… huyu baba anafanya wapi kazi mbona anatupa sana hela au free mason? Milion 50 kwa kununua uroda? Dah hapa kuna kitu sio bure!
Saa 7 ilipofika Bindada akaja kuchukuliwa, akaniomba nimsindikize Aiport nitarudi na gari ya hapa, akaniomba sana hizo hela nikae nazo kila week niwe naziweka bank milioni tano tano alafu risiti nimuwekee!
Grace: sinaga makuu nikamkubalia, tukadondoka Aiport kweli namwona JITU kaletwa na taxi pia, nikamuaga Harrieth sikutaka JITU anione, wakaondoka haooo wakaingia ndani ya Airport tayari kwa safari!
Nikarudishwa hotelini na gari ya Hoteli, nikapanda kulala hapo saa 8 kamili usiku, najiambia kweli mtu chake masikini Ulumbi!
ITAENDELEA KESHO TAR 14 SEPTEMBER 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
__________________________________________________________________
B. VYA BURE VINA GHARAMA
Asubuhi nikashituka, kuamka ni simu
inaita, nikaipokea haraka haraka nikidhani kuwa Harrieth karudi!
Kuangalia simu eh ni Shangazi,
ananikumbushia kuwa kwake leo kuna sherehe, mjomba amechinja Wanyama anataka
kufurahi na watoto wake wote na wajukuu, nikamwambia sawa najiandaa nitoke
Kucheki simu whatsapp hamna cha message
ya Harrieth wala nani, hata simu ya Ulumbi haikuwepo!
Nikiangalia saa ni saa 5 asubuhi, nikaoga
fasta nirudishe funguo ya watu saa 6 mchana, mara naskia hodi kufungua wameleta
breakfast! Doh aibu mtu mzima nikala fasta nikakusanya hela na mikoba yangu
nduki mpaka kwangu, njiani roho inanidunda nisije pokonywa maana hela za watu
hizi! Nikafika salama nikawahi kuzifungia kwenye safe yangu, jamani Milion 50
sio ya kitoto, oneni tu watu wanaandika kwenye makaratasi lakini ukipewa
mkononi unaweza ukafa ukachanganyikiwa!
Nikajiandaa kubadilisha nguo nikaanguka
kwa mjomba kwenye sherehe! kufika baada ya kumsalimia Mjomba na shangazi ile
nataka kuomba kazi nisafishe chochote au nisaidie chochote nikavutwa mkono na
binamu;
Binamu: we jinga kweli Grace embu twende
kuna umbea chumbani, hatujaitwa kupika tumeitwa kula na kunywa washapika
waliolipwa
Haooo tukadondoka chumbani, doh chumba
kikubwa cha binamu yetu wamejaa mabinamu huku utadhani kikao cha harusi cha
wachaga!
Baada ya masalimiano na nene! Topiki
ikaanza kuzungumzwa, si unajua tena mabinamu tukikutana, mnajazana habari za
tangu mlipoachana mpaka leo!
Ila Mabinamu wangu ni wazuri jamani! Yani acha sina mfano wa
kukuelezea! Ni Visu Balaaa! Yale matoto ya
Singida balaaa, si mnajua watoto wa Singida walivyoo eee, wako wamgawanyika flani hivi amaizing kama wale katuni wa kwenye magazeti ya SANI, kiuno dondolaaa, Chura Mashaalaah, Mahispi Don’t Lie akajiimbia Shakira!
Singida balaaa, si mnajua watoto wa Singida walivyoo eee, wako wamgawanyika flani hivi amaizing kama wale katuni wa kwenye magazeti ya SANI, kiuno dondolaaa, Chura Mashaalaah, Mahispi Don’t Lie akajiimbia Shakira!
Rangi zao sasa, wengine weupe ila maji ya
kunde ndio wengi, ndio akina sisi!
Hawa ni ndugu zangu upande wa Mama yangu,
Mama yangu mzazi ni Mtu wa Singida, Baba ni Mchaga, kwahiyo mimi Grace unaweza
niita Halfcast wa Kichaga… ila hao mabinamu zangu ni watu wa Singida Pure …
Nikisema Pure namaanisha Baba yao wa Singida na Mama yao wa Singida, okay?
Katika ongea ongea za hapa na pale, kila mtu kafunguka kuanzia tulipochana mpaka leo tumekutana na nini basi Binamu wa miaka 28 akaomba ushauri:
Binamu Miaka 28:
Katika ongea ongea za hapa na pale, kila mtu kafunguka kuanzia tulipochana mpaka leo tumekutana na nini basi Binamu wa miaka 28 akaomba ushauri:
Binamu Miaka 28:
Samahani naomba niwe mkweli nina shida,
naombeni mnisaidie kama ndugu yenu wala sijataka kuongea mnifikirie vibaya!
Jaman mimi nina tatizoo, mwenzenu kila
nikipata bwana tunaenda vizuri tuuu ila tukifika kwenye michezo ya wakubwa
a.k.a Mechi naogopaaaa! Nakimbiaaaa!
Mpaka sasa sijawahi hata kufanya kitu
inaitwa Romance hata kukiss sijui!
Mabinamu
Wote:
lahaulaaa! … akyanani… Mukombi wa nene?
….Aiseee… ahahahhahahaha…. Majanga haya… Mungu weee… kwahiyo wewe ni Bikra?...
Yeeessuuuu na Maria… Mwehu kabisa… unatuaibisha…. Fcku …stupid girl… shubatra
…bitch… oh Lord….Jeesuuus criiipeers…Jinga sana wewe.,… huyu kazaliwa saa
ngapi?...
Hapo kila binamu aliongea kwa staili yake
mimi nikabakia namshangaa Binamu alivyo mzuri jamani Zari Mke wa Diamond Platnumz
atasubiria miaka buku! Alafu anasema ni Bikra?! Hii ni mupyaaa!
Binamu Miaka 28:
Mwanaume akitaka kunibusu nasingizia
naumwa meno, anahama anahamia kwingine… ila akishatoa mgobole wake tu dooooh!
Nikiliona tu nakimbiaaaa naachaga na viatu hapo hapo!
Mabinamu:
hahahahahahahah, oooooooooooooooooooooooo mamaaa ahahahahahhaha yani walicheka mpaka shangazi akaja kusema punguzeni makelele tafadhali.
hahahahahahahah, oooooooooooooooooooooooo mamaaa ahahahahahhaha yani walicheka mpaka shangazi akaja kusema punguzeni makelele tafadhali.
Shangazi alipoondoka tukaendelea na mastori!
Grace: Kwani shida ipo wapi
kwa huyu kuwa bikra?
Kayaleta tumsaidie, kama nduguzake mnatakiwa mumsaidie,
tujadiliane jinsi ya kumsaidia kumtukana
haileti suluhu, hapa ana miaka 28..bado miaka 2 achungulie 30, hana mume, hana
mtoto, wenzake wanaolewaaa wanazaaa yeye yupo
Binamu Miaka 28:
Tena napataga wanaume very potential,
wealthy, rich, alafu wanakuwaga wakubwa kwangu kuanzia miaka 40 mpaka 45 ila
wakisikia mimi bikra wanakimbiaaa!
Binamu Mchafu: Kwanza embu tueleze mwana wewe una bikra ipi labda?!
Binamu Miaka 28: Kwani kuna bikra ngapi si ipo moja tu?
Wote: wakacheka hawana mbavu… uuuwi kazi ipo
hapa ndugu hatuna, muhahahahhahahahhahaha
Binamu Mkubwa: My dia
Bikra zipo 6, nitafute kwea muda wako nitakutajia!
Binamu Miaka 28: heee?!
Binamu Mkubwa:
umebakisha ngapi sasa tujue jinsi ya kukusaidia?
Binamua Miaka 28: Zote
zipo!
MABINAMU WOTE: tunakusahuri uzitoe tu angalau toa 1 basi yaishe… ila ukiitoa moja automatically utakuwa umeshazitoa 5 jumla, utakuwa umebakisha moja ya nyuma! toa wewe, acha uboya toaaa.
MABINAMU WOTE: tunakusahuri uzitoe tu angalau toa 1 basi yaishe… ila ukiitoa moja automatically utakuwa umeshazitoa 5 jumla, utakuwa umebakisha moja ya nyuma! toa wewe, acha uboya toaaa.
Binamu Mchafu: kuna
mangi mtaa wa 3 nikupe akutoe vzuuri?
Binamu Mkubwa: Mdogo wangu jamani, ujue wanaume watu wazima hawapendi mabikra sikuhizi, wanawasiwasi akishakutoa je utatulia au utamuacha hapo?! Labda akuoe akakutoe, watu wazima sikuhizi wanapenda wale waliotumika, ili wakapige show za kichokoraa na show zingine tofauti na wanazopiga kwa wakezao!
Binamu Mkubwa: Mdogo wangu jamani, ujue wanaume watu wazima hawapendi mabikra sikuhizi, wanawasiwasi akishakutoa je utatulia au utamuacha hapo?! Labda akuoe akakutoe, watu wazima sikuhizi wanapenda wale waliotumika, ili wakapige show za kichokoraa na show zingine tofauti na wanazopiga kwa wakezao!
Yani watu wazima
wanaona bora akachukue kuberu lililoshindikanaaa mtaani,
limepiga round maishani weeeee na mielekaaa yakutosha likachoka maana wanajua
Kuberu likiwekwa ndani litatuliaaa kuliko wewe! Wanakuwa na wasiwasi huooo tu
mdogowangu! Dah ila bora umelileta tutakusaidia, damu nzito jamani kuliko maji!
Lazima tumsaidie wa kwetu asijeakatuletea aibu!
Binamu Mchafu: Kwa kuanzia atafute mwanaume wa maana kuanzia miaka 37-39 amtoe bikra alafu ampige round weeeeee alafu baadae arudi kwa hao watu wazimaaa. Umri niliokutajia kidogo wanauwezo wa kukutunzia siri na kuwa na speed ya kuitoaa … lakini hapo watachukua kwa kukadiria kima cha chini siku 2.. ukiwapata wale wa 41 kuja juu wanaogopaaa maana speed yao ya kutoa malaika imeshapunguaaa, tena bikra ya miaka 28 mama sio mchezo kuimwagaaa, inahitajika mwanaume mwenye nguvu zakee hawa 40+ washachokaaa, goal 1 hoi, case yako anatakiwa bro aliejaaa akiisimamia masaa 3 inatoka yoteee tena ukafungie bagamoyoo maana maumivu yake utapiga yowe Dar es salaam yote tutaskia!
Binamu Mchafu: Kwa kuanzia atafute mwanaume wa maana kuanzia miaka 37-39 amtoe bikra alafu ampige round weeeeee alafu baadae arudi kwa hao watu wazimaaa. Umri niliokutajia kidogo wanauwezo wa kukutunzia siri na kuwa na speed ya kuitoaa … lakini hapo watachukua kwa kukadiria kima cha chini siku 2.. ukiwapata wale wa 41 kuja juu wanaogopaaa maana speed yao ya kutoa malaika imeshapunguaaa, tena bikra ya miaka 28 mama sio mchezo kuimwagaaa, inahitajika mwanaume mwenye nguvu zakee hawa 40+ washachokaaa, goal 1 hoi, case yako anatakiwa bro aliejaaa akiisimamia masaa 3 inatoka yoteee tena ukafungie bagamoyoo maana maumivu yake utapiga yowe Dar es salaam yote tutaskia!
Alafu
usikubali kwenda gesti uchwara sijui manzese sijui kariakoo, kariakoo yote
watajuaaaa! lakini umri chini ya 35 watakutangazaa utaisoma nambaaa utachukia
Mji unaoishi!
Hivi tukuulize kwanini umeamua kukaa na
Bikra mpaka umri huu lakini?
Binamu Miaka 28:
Nimeokoka Yesu anakataza kuzini kabla ya ndoa!
Binamu Mchafu: huko Kanisani
hamna jamaa akuoe sasa?
Binamu Miaka 28: ah
siwapendi hawana hela, wavivu na hawana focus ya maisha!
Binamu Mkubwa:
ninachompendea Binamu yangu huyu ni mkeli kuliko maelezo sasa wewe vya Mungu
unataka vya shetani unataka, Kanisani hamna wanaume wenye hela kusema ukweli na
ukimkuta aliepo kila mwanamke anamtaka aolewe nae huku kwa shetani wamejaa
kibao ila ndio wanamatatizo mwanzo mwisho!
Binamu Mchafu: Huku
kwa shetani mami, huolewi bikra yani ukiolewa bikra una bahati sana, yani wewe
Mungu akushukie mwanaume wako awe mwelewa sana msikae kwenye mahusiano kwa
zaidi ya mwezi ndio utaolewe bikra… la sivyo jiandae kubanjuliwa unapigwa puli
mama utanyooshwa mieleka miaka nenda rudi, utalia wewe umeumizwa utalia wewe
kwa Mungu mpaka uje umpate wa kukupenda atake kukuoa itakuwa kama huna mimba
basi bahati yako imefika!
Kwa shetani pagumu
ndugu bora ubakigi huko kwa Yesu .. najua hamuamini kubadilisha mwanaume
unachoweza kufanya ni kumchukua mtaani na kumpeleka kwa Yesu ila wasanii nao
kibao, anaweza kukuaktia akishakuoa anafungua mikucha!
Inabidi uwe mpole ukubali kubaki sehemu
mmoja, naona hata Yesu hakupi wa kukuoa kwasababu bado huna maamuzi mazuri,
akikupa aliefulia utamkimbia akikupa mwenye hela utakasirika! Anaona bora
akuache tu.
Binamu Mpole: Ah mimi nakumbuka Bikra yangu nilitolewa kijijini kule
mtoni, Malaika anachomolewa roho inamwagika inadondokea mtoni.. enzi hizo
nilienda Arusha kwa shangazi, doh siwezi sahau, ila hongera sana umejitunza
yangu ilitoka nikiwa na miaka 16
Binamu Mjeuri: eh 16? Yangu ilitoka miaka 13, kwenye michongoma kijijini,
maumivu mara 3, maumivu ya bikira, maumivu ya mchongoma na maumivu ya machine!
Binamu Mchafu: Yangu nilitolewa kwenye holi la ng’ombe!
Wote: wakacheka ahahahhaha uuuwi Yesu alipozaliwa sio?
Binamu Mchafu: yani sikuhio mimi na ng’ombe tulikuwa tunapokezana zamu ya
kulia uzuri mvua ilikuwa inanyesha alafu usiku wa manane! Ila bira imetoka,
ningeishia kuwa mbululaz kama huyu bibie hapa! Amekaa kama makamasi yupo yupo
tu kila siku anaota!
Enhe Grace tuambie yako ulitolewa ulikuwa wapi?
Grace: Mlima Kitonga kule njia ya kwenda Singida?
Wote: ahahahahhahahaha uuuuwi huyu mchawi huyu ahahahahhaha
Grace: Ajali zilizidi kuwa
nyingi nikaamua kwenda kuachilia tambiko pale, nikanyofolewa usiku wa saa 6..
ajali zikakata, so Bikra yangu
imeponyesha wazawa wengi, kweli nakwambia hamnaga ajali za kizembe tena tangu
sikuhio mpaka leo
Wote: ahahahahahahahahah, tunaomba umpeleke na huyu bibie
akafanye tambiko kwengine kwenye matatizo ahahhahahah
Shangazi akaingia haya twendeni mkale
Mchungaji ameshakuja anataka aombee nyumba alafu tuingie kula mnapiga makelele
sana, twendeni;
Basi kila mmoja akanyanyuka, mimi
nikabakia nasubiria wote watoke, nikaona kama Binamu wa Miaka 28 amekasirika,
nikamfuata kuongea nae,
Grace: Nambie mami mbona umekasirika, wala
usijali, sasa kwanini unataka kuitoa labda nikiuliza? Unaharakia wapi?
Bikra miaka 28: Grace nimeshakuwa mkubwa sioni hata
haja ya kukaa nayo!
Nimemaliza shule, nina Degree, Masters,
nipo na kazi yangu nalipwa mil 3 Gross Salary, nina Gari, nina Kiwanja nataka
kuanza kujenga, ninachomiss ni Mume na watoto!
Grace: sasa unataka nini? Mume au watoto?
Unataka kuzaa kwanza ndio uolewe? Ujue kuna single mothers wengi wanahangaika
mtaani.. leo una kazi kesho ukaachishwa kazi utamleaje mtoto? Unataka nini
kwenye maisha yako?
Binamu Miaka 28: Napenda niolewe nipate watoto ndani ya
ndoa!
Grace: Nikikushauri utanisikiliza au
umeshaamua kufanya maamuzi yako? Achana na hawa machokoraa wanaokucheka
wanakuonea wivu!
Ni kweli hamna mwanaume wa miaka
kuanzia 40 atataka apate bikra, washakuwa na wake zao wakitoka nje wanatafuta
pa kupoozea sasa hataki kuja kupooza kwenye mihangaiko tena!
Na kumpata mwanaume ambae hajaoa
kuanzia miaka 40 ni wachache sanaaa!
Binamu Miaka 28: Kwahiyo unanishaurije nitakusikiliza,
nisaidie Dadangu!
Grace: Kaa ujue mapema kuwa wanaume
wote ni washenzi, tena hao watu wazima wako ndio balaa… na wewe umejitunza
alafu uje umpate mshenzi best unaweza ukanywa sumu ukafa, nakushauri usitoe
bikra yeyote kwanza zaidi ya akili, lazima ubadilishe akili yako kwanza, uache
kuwa innocent sana, jifunze uchakaramu wa akali… nataka uwe chakaramu kama
machangudoa, wanaume wanaogopaga wanawake machakaramu, ukiwa mchakaramu utajua
na kumpata atakaekupenda, na ukimpata usikimbilie kulala nae, atakuumiza…
mkazie kwanza mvute vute yani unamkazia mwanzo mwisho, akichoka ndio unajidai
unataka kumpa lakini usimpe
Hio nakuachia Home work, ila uchakaramu
usiwafanyie watu wazima, wanaume watu wazima kwa sasa wablock! Achana nao we
kimbizana na hawa umri wako 30 mpaka 39 hao hao ukifanikiwa hapo niite nitakupa
mrejesho!
Jinsi ya kuwa chakaramu:
Soma vitabu vya uchakaramu, angalia
movies za kichakaramu lakini sio za ngono huko utachanganyikiwa, sikiliza audio
za kichakaramu, plz usivae wala kukaa uchi sijui nini hapana, ila akili ya
kuambiwa uchanganye na ya kwako best ila usiitoe kwanza nakushauri, mimi nina
uhakika kwenye hao hao marafiki zako yupo kijana anaekupenda ni vile
unatanguliza kusema wewe bikra
Basi tukaondoka kwenda kula tukanywa na
kufurahi, sherehe ikaisha kila mtu akarudi makwao..
Baada ya wiki tatu nikapata simu ya
binamu yangu yule wa miaka 28, akaja nyumbani kwangu, ananiambia amefanya yote
niliyomfundisha na amepata bwana
Grace: nikakaa kitako nimjue mjanja anaetaka
kumsakramenti mdogowangu ni nani, kupewa picha nikachoka! Kweli shetani ni Yule
Yule lakini anatumia njia nyingi kumaliza watu wangu wa nguvu, huwezi amini ile
Picha ilikuwa ya JITU!
Ndio, JITU mume wa Ulumbi bwana wa
Harrieth!
Grace: wow! Huyu ni nani? (Hapo najifanya
simjui)
Binamu Miaka 28: Nimempata juzi nilitoka out nilienda
South Beach Kigamboni… nipo na marafiki zangu nakula good time na nini mara
nashangaa mtu mrefu anakuja anaomba kuongea na mimi, nikajongea kumsikiliza
maneno yale yale anaomba namba yangu, nikamkazia kama ulivyonifundisha,
akanilazimisha sana, nikamwambia sawa nikampatia akaniomba twende kutembea
ufukweni mwa bahari, akanitongoza mpaka, ananiambia atanibadilishia maisha ana
hela sana, mimi nikamsikiliza tu lakini naona kwake akili imeganda!
Grace: akili imegandaje?
Binamu Miaka 28: ananipa attention mbayaa, sijawahi
kupewa attention kiasi hiki, anapiga simu kutwa mara 10, hadi aibu ofisini,
yani hizi wiki 3 zimekuwa amazing kwangu..
Grace: okay! So ushatembea nae?
Binamu Miaka 28: Hapana ulinikataza!
Grace: Umempenda?
Binamu Miaka 28: mmmh sijui kwakweli ila ameniambia
yupo singo
Grace: umeshatoka nae Out tangu muonane
Kigamboni?
Binamu Miaka 28: ndio kila siku tunaonana nikitoka
kazini ananinunulia dinner, tuna kiss ananihug narudi kwangu, sikuhizi
ananifuata asubuhi saa 12 nanusu ananipeleka kazini na kunirudisha usiku home
baada ya kutoka kula dinner.. ananipenda ananijali wala hajawahi kunilazimisha
kulala nae
Grace: ushamwambia wewe ni Bikira?
Binamu Miaka 28: Never sijawahi kumwambia
Grace: umemfanyia mavurugu kama nilivyokufundisha?
Binamu Miaka 28: Ndio
Grace: na akawa anasemaje ukimfanyia
mavurugu?
Binamu Miaka 28: anayapenda mafujo yangu sana tu
Grace: kimoyomoyo nasema tobaaa, huyu mjinga
anamlia bisi akimkamata mdogwangu atachukia wanaume milele dah sio kwa lile
punda la JITU!
Mdogowangu unajua kuna wanaume
wanatembeaga na ukimwi! Nadhani hilo bado sijakufundisha!
Sikiliza mdogowangu, huyu JITU
namfahamu vizuri sana, ni mume wa rafiki yangu ana Ukimwi, sasa
nakuongezea akili ya ziada, wewe mpige hela zake lakini usionane nae ana kwa
ana tenaaa… yani upo steji ya mwisho mwisho kubakwa! Yule anakulia timing
ahakikishe umekuwa comfortable nae huogopi kuonekana nae unamwamini kifupi
ameshakujengea mazingira ya kujiaminisha kwako, Plz plz nakuomba kama huamini
hautamaliza wiki huyu bwana atakubakua mpaka utaomba ufe na usiniite!
Kwanza umeharibu kumwonyesha unapofanya
kazi na unapoishi, huwezi hamisha ofisi ya watu ila unaweza hama unapoishi,
nakushauri hama unapoishi, usionane nae tena live plz plz plz, alafu pokea simu
zake mtangazie njaa mwanzo mwisho, baada ya wiki 1 omba likizo mimi na wewe
tutasafiri, kumbuka hela ya JITU ni kama ina mashetani, anaeila lazima anailipa
na sidhani kwa hali yako kama utaweza malipo ya JITU!
Nakushauri vitu viwili:
1.
Mpige hela ndefu hata milioni 100 hata
million 800 we mpige utapewa, akikupa hela nyingi hama namba, mimi na wewe
tutasafiri kwa siku 28 hatutakaa hapa Bongo, plz fanya navyokwambia ukikosea
umeisha!
2.
Achana nae yani kata mawasiliano nae
usimpige hela zozote, yani kata tu mawasiliano nae akija kwako usifungue mlango
mpotezee, akituma hela usimrudishie, akipiga simu usipokee, meseji usijibu
akija ofisini kwako usitoke, mkwepe mwanzo mwisho ataacha, itachukua hata miezi
6 lkn ataacha!
Binamu Miaka 28: akaanza kuogopa nikamweka sawa
akatulia
Nakushauri kwa mara ya mwisho kwa Jitu
hama, yani kimbiaaa kama ulishawahi kukimbia pale paaaaa, paaa omba Mungu akupe
mabawa!
Dogo akakubali fresh, akaondoka!
Baada ya wiki 3 nikapokea simu ya
Harrieth ananiambia amerudi nimpelekee hela zake kwake, nikaondoka mdogo mdogo
mpaka kwa Harrieth, kufika nikamkabithi akahesabu akashukuru, wakati tunataka
kuanza stori za London simu yangu ikaita kuangalia ni Binamu wa Miaka 28,
nikapokea haraka haraka ananiambia Grace njoo sehemu flani huku Sinza kumekucha
kuna gesti yupo hapo amekwama
Tukaondoka na Harrieth mpaka Sinza
kwenye hicho kihotel hapo najua binamu kaharibu mbaya
Kufika naona wasichana 2, wamelala
wanalia kumwangalia Binamu wa 3 amekaa pembeni analia.. kuuliza kulikoni watu
hawaongei nikataka kuita nguvu ya dola ije isaidie maana ni mikelele tu kama
mapaka ya usiku
Harrie akafanya kazi ya kuwanyamazisha,
wakanyamaza wakakaa sawa, wakaanza kuongea
Binamu wa miaka 28:
Grace dadangu huwezi amini, mimi
nimetoka zangu kazini, napata simu ya shogangu ananiambia nije sinza nikaja
hapa nakutana na bi shoga mwingine nae kapigiwa simu kaambiwa aje kuingia ndani
tunamwuliza mwenzetu vepe uzuri mimi nilikuwa nimesimama mlangoni sijaufunga
mara namwona JITU anatokea bafuni yupo mtupu doh kumwangalia na Punda lake
nikahisi nakosa nguvu!
Jitu akawa anasema sisi wote
tumemchezea na kula hela zake kwa muda mrefu ni siku ya kulipa leo, eh kusikia
kulipa huyu mwenzangu akadakwa na Jitu mimi nikakimbia nje!
Nikawa nawaza niite Meneja nikajua tu
huyu bwana atakuwa ameshajipanga na Meneja kalipwa asisumbuliwe, basi nikapanga
kwenda kuita polisi lakini nikahisi na kule atakuwa anamtu ndio nimekupigia
Harrieth: imekuwaje? Mmebakwa au?
Grace: Bwana wako kaumiza watoto wa watu ona
walivyochanika maskini!
Harrieth: ahahahahha! Uuuwi maskini ya Mungu
jamani watoto mmezidi lakini mnalipia tama
Binamu Miaka 28: Mimi nimeponea chupuchupu ila kama
wanaume wote Duniani wapo kama JITU, naghairi kuolewa bora nizae kwa
kupandikiza!
Wote: tukacheka maskini huku watoto wa watu
wamelala wanaskilizia maumivu
Tukaishia kuwazoa zoa warembo
tukaondoka, nikamwambia Harrieth apitie polisi akawaandikishe wamebakwa ila
ndio warembo wajiandae kukutana na waandishi wa habari
Warembo wakakataa katu katu hatutaki,
tupeleke kwa rafkietu tukalale, rafkiao akakataa akasema bora twende kwa Dada
Grace mimi pale nimeshahama na sitaki mtu ajue!
Baada ya kufika nyumbani kila mtu akiwa
ameshatulia na kula chakula tukawauliza imekuwaje, wakaanza kutuhadithia kuwa
walimfahamu JITU kupitia Binamu wa miaka 28, sikuile walipokuwa Soth Beach
Hotel, Binamu alivyoondoka mmoja wa rafkiako alibakia, Jitu alipomwona
akamfuata na kuanza kumtongoza akakubali
Rafiake mwingine na Binamu nae akasema
sikuwahi kutongozwa na JITU lakini nashangaa niliona ananipigia simu wiki 3
zilizopita ananifuata kazini anakuja kunitoa out michezo kama aliofanyiwa
Binamu lakini wao hawakujua kuwa Michezo ya JITU mwisho wake ni malipo!
Jitu aliwaosha kwa pesa na pesa kila
siku anawapa pesa wakaona bwana wa kumchuna ndio huyu kumbe kuna siku yao ya
kuchunwa!
Sasa hotelini alienda na mmoja wakawa
wanajiandaa kwa mechi rafkiake Binamu alipoingia bafuni JITU akachukua simu
akatuma sms kwa rafkiake mwingine na Binamu na Binamu pia kuwa waje guest house
namba flani, haraka kuna mtu amemkamata, ndio wote wanakutana na kuingia
kumkuta mwenzao amelala mtupu analia, walipomsogele JITU akatokea bafuni
akamkamata mmoja na Binamu akakimbia
Watoto wa watu walipigwa Punda kwa
kubadilishana alafu kawafungia na kuwarekodi! Anawaambia Pesa zangu mmekula,
shopping nimewapeleka leo na mimi nataka mnipe raha.. wakiwa wanaongea simu zao
zikaingia message whatsapp, kuangalia ni video toka kwa JITU, kawarekodi
maskini walivyokuwa wanapigwa mechi watoto wa watu wanalia mbayaa, wanapiga
mikelele Jitu unatuua mpaka wanamaliza na JITU anaondoka anawaacha wanalia na
kupumulia mdomo na maskio
Nikaiangalia ile video nikaona jinsi
gani shemji yangu JITU alivyo katili, huyu baba sijui free mason au sijaelewa
alafu anarekodi watoto wa watu yeye amejificha sura amevaa mask, dah akaniachia
mawazo huyu shemeji, sijui Harrieth huko London kulikuwaje..
Binamu Miaka 28: akanifuata akanikumbatia, ananiambia
asante sana dada Grace nisingekusikiliza leo ningekuwa nakandwa kama wenzangu
wanavyokandwa na Harrieth huku wanalia
ITAENDELEA KESHO TAR 15 SEPTEMBER
2018 SAA 8 MCHANA
YA TANZANIA
____________________________________________________________
C. MOON LIGHT LADY- 1985
C. MOON LIGHT LADY- 1985
Baada ya
lile sakata la jana nikawaacha warembo wamelala, Harrieth kaondoka kaniacha
kaenda kuongea na JITU anataka kumchamba kwanini amewarekodi watoto wa watu
kwenye simu
Mimi
nimemkataza lakini hajasikia.. nikaona usiku ni mwaka nikaamua kwenda kumalizia
sikukuu yangu mjini, nikampigia simu shogangu aje anipe kampani;
Nikadondoka
mpaka IT PLAZA, HIGH SPIRIT LOUNGE nikakaa zangu huku
Napata wine na kusikiliza mziki mzuuuri huku napunguza stress.. wakati nimekaa
nasikiliza Mziki huku namsubiria shogangu mara wakaingia wakaka kama 4 wakaja
wakakaa nyuma ya kochi nililokaa, mimi nipo buzy nawaza na kuwazua jinsi JITU
alivyowatenda watoto wa watu na jinsi gani Binamu yangu ameponea kwenye mdomo
wa mamba, sijui alichukua pesa za JITU au alikataa kama nilivyomuelekeza, unajua
hawa watoto bwana akili zao wanazijuaga wenyewe lakini!.. anaweza akasema
hajachukua kumbe ameshakula hela kibao, na anaweza akasema ni bikra kumbe
ameshabingirita mudaaa sasa anajikosha, nikiwa nawaza na kuwazua hawa watoto
siwamalizi mara nikashtushwa na maongezi ya wakaka waliokaa nyuma ya kochi
langu wakiwa wanabishana. Maongezi yao yalikuwa hivi;
MJEDA
WA KWANZA
mwanamke mwenye ngozi nyeupe sio mtamu kama mwenye ngozi nyeusi
MJEDA WA PILI
Mwanamke mweusi sio mtamu kama mwanamke mweupe
MJEDA WA TATU
Mwanamke maji ya kunde ndio mwisho wa matatizo
mwanamke mwenye ngozi nyeupe sio mtamu kama mwenye ngozi nyeusi
MJEDA WA PILI
Mwanamke mweusi sio mtamu kama mwanamke mweupe
MJEDA WA TATU
Mwanamke maji ya kunde ndio mwisho wa matatizo
Wakabishana hapoo mara
shogangu akaingia, shoga kapendeza kaulamba mbayaa! Walipomwona shogangu wote
wakageuka wanamtizana maskini shogangu kidogo aanguke maana sio kwa ile
minjicho!
Shoga: niaje we mnyama!
Grace: nikacheka maana
shogangu ana fujo balaa, nakuona sikuhizi umekuwa mswahili ukiitwa unachelewa
lisaa li1
Shoga: yani we acha tu
nilikuwa nampa utamu shemeji wako si unajua mpaka nikombeleze utamu ndio naweza
kutoka, nimemwacha amelala anahemea pua mdomo na masikio… vp wewe mumeo
umemtupa wapi mbona simwoni?
Grace: yani wewe hujaacha
tu, huku wale wakaka wanamwangalia bado shogangu.. nikamsogelea shoga
nimamwambia hawa wakaka wamekuelewa kweli unaonaje ukiwaalika waje wakae hapa
walikuwa na topiki yao walikuwa wanadiscuss wewe ndio umekuja kuwavurugia!
Shoga: akageuka, hello
Boys! Hw are you?
MIJEDA: hi, hey, mambo,
niaje mrembo
Shoga: Mnaonaje mkija kukaa
na sisi tukaendeleza ile topic mliokuwa mnadiscuss kabla sijaja?
MIJEDA: wakashangaa, mmoja
akainuka na mwingine na mwingine wakaisha!
Tukasalimiana pale wanaume
wakajitambulisha
MJEDA WA 1: Naitwa Moses
MJEDA WA 2: Naitwa Hassan
MJEDA WA 3: Naitwa Baraka
Grace: oh jaman nashukuru
kuwafahamu, naitwa Grace na huyu ni best yangu sana anaitwa Money Stars!
WAJEDA: Money Stars?!
Shoga: Yes ndio jina langu,
kwahiyo mlikuwa mnaongelea utamu wa rangi za wadada mmeishia wapi sasa?
Moses: Mimi naona wadada
rangi yako watamu sana
Hassan: we si ulisema weupe
ndio watamu huyu dada sio mweupe ni maji ya kunde
Moses: Na wewe Hassan ulisema weusi ndio wazuri sasa
kwa Money Stars unatafuta nini?
Baraka: Mimi pekeyangu
nilisema rangu ya Money Stars hapa ndio tamu au sio my dia?
Money Stars: ahahahahahaha!
Kwahiyo nyie wote mabikra au?
MIJEDA: hapana
Money Stars: nyie wote
mmetembea na wanawake wangapi mpaka sasa?
Moses: 15
Hassan: 35
Baraka: 20
Money Stars: na mna umri
gani?
Moses: 29
Hassan: 32
Baraka: 35
Money Stars: ndio maana mna
maongezi ya kitoto! So nyie wote mmeoa au?
MIJEDA: noooo bado
Baraka: wanawake wa sikuhizi
pasua kichwa hatuwezi kuoa kabisa,
Money Stars: kwahiyo nyie
wote hamna mademu mnapiga na kukimbia sio?
MIJEDA: hapana, ila wanawak
wa sikuhizi wanatupa mazingira ya kuwapiga na kuondoka… hatujawahi kuwapata
wale wife material, hawapo!
Money Stars: mnadhani mimi
ni wife material au?
MIJEDA: wewe ni zaidi ya
Wife material
Hassa: Money kwani wewe
umeshaolewa?
Money Stars: nimeolewa mama
watoto 3 na wajukuu 5
MIJEDA: NOOOOOOO WAAAAAAY,
unadanganya!
Money Stars: nina miaka 48
MIJEDA: huo uongo sasa
Money Stars: hii hapa
driving licence yangu angalieni
MIJEDA: wakaidaka fasta
fasta, wakaangalia kweli kazaliwa mwaka 70, duuu! Mbona mzuri hivi… dah wajanja
wanajua kuwahi na kutunza
Money Stars: Mnadhani
mkipata mwanamke mnaweza kuwapenda na kuwatunza wakifika 48 wafanane kama mimi
au mnaongea tu? Tatizo lenu nyie mnaonekana waoga hata nikiwapa mdogowangu
mtampiga mtakimbia
MIJEDA: Hapana Dada, tupe
tu! Lakini Dah shemeji huyo tunaomba ututambulishe maana sio kwa uzuri huu
utadhani una miaka 25?
Money Stars: ahahahahahha,
ila kwa kujibu Maswali yenu ni kwamba hakuna uzuri wa mtu kumzidi mwingine kila
mwanamke Mungu kamuumba Mzuri na ana utamu wake! Ni kwamba nyie wote
hamjakutana na wake zenu, mkiwapata hata akiwa albino mtasema ni mtamu kuliko
mwenzake!
Ni muda tu ukifika
hamtaongea kama mnavyoongea sasa!
Mwisho wa siku mtaendelea
kubadilisha mabucha wakati nyama ni ile ile!
MIJEDA: basi tunaomba
utusaidie namba ya wadogo zako kama hutojali maana kama dada mtu yupo hivi hao
wadogo sijui itakuwaje!
Wote: tukacheka, na
kuendelea kuongea pale, Money Stars akawaahidi kuwapa wadogo zake ambao hana
kama wataonana tena, wote wakabadilishana namba na Money Stars, wakarudi kukaa
kwenye kochi zao wakiamini kabisa atawapa wadogo zake.. sisi tukaendelea na
maongezi yetu!
Money Stars: mama mbona waonekana umechoka au shem karudi nini?
Money Stars: mama mbona waonekana umechoka au shem karudi nini?
Grace:
goooooooooooooooooorl, goooooooooorul! Acha tu nipo na wadogo zako hapo
nyumbani kwangu natamani hata kuhama mtaa, nikamweleza A to Z za yaliotokea…
nikamwelezea kuhusu Shogangu Ulumbi… nikamwelezea kuhusu Harrieth… nikaja
kumwelezea kuhusu shemeji yangu pasua kichwa anaitwa JITU!
Money
Stars: JITU MANYANGA?
Grace:
Yes unamjua?
Money
Stars: kakutaka au?
Grace:
of course nikamkataa
Money
Stars: Unakataa hela?
Grace:
hey! Embu nambie kwanza umemjuaje JITU
Money
Stars: hakuna asiemjua JITU, we mwulize JITU kuhusu Money Stars atakueleza
nilichomfanya!
Grace:
ulichomfanya?
Money
Stars: nishakula hela zake sana hakuna bwege kama Yule! Kabla hajamuoa huyo
shogako ULUMBI, Yule bwanake alikuwa anataka kunioa mimi
Grace:
oh nooo! Kwahiyo na wewe ushapita kwa JITU
Money
Stars: unataka niongee au utaongea wewe?
Grace:
basi endelea mama
Money
Stars: Yes nilishmdate JITU miaka ya zamani kabla sijaolewa, kwao wazazi wake
wanahela chafuu, Jitu kwao wana hela mbayaaa,
Bikra ya kwanza JITU nimetoa mimi upoo?
Grace:
Money staaaars! Wewe wa kumtoa JITU BIKRA si amekuharibu?
Money
Stars: kaniharibu?
Grace:
ina maana wewe una bwawa?
Money
Stars: skuelewi unaongea nini anti bwawa ndo kivipi?
Grace:
kwani hujui kuwa JITU ana machine kama ya PUNDA? Ameliza kila mtu kuanzia
mkewe, Harrieth mpaka marafiki za binamu yangu!
Money
Stars: ahahahhaha kumbe ni JITU makubwa! JITU katoa wapi dude kubwa?
Grace:
kwani zamani alikuwa na bamia?
Money
Stars: ndio tulichoachania nacho!
Grace:
heee!
Money
Stars: habari ndo hiyo!
Grace:
nimechanganyikiwa jamani embu rudia tena
Money
Stars: bwana unanichosha! Unanilipa au ujue me nina uchaga nusu!
Grace:
how much unataka?
Money
Stars: unauhakika unaweza kunilipa?
Grace:
taja bei
Money
Stars: Milion 5
Grace:
unakichaa
Money
Stars: unataka ukweli?
Grace:
sina hela
Money
Stars: kachukue kwa jitu
Grace:
nooo sio kwa lile punda
Money
Stars: akanipokonya simu yangu, ukitaka nimfanye JITU aache kutesa watoto wa
watu nahitaji Milion 5 nitakusaidia, akaanza kutafuta namba ya JITU akasevu kwake,
akatuma sms kwa JITU akahakikisha imeenda akanirudishia, ole wako utume kingine
nasubiria jibu ndio nikuhadithie
Grace:
nikachoka huyu mwanamke sijui vepe ananiharibia, kucheki nikakuta kaandika - MoonLight
Lady – 1985
Nikiwa katika
kushangaa, mara simu ikapigwa nikaitupa kwa Money Stars, haya sasa ongea nae
anapiga
Money
Stars: akapokea,
JITU:
Money is this you?
Money
Stars: I miss you!
JITU:
what? How? Si umekufa wewe?
Money
Stars: Sijafa!
JITU:
haiwezekani na kaburi lako wamenionyesha
Money
Stars: kwani huyu unayeongea nae ni nani?
JITU:
Grace unanichezea akili au?
Money
Stars: wala huhitaji kujichetua,
JITU:
Siamini Money Stars kama upo live
Money
Stars: nipo
JITU:
nataka kukuona!
Money
Stars: haiwezekani
JITU:
Kivipi?
Money
Stars: Dola laki 1 kuniona
JITU:
Sielewi
Money
Stars: unakumbuka ile joint akaunt tulifunguaga pamoja?
JITU:
ndio
Money
Stars: kaniwekee dola account yake ninayo unabadilisha tu pale kwenye…. Kila week
weka dola 5000 zikishafika dola laki 1 nakupigia kwa namba yangu uje kuniona..
nikakata simu
Grace:
macho yanamtoka, JITU akapiga tena, Money stars akachukua simu yangu akaiblock
ile namba,
Money
stars: hama namba kesho sawa?
Grace:
siwezi hama namba
Mone
Stars: tena hama namba andikisha jina la mwanao Yule wakike usiandike lako huyu
mjinga ataenda kukufuatilia
Grace: unajua umeniudhi leo umeniletea makesi ya kijinga mimi nina matatizo ya kunitosha
Grace: unajua umeniudhi leo umeniletea makesi ya kijinga mimi nina matatizo ya kunitosha
Money
Stars: hayanihusu matatizo unayalea mwenyewe na ukiendelea kukaa na hio namba
huyu mjinga atakusumbua mpaka kwanza ataanza kukutrack simu yako kila ukienda
anajua hama namba nakuambia yani kama mimi wewe leo leo ningechomoa nikaitupa
kwenye sinki la chooni hapa hapa
Grace:
unajua nimekasirika
Money
Srats: dola kai 1 kwa rate ya leo inasoma tsh 2200 kwahiyo nitapata million 220,000,000.
Grace:
hawezi kuweka!
Money
Stars: umemzaa au?
Grace:
hapana
Money
Stars: Mbona unamsemea?
Grace:
hela nyingi sana
Money
Stars: hela zangu au zake? We inakuhusu nini?
Grace:
unajua Yule ni free mason, kila mtu anaeshika hela yake lazima ailipe!
Money
Stars: na mimi ni Free Jesus, aje na makorokocho yake name nakuja na Damu ya
Yesu
Grace:
Damu ya Yesu haifanyi kazi kwa wapiga panga kama wewe
Money
Stars: Yesu mwenyewe alisema muwe wajanja kuliko nyoka! Sasa kama JITU ni nyoka
mimi zaidi ya nyoka!
Grace:
sasa nikishachomoa line
Money
Stars: kwanini hujampiga hela zake lkn?
Grace:
sina tama
Money
Stars: ndio maana umebakia na shida zako, doh, kazi huna, hela huna, umeachika,
upo upo tu
Grace:
sasa unavuka mipaka
Money
Stars: nisipovuka mipaka utakuja kuhamia kwangu, wewe una miaka 33 hujisomi
unajidai umeokoka umekuwa fala kabla hujaokoka! Si bora urudi kuwa wa zamani? Alafu
unaokokaje hauishi na mumeo wa ndoa
Grace:
haya hayakuhusu
Money
Stars: alafu mwisho leo kuniomba hela ya rent kama unaniambia hayanihusu
Grace:
poa
Money
Stars: Ngoja niondoke nirudi kwa mume wangu, wengine tunachunga ndoa zetu maam
nakushauri uchunge na yako.. akaondoka ameniachia matatizo juu ya matatizo hata
kurudi nyumbani naogopa!
Nikakaa
pale kama lisaa limoja natafakari maneno yake, akaja waiter nikalipa hela yangu
nipo tayari kuondoka mara namwona JITU huyo anaingia mwenyewe kama anatafuta
mtu!
Doh
Grace kidogo ninye, nikainama, akapita akaenda chooni nikakimbia nikatoka, nipo
kwenye lift nikakumbuka kuchomoa like, dah nikachukua peni fasta nikajiandika
namba ya simu ya mume, mama na baba nikazima simu nikachomoa line lift
ikafunguka nikaitupa line ndani ya lift nduki, nikaingia kwenye gari, ile
natoka namwona JITU anashuka kwenye lift ameshikilia sim card anacheka doh
Money Stars noma, pa kwenda sina naona kama atanikamata JITU, nikaenda moja kwa
zote kwa Money Stars, kufika mumewe anashangaa vepe Grace mbona umetujia usiku
wa saa 7 kuna nini?
Grace:
namtafuta mkeo
Money
Stars: mama umekuja kunitukana na kwangu?
Grace:
amenifuata Yule mtu
Money
Stars Mume: nani anakufuata?
Money
Stars: mmh! Haya twende ukalale, huyu amelewa mume wangu twende huku
Nikapelekwa
chumba cha kulala, Money Stars ananivuta na kunifinya ole wako uongee chochote
kwa mume wangu ntakuchinja stupid girl! Kufika chumba cha wageni nikatupwa
kwenye kitanda kama gunia, asubuhi mume akiondoka tutaongea lala, akachukua
simu yangu akaondoka nayo!
Grace:
sikujua saa ngapi nililala lakini asbh niliamshwa kama nipo jeshini nimemwagiwa
maji ya bariiidi dah na zile hangover za jana nilitamani kulia… bibie amesimama
mbele yangu ameshikilia Panadol
Money
Stars: Meza hizi dawa, una masaa 3 kukaa kwangu uondoke
Grace:
nikafanya kama alivyotaka, nikaingia kuoga kurudi nakuta ameniwekea mfuko, gauni
na kikoti, nikavaa nikakusanya virango vyangu huyo nikajongea sebuleni
Money
Stars: chai hii kunywa uondoke!
Grace:
nikakaa kunywa chai maskini
Money
Stars: simu yako nimeitupa, hii simu nyingine na line kanunue kwa jina la
mwanao, umeniingiza kwenye matatizo mimi nilishakufaga mwaka 90 sasa ole wako
ukaongee kwa mtu yeyote…
Grace:
macho yananitoka kuangalia ni Iphone6s.. simu ambayo nimeitamanije, sijawahi
kuwaza kuimiliki na hizi ni Milion5,
Money
Stars: Pale ulipo umeshahama. Taxi ikija itakupeleka… ukifika mwulizie… mwambie
nimekuja kwa ajili ya nyumba… utakaa hapo mpaka nikwambie uhame… Yule JITU ameshaweka
dola 5000 kwenye akaunt leo asubuhi.
Binamu yako
nimeshaongea nae leo asubuhi nimemwambia umesafiri simu umepoteza kama kuna
chochote ongea na mimi, virago vyako vipo kwenye gari yangu taxi ikija
utahamishia, hamna kuwasiliana na mtu zaidi ya mumeo, wazazi, mtoto na mimi..
Harrieth mpotezee kwa sasa na Ulumbi..Ukiharibu usikanyage kwangu nitakufukuza
kama mbwa hunijui ee?
Grace:
macho yananitoka najiuliza bado naota au nimeamka!
MWAKA 1985
Nikiwa na miaka 15, nilikutana na JITU akiwa na miaka 20
Tulipendana sana, tukakaa kwenye mahusiano miaka 2 mechi
zote tumepigana lakini hakuwa na PUNDA nashangaa umenionyesha kituko jana
kwenye simu sijaelewa katoa wapi, nikajua tutaoana, sikumoja akanikaribisha
kwao nikapokelewa vizuri na Mama yake akanipenda sana ila Baba yake sikumwona
niliambiwa amesafiri kikazi.. kwao kulikuwa kuzuri mno kama ulaya ndogo!
Tukawa kwenye mahusiano yeye yupo Chuo Kikuu Mlimani mimi
namalizia form 6 Tambaza High School,
Shule ilipoisha na kumaliza mitihani mimi na mashosti zangu
tukaenda kujirusha Mziki mambo ya Happy time, usiku wa Ijumaa tunaenjoy
groove night na nini tunajikumbushia miziki ya kikwetu kwetu old school Fulani hivi
amaizing… Mara akaja Baba m1, akakaa pembeni anatuangalia tunavyoserebuka! Mimi
sikumwona na siku hio JITU hakuwa na mimi nilijiiba na marafiki zangu tukatoka,
JITU alikuwa na pepa ya j3 yake nikaona nisimsumbue!
Lile
libaba likaja moja kwa moja kwangu,
Baba:
hey you
Money Stars:
Hi (Ya Mkato)
Baba:
naomba nicheze na wewe, maana katika wadada wote hapa mimi nimekuona wewe
tu,
Mashosti:
aaaaah embu kwenda zakoo
Baba wa watu haogopi wala
nini, kaning'ang'ania mpaka nikaenda kucheza nae
Nikiwa nainuka Yule Baba akawaambia
she's my moonlight lady, hata sijali mtakachosema:
Mashosti wakawa wanacheka
Hapo nimevaa bonge la
umini, baba amekolea anacheza mara anishike kiuno basi vurugu. Tukacheza mziki
wa Moon Light Lady wa JULIO IGLESIAS
Tukiwa tunacheza akaniambia
jina lake Mr Manyanga! Sikuelewa hilo jina maana sikuwahi kujua kuwa jina la
JITU ni Manyanga, aliniambia anaitwa JITU Peters!
Nikamwambia nashukuru
kukufahamu Mr Manyanga,
Mr Manyanga: wewe ni
msichana mzuri sana, nimekuona tu nimekupenda, una miaka 15 tu au?
Money Stars: nikashangaa
huyu baba kajuaje umri wangu?
Mr Manyanga: nataka kukupa
ofa nzuri sana itakayobadilisha maisha yako!
Nataka uachane na mwanangu
JITU
Money Stars: nikasimama
kucheza, unasemaje we baba?
Mr Manyanga: umeniskia
sana, narudia nataka uachane na mwanangu JITU
Money Stars: kwanini?
Mr Manyanga: Mwanangu
hawezi oa kwenu! Ndoa yake ilishapangwa mud asana akimaliza shule nampeka
Uingereza anaenda kufundishwa kitajiri, wewe ndio unamzibia bahati yake
Money Stars: Nikataka
kuondoka akanishika mkono kwa nguvu, kama unataka kubaki mjini nifuate!
Money Stars: kuangalia
pembeni naona ma-body guard wanamsubiria nikajua leo nafwa maana hata nikipiga
kelele haisaidii kuna mziki mnene!
Nikaongozana na Yule mzee
mpaka alipokaa, akachukua kitabu chake cha benki akaniuliza ulishatamani kuwa
na hela kiasi gani kwenye maisha yako?
Money Stars: mbona
sikuelewi baba kuna sehemu nimekukosea au?
Mr Manyanga: Taja au
unataka nikuondoe bila malipo sina muda wa kupoteza! Huyu ni mwanangu wa pekee
wa kiume na hakuna kitu kitakachoingilia na mipango yangu!
Money Stars: Nataka
Mr Manyanga: Yes ngapi?
Money Stars: nampenda sana
mtoto wako siwezi kuondolewa kwake kwa pesa, upendo wetu hauwezi kununuliwa kwa
pesa wala mali
Mr Manyanga: Jitu anajua
upo hapa na mimi?
Money Stars: hapana
Mr Manyanga: kwahiyo
umemdanganya? Ina maana humpendi mwanangu
Money Stars: ana mitihani
j3
Mr Manyanga: milioni ngapi
kuondoka kwenye maisha ya mwanangu?
Money Stars: Milion 800
(Niliitaja nikijua hana)
Mr Manyanga: akaandika
cheki 10, kila moja ina million 80 nikajua huyu anazingua haya makaratasi tu na
mimi najuaje kuhusu pesa ndio kwaaanza nimemaliza form 6 cheki hizi sijui
kutumia
Mr Manyanga: akaunt namba
yako mpya ni hii, kila baada ya miezi 6 peleka cheki moja moja watauliza
waambie nimetumwa na Mr Manyanga
Money Stars: kama ya uongo
je?
Mr Manyanga: uje nyumbani
kwangu unishitaki kwa mke na mwanangu, sijawahi kuwa mwongo ni vile hunijui
Hizi hela ukizitumia vizuri
utasoma kokote Duniani na utafanya biashara yeyote Duniani
Na ukitaka niwe referee wako
maishani mwako niambie
Ila kaa na mwanangu mbali
Money Stars: plz naomba
basi niwe nae mwisho mwisho amalize mitihani yake tafadhali
Mr Manyanga: sawa, na
ukijibebesha Mimba utaniona kwa rangi nyingine
Money Stars: ivi namuachaje
mtu nimependana nae?
Mr Manyanga: akimaliza
mitihani, mwambie aje Hotel Kilimanjaro, chumba namba… tutakuwa wote,
atatufumania, atakasirika atakuacha na wewe utaondoka
Money Stars: kuna msamaha
Mr Manyanga
Mr Manyanga: Binti yangu
hujawahi kutana na fumanizi, maandalizi yake nitakusaidia!
Tangu hapo sijawahi kumwona
tena Mr Manyanga, nachojua nilipoenda kuweka cheki ya 1 ikakubali na ile akaunt
ya benki alinifungulia ilikuwa ya kweli maskini, nikawekewa hela zangu za
kwanza mil 80 zikaingia ndani ya miezi 2… sikuamini, nikaenda kutoa laki 2
sikuamini.. kweli kuna MaDON sikuwahi kuamini!
Nikarudi nyumbani kumweleza
sista wangu akaniambia hapo hapo kwani Tsh ngapi?
Usiku wa Tukio la kufumania
ukafika bwana, hapo kweli ndio niliona rangi nyeusi ya Mr Manyanga!
Kweli JITU akaja kweli
akatufumani kama Baba yake alivyopanga, JITU alikasirika sana, akaniuliza
kwanini baba yangu? Nikamwambia hauniridhishi kama Baba yako, Baba yako ana
Machine kubwa wewe una ndogo siwezi tena,
Jitu alikasirika, akaanza
kupiga vitu anatupa meza, anarusha chupa, mimi nalia maskini JITU, Baba yake
akavaa pensi akashuka kumshika,
anambembeleza, mimi nikanyata nikavaa nguo fasta, ile nataka kutoka
nikashikwa na JITUu nikapigwaa Baba yake amekaa pembeni anavuta sigara,
nilipigwaa mpaka nikazimia, ndio babake akainuka, akamzuia, kunishika
akamwambia hapumui mwanangu umeua!
JITU: akachanganyikiwa
hakuamini, mimi nimekaza roho sipumui si moja ya mpango, Baba yake akamtoa
haraka, nenda kaite mabodi gadi, wakaja JITU kachanganyikiwa, Mabodi gadi
wakanitoa fasta kama napelekwa hospitali, JITU na Babake haooo wakaondoka..
mimi nikashushwa kwa sista, yeye na babake wakaenda kwao!
Mr Manyanga akatengeneza
msiba feki uswazi akamwonyesha mwanae, mwanae akaenda kutoa pole zake
akaondoka, baada ya mwezi mmoja JITU akaonyeshwa kaburi na babake pale Kisutu
kwa nyuma makaburi ya Upanga! Kaburi feki limetengeneza na jina langu kabisa!
Ndio JITU akaamini
nimekufa, shule yake iliisha akaondoka kwenda kufanya Masters Uingereza na mimi
nikaenda kusoma Marekani kwa Dada yangu!
Aliesimamia Visa ya
Marekani ni Mr Manyanga na Bank statement alitoa Baba Yake JITU!
Stori ya alimuoaje Ulumbe
anayo mwenyewe JITU, utafuatilia kwa muda wako..
Na hilo dudu atakuwa
ameongezea alipoenda kusoma Masters nina uhakika, nadhani ameongeza kwa
kunikumbuka! Ahahahahah JITU BWANA! Ameenda extra mile kuwakomesha watoto wa watu!
Akijua sikufa anaweza akaua mtu asee!
Yule bwana bado ananipenda
mpaka leo kaweka hela natamani sana kuonana nae ila ndio mume asijue!
Sasa wewe unataka
kuniharibia kuwa nimefufuka, unataka kuua wazee wa watu au?
Grace: JITU amejuaje akaunt
namba yako?
Money Stars: Baba yake
alifungua hio akaunt alifungua zinafanana
Grace: Moon Light Lady
maanake nini? Kwanini umeandika Moon Light 1985 Akakumbuka na kupiga?
Money Stars: Tulifahamiana
1985 na kupendana na huo wimbo ndio ulikuwa wimbo wetu tunaupenda, tulionana
wakati huo wimbo unapigwa mziki!
Baba yake alifanya kukopi …
sijui Yule Mzee Manyanga bado yupo au amekufa sijamwona miaka 30 sasa!
Taxi imeshakuja mama
tutawasiliana ukishapata namba nipigie!
Grace: nikaondoka nimejaa
stori za ajabu kichwani nimechanganyikiwa naona dah mbona kama ni uongo lakini
kama ukweli!
TUONANE KESHO TAR 27 SEPTEMBER 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
_______________________________________________________
D. KUTAPELIWA KIMAPENZI
Grace
mimi nikakaa benchi kwenye nyumba nisioijua miezi 6, Kazi yangu ni kuangalia
Tv, kusikiliza Redio na kulala…kila week Money Stars anakuja ananichungulia
naendeleaje analeta msosi anarudi kwake.. sijakanyaga kwenye nyumba ya ibada
nina miezi 6, uzuri kila siku nawasiliana na mtoto wangu.
Kazi mkataba
umeisha, Ile hela aliokuwa anawekewa Money Stars na JITU ndio nilikuwa nalipwa
mshahara mimi na kuzidi ijapokuwa sikuwa napewa hela yote kwahiyo muda mwingi
nilikuwa nakaa ndani kama mwali.
Ijumaa
moja jioni nikapata simu toka kwa Money Stars kuwa nijiandae kuna nguo ameiweka
Kabatini, hata sikujua ameiweka saa ngapi, kwenda kucheki ipo kiwalo kizuri
nakwambia, akaniambia nijiandae nichukue Taxi tuonane Samaki Samaki Mbezi
Beach.. nikafanya kama alivyonielekeza, nikatua Samaki Samaki natetemeka sijui
kuna nini… nikiwa nashangaa shangaa gari ikaja miguuni mwangu ikasimama, mara
simu ikaita, kupokea naona ni Money Stars, ananiambia Ingia ndani ya gari!...
mmh nikasita sana akaanza kunitukana kama kawaida yake, nikaingia ndani
kuangalia ni yeye kaka siti ya abaria ya mbele
Money
Stars: sasa unaogopa ogopa nini, huniamini au?
Grace:
Kimya!
Mara
simu ya Money Stars ikaita akapokea akaweka Loud Speaker
Money
Stars: enhe?
Simu: We Mchawi ipo wapi?
Money
Stars: shida?
Simu:
Tupo Serena njoo,
Money
Stars: poa
Tukadondoka
mpaka Serena Hotel, gari ikaondoka tukaingia ndani, kufika nakutana na wadada,
wadada visuuu balaaa, doh! Hawa wadada nawaonaga kwenye TV kama sio magazeti
yale ya SANI! Wazurije! Mimi mwenyewe nasubiria sanaaa, nikawapenda bure, tukasalimiana
alafu tukakaa
Wakaongea
na Money Stars weeeeee, yani huwezi amini maongezi yao, wana majeraha mtindo
mmoja, topiki iliokuwa inaongelewa ni matatizo ya wanaume!
Dada wa 1: wanaume
hata siwaelewi Money Stars, nipo na mume wa mtu ni wapenzi wangu tuna kama
miaka 3 sasa, amenipangia nyumba hapo Mikocheni, yeye anaishi Upanga na mke
wake na watoto 4… ameninunulia gari, analipa kodi ya nyumba, ndio nina kazi yangu lakini kila mwezi
nawekewa hela kwenye akaunt yangu sio chini ya million 3…
Money
Stars: du! Sasa shida iko wapi mke wa pili? Au unataka
ndoa?
Dada wa 1: Sitaki ndoa mimi, sio kwa hizi stress…
Siku 1 akaja kuniambia anataka nimpe michezo ya Sodoma na Gomora! Hapo ndio niliona Dunia imebadilika rangi na jua limekuwa jeusi, miaka 3 hajaniomba michezo ya kipuuzi leo hii ameamkia wapi na kutaka kuniharibu?
Dada wa 1: Sitaki ndoa mimi, sio kwa hizi stress…
Siku 1 akaja kuniambia anataka nimpe michezo ya Sodoma na Gomora! Hapo ndio niliona Dunia imebadilika rangi na jua limekuwa jeusi, miaka 3 hajaniomba michezo ya kipuuzi leo hii ameamkia wapi na kutaka kuniharibu?
Yani
nimechoka mazimaaa! Nimekataaa wanaume weeengi kisa upendo wangu kwake na
kukubali kuwa Mchepuko wake (Side Chick) alafu ananiletea habari za kiduwanzi
kaniudhii!
Money
Stars: ahahahahahha ukamfanyaje baada ya kuudhika?
Dada wa 1:
Nikamfukuza nikamwambia akiendelea kuniletea habari za kishetani naondoka
kwenye maisha yake… hapa nina stress akiondoka life style yangu ya maisha
inabadilikaje! Sijui nafanyaje unanisharije Money Stars?!
Money
Stars: Du! Hapo pagumu! Ngoja nisikilize wengine
nitakujibuni wote!
Dada wa 2: Mimi matatizo yangu kama ya bishouger! Lakini natofautiana kiduchu sana, Hapa nilipo nipo na waume za watu 2,
Wote:
wakamuangalia kwa mshangao!
Dada
wa 2: Mtanisamehe wamejileta wenyewe sijawafuata, mmoja
wa mahitaji yangu ya kila siku mwingine wa maisha yangu ya ziada ya hali ya juu
(exclusive life)... Nikawapanga hawajuani wote !
Sasa
juzi kati nikaja kufumaniwa na wote wawiliii,
Haikuwa kasheshe kama mnavyodhani, tukaongeaaa kikubwaaa nikawaambia ukweliii, wote wakataka walale na mimi ili waniaonyeshe nani mkali halafu ataniachia nichague mojaaa, katika mechi heeee nashangaa nataka kuliwa Sodoma, weeee nilicharuka na mashetani yangu ya kichaga hakuna mfano ...
Tulivyoishia hakuna hata m1 aliepata huduma mpaka leo nakuadithia sina mawasiliano na wale watuuu, nina wiki 1 ila hapa nishapanikiii... sijui shetani gani wa sodoma amepita huku Bongo mbona wanaume wanaudhi hivi?
Haikuwa kasheshe kama mnavyodhani, tukaongeaaa kikubwaaa nikawaambia ukweliii, wote wakataka walale na mimi ili waniaonyeshe nani mkali halafu ataniachia nichague mojaaa, katika mechi heeee nashangaa nataka kuliwa Sodoma, weeee nilicharuka na mashetani yangu ya kichaga hakuna mfano ...
Tulivyoishia hakuna hata m1 aliepata huduma mpaka leo nakuadithia sina mawasiliano na wale watuuu, nina wiki 1 ila hapa nishapanikiii... sijui shetani gani wa sodoma amepita huku Bongo mbona wanaume wanaudhi hivi?
Money
Stars: hao wanaume zako wameoa? Au mabachela sugu?
Dada
wa 2: Wote waume za watu
Money
Stars: ahahahahha, sawa nitarudi na kwako usijali enhe na wewe mwana yapi
yanakusibu?!
Dada wa 3: Mimi nipo na huyu alieachana na Baby mama wake, lakini ni Kipusaaaaaa (Pervert) ibilisi atarudi kwa shetani kuchukua darasa.. Tuna miezi 2 anadai azame Sodoma bila Sodoma haoni raaaahaaa ... Nimemweleza ukweli lakini bado anang’ang’ania
Dada wa 3: Mimi nipo na huyu alieachana na Baby mama wake, lakini ni Kipusaaaaaa (Pervert) ibilisi atarudi kwa shetani kuchukua darasa.. Tuna miezi 2 anadai azame Sodoma bila Sodoma haoni raaaahaaa ... Nimemweleza ukweli lakini bado anang’ang’ania
Ndio
kanipangia nyumba na nini, gari kaninunulia naishi appartment Masaki, kazi
kaweka mkono yeye nipo NG'O nalipwa mil 4 kwa mwezi, lakini all my life
hajawahi kuniambia habari za Sodoma wala nini, nilichooooka, hapa nime-give up ujana
wangu kuwa na hili bwana alafu mwisho wa siku linataka - mavi? This is
disgusting!
Money
Stars: kwahiyo hapo ndio mmekwaaama wenyewe!
Wadada: kumbe
je! Au ulitaka tutii maagizo yao
Money
Stars: me sioni tatizo hapo kabisa!
Wadada: kwahiyo unataka
tufanyaje?
Money
Stars: nyie mnataka
mfanyaje?
Wadada: wakaangaliana, hatuwezi kutoa huduma ya mavi
Money
Stars: achaneni nao basi
Wadada: Itatucost
Money
Stars: miaka yooote hio
mmekaa nao hao majinga bado tu
hamkuwa na akili ya kusevu pesa?
Wadada: kimyaa!
Money
Stars: kama hamkutumia
akili za kuzaliwa poleni, ila mimi kama dada yenu siwashauri mfanye kitu
ambacho hampendi, na msiruhusu mwanaume yeyote awaharibu! Mnaharibiwa alafu
hata hamjazaa watoto, mkija kuharibiwa huko kuzaa mtapata shida nyie, labda
mtumie C-Section lakini siwashauri, kuzaa kawaida kuna raha yake asiwadanganye
mtu!
Kwanza hawa wanaume wanataka kuwaoa au?
Dada wa 2
& 3: hawana hata mpango
Money
Stars: na nyie mnataka kuolewa
au ndio mmejitoa sadaka kwao kuishi bila kuwa na ndoa maisha yenu yote?
Dada wa
2& 3: tunataka ndoa na
watoto
Dada wa 1:
sitaki kusikia ndoa ila watoto nataka
Money
Stars: Achaneni na hao majingas,
kwanza haweawapendi, mimi nipo na Mume wangu na ndoa miaka 30 sasa … mume wangu
hajawahi kuniomba mavi hata siku moja!
Mwanaume anaekupenda hawezi kukuomba michezo michafu ya
Sodoma!..
Angalieni maisha yenu.. fanyeni yenu mbeleni mtapata
mabwana wa kuwapenda, ingawa itawacost ukiachana na mtu umemtegemea asilimia
100 ujiandae kushuka chini na kuishi maisha ya kawaida.. hao wanaume
wanawapotezea muda, yani kwanza ningekuwa mimi ningewavutia hela ndefu ya
kuwapotezea muda alafu ningesepa!
Wazuri wanazaliwa kila siku, wanawanyonya damu hao kesho
mtakuta wamewapangia nyumba vimwana wengine wazuri zaidi yenu, msibweteke kwa
uzuri mlio nao wazuri wanazaliwa kila siku, najua hamtapata shida ya kupata
watu wa kuwapenda, ila hapo mnapoishi kodi ikiisha tafuteni sehemu zenu muhame,
hao majamaa wapigeni chini, kwani wamewaumba mpaka wawaumize vichwa?!
Sawa?
Wote: sawa
Money
Stars: huo ndio ushauri wangu,
ila kama bado mnawaza kuaibika shaurienu nendeni mkatumbukizwe Sodoma muone
mbeleni mtakuwaje!..
Akili za kuambiwa changanyeni na zenu za kuzaliwa jamaa, eh
haya!
Wadada: Sawa dadaetu tunashukuru
Money
Stars: wakirudia kuwaomba tena
sodoma waambieni waende maji taka, mavi yanapatikana mengi tu pale Msasani kuna
Maji taka!
Wadada: wakacheka sana, maana hawakuamini kama ataongea hivyo!
Basi wale mabinti wakashukuru wakaaga wanarudi makwao maana
wamekaa pale muda mrefu sana, Grace macho yananitoka doh, warembo kama wale
wanafanyiwa unyama sie wenye sura kama za mamba itakuwaje?
Walipoondoka tukawa tumekaa tunaskiliza mziki, tukaagiza
chakula tukala, baada ya msosi Money Stars akaanza kuniuliza maswali:
Money
Stars: Anti nimechoka kuwa dada
wa kazi wako.. muda umefika uanze kutoka, ila kabla hujatoka lazima uelewe Yule
JITU ameshaweka hela zote kwenye ile akaunt, lakini sasa hapa usikae nataka
ukakae kwa mumeo huko Mkoa, kwani yupo mkoa gani?
Grace: anaishi Mbeya!
Money
Stars: huko hata JITU akiota
hawezi kufikiria kukupata
Grace: huko siwezi kwenda mume wangu tumeacha
Money
Stars: eh! We mbona unakuwa
mzembe wa kufikiria? kwani nimekwambia ukaishi nae nyumba moja? Kapange kwengine
lakini mkoa mmoja!
Grace: nataka kuishi dar staki kwenda huko
Money
Stars: mmmh! Ivi wewe na
bwashemeji mliachanaje.. ah ngoja kwanza niambie mlifahamianaje?
Grace: kimya!
Money
Stars: usipoongea hautasaidiwa
mama, usiri unakuumiza bora uongee tu tusaidiane! Vitu vingine nashindwa
kukusaidia kwasababu sijui!
Hivi haum-miss mumeo kweli Grace?
Grace: not a bit
Money
Stars: una bwana mwingine zaidi
ya JITU?
Grace: sina
Money
Stars: haja zako unamalizia
wapi?
Grace: nafanya mazoezi!
Money
Stars: aisee! Hata mimi
unanidanganyia mazoezi? Au ndio mnapunguzana na Yule demu anaitwaje sijui
Harrieth sijui nani?
Grace: sijawahi kuwa changudoa wa wanawake
Money
Stars: unasema umeokoka,
unaokokaje unamwacha mume? Yesu anapenda kuachana?
Grace: hapo ndio mimi tunaishia kugombana
Money
Stars: nambie ilikuwaje? Walokole
tunaowajua walokole wa kweli hawaachanagi wanavumiliana mpaka Yesu anarudi au
kifo kiwatenganishe sasa wewe mbona unatuchanganya mama? Embu kuwa mkweli
usaidikike, si umeona hawa wadogo zako na matatizo ya wanaume hayaishi, lazima
upambane… kwani wewe mwana wa Mungu roho ya Uvumilivu hujapewa na Roho
Mtakatifu? Sasa si ungemvumilia mumeo tu yaishe?
Grace: akaanza kulia.. kalia kwa nguvu kwa sauti watu wote
wanageuka kumshangaa… du kweli starehe imeingia mchanga!
Money
Stars: ohooo! mambo ya
kubembelezana nyumba za starehe tena bwana mimi sipendi jamaa si ungelia
nyumbani Grace, aya nyamaza basi! Nikambembeleza hapo mara akaja waiter kuleta
vinywaji, Grace akajifuta haraka asionekane analia, Yule waiter akamuangalia
anaona kama anamjua
Waiter: Grace?
Grace: akamwangalia, ah Mary mambo?
Waiter: poa upooo?!
Grace: yah nipo kwanini?
Waiter: sijakuona nina mwaka au ulienda mkoani kwa mumeo?
Grace: hapana nipo buzy tu na kazi
Money
Stars: Grace unamjua huyu
Grace: namjua
Waiter: mtoto wa Babangu Mkubwa huyu
Money
Stars: oh nashukuru kukufahamu
mpendwa, naona Grace hajiskii vizuri, karibu ukae mpenzi
Waiter:
hapana nipo kazini
Money
Stars: hamna neon kaa tu
umsalimie ndugu yako mimi naenda msalani mara moja nakuja!
Waiter: akakaa wakawa wanaongea na Grace
Money
Stars: nikaondoka moja kwa moja
mpaka kwa waiter mwingine, nikaongea nae nikamwulizia yule dada anaeongea na
Grace anafanya kazi hapa?
Nikajibiwa ndio tena ni dada wa muda mrefu ana miaka zaidi
ya 3
Nikamwomba sana kama nitaweza kupata namba yake ya simu, Yule
waiter akawa kama ana sita nikamdanganga nikamwambia Yule dada anaelia babake
amefariki, sasa nataka namba ya Yule bindada, nimpigie wakati shogangu hayupo
tupange tunamwekaje sawa mfiwa! Akakubaliana na ombi langu akanipa namba ya Yule
ndugu wa Grace, nikaisave nikamshukuru nikampa laki 1 mwenyewe anashangaaa tip
ya leo vipi?
Nikaenda msalani uongo na kweli nikarudi kumchukua Grace
maana pale hapafai tena! Tukaondoka nikamwacha Grace kwake bado analia
nikaingia kwangu… Kesho asubuhi nikampigia Yule waiter ndugu wa Grace kwa
kutumia namba ya Land Line, nikamwomba tuonane maana kuna dharura akajua labda
ya kumhusu Grace
Tukaonana Samaki Samaki Mbezi Beach, mwenyewe kaja na Boda
Boda ananiwahi, doh!
Money Stars: Pole mpenzi naona nakuchosha
Waiter: Hamna
vipi kuna nini mami?
Money Stars: Grace nduguyo
Waiter: Hee
amefanyaje?
Money Stars: Yupo poa ameamka poa, usijali
Waiter: oh
nimeshtuka alafu Yule kaka ulimwomba namba yangu jana aliniambia baba yake
Grace amekufa ndio maana nimekuja fasta fasta!
Money Stars: oh! Hamna bwana nilitaka tu kuipata namba
yako
Waiter: Enhe
kuna nini?
Money Stars: Kazini unaingia saa ngapi?
Waiter: usiku
saa 3
Money Stars: ok samahani nimekusumbua maana jana
ulionekana kushtuka kumwona Grace
Waiter: Yah
Grace bwana, hahah yani Yule mwanamke msiri sana
Money Stars: eti ee? Jamaan, yupo hivyo tangu zamani
au sikuhizi
Waiter: Tangu
tupo wadogo, na usiri wake ndio umemponza
Money Stars: Umemponzaje?
Waiter: wewe ni
rafiki yake?
Money Stars: hapana Grace nilisomaga nae Sekondari
tu, tumekuja kuonana ukubwani nilikutana nae anasubiria daladala nikamsalimia
nikampa lift maana mabasi yenyewe yalionekana hamna katika kuongea ongea
nikahisi ana shida, nikaenda nae hotelini nikanunua chakula, tukala, tukaanza
kuongea mambo ya zamani tangu tumeachana yupo wapi anafanya wapi
Akanieleza
tangu tumeachana mpaka pale, tumekutana, akasema anamtoto m1 ila mume
waliachana sikuelewa kwanini, wakati tunamaliza kula nikamwuliza anpoishi
akaniambia anaishi mwana nyamala amepanga, doh nilijiskia vibaya sana,
nikampeleka mpaka kwake ile nyumba yenyewe sasa anayoishi gari kwanza haifiki
ilibidi nipaki petrol station ashuke atembee!
Nikatoa kwenye
pochi mil 1 nikampa na namba yangu ya simu nikampatia nikamwambia ukiwa na
shida tutafutane me nipo tu
Tangu
siku hio Grace akiwa na shida ananitafuta,
Waiter: oh
jamaan we dada una roho nzuri! Usawa huu unampa mtu mil 1 tu kisa umesoma nae?
Money Stars: Hamna Bwana Grace tulipotezana baada ya
kumaliza Form 4 ila hatujaonana tena alikuwa rafiki yangu mzuri sana ingawa
kwao aliniambia ni mkoa
Waiter: mkoaaa?
Du!
Money Stars: anaishi wapi kwani?
Waiter: wazazi
wake wanaishi Magomeni, pale Mapipa! Grace Mtoto wa Dar ujue!
Money Stars: oh sasa kwanini alidanganya?!
Waiter: Grace
Msiri mama
Money Stars: Mume wake kwanini waliachana?
Waiter:
wameachana? Hahahaha ndio kakwambia
Money Stars: ndio amesema walizaa nae mtoto mmoja
yupo huko Mbeya
Waiter: Mbeya? Ahahahah
ivi Grace unamjua au unamsikia? Unajua nashindwa sasa kuongea ila kwasababu
unaonekana hujui kitu ngoja nikusaidie tu ila usije niletea matatizo Yule ni
ndugu yangu kabisaa!
Money Stars: Hamna neno sitamweleza
Waiter: Grace
stori yake ndefu sana, ila dah naona aibu kukueleza
Money Stars: niambie bwana nimsaidie:
Waiter: ok
ngoja nikueleze ili na wewe umjue rafiki yako!
MWAKA 1995:
Grace
alimaliza chuo, kwanzaa Grace kwao kama nimekueleza ni Magomeni Mapipa, wazazi
wake wote wapo hai, kwao walizaliwa 5, wote walishaoa na kuolewa, Grace ndo
mtoto wa mwisho pale… Grace mtoto wa Dar ujue, asikudanganye haijui Dar ni
mwongo
Grace
kama unavyomwona ni mzuri sana, alipomaliza Chuo pale Magomeni akapataga
wanaume 3 wanataka kumwoa, Grace akawakataa, Grace anapenda mambo makubwa pale
akawa anangojea apate bonge la bwana (Bwana mwenye hela), basi kwa kuwa wale
mabwana 3 walikuwa watu wa kawaida hawana hela kama anazozitaka Grace na
sijawahi kuelewa walimsomaje Grace sijui nae yule alikuwa anawaambia hata
simwelewi!
Mwisho
wa siku wale majamaa wa3 wakaja kujuana kijiweni kuwa wote walimchumbiaga Grace
wakakataliwa wakawa wanajiuliza kwa nini wakati Grace hakuonekana wa maringo!
Wakajiambia
labda kwasababu ya hali zao ndio maana wamekataliwa, wakaamua kumpanga mtu
mwenye hela, wakamchangia kweli akaenda Yule jamaa, kufika kwa Grace kuongea
nae na lile Gari la Benzi Grace akaona hapa hapa, akamkubalia, wakaenda kwenye
mahusiano Yule bwana kweli akamtafutia ajira, Grace akaona haya ndio maisha!
Yule
jamaa akawa anarudisha mrejesho kila week kwa wale waliomtuma, Yule jamaa
alipoona Grace anataka kuolewa jamaa akachomolewa aondoke! Jamaa hakuonekana
tenaaa!
Kati ya
wale wanaume 3 waliotaka kumuoa mmoja akarudi bwana, akamtafuta Grace hapo
kachanganyikiwa kweli kweli, akaja kuongea na Grace
Yule
kaka alierudi anaitwa Haji!
Akamdanganya
Grace anaitwa Innocent, lakini alirudi ana helaaa! Akaongea na Grace
kambembeleza wee Grace kweli kaona hela na magari mazuri kaka anaishi
Kijitonyama akaona eh Mungu kanikumbuka, kumbe shetani amemuandama mwanzo
mwisho
Wakaendelea
na mahusiano weee, mpaka Yule jamaa kaleta tena barua nyumbani kwa Baba Mkubwa
Grace kuulizwa akakubali, wazazi wa Grace wakamwuliza mara 3 tatu Grace akasema
sawa nimekubali!
Basi
harusi ikafungwa Kanisani Kubwaaa ukumbini tunashangaa kweli Grace Mungu
kamjibu maombi, Upo mama?
Sisi tukaserebuka
nakwambia Grace anaolewa na Bonge la Bwana! Na wazazi wa Innocent walikuwepo!
Mahusiano
ya miezi 2 ndoa ikafungwa wakaenda Honey Moon Kenya!
Kurudi
wakafikia nyumba ya Sinza, Grace kuuliza kule kwa mwanzo akaambiwa ile nyumba
haitoshi kukaa na familia akiangalia ile ya Sinza ni nzuri kuliko ya
Kijitonyama!
Wakaishi
mwezi wa kwanza, maisha mazuri, sisi tunaenda kumsalimia Grace kanunuliwa Gari
nakwambia Toyota Prado zile za kwanza kwanza sio hizi za sasa, maisha mazuri …
mwezi wa 2…mwezi wa 3… mwezi wa 4 mume akaaga anasafiri kwenda kikazi Nairobi,
hapo Grace teyari ana kamimba kachanga cha miezi 3… upo mama?
Mwanaume
akaenda akakaa miezi 3 akarudi Grace ana mimba ya miezi 6
Akaaga anasafiri
tena anaenda Uganda kikazi atarudi baada ya miezi 2 akaenda kurudi, Grace ana
mimba miezi 8.. akirudi uzuri anakaa mwezi anasafiri
Mwanaume
akaaga anasafiri mwezi m1 awahi pale Grace kabla hajajifungua!
Kweli kaenda
mwezi kurudi Grace akajifungua mtoto wa kike! Wakaishi miezi 2 ndio miezi ya
mwisho Yule mwanaume akaaga naenda Afrika Kusini atarudi baada ya wiki 1 lakini
hakurudi!
Grace
akipiga simu namba aliopewa feki haipo! Akaita wazazi akawaeleza wakaenda
kucheki kunakohusika, kumbe jina la Innocent aliloambiwa ni la marehemu
alishakufaga miaka 5 nyuma na hawana undugu wowote na mwanaume aliemuoa Grace
Kupigia wazazi
wa Innocent hamna kitu kumbe walinunuliwa tu!
Dah
babake na Grace alipaniki, mpaka akaumwa Stroke, ndio Grace kuhama pale Sinza
maana kodi ya nyumba ilishaisha kabisa, akarudi akawa analea mwanae na wazazi
wake
Kazini
kule mkataba ukaisha akatemwaaa, upoo? Baba ana Stroke, mama hana ajira Grace
chali ndio kikao cha familia kikakaliwa na ndugu zake wakawa wanamchangia Grace
kumlea mwanae na Grace akapewa kazi ya kumwangalia Baba Mkubwa na Mama Mkubwa!
Baada ya
miaka 10 kupita, Grace akiwa anatoka sokoni akamwona mtu kama Innocent,
akamfuatilia huku anajificha, akaona anaenda kuingia nyumba ya Tandale ndani
ndani..
Sikunyingine
akarudi tena pale pale akamkuta Yule Innocent, akachukua simu anataka kupiga
nyumbani anashindwa!
Ndio
akanipigia mimi, nikaja fasta, kweli kumcheki ndo mwenyewe, tukamfuatilia
tukajua anapoishi tukaenda kuleta afande raia!
Akaja akaangalia,
akacheka sana baadae akasema tutakuja kumkamata huyu Innocent tukamwulize
maswali kwa muda wetu alafu tutawapigia!
Kweli Yule
afande akafanya yake baada ya wiki tukapigiwa simu!.. kwenda tunamwona Innocent
yupo ndani, tulikusanyana kikundi, familia ya Grace yote kasoro baba yake
walimficha, Mchungaji aliewafungisha ndoa yani palijaa!
Wakamhoji
Innocent unamjua huyu dada anakataa!
Wakaanza
kumtishia akaongea ukweli wote:
Innocent: Mimi
naitwa Haji, ni Dalali pale Tandale, maisha yangu ni ya kuzurura na kuhangaika
tu! Sio tajiri kama nilivyoonekana, ila nilichangiwa na wale marafiki zangu 2
tuliokuja kulipia mahari ili tumpate Grace maana alituringia kwa hali zetu duni,
tukaamua kujiongeza!
Wanafamilia: hawana
hamu kila mtu analaani kivyake!
Akaulizwa
kwahiyo utaenda na huyu mama mkalee mtoto? Maana ulishamuoa tena Kanisani
kwanza umefanya uhalifu wa hali ya juu sana ina maana wewe sio tu tapeli wa
mapenzi bali ni jambazi wa kutupwa wewe na wenzako.
Innocent: kimyaaa!
Grace
hapo analia hali hana… ameumbukaje aibu! Aibu my dia aibu! Ameharibiwa maisha
kijinga!
Basi
wakaongea pale wazazi wakalaumiwa imekuwaje mnaoza mtoto hata kumchunguza huyu
bwana mpaka anawafanyia utapeli na nyie mpo hapa hapa Dar
Kaka
zake: wakasema kuwa walimwuliza Grace mara 3 tatu na Baba wa Grace alimwuliza
Grace akasema huyo huyo anamtaka kwa hiyo wao hawakuona haja ya kwenda
kumchunguza kokote!
Basi
Maongezi na lawama na maushauri yakatolewa pale wakamaliza, Grace akaamua
kumshitaki kwa makosa 2:
1. Kutumia
jina la Marehemu wa watu kumuolea
2. Kumtapeli
kimapenzi
Money
Stars: du! Maskini Grace! Alikubali kuishi nae baada
ya kumtoa Jela sasa?
Waiter: Wapi?
Grace unamjua unamsikia?! Yule Haji alifungwaga ujue, mpaka leo yupo jela maana
hela ya kumlipia fidia hana na wale wenzake 2 walienda kukamatwa wakafungwa
pamoja na yule Haji! Ndio Grace akatulia!
Baadae ndugu
za Grace walichanga akapatikana mwana sheria akamtalaka Yule Haji akiwa Jela, ndio
sasa hivi Grace yupo huru kuolewa na mtu yeyote!
Money
Stars: na mtoto je?
Waiter: anaishi
kwa mama yake Grace Magomeni, ndio alimchangamshaga Babake Grace mpaka kapona
stroke!
Money
Stars: ivi maneno umenieleza ni ya kweli?
Waiter:
sijakudanganya kama hauamini nakupa address ya nyumbani kwao magomeni mapipa…
akachukua karatasi akaandika akanipa
Mama chonde
chonde naomba usinitaje huko we utaangalia jinsi ya kumsaidia ila Grace yupo
Frustrated! Kwanza namba yake ya simu alibadilisha tu pale alipotalakiana na Yule
Haji!
Pili
kwenye sherehe za familia hajagi… nilishangaa kumwona juzi alikuja kwa mjomba,
hajagi ana miaka 7 sasa mwaka huu ametu-surprise alafu akawa yupo buzy na dogo
mmoja sijui wanaongea nini?!
Nikamsalimia
nikasepa zangu maana kazini nako kulikuwa kunanisubiria!
Money
Stars: asante sana ndugu.. Ubarikiwe sasa kazi hana?
Waiter:
alitafutiwa na kakake mkataba ukaisha miezi 6 iliopita!
Sijui labda
kama amepata upya hakutaka kuendelea kufanya pale walikuwa wanamnyanyasa
nyanyasa akaamua kuondoka mkataba ulipoisha!
Money
Stars: Doh! Maskini ya Mungu, dah naumia kusikia
mwenzangu amefanyiwa unyama
Na wewe
sasa umeolewa?
Waiter: ndio
mimi niliolewa na maskini mwenzangu zamani kabla ya Grace tena Grace alinicheka
sana, sasa hivi Mume wangu ni Meneja Benki na mimi nafanya hapo Hotelini,
mkataba ukiisha naacha kazi nataka nirudi kwenye biashara ambazo nazifanya
wakati nimeajiriwa, nazifanya nje ya ajira hamna anaejua zaidi ya wazazi wangu
na mume wangu.. Grace hajui plz usimwambie maana atazidi kuumia, unajua mimi na
mume wangu tumeanzia chinii, mimi nilikuwa housegirl kwenye majumba ya watu, na
mume wangu alikuwa ameishia form 6 wazazi wake wakafariki, akahangaika anagusa
hapa na pale akapata hela akaenda kusoma Cartificate mpaka Degree na sasa ana
Masters… tulioana Baada ya miaka 3 akiwa anafanya kazi dukani kwa mhindi
anatumwa tumwa usiku anaingia Darasani, Grace akawa ananicheka unaolewaje na
mtu hana maisha lakini sisi tulikuwa na malengo yetu na tunapendana!
Money
Stars: nikamshukuru ndugu ya Grace, nikampa laki 3
akaondoka anafurahi mwenyewe
Waiter: Tuwasiliane
jamani tumeshakuwa ndugu tujue jinsi ya kumsaidia Grace maana jana alikataa
kabisa kuongea na mimi kwanini alikuwa analia
Yule
waiter akaniachia mawazo sijui namsaidiaje Grace masikini na sikuelewa kwanini
alikuwa anamtaka JITU!
Kweli
baada ya mwezi mmoja wa kufuatilia Grace alipozaliwa na kuishi nikakuta kweli
taarifa za Yule Dada waiter ni za kweli, kweli alizaliwa na kuishi Magomeni; na
wazazi wake wanaishi pale pale bado!
Doh
kweli kwenye maisha hatufanani!
ITAENDELEA
TAR 5 OKTOBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
_____________________________________________________________________________________________
E. MIPANGO NA UKOSEFU WA MAPENZI YA KWELI…
“Baada
ya lile sakata la kufanya usnichi juu ya Grace nikaamua kuchanja ramani mpya
kumsaidia Grace.
Lakini
Grace bwana mimi mbona namwona kama anajua anachokifanya kwenye maisha yake?
Huu mchezo wa anti huruma naotaka kuuanzisha sidhani kama utaniacha salama
lazima kuna mjinga ataumia na Mungu anisadiei naomba isiwe mimi, nikijikuta naumia
lazima wote tuumie tu!
… unajua
mtoto wa kike usimhurumie sana, hawa watoto wa kike wanakuwaga na akili nyingi
sana, unaweza kudhani unamsaidia kumbe anasubiri kukupandia kichwani akupiku
akae juu yake sidhani kama Grace pale ana penda maisha yangu wala ya Ulumbi
shogake, ngoja kwanza nipange mipango yangu.
Aku
kwani Napata kitu gani kumsaidia Grace mtu tu ambae nilisomaga naaae zamaaaan
ya nini, ila huyu demu bwana ameniingilia sekta moja tu ambayo hata mimi nataka
kujua yalikuwaje?
Sekta
yenyewe ni JITU!
JITU
bwana nataka kufahamu tangu kuondoka amekuwa na maisha gani? Na kusikia
anaongeza machine yake hapo ndio nazidi kushangaa, why why waaaaaaaai?
Nikaendelea
kuumiza kichwa na kupanga na kupangua nikaishia kupanga Mbinu A… B… C… D… E…
F...na G ya mwisho, shughuli ya kupanga mchujo na mchekecho sio wa kitoto,
ikanichukua siku 3 mpaka 5 kupanga na kupangua!
Nilipomaliza
nikalala, kuja kushtuliwa na simu ya shostisto wangu flani hivi tulikuwaga
tunaishigi wote Upanga miaka ya zamaani za kale! Nikawa nasita kupokea maana
hawa watoto wakipiga simu buana hawamalizi simu itakuwa ya moto utaweka kwenye
chaji huku bado wanataka kuongea
Simu
ikaita ikakata, ikaita tena ikakata, ikaita tena kwa mara ya 3 ikakata mara ya
4 nikaipokea;
Simu: We
Mwali umefungiwa wapi? Mwingine anaongea nyuma ya simu njoo hapa we chizi wee
kalewa mbayaa, nikaona ohooo hapa kushakuja wakaniita niende huko wameweka hema
huko Sinza ndani ndani dah hapo nina usingizi balaa,
Baada ya
masaa 2 nikajongea Sinza kuniona wanalaumu wanatukana unatuweka masaa 2 kwani
sisi tupo leba tunasubiria uchungu, wanatukana dah mademu wanatukana wale
utadhani walizaliwa Kuzimu!
Sikuongea
si unanijua mimi Money Stars, kuniita unite alafu unitukane, nikawa nawaangalia
wanavyoongea wanalalamika;
Mashosti: Oh!,
hamna mapenzi ya kweli sikuhizi, wanaume wanapiga bubaaa na kuondoka,
wanatupiga mijeledi wanasepa, wanapiga Sodoma wanacheua, wanakupiga round 3, 4
mpaka 7 wanahakikisha wamekuweka sawa kuja kushituka wameshasepaaa unaachwa kwenye mataa
ukiwa na matumaini upo kwenye mahusiano, kwani wanaume wamekuwaje lakini?
Mwanaume akianza na wewe anaanza kwa moto mkali anakufukuzia mpaka unanyegeka, mkishakuwa kwenye pick season yani honemoon stage, love on cloud 9, na akishajua tu unampenda anaanza kupunguza mapenzi mdogo mdogo mpaka anapotea. Hamna real love anymore ni drama all the way, natamani ningezaliwa miaka ya 60' or 70's kule angalau wanaume walikuwa wakweli sio mijambazi ya miaka hii.. yani wanaume wa Kibongo matatizo mwanzo mwisho.
Shoga Naive: Lakini Mapenzi ya kweli yapo jamaa, yapo hata sasa..
Shoga Alievurugwa: Mapenzi ya kweli yapo kwenye sinema tuu, Kweli nakwambia hamnaga Mapenzi ya kweli tena hata Yesu alisema siku za mwisho Upendo wa wengi utapoaaa, sikuhizi mambo ni ku-compromise na kuhemeana tu!
Mwanaume akianza na wewe anaanza kwa moto mkali anakufukuzia mpaka unanyegeka, mkishakuwa kwenye pick season yani honemoon stage, love on cloud 9, na akishajua tu unampenda anaanza kupunguza mapenzi mdogo mdogo mpaka anapotea. Hamna real love anymore ni drama all the way, natamani ningezaliwa miaka ya 60' or 70's kule angalau wanaume walikuwa wakweli sio mijambazi ya miaka hii.. yani wanaume wa Kibongo matatizo mwanzo mwisho.
Shoga Naive: Lakini Mapenzi ya kweli yapo jamaa, yapo hata sasa..
Shoga Alievurugwa: Mapenzi ya kweli yapo kwenye sinema tuu, Kweli nakwambia hamnaga Mapenzi ya kweli tena hata Yesu alisema siku za mwisho Upendo wa wengi utapoaaa, sikuhizi mambo ni ku-compromise na kuhemeana tu!
Wanaume
wanaangalia wapi pa kuhemea, pa kutulia, wapi kuna ganda la ndizi wanahemea
hapo hapo, wanaume sikuhizi wanalenga kwanza, wanatafuta mwanamke ambae kwao
ana heeeeela au mwanamke mwenye helaaaa anajibanza hapo hata kama mwanamke anasura
mbaya hajali
Shoga mwenye Hasira: Naive Shoga embu twambie, unamjua nani ambae mahusiano yake yamebadilika kwa usiku mmoja?
Shoga mwenye Hasira: Naive Shoga embu twambie, unamjua nani ambae mahusiano yake yamebadilika kwa usiku mmoja?
Nani?!
Hapo
shoga mwenye hasira kanuuuuuna, kaviiimba usoni kafura hasiraje? uuuwi!
Naive Shoga: kweli Mapenzi ya kweli yapo unajua imetokea kwa shoga yake shogangu Kelly, wanaishi happy ever after ….kweli jaman kweli
Shoha Mwenye Hasira: yah ni kweli kweli kabisa, yani sikuzote ukisikia kuna mapenzi ya kweli utaambiwa ilitokea kwa rafiki wa rafiki ya rafiki unaemjua!
Naive Shoga: kweli Mapenzi ya kweli yapo unajua imetokea kwa shoga yake shogangu Kelly, wanaishi happy ever after ….kweli jaman kweli
Shoha Mwenye Hasira: yah ni kweli kweli kabisa, yani sikuzote ukisikia kuna mapenzi ya kweli utaambiwa ilitokea kwa rafiki wa rafiki ya rafiki unaemjua!
Nakwambia
hapo utaambiwa walikutana kwenye mvua wakapendana waka-kiss, sikunyingine
wakakutana kwa maua wakafanya na picnic wakala, wakanywa, jua lilipozama
wakakimbia kuelekea jua linapozamia.. hizo ni stories kama sio movie …. Kwenye
maisha ya kweli hamnaga kitu kama hichoo … ukitaka tukuamini tuambie nani mahusiano
yake yalibadilika mara moja!
Naive Shoga: Money Stars hapa!
Money Stars: Nikashtuka! Mimi? Kwanini mimi?
Naive shoga: Angalieni maisha ya Money Stars na Bwana wake Handsome!
Wote: wakanyamaza kimya wananiangalia Money Stars!
Mimi nipo buzy nawaza, je ni kweli hamna Mapenzi ya kweli tena?
Naive Shoga: Money Stars hapa!
Money Stars: Nikashtuka! Mimi? Kwanini mimi?
Naive shoga: Angalieni maisha ya Money Stars na Bwana wake Handsome!
Wote: wakanyamaza kimya wananiangalia Money Stars!
Mimi nipo buzy nawaza, je ni kweli hamna Mapenzi ya kweli tena?
Money
Stars: Bwana embu niacheni na ndoa yangu, mnavyoiona
kwa nje ndio ivyo ivyo hamuijui, kwahiyo mimi sina cha kuwaeleza, tatizo lenu
nyie mnapaniki sana, yani akili zenu zinatafuta, zipo kwenye mawindo ya kupata
mapenzi ya kweli, kwanini msijikite kwenye maendeleo?
Maendeleo
ya Binafsi maendeleo ya jamii maendeleo ya familia maendeleo ya ukoo, kuweni
buzy na mambo tofauti na mapenzi muone kama mtawakagua wanaume na tabia zao…,
mimi nipo buuuzy na kazi zangu, nikirudi nyumbani nimechoka, au nisipotoka nipo
buzy nafanya kazi zangu nyumbani..
Kwanza
nyie wote hapa mna AJIRA, kama ajira zenu mmezizoea si mtafute kazi zingine
ambazo zinawapatia changamoto zaidi kwenye makampuni mengine?
Au kama
kupata kazi nyingine ni shida, basi fungueni vioski vyenu ambavyo vitakuja
kuwasaidia baadae mkiacha kazi au mkistaafu.. mtumie huo muda wa bure mlionao
kazini kupanga maendeleo yenu.
Sasa
kama muda wooote mnakuwa na stress za wanaume, wanaume, wanaume kila saa
wanaume wamekwenda mbele wamerudi nyuma huko kwenye ajira mnafanya kazi za watu
vizuri kweli au ndio mnalipua?
Sidhani
kama mtu akiwa na stress za mapenzi hata kazi zinafanyika, mimi naona kama
mnawaibia waajiri wenu mnaenda ofisini kuweka saini ili mwisho wa mwezi mlipwe
mshahara namna hii mtaishia kuwa na performance mbaya ofisini na kufukuzwa
kazi.. sasa ufukuzwe kazi alafu na stress za mapenzi juu si mtajiua nyie? Acheni
ujinga, nyie ni watu wazima wote hapa endesheni maisha yenu kiutu uzima!
Wote: Kimyaa!
Money
Stars: Huo ndio ushauri wangu kwenu!
Wote: Lakini hatujui kuhusu Biashara sisi akili
zetu zote zimeshalala kwenye ajira!
Money
Stars: kwahiyo mnasemaje sasa?
Wote: labda utusaidie cha kufanya utupe aidia ya
Biashara!
Money
Stars: Nikawauliza wanapenda kufanya kitu gani nje ya
ajira, kila mtu akataja yake, nikawashauri wafanye biashara ya vitu
wanavyovipenda itawasaidia kuifanya kwa moyo zaidi hata kama wakikutana na
changamoto watajua kuikabili maana ni biashara wanayoipenda!
Wote: sawa
shoga, lakini sasa hela hatuna
Money
Stars: Hee?! Mmekaa kwenye ajira mnakula
mshahara wote mnatumbua tu hamsevu hela?
Wote: Kimyaa!
Money
Stars: ndio maana basi hao wanaume wanawakimbia, yani
nyie majinga kweli, mkipokea hela tu mnaweka kwenye tumbo, hamjui cha kulipa
kodi ya nyumba, umeme, maji, mafuta kwenye gari si ndio?
Wote: ndio
maana wanaume wapo!
Money
Stars: sasa kama wanaume wapo hizo hela zenu
mnapeleka wapi? Au mnajenga makwenu?
Wote:
hatujajenga!
Money
Stars: kwahiyo nyie hamna tofauti na magoli kipa
sio?
Wote: sasa
unatutukana sisi tuna kazi zenu
Money
Stars: mmekaa kazini miaka mingapi
Wote: zaidi
ya 5
Money
Stars: na hamna hata 100?
Wote: kimya!
Money
Stars: kwahiyo mnataka mimi niwasaidiaje maana nondo
nilizowapa mpaka sasa mlitakiwa mnilipe!
Wote: aaah we
nae, si unatusaidia shogaetu
Money
Stars: kwani nyie shule mlisoma mpaka wapi?
Wote: chuo
tulimaliza
Money
Stars: kwahiyo nyie wote mna Degree au certificate au
Diploma au?
Wote: tuna
Diploma
Money
Stars: kweli kazi ipo!
Mnaonaje
mkijisomesha? Mkajiendeleza na elimu
Wote: oh! hapana
bwana akili zetu zimeshazeeka sisi tunawaza machine na burudani kusubiria kufa
Money
Stars: kwahiyo sasa mnataka nini kwangu maana kila
kitu naona mmeshajipangia… kama ajira mnazo na machine mnapata.. subirini kufa
msiwalalamikie wanaume
Wote: sasa
unasusa Aunty?
Money
Stars: mimi naona mnacheza na akili yangu hampo
serious na maisha yenu, ngoja mimi niondoke niende kwangu; hapa mnanifilisi na
kuninyonya damu kimaarifa na kucheza na akili yangu, mkiwa serious na maisha yenu
mtanitafuta tena mnilipe kwa kila ushauri laki 3 kwa kila mmoja tena hapo
nimewapunguzia ningewafanyia laki 5…. La sivyo endeleeni kulalamikia wanaume
mpaka mfe… mkitaka kuishi mnajua pa kunipata!
nawaambia
mkiamua kufunga milango ya wanaume mkawa buzy na kazi zenu na maendeleo yenu
mtashangaa wanaume wa maana wasio-pasua kichwa watakuja tu
Mkiendelea
kuweka vichwa vyenu kwenye mambo ya wanaume sijui wamefanyaje mtakufa mkiwa hai
mnajiona, huo ndio ushauri wangu…
Wazungu
wanasema the Opposite Attracts, unataka Mume mwema mwombe Mungu alafu
jishughulishe na mambo mengine tofauti na mapenzi, ukijikita kwenye mambo
mengine tofauti na mapenzi buzy na mambo yako mambo ya Mapenzi yatavutika kwako
ndio maana ya Opposite Attracts!
Anywho nawahi
kwangu nikaangalie familia…
Mashoga: Oh
Penny baki tafadhali tutakulipaa…utupe maujanja ya biashara na mambo mengine ya
maendeleo plz plz plz….
Money
Stars: Nikibakia hapa wekeni laki 6 mezani ndio
nabaki.. na elfu 30 ya fuel na chakula nakula hapa na vinywaji mnaninunulia
hapa…
Mashoga:
wakashauriana hapo wee wakateta amimi nipo buzy na simu, mara naona wanaingiza
mkono mfukoni, wanatoa hela, wakakusanya mmoja wao akanipatia laki 6 cash! Mwingine
anaita waiter njoo msikilize taajiri yetu hapa, mwingine anasema enhe shoga
tupe nondo mama tukawatese wanaume wametusumbua sana!
Money
Stars: Nikapokea laki 6, na elfu 30 juu ya mafuta ya
gari, nikahesabu si unanijua halfa cast wa kichaga mimi, kweli laki 6 na elfu
30 nikaweka kwenye mfuko wangu wa Jeans, Kinywaji kikaja nikaanza kunywa
taratibu, mashoga wamefungua ma-Ipad zao wanasubiria kuandika
Nikawapiga
darasa pale, warembo wakakolea, pombe zote zikaisha kichwani walizokuwa
wanakunywa wakahamia kwenye maji ya kunywa!
Darasa
nikaliendesha pale kiroho safi, tena kwa pozi na kuku choma ikaja nikaitafuna
vzuri sana, haina kuremba, naanzaje kuremba labda? Fursa ikija lazima ujitoe kimaso
maso!..
Mpaka
masaa 2 yanaisha, watu wanaliaaaa, tulikuwa wapi, jamaaani, hatuelewi, hawa
wanaume wametuloga, basi kila mtu analalamika kivyake!
Money
Stars: hawajawaloga wanaume wala nini, mmejilogesha
wenyewe kwa wanaume, kwani nyie si mnazo akili za kuzaliwa? Mwanaume ameishikiliaje
akili zenu ni nyie mmewaruhusu wawaburute ndio maana mnateseaka
Mashoga: oh
Bibie punguza basi maneno makali ujue pombe zishaisha akilini hata usingizi
hamna, wakakubali kujisomesha, kuhama nyumba walizokuwa wamepangiwa na wanaume
zao na kuanza maisha yao mapya na kufanya kazi kwa bidii maana walikuwa
wanalalamika mishahara midogo kumbe utendaji kazi wao ni mbovu…
Money
Stars: sasa wapendwa, mimi nina deal la hela, kwa
nyie mnaotaka kufanya biashara hamna mtaji hili deal litawaingizia mamilioni ya
hela mnaweza hata kuacha kazi, lakini sijasema muache kazi, nikiona unaniletea
mambo ya kipuuzi mambo ya kijinga nakutoa fasta na ukiniharibia tu urafiki na
wewe umeisha, je mnalitaka hili dili?
Wote: Leta
Pesa hio tupe tupe tuchangamshe akili maana we mtoto una akili wewe mjinga una
akili wewe embu tuamshe mama tumelala sana..
Money
Stars: lakini hamna kuacha kazi, mkiacha kazi
nawakata kwenye deal langu
Wote: eh
tukale wapi? Hatuachi!
Money
Stars: Nikawapa kiduchu cha
mipango yangu juu ya JITU, Ulumbi, Harrieth na Grace!
Nikawaeleza kiduchu kuhusu JITU na jinsi alivyowatandika
watoto wa watu na machine yake kubwa, anawaumiza vichwa wadada mjini kwa hela
yake
Shoga
mwenye Hasira: hio ndio nyama yangu
naitaka salama nimpigeee nimalizie mahasira yangu yote juu ya wanaume
Shoga Naïve: Stars hii show kali nahisi ntaishia njiani sitaweza, Punda
tena?
Shoga
Alievurugwa: Mimi show yeyote
napiga niambie nakaa mlango gani wala hutajuta! Ila mshahara ngapi mama?
Money
Stars: ELfu 30 kwa siku
Wote: Nini? Hata kazini hatulipwi hivyo
Money
Stars: lakini sio kila siku
maana mmeajiriwa hizi kazi zitafanyika usiku na weekend sana, sasa kama mnasoma
hamtaweza!
Wote: hio ndio nzuri Overtime yetu!
Money
Stars: lakini kuna jambo moja
tu!, kila weekend kabla hamjaingia kwenye kazi lazima niwape brief
Wote: sawa hamna shida Boss
Money
Stars: na tukianza hamna kuacha
atakaeacha atanilipa! Hii safari sio rahisi kama mnavyodhani jamani kweli
mtaweza?
Wote: Poa tunaweza na tutaifanya vizuri sana usijali
hatutakuangusha…
Money
Stars: ok tuonane kesho tusaini Mkataba
maana nyie nahisi mtaniharibia mbaya hasa huyu Naïve! Kesho j2 tukutane …
nitakuja na mwanasheria wangu … atawapa makaratasi mtasoma mkikubali msaini,
mkikataa poa siwafosi…
Wote: Poa Boss wetu kesho saa ngapi
Money
Stars: saa 8 mchana sharp
ukichelewa ushafeli interview
Wote: asante sana
Money
Stars: msinishukuru sasa,
mnishukuru Baadae mambo yenu yakikaa sawa, plz alafu kama kazini hamfanyi
vizuri nawatoa kwakweli sitaweza
Shoga Alievurugwa:
kwahiyo kama ukitaka kufanya kila siku
kazi kwako je tunaruhusiwa
Money
Stars: yah lakini si umeajiriwa
mama
Wote: Wakaangaliana, wakamwambia bora useme ukweli mama
Shoga
Alievurugwa: My dia, mimi kazi
sina, nimefukuzwa jana
Money
Stars: heeeee?!
Shoga
Alievurugwa: mimi nimevurugwa hapa
nina stress za mapenzi na kazi doh yani hapa ulipoongelea pesa nashukuru kweli…
kwahiyo mimi nitakufanyia kazi full time…ndio hawa wakaamua kunitoa out
wanipoze nipunguze stress
Money
Stars: doh! Hii kazi lakini poa
ila mimi silipi kodi yako ya nyumba wala hela ya usafiri, mshahara naokupa
ukutoshe
Shoga
Alievurugwa: embu ngoja, elfu 30
mara siku 30 ni Tsh laki 9 (Fair).. hamna shida nitafanya..
Money Stars: tutaonana kesho warembo, we bibie uliovurugwa
hii hapa laki 2 yako itakusaidia nauli kuja kesho na safari zingine zote,
malipo yenu ya kazi mwisho wa mwezi alafu sina huruma na kazi zangu,
ukinizingua nakudunda kweli kweli..
Wote: sawa boss
Money
Stars: tuonane kesho saa 8
mchana sawa?
Wote: Sawa Boss Lady!
ITAENDELEA
KESHO TAR 20 OKTOBA 2018 SAA 12 JIONI YA TANZANIA.
_______________________________________________
F. GANG-SISTERS A.K.A 3L…
Kesho yake saa 7 dk 45 mchana warembo wakaja
mhali tulipokubaliana… Shoga alievurugwa, shoga mwenye hasira na
shoga Naïve wamependeza wenyewe
wana hasiraje na wanaume.. ahahhaha utadhani wanakuja Beijin kupanga sheria za
Haki za akina Mama na wanawake bwana au wanakuja kuonana na Muumba kuleta madai
yao
Shoga alievurugwa:
amefunga usongo utadhani Rambo anaenda vitani, hahahahaha
Shoga Naïve amevaa Miwani asije onekana na watu
wanaomjua
Shoga mwenye hasira amevaa
jeans na lipstic nyekundu! Si unajua tena rangi nyekundu inakuwa na maana gani,
hahahah warembo wamejipangaje?! Wanasukuma masanduku yao kama wanaenda Ulaya
kumbe hapa hapa kwetu…
Mimi na Mwanasheria wangu
tulishatengeneza ramani yetu kuubwa tu, tukawa tunacheka kuwaona
walivyopigilia, wameshasahau hatuishi vitani, hawa mademu wa wapi?
Wakaja tukasalimiana na kutambulishana
nikaanza kuwatania, wenyewe wamenuna nyuso za mbuzi wapo serious wanasubiri
kusaini mikataba! Mikataba hio vipi?
Baada ya Utambulisho mrefu, wakaanza kusoma
makaratasi, kwani wanaelewa sasa? Kidhungu kitupu! Wakaomba watafsiriwe,
wakatafsiriwa uongo mtupu mimi kicheko kimenibana haki nachekea tumboni, wao
wapo makini jomooni elimu wakati mwingine usipo kuwa nayo unaumizwa vibaya mno!
Wakadanganywa hapo wakasaini kweli
Mwanasheria wangu wa kuunda unda akaondoka,
Money Stars: hawa
warembo bwana wanamajina yao,
Shoga alievurugwa anaitwa Lina
Shoga Naïve anaitwa Lola
Shoga Mwenye Hasira anaitwa Lila
Money Stars: Lina
wewe unaondoka na mimi na masanduku yako, tunaenda kwenye nyumba moja ivi,
utakuwa unaishi huko na Lola na dada mmoja anaitwa Grace… nyie wawili hamna
kuwasiliana na mabwana zenu wa zamani, mkiwasiliana nawatoa mkataba wenu na
mimi umeisha… nyie wawili namba zenu za simu ni hizi hapa na hizo simu zenu
naziomba, nikapewa simu zao nikaweka mfukoni, nikawapa mamba zao na simu zao
mpya za tochi.. wakaniangalia kama natania au nipo serious?! Kumbe mimi
nimemaliza!
We Lila, funguo yako ya nyumba mpya hii
hapa, utakuwa unaishi Kijitonyama ndani ndani huko, hamna kuwasiliana na
mabwana wako wa zamani tena, alafu mambo ya kujishaua kujiongelesha ongelesha
kwa majirani kama hauna akili nzuri, nikiskia nakutoa!
Lila kimyaaa! Baadae akajibu sawa madam
boss leide!
Tukamsindikiza Lila mpaka kwenye nyumba
yake mpya, akachoka, chumba kimoja kina choo ndani, hamna Tv hamna nini,
kalalamika mwenyewe nikamwambia hela nayokulipa nunua Tv, nunua Gari, nunua
masufuria hainihusu we si unataka ajira bwana, kwaheri, tukaondoka na Lola na
Lina haooo mpaka kwa Grace
Grace anashangaa anagongewa mlango
utadhani hajalipa kodi, kufungua nikamsukuma namwambia wasaidie ndugu zako hao
wametoka chuo!
Wakasaidiana masanduku, kila mmoja
akaonyeshwa anapolala,
Money Stars: oya! Mwisho
wa mwezi nakuja kuchukua kodi, wewe Lola andaa laki 3, Lina andaa laki 3, we
Grace andaa laki 3…
Grace: Mimi sina ajira
Money Stars: hawa
unaowaona ni ndugu zako, wamepata ajira leo, na wewe kazi nimeshakutafutia,
kuanzia kesho j3 unaanza kazi
Grace: akafuraaaahi mwenyewe, mshahara bei
gani?
Money Stars: huyu
anaitwa Lola na huyu anaitwa Lila ndio room mate zako, mkae kwa amani nisiskie
mnaibiana mabwana sijui mnapigana mkipigana tu nawatoa sawa?
Wote: sawa Boss Lady
Money Stars: we
Grace mshahara wako kwa siku elfu 10,
Grace: kazi nafanya lini mpaka lini? Likizo vepe?
Money Stars: we
unataka kazi au unataka kurudi kwa wazazi wako? Mbona maswali kama polisi?
Grace: sawa madam nakusikiliza
Money Stars: Kesho mtafute shogako Ulumbi, mwambie unataka ajira, hata
ya usafi nyumbani kwake mwombe
Grace: uuuwi Money Stars,
unanipeleka kwa JITU tena?
Money Stars: usiponisikiliza huyo JITU utaishia kubakwa kiboya boya
yani usiponiskiliza wewe utakuwa unaumizwa kila siku sasa wewe jifanye machi
nooo, endelea kuongea kama hutaki hapa kwangu ondoka usituletee usiku sina
huruma na wewe kabisa
Grace: sawa Boss Lady!
Money Stars: Kesho unaondoka na Lina muende kwa Ulumbi kesho saa 5
asubuhi anawasubiria pale The Slip Way, mkifika mwambie Lina ni mdogowako wa
kijijini wote mnatafuta ajira hawezi kukunyimeni, ila lazima mlie lie mpaka
mwisho mkijidai mmeshiba imekula kwenu na mkiondoka kwa Ulumbi hamna ajira
tusijuane!
Lina utakuwa House
Girl kwa Ulumbi na wewe Grace utawekwa kwenye ofisi ya Ulumbi,
Grace ukiulizwa
unaishi wapi mwambie unaishi Sinza na Lina ukiulizwa unaishi wapi mwambie
unaishi Mpwapwa kijijini!
Lola, nataka uongee
na Grace, akueleze kuhusu Harrieth muwe ma best, mkishakuwa ma best nipigie
nitakupa ramani
Lila ukishaenda
nyumbani mwa Ulumbi kama tulivyoongea naomba umkatalie JITU, usitembee nae
kabisa, ukitembea nae umeharibu, wewe fanya juu chini usitembee nae, kwanza Yule
bwana ana ukimwi, sasa nenda kachizike na zile hela umeumia sawa mama?
Lila: Sawa boss!
Money Stars: Na hili Body lako, sema una miaka 58, bibi wajukuu 3,
watoto wako wanaishi Arusha, mumeo alishafariki miaka 5 iliopita, mfanye JITU
awe rafiki yako na sio mpenzi wako, mshauri kwa kila kitu, akishakuwa rafiki
yako nipigie simu nitakuambia cha kufanya
Lila: sawa boss leide!
Money Stars: Lila, mama
usiharibu tafadhali tafadhali! Nakujua akili zako zimechelewa kukua, mtu
unaeenda ku-deal nae ni mwehu zaidi ya mwehu, alafu ana akili mbaya, kwahiyo
wewe nenda nae mpwela mpwela hivyo hivyo jidai akili huna zinachelewa lakini
nataka akili yako ipae, akikutukana wewe mpende, akikudharau wewe mpende,
mwisho wa siku atakuona zoba, jinga, ataanza kukutumia, ukifika hapo nipigie
simu akiwa hayupo nitakusaidia cha kufanya next!
Money Stars: nikawaaga nawaambia
mwisho wa mwezi naja chukua change laki 9 staki ujinga asietoa laki 9 namtoa!
Nikaondoka nikawaacha wanaongea wanafahamiana wanapeana majukumu.
Kesho yake saa 4
asubuhi kweli nikadondoka The Slip Way, nikaenda kujibanza sehemu, namwona
anaingia Ulumbi akakaa akaagiza kinywaji, mara akaingia Grace amevaa choka
choka Fulani hivi kumwangalia Lina sikuamini, kama kibibi cha kijijini kila mtu
anamwangalia huyu mama ametokea wapi?
Wakafika kweli
wakaongea na Ulumbi, ulumbi anashikilia pua kuashiria Lina ananuka, anamwuliza
Grace umemtoa wapi mimi mbavu sina!
Wakaongea kama lisaa
limoja, wakaondoka wote wa-3, nikawa najiandaa kutoka niondoke mara namwona
JITU na Harrieth wanaingia, wameshikana mikono wanacheka wanatembea, doh
nilisikia moyo umesimama! Jitu akiniona hapa itakuwa msala mkubwaa, nikampigia
simu Lola, akaniambia yupo maeneo ya Masaki,
Money Stars: Njoo fasta kama unajipenda,
Baada ya dk 20 Lola
akaja, akakaa kwa pembeni akamcheki Harrieth anavyojishebedua na kujichekesha
kwa JITU, akasoma ramani nzima ya pozi lao na waiter anaewahudumia, akasubiria waiter
wao arudi tena, akamfu kwa nyuma, alipofika kwa akina JITU akamkuta waiter
anamwekea kinywaji Harieth… akamsukuma waiter akamwagia Harrieth kinywaji chake
na waiter akaanguka chini,
Harrieth: akapiga makelele
nakwambia utadhania yupo labor!
Huo ugomvi wake sasa
doh!
Harrieth anatukana
mwanzo mwisho aibujeee!
Lola nae alishajiangusha
chini, JITU akamwona akaamka haraka haraka akamwinua Lola, Harrieth kanuna
anagombana na waiter watu wanawashangaa, baadae Lola akamwinua waiter akamwomba
msamaha, Manager akaja pale anaulizia ulizia kuna nini, waiter akaombwa
aondoke,
Manager anaomba
msamaha pale na nini, wakabakia Lola, Harrieth na Jitu!
Jitu sasa
anavyomwangalia Lola, utadhani sijui nini?
Lola: akaomba msamaha
kwa Harrieth, akatoa kwneye pochi yake top nzuri nzuri, pole my dia, kama
hautojali naona shirt yako imeharibika twende toilet ukabadilishe hii Top uvae
yangu sio vizuri kukaa na nguo chafu,
Harrieth
akamwangalia Lola, Jitu akamruhusu aende wabadilishe kweli ile nguo wakaondoka!
Money Stars: baada ya kuona JITU amebakia mwenyewe nikasema sasa huu
ndio muda wa kwenda kumfunga paka kengele, nikainuka na kofia yangu na miwani
uzuri meza ya JITU ilikuwa mbele yangu kwa sana, nikaenda nikachukua kinywaji
cha mtu mwingine nikatembea mpaka kwa JITU, nikasimama mbele yake hakuniona
alikuwa buzy na simu
Money Stars:
Manyanga mzima?
JITU: akainua shingo
aangalie nani huyu? Aliponiona alishtukaa, nikachukua kile kinywaji nikammwagia
machoni akaanza kuhangaika kufikicha macho mimi ndukiii, akaja Meneja nadhani
aliona, akaanza kumsaidia mimi nishafika mbali namchungulia JITU anavyohangaika
na macho!
Alipokaa sawa
anamwuliza Meneja kuna demu alikuwa hapa amenimwagia kinywaji yupo wapi?
Meneja: ameondoka Yule,
JITU akainuka anikimbilia Meneja akamtegeshea mguu akaanguka chini Meneja
akaondoka, mara akina Harrieth na Lola haooo wakarudi wanacheeka wenyewe
wanafurahi, walishapatana Chooni walipoenda wanashangaa kumkuta JITU ameanguka
chini anahangaika kuamka!
Harrieth: akamzoa
zoa pamoja na Lola, wakamweka kwenye kiti wanashangaa mbona Macho ya JITU
yamekuwa mwekundu, hapo hamna tena cha kusubiria Harrieth anataka JITU aende
hospital, Lola akamwambia Harrieth mimi nitaendesha gari yangu twendehi
Hospital, wakawahi kwenye gari ya Lola, hao mpaka Hospital
Baada ya masaa 2
namwona Ulumbi nae anakuja fasta, mimi nipo kwenye Parking na dereva naona kama
movie vile!
Nikakaa Parking
masaa 4 ndio naona Lola anaondoka na Harrieth wanakimbia!
Baada ya Nusu saa
namwona Ulumbi anatoka na mumewe JITU, amevaa miwani! Ameshikiliwa haoni!
Money Stars: nikashika midomo nasema Mungu weee nimeuaaaa! Baba wa watu
masikini, wakaingia kwenye gari na mkewe Ulumbi haooo mpaka kwao, nikarudi
zangu kwangu!
Baada ya wiki 3
nikapigiwa simu na Lola, kuwa yeye na Harrieth walishakuwa mabest
Baada ya wiki 4
nikapigiwa simu na Grace kuwa amepata kazi kwenye kampuni ya JITU, kama
Secretary Msaidizi wa JITU…
Lina anafanya kazi
kwa JITU kama House Girl Incharge anapika, anafua, anapeleka mtoto shuleni, ila
usafi wanakuja kampuni ya usafi inafanya usafi!
Money Stars: nikasema safii.. kila kitu kinaenda kama nilivyopanga,
nashukuru Mungu kwa ajili ya hawa warembo akina Lina, Lola na Lila - a.k.a 3L.
TUONANE KESHO J2 TAR 21 OKTOBA 2018
SAA 10 JIONI YA TANZANIA..
_______________________________________________
G. HUJAFA HUJAUMBIKA...
Money Stars:
Baada ya Sakata la Jana, dah roho iliniuma, nikajiambia hii sasa tushafika mbali pabaya, hii kesi ishakuwa sasa!
Nikampigia simu Grace kumwuliza yaliojiri baada ya wiki 10 kupita na kudai hela yangu ya kodi ya nyumba:
Grace: Jioni uje uchukue nyumbani sasa hivi nimebanwa na kazi nitakupa habari zote za JITU!
Money Stars: nikampigia na Lina, kusikia mrejesho wa JITU na mkewake
Lina: JITU tumeshakuwa rafiki, ila kama unavyojua mamcho yake haoni vizuri, huu ndio muda mzuri wa kuja kuongea nae
Money Stars: mke wake yupo wapi? Naanzake kwanza kuja?
Lina: nimewaambia nina binti mkubwa anaishi Arusha, wewe utakuwa binti yangu, mkewe ameenda mkoa kumchukua baba yake na JITU, huu ndio muda wa wewe kuja wanarudi baada ya siku 3
Money Stars: sawa nitakuja usiku saa 3, hakikisha hizo CCTV zimezimwa staki matatizo mimi…nikakata simu roho inaniumaje!
Nikamcheki Lola na Harrieth wamefikia wapi,
Lola: tupo pazuri Boss lady usiwe na wasiwasi, hawajaonana na JITU tena, sasa hivi Harrieth yupo na Bwana Mwingine
Money Stars: utanipa feedback, jitahidi asijue unapoishi
Lola: sawa madam!
USIKU SAA 3:
Nikaingia kwa kupitia geti la nyuma nyumbani kwa JITU, mtoto ameshalala, Ulumbi hayupo, walinzi wapo upande wa pili anakula, nyumba iko kimyaaaa!
Nikapelekwa chumba cha JITU alikuwa amekaa kwenye kiti anaangalia dirishani
Lina: Fanya haraka madam, mlinzi akimaliza kula anarudi getini itakuwa shida kukutoa na CCTV hazizimwi zaidi ya lisaa limoja kampuni itaanza kupiga imu, una dk 20 tu…
Money Stars: nikamsogelea JITU, nikamshika mgongoni,
JITU: akashtuka, haoni kweli anauliza nani wewe ni Lina?
Money Stars: Manyanga nimefurahi kukuona! Pole sana na kuumwa
JITU: Money Stars? Ni wewe?
Money Stars: Akanishika mkono kwa nguvu hataki kuniachia, nikapiga magoti nikaweka mikono yake kwenye uso wangu, akawa ananipapasa masikio, macho, mashavu… ndio ni mimi
JITU: noooo, haiwezekani, wewe ulishakufa miaka 30 iliopita
Money Stars: Manyanga bwana hauachi,
JITU: kweli sauti kama ya Money Stars, umefufuka? Haiwezekani akaanza kutoa machozi, kweli ni wewe!
Money Stars: nikapapaswa mpaka kusikopapasiwa na mtu asie mumeo wako, tobaaa!
JITU: ni kweli ni wewe, ingawa sioni lakini ni wewe, imekuwaje nimeambiwa umekufa,
Money Stars: nikainuka nikamkalia kwenye mapaja, imekuwaje unatesa watoto wa watu, imekuwaje umekuwa kipofu Manyanga?!
JITU: hata mimi sielewi nimekuwaje kipofu, kuna mdada alikuja pale slip way akaniita jina akanimwagiwa wine usoni, lakini huyo dada alikuwa kama wewe, ana sauti yako
Money Stars: una maana mimi ndio nimekuweka ulemavu?.. nakuweka ulemavu wakati mimi nimeshakufa?
JITU: lakini uko hapa nakushika nakusikia
Money Stars: hilo ndio tatizo, mimi nilishakufa miaka 30 iliopita,
JITU: haiwezekani, wewe ni nani mbona unaongea kama money stars?
Money Stars: inabidi uwe na imani na maneno yangu na uwe mwangalifu na unayoyasema la sivyo sitakuja tena kwenye maisha yako!
JITU: kweli wewe ni Money Stars, nimekumiss mpenzi wangu… ulienda wapi?
Money Stars: shhhh! Nikamkumbatia, baada ya muda nikamwinua, tukaanza kucheza blues, huku naimba wimbo wa Moon light lady, nikimwangalia JITU anatoka machozi haamini….. nitakuja kukutembelea kwa masharti tu, kama hautasema kwa mtu kuwa nimekuja kukuona….
JITU: usiondoke tafadhali mke wangu hayupo
Money Stars: inabidi niondoke ikifika saa 6 usiku, na sasa ni saa 5 dk 55.. nina dk 5 tu
JITU: kwanini ulikufa mpenzi wangu
Money Stars: kwanini umeongeza sehemu zako za siri Manyanga? Ina maana bado haujanisahau?
JITU: akanyamaza kwa muda… baadae akajibu ni kwa sababu yako, nilikupenda sana ukaenda kulala na baba yangu, ukaniambia nina kibamia
Money Stars: Maisha yameshaenda miaka 30 bado haujanisahau? Una mke na mtoto mmoja kwanini unawatesa namna hii?
JITU: Huyo sio mtoto wangu
Money Stars: ina maana mke wako amechepuka ukiwa kipofu?
JITU: Mke wangu amezaa na baba yangu mzazi, niliempenda alitembea na baba yangu mzazi, sina maisha tena.. nipo nipo.. hata ingekuwa ni wewe lazima ungechanganyikiwa kama mimi…
Money Stars: kimoyomoyo nasema tobaaa! Kweli Mzee Manyanga Senior ni noma ana-njaa kweli na ulafi na vitoto vidogo vidogo du! huyu mzee habadiliki?!…
JITU: tangu nimuoe Ulumbi, sijawahi kutembea nae, nilimwoa siku hio hio ya Honey Moon amelala na mimi usiku akachomoka akaenda asipokujua, kumfuatilia kumbe yupo chumba cha pili na baba yangu mzazi….Na wewe Ulikufa…hapa nilipo nilishafeli kabisa kwenye suala la kukusahau.. kama haujafa kweli turudiane tafadhali sina raha sina amani nipo nipo tu…
Money Stars: Nikamwangalia JITU analia hana raha, kwanini usiachane na Mkeo mambo yote hayo mmefumaniana kwanini mnakaa pamoja kama hampendani?
JITU: acha tu! Nikiachana nae tunapasuana mali nusu kwa nusu…na nikiachana nae ataenda kwa Baba yangu kuvunja ndoa ya mama yangu na kuwa mke wa pili…
Money Stars: Manyanga, pole sana lakini ndoa yako ilishakufa kabla hamjaoana!... mali kitu gani achana nae, utakuja kufa mapema kabla siku si zako!...Muda wangu wa kurudi nilipotoka umefika, tutaonana tena siku nyingine…
JITU: plz usiondoke tafadhali, nasikia raha kukaa na wewe!
Money Stars: nitakuja kukuona kwa masharti kama hautamwambia mtu yeyote…
JITU: sitomwambia mtu tafadhali usiondoke… baki na mimi
Money Stars: kama kweli bado unanipenda, usiumize watoto wa watu kwa machine yako ulioiongeza, plz
JITU: sawa… tafadhali ukae
Money Stars: utanisubiria na utakuwa mwaminifu kweli?
JITU: kweli nitakusubiria mpenzi,
Money Stars: Nitakuwa nakuangalia kutoka juu, ukitembea na mwanamke nje ya ndoa sitakuja tena..
JITU: nakuahidi sitatembea na mwanamke mwingine mpaka urudi
Money Stars: chukua hii dawa, uwe unapaka, asubuhi ukishaamka na usiku ukiwa unaenda kulala, kwa muda wa mwezi mmoja, alafu…
Lina: akaingia, Boss mbona umesimama unaongea na nani?
JITU: nani wewe? Nani kakuita (kwa ukali)
Money Stars: nikamwachia mikono fasta nikakimbia
Lina: nimeskia kama unaniita
JITU: sijakuitaaa tokaaa,
Lina: akamsogelea, boss umesimama ngoja nikusaidie ukae
JITU: kanuna anatafuta tafuta hakumpata anaemtafuta, akaishia kupanda kitandani, Lina akamfunika shuka, huku ameishikilia ile dawa kwa uaminifu akalala
Lina: akatoka na mimi, kuangalia mlinzi nae anakuja kurudisha sahani ya msosi, kaa hapa nyuma ya mlango, akishapita wewe toka
Mlinzi: mamaa, asante kwa chakula,
Lina: Kaka ingia naomba uje unisaidie boss ameanguka njoo
Mlinzi: akaingia fasta anapanda ngazi kuelekea chumba cha JITU,
Money Stars: nikatoka nduki mlango wa nyuma huyoooo, hapo saa 4 kasoro usiku, nikaenda kukutana na dereva wangu mbelee tukarudi nyumbani…
Baada ya mwezi 1, Lina akanipigia simu kuwa tangu niondoke, JITU amekuwa na furahaaa, akipelekwa Hospital maendeleo yake mazuri, anakula, anacheza na mtoto, amebadilika kweli kwani umempa nini Boss Lady?
Money Stars: wewe fanya kazi yako, baba mkwe ameshakuja hapo
Lina: yupo, kuna makubwa huku yanaendelea Money Stars hata sielewi nikuelezeje
Money Stars: enhe kuna nini?
Lina: kwani huyu Mke wa JITU anatembea na baba mkwe wake?
Money Stars: weeee! Usiniambia! Umewaona wapi?
Lina: kila siku usiku huyu bin Ulumbi anaingia chumbani kwa baba mkwe saa 6 usiku anatoka saa 11 alfajiri
Money Stars: weeee! Sasa best embu nipatie izo video au picha basi za huyo mama kuingia kwa baba mkwe, na mama mkwe yu wapi?
Lina: Mama mkwe aligoma kuja akadai JITU aende kijijini yeye hawezi kuja hapa.. hata hivyo Ulumbi alishafukuzwa kijinini aliishia mjini, akamsubiria baba mkwe wake aje mjini wakaja nae huku
Money Stars: nakuomba sana kama itakuwa kwenye uwezo wako, nitafutie picha za huyu ulumbi na baba mkwe wamelala pamoja, unadhani utaweza?
Lina: nitajitahidi
Money Stars: ukizipata niambie tuonane
Lina: Madam kesho tunaenda hospital na JITU na dereva, utataka muonane?
Money Stars: nitakuja hospital, nipe jina la Dokta wa JITU kwa sms le oleo kesho tutaonana huko hakikisha dereva haji
Lina: sawa Madam!
Baada ya nusu saa Lina akanitumia jina la Dokta wa JITU nikaanza kuhangaika nae,
Kesho yake, nikajiwahisha kabla ya Muda, wakaingia JITU na Lina na dereva, Lina akamwambia Dereva asubirie nje kwenye gari, wakaingia kwa Dokta baada ya Dk 10 dokta akaja kunichukua tukaingia wote, akaongea na JITU maendeleo yake ya macho na nini akaambiwa kuhusu opereshen JITU akakataa anataka akafanyiwe opereshen nje ya Africa, Dokta akamsihi wamfanyie hapa lakini wapi
JITU: nina wiki 2 zimebaki nimeshabook appointment na dokta wangu nje nikafanyiwe opereshen
Dokta: sawa Bwana JITU, nisubirie hapa nikaprint barua yako nije kukupa tayari … dokta akatoka akabakia Lina, Jitu na mimi
Money Stars: nikasogeza kiti, nikamshika mkono Jitu, Manyanga mzima? Usishituke hamna mtu anaeniona dada yako ametoka na dokta
JITU: Money umerudi
Money Stars: nimefurahishwa na maendeleo yako tangu tumeachana
JITU: Nilikuahidi mimi ni mtu wa ahadi
Money Stars: unaenda wapi kufanyiwa opereshen ya macho?
JITU: naenda Uingereza,
Money Stars: nani anakusindikiza?
JITU: naenda na Lina na Mama yangu Mzazi
Money Stars: pole sana, ukirudi mambo yatakuwa yamekaa sawa
JITU: nikirudi nitakuona Money wangu
Money Stars: nitakuwepo kwenye opereshen yako usijali
JITU: akafurahi mwenyewe
Money Stars: ila sitokaa sana, muda wangu wa kukaa kwako umeshaisha
JITU: usiondoke mpenzi kaa tu si umesema hamna anaekuona
Money Stars: na Ulumbi nae haendi Uingereza?
JITU: sitaki hata kumwona kila siku anatembea na baba yangu mzazi
Money Stars: huu ndio ulikuwa wakati wa kumkamata Ulumbi, umejuaje anatembea nae wakati wewe hauoni?
JITU: halali kitandani kwangu, usiku anaondoka anarudi kumeshapambazuka, namsikia anavyoondoka na anavyorudi ijapokuwa najidai nimelala
Money Stars: JITU tutaonana, nikainuka nikaondoka, ile nimetoka tu nimeshasogea mbele namwona Baba yake mzazi JITU anaingia na Ulumbi, dah bado kidogo nikamatwe huo ungekuwa msala mkubwa haujawahi kutokea!
Sikuonana na JITU tena tangu siku ile ya Hospital, mpaka anaondoka Airport kwenda kwenye matibabu Uingereza, kweli alipelekwa na mama yake mzazi na Lina baasi… nilimhurumia JITU sio kwa yale mateso, doh wanawake wengine wana roho ngumu, unatembea na baba mkwe wako mpaka unazaa nae kabisa na bado mume hakuachi?!
Shikamoo Ndoa za Kikristo!
Baada ya wiki 1 Lina akanitumia email ya picha za Baba yake JITU na Ulumbi wanatembea pamoja na videos whatsapp, … aibu mpenzi msomaji aibu huyu ULUMBI kama Jezebel wa siku za mwisho, hajali analenga sana, ila nani wa kumfunga paka kengele kama sio rafikiwa Ulumbi?!
Ngoja JITU arudi anaona tuanze kumchezea Ulumbi akili mpaka aachane na JITU, JITU ameteseka vya kutosha miaka 30 mtu anateseka tu, ila wanaume wana-moyo! Huyu JITU akifika miaka 50 na akaendelea kukaa kwenye mateso atakufa na umri mdogo kwa stress…
Baada ya wiki 1 nikaambiwa na Lina kuwa Opereshen imeenda vizuri na JITU anaanza kupona anaanza kuona kwa mbali sana…
Nikakwea pipa nikadondoka Uingereza moujaaaa!
Tuonane KESHO Tar 23 OKTOBA 2018, Saa 1 usiku ya Tanzania
_______________________________________________
SEHEMU YA 2
A. PLAN A – KALALA TAJIRI, KAAMKA MASKINI
Kufika Uingereza, najiandaa sasa niende Hospital hapo nimechoooka
kweli kweli (Jet Lagged) … nguvu zikaniishia nikaamua kujituka kitandani na
kulala..
Baada ya masaa 3 nikaamka, nikajiandaa, naangalia whatsapp nakuta
missed call kibao toka kwa Lawyer wangu…
Kumpigia hapatikani, kufungua sms nakuta sms kibao… kilichonichosha ni
jumbe nilizozikuta huko kwa whatsapp na picha na video kibao zilinichanganya
nikataka kurudi kwetu siku hio hio lakini dah!
Huwezi amini nimetumiwa picha za Baba yake
JITU na Ulumbi waki-DO!
Nimetumiwa Picha za Lina na JITU
waki-DO pia!
Nimetumiwa picha ya Lola na Harrieth
wakisagana!
Yeeeesu nilichanganyikiwa, nikiwa katika hali ya kuchanganyikiwa
Lawyer wangu akanipigia kunielezea mkanda mzima,
Lawyer: Best, hawa madada 3 wanakuzunguka, Ni
Mashangingi walioshindikana mjini, kama unataka kuendelea nao lazima uangalie
akili ya ziada, ukienda nao kama unavyoenda lazima kuna sehemu utaangukia pua,
kumbuka ni JITU pekee anayefahamu kuwa wewe ni marehemu, ni muda wa kuendelea
na Plan A kwa haraka umefika.…hakikisha unakuwa rafiki na
Mama wa JITU bila JITU wala Lina kujua…
Money Stars: Akyanani, ku-deal na mashangingi wa mjini
ni shida …maana ni pasua kichwa, umezipata wapi hizi habari wewe?
Lawyer: kuna mlinzi pale anafanya kazi kwenye
kampuni ya rafiki yangu… nikaongea na rafkiangu aongee na mlinzi anisaidie
maana sijawaamini wale masister tangu siku ya kwanza tumekutana wanaonekana
wengi sana wa akili na wajanja wajanja na wana njaa sana, yani masister wa
kupiga na kubabua… sasa pale sijui utafanyaje ikiwezekana tukae pembeni kwa
muda, au tuendelee kujifanya kama hatujui?
Money Stars: na Grace je?
Lawyer: huyo nitakuelezea bado sijakamilisha
file lake lakini jua wewe hapo uko pekeyako na kama JITU ataenda kuona sio
vizuri ukaonekana kwake, utaharibu kila kitu!
Money Stars: haina noma mtu wangu, we kwa sasa
nitafutie ex wa Ulumbi na Grace anamdogowake anaitwa Suzzane, nitafutie habari
zao mpaka sasa wako wapi, huku mimi siondoki mpaka kieleweke, tuwasiliane
ukishapata habari zote 3…
Lawyer: sawa boss lady!
Money Stars: Siku hio nikawaza na kuwazua,
nakuwaza na kuwazua mwanzo mwisho nikaona huu ndio mwafaka wa kuanza na Plan A nikiwa huku kwa Queen…
Usiku wa manane nikaondoka kuelekea hospital aliolazwa JITU, kufika
namwona JITU anatembea tembea toka kitandani kwenda dirishani na kurudi, Lina
amelala kwa pembeni maana ilikuwa saa 8 usiku; kuangalia pembeni simwoni Mama
yake JITU, nikaondoka kwenda kumtafuta nikamkuta amekaa cafeteria wanapouza
chakula, nikaenda kununua chai, nikamsogelea nikamsalimia
Money Stars: sorry is this seat taken?
Mama JITU: Nooo,
Money Stars: Nikajisogeza fasta nikakaa na Mama
JITU, alionekana ana mawaza mia kidogo…nikamkaribisha chai wala habari hana
Mama are you alright?
Mama JITU: Yes am fine
Money Stars: You look so worried, what’s wrong?
Mama JITU: ah we mama embu niache, matatizo
yangu ni mengi niache, hautanielewa
Money Stars: what? I don’t understand you!
Mama JITU: nimekwambia niache ah we nawe mbona
mbea hivi?
Money Stars: Kimyaa! Kama sijui Kiswahili vile
Mama JITU: akaongea hapo Kiswahili wee
analalamika na kutukana, analia na kunyamaza
Money Stars: namwangalia kama sisikii kumbe nasikia..
nikamaliza chai yangu fasta, nikamuaga kwa kidhungu
Mama JITU: wewe nenda tu mama, wasalimie
Money Stars: nikaondoka kurudi wodini na kukuta
kweli Lina na JITU wana-do! Hapo ndipo nilipomwelewa Lawyer wangu, kama kawa
kama dawa saa 9 usiku hapo nikachukua video camera yangu nikawarekodi
wapendanao wawili..
Dah kweli Lina ni binti alievurugwa, ila amesahau mimi nimevurugwa
mara 100 yake, lazima nimnyoshe akikutana na mimi lazima aniamkie mara 100..
Ila Lina ni noma na ule mjoka wa JITU mtu amesimamia kabisa ukucha?! Kha!
Embu mwangalie JITU, nina uhakika asilimia 100 kichwani kwake
nimemjaa!.. Lina anadhani anamchanganya JITU kumbe anajichanganya mwenyewe,
nikakiangalia chumba weee kina CCTV za wenyewe.. nikasikia watu wanaongea kuja
nikazima camera nikaondoka fasta, nikarudi reception nikakaa, kuangalia mchongo
mzima wa ile hospital, masaa 3 nasoma ramani ya pale reception, kweli ULAYA
ULAYA tu, naanzaje sasa kukamata file la JITU? Nikiwa katika kuwaza na kuwazua
mara namwona mama mkwe anapita kuelekea wodini, nikaamua kumsindikiza, kufika
anachungulia ndani anashindwa kuingia akatikisa kichwa akaondoka zake… nikaamua
kwenda kuchungulia nakukuta JITU na Lina wamelala pamoja.. yani hawa watu
wanajisahau sana…
Kumfuata Mama JITU, namkuta yupo chooni analia, kweli maisha magumu
jamaa, mama huyu hana raha, nikaingia chooni hakuniona nikaanza kumwongelesha
kizungu kumwuliza analia nini?
Mama JITU: kimyaaa!.. Mama amebeba siri nyingi
sana za familia yake, akilia inamsaidia kuondoa stress
Money Stars: Nikajifanya naendelea na shughuli
zangu za chooni nikatoka namwacha amekaa chini kabisa kwenye sakafu,
Nikarudi wodini kwa JITU na Lina, bado wamelala, uzuri taa ilikuwa
imezimwa, nikajifunga shungi nisionekane na miwani, nikaingia nikachukua pochi
ya Lina na Wallet ya JITU, wakati naondoka nikabonyeza kengele ya kumwita nesi
nikakimbia hakuna alieona wapo buzy wamelala
Nesi kufika anakutana na watu wamelaliana kama hotel, akaenda kuita
boss wake wakaanza kuamsha amsha, amsha na wewe ishakuwa kesi mara Mama JITU
nae huyo akarudi, ikabidi Lina afukuzwe, katika fukuzwa fukuzwa Lina anaangalia
pochi yake haioni, wakaanza kugombana na nesi.. nesi anasema sijachukua Lina
anasema umechukua
Wakati huo mimi nipo zangu nje ya Hospital nakagua pochi ya Lina,
nikakutana na Passport, tiketi ya ndege, wallet ya JITU kuna hela nyingi…
nikaondoka zangu kurudi Hotelini maana pale Hospital kumeshanuka!
Baada ya siku 3, nikampigia simu Lina aje Aiport, afunge virago vyake
vyote atanikuta airport,.. kweli akaja na sanduku lake kuubwa mshamba wa
Uingereza sijui kajaza nini, macho mekunduuu namwuliza vepe mama kulikoni JITU
kafa au?
Lina: hapana nimepoteza Passport yangu hata
sijui nafanyaje
Money Stars: Tiket yako hii hapa na Passport yako
hii hapa, ndege yako inaondoka baada ya dk 20, safari njema tunaonana Nyumbani
Lina: Akashangaa anatoa macho kwanza
hakujua nimekuja saa ngapi Uingereza, kwani kuna nini Madam mbona ghafla ghafla
ivyo? Au kuna mahali nimekukosea?
Money Stars: tutaongea nyumbani, ukifika Airport
kesho kuna mtu atakuja kukupokea …atakupeleka kwenye nyumba yako mpya utaishi
hapo mpaka nitakaporudi, kule unapoishi hama wala usiwasiliane na wale watu
uliokuwa unaishi nao tena..
Lina: Madam kwani kuna nini?
Money Stars: Hamna kitu mbaya, kuna kazi ya haraka
ya kufanya kule nyumbani, naomba uwe mwaminifu na maelekezo unayopewa ukifika
sawa?
Lina: sawa madam, nashukuru sana
Money Stars: nikahakikisha kuwa Lina anapanda
ndege anaondoka Uingereza, maana janamke kama lile halichelewi likawa likimbizi
ghafla, alipoondoka nikaamsha hema mpaka hotel aliokuwa anakaa JITU na mama
yake mzazi… nikamtumia sms Lawyer kwa whatsapp kumkumbusha ampokee Lina
ampeleke kule tulipokubaliana…
Kufika Hotelini na kuulizia nikaambiwa JITU na Mama yake wamekaa
Restaurant wanapata Lunch, nikazama huko huko waliko, nikakuta JITU amenipa
Mgongo na mama yake ananiangalia kwa mbali
Nikasogea mpaka kwenye meza yao, nikawasalimia nikasogeza kiti nikakaa
nikiwaangalia wote 2
Mama JITU: samahani we nani?
JITU: Money Stars?! Haiwezekani! Wewe si
umekufa?
Money Stars: Shikamoo Mama
Mama JITU: marahaba wewe nani mbona unavamia
meza za watu?
Money Stars: Mama kwani haunikumbuki?
Mama JITU: akaniangalia, hapati picha,
Money Stars: Nikamkumbusha kuhusu siku 3
zilizopita hospital,
Mama JITU: oh yah! Nimekukumbuka, hujambo binti?
Money Stars: Sijambo, umeacha kulia sasa?
Mama JITU: akacheka sana, unaitwa nani mrembo
JITU: anaitwa Money Stars, Money ni wewe
kweli?
Money Stars: Mama kwani unaongea na mtu au jinni
Mama JITU: naongea na wewe hapo si unaona ni mtu
akaanza kumshika Money Stars, kwani vipi mwanangu mnafahamiana na huyu dada?
JITU: kimyaa!
Money Stars: haya mama nashukuru umeacha kulia …
nimefurahi kukuona unafuraha sasa, pole sana kwa matatizo
Mama JITU: asante sana Binti yangu
Money Stars: nikainuka niondoke nilikamatwaje
Kiuno na JITU
JITU: plz usiondoke, haiwezekani ukawa hai
Mama JITU: kwani mwanangu kuna nini mbona
unamtabiria mtoto wa watu mauti unamjua au?
JITU: Money tafadhali usiondoke
Mama JITU: we JITU unashida gani na mtoto wa
watu
Money Stars: we JITU nini hiki kwenye kifua chako
JITU: akageuka.. alipogeuka tu Money Stars
nikamponyoka fasta! Kugeuka nishafika mlangoni alichokaaa! Anamwuliza Mama yake
ninaota au? Kuna dada alikuwa hapa mzuri mzuri ee?
Mama JITU: kwani shida iko wapi JITU mnajuana na
huyu dada?
JITU: sio tu namjua, nikimpata lazima
nimuoe huku huku uingereza!
Mama JITU: akacheka sana, leo umejua
kunichekesha mwanangu sijacheka muda sana
JITU: mama ukikutana na huyu dada naomba
mkamate kwa maneno na kila kitu mpaka nije ikiwezekana mlete mpaka nilipo..
huyu ni furaha yangu ya miaka 30 iliopita, akaanza kumwelezea kuhusu Money Stars,
Mama yake akakumbuka alikuwa na girlf friend akiitwa Moon Light Lady!
JITU: ndio huyu sasa
Money Stars: sasa mbona unamwita Money Stars?
JITU: yani mama stori ni ndefu, natakiwa
nimpate huyu binti, dah! Akitokea akakufuata Mama nakuomba usimwache aondoke
zake, sawa mama?!... huyo ndio tiket yangu ya furaha ya milele, kwingine napita
tu Mama wala usijali
Mama JITU: Sawa Mwanangu… hahaha leo nimecheka
sijawahi kukuona ukiwa hivi Mwanangu kwa muda sasa, am happy for you
HUKO BONGO:
Lina alipofika, alipokelewa na Lawyer
akajiona wa Muhimu kweli hakujua anapopelekwa, baada ya dk 45 za kutoka Aiport
mpaka alipotakiwa aende, alijikutwa amebwagwa Manzese ndani ndani uswazi,
hakuelewa kwanini akaambiwa akae pale pale mpaka Money Stars atakaporudi
atapigiwa simu
Lina alichoka, hakujua cha kufanya, maana
alirudi Bongo simu hana si aliibiwa!
Baada ya kusota wiki nzima ya maisha ya uswahilini, Lina akaletewa simu ya touch na Lawyer, akaonekana kuchangamka,
alipoambiwa kuna msg zako whatsapp akachangamka zaidi, kufungua anakuta video
na picha zake na JITU wanapeana raha, sura ikaanza kubadilika ghafla..
alipoanza kulia Lawyer alishaondoka muda wananchi wakajaa wanamshangaa aunt
analia nini tena?
Hapo hana mia hana nini, nyumba yenyewe imepangishwa hajui inalipwaje,
akiangalia kwenye akaunt yake ya bank hafikishi laki 3… kweli kulala tajiri na
kuamka maskini hakujawahi kumwacha mtu salama…
Baada ya wiki 3 kupita nikarudi Bongo, sikuonana tena na JITU wala
Mama yake kama walivyodhania itakuwa, kufika nyumbani kwangu Lawyer akaja
kunipa mkanda mzima wa Grace, Harrieth, Bwana wa Harrieth, Lola na ndugu wa
Grace Suzzane
PICHA LIPO HIVI:
1.
Baada ya kugundulika kuwa Lola na Harrieth wanasagana, Lawyer akaenda
kumtifua Bwana wake Harrieth wa zamani ambae walipendana sana, Harrieth
alipompata JITU akambwaga ex wake… Lawyer akaongea kikubwa na ex wa Harrieth
akamweleza kila kitu kuhusu mahusiano yake na demu mwenzake na kuwa kama
anataka kumlipiza kisasi Harrieth ni sasa, anatakiwa amfuatilie sana Lola
amfukuzie mpaka amkubali alafu awe mpenzi wake, Jitihada zikafanyika mpaka Ex
wa Harrieth akampata Lola, maana alikuwa anampa attention za level ya kizungu
Lola akachizika.. siku moja Lola na Ex wa Harrieth wakalewa wakarudi nyumbani
anapoishi Lola, wakaingia kulala, kulala na wewe Harrieth akiwa amesafiri, ndio
ikawa tabia yao mpaka siku Harrieth anawafumania wana-do kitandani kwa
Harrieth, ugomvi ukawaka usio na mwisho, ikabidi Lola ahame nyumbani kwa
Harrieth akaishi kwa Ex wa Harrieth, haya yote yalitokea na kumfanya Harrieth
kuchanganyikiwa zaidi maana aliporudi kwa JITU, JITU alimkataa… akili ya JITU
bado inamtafuta Money Stars kwa udi na uvumba..
Baada ya Mizei 3 ya mahusiano kati ya Ex wa Harrieth na Lola, Ex wa
Harrieth akaaga anasafiri kikazi kwenda Ethiopia, akamwambia akae pale kwani
ile nyumba ni yake hakuna wa kumsumbua…
Lola alivyo na akili kama upepo akaamini, baada ya wiki 1 ya kuishi
pale mwenyewe akaja mwenye nyumba na kumtoa kwa nguvu, alivyompigia simu Ex wa
Harrieth hapatikani na namba haipo hewani wakati ni jana yake tu waliongea
kwenye hio hio namba ya simu aliompigia… Lola akarudi kumtafuta Money Stars
hapatikani kwenye simu.. kurudi kwa Harrieth hawezi, akafukuzwa kwenye nyumba
asioijua na mtu asiemjua akidai ni mwenye nyumba akarudi kupanga Sinza… uzuri
alikuwa na ajira yake ndio kilichomsaidia, mpaka sasa anamtafuta Money Stars
ambae bado hapatikani!
2.
Grace bado anafanya kazi kwenye kampuni ya JITU, siku JITU alipomwona
ofisini kwake alimwangalia tu kama mahindi ya kuchoma ingawa Grace alijua
atasumbuliwa, ikapita wiki, mwezi, miezi JITU haangaiki nae.. hakuelewa kwa
nini… sikumoja akaamua kumfuata ofisini na kumsalimia kimahaba, JITU hamu hana
wala hamtaki akaamua kumfukuza ofisini kwake kabisa akamwambia nikikuona
nakuweka ndani … Grace akaondoka kurudi kwenye ile nyumba aliopangiwa na Money
Stars, akakuta nyumba haipo, imechukuliwa na mwenye nyumba, macho yakamtoka,
akimpigia Lola na Lina hawapatikani, akarudi kwa Ulumbi kumwelezea matatizo
yake, Ulumbi akamwambia hatoweza kumsaidia tena, akamtafuta Money Stars hayupo
kwenye simu hapatikani…Grace akaamua kurudi nyumbani kwao magomeni kuishi na
wazazi wake..
3.
Bikra wetu Suzanne, ndugu wa
Grace ndio ambae amebakia, mpaka sasa yupo kwenye mahusiano na Lawyer, Lawyer
ameamua kumweka sawa kwanza, anampa attention za kufa mtu ili akija kumbwaga
anataka aangukie miguuni mwa JITU, … ila Lawyer nae ana roho mbaya! Mara ya
mwisho nilipoongea na Lawyer akaniambia Suzzane Bikra alishaiondoa muda sana,
kwa sasa ana bikra moja tu Mungu mwenyewe ndio anaijua!...
Lawyer: Best imebakia miezi 3 sasa tuingie
kwenye Plan B maana wale mashangingi sidhani kama watakuachia tu wakae kwenye
umasikini wakati walishaonja Mbingu kabla ya hapo.. lazima watarudi kukumaliza
ushike adabu yako… hapo walipo wamechoka best utadhani wametoka kijijini leo,
fanya tuingie Plan B watakuheshimu wakitoka hapo
Money Stars: bado tusogezi mpaka mwaka na miezi 6
upite na hela zao zote ziishe kwenye miliki yao…hawajajifunza wakishika adabu
watanitafuta hata kuzimu.. kwa sasa waendelee kupata taabu sana!
TUONANE JUMAMOSI TAR 27 OKTOBA
2018 SAA 6 MCHANA YA TANZANIA..
_______________________________________________
B. PLAN B
– TUWACHANGANYE AKILI ZAO KWA MUDA
Baada ya miezi 6 kuisha, tukapanga kuonana na Lawyer mjini kupata
Lunch na kuongelea mikakati yetu ya sasa
Money Stars: Mwana Mwana! Lawyer ni wewe lakini
kuchelewa unajua kweli kweli!
Lawyer: we acha tu, ushukuru Mungu nimefika
Money Stars: Mara ya mwisho kuongea na wewe
umenipa maneno magumu sana..
Lawyer: hahahahahaha, Star bwana!
Money Stars: kwahiyo amebakiwa na bikra 1 tu Mungu
mwenyewe ndio anaijua? Hayo sio makubaliano yetu ujue! Ushafeli hapo!
Lawyer: unajua ndio maana tumeonana, mambo
haya ya simu sio mazuri, nilihisi simu yangu imehakiwa ndio maana nikakujibu
vile… ila usikonde mambo yapo vizuri, isingekuwa ni kazi mimi ningeshamuoa Yule
binti Suzzane… unajua aliumia sana pale nilipomkimbia, nikambwaga nikarudi
baada ya mwezi tukakaa miezi 2 nikambwaga tena nikarudi baada ya miezi 3 na
juzi nimembwaga kikubwa, nikamwambia nimeoa!
Ila Stars bwana unajua kunidatishaga na vimwana wako, nitaoa kweli?
Money Stars: Kwanini umemfumua mtoto wa watu?!
Lawyer: ndio nachojaribu kukueleza Yule binti
bado sijamgusa
Money Stars: Miezi 8?! Hujamgusa? Hajakuhisi wewe
sio mzima?
Lawyer: Kazi ulionipa ni ngumu sana Star, ni
vile tunaheshimiana ila muda sana ningeshakula tunda
Money Stars: Kwahiyo?
Lawyer: Kila siku nampa excuse nampiga
kalenda mtoto wa watu mpaka naona aibu ndio maana namkimbia naibuka, mtoto Yule
mchumba ujue! Mzuri sana Yule binti, yani kukaa na demu mzuri kama Yule alafu
unamwangalia kama Picha ya Yesu inahitaji imani sana ujue?! Mnanitia majaribuni
buana!
Alafu uache mambo zako za sizitaki mbichi hizi, unaniwekea ndizi
mbaaali unanifanya sungura nizifikie!
Money Stars: hahahahahha, usijali nitakuozesha
yale mashangingi mengine yale ndio mazuri
Lawyer: oh! Wale tena,. Alafu ushawasiliana
na warembo wako?
Money Stars: wapi?! Kimyaa! Habari sina! Kwani wapo
wapi hawajanitafuta kwenye simu maana namba ya simu nilishabadilisha kipindi
kile tumemaliza kuongea nikaitupa chooni nikaflush!
Lawyer: dah! We mwana wewe! Ila poa tu
Lawyer wako nipo kukudaka usianguke
Money Stars: Vp kwani nini kimetokea?!
Lawyer: Mengi yameytokea Star kwanza
sijaamini kama tunaoana leo, wale majinga yamekuzunguka mbayaa!
Money Stars: aaa?! Imekuwaje tena?
Lawyer: una muda?!
Money Stars: siku hii ni kwa ajili yako!
Lawyer: dah yametokea makubwa na madogo pia!
Money Stars: Am all Ears!
Lawyer: Tulipoachana nikaendelea kuwafuatilia
wale mamama wa mjini,
Money Stars: Enhee!
Lawyer: wote walirudi kwa JITU kila mtu kwa
kalenda yake
A.
Harrieth aliomba appointment
kwa JITU akaambiwa aende nyumbani kwa JITU kumbe alikuwa na mpango wa kumrubuni
alale nae, hakujua kuwa ULUMBI yupo mule mule ndani
Harrieth akafanya yake kamrubuni JITU wakaingia chumbani kwa JITU,
wakawa wanafanya yao weee mara Ulumbi akaingia, akawafumania, vurugu zikaanza
Ulumbi anadai chake, Harrieth nae anatema chehe zake anazozijua
Wakagombana kwa maneno wakaingia kwenye ngumi.. wakadundana wee JITU
anawachukua video camera, walipomaliza JITU akainuka akawala wote 2 kila mmoja
kwa wakati wake, mambo ya three sum nene kwa mara ya kwanza ULUMBI ametembea na
mume wake!
Money Stars: acha kusema uongo bwana unajua
unaniudhi
Lawyer: akatoa flash, hii falsh ina kila
kitu, akafungua laptop yake akaniambia angalia kama nakudanganya, doh kucheki
kweli JITU kafanya three sum alafu kawaacha wote hoi!
Money Stars: ivi Lawyer unatoaga wapi haya
maigizo?
Lawyer: Mil 5 niandalie sijafanya hii kazi
kwa bure
Money Stars: usijali, enhe kwahiyo ikaishiaje
Lawyer: Baada ya lile zoezi Ulumbi na
Harrieth hawaongei, Ulumbi akaishia kugombana na mumewe kuwa amemcheat anataka
talaka na talaka ikipita ni nusu mali tunapasua, JITU akamwambia nenda
kashitaki kokote hata mimi nimekuchoka, ila hautapata hata Tsh 10 yangu
Money Stars: kwahiyo sasa?
Lawyer: Ulumbi akakasirika akaenda kukaa
hotelini, JITU anakaa pale na mtoto, siku moja akamchukua mtoto akampeleka
kufanya DNA test Afrika Kusini, akaondoka na nywele na kucha za Baba yake mzazi..
kweli akakuta mtoto sio wake ni wa baba yake mzazi!
Money Stars: Kudadeki! Baada ya hapo
Lawyer: akarudi zake mjini, akampeleka mtoto
kwa mama yake hotelini alipokuwa anakaa na barua ya DNA akamwambia subiria
talaka na kwangu usikanyage mpeleke mtoto kwa baba yake!
Ulumbi kachanganyikiwa akapanda ndege mpaka kwa Baba yake JITU akaenda
kumweleza kila kitu, kikao kikaletwa mjini nyumbani kwa JITU
Wazazi wakaongea Mama ake mzazi JITU analia tu, kujua mumewe ana mtoto
mdogo na umri ushaenda ana miaka 75 baba JITU, ataleaje anamtegemea JITU ndio
awasaidie
Wakaita mwanasheria wa familia kuamua kesi, ULUMBI akajua hapa lazima
napewa change naendelea kuwa taajiri!
Mwanasheria wa familia akamwambia ULUMBI talaka yako hii hapa, JITU
ameshakutalaka kwa sababu ya kutembea nje ya ndoa tena na baba yake mzazi, ana
haki ya kukushitaki kwahiyo kwenye ndoa hii hauna chako
Ulumbi akalia lia lakini mtoto wangu ni mtoto wa familia
Mwanasheria akamwambia mali zote za Mzee Manyanga alishamkabidhi
mwanae JITU miaka 15 iliopita kwasababu ya uzee wake na katika urithi wake
hakuwa amemwandika mwanao kabisa na huyu mtoto ana miaka 10, urithi
ulishakabithiwa kwa JITU miaka 5 kabla ya mtoto kuzaliwa… kama anataka mwanao
aangaliwe ni makubaliano yako na mzee Manyanga, mali za familia zipo mikononi
mwa JITU tu kwa sasa!
Itabidi wewe na mwanao mkalelewe na Mzee Manyanga huko kijijini
awalishe awavishe ndio uwezo wake ulipo..
Ulumbi akalia sana maana alijua maisha yatamwendea mteremkoni!
Mama JITU na JITU wakakumbatiana, Ulumbi akaondoka kwa hasira akisema
ataenda mahakamani kushitaki, mtoto wake apate haki zake kwa Mzee Manyanga!
Money Stars: Maskini Ulumbi, sijawahi kuonana nae
lakini simpatii picha na hopes zake maskini!
Lawyer: baada ya mwezi m1 wakaenda
mahakamani, kesi ikasikilizwa, ikapaishwa mbele, mwezi wa 2, kesi ikapaishwa,
mwezi wa 3 kesi ikapaishwa, mpaka kufikia mwezi wa 5 Ulumbi hana hela ya
kumlipa Lawyer! Mpaka kuja kusomewa hukumu, ikaamuliwa mtoto alelewe na baba
yake mzazi na mama yake na sio kaka wa mtoto!
Na mali alizonazo Mzee Manyanga ni shamba 1 analolimia kijijini alilolinunua
hivi karibuni, ndio anaweza pewa huyu mtoto
Ulumbi hakuamini, anaenda kijijini, akakataa, akaleta jeuri hataki
hata hilo shamba, mwisho wa siku Mzee Manyanga akafariki huko kijijini,
wamezika wiki 3 zilizopita!
Money Stars: weee! Mzee Manyanga amekufa hata
sijazungumza nae?
Lawyer: ulikuwa kimya mimi nakutafuta kwenye
simu haupatikani
Baada ya Mazishi, Mwanasheria wa Familia akaja kuandika lile shamba la
mzee Manyanga jina la MAMA JITU na kama Mama JITU atafariki atapewa JITU!
Money Stars: makuuubwaa! Ina maana ULUMBI kweli
kakataa hata kashamba mjinga kweli… sasa Ulumbi yupo wapi na Harrieth yupo
wapi?
Lawyer: Ulumbi hajulikani hayupo na mwanae,
Harrieth yupo mjini anadanga!
Money Stars: anamdangia nani sasa? Nani anataka
wazee!
Lawyer: ameokota lizee limoja limestaafu ndio
yupo nae na Zungu moja hivi, anatoa huduma kwa zamu, wiki hii yupo kwa zungu
wiki ijayo yupo kwa mstaafu, hataree angalau anaishi hela ya kodi ya nyumba,
mahitaji ya kila siku anapata lakini sio life la zamani kwa JITU hatopata!
Money Stars: JITU je?!
Lawyer: mpaka jana nimeambiwa JITU yupo
Arusha ameenda kujipumzisha kuondoa stress za kufiwa na baba yake, Mama yake
anaishi nae hapa hapa mjini ameondoka kijijini ndio anamkazania aoe tena ila
yeye anasema anakutafuta wewe stars hakupati
Inabidi uende Arusha ukaongee na JITU, hana raha hataki kitu
anakutafuta, kaongee nae sasa hivi hamna ishu sana yupo huru!
Money Stars: Suzzane ana ishu gani wiki hii?
Lawyer: yupo tu amechukua likizo kazini, vp
unataka kuonana nae?
Money Stars: nataka nipande nae Arusha akanisaidie
kuonana na JITU!
Lawyer: na mimi je?
Money Stars: kama tulivyopanga, niandalie vijana
wako 4 waliovimba kifua, nipande nao, JITU mjinga sana asije akanibaka, panda
nao na Suzzane pia, tuonane ARUSHA kesho tumalizane na Plan C yetu!
Lawyer: sawa Boss!
Money Stars: kuhusu wale manyambizi tutaongea
sikunyingine natakiwa kumuwahi JITU asije akajidhuru!
Lawyer: sawa boss lady!
Money Stars: nitakulipa tukirudi Mjini ngoja
tukamalizane na Arusha kwanza!
Lawyer: sawa boss wangu!
Tukaagana tukaondoka, nikaenda kuwazungukia akina Grace… Lola…. Lila…
Lina!
Kweli wanatia huruma afadhali na Lila ana kazi yake lakini hao wengine
wa3 wanatia huruma! Anyway hicho ni kiporo cha baadae, angalau wapo!
Ila acha waendelee kuumia wakiniona wajue kuniheshimu, wanaonekana
wamechanganyikiwa sio kitoto, manyambizi kama yale kuangukia uswaz mchezo?!
Usiku huo huo nikaaga kwa mume nasafiri naenda Arusha kufuatilia
biashara flani hivi, Mume akaingia line kweli, Alfajiri nikapelekwa Airport
nikapanda ndege asubuhi ya kwenda Arusha… baada ya masaa kadhaa nikatua Arusha,
Arusha kuna baridi jamaaani, uuuwi!
Nishazoea kwetu jotoooo, nimekutana na Baridiii! Nikamwa nawaza kwa
sauti nah ii baridi nikikutana na PUNDA ya JITU si nafwaaa?!
Uuuuuuuwi, Kiru! Half-Cast wa kichaga nimeingia Arusha!
TUONANE TAR 5 NOVEMBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
________________________
C. PLAN C ~ KUONANA NA JITU NA KUTOLEWA MAHARI
Half cast wa Kichaga nikatua
Arusha, sikufikia hotelini
nilifikia kwa somo yangu
mmoja ivi alinifundishaga
kitchen pati wakati naolewa
Somo huyo ni noma,
amefundisha wadada wengi
mjini na asilimia 80 ya
aliowafunda wana ndoa zisizopungua miaka 15
Sikumoja nikiwa ulaya nikamkumbuka kumsalimia akaniambia ameshaolewa na yeye alipataga mzee mwenzake. .. huyo mzee alifiwa na mke akabakia mwenyewe kulea hawezi ndio wakakutana na somo yangu
Nikisema Somo kwangu mimi namaanisha mfundaji wangu wa Kitchen Pati cha ndani...
huyu Mama alinifundishaga miezi 2 mafundisho ya ndoa yote mpaka ya enzi za kale, kabla hatujatoka kitchen pati cha ukumbi ni noma asikwambie mtu ni vile ameacha hio kazi ila sikuhizi amefungua grup lake la WhatsApp amewaweka watu wote aliowafundaga ingawa wengine walishafariki lakini tuliohai tupo WhatsApp tunakula good time
So nikaaga kwa mume nikamwambia nafikia kwa Somo yangu akapata utulivu wa moyo
Kufika kwa somo mumewe alikuwa amesafiri nikampa mkanda wote wa JITU
Somo: My dia hapo usiingie kabisa ni sawa na kuchezea waya wa Tanesco ukasema haurushwi huyo atakuharibu mbaya ni bora nikodishe nyumba umwite muyajenge kwenye hio nyumba nikiwepo ajue kweli umefikia kwangu maana najua ukimwonyesha hapa atakuja anisumbue
Basi tukapanga na kupangua, akaenda kutafuta nyumba huko Mushono nyumba kapata mbaya mbaya nakwambia alafu kuna bonge la shamba na mazao kibao ah sikuamini
Tukakaa hapo siku 5 tukazoea na mazingira kabisa ili asishituke, nikaja nikampigia
Lawyer nikamwambia mambo yamekaa poa ampelekee barua JITU amwelekeze pakuja
Kweli Lawyer akafanya yake kama kawaida akamuagiza kijana wake akaipeleka barua hotel aliokuwepo JITU, JITU akaipokea akaiweka pembeni, kijana wake alipoona hatilii maanani akamwambia imetoka kwa Moonlight Lady, ndio JITU anashituka akataka kumshika kijana akamponyoka akakimbia
JITU: akaichukua ile barua akaisoma maelekezo yote ya kuonana. .. siku hio hio akachukua gari yake na ma body guard 3 wakaja kule Mushono Arusha ndani ndani huko wakafika na Land Rover yao nzurije,
Wakashuka wakapokelewa na Somo, Somo kwani utamjua amekaa kama bibi wa kijijini, hapo keshalipwa Milioni zake 5 anaitumikiaje hela sasa? !
Wakapokelewa wakakaribishwa ndani wakakataa, JITU anataka kuonana na Moonlight Lady,
Somo: yupo ndani, lakini utaingia pekeyako, hawa hapana
JITU: akawaambia ma body guard zake waingie ndani kukagua kwanza wakafanya yao wakatoka kumwambia pako sawa kuna Mama amelala ndani
JITU: akaingia ndani fasta akijua Leo anamzimua mpenzi wake wa miaka mingi kwa mahaba makubwa, akashangaa kukutana na Bibi amelala
Akamsogelea labda hajaona vizuri, bibi akamnyooshea kidole dirishani, JITU kuangalia dirishani akaona mdada amekaa shambani
Akatoka fasta fasta kukimbilia shambani huku wafuasi wake mabodigadi wanamfuata Kufika akanikuta nimekaa sina papara wala sikugeuka kumwangalia
Money Stars: umekuja kunidhuru au kwa amani? ! Naona aumenijia na vijana wa ulinzi
JITU: money stars?! Ni wewe? ! Siamini
Akasogea kuaniangalia kweli
Mpenzi Ni wewe?!
Akanikumbatia mwenyewe anatoa machozi ananiangalia hanimalizi
Akawaambia Body Guard wake, mkanisumbirie kule kwenye ile nyumba na muhakikishe hakuna mtu anakuja huku shambani, kama mtakula pale kuleni msije mpaka nije mwenyewe
Mijemba ikaondoka kwa oda chezea pesa wewe hata ukisema waning'inie kwenye miti kama masokwe wataning'inia tu
JITU: Bebi, nimekumiss sana... huku ananipapasa mikono, macho, mashavu, shingo dah ukaguzi sio wa nchi hii mwisho wa siku akajua kweli mimi ndio mimi sio mzuka au jini anaetembea,
Kukumbatiwa sasa kiru utadhani nitamponyoka anakumbatia kwa nguvu utadhani bikra wa kiume bwana!
Money Stars: unaniumiza JITU bwana acha ujinga,
Nikajinyofoa kwa JITU, hivii hukui tu na mambo yako ya kitoto?!
JITU: sio hivyo mpenzi mimi nakupenda sana na nimefurahi kukuona upo hai, niliambiwa umekufa na tangu niambiwe umekufa ulikufa na mimi mpenzi
Money Stars: well, sijafa kama unavyoniona na acha kunishika shika bwana unanichosha we vipi?! Embu niachie
JITU: akaniachia kwa woga huku ananiangalia, basi naomba nikushike mkono basi
Money Stars: JITU, hivi unataka nini kwangu?!
JITU: nakupenda, nataka tuoane
Money Stars: JITU si unafahamu kuwa mimi Ni mkristo?!
JITU: ndio mpenzi
Money Stars: na wakristo hatunaga ndoa 2 sio?!
JITU: ndio lakini mimi sijaoa
Money Stars: najua ulishaoa na umeacha, lakini mimi Ni mke wa mtu, mama watoto 3, unachokitafuta kwangu Ni ngumu kukipata
JITU: oh jamaan Ni kweli ulishaolewa mpenzi, hapana usiseme hivyo kunifukuza mpenzi
Huku ananichum kwenye shingo mara shavuni machozi yanamtoka, siwezi kukukosa kwa mara ya 2 haitawezekana bora nife nikalale na baba zangu kuliko kuishi bila wewe
Money Stars: bado una akili za kitoto umeghairi kukua sio?!
JITU: sio utoto nakupenda mpenzi,
Money Stars: JITU akanisogelea akakaa kwa mbele yangu ananikumbatia mambo ya 0 distance nene, huku ananichum kwenye shingo dah, nguvu zikaanza kuniisha nikasema Leo nabakwa mana mtu ameshakuwa wamotoooo na machine imesimama mbayaa suruali itatoboka sasa hivi, nikaamua kuyamaliza kiutu uzima alafu nimkimbia
Nikaamua kumchum, ikawa kosa na yeye akazidisha dozi ya mabusu... mabusu yalipozidi akainuka akanibeba kuelekea shambani ndani ndani ambapo hatuonekani
Kweli JITU alikuwa amenimiss, kusika na kufika katoa nguo zake zote kabakia na boxa, doh kuangalia machine yake nje ya boxa nikasema Leo nakufaaa uuuuwi halfcast wa kichaga natobolewa kizazi leo
Tukiwa tumezama kwenye Hot Romance nikakumbuka miaka ya zamani ndio tumeanza ki-do, JITU anakupa raha mpaka tone la mwisho, mjinga yupo vizuri kwenye sekta ya Romance
Utamu kolea Money Stara nikaishiwa na nguvu, namwona kabisa hapa huyu mjinga anataka kuniingia na mjini nimeacha ndoa alafu JITU hana hata mpira... mambo ya kuja kutafuta mimba za uzeeni sitaki Nikajinyofoa kama kawaida
yangu lakini JITU alikuwa na nguvu sana
Huwezi amini alipovua Boxer lake ndio nilijionea miujiza. .. doh bonge la machine jamaan
khaaaa nikamstopisha
namwuliza, we JITU nini hiki sasa
JITU: anachekelea utadhani mazuri
Money Stars: nikawa najiweka sawa narudishia nguo za juu, JITU nae yupo buzy kunivua na mie nakataa kuvuliwa...kha!
Nani anataka kubakwa na JOKA?!
Money Stars: we JITU nini hiki tena? !
JITU: kwani vipi mpenzi wangu
Money Stars: he?! Saa ngapi umepata hii kitu? !
JITU: usijali bwana haina shida hii haiumizi usijali
Money Stars: nikaruka, heee embu niache tafadhali kha unataka kunitoboa utumbo na mapafu yangu au?!
JITU: anakazana kunipetipeti kimahaba, Money bwana Acha utoto
Money Stars: ukitaka usinione tena nidumbukizie ujinga wako kwenye mwili wangu
JITU: ah usiseme hivyo bwana dah yani unamwona anavyohangaika sasa hapo machine imesimama balaa, anahangaika hana pa kuiweka
Money Stars: mimi nimekuwa mbogo balaa, nampiga kwa mazao yaliokuwepo yeye anazuia na kukwepa Mengine yanampiga vurugu mechi mtindo mmoja
Nikaona hapa nitabakwa vibaya sana alafu litakuja kutubu baadae, nikakimbia kuelekea kwenye nyumba, akanikimbiza mara ya Kwanzaa akanikosa mana hana nguo, akarudi kuchukua nguo zake, akavaa mimi nikakimbia kwenda kwenye kile kijumba chetu nikaingia ndani Somo akanifuata mabody guard wakamkimbilia boss wao
Baada ya dk 15 JITU akaja anagonga anataka kuonana nami, nikakataa akafosi akaingia ndani dah padogo na yule bibi pale kuongea anashindwa akaniomba sana tuongelee hata kwenye gari
Money stars: nitaongea na wewe kesho, leo niko na mshituko na bibiyangu hapa anaumwa naomba uondoke
JITU: mpenzi mimi siondoki, nalala hapa hapa kwako, kesho ukiamka utanikuta..
Money Stars: sikuhio sikutoka ndani, Somo alitoka akapika, nikasikia wanaongea nje na JITU,
Baada ya muda wakina JITU na Body Guard wakala, mimi na yule bibi tukaletewa msosi ndani tukala tukalala,
Usiku wa Saa 7 Somo akaniamsha
Somo: huyu kaka bado amelala nje ya mlango wale mabody guard wake wamelala kwenye gari...amekataa kula chakula mpaka wewe ulipomaliza kula ndio akala. .. JITU anakupenda sana ungekuwa hujaolewa na hauna familia ningekuambia uende nae
Money Stars: Somo hujakutana na wasanii bado ila tutayamaliza yote hapa hapa, tulale
Asubuhi nikaamka Saa 12 kufungua mlango namwona kweli kalala mlangoni hamna pa kupita, nikachukua maji ya baridi na lile baridi la Arusha nikamwagia
JITU: ah bebi ni wewe?!
Money Stars: nifuate
Tukaongozana mpaka shambani,
JITU: umeamkaje mpenzi naona upo na nguvu alfajiri hii
Money Stars: ukitaka niachane na Mume wangu niambatane na wewe hio kitu yako ulioongeza uirudishe kama zamani
JITU: nini?!
Money stars: umeniskia vizuri na najua umenielewa
JITU: haitawezekana
Money Stars: hio sio shida yangu ni yako
JITU: money tafadhali, siwezi kuwa na mwanamke mwingine zaidi yako
Money Stars: nikamgeukia, nikamkumbatia, nikamwangalia machoni kwa macho ya huruma, nikamwambia najua na ndio mana nataka unisaidie na kitu kimoja tafadhali
JITU: chochote mpenzi nitafanya kwa ajili yako
Money Stars: kweli Mpenzi?!
JITU: kweli si unajua nakupenda sana
Money Stars: nataka uoe
JITU: kuoa? ! Nakuoa wewe au?!
Money Stars: kwasababu mimi na wewe
Imeshindikana, nataka umuoe mwanangu mtoto wa dadangu
JITU: sielewi unanichanganya me nilidhani kwenu mpo wasichana 2 tu
Money Stars: kwa hali ulionayo ambayo huwezi kuirudisha nyuma ukabadilika ukarudi kama nilivyokuacha, na kwa hali ambayo nipo nayo ya ndoa ambayo haiwezi kubadilika, lazima tukubaliane kusaidiana na kufikia muafaka kuliko kuumizana
JITU: nakuskiliza
Money Stars: kama ambayo unanipenda mimi, naomba umpende zaidi mtoto wa Dada yangu ninaekupatia tafadhali... hauna mwanaume anaetaka kukaa pekeyake JITU utakufa na stress mpenzi, usijiharibie maisha kwasababu yangu, maisha ya mateso uliopitia yanatosha kwa sasa, tafadhali nakuomba unikubalie ombi langu
JITU: hapana bwana mimi nakupenda wewe
Money Stars: najua unanipenda ndio mana nimekuomba plz plz JITU, kama unanipenda niamini na huyu binti hana shida na hautakuja kujuta nakuahidi plz, huku namchumu kwenye shavu
JITU: sasa natafutiwaje mke kwani mimi siwezi kutafuta?!
Money Stars: tumeshayaona kwa Ulumbi
JITU: hujui chochote kuhusu Ulumbi, akaanza kujawa na hasira
Money Stars: nikamkumbatia, tafadhali rusirudi Misri tumeshavuka bahari ya shamu tunaelekea Caanani... plz
JITU: akatulia na hasira ikaanza kushuka, akaniangalia machoni, navyotia huruma maskini kwa muda ... mwone Kwanzaa ulivyo mzuri, hapa una watoto 3 uko hivi, ila huyu mumeo kakunenepesha kwanini lakini
Money Stars: Yes or No?!
JITU: nikisema No?!
Money Stars: then mimi na wewe tumeshamalizana hautaniona tena narudi kwa Mume wangu Uingereza
JITU: kumbe ilikuwa ni wewe Uingereza?
Money Stars: hapana malaika wangu, plz huku namrembulia macho
JITU: akacheka sana, unajua kuninyong'onyeza unavyonirembulia ... si bora nikafanyiwe opereshen nikarudishiwa machine yangu ya zamani je?!
Money Stars: najaribu kukusaidia naona hatuelewani, nampenda sana Mume wangu na watoto wangu siwezi kuwaacha kwa kitu chochote
JITU: kama unampenda sana mumeo kwanini upo hapa na mimi?! Ina maana hata mimi unanipenda vile vile na mimi pia namasharti yangu nataka kukuoa wewe
Money Stars: No
JITU: Yes
Money Stars: Ndege yangu inaondoka kesho saa 10 jioni kwenda Uingereza, utanipa jibu kama hapana hautaniona tena kama ndio tupange yanayofuata
Nikaondoka toka shambani kurudi ndani nimemuacha JITU shambani anawaza na kuwazua...ilipofika saa 3 asubuhi nikamwona Body Guard ananiita kuwa Boss wake anataka kuongea nami shambani
Kufika Kwanzaa nikapokelewa na mabusu motomoto nikabebwa juu juu kama kigunia, nikaenda kuwekwa kwenye mahindi buana... doh! Salala, nilipigwa Romance ya kibabe hakuna mfano
Ambacho umesahau mpenzi msomaji ni kwamba mwanaume anaekupenda sana hawezi kukufanyia kitu ambacho wewe uliependwa haukipendi ... sikupenda anipe machine yake hakunipa machine yake
Ila unamwona mtu kabisa anavyokupa raha ya romance unaona ni kiasi gan anaumia kukukosa... lakini atafanyaje ndoa ya mtu lazima uiheshimu
JITU: Aliopomaliza akaniambia nimeishiwa na nguvu juu yako, kukupata siwezi kukufaidi siwezi, kukupenda naweza, sawa nionyeshe mtoto wa dadako nitamuoa
Money Stars: nikafurahi lakini sikuwa na uhakika kama ni ya kweli anayoyaongea JITU au hapana!
Nikamkumbatia na kumshukuru kwa yote, nikamwomba tafadhali muangalie vizuri mtoto wangu, nampenda sana na hajui mwanaume wewe utakuwa wa Kwanzaa
JITU: Akaniangalia kwa mshangao, we Money unaniletea Bikra?
Money Stars: hata sijui wewe ndio utaniambia
Tukaondoka kurudi ndani, akaomba chai ya pili akapewa akanywa kwa furaha mpaka yule bibi anamshangaa alivyo na furaha
Somo akajua tumedo maana sio kwa ile furaha aliokuwa nayo JITU
Jioni yake akaomba tuondoke wote twende Arusha mjini nikamtambulishe kwa mtoto wa Dadangu, atanirudisha Dar kwa Ndege, tukaondoka na Somo na JITU na ma body Guard wake wote tumeshamwita mwenye nyumba aje akae na bibi tutarudi wiki ijayo
Tukaingia hotelini Somo kakodiwa chumba chake, mimi nikaambiwa nitalala na JITU nikakataa nikagoma,
Baada ya muda nikampigia Lawyer amlete Suzanne mishen imeshatiki upande wangu
Tukiwa kwenye kumsubiria Mwali akuje na JITU akiwa chumbani kwake na sisi kwetu, Somo akaniuliza yaliojiri nikamweleza
Somo: nyie hamja-do kweli?
Money Stars: hapana, ameniheshimu kwa hilo, tena amejikaza kweli ni sawa na kumsusia Mwili mwanaume anaekupenda alafu akatae kula chakula
Somo: du hii mpya, Ila sio bure, huyu mwanaume atafanya unachotaka kukuridhisha Ila lazima sikumoja atakukamata tu kwenye ango yake ... usikubali tena kuonana nae mkiwa wawili
Money Stars: sawa Somo yangu nashukuru sana kwa msaada wako
Baada ya Lisaa limoja akaingia mwali Suzzane kapendeza kweli kweli utadhania sio Bikra,
Tukaongea nae akaelewa, tukamwita JITU tumtambulishe kwa Suzanne akaja akamwona akamfurahia JITU nae ni mchangamfu Bala, akamfanya Suzanne asijiskie aibu
Money Stars: namwangalia JITU namwangalia na Suzanne nacheka kimoyomoyo mbayaa doh siamini naona kama naota jamani kweli JITU ndio anaenda na Suzanne? !
Uuuuwi PLAN C ndio umeniendea sawa sawia, nashukuru Mungu kwa yote
Kesho yake mimi, Suzanne, JITU tukarudi jijini kwa Ndege, nikafikia Hotelini na JITU, Suzanne akaenda kwao, akaenda kuwaeleza wazazi wake kwa amepata mchumba anataka kumleta nyumbani kumtambulisha
Wazazi wakakubali, aje tutampokea
Wiki iliofuata JITU akaingia nyumbani kwa akina Suzanne na washenga akapeleka barua, ikapokelewa Baada ya siku 3 ikajibiwa,
Siku ya kuleta Mahari, Grace alikuwepo lakini mimi sikuwepo, naskia alipojua ni JITU anamuoa nduguyake Suzanne alizimia kwa mshutuko!
Chezea Punda wewe?!
Tuonane Kesho Tar 8 Novemba 2018 saa 1 usiku ya Tanzania
-----------------------------------
D. KUWEKWA HURU NA HARUSI YA PILI
Baada ya sakata la Arusha na Dar na mahari ya Suzanne bado nilikuwa naishi hotelini kwa malipo ya JITU nikaambiwa Grace amelazwa hospital moja hapa mjini
Nikaamua kuuvaa ubinaadam nikaona niende kumchungulia bila yeye kujijua, kufika wamejaa ndugu kibao na mama yake anamwuguza
Akiulizwa vepe mbona ulizimia anasema alikuwa amechoka na sikuhio hakula kabisa kabla ya kuja kwenye mahari si unamjua Grace alivyo msanii kama kawaida yake lazima adanganye
Nikaondoka kwenda kumtafuta Lawyer
Money Stars: mwana mwana!
Lawyer: ah boss wangu niaje?!
Money stars: Leo mkono wangu wa kulia unaniwasha mbaya
Lawyer: sawa taajiri nakuja nakuja
Baada ya nusu saa tukaonana kijiweni kwetu Mbagalaa, ndio Mbagalaa kwani Mbagalaa kuna nini?!
Tukaongea kwa muda wa lisaa limoja tunapanga na kupangua
Money Stars: hivi Lawyer una mpango wa kuoa lini? !
Lawyer: doh Boss Lady ulisema mkono upi unakuwasha!?
Money stars: wa kulia
Lawyer: hivi pesa inamtokaga mtu mkono gani ukiwasha?
Money Stars: we bwana unaoa lini?!
Lawyer: ah sina wa kumuoa, sijapata binti wa kupenda nae we si umeninyakulia mtoto Suzanne bwana
Money Stars: nipo serious bwana
Lawyer: na mimi pia
Money Stars: unamwonaje Grace
Lawyer: sipendagi baby mamas nataka mabikra
Money Stars: we unayo?!
Lawyer: ah bwana me sijampenda huyo Grace wako Kwanzaa anaonekana ana roho mbaya
Money Stars: Ulumbi je?!
Lawyer: khaaa! Uyo aliekuwa anahemewa na wazee... staki laana mimi
Money stars: yale manyambizi hujayaelewa?!
Lawyer: ah bwana ngoja nipate wangu
Money Stars: sawa hivi Ulumbi yupo location gan kwa sasa?!
Lawyer: yupo mkoa, bado naendelea kumtafuta kuna mikoa 2 nimebakisha nahisi yupo huko
Money Stars: usisahau kunifahamisha sasa nipelekee hizi barua kwa Lola, Linda na Lila
Hakikisha naonana na kila mmoja kwa siku niliowaandikia na wasichelewe, wakichelewa utawalipia
Lawyer: sawa boss
Money Stars: hela zao za kuwatoa kwenye uchafu hizi hapa na walipie kodi zao wanazodaiwa na wenye nyumba was
Lawyer: sawa boss
Money Stars: saa 1usiku nataka kuonana na Lina nadhani yeye ndio anafanana na mimi zaidi kiumbo
Lawyer: kweli boss umejuaje?!
Basi kikako kikaisha tukarudi town, kurudi hotelini namkuta JITU amekaa kitandani kwangu ananisubiria
Money Stars: samahani nimekosea chumba
JITU: hapana ni chako
Money Stars: huku umeingiaje? !
JITU: usijali, tunahitaji kuongea,
Money Stars: sawa, lakini tunaongelea pale nje restaurant humu sitarudi tena
JITU: doh! Sawa Mama watatu
Baada ya muda wa kushuka restaurant malumbano yaliendelea kwa chini chini maana JITU sijui alikuwa amekunywa pombe au amelewa mvinyo sikuelewa alipandwa na nini sikuhio
Anasema eti hataki kumuoa Suzanne hajampenda ananipenda mimi, nikaendelea kumsihi afanye kama tulivyokubaliana lakini si unajua mwanaume aliekunywa pombe anavyokuwa nikaona hapa napoteza nguvu zangu bure
Tukaendelea kuongea baadae JITU akaanza kutoa masharti yake:
JITU: sawa nitamuoa kama unavyotaka lakini jua simpendi ila nitampenda sababu yako
Money Stars: ukitaka kuiona hii sura yangu tena
Nataka ufanye kama tulivyoongea... umpende kama ambavyo ungenipenda mimi,
Umlinde kama ambavyo ungenilinda mimi
Umthamini kama vile ambavyo ungenithamini mimi
Umtumikie na kumheshimu kama ambavyo ungeniheshimu, ungejitoa na kunitumikia mimi na mama yako mzazi
Wewe sio mtoto tena na hauna miaka 18 tena
Pamoja mtazaa watoto wa kike na kiume kadri ya Mungu atakavyowajalia nawaombea
Siku utakayomtesa au kumpiga Suzanne utakuwa umenitesa na kunipiga mimi
Siku utakayochepuka kwa Suzanne ni siku ambavyo utakuwa umenichepukia mimi
JITU: mbona masharti magumu kama jini mtoa roho
Money stars: kama hautaki me na wewe tuachane utajiju na maisha yako
JITU: doh hapo pagumu
Money Stars: ukitaka urafiki na mimi tuwe family friends na nini, we nikubalie ombi langu
mara simu yangu ikaita,
Samahani napokea simu maramoja
Nikasogea pembeni nikaskiliza simu kumbe Lawyer ameshamleta Lina
Sawa mpeleke chumbani na mwambie asikosee.. akiharibu hapa tusijuane... simu ikakatwa
Nikarudi kwa JITU, sasa mimi naondoka na harusi yako ni kesho, ngoja nikalale nimechoka sana... usiharibu plz tumeipanga hii harusi kwa muda wa miezi 2 na wala mume hajui narudi lini Uingereza usiniangushe
JITU: sawa Basi angalau niachie usiku huu niwe na wewe basi
Money Stars: usiku mwema Bwana harusi, tuonane kesho ukumbini... usisahau mimi ni mtoto wa Baba Mkubwa wako sawa?!
Huyoo nikapanda juu kufika namkuta Bimdashi Lina ameshafanya yake, nikakusanya kila kilicho changu nduki, ile nakaribia kwenye lift namwona JITU anapanda
Ngazi kuja kulala, nikacheka sana
Nikaondoka kulala hotel nyingine kabisa
Usiku wa saa 6 napigiwa simu na Lawyer kuwa Lola na Lila wamekubaliana na ule mpango wetu kesho watafika saloon na Suzanne amewakubali pia
Money Stars: Grace vipi?!
Lawyer: bado yupo hospital amesema hatoenda kwenye harusi
Money Stars: usiku mwema taajiri yangu simu ikakatwa
Asubuhi nikaamshwa na simu ya Lawyer;
Lawyer: mama amka wee tuna harusi ya kwenda
Money Stars: Lina je?!
Lawyer: anasema JITU hajagundua chochote alikuja pale chumbani kwako akidhania umelala, akaingia mazima mazima akafanya yake na Lina akafanya kama alivyoelekezwa alfajiri kabla JITU hajaamka akawa ameshaondoka mahala pale
Money Stars: utanisindikiza kwenye harusi kama mume wangu... Jiandae
Lawyer: poa boss kubwa shukrani
Baada ya masaa kadhaa tukadondoka kwenda kanisani na Lawyer kushuhudia ndoa ya JITU na Suzzane Bikra, kama kawaida maids ndio hao hao mashosti Lola na Lila... baadae wakaingia maharusi kanisani ibada ikaanza na litrugia tele kikaingia kipindi cha kufungishwa ndoa
Mchungaji akauliza kama kuna mtu yeyote mwenye kupinga ndoa hii aseme sasa au akae kimya milele
Watu wote kimya, tukasubiri kama dk moja mara tukasikia Mimi hapa napinga, kuangalia ni Grace
Watu wote hoi, Grace?!
Grace: akasogea mbele kuelezea kwanini anapinga akasema kuwa anamfahamu sana bwana harusi na bi harusi ni mdogowake
Bwana harusi atamtesa mdogowake mana Bwana harusi ana machine kubwa sana na bi harusi ni Bikra
Watu: wakaanza kuning'ona aibuje
Mimi nipo na Lawyer nyuma tunacheka mbavu hatuna
Mchungaji: unajuaje kuwa bwana harusi ana machine kubwa?!
Grace: nilishatembea nae sio chini ya mara 5
Wageni: wananong'ona aibu,
Mamake JITU: anaona aibu mpaka anaangalia chini
Money Stars: aisee embu kamtoe Grace bwana ameshajiaibisha vya kutosha kwa nduguze
Mchungaji: binti mnahamhusiano na bwana harusi?!
Grace: ndio... hapana
Mchungaji: kipi ni jibu sahihi?! Mbona majibu yako hayajitoshelezi?!
Grace: nilikuwa baadae nilipojua ameoa tukaachana
Mchungaji: bwana harusi umeoa?!
JITU: nimeshatalakiana na mkewangu kwasababu alizaa na Marehemu Baba yangu na talaka yangu hii hapa
Wageni: kimyaaa na mishangao juu
Mchungaji: binti una lingine la kuzuia ndoa hii?! Maana kama ni machine kubwa ya bwana harusi naona umetushangaza wengi lakini sio sababu ya kufanya ndoa isifungwe ... hawa wawili ni watu wazima mpaka kuchukua hatua ya kuoana ina maana wameshafahamiana na kuja huku kufunga ndoa
Grace: akanyamaza kimya huku akiwaangalia JITU na Suzzane mdogowake... akamjibu mchungaji hapana akarudi kukaa kwenye kiti cha kanisa
Mara wakaja mabaunsa wa JITU kumtoa Grace nje, Lawyer akawafuata nje.. mimi nikabakia ndani kushuhudia harusi ya JITU na SUZZANE kama ilivyopangwa!
Mchungaji: akarudia swali tena kama yupo wa kupinga ndoa aseme sasa akiwa na sababu za muhimu zaidi ya hii alioitaja Binti aliepita
Wageni: kimyaaa
Baada ya muda kupita hakuna aliejitokeza, Mchungaji akafungisha ndoa Baada ya madakika machache mbele JITU na Suzzane wakawa
Mr & Mrs JITU MANYANGA
Wamama: vigelegele nene kwa sana
Money Stars: nilipoona wameshasaini vyeti vyao vya ndoa na kuonyesha umati nikatoka nje kumtafuta Lawyer hayupo Kumpigia simu haipatikani
Kumpigia simu hapatikani, nikaona huu msala sasa nikikaa hapa wakatoka mambo yangu mengi yataharibika nikachukua taxi mpaka hotelini kwangu, namkuta Lawyer na Grace wanaongea
Money Stars: simu umeibiwa au?! He Grace upo? ! Sikujua kama mnafahamiana na huyu kaka
Grace: analia machozi Acha!
Money Stars: kulikoni Mbona mnalia lia?!
Lawyer: mambo yameharibika Money,
Money Stars: nini tena?
Lawyer: Grace ni mjamzito wa miezi 2 na anasema mimba ni ya JITU
Money stars: nikashtuka lakini nikajikaza kisabuni, nikajibu mmmh tutajuaje kama ni ya JITU?!
Najua Grace sio Muhuni ila nina miezi mingi sijamwona kwahiyo sijui huko alipokuwa
Grace hii mimba ya JITU kweli?!
Grace: ndio
Money Stars: ina maana umelala nae miezi 3-2 iliopita?!
Grace: ndio
Money Stars: nikiwaza hio miezi ndio JITU Alifiwa na Baba yake inawezekanaje?! Mmmh huenda kweli au la lakini sidhani kama mimba ni ya JITU na ingekuwa kweli ya JITU Grace angeongea pale Kanisani kwanini alinyamaza?!
Grace yupo very selfish asingenyamaza nakwambia ila haya yote tutayajua siku Za usoni,
Grace, nakushauri rudi nyumbani ukapumzike nitakutafuta tutafanya DNA test kama mimba ni ya JITU nakuhakikishia haki za mwanao zitapatikana usijali sawa? !
Grace: sawa
Money Stars: wala usikasirike, JITU sio mara ya Kwanzaa anaoa, hii hapa namba yangu
Tutawasiliana sawa mami?!
Grace: sawa
Akakubali kurudi kwa wazazi wake magomeni kupumzika
Mimi na Lawyer tukarudi ukumbini kuendelea na sherehe, harusi ilikuwa nzuri sana, kubwaaaa nzuri kagharamia mwenyewe JITU kila kitu
Alivyomjinga katika utambulisho akasahau kunitambulisha kabisaa doh basi nikawa buzy na Lawyer tunakunywa wines nakucheka hapo tunamshukuru Mungu dili tulilojitahidi kulipanga limefanikiwa doh nilipumuaje sikuhio mpaka kunywa wine sio mchezo ati. ..
Nilijiona nimetua mzigo mkubwa saanaaa roho yangu ilipumuaa huuuu nikaanza kupata raha moyoni mwangu
Nikiwaangalia Suzanne na JITU wanavyocheza Blues naskia raha sana na kumshukuru Mungu, hatimaye Imekuwa. .. asante sana Mungu
TUONANE TAR 13 NOVEMBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
Wamama: vigelegele nene kwa sana
Money Stars: nilipoona wameshasaini vyeti vyao vya ndoa na kuonyesha umati nikatoka nje kumtafuta Lawyer hayupo Kumpigia simu haipatikani
Kumpigia simu hapatikani, nikaona huu msala sasa nikikaa hapa wakatoka mambo yangu mengi yataharibika nikachukua taxi mpaka hotelini kwangu, namkuta Lawyer na Grace wanaongea
Money Stars: simu umeibiwa au?! He Grace upo? ! Sikujua kama mnafahamiana na huyu kaka
Grace: analia machozi Acha!
Money Stars: kulikoni Mbona mnalia lia?!
Lawyer: mambo yameharibika Money,
Money Stars: nini tena?
Lawyer: Grace ni mjamzito wa miezi 2 na anasema mimba ni ya JITU
Money stars: nikashtuka lakini nikajikaza kisabuni, nikajibu mmmh tutajuaje kama ni ya JITU?!
Najua Grace sio Muhuni ila nina miezi mingi sijamwona kwahiyo sijui huko alipokuwa
Grace hii mimba ya JITU kweli?!
Grace: ndio
Money Stars: ina maana umelala nae miezi 3-2 iliopita?!
Grace: ndio
Money Stars: nikiwaza hio miezi ndio JITU Alifiwa na Baba yake inawezekanaje?! Mmmh huenda kweli au la lakini sidhani kama mimba ni ya JITU na ingekuwa kweli ya JITU Grace angeongea pale Kanisani kwanini alinyamaza?!
Grace yupo very selfish asingenyamaza nakwambia ila haya yote tutayajua siku Za usoni,
Grace, nakushauri rudi nyumbani ukapumzike nitakutafuta tutafanya DNA test kama mimba ni ya JITU nakuhakikishia haki za mwanao zitapatikana usijali sawa? !
Grace: sawa
Money Stars: wala usikasirike, JITU sio mara ya Kwanzaa anaoa, hii hapa namba yangu
Tutawasiliana sawa mami?!
Grace: sawa
Akakubali kurudi kwa wazazi wake magomeni kupumzika
Mimi na Lawyer tukarudi ukumbini kuendelea na sherehe, harusi ilikuwa nzuri sana, kubwaaaa nzuri kagharamia mwenyewe JITU kila kitu
Alivyomjinga katika utambulisho akasahau kunitambulisha kabisaa doh basi nikawa buzy na Lawyer tunakunywa wines nakucheka hapo tunamshukuru Mungu dili tulilojitahidi kulipanga limefanikiwa doh nilipumuaje sikuhio mpaka kunywa wine sio mchezo ati. ..
Nilijiona nimetua mzigo mkubwa saanaaa roho yangu ilipumuaa huuuu nikaanza kupata raha moyoni mwangu
Nikiwaangalia Suzanne na JITU wanavyocheza Blues naskia raha sana na kumshukuru Mungu, hatimaye Imekuwa. .. asante sana Mungu
TUONANE TAR 13 NOVEMBA 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
-----------------------------------